Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1217 | 1218 | (Page 1219) | 1220 | 1221 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Wawakilishi kutoka Taasisi mbalimbali za Umma nchini wakifuatilia mada
  Mkurugenzi Msaidizi Bi. Veila Shoo akiwasilisha matokeo kuhusu Ufuatiliaji wa Mifumo na Viwango vya utendaji kazi kwa Taasisi za Umma nchini.Wanaomsikiliza ni sehemu ya wawakilishi kutoka katika Taasisi za Umma.

  Taasisi za Umma zimehimizwa kutumia ipasavyo mifumo ya utendaji kazi iliyowekwa ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

  Mkurugenzi Msaidizi ,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Veila Shoo alisema hayo wakati akitoa takwimu za matumizi ya mifumo hiyo katika kikao kazi kilichohusisha wawakilishi kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala za Serikali na kufanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

  Bi. Veila alieleza kuwa ufuatiliaji wa mifumo umefanyika katika Idara Zinazojitegemea 16 ambapo imebainika baadhi ya mifumo inatukima ipasavyo wakati mingine bado.

  Awali, akifungua kikao kazi hicho Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Bw. Mick Kiliba alisema kuwa zoezi la kufanya ufuatiliaji wa mifumo ni endelevu na watendaji wanatakiwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kutumia mifumo hiyo.

  Alisema lengo la tathmini hiyo ni kupata takwimu za utekelezaji wa mifumo na viwango vya utendaji kazi, kutambua mifumo yenye changamoto za utekelezaji, kutoa hamasa ili kuboresha utoaji huduma na kutoa mrejesho kwa taasisi jinsi ya kuimarisha mifumo.

  Mifumo iliyofanyiwa tathmini ni pamoja na:- Mpango mkakati Mkataba wa Huduma kwa Mteja; Mfumo wa wazi wa Tathmini ya Utendaji kazi; Uboreshaji wa michakato ya Utoaji huduma; Tathmini ya Utoaji huduma wa Taasisi; Tathmini ya ndani ya Taasisi; Ushirikiano wa Taasisi ya Umma na Asasi za Kiraia(AZAKI); Waraka Namba 1 wa mwaka 2012 kuhusu Ununuzi wa Samani za Ofisi; na Usimamizi wa Fomu za Serikali.

  0 0

  Na EmanuelMadafa,Mbeya(Jamiimojablogu)

  SERIKALI Mkoani Mbeya imeagiza kufutwa kwa hati ya kiwanja kilichotolewa na halmashauri ya Jiji la Mbeya kwenye chanzo kikuu cha maji kilichopo eneo la Nyibuko kata ya Mwakibete kwa matumizi ya makazi.

  Agizo hilo, limetolwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala mara baada ya kutembelea na kukagua chanzo kikuu cha maji cha Nzovwe, chenye uwezo wa kuzalisha mita 12 za ujazo kwa siku na kusambaza maji kwa asilimia 41 kwa wakazi wa jiji la Mbeya wapatao zaidi ya 200,000.

  Kiwanja hicho ambacho kipo karibu na eneo la chanzo cha maji cha Nzovwe, kilitolewa na maafisa ardhi, idara ya mipango miji kwa ajili ya matumizi ya makazi na kumilikiwa na mtu binafsi aliyetajwa kwa jina moja la Mwakasala.

  Makala amesema, chanzo hicho cha maji ndio tegemezi kwa kusambaza huduma ya maji kwa wananchi wa Jiji la Mbeya, hivyo kama kitaachwa na kuharibiwa, wananchi zaidi ya 200,000 wapo hatarini kuikosa huduma hiyo ambayo ni haki yao ya msingi.

  Mkuu huyo wa Mkoa amesema Serikali iliwaondoa wananchi wote waliokuwa wanaishi au kuendesha shughuli zao za kiuchumi ndani ya mita 60 na kuwalipa fidia zao hivyo hatua ya wananchi hao kuendelea kuishia mahali hapo ni kukaidi agizo la serikali.

