Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

WHO NA JUMUIA YA ALYAMIN WATOA VIFAA VYA KUCHUNGUZIA MAJI NA MAJI YA KUNYWA KATIKA JUHUDI ZA KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU ZANZIBAR.

$
0
0
MWENYEKITI wa Jumuia ya Alyamin Dkt. Omar Swaleh akimkabidhi Waziri  wa Afya Mahmoud Thabit Kombo Msaada wa Maji na vidonge vya kutibu maji ya kunywa kwa ajili ya wagonjwa wa kipindupindu, (kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Juma Malik Akili. 
MWAKILISHI wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Andemichael Ghirmay, akizungumza na Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo alipofika ofisini kwake kukabidhi Vifaa vya kuchunguzia Maji.
MWAKISHI wa WHO Zanzibar Dkt. Andemichael Ghirmay akimkabidhi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo moja ya Vifaa vya kuchunguzia Maji katika hafla ilioyofanyika Wizara ya Afya Mnazi mmoja mjini Zanzibar.
MTAALAMU wa Maji wa WHO Michael Habtu, akikifanyia majaribio kifaa cha kuchunguzia maji huku Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiangalia kwa furaha.
MTAALAMU wa Maji kutoka WHO Michael Habtu, akiwaonesha matokeo ya Maji alioyapima kwa kifaa cha kuchunguzia maji huku Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiangalia, wakwanza (kulia ) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili na Mwakilishi wa WHO Dkt. Andemichael Ghirmay
SHEHENA ya Msaada wa Maji ya kunywa uliotolewa na Jumuia ya Alyamin kwa ajili ya wagonjwa wa kipindupindu Zanzibar.
 

PICHA NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

TAASISI ZA SERIKALI ZILIZOUNGANISHWA NA MFUMO WA ITIFAKI YA INTANETI ZATAKIWA KUTUMIA HUDUMA HIYO KUPUNGUZA GHARAMA YA MAWASILIANO.

$
0
0

Mtaalam wa TEHAMA katika moja ya Ofisi za Serikali akiwa kazini.

………………………
Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.

Serikali kupitia Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) imezitaka taasisi zote zilizounganishwa kwenye mfumo wa simu zenye itifaki ya intaneti (Internet Protocol (IP) ambazo zinatumia intaneti kuzitumia simu hizo katika mawasiliano yao kila siku ili kuboresha utendaji kazi na kupunguza gharama za mawasiliano Serikalini.

Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bi. Suzan Mshakangoto amesema kuwa Serikali imeamua kusisitiza matumizi ya simu hizo ili kuziwezesha taasisi za Serikali kuwa na mawasiliano yaliyo bora, salama na kupunguza gharama za mawasiliano.

Amesema kuwa Serikali kupitia Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) imeunganisha taasisi za Serikali 72 ambazo zinajumuisha Wizara, Idara zina zojitegemeana na Wakala za Serikali na kuongeza kuwa taasisi hizo zimeunganishwa na Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali yaani ‘Government Communication Network (Govnet)’ unaowezesha mfumo wasimu hizo kufanya kazi kwa ufanisi.

“ Kupitia mfumo wa simu hizi zenye itifaki ya intaneti mtumishi wa taasisi iliyounganishwa anaweza kupiga simu kwenda taasisi nyingine ya nje ikawa kama amepiga simu ya ‘extension’ ndani ya ofisi moja” Amesema Bi. Suzan.

Aidha, amesema Taasisi za umma zitanufaika moja kwa moja na simu hizo kwa kuwa, taasisi hizo zitaweza kubadilisha na taarifa kupitia mtandao mmoja tuwa Mawasiliano wa Serikali kwa usalama na uhakika. Pia simu hizo zitawawezesha watumishi wa taasisi mbalimbali kufanya mkutano kwa njia ya simu wakiwa kwenye ofisi zao na hivyo kuokoa muda na gharama za usafiri.

Hata hivyo amesema taasisi za umma zilizopo katika mtandao wamawasiliano wa Seikali zitaendelea kuwasilia na na taasisi zilizo nje ya mtandao huo kwa kupitia mtoa huduma wa simu za mezani (PSTN Provider) kama vile TTCL.

