Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1220 | 1221 | (Page 1222) | 1223 | 1224 | .... | 3270 | newer

  0 0


  0 0

  Tarehe 23 April, 2016.... ilitimia miaka 400 tangu gwiji wa fasihi, mashairi na tamthiliya, mwandishi maarufu wa Kiingereza, William Shakespeare alipofariki. Mwasisi wa taifa la Tanzania ,Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kutafsiri Kiswahili kazi mbili za Shakespeare :” Mabepari wa Venice” (Merchants of Venice) na “ Julius Kaizari” (Julius Caesar) ... 
  Wasanii mbalimbali duniani wamekuwa wakijumuika kutukuza kazi za nguli huyu asiyechuja kwa visa, lugha, nahau, misemo na mada za kila namna. Miongoni mwao ni kundi maalum - “Bards without Borders” (Watenzi Wasio na Mipaka), jijini London. Ndani wamo washairi wa Somalia, Nigeria, Bangladesh, Zimbabwe, Jordan, Colombia, Afghanistan, Bosnia, Ujerumani, Jamaica, Uingereza, India na Tanzania. 
  Mwakilishi wa Tanzania ni mwandishi Freddy Macha. Anatumia muziki wa ala mbalimbali ikiwemo Ngoma kumnadi Shakespeare. 
  Wakati maonesho mbalimbali yakiendelea kwa kasi Uingereza, Macha ametafsiri kazi zake Shakespeare kwa Kiswahili na pia kuandika tenzi mpya na kikundi hiki. 
  Moja ya tukio lililofanyika April 23 , klabu mashuhuri ya Rich Mix, London mashariki, Macha alichanganya mapigo ya Ngoma kadhaa za Kiafrika ikiwepo Sindimba ya Tanzania kutambika na kumsifia gwiji William Shakespeare. 

  0 0

  Mwili wa marehemu ukiingizwa katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es salaam leo tayari kwa kuswaliwa kabla ya mazishi.
  Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete (kushoto) akimfariji  baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi. 
  Mama wa marehemu (aliyevaa nguo nyeupe) akiwa na ndugu wa karibu wakiomboleza. 
  Baba wa marehemu akiwa na viongozi wa dini wakiombea mwili wa marehemu dua.
  Mke wa Rais mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na ndugu wa marehemu. kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

           
   Kiwanda cha bia aina ya serengeti kilichopo chang'ombe wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam kimepigwa faini ya shillingi za kitanzania millioni kumi na sita(16)na Baraza la usimamizi wa mazingira Nchini(NEMC)baada ya kutokutimiza masharti ya sheria ya mazingira ya mwaka(2004)na kanuni zake.   
         

  Uamuzi huo umefikiwa baada ya  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na mazingira Mh.Luhaga Mpina kupata malalamiko kutoka kwa wanainchi wanaozunguka maeneo ya kiwanda hicho na kuainisha uchafuzi wa mazingira yanayowazunguka wananchi hao na kuhatarisha  usalama wa afya zao,ambapo ilimlazimu naibu waziri kufanya ziara ya kushtukiza  kiwandani hapo,huku akiambatana na Wakurugenzi kutoka Baraza la usimamizi wa mazingira nchini(NEMC)na kujionea uharibifu huo. 
                    

  Mh.Mpina  ameagiza kiwanda hicho kulipa faini hiyo na kurekebisha miundo mbinu hiyo ndani ya siku arobaini na tano kusiwepo tena na utiririshaji maji machafu na yenye kemikali kali za sumu ambayo yanatoa harufu mbaya inayohatarisha afya  za wakazi wa chang'ombe wilaya ya temeke.                


  Pia mkurugenzi wa mazingira Bw. Boniventure Baya ametoa siku saba kwa kiwanda hicho kiwe kimelipa faini hiyo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kutokana na kwamba wamekua wakikaidi maagizo yanayotolewa na Baraza hilo la mazingira nchini(NEMC)na kuwataka kufanya hivyo haraka iwezekanavyo baada ya kukiuka sheria ya utunzaji mazingira ya mwaka(2004) na kutokutimiza masharti waliyopewa takribani miaka miwili iliyopita.      
       