  Amebainisha kuwa kiwango kikubwa cha upotevu wa maji kwa asilimia 31 inatokana na baadhi ya vyanzo vya maji kuharibiwa kwa kufanyika kwa shughuli za kibinadamu, kulisha mifugo au kujenga nyumba za makazi pamoja na mabadiliko ya kihaidrolojia.

  Hata hivyo, Mkuu huyo aliutaka uongozi wa mamlaka ya maji kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya, kuhakikisha wanalisiamamia zoezi hilo la kumondoa mvamizi huyo ndani ya siku tatu.

  “Wananchi wengine wameondoka tena kwa hiari yao wenyewe, sasa kwa nini huyu atuchezee mchezo mchafu?.. kwa hili sikubaliani nalo, huku akiwataka wananchi ambao ni vijana kulilinda eneo hilo na kuwaonya wale ambao watakubali kutumiwa na mtu au watu kufanya fujo,”alisema.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (Picha Maktaba) 

   

  0 0

  TAARIFA KWA WADAU WA HABARI MKOA WA SHINYANGA KUHUSU WATU WASIO WAANDISHI WA HABARI KUTUMIA JINA LA UANDISHI WA HABARI KWA MANUFAA YAO BINAFSI.

  Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club-SPC) inapenda kuwataarifu wadau wa habari mkoa wa Shinyanga kuwa makini na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakidanganya kuwa ni waandishi wa habari wakati siyo waandishi wa habari.

  Miongoni mwa watu wanaotumia majina ya vyombo vya habari kutapeli na kujipatia fedha ni Emmanuel Mpanda ambaye kwa nyakati tofauti amelalamikiwa na wadau wa habari pamoja na baadhi ya waandishi wa habari kuwa amekuwa akijiita mwandishi wa habari akitumia majina mbalimbali ya vyombo vya habari hasa Televisheni na kusababisha usumbufu pale wadau wanapohitaji kuona habari zao.

  Klabu hii pia inafuatilia mienendo ya watu wengine wawili ambao pindi uchunguzi wetu utakapokamilika na kubaini udanganyifu wanaoufanya kwa wadau wa habari kwa kuwahadaa kuwa ni waandishi wa habari nao tutawaweka hadharani na kuviomba vyombo vya dola kuwachukulia hatua za kisheria.

  Tunapenda kuwatahadharisha kuwa makini na watu wa namna hiyo ambao wanajiita waandishi wa habari wakati siyo waandishi wa habari kwani mbali na kuvichafulia majina vyombo vya habari pia wanashusha thamani taaluma ya Habari,huku wakitutia doa tunaohusika na tasnia hii kwa  kuonekana sote hatufai.

  Ili kuhakikisha kuwa jamii inapata taarifa sahihi na kwa wakati muafaka tunaomba wadau wote wa habari muendelee kushirikiana na waandishi wa habari kwani jamii bila habari ni sawa na usiku wa giza.

  Tunaomba wadau wa habari pale panapotokea shughuli ama tatizo lolote msisite kuwasiliana na ofisi ya Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kwa kufika moja kwa moja ofisini au kupitia mawasiliano yaliyopo hapo juu.

  Tunatoa rai kwa waandishi wa habari kuwa na uchungu na taaluma yao na kutoruhusu tasnia ya habari kuchezewa kwa kuona haya kuwafichua Makanjanja ama kwa lugha nyingine “Waandishi wa Habari Hewa”,wanaodhalilisha taaluma hii.

   Lakini pia hatutasita kuchukua hatua kwa waandishi wa habari wanaoshirikiana na waandishi hewa kwa shughuli za kiuandishi wa habari.

