Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1225 | 1226 | (Page 1227) | 1228 | 1229 | .... | 3283 | newer

  0 0

   Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) Kuhusu makusudio ya Tume hiyo kuvifuta vyama 1862 katika daftari la vyama vya Ushirika vyama ambavyo vimekiuka matakwa ya sheria ya vyama vya ushirika No.6 ya mwaka 2013. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
   Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) Kuhusu makusudio ya Tume hiyo kuvifuta vyama 1862 katika daftari la vyama vya Ushirika vyama ambavyo vimekiuka matakwa ya sheria ya vyama vya ushirika No.6 ya mwaka 2013. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa na kushoto Afisa Uhusiano wa Tume hiyo Bw. Bunyanzu Ntambi.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo.PICHA NA HASSAN SILAYO- MAELEZO

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colasso akiongea wakati wa kutambulisha Mr Money anayehakikishia wateja na watumiaji wa huduma za Airtel Money uhakika na gharama nafuu katika huduma za kifedha.

  Airtel Tanzania imemtambulisha “Mr. Money” rafiki na mtoa habari njema atakayewasaidia wateja kutatua changamoto zao na kuwaelimisha kuhusu faida mbalimbali zinazotolewa kupitia huduma ya Airtel Money

  Mr. Money ametengenezwa kuonyesha utofauti katika huduma za kifedha na kuondoa matabaka katika huduma tunazozitoa sokoni na kuzifanya ziwe zinafanana.

  Mr. Money ataweza kuongea na watu katika umri tofauti vijana kwa wazee na kuleta uhai na thamani pindi wateja watakapotumia huduma zetu za kifedha. Kupitia mkakati huu mpya tunategemea huduma ya Airtel Money itakuwa zaidi

  Akiongea wakati wa uzinduzi, Bwana Sunil Colaso, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania alisema “Mr. Money atakuwa msaidizi ambaye atakusaidia kufanya mambo mengi zaidi kupitia huduma ya Airtel Money. atashughulikia changamoto zote na kutoa ufafanuzi juu ya faida mbalimbali zinazopatikana kupitia huduma ya Airtel Money na atasimamia mambo makuu mawili Uhakika na gharama nafuu katika huduma ya Airtel Money”.

  Moja kati ya huduma za uhakika nafuu na zakibunifu zinazotolewa na Airtel Money ni pamoja na Mkopo ya Airtel Timiza, huduma hii ni mikopo isiyo na dhamana kwa wateja na mawakala wa Airtel Money ikifatiwa na Airtel Money Tap Tap pia ni huduma nyingine ya kibunifu inayotoa nafasi kwa wateja kufanya malipo kupitia kadi maalumu

  Mr. Money ameshaanza kupasha habari njema kwa wateja wake kwa kuwawezesha wateja wake kupata Luku uniti za ziada pale wanaponunua LUKU kupitia Airtel Money, Mr. Money anaendelea na dhamira yake ya kutoa nyongeza ya ziada ya uniti za LUKU, na nyongeza za ziada za muda wa maongezi mteja atakapoongeza muda wa maongezi kupitia huduma ya Airtel Money, pamoja na kupata muda wa maongezi wa bure pale atakapotumia Airtel money kufanya malipo, kutuma pesa kwa wapendwa wao bure bila gharama yoyote na kuwawezesha wateja wake kufaidika kwa kiasi kikubwa na hivyo kuleta kutoa huduma zenye gharama nafuu zaidi sokoni

  Usikose kupata habari njema kutoka kwa Mr Money kuanzia sasa kwani tunaamini kwa namna moja au nyingine zitabadili maisha yako.
  kufurahia huduma mbalimbali zinazotolewa na Mr Money piga *150*60#

  0 0

   Sehemu ya Wakimbiaji wa Mbio za Mwenge, wakiwa tayari kuupokea Mwenge huo ulipowasili kwenye Kituo uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, kilichopo eneo la Ukuni, Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani Mei 19, 2016. Zaidi ya vijana 40 waliokuwa wameathiriwa na matumizi ya Madawa ya kulevwa wanalelewa katika kituo hicho.Picha zote na Othman Michuzi - MMG.
   Mmoja wa wakimbiza Mwenge huo, akiongoza mbio hizo wakati Mwenge wa Uhuru ulipokuwa ukiwasili kwenye Kituo uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, kilichopo eneo la Ukuni, Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani Mei 19, 2016.
  Mmiliki wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, Al Karim Bhanji, akitoa taarifa fupi ya kituo hicho kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima (hayupo pichani) wakati Mwenge huo ulipotembelea kituo hicho Mei 19, 2016.
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima (kushoto) akimkabidhi Mwenge, Mmiliki wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, Al Karim Bhanji, wakati wa hafla fupi ya Mwenge huo ulipotembelea kituo chake hicho. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanaga.