  Naye mbunge wa Temeke(CUF) Mh.Abdallah Mtolea alisema kiwanda hicho kimekua na mahusiano mabaya na wananchi wanaozunguka  maeneo jirani na kiwanda hicho hivyo kupelekea kuwa na mgogoro wa muda mrefu na uongozi  kiwandani hapo na  kumuomba Naibu waziri kutatua tatizo hilo ambalo limekua likifanywa kwa makusudi na na uongozi wa kiwanda hicho ilihali wanajua madhara ya wanayoyapata wananchi.                                                          

  Aidha kwa upande wake afisa mazingira wa kiwanda hicho Bw.Simon Peter alipinga vikali tuhuma hizo ambazo zimeelekezwa katika kiwanda hicho na kusema uongozi wa kiwanda hicho unafanya kila jitihada ili kuweza kutatua kero hiyo na si kweli kwamba hawashughulikii tatizo hilo la mazingira jirani na wakazi hao.               


  Kwa upande wao wananchi kupitia kwa Bi.Emanuela Peter,walisema hiyo ni kero kubwa sana kwao ambapo imekuwa ikiwalazimu kuyahama makazi yao hasa wakati wa kipindi cha masika ambapo maji ya mvua na yale ya kiwanda huchanganyikana na kujaza uchafu wote majumbani mwao kutoka kiwandani na kuhatarisha afya zao hivyo kuhamia kwenye nyumba za kulala wageni kwa muda,hivyo wameiomba serikali kuangalia kwa makini na kuweza kulipatia ufumbuzi.                     


  Vilevile Mh.Luhaga alifanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha Cement Wazo kilichopo Tegeta wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam,hata hivyo hakuweza kukutana na kiongozi yeyote wa kiwanda hicho kwa madai kua walikua nje ya mkoa wa Dar es salaam,aidha Mh.Mpina alitoa tamko la serikali kuwa,serikali ya awamu ya tano haina uadui na wafanyabiashara pamoja na wawekezaji kama inavyozaniwa na watu wengine,bali inachotaka ni kufuatwa kwa Sheria,taratibu na kanuni kama inavyostahili.

   Naibu Waziri Wa nchi Ofisi ya Makamu wa rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina(katikati) akipata maelezo kutoka kwa Afisa mazingira wa kiwanda cha serengeti Bw.Simon Peter mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo.                      
   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina wa kwanza kushoto,katikati aliyevaa kanzu ni mbunge wa Temeke(CUF)Mh.Abdallah Mtolea wakitembezwa sehemu mbalimbali za kiwandani hapo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza.           
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akipata maelezo jinsi gani kiwanda hicho kinavyochuja maji kwa njia ya kisasa kabisa kwaajiri ya matumizi na uzalishaji kiwandani hapo.

   


  0 0

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Ukarabati mkubwa wa kivuko cha MV Magogoni umeanza rasmi mara baada ya kusitisha huduma zake hivi karibuni.

  Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo la bandari kujionea kazi ya ukarabati kwa kivuko hicho, Kaimu Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase Ole-kujan amesema kazi ya ukarabati wa kivuko hicho umeanza kwa hatua za awali za kukifanyia usafi ili kuona maeneo yaliyoharibika na kuyafanyia ukarabati.

  “ Muda wake wa matengenezo umefika na ni wakati muafaka kwa kivuko kufanyiwa matengenezo ni muda mrefu kimehudumia wananchi wa Jiji la Dar es Salaam lakini mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake kitarudi kutoa huduma kama kawaida” Alisema Mhandisi Manase.

  Mhandisi Manase ameongeza kuwa ukarabati huo utazingatia viwango vya kimataifa ili kukiwezesha kivuko hicho kudumu kwa muda mrefu bila ya kupatwa na hitilafu yoyote ya kiufundi na kuwaasa wahandisi husika kufanya ukarabati huo na kukamilika kwa muda uliopangwa.

  Aidha Mhandisi Mkuu Kutoka kampuni ya Songoro Marine Boat yard LTD Major Songoro amesema kwa kushirikiana na waandisi kutoka TEMESA watahakikisha wanamaliza kazi ya ukarabati kwa wakati na kwa ufanisi wa hali juu ili kurejesha huduma ya Kivuko hicho.