  Tunaahidi kushirikiana na vyombo vya dola katika kuhakikisha kuwa taaluma ya uandishi wa habari inaheshimika.
  Imetolewa na
  Kadama Malunde
  Mwenyekiti SPC
  11.05.2016

  0 0

  Na  Bashir  Yakub.
  Mara  kadhaa  nimeliona  hili.  Hata  we  pia  ni  imani   umeliona.  Tunaliona hili  katika  vyombo  vyetu  mbalimbali  vya  usafiri .Tunashuhudia   askari  wetu   wakikataa  kutoa  nauli.  Na hii  ni  kwa jeshi, polisi ,  magereza   na hata  wale  wa  barabarani.  Hata hivyo  sio wote wapo  wanaotoa  .  Na zaidi hawatoi wakiwa  wamevaa  sare.

  Lakini  mbona  hawatoi  kwenye  magari tu na si  kwenye Fast jet au Emirates. Sijui  ni kwa nini.

   Tunahitaji  ufafanuzi  wa  kisheria  kulijua  hili. Tunahitaji  maelezo   ikiwa  inaruhusiwa  kwao  kufanya  hivyo  au  hapana.


  1. SHERIA INAYOONGOZA JESHI LA POLISI.

  Jeshi  la  polisi  hutekeleza  kila  jukumu  lake  kwa  mujibu  wa  sheria.  Sheria  kuu  inayoongoza majukumu  yao   ya kila  siku  hujulikana  kama  Sheria  ya  Jeshi  la  Polisi   sura  ya  322.  Humu  umeelezwa  wajibu  na  haki  zao.  Imeelezwa  nini wafanye , nini wasifanye na nini wafanyiwe.

  Sambamba  na  sheria  hiyo  pia  zipo  sheria  nyingine  ambazo   hueleza  wajibu  wao  katika  majukumu yao.  Ipo  sheria  ya  kanuni  za  adhabu  sura  ya  16,  ipo  sheria  ya  mwenendo  wa  makosa  ya  jinai   pamoja  na  sheria  ya  ushahidi. Hii  ni  kwakuwa  hawa hushughulika  na   makosa  ya  jinai .

  Kwa  hiyo  kama  kuna  jambo  lolote  tunahitaji  kujua  kuhusu  hawa basi tunataraji  kulipata  katika  sheria  hizi.  Na  kama  halipo  humu  basi  itabidi   watueleze walikolipata.
  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwenye kikundi cha ngoma za asili mara baada ya kuwasili kwenye Ikulu ya nchini Uganda.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Maafisa mbalimbali waku wa vyombo vya Ulinzi wa Serikali ya nchini Uganda mara baada ya kuwasili nchini humo.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo za mataifa mawili pamoja na ule wa Afrika Mashariki ukipigwa katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika Ikulu nchini Uganda.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
  0 0

  JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

  KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

  Taarifa kwa Vyombo vya Habari

  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa kutakuwa na Semina ya wiki moja ya Wakuu wa Kamandi wa majeshi ya Nchi kavu Afrika itakayoendeshwa Mkoani Arusha katika Hoteli ya Mount Meru kuanzia tarehe 13 hadi 19, Mei 2016.

  Lengo la Semina hiyo ni kuwakutanisha Wakuu wa kamandi hizo Afrika ili kujadili na kuendeleza ushirikiano katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayolikabili bara la Afrika katika Nyanja ya ulinzi.
  Kauli Mbiu ya Semina hiyo ni Ujenzi wa Usalama Afrika kupitia Ushirikiano.
  Semina hii hufanyika kila mwaka katika mojawapo ya nchi za Afrika, ili kuwajengea makamanda hao ushirikiano katika kutatua changamoto mbalimbali za kiulinzi zinazotokana na mabadiliko katika Nyanja za kiusalama.

  Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
  S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.

