Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1218 | 1219 | (Page 1220) | 1221 | 1222 | .... | 3270 | newer

  0 0
  0 0

   Mkuruzenzi wa Kliniki ya Meno ya ABC ya Jijini Dar es Salama, Dr. Gombo Felician (kulia) akizungumza na wanafunzi wapatao (71) wa  Shule ya Msingi Fedha ya Kawe, kabla ya kufanyiwa uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno bure , ikiwa ni moja ya wanafunzi hao kutembelea kliniki hiyo kwa  kujifunza jinsi ya utunzaji wa kinywa na meno na kuwapa hamasa ya kupenda Udaktari na kati ya  wanafunzi 71, wanafunzi 45 wamekutwa na matatizo ya kinywa na wengine meno yamezibwa. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
   Mmoja wa wanafunzi hao akifanyiwa uchunguzi wa Kinywa na Meno
   Rehema Mgaya, ambae ni Mwalimu alieongozana na wanafunzi hao akifanyiwa uchunguzi wa kinywa na Meno ambapo amefurahishwa na huduma hiyo na kuwaomba waalimu wengine na Taasisi kuwapeleka wanafunzi na hata wafanyakazi kufanya uchunguzi kila mara wa Afya ya Kinywa na Meno kwa kutembelea Kliniki hiyo.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye Uwanja wa Kololo jijini Kampala kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
   Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo.  
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassani Mwinyi kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Rais Mstaafu Mwinyi alihudhuria pia sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Rais Mstaafu Kikwete pia alihudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wa mataifa mbalimbali katika viwanja vya Kololo jijini Kampala.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa viongozi wa dini wa Taifa la Uganda katika viwanja vya Kololo jijini Kampala. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Picha na IKULU


  0 0


  0 0

  Wanafunzi 42 wa mwaka wa tatu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanaosomea fani za Uhandisi Migodi na Uhandisi Uchenjuaji Madini, wakiambatana na wahadhiri wao walipata fursa ya kutembelea migodi ya dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi inayomilikiwa na kampuni ya uchimbaji ya Acacia.

  Katika ziara hiyo ya mafunzo iliyofanyika tarehe 11 na 12 mwezi huu, wanafunzi hao pamoja na wahadhiri wao walijionea shughuli za uchimbaji wa madini wa chini ya ardhi katika Mgodi wa Bulyanhulu (Underground mining) na uchimbaji wa juu wa ardhi (Open pit mining) katika Mgodi wa Buzwagi. Wanafunzi hao vilevile walipata fursa ya kujifunza namna ya uchenjuaji wa dhahabu katika migodi yote miwili.

  Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia ina Mkataba wa Makubaliano (MoU) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama sehemu ya mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii. Katika makubaliano hayo Acacia hufadhili ziara za mafunzo kwa wanafunzi wanaosomea fani za Uhandisi Migodi na Uhandisi Uchenjuaji Madini kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam kwa mwaka mara moja na kutoa fursa kwa wanafunzi hao ya kujifunza kwa vitendo kwa muda wa miezi miwili kila mwaka katika migodi yake.

  Kampuni ya Migodi ya Acacia ndio kampuni kubwa zaidi ya uchimbaji wa dhahabu nchini na inamiliki migodi mitatu ya Buzwagi na Bulyanhulu iliopo katika wilaya ya Kahama Shinyanga na ule wa North Mara uliopo Nyamongo mkoa wa Mara.
  Kundi la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliotembelea Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu wakielekea chini ya mgodi.
  Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakiwa katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu wakimsikiliza kwa makini Afisa Mafunzo wa Mgodi huo, Caroly Chundu wakati akitoa maelezo kuhusu maswala ya usalama kabla ya kuingia mgodini
  Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salam wakipata maelezo kutoka kwa Amos Mokoge, Mtaalam wa uchenjuaji katika kinu cha Uchenjuaji dhahabu kuhusu motor ya kinu cha Uchenjuaji wa dhahabu.
  Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Migodi Karim Mleli katika bwawa la tope visusu ambalo linatumika kuhifadhi maji yanayotoka kwenye mtambo wa kuchenjulia dhahabu katika mgodi wa Buzwagi.
  Wanafunzi waliotembelea Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa wa mgodi huo.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO         
  VIWANGO VYA TOZO KWA WATUMIAJI WA DARAJA LA NYERERE 
  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na Wadau wa Sekta ya Usafiri imeidhinisha viwango vya Tozo kwa watumiaji wa Daraja la Kigamboni vitakavyoanza kutumika rasmi kuanzia Jumamosi tarehe 14 Mei, 2016. 