  0 0

  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akiwa ameshika medali ya Dag Hammarskjold waliyotunukiwa mashujaa watatu watanzania ambao wamepoteza maisha mwaka jana wakati wakihudumu katika Misheni za kulinda Amani za Umoja wa Mataifa. kushoto kwa Balozi ni Luteni Kanal George Ita'ngare, mshauri wa masuala ya kijeshi katika Uwakilishi wa Kudumu na kulia ni Bw,Herve Ladsous, Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Operesheni za Ulinsi wa Amani za Umoja wa Mataifa.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akimvisha Bibi Yacine Mar Diop medal maalum ya Kapteni Mbaye Diagne ambaye alikuwa ni mume wa Bibi Yacine, Kapteni Diagne aliuawa mwaka 1994 wakati wa mauaji ya kimbali ya Rwanda. medali hiyo maalum imebuniwa na Baraza la Usalama kwa kutambua ushujaa na uthubutu wake na kujituma kwake kwa hali ya juu hadi kupelekea kupoteza maisha. Kapteni Diagne anakumbukwa kwa namna alivyookoa maisha ya mamia ya wanyarwanda kwa kuwaficha kwenye lori na kuwapeleka mahali salama kabla ya yenye mwenyewe kuuawa.
  Sehemu ya washiriki wa hafla ya siku ya Kimataifa ya Walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa hafla hiyo ilifanyika jana Mei 19.
  Balozi Tuvako Manongi akiandika katika kitabu cha kuwaeni walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa waliopotea maisha mwaka jana. miongoni mwa mashujaa 129 waliokumbukwa wapo watanzania watatu ambao ni Sgt. Musa Abdrahamani Yusuf, Cpl John Leornad Mkude na Pte. Juma Ally Khamis.

  Na Mwandishi Maalum, New York

  Umoja wa Mataifa, jana Mei 19 umefanya hafla maalumu ya siku ya Kimataifa ya Walinzi wa Amani wanaohudumu katika Misheni mbalimbali za Kulinda Amani chini ya kofia ya Umoja wa Mataifa. Katika hafla hiyo jumla ya walinzi 129 wanajeshi na polisi waliopoteza maisha mwaka jana kwa kushambuliwa na makundi ya wapiganaji wenye silaha, matukio ya kigaidi, ajali na kuumwa walikumbukwa na kuenziwa kwa mchango wao.

  Miongoni mwa Mashujaa hao 129 kutoka nchi 50, wapo mashujaa watatu kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mashujaa hao ni Sgt. Musa Abdrahamani Yusuf, Cpl. John Leornad Mkude na Pte. Juma Ally Khamis.

  Hafla hiyo maalum ya kutambua mchango wa walinzi hao wa Amani na ambao wamejitolea maisha yao kwaajili ya kuwalinda na kuokoka maisha ya wananchi wasiokuwa na hatia katika nchi zinazokabiliwa na vita na migogoro ya wenyewenye kwa wenyewewe iliongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon.

  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, ndiye aliyepokea medali maalum za mashuja hao watatu kwa niaba ya familia zao. Medali waliyotunukiwa mashujaa hao na wengine inatambuliwa kama medali ya Dag Hammarskjold.

  Hafla ya mwaka huu, pamoja na kutambua mchango wa mashujaa hao 129 , pia ilitambua kwa namna ya pekee na kwa mara ya kwanza, mchango na kujitolea wa hali ya juu ulikofanywa na Kapteni Mbaye Diagne raia ya Senegal, aliyepoteza maisha mwaka 1994 wakati akiokoa maisha ya wanyarwada wakati wa mauaji ya kimbali.

  Kapteni Mbaye Diagne ameeziwa rasmi katika maadhimisho ya mwaka huu kwa kupewa medali maalum iliyopewa jina la Medali ya Mbaye Diagne, medali ambayo alikabidhiwa mjane wa Mbaye Bibi Yacine Mar Diop huku akishuhudiwa na watoto wake wawili.