  0 0

  Marehemu Askofu mstaafu Christopher Ruhuza

  02/02/1922 - 06/03/2016

  Familia ya Marehemu Askofu Mstaafu Christopher Gwassa RUHUZA wa Dayosisi ya Kanisa Anglikana Kagera, Ngara, inapenda kukualika kushirikiana nayo kwenye misa Maalum ya kumaliza msiba wa Baba/Babu yao CHRISTOPHER RUHUZA aliyefariki tarehe 06/03/2016 na kuzikwa tarehe 11/03/2016 Kanisa Kuu Anglikana Murugwanza Ngara.
  Misa hiyo kwa Dar es Salaam itafanyika Kanisa Anglikana St Albans iliyopo maeneo ya Posta mpya katikati ya Mji.
  Misa itafanyika Jumamosi, tarehe 14/05/2016, saa tatu na nusu asubuhi.
  Ushiriki wako kwenye misa ni faraja kubwa sana kwetu.
  Mungu akubariki sana.

  Zaburi 23.

  0 0

  Mhe. Makamu wa Rais leo ametembelea Wilaya ya Sengerema kata ya Sima ambapo usiku wa kuamkia jana kulifanyika mauwaji ya kinyama ya watu saba wa familia moja ya Mama na watoto zake kuuwawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.Mhe. Makamu wa Rais Mama Suluhu Hassan ametoa masaa 24 kwa uongozi wa mkoa wa Mwanza pamoja na jeshi la polisi na vyombo vingine kuwatia nguvuni wale watu wote waliohusika na mauaji hayo.
  Pichani ni makaburi yakiandaliwa kwa ajili ya kuzikwa kwa miili saba ya familia moja mapema leo Wilayani Sengerema .
  Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu akisalimiana na kuwapa pole ndugu jamaa na marafiki kufuatia mauaji hayo ya watu saba wilayani Sengerema
  Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi Zainab Telack pamoja na Mkuu wa mkoa wa jiji la Mwanza Mh.John Mongella wakiwa na Mgeni wao Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu alipokewenda kutoa pole kwenye tukio la mauwaji ya kinyama ya watu saba wa familia moja ya Mama na watoto zake kuuwawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana ndani ya wilaya hiyo katika kijiji cha Sima mkoani Mwanza .
  Makamu wa Rais Mh Samia Sulluh akizungumza kwenye tukio la mauwaji ya kinyama ya watu saba wa familia moja ya Mama na watoto zake kuuwawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Mh.Samia ametoa saa 24 kukamatwa kwa wale wote waliohusika na tukio hilo la Kinyama.

  0 0

  NAIBU Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameliambia Bunge Mjini Dodoma, leo tarehe 12 Mei, 2016, kwamba serikali inaandaa sera ya Taifa ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2016, itakayosimamia na kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo

  Alisema kuwa sera hiyo itawasilishwa mbele ya Baraza la Mawaziri hivi karibuni kabla ya kupelekwa bungeni hatimaye itapatikana sheria ya kusimamia taasisi ndogo za fedha-microfinance Act, 2016.“Serikali inatambua changamoto ya taasisi binafsi za fedha zinazosumbua wananchi, hivyo sheria hiyo ikitungwa itasaidia kuondoa matatizo hayo” alisisitiza Dkt. Kijaji

  Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Mhe. Rahisa Abdalah Musa (Viti maalumu), aliyetaka kujua serikali ilikuwa na mpango gani wa kudhibiti utitiri wa taasisi za fedha pamoja na mabenki ili yalete tija kwa Taifa kwa kuwakopesha wananchi

  Akijibu swali la msingi na maswali ya nyongeza yaliyoulizwa na Mhe. Faida Mohamed Bakar (Viti maalumu) aliyetaka kujua mikakati ya serikali ya kuanzisha benki ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo ili kuwawezesha kupata huduma bora, Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa serikali haina mpango wowote wa kufanya hivyo.

  Alisema kuwa badala yake serikali inafanya jitihada za kuimarisha benki zake zilizopo ikiwemo Benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB) na Benki ya Rasilimali (TIB) ili kukidhi mahitaji ya wafanyabiashara wa kada mbalimbali.