Rais Magufuli afanya ziara ya ghafla Uwanja wa Ndege JNIA Leo

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja dhidi ya dosari za ukaguzi zilizopo katika kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (Terminal One) Jijini Dar es salaam.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 13 Mei, 2016 alipofanya ziara ya kushtukiza katika uwanja huo na kubaini kuwa mashine za ukaguzi za sehemu ya kuwasili abiria na mizigo hazifanyi kazi kwa muda mrefu.

Maafisa wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere waliokuwa wakitoa maelezo juu ya hali ya kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja huo, walikuwa wakitoa taarifa zinazotofautiana kuhusu utendaji kazi wa mashine za ukaguzi, hali iliyosababisha Dkt. Magufuli aamue kuiagiza wizara husika kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja.

"Unajua mimi sipendi kudanganywa, ni vizuri uzungumze ukweli tu, kwa nini nimeanzia hapa huwezi ukajiuliza? eeeh sasa sipendi kudanganywa, ukinidanganya nitachukia sasa hivi, wewe umenidanganya kwamba hiyo ndio mbovu na hii ndio nzima, nikawaambia muiwashe hiyo nzima, akaja huyu mwenzako amezungumza ukweli kabisa, akasema hii ni mbovu kwa miezi miwili. Dkt. Magufuli aliwahoji Maafisa wa uwanja wa ndege.

"Kwa hiyo mizigo inayoingia humu huwa hamuikagui kwa namna yoyote ile, kwa hiyo mtu nikiamua kuja na madawa yangu ya kulevya, nikaja na dhahabu zangu, na almasi zangu na meno ya tembo kwa kutumia hizi ndege ndogondogo napita tu" Rais Magufuli aliendelea kuwabana maafisa hao wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. 

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara hii ya kushtukiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Jijini Kampala nchini Uganda ambako jana alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
13 Mei, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mashine ya ukaguzi wa mizigo katika sehemu ya kuwasili abiria ya uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, upande wa uwanja wa zamani (Terminal One) wakati wa ziara yake ya ghafla aliyoifanya Ijumaa tarehe 13 Mei, 2016. Kulia kwa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda na kushoto ni Kaimu Meneja uendeshaji Lilian Minja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuuliza maswali Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha, kuhusu dosari zilizopo katika mashine za kukagulia mizigo ya wageni wanaowasili kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, upande wa uwanja wa zamani (Terminal One)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwabana maswali maafisa wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuhusu dosari ya kutofanya kazi kwa mashine za ukaguzi katika sehemu ya kuwasili abiria ya uwanja wa zamani (Terminal One)
.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI MBALIMBALI LONDON NCHINI UINGEREZA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa wa Uingereza (Minister of State for International Development) , Justine Greening katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje , Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki,Kikanda naKimataifa, Augustine Mahiga na watatu kushoto ni Jaji Mkuu,Mohamed Othman.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (kulia) wakizungumza na Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika London Uingereza, May12, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Norway,Erna Solberg katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg (kulia) katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika  kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016. anne  kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman na watatu kushoto ni  Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika `Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI YAPATA BILIONI 1.71 KUTOKANA NA MAONESHO YA VITO JIJINI ARUSHA.

$
0
0
Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa madini Tanzania (TAMIDA) iliendesha Maonesho ya tano ya Kimataifa ya Madini ya Vito yaliyofanyika Jijini Arusha katika Hoteli ya Mount Meru kuanzia tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016. Maonesho haya hufanyika kila mwaka Jijini Arusha na hukutanisha washiriki mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wachimbaji, Wafanyabiashara wa madini ya vito wa ndani na nje, wanunuzi wa madini wa ndani na nje, na wataalam mbalimbali wenye uzoefu wa shughuli za madini ya vito. 

Maonesho hayo yalihudhuriwa na washiriki 813 kutoka katika nchi 26 duniani ambazo ni Tanzania Marekani, Sri Lanka, India, Kenya, China, Ujerumani, Namibia, Australia, Austria, Israel, Italia, Uingereza, Hong Kong, Switzerland, Zambia, Madagascar, Afrika Kusini, Msumbiji, Urusi, Cameruni, Canada, Malawi, Sudani, Malta, na Thailand). Aidha, wanunuzi (buyers) wa madini walikuwa 353, Walioshiriki kuonesha madini kwenye mabanda (Exhibitors) 300, na wageni mbalimbali 160.