  Kivuko cha MV Magogoni kinachotoa huduma eneo la Magogoni na Kigamboni Jijini Dar es Salaam kimesitisha kutoa huduma kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo makubwa na kwa sasa kivuko cha MV Kigamboni kinashirikiana na MV. Lami kutoa huduma kwa wananchi.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela amefunga  mafunzo ya "Kungfu" yaliyokuwa yanaendeshwa na SHOKINJI KEMPO. Washiriki kutoka Dares salaam na Dodoma walionyeshana ufundi wa kung Fu na wengine walipandishwa madaraja. katiba hotuba yake aliwaomba Kemp hiyo kuwa walinzi wa amani kwani sifa kubwa ya wacheza kungfu ni kuhakikisha amani. Mwanzilishi wa Shokinji Kemp alifariki tarehe 14 mwezi wa 5 miaka 60 iliyopita huko Japan.
  Mwenyeji wa mashindano hayo Diwani wa Kitanzini ambaye yupo daraja la juu (Mkanda mweusi) alishukuru sana uwepo wa Mkuu wa wilaya na kuahidi kumsadia katika kulete amani na utulivu pamoja na kuzuia vijana kuingia kwenye tabia mbaya za uvutaji bangi na ulevi.
   Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akitoa zawadi ya mpira kwa mwakilishi wa kituo cha watoto taima cha Korongoni kwenye hafla hiyo
   Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiwa na wanamichezo wa Kungufu wenye mikanda myeusi na Kijani  kwenye hafla hiyo

  washiriki watoto wakionyesha umahili wao wa kungfu
   Diwani kata ya Kitanzini Manispaa ya Iringa (kulia)  akionyesha umahili wake wa Kung fu.


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza  uliopo London wakati alipowasili ubalozini hapo  kuzungumza na watanzania  waishio  nchini humo Mei  14, 2016.. Kushoto  ni  Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Msafiri Marwa
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitia saini kitabu cha wageni wakati alipowasili kwenye ubalozi wa Tanzania  nchini Uingereza uliopo London kuzungumza na Watanzania Mei 14, 2016. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki , kikanda na Kimataifa, Dkt Augustine Mahiga na kushoto ni Jaji Mkuu wa Tamzania Mhe. Mohamed Chande Othman
   Baadhi ya Watanzania waishio nchini Uingereza wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ubalozi wa  Tanzania uliopo London   Mei 14,2016
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania Waishio  nchini Uingereza  kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo London Mei 14, 2014.   Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Kikanda na Kimataifa, Dkt Augustine Mahiga. Kushoto ni KaimuBalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Msafiri  Marwa.


  0 0

  Mwanamke kutoka Tanzania Lilian Makoi Rabi amekuwa miongoni mwa washindi wa  tuzo ya ubunifu wa kuleta mabadiliko kwenye jamii inayotolewa na Kongamano la Uchumi Duniani linalofanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu limefanyika mjini Kigali nchini Rwanda.

  Shindano la kuwania tuzo hiyo linahusisha taasisi na kampuni ndogondogo zinazotoa huduma mbalimbali za ubunifu wenye kuleta mabadiliko kwenye jamii katika sekta mbalimbali.

  Lilian  kutoka taasisis ya bimaAFYA ametunukiwa tuzo kutokana na ubunifu wake katika kuboresha huduma za bima ya afya nchini kwa kuweka mfumo usio na urasimu wa kuwawezesha wananchi wenye kipato cha chini na wasio na ajira katika sekta rasmi kuweza kujiunga na mfumo wa bima ya afya na kupata matibabu tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo huduma hiyo iliwafikia waajiriwa waliopo kwenye sekta rasmi pekee.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kongamano la Uchumi duniani imeeleza kuwa ubunifu huu umeonekana unaweza kusaidia kuboresha huduma za bima za afya katika nchi mbalimbali za Afrika na kuanzia sasa mpaka mwaka ujao huduma za bimaAFYA zitaanza kutolewa katika nchi za Kenya,Uganda,Rwanda,Nigeria na Ghana.