  “Serikali imeiboresha kimuundo, Benki ya Rasilimali (TIB) kwa kuunda kampuni tatu zinazofanyakazi kwa kujitegemea lakini kwa ushirikiano wa karibu” alisisitiza Dkt. Kijaji

  Alizitaja kampuni hizo kuwa ni TIB Benki ya Maendeleo itakayotoa mikopo ya muda wa kati na mrefu kwa wafanyabiashara wakubwa na wa kati, TIB Benki ya Biashara itakayowahudumia wafanyabiashara wakubwa, wa kati na wadogo na TIB Rasilimali itakayohusika na masuala ya ushauri kwenye Soko la Hisa na Mitaji la Dar es salaam

  “Pamoja na mambo mengine, kampuni hii inawajibika kuwashauri wafanyabiashara, hususan wa sekta ndogo ya fedha kupata mitaji kupitia Soko la Hisa la Dar es salaam” aliongeza Dkt. Kijaji

  Dkt. Kijaji alisema kuwa pamoja na juhudi za serikali za kuboresha benki hizo, ikiwemo Benki ya Posta, Serikali kupitia Benki Kuu (BOT) inaendelea kuweka mazingira wezeshi ikiwemo kutunga sheria, kanuni na taratibu za kusaidia nguvu za wananchi na sekta binafsi kuanzisha benki au taasisi za fedha katika maeneo yao

  “Ni matarajio yetu kuwa wananchi wanatumia fursa ya mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo nchini kuwekeza wao wenyewe au kuzishawishi benki za biashara kuanzisha huduma za kibenki katika maeneo yao” alisema Dkt. Kijaji

  Kuhusu ombi la mbunge huyo kuitaka serikali iingilie kati masuara ya riba zinazotozwa na taasisi za fedha na kuwaumiza wananchi, Dkt. Kijaji alisema kuwa serikali haiwezi kudhibiti wala kuingilia jambo hilo.

  Alisema kuwa Serikali ilijitoa katika uendeshaji wa moja kwa moja wa shughuli za kifedha tangu mwaka 1991 ili kuruhusu ushindani huru na kuboresha huduma katika sekta ya fedha hivyo viwango vya riba na mikopo vinavyotozwa na benki hizo na taasisi nyingine za fedha zinapangwa kutokana na nguvu ya soko.

  Dkt Kijaji alieleza kuwa katika upangaji wa viwango vya tozo na riba mbalimbali benki na taasisi za fedha huzingatia gharanma za upatikanaji wa fedha, halikadhalika gharama za uendeshaji na sifa alizonazo mkopaji”Alisisitiza Dkt Kijaji

  Imetolewa na:

  Benny Mwaipaja
  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Fedha na Mipango

  DODOMA
  12/5/2016

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia madini, Prof. James Mdoe ( wa nne kutoka kulia) akisoma hotuba ya ufungaji wa mkutano wa siku tatu uliokutanisha wataalam wa masuala ya jotoardhi kutoka katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Eritrea, Marekani, New Zealand na Djibouti kwa ajili ya kujadili taarifa ya mtaalam mwelekezi kuhusu utafiti uliofanywa katika Ziwa Ngozi lililopo mkoani Mbeya ambapo kuna viashiria vya jotoardhi pamoja na eneo la Kibiro nchini Uganda.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia madini, Prof. James Mdoe (kushoto) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akifunga mkutano huo. Kulia ni Mjiolojia Mkuu kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Jacob Mayalla.
  Sehemu ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungaji iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia madini, Prof. James Mdoe (hayupo pichani)

  0 0

  Mganga Mkuu wa Zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha Dkt. Mohammed Alawi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani, ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
  Mganga Mkuu wa Zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha Dkt. Mohammed Alawi akiongea na baadhi ya waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani, ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
  Mwandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani Lyndsey Wajert akiwa tayari kufanyiwa vipimo vya malaria na Mtaalamu wa Maabara Apolinary Mushi katika zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha wakati wa ziara ya waandishi wa Habari hao ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
  Mtaalamu wa Maabara Apolinary Mushi anayefanya kazi katika zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha akifanya mahojiano na mwandishi wa habari Katy Migiro wa Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakati wa ziara mkoani Arusha kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
  Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakiwa tayari uwanja wa ndege wa Arusha kwa safari ya kuelekea mkoani Tanga.
  Eneo la ukingo wa Bahari ya Hindi mkoani Tanga ambapo karibu na eneo walipofikia waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakati wa ziara yao mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Tanga)