  Kapten Mbaye Diagne alikuwa mwangalizi wa Amani nchini Rwanda, kwa ushujaa mkubwa na bila ya kujali hatari iliyokuwa ikimkabili alitumia lori kuwaficha na kuwapeleka mahali salama mamia ya wanyarwada wakati wa mauaji ya kimbali ya Rwanda.

  Kwa kutambua ushujaa na uthubutu wake huo, Baraza la Usalama lilibuni mwaka 2014 medali ya Kapten Mbaye Diagne ambayo watakuwa wanatunukiwa wanajeshi, polisi na raia ambao wameonyesha uthubutu na ushupavu wa hali ya juu kiasi cha kupoteza maisha yao wakati wakitekeleza majukumu yao.

  Akizungumza wakati wa halfa hiyo ambayo ilibeba majonzi ya aina yake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, alieleza kwamba, hadi kufikia mwezi wa nne mwaka huu, jumla ya walinzi wa Amani 3,400 wakiwamo wanajeshi, polisi na raia walikuwa wamepoteza maisha tangu kuanzishwa wa shughuli za ulinzi wa Amani kwa kofia ya Umoja wa Mataifa miaka 70 iliyopita.

  “Wakati leo tunawaenzi na kuwakumbuka mashujaa hawa 129 kutoka mataifa 50 waliopoteza maisha yao mwaka jana wakati wakitekeleza jukumu la kuwalinda wananchi wengine, jana ( Mei 18) walinzi wengine watano wanaohudumu huko Mali wamepoteza maisha baada ya kushambuliwa”. Akasema Ban Ki Moon kwa huzuni.

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Himo ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa Miembeni akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfuko wa kikundi cha Miembeni kilijulikanacho kama Miembeni Uchumi Society.
  Baadhi ya wananchi ambao ni wakazi wa Mtaa wa Miembeni katika mji mdog wa Himo mkoani Kilimanjaro wanaounda kikundi cha Miembeni Uchumi Society.


  0 0

  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imeanza kusajili Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; wakati wakiendelea na kikao cha Bajeti.

  Katika Usajili huo NIDA inategemea kusajili wabunge wote ambao hawakuwahi kusajiliwa awali na kupata vitambulisho vya Taifa, pamoja na kugawa vitambulisho Wabunge wameonyesha mwamko mkubwa katika kutumia fursa hii adhimu, kwa kuhakikisha kwamba wanakuwa mstari wa mbele kutimiza haki yao ya kikatiba ya kusajiliwa na kupata kitambulisho cha Taifa; ambacho kimekuwa na faida nyingi kiuchumi, kijamii na kisiasa.

  Mpaka sasa NIDA imeshatoa zaidi ya vitambulisho zaidi ya milioni 2.5 na kwa sasa NIDA iko mbioni kuanza usajili kwa kutumia mtaji wa taarifa toka NEC ambapo zaidi ya wananchi milioni 22 watasajiliwa na kupewa namba ya utambulisho ili kuanza matumizi mbalimbali.
  Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe (Mb) akiwa na Afisa Usajili Bw. Surera wakati akipata huduma ya usajili kwenye ukumbi wa Bunge. Katika zoezi hilo mbali na kujaza fomu za maombi ya Utambulisho, pia walichukuliwa alama za kibaiolojia picha na saini ya kielektroniki.
  Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh. Saed Kubenea akisaidiwa kujaza fomu za maombi za Vitambulisho vya taifa na Afisa Usajili Bi. Hadija Bauji.
  Mh. Saed Kubenea akisaidiwa na Afisa Usajili Bw. Surera kuchukua alama za vidole wakati wa hatua ya uchukuaji alama za kibaiolojia.
  Waziri wa Katiba na Sheria, Dr. Harrison Mwakyembe (Mb) akisaidiwa kujaza fomu na Meneja Usajili Vitambulisho vya Taifa, Bi. Julian Mafuru.

  0 0


  0 0

  KAMPUNI ya Peri hapa nchini inayojihusiaha tecknolojiia ya ujenzi hapa imezinduliwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Uvumbuzi wa shirika la Nyumba nchini, Issack Peter.


  Kampuni ya Peri ni ya nchini Ujerumani yenye makao makuu yake maeneo ya Makumbusho jijini Dar es Salaam 

  kampuni hiyo inaweza kupunguza uharibifu wa mazingira kutokana na teknolojia wanayoitumia katika ujenzi wa Majengo marefu mbalimbali kuwa katika teknolojia yao haitumii mti kwaajili ya ujenzi.
  Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Uvumbuzi wa shirika la Nyumba nchini (NHC), Issack Peter (katikati) Mkurugenzi wa Kampuni ya Peri, Theunis Visser (Kushoto) na kulia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Peri, Giuseppe Rosiello wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampuni ya Peri hapa nchini.
  Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Uvumbuzi wa shirika la Nyumba nchini, Issack Peter akizungumza katika uzinduzi wa Kampuni ya Kijerumaji hapa nchini ya Peri jijini Dar es Salaam.