Lengo kubwa la Maonesho haya ni kama ifuatavyo: kufanya Arusha kuwa kitovu cha madini ya vito katika Afrika ili hatimaye iwe ni kitovu cha biashara ya madini hayo; fursa ya masoko kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa mdini ya vito nchini; na kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini ya vito hapa nchini.

Katika maonesho hayo, madini yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 4.5, sawa na Shilingi Bilioni 9.9 yaliuzwa.

Serikali ilipata jumla ya Shilingi bilioni 1.71, ambapo Shilingi bilioni 1.3 zilitokana na mnada wa madini yaliyokamatwa na kutaifishwa na Serikali, Shilingi milioni 388 zilitokana na mrabaha uliolipwa kutokana na madini yaliyonunuliwa, na Shilingi milioni 26 zilitokana na vibali vya kusafirisha madini nje ya nchi.

Manufaa mengine yaliyopatikana wakati wa maonesho ni pamoja na wageni kuingiza fedha za kigeni hapa nchini ambazo hutumika kwa ajili ya malazi, usafiri, chakula na kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii hapa nchini.

Ili kuweka utaratibu utakaodhibiti shughuli za madini ya vito hususani tanzanite, Serikali inakusudia kuanzisha minada ya ndani mbali na mnada unaofanyika wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Vito Jijini Arusha. Minada hiyo itatoa fursa kwa wafanyabishara wa ndani kununua madini kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani madini hayo na kutengeneza vidani mbalimbali. 

Ili kuimarisha shughuli za uongezaji thamani madini ya vito nchini, Serikali inakusudia kuimarisha Kituo cha Jimolojia kilichoko Arusha (Tanzania Gemmological Centre -TGC) ili kufundisha na kuzalisha vijana wa Kitanzania wa kutosha wenye ujuzi wa kusanifu na kung’arisha madini ya vito. Tayari vijana 29 wameshapata mafunzo ya miezi 6 ya ukataji wa madini ya vito kutoka kwenye kituo hicho tangu 2014. Wanafunzi wengine 18 wanaendelea na mafunzo ya miezi 6 yaliyoanza mwezi Machi, 2016.

Aidha, upo mpango wa kuanzisha EPZ eneo la Merelani ambapo ni karibu na machimbo ya tanzanite kwa lengo la kupata eneo maalum ambapo shughuli za biashara ya madini na uongezaji thamani madini ya tanzanite zitafanyika kwa uhuru na wazi. Pamoja na juhudi zote hizo, Serikali itaendelea kudhibiti vitendo vya utoroshaji wa madini mbalimbali nje ya nchi ikiwemo Tanzanite kwenye viwanja vya ndege na kwenye migodi ambapo madini yanazalishwa. 

Wito wa Serikali ni kuwataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuzingatia sheria zilizopo wakati wa kufanya shughuli zao.

Imetolewa na;
KAIMU KAMISHNA WA MADINI
MHANDISI ALLY SAMAJ
Kaimu Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ally Samaje akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu Tathmini ya maonesho ya tano ya kimataifa ya madini ya vito yaliyofanyika Jijini Arusha mwezi April mwaka huu yaliyohudhuriwa na washiriki 813 kutoka nchi 26 duniani. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo Bi. Asteria Muhozya.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huoPICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

VOA: Zulia Jekundu S1 Ep 76: Justin Bieber, Lamar Odom, Mila Kunis, 50 Cent, Tom Hardy, Blac Chyna

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

1 of 169 Print all In new window MKONGWE WA DANSI NCHINI, ZAHIR ALLY ZORO ATAKA MUZIKI WA DANSI KUFUFULIWA MKOANI MWANZA

$
0
0
Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa dansi nchini Tanzania, Zahir Ally Zorro (Kushoto) akizungumza na George Binagi @BMG (Kulia).

Mwanamuziki mkongwe wa dansi nchini, Zahir Ally Zorro, amewahimiza wadau wa muziki wa dansi Mkoani Mwanza, kuwaunganisha wanamuziki wa muziki huo ili kuurudisha kwenye chati kama zamani.