  0 0
 • 05/12/16--11:00: Article 19


 • 0 0

   Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah akizungumza na wadau wa Habari kutoka Jukwaa la Wahariri, TMF, Sikika, Baraza la Habari Tanzania, Jukwaa la Katiba na TAMWA.
   Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah akimsikiliza Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw Deus Kibamba wakati alipokutana na wadau wa Habari Ofisini kwake.
   Katibu wa Jukwaa la Wahariri Bw Nevelle  Meena akizungumza wakati wa Mkutano kati ya Katibu wa Bunge na wadau wa Habari.
   Mkurugenzi wa Sikika Bw. Irenei Kiria akizungumza 

  akizungumza wakati wa Kikao kati ya Katibu wa Bunge na wadau wa Habari.

   Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah akibadilishana mawazo  na wadau wa Habari kutoka Jukwaa la Wahariri
  Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah akisalimiana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw Theophil Makunga wakati wa Kikao kati ya Katibu wa Bunge na wadau wa Habari.

  0 0


  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Mei, 2016 amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni muda mfupi baada ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais huyo iliyofanyika katika uwanja wa Kololo Jijini Kampala.
  Katika Mazungumzo hayo Rais Magufuli amempongeza Rais Museveni kwa kuapishwa kuwa Rais wa Uganda kwa kipindi kingine cha miaka 5 na kumhakikishia kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi Uhusiano, ushirikiano na udugu wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo.

  Viongozi hao pia wamezungumzia mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima (Ziwa Albert) nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania ambapo pamoja na kuishukuru Uganda kwa uamuzi wake wa kuamua bomba hilo lipitie Tanzania, Rais Magufuli amemshauri Rais Museveni kufupisha muda wa ujenzi wa mradi huo, kwa kutumia mbinu inayojumuisha usanifu na ujenzi (Design and Construct method) na kutumia wakandarasi wengi watakaogawanywa katika vipande tofauti badala ya kutumia mkandalasi mmoja.

  "Nashauri tutumie mbinu ya usanifu na ujenzi pamoja, hii ni njia ya haraka zaidi, na pia tugawe vipande vya ujenzi kwa njia yote ya bomba la mafuta yenye urefu wa kilometa 1,410 tunaweza kuwa na Wakandarasi watano mpaka sita ambao watatumia njia hiyo mpya ya usanifu na ujenzi.
  "Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumepunguza muda utakaotumika kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta, inaweza hata kuchukua mwaka mmoja tu" Amesema Rais Magufuli.
  Rais Magufuli amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo faida za mradi huo wa mafuta zitaanza kupatikana mapema badala ya kusubiri miaka miwili au mitatu ijayo, na kwamba hiyo itakuwa inaendana na kauli mbiu yake ya "Hapa Kazi Tu"Pia Rais Magufuli amemshukuru Rais Museveni kwa uamuzi wa nchi hiyo wa kuipa Tanzania umiliki wa asilimia 8 katika mradi huo wa bomba la mafuta.
  Kwa upande wake Rais Museveni amesema amefurahishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo, na pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake kubwa ambazo amezifanya katika mapambano dhidi ya rushwa nchini Tanzania.
  "Napenda kasi yako ya uongozi, napenda jinsi unavyopambana na rushwa, kwa sababu rushwa ilikuwa inazaa matatizo mengine kama vile ucheleweshaji wa mizigo bandarini na vikwazo vya mpakani, hivyo nakupongeza sana kwa hilo" Amesema Rais Museveni.
  Katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais Museveni iliyofanyika kabla ya mazungumzo hayo, pamoja na Rais Magufuli viongozi wengine kutoka Tanzania waliohudhuria ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa na Mkewe Mama Salma Kikwete na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU
  Kampala
  12 Mei, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni jijini Kampala mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uapisho wa Rais Museveni.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni jijini Kampala mara baada ya kumaliza mazungumzo yao nchini Uganda. PICHA NA IKULU.