  Amesema kuwa Shirika la nyumba hapa nchini lipo katika mpango wa kuendeleza nyumba 6000 hapa nchini kwaajili ya makazi na Biashara na nyumba hizo zipo za Gharama nafuu, gharama za kati pamoja na gharama za juu.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Peri, Theunis Visser akizungumza katika ufunguzi wa kampuni ya Peri jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kampuni ya Peri ni kampuni inayo saidia katika kupunguza uharibifu wa mazingira hasa kupunguza ukataji wa miti pia inaendeleza majengo mbalimbali.

  0 0

  Shughuli za uchimbaji wa madini anuai maeneo mbalimbali ya Tanzania. Shughuli za uchimbaji wa madini anuai maeneo mbalimbali ya Tanzania.

    Na Mwandishi Maalumu.
  MAPATO ya Serikali ya Tanzania yanayotokana na shughuli za uchimbaji yameongezeka kwa asilimia 28 katika kipindi cha mwaka 2013/14, kwa mujibu wa ripoti ya sita ya asasi nayoshughulika na biashara hiyo – Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI) - kwa kipindi kinachoishia Juni 30, mwaka jana. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo iliandaliwa na BDO East Africa na kutolewa mjini Dar es Salaam na TEIT, licha ya kushuka kwa asilimia 10 kwa idadi ya kampuni zinazohusika, mapato ya serikali kutokana na sekta ya uchimbaji yaliongezeka kutoka Sh. bilioni 956 mwaka 2013 hadi kufikia Sh. bilioni 1,221. Ripoti hiyo inasema ongezeko hilo kubwa lifikialo Sh. bilioni 265 linatokana na ongezeko la uzalishaji wa dhahabu katika kipindi cha mwaka huo kwa asilimia 10 hali kadhalika na malipo ya kodi ya taasisi yaliyofanywa na Kampuni ya Ophir Tanzania (Block 1) ltd ya Sh. bilioni 361. Ripoti hiyo ya TEITI inalenga kusawazisha data iliyotolewa na kampuni hizo za migodi na ile ya wizara na mashirika husika. Malengo ya jumla ya zoezi hili la usawazishi ni kuisaidia serikali itambue mchango chanya unaotolewa rasilimali za madini katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi na kuelewa uwezo wake katika kuboresha usimamizi wa rasilimali ili kujumuisha na kutekeleza kikamilifu misingi na vigezo vya TEITI.
   Mwelekeo wa stakabadhi za serikali kutokana na biashara ya uchumbaji katika ripoti sita za EITI zilizochotwa kutoka katika ripoti za TEITI zinaonesha kumekuwa na ongezeko la jumla ya mapato kwa asilimia 854 tangu kuwasilishwa kwa ripoti ya kwanza mwaka 2009. Ukijumlisha kampuni zote za gesi na mafuta Kumekuwa na ongezeko la jumla la kampuni za gesi na migodi kutoka 11 mwaka 2009 hadi kufikia kampuni 59 mwaka 2014. Hata hivyo, ripoti hiyo inabainisha kwamba kampuni zilizohakikiwa mwaka 2013 zilikuwa 65. Kodi ya taasisi iliyolipwa serikalini ilikuwa Sh. bilioni 492.490, ikiwa ni asilimia 42.49 ya mapato yaliyokusanywa ambapo kodi ya mapato (PAYE) na SDL zilichangia Sh. bilioni 162.885 ambazo ni sawa na asilimia 14.05 ya mapato yote, kwa mujibu wa ripoti hiyo. “Orodha ya kampuni za uchimbaji zilizoteuliwa na shirika la Multi-Stakeholder Group (MSG) kwa zoezi la usawazishi lilijumuisha kampuni 38 za uchimbaji na 21 za mafuta na gesi na kufanya jumla ya kampuni kuwa 59. Karibu kampuni zote zilizohusishwa katika zoezi hilo zimeshawasilisha taratibu zao za kuripoti, isipokuwa nne. [caption id="attachment_71800" align="alignnone" width="800"]Shughuli za uchimbaji wa madini anuai maeneo mbalimbali ya Tanzania. Shughuli za uchimbaji wa madini anuai maeneo mbalimbali ya Tanzania.