  vitakavyoanza kutumika rasmi kuanzia Jumamosi tarehe 14 Mei, 2016.

  S/NA

  AINA

  KIWANGO CHA TOZO

  1

  WATEMBEA KWA MIGUU

  HAWATALIPIA

  2

  WAENDESHA BAISKELI

  300/=

  3

  PIKIPIKI

  600/=

  4

  MIKOKOTENI

  1,500/=

  5

  GUTA

  1,500/=

  6

  BAJAJI

  1,500/=

  7

  MAGARI AINA YA SALOON

  1,500/=

  8

  PICK-UP HADI TANI 2

  2,000/=

  9

  STATION WAGON

  2,000/=

  10

  GARI LA ABIRIA WASIOZIDI 15

  3,000/=

  11

  GARI LINALOBEBA ABIRIA ZAIDI YA  15 – 29

  5,000/=

  12

  GARI LINALOBEA ABIRIA ZAIDI YA 29

  7,000/=

  13

  TREKTA LISILO NA TELA

  7,000/=

  14

  TREKTA LENYE TELA

  10,000/=

  15

  MAGARI YENYE UZITO ZAIDI YA TANI 2 – 7

  7,000/=

  16

  MAGARI YENYE UZITO ZAIDI YA TANI 7 – 15

  10,000/=

  17

  MAGARI YENYE UZITO ZAIDI YA TANI 15 – 20

  15,000/=

  18

  MAGARI YENYE UZITO ZAIDI YA TANI 20 – 30

  20,000/=

  19

  LORI AINA YA (SEMI – TRAILER)

  25,000/=

  20

  LORI LENYE TRELA

  30,000/=

  21

  MITAMBO

  40,000/=

  22

  MAGARI YENYE VIPIMO VISIVYO VYA KAWAIDA (ABNORMAL LOAD)

  75,000/=

   Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawaomba watumiaji wa Daraja la Nyerere na Umma kwa ujumla kuzingatia tozo hizi kwa kadri ilivyoelekezwa;  Aidha, watumiaji wa Daraja la Nyerere wanaaswa kuzingatia Sheria na Kanuni za Usalama barabarani kwa kutunza na kulinda miundombinu na mazingira ya daraja wakati wote.

  Imetolewa na:
  Eng. Joseph Nyamhanga
  Katibu Mkuu (Ujenzi), 
  11 Mei, 2016.

  0 0

  Mkurugenzi wa Kinga Jeshini, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Kanali Charles Emilio Mwanziva akiongea na mwandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani Luis Velarde wakati wa ziara ya waandishi hao katika zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
  Mtaalamu wa maabara katika zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo mkoani Tanga akiendelea na kazi ya kufanya vipimo vya malaria kwa kutumia vipimo vinavyotoa majibu kwa haraka (MRDT) ambayo majibu yake hutolewa baada ya dakika 15.Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakiwa tayari wamewasili Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Korogwe.
   

  0 0

  Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah akizungumza na wadau wa Habari kutoka Jukwaa laWahariri, TMF, Sikika, Baraza la Habari Tanzania, Jukwaa la Katiba na TAMWA.
  Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah akimsikiliza Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw DeusKibamba wakati alipokutana na wadau wa Habari Ofisini kwake.
  Katibu wa Jukwaa la Wahariri Bw Nevelle Meena akizungumza wakati wa Mkutano kati yaKatibu wa Bunge na wadau wa Habari.
  Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah akisalimiana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw Theophil Makunga wakati wa Kikao kati ya Katibu wa Bunge na wadau wa Habari.Picha na Ofisi ya Bunge

  0 0


  0 0


  Jana May 13,2016 Tanzania imeungana na Mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha "SIKU YA WAUGUZI DUNIANI" ambapo Kitaifa Maadhimisho hayo yamefanyika Mkoani Geita.

