Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live

IN LOVING MEMORY

$
0
0

THEODORE MAGANGA WATUGULU

(Passed away on 3rd May 2005)


It is exactly eight years since you suddenly and painful left us. We loved you very much, we remember you each day and look back and cherish the love, wisdom and good examples you demonstrated to us. With great respect, we truly thank God for the time we shared together, to see and appreciate your love, hard work, and good values as a husband and father. You are fondly remembered by your wife Mary, Children Doreen and Denis, your mother Paulina, brothers, sisters, relatives and friends.


GOD HAS GIVEN AND GOD HAS TAKEN LET HIS NAME BE PRAISED


AMEN.


CSSC yashinda Tuzo ya SADC kutambua mchango wa mashirika ya dini katika masuala ya jinsia

$
0
0
Afisa uhusiano wa CSSC Bi. Rachel Mkundai akikabidhiwa Tuzo kutoka kwa waandaji “Gender Links”

Afisa uhusiano wa CSSC Bi. Rachel Mkundai akitoa neno la shukurani  kwa waandaji “Gender Links”
 Bi. Rachel Mkundai akikabidhi Tuzo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC Bw. Peter Maduki.
Afisa uhusiano wa CSSC Bi. Rachel Mkundai akikabidhiwa Tuzo kutoka kwa waandaji “Gender Links”
--
Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) imeshinda Tuzo ya kutambua mchango wa mashirika ya dini katika kuwawezesha wanawake kutambua haki ya afya ya uzazi. Tuzo hiyo imetolewa na Shirika linalotetea  masuala ya jinsia (Gender links) ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) lenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini.

CSSC ilitangazwa mshindi na kukabidhiwa Tuzo hiyo wakati wa kilele cha mkutano mkuu wa masula ya jinsia ya ukanda huo uliofanyika nchini Afrika ya Kusini.

Mashindano hayo yalihusisha washiriki 213 kutoka nchi 13 ambazo ni wanachama wa SADC, na CSSC iliibuka mshindi katika kupengele cha mashirika ya dini na kuwashinda wengine 13 katika kipengele hicho.

Ushindi wa CSSC umepatikana baada ya kuwasilisha makala ya filamu (Documentary) kuhusu namna ya kumsaidia mtoto aliyezaliwa  kabla ya miezi tisa (Pre-mature) kukua na kuongezeka uzito unaostahili kwa kutumia njia ya asili maarufu kama “Kangaroo method” Njia hii inatumika katika hospitali ya wilaya ya Sengerema inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Geita.

Na
Renatus Sona
Afisa Habari -CSSC

Article 17

Uvutaji pumzi - Kuimba na Kuongea

$
0
0

Mwandishi nguli na mwanamuziki Freddy Macha adokeza mambo mawili muhimu katika na tizi la pumzi katika kuimba na kuzungumza...

kumbukumbu

$
0
0

HAYATI SARAH .L. GELLEGE
Leo mama yetu mpendwa imetimia miaka 2 kamili tangu uitwe na MUNGU. 
Kwa kweli ni ngumu kuzoea kuishi bila wewe lakini tunamshukuru sana sana MUNGU kwani anazidi kutupigania na kututia nguvu kwani ndio tegemeo letu. Pengo uliloliacha kamwe halitozibika kwani tunakumbuka ucheshi wako na juhudi zako na ushauri wako katika kupambana na maisha na tuliona juhudi zako mama!!
Unakumbukwa sana na wanao Luther(Mtua), Lamson(Ipyana) na Ruth. Pia unakumbukwa sana na wajukuu zako ambao hawaachi kuuliza bibi wa Ukonga mbona haji siku hizi kwani kaenda wapi? Unakumbukwa sana pia na dada zako,kaka zako,wadogo zako,wifi zako,shemeji zako,wajukuu zako,
watoto zako,wakwee zako,ndugu,jamaa,majirani na marafiki kwakweli wanakumiss sana!!!
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE!!!!. 