   Kampuni nne ambazo zimesimaisha shughuli zao nchini Tanzania na ambazo hazipo kabisa nchini hazikuwasilisha taratibu zao. Hata hivyo, jumla ya mapato yaliyopokelewa na kutangazwa na taasisi za serikali kutoka kampuni hizo, yalikuwa Sh. bilioni 2.5, ambayo ni sawa na asilimia 0.20 ya jumla ya malipo yote yaliyofanyika serikalini. Kampuni hizo nne ni Tanzanite One Trading Ltd., Songshan Geology Minerals Co. Ltd., Afren Gabon Ltd, na Siwandu Metal Ltd. Ripoti hiyo inasema kumekuwa na kuhitilafiana kuhusu malipo halisi kati ya yale yaliyotajwa na kampuni za uchimbaji na yale yanayofahamika na serikali mwanzoni mwa usuluhishi ambapo tofauti ilikuwa ya asilimia 1.69 ya mapato yote yaliyotangazwa na serikali. Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika hitimishoo la usuluhishi, tofauti halisi ikawa Sh. 2,428,572,571, ikiwa ni asilimia 0.20 ya jumla ya malipo yote yaliyotangazwa na serikali Ripoti hiyo pia inasema kumekuwa na upungufu wa asilimia 10 katika ukusanyaji mapato licha ya ongezeko la uzalishaji dhahabu kwa sababu ya kuporomoka kwa bei ya dhahabu mwaka 2014. Jumla ya mapato yaliyoripotiwa na kampuni hizo yalikuwa dola za Marekeni 2,146,062,181 mwaka 2014 ikilinganishwa na dola 2,361,169,479 mwaka 2013. Kwa mujibu wa wastani wa bei ya dhahabu iliyokokotelewa kwa msingi wa takwimu za kila mwezi, watani wa bei ya dhahabu ilipungua mwaka 2014 ikilinganishwa na mwaka 2013 kutokana na wastani wa dola 1,530.88 hadi dola 1,264.99 kwa onzi ya trei, ambapo ni upungufu wa asilimia 17. Wakati upungufu wa mapato yatokanayo na madini unasababishwa zaidi na kushuka kwa bei ya madini hayo mwaka 2014, kulikuwa pia na upungufu wa idadi ya kampuni za migodi, kutoka kampuni 46 mwaka 2013 hadi kufikia 38 mwaka 2014 kwa sababu baadhi yao zilifunga shughuli zake nchini Tanzania. Ophir Tanzania (Block 1) Ltd ilifanya malipo ya jumla ya Sh. 361,938,833,000.00 (30%) kwa serikali ikiwa ya kwanza katika orodha ya walipaji kumi bora wa kodi kwa mwaka 2014, ikifuatiwa na Geita Gold Mine – Sh. 195,618,242,000 (16%), Bulyahulu Gold Mining Sh. 105,602,231,000 (9%), Pan African Energy Tanzania Ltd Sh. 76,907,992 (6%), na North Mara Gold Mine Sh. 66,835,788 (5%). Kampuni nyingine katika orodha hiyo ya kampuni bora katika ulipaji kodi kwa mwaka 2014 ni pamoja na Pangea Minerals Ltd., Songas Limited, Tanga Cement Company Ltd, Tanzania Portland Cement Ltd., Statoil Tanzania AS na Resolute Tanzania Ltd. Tanzania ilijiunga na TEITI mnamo Februari 2009 kufuatia mapendekezo yaliyokuwa kama sehemu ya utekelezaji wa upembuzi yakinifu wa kuhakiki sekta ya madini kwa mwaka 2007. Kundi la kazi la wadau - Multi-Stakeholder Working Group (MSG) – liliundwa kusimamia utekelezaji wa EITI nchini Tanzania na liliwajumuisha wawakilishi kutoka asasi za kijamii, kampuni za uchimbaji na serikali yenyewe.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Daud Msangi ambaye ndie mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi akisisitiza Jambo wakati wa Mkutano Huo, Uliofanyika makao makuu ya Mfuko huo, Jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wajumbe wa tawi la Tughe katika mfuko wa Pensheni wa GEPF wakifuatilia agenda za mkutano zilizojadiliwa.
  Timu ya wanachama wa tughe katika tawi la Mfuko wa GEPF pamoja na menejimenti katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kikao cha tano cha baraza la wafanyakazi.