  0 0

  Dear Colleagues,
  Have you got your passport renewed?  Your Bank can renew it for you, It’s easy just use your card at any of the below channels and win a grand prize trip to Dubai and South Africa with your family of three people for three days and many more prizes. All you need to do is to perform a minimum of 20 transactions every month at FahariHuduma Wakala, POS and purchase/pay online. 
  Hurry; do not miss this opportunity. Register NOW for online purchase and start using your TemboCard. CLICK HERE

  0 0

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimelaani vikali tabia ya baadhi ya watu wanaotumia vibaya jina la Chama hicho kuwatapeli wananchi kutoa fedha ili wapatiwe nafasi za ajira katika Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) jambo ambalo sio sahihi.
  Kimewataka wafuasi wa Chama hicho na wananchi kwa ujumla kuacha tabia ya kuwaaminisha watu  kwamba CCM inatoa nafasi mbali mbali za ajira kwani kufanya hivyo ni kuwagombanisha viongozi na wananchi wao.
  Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai alisema Chama hicho hakihusiki na utoaji wa ajira ya aina yoyote, hivyo watu wanasambaza utapeli huo kwa njia ya simu na mitandao ya kijamii lengo lao ni kuchafua taswira njema ya chama hicho.
  Akifafanua zaidi Ndugu Vuai amesema suala la ajira katika taasisi za kiserikali na binafsi zinazolewa kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa hasa baada ya kutolewa matangazo maalum kulinga na nafasi za ajira zilizopo na sio kutumia simu za mkononi kuwapigia watu ili waweze kutoa fedha kwa ajili ya kuwapatiwa ajira hizo.
  “Nimepigiwa simu nyingi na baadhi ya watu wangu wa karibu wakiniuliza juu ya taarifa za Chama kuwa kuuza nafasi za ajira, taarifa ambazo nimezipokea kwa mshangao mkubwa kwani ndani ya chama chetu hakuna utaratibu huo” na kuongeza kusema kwamba “nawataka wananchi kuwa macho na makini na matapeli wanaotumia hila tofauti kuwaadaa watu kwa nia ya kujipatia fedha kwa njia za 
  udanganyifu”. Alisisitiza Vuai.
  Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar, alitoa wito kwa wananchi kuwa makini na matapeli hao na mtu yeyote atakayepigiwa simu na kuambiwa atoe kima chochote cha fedha kwa lengo la kupatiwa ajira na CCM asikubali kufanya hivyo na badala yake atoe taarifa haraka katika vyombo vya dola, ili sheria ichuke mkondo wake.
  Aliwasihi wananchi kuendelea kuamini  kwamba CCM ni Chama kilichokomaa kisiasa na uzoefu mkubwa wa kusimamia demokrasia ya kweli, usawa, haki, utawala bora, a hivyo hakiwezi kujihusisha na vitendo viovu kwa jamii.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM alisisitiza kua; suala la ajira za JWTZ, Idara Maalum za SMZ na zile za Taasisi nyengine za seriikali, zote hizo zinatolewa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW).
  Alisema kuwa haiwezekani hata kidogo Chama hicho (CCM) kitowe ajira na kuongeza kuwa taarifa hizo zinazosambazwa na watu ni za kitapeli na zinalenga kuchafua jina la Naibu Katibu Mkuu huyo pamoja na CCM kwa jumla.
  Aliwaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo na wawe macho na utapeli wa aina hiyo uliozagaa Zanzibar na maeneo mengine nchini, kwani unafanywa na wapinga maendeleo ya CCM na Taifa kwa jumla.