Alitoa kauli hiyo jana Jijini Mwanza, wakati akizungumza na BMG, ambapo alisema muziki wa dansi nchini umepotea sokoni hivyo jitihada zote zinafanyika ili kuurudisha katika soko, akitolea mfano Mkoani Mwanza ambapo kuna uhaba wa band za muziki wa dansi.

"Muziki wa dansi upo na tunajitahidi kuurudisha katika soko. Mwanza kuna vijana wengi wanafanya muziki wa dansi, wanaposhindwa kusikilizwa na media inauma sana hivyo ni vyema wakaunganishwa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya muziki wa Mwanza". Alisema Zorro.

Mbali na hayo, Zorro ambae alianza muziki tangu mwaka 1968, yuko Jijini Mwanza kikazi ambapo leo jumamosi May 14,2016 atakuwa na show kali ndani ya Kilimanjaro Club iliyopo Nyegezi, atakapokuwa akinyukana na wenyeji wake Twiga Band.
Picha na Iman Hezron

BLOGGERS WATINGA BUNGENI KWA MWALIKO WA WAZIRI NAPE

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (aliyevaa tai) akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa Blogs (Bloggers) aliowaalika wakati wa kuwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha wa 2016/2017, bungeni Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Annastazia Wambura. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Baadhi ya Bloggers wakiwa bungeni wakati wa Bajeti ya wizara hiyo
Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’ akisoma taarifa ya maoni ya upinzani kuhusu wizara hiyo.
Baadhi ya Bloggers wakisikiliza mwenendo wa bunge. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Muda wa Chama cha Wamiliki wa Blogs Tanzania a.k.a Tanzania Bloggers Network (TBN), Bw. Joachim Mushi.
Nape akiwa na Bloggers pamoja na wasanii bungeni Dodoma

RAIS DKT. MAGUFULI AONDOKA KAMPALA KUREJEA NCHINI TANZANIA, AAGWA KWA NDEREMO KAMPALA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Kikundi cha ngoma za asili cha Entebbe nchini Uganda wakati akiondoka kurejea nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita mbele ya gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili ya kumuaga katika uwanja wa ndege wa Entebe wakati akiondoka kurejea nyumbani Tanzania.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa makofi na baadhi ya  viongozi mbalimbali wakati alipowasili kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa Viongozi wakuu wanchi mbalimbali siku walipowasili Kampala nchini Uganda.
Waandishi mbalimbali wa Habari kutoa nchi tofauti wakiwa na shauku ya kupata picha ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni zilizofanyika kwenyeuwanja wa Uhuru wa  Kololo, Kampala nchini Uganda. Katika Picha hiyo Rais Dkt. Magufuli alikuwa akizungumza na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. 
Picha na IKULU.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA UWANJA WA NDEGE DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja dhidi ya dosari za ukaguzi zilizopo katika kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (Terminal One) Dar es salaam.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 13 Mei, 2016 alipofanya ziara ya kushtukiza katika uwanja huo na kubaini kuwa mashine za ukaguzi za sehemu ya kuwasili abiria na mizigo hazifanyi kazi kwa muda mrefu.

Maafisa wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere waliokuwa wakitoa maelezo juu ya hali ya kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja huo, walikuwa wakitoa taarifa zinazotofautiana kuhusu utendaji kazi wa mashine za ukaguzi, hali iliyosababisha Dkt. Magufuli aamue kuiagiza wizara husika kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja.
“Unajua mimi sipendi kudanganywa, ni vizuri uzungumze ukweli tu, kwa nini nimeanzia hapa huwezi ukajiuliza? eeeh sasa sipendi kudanganywa, ukinidanganya nitachukia sasa hivi, wewe umenidanganya kwamba hiyo ndio mbovu na hii ndio nzima, nikawaambia muiwashe hiyo nzima, akaja huyu mwenzako amezungumza ukweli kabisa, akasema hii ni mbovu kwa miezi miwili."Dkt. Magufuli aliwahoji Maafisa wa uwanja wa ndege
“Kwa hiyo mizigo inayoingia humu huwa hamuikagui kwa namna yoyote ile, kwa hiyo mtu nikiamua kuja na madawa yangu ya kulevya, nikaja na dhahabu zangu, na almasi zangu na meno ya tembo kwa kutumia hizi ndege ndogondogo napita tu” Rais Magufuli aliendelea kuwabana maafisa hao wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara hii ya kushtukiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Jijini Kampala nchini Uganda ambako jana alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

DONDOO ZA MAGAZETI LEO.