  Washindi wengine wa tuzo hii  ya ubunifu  wenye kuleta mabadiliko ni Natalie Bitature (Uganda),Audrey Cheng (Kenya),Nneile Nkholise (Afrika ya Kusini),Larissa Uwase (Rwanda)


  Taarifa ya Kongamano hili imeeleza kuwa mabadiliko ya Afrika yataletwa na vijana ambao ndio wenye idadi kubwa ya  watu wanaoishi barani Afrika na ndio maana imeanzisha shindano la kuyaenzi makampuni yanayofanya kazi  kwenye nchi mbalimbali za Afrika yakiwa yanatoa huduma zenye ubunifu wenye kuleta mabadiliko  na kuwa inafurahisha kuona wanawake wajasiriamali hawajaachwa nyuma katika kuanzisha taasisi na kampuni zenye huduma za kuleta mabadiliko.


  “Karne ya 21  itakuwa karne ya Afrika,hivyo vijana popote walipo wanapaswa kuamka na kuhakikisha wanafanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kulifanya bara la Afrika kusimama  na kujitegemea katika Nyanja mbalimbali”.Alisema Elsie Kanza,Mkuu wa kongamano hilo katika ukanda wa bara la Afrika.

  Washindi wote wa tuzo  na washiriki wa shindano hilo waliofanya vizuri walialikwa kwenye Kongamano la Uchumi Duniani nchini Rwanda lililokuwa na washiriki Zaidi ya 1,200,000 kutoka nchi Zaidi ya 70 duniani ambapo walipata fursa ya kukutana na kubadilishana uzoefu wa shughuli zao pia

  0 0

  Mkazi wa Kijiji cha Kemuyak wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha Bwana Kalangangwe Lanya Vii akitoa maoni yake kwa Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 kuhusu suala la kupewa kipaumbele utoaji wa hati miliki kwa wanavijiji hasa wafugaji.
  Wakazi wa kijiji cha Oldonyo Sambu wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha wakijaza dodoso la kukusanya maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kuwa na Sera ya Ardhi itakayotatua changamoto zao na nchi kwa ujumla.
  Betha Muluu Afisa Ardhi na Maliasili wilaya ya Ngara mkoani Kagera akitoa maoni yake kwenye Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ilipokuwa mkoani Mwanza.
  Mjumbe wa Kamati ya kukusanya maoni Baadhi ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 Bw. David Malisa (shati ya mistari) akimpa maelekezo jinsi ya kujaza Dodoso la Kukusanya Maoni Mkazi wa Kijiji cha Nyanguge Magu Mkoani Mwanza.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo akimuapisha Radhia Rashid Haroub kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi hati ya kiapo Bi. Radhia Rashid Haroub baada ya kumuapisha rasmin leo kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ leo katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
  Bi,Radhia Rashid Haroub baada ya kumuapisha rasmin leo kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.

  0 0

  Usikose leo jumapili Mei 15,2015 kuanzia saa 12 jioni ndani ya CHECK INN PUB Kilimahewa, Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.
   Kutakuwa na show kali ya muziki wa dansi ambapo bendi ya African Artists Academy ya Jijini Mwanza itatoa burudani kwa wanamwanza kwa kiingilio cha shilingi 3,000 tu.
  Bonyeza HAPA Kwa Maelezo Zaidi.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikagua machinjio ya Vingunguti baada ya kuzungumza na wananchi wa Kata ya Mnyamani Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto.


  Na Dotto Mwaibale

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanawake wamekuwa ni chanzo cha ufisadi nchini kutokana na kupokea zawadi zitokanazo na fedha za kifisadi.

  Makonda aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnyamani Vingunguti Dar es Salaam jana katika mkutano wa kujadili namna ya kupata mikopo mbalimbali kutoka Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).

  " Ninyi wakina mama mmekuwa chanzo cha ufisadi kwa vile mmekuwa mkipokea fedha na zawadi mbalimbali kutoka kwa watoto wenu lakini mmekuwa hamuwahoji wanako zitoa fedha hizo kwani zingine zinakuwa za kifisadi" aliseama Makonda.

  Makonda aliwaambia wanawake hao kuwa hata katika suala zima la usafi linaanzia na malezi ya usafi ya wakina mama kwa watoto wao tangu wakiwa wadogo jambo ambalo lingesaidia kipindi hiki ambapo kunachangamoto kubwa ya kusafisha miji yetu.