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE AKUTANA NA BALOZI WA CANADA NCHINI MHE ALEXANDRE LEVEQUE LEO

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe Alexandre Leveque aliyemtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo asubuhi. Balozi Leveque aliongozana na Mkurugenzi Mwandamizi na Mkuu wa Ushirikiano wa Canadian International Development Agency (CIDA), Bi Patricia McCullagh. Wa pili kushoto ni Balozi Dorah Msechu, Mkurugenzi katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa anayeshughulikia kurugenzi ya Nchi za Ulaya na Amerika, akifuatiwa na ofisa dawati Bi Upendo Mwasha. Picha na Ikulu

Warembo Miss Tanga 2013 kuanza mazoezi Mei 8

$
0
0
Na Mwandishi Wetu 

 MAZOEZI kwa ajili ya kujiandaa na shindano la kumsaka malkia wa Mkoa wa Tanga mwaka huu "Redd's Miss Tanga 2013" yanatarajia kuanza Jumatano Mei 8 kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga. 

 Akizungumza na Ripota wa Globu ya Jamii, Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula ambae ndie Mratibu wa shindano hilo, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri. Kigundula alisema kuwa walimu watakaosimamia warembo hao ni Miis Tanga 2012 Teresia Kimolo na Miss Tanga 2011 Zubeda Seif. 

 Alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri, ambapo warembo wameanza kuitikia wito wa kushirikishi shindano hilo. Kigundula alisema kuwa mpaka sasa jumla ya warembo 8 wamejitokeza kushiriki shindano hilo ambapo nafasi bado iko wazi kwa wasichana wote wenye sifa za kushiriki.

 "Kila kitu kinaendelea vizuri, ikiwa na warembo kuendelea kujiandikisha kushiriki shindano la mwaka huu, ambalo nina hakika litakuwa la aina yake"alisema Kigundula Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.

 Pia alisema fomu zinapatika katika ofisi ya Mwananchi iliyopo Bandari Tanga ghorofa ya Nne, Five Brathers kwa Nassa Makau iliyopo jijini humo, kwa Dar es Salaam zinapatikana katika ofisi za Jambo Leo zilizopo Jengo la Hifadhi Hause Posta.

Baraza la Biashara latoa Elimu ya Mashirikiano ya ushindani wa Kibiashara kwa Mikoa ya Kusini,Lindi,Mtwara na Ruvuma

$
0
0
Wadau mbalimbali wa Serikali,Wafanyabiashara na wanahabari toka Mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma wanakutana leo katika warsha ya mashirikiano ya kibiashara kwa mikoa hiyo wanakutana leo ili kujenga na kubadilishana mawazo kwa lengo la kujenga uelewano na Ushirikiano ambao utasaidia kutekeleza Dira ya kibiashara kwa Ufanisi.

Majadiliano hayo ya ushirikiano yatachangia katika kusukuma mbele utekelezaji wa Dira ya Tanzania ya Maendeleo 2025 pamoja na juhudi mbalimbali kuendelea utekelezaji wa Dira hiyo hauendani na shabaha ya kuiwezesha nchi ya kipato cha kati inayojivunia maendeleo makubwa na maisha bora ya wananchi.

Katika warsha hii mada kuu ni kuhamasisha Teknolojia kwa mageuzi ya kiuchumi na kijamii Tanzania itawasilishwa ikienda sambamba na mada ndogondogo ikiwemo Umuhimu wa Ubunifu katika mageuzi ya kiuchumi na kijamii,Mchango wa Tehama,Ubora wa Viwango katika wilaya,usalama wa watu na mali zao ikiwa pamoja na majadiliano ya Vikundi mada ambazo zitatolewa na UDSM,COSTECH,TCRA,TBS na Polisi Makao Makuu
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Kanali Joseph Simbakalia akifungua Warsha ya Majadiliano ya Ushirikiano wa Kibiashara kwa Manufaa ya Umma Kikanda kwa Wawakilishi toka Mikoa ya Lindi,Ruvuma na Wenyeji Mtwara,Kulia ni Samson Chemponda,Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara na kushoto ni Saidi Masudi Nahunda,Mwenyekiti wa TCCIA-Mtwara.
Wadau mbalimbali wanaohudhuria kikao cha mashirikiano ya kibiashara kutoka mikoa ya Lindi Mtwara na Ruvuma kinachoendelea katika Ukumbi wa Makonde Beach Resort-Mtwara.  Na Abdulaziz Video-Mtwara

Shoe Shine kazini

$
0
0
Kamera yetu ilimnasa Shoe Shine huyu akipiga kiwi buti za kutembelea kwenye maji za mteja wake maeneo ya Mabibo Soko la Ndizi jijini Dar.