LUHWAVI AWASILI TANGA LEO, ASIKILIZA MAFANIKIO NA KERO ZA WAFANYAKAZI WA CCM WILAYA ZOTE ZA MKOA HUO

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akisalimiana na Kada wa CCM, Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Tanga, Shija Othman
Vijana wa Umoja wa CCM mkoa wa Tanga, wakimfanyia mapokezi maalum, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo.
Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Tanga, akila kiapo cha utiifu wakati walipomfanyia mapokezi rasmi Katibu Mkuu wa CCM- Bara, Rajabu Luhwavi, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo. 
Kijana wa wa UVCCM, Mwanakombo Mwakulo akimvisha Skafu Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara, Rajab Luhwavi, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo. Kulia ni kada wa CCM Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella.
 

MTAA KWA MTAA YA MICHUZI TV NA BEI YA MCHELE,VIAZI,NDIZI,MAHINDI NA MAHARAGE KWA SASA JIJINI MBEYA.

WIZARA KUPIMA VIWANJA 2180 CHASIMBA

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho-MAELEZO

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeazimia kupima jumla ya viwanja 2180 katika Kijiji cha Chasimba,wilayani Kinondoni baada ya kuisha kwa mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na Kiwanda cha Saruji (Twiga Cement).

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Usanifu wa Miji wa Wizara hiyo, Bi.Immaculata Senje alipokuwa akifafanua juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu kukosa huduma za umeme na maji katika eneo hilo.“Baada ya kupatikana kwa suluhisho la mgogoro huu, zoezi la upimaji viwanja linaendelea ambapo hadi sasa tumeshapima jumla ya viwanja 370 kati ya viwanja 2180 vinavyotarajiwa kupimwa kwenye Kijiji hicho,”alisema Bi Senje.

Bi Senje aliongeza kuwa kazi ya kupima viwanja hivyo ilianza mwezi Agosti mwaka jana baada ya Wizara kuunda timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ili waweze kutambua mipaka ya eneo kwa ajili ya kuweka miundombinu.

Aidha, Bi. Senje amesisitiza kuwa wananchi wawe wavumilivu kwani huduma za miundombinu kama vile maji, umeme na barabara zitawekwa baada ya upimaji wa viwanja hivyo kukamilika.Mgogoro huo ulimalizika mnamo Juni 13 mwaka jana baada ya uongozi wa Wizara kuweka kikao na uongozi wa Kiwanda cha Saruji pamoja na wananchi wa Chasimba ambapo uongozi wa Kiwanda ulikubali kuachia sehemu ya ardhi ambayo ilishaendelezwa na wakazi wa eneo hilo kwa makubaliano ya kupewa fidia na Wizara.

YANGA YAWAKUNA MASHABIKI WAKE,WAIBUKA NA KOMBE LA LIGI KUU MSIMU WA 2015/2016

$
0
0

KOMBE LATUA JANGWANI: Chereko na nderemo uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati Waziri wa Kilimo Mwigulu Nchemba akiikabidhi Yanga Kombe la Ligi Kuu. Huu ni ubingwa wa 26.Yanga walikabidhiwa kombe hilo na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh Mwigulu Nchemba, ambae ndie alikuwa mgeni rasmi.

TANZANIA KUSHIRIKIANA NA JUMUIYA YA MADOLA – MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Jumuiya ya Madola inaweza kuiga mbinu ambazo Tanzania imetumia katika kupambana na rushwa zikiwemo za kujumuisha wadau tofauti kwenye vita hiyo.

Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Bibi Patricia Scotland walipokutana kwenye mkutano wa kimataifa uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.