  Katika hatua nyingine Makonda alitoa pongezi kwa Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto kwa kuwa jirani na wananchi wa kata yake kwa kufanya maendeleo bila ya kujali itikadi za vyama hasa katika kujipatia mikopo kutoka katika Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).

  "Nimefurahishwa na diwani wenu Kumbilamoto kwa kushirikiana nanyi ili  kujiletea maendeleo ni jambo zuri na wakati huu ni wa kukutana kubuni na kuangalia jambo gani litawakwamua kiuchumi badala ya kuwaza maandamano yasiyo na tija" alisema Makonda.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto (wa pili kulia), akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuzungumza na wananchi. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mnyamani, Shukuru Dege, RC. Makonda na Meneja wa Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB), Tawi la Ukonga, Das Ndazi.
  RC Makonda akipatiwa maelezo kuhusu mitambo ya kuchinjia iliyopo kwenye machinjio hiyo.


  0 0

  Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Dkt. William Kisinza akiongea na waandishi wa habari kutoka Kituo cha Waandishi wa Habari wa Kimataifa (ICFJ) na Taasisi ya “Malaria No More” kutoka nchini Marekani ambao walitembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa huo.
  Dkt. Robert Malima akitoa maelezo ya namna watafiti wanavyofanya utafiti na kuwakusanya mbu katika chumba maalum cha kufanyia utafiti kwa waandishi wa habari kutoka Kituo cha Waandishi wa Habari wa Kimataifa (ICFJ) na Taasisi ya “Malaria No More” kutoka nchini Marekani walipotembelea Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga mwishoni mwa wiki kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa huo.
  Mfanyakazi wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Masha Mfinanga akichambua viluwiluwi vya mbu na kuviweka kwenye kifaa maalum tayari kwa hatua nyingine za utafiti.

  BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(Katikati)akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,(hawapo pichani) wakati wa kutangaza baadhi ya wanamuziki nchini ambao watatoa burudani pamoja na Mwanamuziki nguli kutoka Marekani NE-YO, katika Uwanja wa (CCM) Kirumba jijini Mwanza kwenye tamasha la Jembeka na Vodacom Festival 2016.Wengine katika picha kushoto ni Mwakilishi wa NE-YO,E.Jay Mathews na Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo,Dkt.Sebastian Ndege.
  Mwakilishi wa Mwanamuzi nguli toka nchini Marekani NE-YO,E.Jay Mathews (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangazwa kwa wasanii watakaotoa burudani pamoja na mwanamuziki huyo katika tamasha la Jembeka na Vodacom festival 2016, litakalofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wapili (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo,Dkt. Sebastian Ndege, Matina Nkurlu Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, George Sozigwa Mkuu wa masuala ya ulinzi na Usalama wa tamasha hilo.
  Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul”Diamond Platinum’s”akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na jinsi atakavyoshiriki kutoa burudani na kuimba wimbo wa pamoja na mwanamuzi NE-YO wa nchini Marekani katika tamasha la Jembeka na Vodacom festival 2016,litakalofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo,Dkt.Sebastian Ndege,Matina Nkurlu Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania.

  Moto wa burudani utawaka katika jiji la Mwanza  Jumamosi ya wiki ijayo ambapo msanii maarufu wa muziki wa Bongofleva kutoka Marekani NE-YO atakapo shusha bonge ya shoo  kwa kushirikiana na wasanii wa hapa nchini katika uwanja wa CCM Kirumba kwenye  onyesho lililotayarishwa na Jembe Media chini ya Udhamini wa Vodacom Tanzania.

  Akiongea juu ya onyesho hilo la kihistoria katika ukanda wa ziwa Magharibi,Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alisema kuwa  Vodacom inayo furaha kudhamini tamasha hili kubwa litakaloleta burudani ya muziki kwa wateja wake na wananchi kwa ujumla.

  Aliwataja baadhi ya wanamuziki watakaowasha moto kumsindikiza NE-YO  kuwa ni  Diamond,Ney wa Mitego,Fid Q,Ruby,Baraka the Prince,Juma Nature,Mr.Blue,Stamina,JJ Bendi na wengineo .