American People Sponsor Jazz Musicians' Visit to Tanzania

$
0
0
The Keri Chryst, (with microphone); and Jeff Hoffman, (playing guitar); performed at the Buguruni School of the Deaf for over 100 students recently. In their performance, Keri and Jeff also interacted with audiences, discussed American culture and geography, and enjoyed welcome singing and dancing performances offered by their hosts. The duo was accompanied by United States Embassy Public Affairs officials, who underscored the United States' commitment to strengthen youth outreach through cultural exchange programs that partner American musicians with Tanzanian musicians and the public. In addition, they donated over 200 books and basketballs to children at the Buguruni School of the Deaf and the Alice Foundation on behalf of the American people who sponsored their visit to Dar es Salaam, Tanzania from April 25 to April 30 through the U.S. Department of State's Africa Regional Services (ARS) based in Paris and the U.S. Embassy in Dar es Salaam.
The Keri Chryst, (with microphone); and Jeff Hoffman, (playing guitar); performed at the Alliance Française before 100 guests recently. In their performance, Keri and Jeff also interacted with audiences, discussed American culture and geography, and enjoyed welcome singing and dancing performances offered by their hosts. The duo was accompanied by United States Embassy Public Affairs officials, who underscored the United States' commitment to strengthen youth outreach through cultural exchange programs that partner American musicians with Tanzanian musicians and the public. The American people sponsored the visit to Dar es Salaam, Tanzania from April 25 to April 30 through the U.S. Department of State's Africa Regional Services (ARS) based in Paris and the U.S. Embassy in Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL APOKEA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA VIJANA WA HARAIKI WA MBIO ZA MWENGE KUTOKA BENKI YA NMB

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea sehemu ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. Milioni 35, kwa ajili ya vijana wa Haraiki ya Mbio za Mwenge utakaowashwa Visiwani Pemba Mei 6, mwaka huu, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa Benki ya NMB, Domina Feruzi, wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Mei 2, 2013. Kushoto ni Meneja wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa benki hiyo, Elieza Msuya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wageni wake kutoka Benki ya NMB, baada ya makabidhiano ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. milioni 35 kwa ajili ya vijana wa Haraiki wa mbio za Mwenge unaotarajia kuwashwa Mei 6, mwaka huu Visiwani Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa Benki ya NMB, Domina Feruzi (wa pili kulia) Meneja wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa benki hiyo, Elieza Msuya (kulia) Ofisa Mahusiano wa benki hiyo, Doris Kilale (wa pili kushoto) na Huruma Mwaihomba, Ofisa Mahusiano wa benki hiyo, baada ya makabidhiano hayo.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Breaking nyuzzzzzzz......:Mfanyabiashara kariakoo ajirusha toka Ghorofa ya tisa na kuangukia Gari mchana huu

$
0
0
Muda mfupi uliopita,Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Shirima ambaye ni Mfanyabiashara katika moja ya Maduka ya Kariakoo jijini Dar es Salaam,amejirusha toka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord iliopo Maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na amekimbizwa hospitali kwa uangalizi zaidi maana haijafahamika kama kapoteza Maisha au bado yu hai.

Mfanyabiashara huyo alijirusha toka ghorofani na kuangkia katika Gari aina ya Toyota Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imepaki nje ya hoteli hiyo,chanzo cha kujirusha kwa mfanyabiashara huyo bado hakijafahamika mpaka sasa.

Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita,wanaeleza kuwa walipatwa na mshuko baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichokuwa kimeangukia gari hilo na waliposogea kushuhudia ndipo walipobaini kuwa alikuwa ni mtu huyo alietambulika kwa jina moja la Shirima.