“Tanzania iko tayari kushirikiana na ninyi katika kujenga timu hii na ili uweze kupata picha halisi, nakukaribisha Tanzania uje ujionee hatua ambazo tumechukua hadi kufikia hapa tulipo kwenye vita hii dhidi ya rushwa,” alisema Waziri Mkuu ambaye alihudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Alimweleza Katibu Mkuu huyo kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kupambana na rushwa kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa wananchi. “Wananchi wanafurahia juhudi za Serikali, vyama vya kiraia pia vinaunga mkono jitihada zetu na vyombo vya habari vinashirikiana nasi katika vita hii,” alisema.

Waziri Mkuu alitoa wito huo baada ya kuelezwa na Bibi Scotland kwamba anataka kuanzisha idara malum kwenye Jumuiya hiyo ambayo itasimamia mapambano dhidi ya rushwa na makosa ya jinai.

“Nataka tuwe na idara yenye watu mahiri wa idara za uhasibu, mahakama yenyewe ikiwemo waendesha mashtaka na wanasheria kutoka kwenye nchi kadhaa ili washirikishane uzoefu kutoka kwenye nchi zao. Ninaamini katika nchi 53 ambazo ni wanachama wetu, sitakosa watu wa aina hii,” alisema.

Alisema ameamua kufanya hivyo ili aweze kuendanana na malengo makuu matatu ya jumuiya hiyo ambayo ni kupiga vita rushwa, kuhimiza utawala bora na usimamizi wa demokrasia.

IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU

JUMAMOSI, MEI 14, 2016.

WAZIRI MKUU MAJALIWA: MAPAMBANO YA RUSHWA YANAHITAJI JUHUDI ZA PAMOJA

$
0
0


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mkutano wa kimataifa uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani ni kiashiria tosha kwamba tatizo la rushwa ni kubwa sana na linataka juhudi za pamoja katika kukabiliana nalo. (It’s a serious graft that needs concerted efforts).

Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Waziri wa Nchi wa Uingereza anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa, Bibi Justine Greening walipokutana kwenye mkutano huo uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.

Waziri Mkuu ambaye alihudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, alimweleza Bibi Greening kwamba viongozi wa Serikali wa awamu ya tano wameamua kwa dhati kupambana na kila ovu linalotokana na janga la rushwa na pia wameamua kuwajibika na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.

“Sasa hivi nchi yetu ina utamaduni mpya wa kufanya kazi na tumeamua kufanya kazi kwelikweli na siyo tena kwa mazoea, tumeamua kuweka utamaduni mpya wa kupiga vita rushwa ili kuleta uwajibikaji na uwazi miongozi mwa watu wetu,” alisema.

Alipoulizwa ni kitu kimechangia kufanya Tanzania ing’are kimataifa katika vita hii, Waziri Mkuu alijibu kwamba Tanzania imetumia mambo manne ambayo ni kuzuia rushwa isitolewe ama kupokelewa (prevention), kampeni za kuelimisha jamii, kufanya mapitio ya sheria na kuwepo kwa utashi wa kisiasa.

“Serikali inachukua hatua za kiutawala na kisheria kama vile kuanzisha mahakama maalum ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi mwezi Julai mwaka huu,” alisema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake, Bibi Greening alipongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kupambana na rushwa na kwamba ndiyo maana Tanzania ilipewa mwaliko maalum wa kushiriki mkutano huo kwa vile baadhi ya mataifa yanaziona juhudi zinazofanywa na Serikali.

Pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Mkuu kwa nia ambayo Serikali ya awamu ya tano imeionyesha katika kuwa na mpango wa kuendeleza viwanda.

Pia alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba nchi yake iko tayari kuisaidia Tanzania kwenye mpango wake ilionao wa kupeleka umeme vijijini (Rural Electrification Programe). “Tuko tayari kuwasiidia kutekeleza mpango huu kupitia taasisi ya Energy Africa Initiative ambayo inapata ufadhili kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID),” alisema.

Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya kimataifa, Bibi Sarah Sewall ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua katika mapambano dhidi ya rushwa na kusisitiza kwamba makampuni mengi ya Marekani yana nia ya kuja kuwekeza Tanzania.

“Ninaamini uwekezahji huu utasaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa watu wetu. Tunampongeza Rais Dk. Magufuli kwa juhudi anazofanya na nipende kusisitiza kwamba ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani utaendelezwa katika maeneo yetu ya siku zote,” alisema.