  0 0

  Chama cha Watanzania Waliosoma China kwa kiingereza China Alumni Association of Tanzania (CAAT) kinapenda kukukaribisha katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 6 (2010-2016) tokea kilipozaliwa.

  Sherehe hiyo itafanyika katika ukumbi wa Cardinal Laurian Rugambwa Social Centre pembezoni mwa kanisa la Mtakatifu  Peter (St Peter), Oysterbay Ijumaa ya tarehe 20-May-2016 kuanzia saa 8 alasiri.

  Sherehe hiyo itahudhuriwa na viongozi wakubwa kutoka serikalini na baadhi ya wageni kutoka ubalozi wa China.

  Pamoja na burudani mbalimbali, maadhimisho hayo yatakuwa na hotuba kutoka viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wa ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China.

  Kwenye sherehe hiyo pia utafanyika uzinduzi wa tovuti (website) ya CAAT. Baada ya chakula cha pamoja cha jioni, vilevile kutakuwa na fursa ya wafanyabiashara, wajasiliamali na wafanyakazi waajiriwa kuonyesha bidhaa au matangazo ya bidhaa au huduma wanazotoa.

  Dhima kuu ya tukio hilo ni:
  Utambulisho wa jumuia ya CAAT ambayo inajumuisha wataalam wa taaluma mbalimbali waliohitimu mafunzo yao katika Jamhuri ya Watu wa China
  Kubaini na Kuainisha fursa zinazopatikana Tanzania na China kupitia CAAT
  Maonyesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za biashara za wanajumuia.

  Wote mliopata kusoma China mnakaribishwa. Hakutakuwa na kiingilio.

  Unaweza kushiriki kwa kuthibitisha uwepo wako kwa kupiga simu kwa Katibu Mtendaji wa CAAT kwa kupitia 0783-992020 au 0715-200090 au emailgsoreku@yahoo.com

  Asante
   George Oreku
  Katibu Mkuu
  Chama cha Watanzania Waliosoma China (China Alumni Association of Tanzania) 
  05-May-2015

  0 0


   Waziri Ummy Mwalim akipanga vizuri nyaraka tayari kuhitimisha majadiliano ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo.

   Viongozi wa wizara hiyo wakifuatilia majadiliano ya wabunge kuhusu bajeti hiyo.
   Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Hamis Kigwangallah akijibu moja ya hoja za wabunge.
   Mbunge wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda (Chadema), Mkoa wa Mbeya, akichangia hoja wakati wa makadilio ya Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa iliyopitishwa bungeni Dodoma
   Naibu Waziri wa Afya, Hamisi Kigwangala akisalimiana na wanafunzi wanaosomea utabibu katika Chuo Kikuu cha Dodoma waliozuru bunge mjini Dodoma. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0   Nyomi ya  mashabiki wa muziki waliofika kwenye Tamasha la Vodacom Kichuo zaidi lillilofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
   .Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul “Diamond Platinum’s” akiwaimbia kwa hisia wakati wa mashabiki wake waliofika kwenye Tamasha la Vodacom Kichuo zaidi lillilofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana.

    Msanii wa muziki wa kundi la Mafikizolo kutoka Afrika ya kusini,Theo  Kgosinkwe  akionyesha umahiri wake wa kucheza muziki  katika Tamala la Vodacom kichuo zaidi lililofanyika  chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) jana
  Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul “Diamond Platinum’s” pamoja na kundila muziki la Mafikizolo wakiimba wimbo wao wa Color of Afrika wakati wa Tamasha la Vodacom Kichuo zaidi lillilofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
  Msanii wa muziki wa kundi la Mafikizolo kutoka Afrika ya kusini,Theo  Kgosinkwe  akitumbuiza katika Tamala la Vodacom kichuo zaidi lililofanyika jana katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)

older | 1 | .... | 1217 | 1218 | (Page 1219) | 1220 | 1221 | .... | 3283 | newer