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe  ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo, Dkt.Sebastian Ndege  aliwataka wapenzi wa muziki kujitokeza kupata budurani ya mwaka katika tamasha hilo na mipango ya tamasha hilo kubwa imekamilika na kuwataka wapenzi wa muziki wa Mkoa wa Mwanza wakae mkao wa kula wa  ya karne.

  Kuhusiana na viingilio alisema kuwa tiketi zitauzwa kwa shilingi elfu kumi na kuongeza kuwa wanamuziki watakaoshiriki onyesho hili wamejipanga kutoa burudani kisawasawa na kukata kiu ya wapenzi wa muziki wote Nchini.

  Alisema tiketi za onyesho hilo zitauzwa katika vituo mbalimbali Nchini yakiwepo maduka ya Vodacom Tanzania,Pia zitapatikana  kupitia huduma ya M-Pesa,Katika kuwapunguzia washabiki usumbufu wa kupanga misururu ya kununua tiketi za onyesho hilo pia zitauzwa kwa kupitia huduma ya M-Pesa bila kuwepo na makato yoyote ya kutumia huduma hiyo ambapo watakaonunua tiketi kwa huduma hiyo kutakuwepo na utaratibu maalumu wa kuingia kwenye onyesho cha muhimu ni kutunza namba zao za kumbukumbu ya mhamala wa malipo.Jinsi ya kujipatia tiketi kwa njia ya M-PESA mteja anatakiwa kupiga  *150*00# na kuchagua LIPA KWA M-PESA
  2.       Chagua MANUNUZI
  3.       Chagua JEMBEKA FESTIVAL
  4.       Weka namba ya kumbukumbu – 200200
  5.       Weka kiasi – 10,000
  6.       Weka Namba yako ya siri  na kwa wale wa tiketi za VIP namba ya kumbukumbu ni 200100 bila malipo yeyote yale.
  v Kwa msaada wa kununua tiketi, piga BURE namba 0800 71 0040

  0 0

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman

  JAJI MKUU wa Tanzania, Mohammed Chande Othman amesema sheria ya mitandao ilipitishwa kwa lengo jema la kulinda watumiaji, wanajamii na usalama wa Taifa la Tanzania.
  Ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Mei 14, 2016) wakati akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa Watanzania waishio Uingereza kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini London, Uingereza.
  Alisema watu watatu kati ya wanne nchini Tanzania wakiwemo watoto, wanamiliki simu za mkononi ambayo ni sawa na watu milioni 35 kati ya milioni 45.
  Alisema sheria hiyo ilitugwa kwa misingi mitatu moja ikiwa ni kumpa mtumiaji uhuru wa kutoa maoni au taarifa, uhuru ambao alisema unalindwa kikatiba lakini akaonya kuwa kila uhuru unaotolewa pia una mipaka yake kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 30(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Alisema sheria hiyo pia inatoa uhuru wa mtu kuwa na faragha (privacy) na msingi wa tatu ni sheria hiyo kuzingatia matumizi ya mitandao ili kulinda usalama wa nchi.
  “Sheria hii inakupa uhuru wa kutumia mtandao kumlinda mwanajamii wenzako. Hapa Uingereza nimeongea na mwendesha mashtaka mkuu ambaye aliniambia kuwa asilimia 60 ya makosa yanayofanyika chini ya sheria ya makosa ya kujamiiana (Sexual Offencea Act) yanatokana na mitandao,” alisema Jaji Mkuu wakati akijibu swali kuhusu sheria ya makosa ya mitandao.
  Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga alisema kuitishwa kwa mkutano wa kupambana na rushwa nchini Uingereza ni mojawapo ya jitihada za Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuanzisha vuguvugu la uanaharakati wa mapambano dhidi ya rushwa.
  “Kukosekana kwa utawala bora, changamoto za ugaidi, biashara za dawa za kulevya, biashara ya kusafirisha binadamu na uwepo wa rushwa na ufisadi ni baadhi ya mambo yaliyofanya dunia ibadilike. Haya mambo zamani yalikuwa hayana mahali pa kuzungumzwa, kwa hiyo vikao kama hivi vitasaidia kukabili tatizo hili,” alisema.