  Imeandaliwa na BMG

  Jijini Mwanza, Maadhimisho hayo yalifanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando ambapo huduma yaliambatana na huduma mbalimbali ikiwemo wananchi kuchagia damu.

  Katika Maadhimisho hayo, Wauguzi katika Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza, walihimiza zaidi kuondolewa kwa matabaka yaliyopo baina yao na Watendaji wengine wa afya wakiwemo Madaktari kwa kupewa thamani sawa hususani kuboreshewa maslahi yao ikizingatiwa kwamba hakuna huduma bora ikiwa Wauguzi pamoja na Madaktari watafanya kazi bila ushirikiano.

  Uongozi wa Hospitali hiyo ulikiri kwamba Wauguzi ni watu muhimu katika sekta ya afya na kwamba mahitaji yao yataendelea kuboreshwa zaidi ili kuendana na umuhimu wao.
  Kauli Mbiu; Maslahi Bora kwa Wauguzi, Vifaa Tiba vya Kutosha, Chachu ya Kutoa Huduma Bora kwa Wagonjwa/Wateja.
  Baadhi wa Wauguzi kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando wakiwa katika Maadhimisho ya Siku ya Manesi Duniani, ambapo waliiomba Hospitali hiyo kuondoa matabaka miongoni mwao na madaktari hususani kuboreshewa maslahi yao ikiwemo malipo ya muda wa ziada kazini kama ilivyo kwa Madaktari.
  Baadhi wa Wauguzi kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando wakiwa katika Maadhimisho ya Siku ya Manesi Duniani, ambapo waliiomba Hospitali hiyo kuondoa matabaka miongoni mwao na madaktari hususani kuboreshewa maslahi yao ikiwemo malipo ya muda wa ziada kazini kama ilivyo kwa Madaktari.

  0 0

  Assalaam Aleikhum,
  Updates za familia ya Ankal Issa Michuzi iliyopatwa na msiba wa kuondokewa na Mtoto wa Ankal, Maggid Muhidin (18),  aliyefariki Jumapili Mei 8, 2016 huko Durban, Afrika Kusini:

  Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa Mei 13, 2016 majira ya saa saba mchana kwa  ndege ya shirika la Emirates kupitia Dubai (kwa kukosekana kwa  ndege za moja kwa moja kuja nchini kutoka Durban). Mwili wa kijana wetu utapokelewa  uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere eneo la Cargo la Swissport, Jijini Dar es salaam.
  Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi saa 10  alasiri katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Taratibu  za kuandaa mazishi zitaanza  saa 4 asubuhi siku hiyo hiyo ya Jumamosi, nyumbani  kwa mama wa marehemu kota za Wazo Hill, Tegeta, ulipo msiba.

  NAMNA YA KUFIKA MSIBANI
  Ukitokea Tegeta Kibaoni kama unaelekea Kiwanda cha Cement cha Wazo Hill, mbele mkono wako wa kulia kuna Kanisa la KKKT na ukienda mbele tena kidogo, utaona Bar yenye uzio wa rangi ya njano ambao umeandikwa "Twiga Cement",  hapo pana bango linaloelekeza njia karibu na kituo cha Bajaji nje. Unaingia upande huo wa kulia mita 250 mbele unakata tena kulia, mita 70 mbele utakuta maturubai, ndipo msibani.

  Innalillah wa inna ilayhi raajiun
  -AMIN.

  0 0
 • 05/13/16--00:19: DONDOO ZA MAGAZETINI LEO.


 • 0 0

  Jumba la kifahari la mapumziko la Shirika la Ndege la Etihad Airways katika uwanja wa ndege wa Melbourne, Australia.