Waziri Mkuu alimshukuru Bibi Sewall na kumsisitiza asiache kusaidia kuwahimiza wamarekani wengi waje kutalii Tanzania na wawekezaji zaidi waje kuwekeza nchini katika nyanja mbalimbali zikiwemo uanzishaji wa viwanda, uongezaji thamani kwenye mazao yanayozalishwa nchini na kuhakiksha kuwa Watanzania wanajifunza teknolojia mpya na za kisasa.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAMOSI, MEI 14, 2016.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA KITUO CHA KISASA CHA HUDUMA ZA MAGARI MKOANI ARUSHA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Matairi ya Magari aina ya BF Goodrich KO2 yanayosambazwa na kampuni ya Superdoll baada kuwasili katika kituo cha kisasa cha huduma za magari na Matairi cha Superdoll mjini Arusha kwa ajili ya kuzindua rasmi kituo hicho. Kusshoto Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akibonyeza kitufe na kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif alipokua akizindua rasmi kituo cha kisasa cha huduma za magari pamoja na Matairi cha Superdoll mjini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif baada ya kuzindua rasmi kituo cha kisasa cha huduma za magari pamoja na Matairi cha Superdoll mjini Arusha.(Picha na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Saddik alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita. Katikati Mkuu wa Mkoa Arusha Mhe. Daud Felix Ntibenda.

UN YAIPONGEZA TANZANIA KWA UHARAKA WA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA

$
0
0

Na Mwandishi Maalum.

Umoja wa Mataifa  umeipongeza Tanzania  kwa namna  ambavyo imechukua hatua za haraka za kukabiliana na  tuhuma za udhalilishaji wa kijinsia zinazowahusisha baadhi ya  walinzi wa amani  wanaohudumu katika Misheni ya Kulinda Amani katika  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo( DRC)
“Tanzania  imeweza  ndani ya siku tano tangu kupokea tuhuma dhidi ya  walinzi wake wa amani kuunda   timu ya kitaifa ya uchunguzi kwajili ya kuzifanyika kazi tuhuma hizo.  Hatua hii na utashi ulioonyeshwa na Tanzania ni hatua nzuri na inayopashwa kupongezwa na inaonyesha namna gani inavyochukulia kwa uzito wa hali juu  tuhuma hizo”.

Pongezi hizo  zimetolewa  mwishoni wa wiki ( Ijumaa) na Bw. Atul Khare,  Naibu Katibu Mkuu  Mwandamizi anayeongoza Idara ya Field Support katika Umoja wa Mataifa.Mwishoni  mwa wiki ,  Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,   aliandaa mkutano  ambao ulikuwa na lengo la kutoa taarifa  ya maendeleo na  mwelekeo wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na  tuhuma za udhalilishaji wa kijinsia  zinazowakabili walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa,   walinzi wa Amani wa Kimataifa,  na wafanyakazi raia.

Katika  taarifa yake,Bw. Khare amesema, utaratibu uliopo unaitaka nchi ambayo walinzi wake wametuhumiwa kujihusisha na vitendo vya udhalilishaji pamoja na   hatua nyingine, kuunda timu yake ya  kitaifa ya uchunguzi ndani ya  siku kumi, lakini  Tanzania  iliunda timu hiyo ndani ya  siku tano  na kuanza kazi jambo ambalo amesisitiza linapashwa kuigwa na nchi nyingine.Akabainisha kwamba kinachosubiriwa sasa  kutoka Tanzania ni  taarifa rasmi ya kukamilishwa kwa uchunguzi huo na hatua ambazo zitakuwa zimechukuliwa kwa walinzi ambao watakuwa wamethibitika kujihusisha na vitendo hivyo.

Tuhuma  za udhalilishaji   wa kijinsia  dhidi ya  baadhi ya walinzi hao wa Amani wa Tanzania  ziliibuliwa na Umoja wa Mataifa  mwezi March mwaka huu.Akizungumza katika mkutano huo, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako  Manongi, amesema utovu wa nidhamu  uliofanywa na walinzi wachache hauwezi kuchafua kazi nzuri na sifa  ya kutukuka  ya  Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Misheni mbalimbali za kulinda Amani chini ya Umoja wa Mataifa.