TAMASHA LA CHEKANAO NA VODACOM LILIVYOBAMBA COCO BEACH

$
0
0
Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature akiwapagawisha mashabiki waliofurika katika ufukwe wa Coco beach wakati wa Tamasha la Cheka Nao lilioandaliwa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Wafanyakazi mei mosi juzi jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji wa bendi ya muziki wa dansi ya Msondo ngoma baba ya muziki Romarii Mng'anda akiwaongoza waimbaji wenzake wakati wa tamasha la ChekaNao liliandaliwa na Vodacom Tanzania ikiwa ni mahususi kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya wafanyakazi Mei mosi hapo juzi na kufanyika katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa Kikundi cha wakali dansi wakionyesha ukali wao wakati wa onyesho la Cheka Nao liliandaliwa na Vodacom Tanzania katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam,Ikiwa ni sehemu ya Kusherehekea sikukuu ya Mei mosi hapo juzi .
Msanii anaechipukia wa Kizazi kipya Dogo Lila toka kundi la TMK Wanaume Halisi akionyesha umahiri wake wakati alipokuwa akiimba kwenye Tamasha la Cheka Nao lililoandaliwa na Vodacom Tanzania katika ufukwe wa Coco Beach jijjni Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi Mei mosi hapo juzi.

Vyuo Mbeya vyakabidhiwa vifaa vya michezo ya Safari Lager Pool Higher Learning

$
0
0

Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Aron Samweli (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo vya mashindano ya Safari Lager Pool Higher Learning Mkoa wa Mbea .Kulia ni Makamu Mwenyekiti , Obmark Malebeja.
Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Aron Samweli (kulia) akimkabidhi tisheti mwanafunzi wa Chuo cha TIA Mkoani Mbeya,Steven Kiasi kwa ajili ya mashindano ya Safari Lager Pool yanayotarajiwa kuafanyika jumapili. 

Watanzania washiriki matembezi ya Yokohama

$
0
0
Katika kuelekea kwenye mkutano wa tano wa kimataifa wa TICAD, watanzania wameshiriki kwenye matembezi ya hisani ya Yokohama na kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Watanzania wanashiriki kwenye matembezi hayo kwa mwaka wa pili mfululizo ikiwa ni wawakilishi pekee wa Bara Afrika kwenye matembezi hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka, safari hii ikiwa ni matembezi ya 61.

Balozi wa Tanzania nchini Japani Mh. Salome Sijaona amewashukuru Watanzania walioshiriki matembezi hayo, na kusema kwa njia hii pia, Watanzania tunatangaza utamaduni. Washiriki walivalia nguo za kiafrika.
Baadhi ya Watanzania waishio Japani wakiwa katika bustani ya Yamashita jiji Yokohama tayari kwa kushiriki kwenye matembezi ya hisani ya Yokohama.

ZIARA YA DKT. SHEIN WILAYA YA KASKAZINI B UNGUJA

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na viongozi wa Tawi la CCM wilaya ya Kaskazini B alipofika kuweka Jiwe la Msingi Tawi hilo,akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuweka jiwe la msingi Tawi la CCM Zingwezingwe wilaya ya Kaskazini B,akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akizungumza na wanachama wa Tawi la CCM Zingwezingwe baada ya kuweka jiwe la msingi Tawi la Kijiji hicho,akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuweka jiwe la msingi tawi la CCM kwa Gube Mfenesini ,akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akijenga moja ya Tofali kama ishara ya uwekaji wa jiwe la msingi Tawi la CCM Donge,akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja leo,(Kushoto) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi .Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO

KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU TAARIFA YA AWALI YA TUME YA TAIFA YA KUCHUNGUZA MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012

Airtel yatangaza mshindi wa million 50 wa promosheni ya Amka millionea

$
0
0
Mwandishi wa Clouds TV Austin Bayadi ( wakwanza kushoto) akibonyesha kitufe cha komputa wakati wa droo kubwa ya mwisho ya kumtafuta mshindi wa shilingi million 50 wa promosheni ya Amka millionea ambapo bwana Layakal Akbar Thawer mkazi wa Dar es salaam aliibuka mshindi wa promotion hiyo. Wakishuhudia ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando(aliyekaa katikati) akifatiwa na mwakilishi wa bodi ya michezo ya Bahati Nasibu Emmanuel Ndaki akifatiwa na Afisa masoko wa Airtel Khalila Mbowe.
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando(katikati) na Afisa masoko wa Airtel Khalila Mbowe kwa pamoja wakionyesha droo ya kumtafuta mshindi wa millioni 50 wa Amka millionea inavyotafuta mshindi wakati wa droo hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Moroco na kushuhudiwa na Waandishi wa habari, akishuhudia kulia ni mwakilishi wa bodi ya michezo ya Bahati Nasibu Emmanuel Ndaki.
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando(aliyekaa katikati) akiongea na wandishi wa habari (hapo pichani) wakati wa droo kubwa ya mwisho ya kumtafuta mshindi wa shilingi million 50 wa promosheni ya Amka millionea ambapo bwana Layakal Akbar Thawer mkazi wa Dar es salaam aliibuka mshindi wa promosheni hiyo. Kushoto ni mshindi wa million 15 wa promosheni ya Amka milionea bwana Juma Ibrahim Hiza mkazi wa Dar es Saalam na kulia ni mshindi mwingine wa shilingi milioni 15 Bwana Adnan Ayub Khan mfanyabiashara Simiyu.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imechezesha droo ya mwisho ya promosheni ya Amka millionea na kumzawadia mshindi wa droo hiyo kitita cha shilingi million 50.