  Shirika la ndege la Etihad leo limefungua rasmi jumba jipya la kifahari kwa ajili ya kupumzikia abiria wake katika uwanja wa ndege wa Melbourne, Australia. Jumba hilo ni mahususi kwa kuwapatia abiria mazingira tulivu ambayo wanaweza kupumzika, kuongeza nguvu, kula, kufanya kazi au kuburudishwa kabla ya safari.

  Ni eneo ambalo limejawa na nuru ya asili yenye vioo tokea sakafuni hadi katika dari, inatoa mtazamo mpana wa eneo la kurukia ndege. Lina zaidi ya mita za mraba 800 yenye viti vya kukaa hadi kufikia wageni 133, ni nyumba ya kupumzika ya shirika la ndege la Etihad ambayo ni kubwa zaidi iliyoko nje ya Abu Dhabi.

  0 0

  JENGO la ghorofa 16 la mtaa wa Indira Ghandi lililokuwa likihatarisha maisha kutokana na kujengwa chini ya viwango. 

  Kufuaatia agizo la Waziri wa Ardhi,  Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi la kuvunja jengo hilo, jengo limekamilika kuvunjwa. Jengo hilo limevunjwa kufuatia pia kuanguka kwa jengo lingine lililokuwepo mita chache kutoka katika jengo hilo ambalo pia lilijengwa ghorofa 16 badala ya ghorofa nane. Jengo hilo liliporomoka na kusababisha vifo vya watu 34,  mwaka 2013.

  Hivi Karibuni Mhe. Lukuvi aliagiza kubomolewa kwa jengo hilo kufanyike ndani ya siku 90. Hatahivyo zoezi la ubomoaji limefanikiwa kukamilishwa kabla ya siku 50.
  Mhe Waziri William Lukuvi akiwa na wataalamu katika ufuatiliaji wa ubomoaji wa Jengo la ghorofa 16  la mtaa wa Indira Ghandi.
  Eneo palipokuwa na Jengo la ghorofa 16- Mtaa wa Indira Ghandi, baada ya kukamilika kwa ubomoaji.
  Mhe. Waziri William Lukuvi akifuatilia ubomoaji  wa jengo la mtaa wa Indira Ghandi ulivyokuwa ukiendelea .

  0 0

    Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Florence Temba (katikati)  akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika Idara ya Habari - MAELEZO mapema leo.Waandishi wa habari wakifuatilia mada. 
   Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa  Kazi  Bw. Micky Kiliba (kushoto) akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye kikao kilichofanyika Idara ya Habari - MAELEZO mapema leo.
   Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa  Kazi  Bi. Veila Shoo (kulia) akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye kikao kilichofanyika Idara ya Habari - MAELEZO mapema leo.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (kulia) wakizungumza na Waziri  Mkuu  wa Norway, Erna  Solberg katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika London Uingereza, May 12, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na  Waziri  Mkuu  wa Norway, Erna Solberg katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016.  Kulia ni  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri  Mkuu  wa Norway, Erna  Solberg (kulia) katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016.  Wanne kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman  na watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya  Ulaya na Amerika katika `Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine.

  0 0


  *Waziri Mkuu kukutana na Watanzania leo, atoa ufafanuzi kuhusu Diaspora

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema viongozi wakuu wa nchini na washiriki wa mkutano wa kimataifa wa kupambana na rushwa wamevutiwa na jitihada ambazo Tanzania imezichukua kukabiliana na janga hilo.

  Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Mei 13, 2016) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wake kwenye mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.Waziri Mkuu alisema katika kikao cha kwanza kilichohudhuriwa na wakuu wa nchi na viongozi wa kitaifa wapatao 20, alipata fursa ya kuelezea jinsi Tanzania ilivyoweza kupambana na rushwa kwa kuzingatia vigezo vikuu vinne.
  Waziri Mkuu alivitaja vigezo hivyo kuwa ni kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria zinazohusu masuala ya rushwa; uanzishwaji wa mahakama maalum ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi Julai, mwaka huu; mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya wananchi na utaratibu wa kubaini wala rushwa kwa kushirikisha jamii ikiwemo kutunza siri za watoa taarifa.
  “Ziko sheria ambazo zinafanyiwa kazi hivi sasa ambazo ni lazima zipitishwe na Baraza la Mawaziri kabla mahakama hii haijaanzishwa, zikishapitishwa na Baraza ndipo zitaanza kutumika,” alisema.Akifafanua kuhusu mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya maendeleo, Waziri Mkuu alisema kwamba katika bajeti ya mwaka huu, Serikali imeweza kuongeza kiasi cha fedha zilizotengwa kwa shughuli za maendeleo kutoka asilimia 27 hadi kufikia asilimia 40.
  “Kuongezeka kwa kiwango hiki ni ishara tosha kuwa tumelenga kutoa huduma kwa Watanzania na muhimu katika rushwa ni udhibiti wa fedha hizo na kuhakikisha zinakwenda kwenye miradi; matuizi mazuri ya fedha za Serikali, matumizi mazuri ya fedha zinazochangiwa na wahisani ili ziweze kutekeleza miradi iliyokusudiwa,” alisema.
  “Tumekubaliana na uwepo wa uwazi na kushirikishana taarifa hasa katika kupeana taarifa za makampuni yanayoanzishwa na kusajiliwa katika nchi zinazoendelea kama njia ya kudhibiti tabia ya nchi ndogo kama Ireland na Panama kupokea na kuficha fedha zinazotoka kwenye nchi zinazoendelea” alisema.Alisema kila nchi imesisitizwa kutumia raia na kuwalinda watoa siri, kutumia mifumo ya kiintelijensia, kutumia wanasheria na kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya watu wanaokamatwa kwa masuala ya rushwa.
  Waziri Mkuu alisema alipata fursa ya kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. David Cameron ambaye mbali na kupongeza juhudi za Serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kupambana na rushwa pia aliahidi kutoa mwaliko ili Tanzania iweze kushiriki kwenye mkutano mwingine wa masuala ya rushwa utakaofanyika Japan, Julai mwaka huu.
  “Anataka Tanzania iende kwenye mkutano huo ili ikaelezee mafanikio iliyoyapata katika kukabili suala hili, ili pia nchi nyingine ziweze kuiga utaratibu ambao Serikali imeutumia hadi tukafanikiwa katika mapambano dhidi ya rushwa,” alisema Waziri Mkuu.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amesema ofisi yake haijahusika na kuandaa mkutano wa wanadiaspora waishio Uingereza kama ambavyo imedaiwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna watu maalum wamechaguliwa kushiriki mkutano huo.
  Amesema mkutano huo umepangwa kufanyika kesho (Jumamosi, Mei 14, 2016) na uko wazi kwa Watanzania wote kushiriki ili waje kusikiliza nchi yao imefanya nini na kama kuna masuala yanahitaji ufafanuzi, watapatiwa fursa hiyo.“Kulikuwa na hofu ya watu wanaotoka mbali kutoweza kushiriki sababu ya gharama, lakini nasema yeyote mwenye uwezo wa kuja aje ndiyo maana tumeuweka muda wa asubuhi ili watu waweze kushiriki na kuwahi kurudi makwao,” alisema.

  IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU

  IJUMAA, MEI 13, 2016.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg (kulia) katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016. Wanne kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman na watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Idara.
  ………………………………………………………
  WAZIRI MKUU wa Norway, Bibi Erna Solberg amemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ahakikishe Tanzania inatuma wawakilishi wa Serikali kwenye mkutano wa uwekezaji unaopanga kujadili fursa za uwekezaji barani Afrika utakaofanyika jijini Oslo, Norway, Oktoba mwaka huu.

  Bibi Solberg ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Mei 12, 2016) alipokutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ya ana kwa ana kwenye mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani.

  Akizungumzia kuhusu mkutano huo, Waziri Mkuu wa Norway alisema mkutano huo umeandaliwa na taasisi binafsi ya Norway Africa Business Association (NABA) na kwamba anazo taarifa kuwa utalenga kujadili fursa za uwekezaji barani lakini focus ikiwa ni Tanzania.