  0 0

  Benki ya Exim Tanzania imeanza kukabidhi zawadi mbalimbali zikiwemo simu za mkononi na fulana kwa washindi wa kampeni ya benki hiyo inayoendelea ikihamasisha matumizi ya kituo chake cha huduma kwa wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu.

  Washindi wa kwanza wa benki hiyo walitangazwa mapema wiki hii mkoani Mwanza na kisha kukabidhiwa zawadi zao zilizoambatana na pongezi kutoka kwa uongozi wa benki hiyo tawi la Mwanza.

  “Kwa sasa kupiga simu kwenye kituo chetu cha huduma kwa wateja humaanisha kupata msaada wa haraka kutoka kwa wahudumu wetu makini na pia ni kujiweka katika nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo simu za kisasa aina ya iPhone 5s,’’ alibainisha Meneja wa benki hiyo tawi la Mwanza, Bw Deogratias Makwaia wakati akikabidhi zawadi hizo, jijini Mwanza.

  Kwa mujibu wa Bw Makwaia lengo la kampeni hiyo ni kuhamasisha matumizi ya kituo cha huduma kwa wateja wa benki hiyo kupitia namba ya simu 0784107600 huku pia wateja wakipata fursa ya kuwasiliana moja kwa moja na wahudumu wa benki ili kupata msaada na taarifa kuhusu huduma za benki hiyo.

  “Bado watu wote wana nafasi ya kuendelea kushiriki kwenye kampeni hii na kujishindia zawadi zilizotajwa. Wanaweza kushiriki pia kwa kutembelea ukurasa wetu wa Facebook au kupiga simu kwa namba tajwa,’’ aliongeza

  Wakizungumza baada ya kupokea zawadi zao baadhi ya washindi hao mbali na kuonyesha kufurahishwa na zawadi hizo walitoa wito kwa wateja wengine wa benki hiyo kushiriki kwenye kampeni hiyo.

  “Nilifurahi sana nilipopokea simu kutoka Exim na kupewa taarifa kuwa nimejishindia simu aina ya iPhone 5s kwa kupiga tu simu huduma kwa wateja tena lengo likiwa na kupata msaada wa huduma ya kibenki…nilipatwa na mshtuko wa furaha,’’ alisema mmoja wa washindi hao Bw Chidiebere Abasirim.

  Meneja wa benki ya Exim tawi la Mwanza, Bw Deogratias Makwaia (Kushoto) akikabidhi zawadi ya simu aina ya Iphone 5s kwa mmoja wa washindi wa kampeni ya benki hiyo inayoendelea ya kuhamasisha matumizi ya kituo chake cha huduma kwa wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa kwenye tawi la benki hiyo jijini Mwanza hivi karibuni.

  0 0

  RAIS Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Dk. Ally Hassan Mwinyi, amesema kuwa benki zimekuwa zikiendeshwa kwa kutoa mkopo bila riba hivyo itasaidia watanzania kujiwekea akiba na kuweza kukopa kwa ajili ya maendeleo yao .

  Mwinyi ameyasema hayo leo , wakati akifungua kongamano la tatu la Taasisi za Kifedha za Kiislam Afrika, lenye lengo la kujengeana uwezo na wadau wa sekta za kifedha kwa watendaji linalofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency kwa siku mbili katika kuwezesha urahisishaji wa usimamizi wa taasisi hizo na fursa ambazo wanaweza kuwekeza katika nchi za Afrika ikiwemo na Tanzania.

  Amesema zipo baadhi ya benki zinatoza riba kubwa, hali inayowafanya wananchi baadhi ya wananchi kujiunga taasisi za kifedha na kuogopa kukopa mikopo kitokana na riba wanazotoza.Aidha amewawahamasisha wananchi kujiunga na benki za kiislaam ili kujiwekea akiba na kukopa fedha bila riba.

  Nae Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bima ya Kiislam Zanzibar, Said Abdallah, amesema asilimia 15 ya wananchi wanaojiunga na mfumo mpya wa bima ya Kiislam ni wapya.“Kuna umuhimu ya kuanzisha bima nyingine za kiislam nchini katika kuwezesha wananchi kujiunga na bima kwa ajili ya maisha yao,”amesema Rais Mstaafu, Mwinyi.Amesema pia sheria ya kuandaa bima za kiislam ni changamoto kubwa na kwamba hawajapata kibali kwa kamishina wa Bima tangu wameanza kufuatilia mwaka 2008 .