Droo hiyo kubwa na ya mwisho ilifanyika katika makao makuu ya Airtel morocco na kushuhudia na waandishi wa habari ambapo mkazi wa Kariakoo Dar es Salaam Bwana Layakal Akbar Thawer mwenye umri wa 60 mafanyabiashara wa duka la rangi aliibuka kuwa mshindi wa millioni 50 na kutangazwa rasmi kuwa mshindi.

Akiongea wakati wa droo hiyo, Mkuu wa kitengo cha Masoko wa Airtel Levi Nyakundi alisema, Mpaka sasa Airtel kwa kupitia promosheni ya Amka millionea imewazawadia watanzania na wateja wengi nchini. leo tunashuhudia bwana Akbar akiibuka kuwa mshindi wa pesa taslimu shilingi million 50 kupitia promosheni hii ya Amka millionea na Airtel. Hii inathibitisha thamira yetu ya kutuoa huduma bora na bei nafuu huku tukiendelea kuwazawadia watanzania na wateja wetu kwa kupitia promosheni mbalimbali ikiwemo hii ya Amka millionea.

Tunaahiidi kuendelea kuboresha huduma zetu na kuhakikisha tunawafikia watanzania wengi zaidi, mpaka sasa kwa kupitia huduma ya Airtel yatosha wengi wamepata unafuu wa gharama za mawasiliano na kuwezeshwa kupiga simu kwenda mitandao yote nchini na kushuhudia kuwa kweli Airtel yatosha.

Tunaamini kwa kuendelea kuongeza ubunifu katika huduma zetu na kuwazawadia wateja wetu kwa kupitia promosheni mbalimbali pamoja na huduma bora zikiwemo za kibenki kupitia Airtel money na huduma ya internet ya kasi zaidi ya 3.75G wateja wataendelea kupata suluhusho la mawasiliano na za kimtandao zilizo bora , za uhakika na gharama nafuu aliongeza Nyakundi.

Akiongea kwa njia ya simu mshindi wa shilling million 50 bwana Layakal Akbar Thawer alisema “ mimi nimekuwa mteja wa Airtel kwa miaka 7 sasa na nafurahia huduma zao, napenda kuwambia watanzania washiriki promosheni hizi nao wananafasi ya kuibuka washindi.

Promosheni ya Amka milionea ilizinduliwa rasmi mwenzi December mwaka jana na kuongezewa muda wake mwenzi machi mwaka huu, mpaka sasa wateja zaidi ya1458 na pesa taslimu zenye thamani ya zaidi ya shilingi million 626 zimezawadiwa kwa washindi walioibuka kutoka katika mikoa mbalimbali nchini.

Mshindi mwingine wa shilingi million 50 alipatikana na kuzawadia mwenzi watatu naye ni Mwalimu wa shule ya msingi na mkazi wa manyara kiteto bwana Grayson Safieli Kabora , huku washindi wa shilingi million 15 wakiwa ni pamoja na Juma Ibrahim Hamza umri wa miaka 30 na mkazi wa kawe Dar es Saalam na Adrian Ayub khan umri wa miaka 25 mfanyabiashara Simiyu.

Dr. Sezibera afungua kongamano la siku mbili katika kuadhimisha Siku Uhuru vyombo vya Habari jijini Arusha

$
0
0
Meza Kuu ikiongozwa na Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera (wa pili kulia) na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen (wa tatu kushoto).
Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera akihutubia na kufungua Kongamano la Siku Mbili linaloenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani.

Viewing all 110019 articles
Browse latest View live




Latest Images