  “Ni vema Tanzania ikatuma wawakilishi kwenye mkutano ili waje kuelezea fursa zilizoko nyumbani. Serikali ilete watu wa kuja kuelezea hali halisi ikoje nchini Tanzania,” alisema.Alisema ili fursa za uwekeaji ziweze kutumika ipasavyo, ni vema Tanzania ikawa na mfumo wa kimahakama unatoa haki bila upendeleo (a fair judicial system) kwani utasaidia kujenga hali ya kujiamini kwa wafanyabiasha wanaokuja kuwekeza Tanzania.

  “Mfumo huu utaleta hamasa kwa wawekezaji, kwani watajua kwamba mitaji yao iko salama na inalindwa kisheria, hivyo hawatakuwa na hofu,” alisema.“Hata hivyo, napenda kusisitiza kuwa makampuni yanayotoka nje na kuja kuwekeza Tanzania hayana budi kuheshimu sheria za nchi yenu pamoja na za huku wanakotoka,” alisisitiza.

  Akijibu hoja hiyo, Waziri Mkuu alisema usawa wa kisheria upo nchini kwa sababu Tanzania imesaini mikataba ya kimataifa ya MIGA na ICSID (International Centre for Settlement of Investment Disputes) ambayo inahusika na usuluhishi wa migogoro ya kibiashara.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa alimweleza Bibi Solberg kuwa Tanzania inahitaji kujifunza kutoka Norway katika suala la uanzishwaji wa mfuko wa ili mapato yatokanayo na rasilmali za nchi yatunzwe kwa ajili ya vizazi vijavyo.

  Naye akaipongeza Serikali ya awamu kwa kuanzisha wazo la kutaka kuanzisha mfuko huo hata kabla ya kuanza kuuza rasilmali hizo. Pia alimtihibitishia Waziri Mkuu kuwa wao wako tayari kubadilishana uzoefu na Tanzania katika suala hilo.

  IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU

  IJUMAA, MEI 13, 2016.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (kulia) wakizungumza na Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika London Uingereza, May 12, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  …………………………

  WAZIRI MKUU wa Norway, Bibi Erna Solberg amesema nchi yake iko tayari kuisaidia Tanzania katika suala la kuendeleza elimu kwa mtoto wa kike.

  Bibi Solberg ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Mei 12, 2016) alipokutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ya ana kwa ana kwenye mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani.

  Akizungumza na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Lancaster House, jijini London, Uingereza, Bibi Solberg alisema: “Malengo yetu kwa Tanzania ni kuendeleza elimu kwa mtoto wa kike,” na kuongeza kuwa mbali ya kuwa ni mdau wa maendeleo kwa miaka mingi, asilimia kubwa ya fedha za bajeti zinazotolewa na nchi hiyo kwa ajili ya misaada ya maendeleo zinaelekezwa Tanzania.

  “Sasa hivi kuna Serikali mpya iliyoingia madarakani. Tengenezeni ajenda zenu na mzilete ili tuone ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia,” alisema.

  Akizungumzia kuhusu mkutano wa kupambana na rushwa, Bibi Solberg alisema ameufurahia mkutano huo sababu umetoa fursa kwa watu kulizungumzia kwa uwazi tatizo la rushwa. “Watu waliouwa hawalizungumzii suala hilo, hivi sasa wameanza kulijadili na kupanga mbinu ya kukabiliana na janga hilo kubwa,” alisema.

  Kwa upande wake, Waziri Mkuu Majaliwa aliishukuru Serikali ya Norway kwa misaada ambayo imekuwa ikiipatia Tanzania kwa kipindi kirefu.Waziri Mkuu Majaliwa alimhakikishia Waziri Mkuu wa Norway kwamba fedha zote za misaada zinazotolewa kwa Serikali ya Tanzania ziko salama na zitatumika kwa uwazi na kwa malengo yaliyopangwa.