  RAIS Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Dk. Ally Hassan Mwinyi akisoma hotuba yake wakati alipozindua kongamano la tatu la Taasisi za Kifedha za Kiislam Afrika, lenye lengo la kujengeana uwezo na wadau wa sekta za kifedha kwa watendaji wa taasisi hizo linalofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency kwa siku mbili.

  Baadhi ya wadau wakiwa katika Kongamano la tatu la Taasisi za Kifedha za Kiislam Afrika, lenye lengo la kujengeana uwezo na wadau wa sekta za kifedha kwa watendaji wa taasisi hizo.

  Baadhi ya wasiriki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
  RAIS Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Dk. Ally Hassan Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo.

  0 0


  Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ubalozi wa Malawi na kupokelewa na mwenyeji wake, Mhe. Balozi Wilfred Ali (hayupo pichani). Dkt. Maalim alimtembelea Balozi huyo wa Malawi kwa lengo la kumshukuru kutokana na mchango mkubwa wa Ubalozi huo katika kufanikisha ufunguzi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Kuwait. Hata hivyo, Balozi Maalim, alimuhakikishia Balozi Ali utayari wa Tanzania kuendelea kushirikiana na Malawi na jamii nzima ya kidiplomasia nchini Kuwait.

  Balozi Dkt. Mahadhi pamoja na mwenyeji wake Mhe. Ali wakiendelea na mazungumzo yao.

  0 0
 • 05/20/16--01:21: YALE YALE.......


 • 0 0  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho, akitoa neno la hitimisho na kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa kufunga mkutano wa kitaifa wa mwitikio wa kudhibiti UKIMWI miongoni mwa vijana May, 2016.
   Mkurugenzi Idara ya maendeleo ya vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana na Ajira, James Kajugusi akifunga rasmi mkutano wa mkutano wa kitaifa wa mwitikio wa kudhibiti UKIMWI miongoni mwa vijana May, 2016
   Wadau wa shughuli za UKIMWI kwa vijana, wakiwa kwenye mkutano wa kitaifa wa mwitikio wa kudhibiti UKIMWI miongoni mwa vijana May, 2016.
  Baadhi ya washiriki walio kabidhiwa vyeti vya ushiriki wakati wa mkutano wa kitaifa wa mwitikio wa kudhibiti UKIMWI miongoni mwa vijana, wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi James Kajugusi wakati wa kufunga rasmi mkutano huo. May, 2016.Picha kwa hisani ya TACAIDS.


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe,Dkt.Asha Rose Migiro alipofika Ikulu Mjini Zanzibar asubuhi ya leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Uingereza  Mhe,Dkt.Asha Rose Migiro alipofika Ikulu Mjini Zanzibar asubuhi ya leo,[Picha na Ikulu.]

  0 0

  Rose Mdami

  Wadau kutoka Sekta mbalimbali nchini leo wamekutana katika kongamano maalumu kujadili suala la Vitambulisho vya Taifa na uwezekano wa kukamilika kwa mradi huo ili kuwezesha taifa kuwa na Kanzidata(database) yenye taarifa sahihi zenye kujibu maswali makuu nini ni nani, yuko wapi na anafanya nini. Lengo ni kurahisha utoaji huduma na kuwezesha wananchi kujishughulisha na masuala ya biashara kwa kuwa na mfumo rasmi unaowatambua

  Akifungua kongamano hilo, Kaimu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Nato Mwamba amesema mfumo wa Usajili na Utambuzi wa Watu ni mfumo ambao umesubiriwa kwa siku nyingi kwani manufaa yake ni makubwa katika mifumo mbalimbali nchini hususani mfumo wa biashara na taasisi za fedha nchini

  Amesema kutokana na kupanuka kwa matumizi ya teknolojia nchini, huduma nyingi zikiwemo huduma za kifedha zinategemea sana kuwepo kwa mfumo wa Vitambulisho vya Taifa ili kuwezesha watu wengi zaidi kunufaika na huduma zitolewazo kwa sasa kwani wengi wanakwama kwa kuwa hakuna mfumo rasmi unaowatambua. 