Akasema  Balozi, ni kwa kutambua  kazi hiyo ya kutukuka na  ambayo pia imepelekea  baadhi ya wanajeshi wa Tanzania kupoteza maisha yao kishujaa wakati wakiwasaidia wananchi wa mataifa mengine kuwa na amani. Tanzania inalichukulia kwa uzito  wa  kipekee   tuhuma za udhalilishaji wa  kijinsia na kwamba wale wote wataokabainika  hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Akaongeza kwamba Tanzania  imeamua kuwaalika wataalamu  kutoka Umoja wa Mataifa kwenda nchini Tanzania  ambapo watashirikiana na wakufunzi wa JWTZ katika kuimarisha mitaala ya ufundishaji inayohusiana na  masuala ya ulinzi wa raia hususani eneo la udhalilishaji wa  kijinsia.

Vilevile Balozi Manongi amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na  Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha kwamba vitendo  hivyo  viovu  dhidi ya raia wasiokuwa na hatia vinakomeshwa ili pamoja na  mambo mengine kurejesha heshima ya  Umoja wa Mataifa na heshima ya nchi zinachochangia  wanajeshi  na polisi katika misheni za kulinda Amani. Lakini kubwa zaidi  kurejesha imani kwa wananchi wanaohitaji ulinzi.

Akielezea kwa ujumla kuhusu kadhia hiyo ya udhalilishaji wa kijinsi, Bw. Khare amesema, nchi nyingine  zinazochangia  walinzi wa Amani  na ambazo  pia  walinzi wao wametuhumiwa   zinaendelea  ushirikiano kwa kuchukua hatua mbalimbali ingawa pia zipo  zinazosuasua. Nchi ambazo zimetoa ushirikiano  ukiacha Tanzania ni Afrika ya Kusini, DRC, Misri na Bangladesh
Amezitaja  hatua hizo kuwa ni pamoja na  kuwafikisha katika mahakama za kijeshi wale wanaokutwa na hatia, kufungwa,  kufukuzwa kazi na kutoshiriki kabisa katika misheni za  kulinda Amani na kutoa misaada kwa  wahanga.

Akaongeza pia kwamba nchi  nyingi  zimeimarisha mitaala ya ufundishaji kwa walinzi wa amani, kuandaa timu za  uchunguzi ambazo zinakuwa tayari wakati wowote  zitakapohitajika, huku nyingine  zikihakikisha kwamba zinakuwa na wataalamu  wa  masuala  ya  sheria miongoni mwa walinzi wa Amani. 

Bw. Khare amesisitiza Umoja wa Mataifa unatambua mchango mkubwa wa walinzi wa Amani pamoja na mazingira magumu ya utekelezaji wa mamlaka  yao. Hata hivyo anasema vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia havipashwi kuvumiliwa wala kufumbiwa  macho na kwamba kila nchi inaowajibu wa kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria  watuhumiwa wanaothibitika  kuhusika na  ukatili huo na kwamba  ushirikiano na misaada  kwa waathirika ni jambo la muhimu sana.
 Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza wakati wa mkutano  wa kupokea taarifa  kuhusu  jitihada zinazofanywa na Umoja wa Mataifa za kukabiliana na  tuhuma za  udhalilishaji wa kijinsia katika misheni za kulinda amani. Katika  mchango wake Balozi amesema Tanzania  haitawavumilia walinzi wa amani  wachache ambao wanaharibu kazi nzuri na sifa ya  kutukuka ya  JWTZ katika Misheni za Kulinda Amani za Umoja wa Mataifa. Na kwamba wale watakaothibitishwa kujihusisha na  tuhuma hizo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.
Naibu  Katibu Mkuu Mwandamizi, Bw. Atul Khare akitoa taarifa kuhusu mwelekeo na hatua zinazochukuliwa kukabiliana na  vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia. katika taarifa yake ameipongeza  Tanzania  kwa namna ambayo iliitikia kwa haraka wito wa kuunda timu ya kitaifa ya uchunguzi ndani ya  siku tano  badala ya siku kumi kama taratibu zinavyoainisha na kwamba hatua hiyo ya  Tanzania  inapashwa kuigwa na  nchi nyingine.
 
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images