  “Malengo ya Serikali ya sasa ni kuleta maendeleo ya kiuchumi lakini pia nchini mwetu kuna amani na usalama kwa sababu kama hakuna amani ina maana hakuna usalama,” alisema Waziri Mkuu.Alimhakikishia Bibi Solberg kuwa Tanzania ni salama na wala hawana haja ya kutilia shaka juu ya uwepo wa amani. Pia alimtaka awahimize wawekezaji kutoka kwao waje kuwekeza kwenye uchakataji wa gesi ya kimiminika (LNG) kwa sababu ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

  Katika mkutano huu, Waziri Mkuu amefuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola, wataalamu wa sekta ya rushwa na wanasheria.

  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU

  IJUMAA, MEI 13, 2016.

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO


  SERIKALI YATOA BILIONI 2.3 KUWALIPA WAFANYAKAZI WA NIDA

  SERIKALI imeipatia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Shilingi Billioni 2.3 (Bilioni mbili na milioni mia tatu) kwa ajili ya kuwalipa waliokuwa watumishi wa muda wa mamlaka hiyo, wapatao 597, waliosimamishwa kazi hivi karibuni.

  Malipo hayo yanahusisha mishahara yao ya miezi minne, ukiwemo mshahara wa mwezi mmoja wa notisi ya kusimamishwa kazi, pamoja na malimbikizo ya madeni yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii.Kabla ya NIDA kuwalipa watumishi hao fedha hizo, Wizara ya Fedha na Mipango iliamua kufanya uhakiki ili kujiridhisha kama madai hayo yalikuwa sahihi.

  Uhakiki huo ulihusisha mahojiano ya ana kwa ana na watumishi hao pamoja na kupitia nyaraka mbalimbali zikiwemo majalada, mikataba ya ajira, madaftari ya mahudhurio, taarifa za kazi za kila siku na namba zao za akaunti za benki zilizokuwa zikitumika kulipa mishahara.

  Katika uhakiki huo imebainika kuwa kulikuwa na kasoro ama changamoto kadhaa zikiwemo za kimikataba kati ya NIDA na watumishi hao.Wakati wa zoezi hilo, jumla ya watumishi 597 walipaswa kuhakikiwa lakini majina ya watumishi yaliyowasilishwa kuhakikiwa ana kwa ana kutoka NIDA, Tanzania bara yalikuwa 565.Hata hivyo, watumishi 516 pekee ndio waliojitokeza katika zoezi hilo na wengine 49 hawakujitokeza.

  Watumishi wa muda 32 kutoka NIDA Tanzania Zanzibar, wanaofanya jumla ya watumishi wa Mamlaka hiyo waliosimamishwa kazi kufikia 597, walihakikiwa kwa kupitia majalada yao yaliyoko ofisi za NIDA Makao Makuu, na kubaini mikataba yao haikuwa na kasoro.

  Kwa mantiki hiyo watumishi 427 kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ndio waliokidhi vigezo vya kulipwa stahili zao za kuachishwa kazi.Aidha, watumishi wengine 121, walibainika kuwa na kasoro mbalimbali ambazo zinapaswa kurekebishwa na Menejimenti ya NIDA kabla ya kufanya malipo hayo.

  Baadhi ya kasoro zilizobainika katika uhakiki huo ni pamoja na kukosekana kwa mikataba na majalada yao katika Ofisi ya mwajiri, kukosekana majina yao kwenye daftari la mahudhurio kazini, kuwa na utata kwenye mikataba (kutofautiana tarehe na sahihi za wahusika), kufanana kwa namba za majarada, na kukosekana kwa barua za kusitishwa kazi.

  Wizara ya Fedha na Mipango imemaliza kazi yake ya uhakiki na kwamba jukumu la kuwalipa watumishi wa NIDA wanaostahili limeachwa mikononi mwa menejimenti ya NIDA.

  Imetolewa na:

  Benny Mwaipaja
  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
  13 Mei, 2016

older | 1 | .... | 1218 | 1219 | (Page 1220) | 1221 | 1222 | .... | 3270 | newer