  Mafanikio ya mfumo huu ni kufungua milango kwa wananchi wengi zaidi kunufaika na huduma mbalimbali zinazoendelea kutolewa nchini zikiwemo huduma za kifedha na hivyo kuwataka wadau hao kuwezesha NIDA kufikia malengo ya usajili nchi nzima kufikia Disemba 31, 2016 ili mfumo wa Utambuzi wa Taifa uweze kuunganishwa na mifumo mingine

  Akieleza mkakati wa usajili kufikia Disemba 31, 2016, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Dkt. Medestus Kipilimba amesema NIDA imejizatiti kutumia taarifa za zilizokusanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuanza usajili utakaowezesha wananchi waliosajiliwa katika daftari la wapiga kura kuhakikiwa na kupata usajili awamu ya kwanza ambao utahusisha namba ya utambulisho kabla ya kupata kitambulisho cha Taifa. 

  Amesema hatua ya kufanya usajili wa awali na kutoa namba ya utambulisho itawezesha wananchi kuanza kufaidi utambulisho wao kwa kuwawezesha kupata huduma mbalimbali. Hata hivyo ili mwananchi kupata utambulisho kamili lazima kukamilisha hatua za usajili kwa kuhakikisha anawasilisha nyaraka muhimu za utambuzi ili kuendelea kupata huduma nyingine

  Kwa mara ya kwanza NIDA itaanza kuzalisha vitambulisho vyenye saini ya mwombaji ambayo itawekwa kwenye uso wa mbele wa kitambulisho na nyumba ya kitambulisho kutakuwa na saini ya mtoaji. Amesema hatua zote katika kukamilisha mpango huo zimekamilika

  Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau toka Taasisi za fedha nchini, TASAF, Wamiliki wa makampuni ya simu nchini, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Benki ya Dunia (World Bank), SSRA, BIMA, Melinda and Bill Gates Foundation, Tanzania Bankers Association( TBA) na wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Serikali.

   Naibu Gavana wa BOT Dkt Natu Mwamba akifungua kongamano la wadau kuhusu vitambulisho vya Taifa lililofanyika leo katika ukumbi wa Benki Kuu na kuhudhuriwa na wadau toka sekta mbalimbali nchini
   Mkurugenzi  mtendaji wa Financial Sector Deepening Trust Sosthenes Kewe akichangia mada wakati wa kongamano wa wadau lililohusu mpango wa Usajili vitambulisho vya Taifa
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Dkt. Modestus Kipilimba akionyesha wadau sampuli ya vitambulisho vyenye saini vitakavyoanza kutolewa hivi karibuni, wakati wa kongamano la wadau kuhusu mpango wa vitambulisho vya Taifa
   Mr. Sanjay C. Rughani Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini akiwasilisha mada wakati wa kongamano la wadau katika mpango wa usajili vitambulisho vya Taifa
   Mkurugenzi wa Fedha toka TASAF Bw. Joshua Nyamko akiwasilisha mada katika kongamano la wadau kujadili Vitambulisho vya Taifa
  Baadhi wa washiriki wa Kongamano la wadau kuhusu mpango wa Usajili vitambulisho vya Taifa wakisikiliza kwa makini mada ya mkakati wa Usajili kufikia Disemba 31,2016 iliyowasilishwa na NIDA.


  0 0

  Profesa Kennedy Gastorn, Katibu Mkuu mpya AALCO 

  Mkurugenzi wa masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kennedy Gastorn amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria katika nchi za Asia na Afrika-‘Asian-African Legal Consultative Organisation-AALCO’.

  Profesa Gastorn alichaguliwa kwa kauli moja wakati wa Mkutano wa 55 wa Jumuiya hiyo yenye jumla ya nchi wanachama 47 uliofanyika Mjini New Delhi, India tarehe 17 Mei, 2016 na kuhudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Baraka Luvanda. 

  Aidha, Profesa Gastorn ambaye alikuwa ni mgombea pekee wa nafasi hiyo baada ya kupendekezwa na Tanzania na kupitishwa na Umoja wa Afrika, anachukua nafasi ya Katibu Mkuu anayemaliza muda wake Profesa Rahmat Mohamad wa Malaysia ambaye muda wake unamalizika rasmi ifikapo mwezi Agosti, 2016 na Profesa Gastorn anatarajia kukabidhiwa madaraka hayo mwanzoni mwa mwezi Agosti, 2016.

  Mkutano wa Jumuiya ya AALCO ulifanyika kuanzia tarehe 16 Mei na kumalizika tarehe 20 Mei, 2016.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Dar es Salaam, 20 Mei, 2016.

older | 1 | .... | 1225 | 1226 | (Page 1227) | 1228 | 1229 | .... | 3283 | newer