  “Rushwa ni kama pweza mwenye vichwa vingi na mikia mingi. Waziri Mkuu David Cameron ameamua kuanzisha movement hii ili kutafuta njia za kukabili janga hili kubwa,” alisema.
  Sote tunatanbua kuwa mataifa mengi yangependa kuwemo katika hii movement lakini ni faraja kuona kwamba Tanzania imo miongoni mwa waanzilishi na hii ni kwa sababu ya uongozi nz ujasiri wa Rais Dk. John Pombe Magufuli ambaye kwa kweli ni game changer  (akimaanisha kuwa amebadili mwelekeo wa Taifa hili) kwani ana utashi wa kisiasa na ana ujasiri wa kukemea maovu,” alisema huku akishagiliwa.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola alisema vita ya rushwa nchini Tanzania ni endelevu na inafanyika kuitikia wito alioutoa Rais Magufuli wakati akizindua Bunge la Tanzania Novemba 20, 2015.
  Alisema wanatumia mbinu mbalimbali kupambana na rushwa lakini kubwa wanayoenda nayo hivi sasa ni kutoa elimu kwa watoto na vijana ili kuwabadilisha tabia na utamaduni uliojikita kwenye jamii.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMAPILI, MEI 15, 2016.

  0 0
  0 0

  Wanafunzi 42 wa mwaka wa tatu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanaosomea fani za Uhandisi Migodi na Uhandisi Uchenjuaji Madini, wakiambatana na wahadhiri wao walipata fursa ya kutembelea migodi ya dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi inayomilikiwa na kampuni ya uchimbaji ya Acacia.

  Katika ziara hiyo ya mafunzo iliyofanyika tarehe 11 na 12 mwezi huu, wanafunzi hao pamoja na wahadhiri wao walijionea shughuli za uchimbaji wa madini wa chini ya ardhi katika Mgodi wa Bulyanhulu (Underground mining) na uchimbaji wa juu wa ardhi (Open pit mining) katika Mgodi wa Buzwagi. Wanafunzi hao vilevile walipata fursa ya kujifunza namna ya uchenjuaji wa dhahabu katika migodi yote miwili.

  Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia ina Mkataba wa Makubaliano (MoU) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama sehemu ya mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii. Katika makubaliano hayo Acacia hufadhili ziara za mafunzo kwa wanafunzi wanaosomea fani za Uhandisi Migodi na Uhandisi Uchenjuaji Madini kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam kwa mwaka mara moja na kutoa fursa kwa wanafunzi hao ya kujifunza kwa vitendo kwa muda wa miezi miwili kila mwaka katika migodi yake.

  Kampuni ya Migodi ya Acacia ndio kampuni kubwa zaidi ya uchimbaji wa dhahabu nchini na inamiliki migodi mitatu ya Buzwagi na Bulyanhulu iliopo katika wilaya ya Kahama Shinyanga na ule wa North Mara uliopo Nyamongo mkoa wa Mara.
  Kundi la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliotembelea Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu wakielekea chini ya mgodi.
  Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakiwa katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu wakimsikiliza kwa makini Afisa Mafunzo wa Mgodi huo, Caroly Chundu wakati akitoa maelezo kuhusu maswala ya usalama kabla ya kuingia mgodini
  Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salam wakipata maelezo kutoka kwa Amos Mokoge, Mtaalam wa uchenjuaji katika kinu cha Uchenjuaji dhahabu kuhusu motor ya kinu cha Uchenjuaji wa dhahabu.
  Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Migodi Karim Mleli katika bwawa la tope visusu ambalo linatumika kuhifadhi maji yanayotoka kwenye mtambo wa kuchenjulia dhahabu katika mgodi wa Buzwagi.
  Wanafunzi waliotembelea Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa wa mgodi huo.

  0 0

  Wananchi na Wakazi wa Kata ya Kisesa, Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, mapema leo wamefunga barabara ya Mwanza-Musoma katika eneo la Kisesa na hivyo kusababisha abiria wanaoingia Jijini Mwanza kutoka Mikoani kukwama barabarani kwa zaidi ya saa moja.
  Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi

  0 0


  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  WADAU wa ardhi, mazingira na mambo ya misitu wanaojulikana kama Maisha Shamba Group wameweka adhma ya kupanda miti milioni 50,000,000 ifikapo mwaka 2020, ikiwa ni mipango yao ya kutunza mazingira na kujikwamua kiuchumi kwa kupitia sekta ya misitu nchini.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, akizungumza jambo katika mkutano wa wanachama wa Maisha Shamba Group wanaojihusisha na mambo ya misitu na mazingira mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Hayo yamesemwa na kiongozi mkuu wa group hilo, Asifiwe Malila, alipokuwa akizungumza na wanachama wake katika mkutano wao wa mwaka, huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, mwishoni mwa wiki, katika Ukumbi wa Shule ya Sheria Tanzania, jijini Dar es Salaam.
  Mdau wa mambo ya ardhi na misitu, Ally Abdallah, akisikiliza kwa makini hutuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, hayupo pichani katika mkutano wa wadau wa misitu wanaojulikana kama Maisha Shamba Group.


  Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, aliwapongeza wadau hao wa mambo ya misitu, akiwataka waendelee kubuni mambo yanayoweza kuwakwamua na kuisaidia nchi katika kutunza mazingira kwa kupitia sekta ya misitu.
  Mheshimiwa January Makamba wakati anaingia eneo la Mkutano huo. Kulia kwake ni mdau wa ardhi na misitu, Ally Abdallah.

  Akizungumzia adhma hiyo, Malila alisema lengo lao linatokana na kujidhatiti kujikwamua kiuchumi kwa kupitia misitu pamoja na utunzani wa mazingira, huku wanachama wote wa group hilo wakimiliki miti 14,000,000, katika wilaya mbalimbali nchini Tanzania.
  Wadau hao wa misitu wakifuatilia mkutano huo kwa umakini.


  “Kwa pamoja tuna mipango kabambe ya kuhakikisha kwamba tunajikita zaidi katika kilimo cha miti, mifugo kama njia ya kukuza uchumi wetu, ndio maana tumeamua kuungana kwa pamoja kushirikiana kwa hali na mali katika sekta hii muhimu,” alisema Malila, katika mkutano huo uliokuwa na lengo la kujadili muungano wao huo sanjari na kupitisha rasmi rasimu ya Katiba kama njia ya kusajili jumuiya kwa ajili ya kujiwekea malengo ya juu kisheria.
  Mheshimiwa January Makamba akizungumza na wadau hao wa misitu, ardhi na mazingira.  Makamba alisema serikali itashirikiana na wadau hao wa misitukwa nguvu zote, huku akiwataka washirikiane na viongozi wao, wakiwamo wabunge, ikiwa ni hatua nzuri ya wizara yake kujiandaa kupeleka muswada wa mabadiliko ya sheria ya mazingira, kuuboresha mfuko wa Taifa wa Mazingira, sanjari na kuuwekea ubora wa utendaji kazi wake, tangu ulipoanzishwa rasmi nchini Tanzania mwaka 2004.
  “Mwaka huu zimetengwa Sh Bilioni 2 kwa ajili ya Mfuko wetu wa Taifa wa Mazingira uweze kufanya kazi, ingawa mahitaji ni zaidi ya sh Bilioni 100, ambapo tunajaribu kutafuta mbinu za kuweza kuzipata fedha hizo kwa sababu mazingira ni jambo nyeti duniani kote, hivyo naamini serikali yetu itashirikiana na wadau wote ili nchi yetu ipige hatua.
  “Endapo tutakuwa na sera mpya, mabadiliko ya sheria pamoja na fedha, hakika yote tunayokusudia tutayafanya kwa wakati muafaka, sanjari na upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira ili sekta hiyo iweze kunufaisha nchi pamoja na wananchi wake, wakiwamo wadau wanaojihusisha na mambo ya mazingira kwa namna moja ama nyingine,” alisema Makamba.

  Aidha wanachama hao wa Maisha Shamba Group walitumia muda huo kumuomba Makamba na wizara yake kuweka utaratibu mzuri na rahisi kwa ajili ya wanachama hao wapewe mapori ya serikali ili wayaendeleze, mafanikio yao yarekodiwe, mashamba yao yapimwe na wataalamu wanaopatikana katika maeneo mbalimbali ya Tanzania, ili iwe njia ya kufanikisha adhma yao ya kuhakikisha kwamba sekta hiyo inapiga hatua nchini.

older | 1 | .... | 1220 | 1221 | (Page 1222) | 1223 | 1224 | .... | 3270 | newer