Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

KUNDI LA MUZIKI LA MAFIKIZOLO LATUA NCHINI KUWASHA MOTO KATIKA UZINDUZI WA MTANDAO WA 4G VODACOM TANZANIA

0
0
 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (wa pili kulia) akiwa na wanamuziki wakundi la Mafikizolo , Nhlanhala Nciza kulia na Theo Kgosinkwe ,(wapili kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye  Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere   jijini Dar es Salaam leo jioni kwa ajili ya kutumbuiza katika hafla ya Uzinduzi wa huduma ya Mtandao wa kasi wa 4G wa Vodacom Tanzania kesho  jioni,Utakaofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City ,Pamoja na Tamasha la Vodacom Kichuo Zaidi litakalofanyika  katika Chuo Kikuu cha UDOM Mkoa wa Dodoma Mei 12 mwaka huu.Kushotoni ni Meneja wa mwanamuziki Nasibu Abdul”.Diamond platinumz “ Sallam Sharaff.
  Mwanamuziki wa kundi la Mafikizolo,NhlanhalaNciza (kulia)  akitete jambo na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu  mara baada ya kuwasilia kwenye  Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere   jijini Dar es Salaam leo jioni kwa ajili ya kutumbuiza katika Hafla ya  Uzinduzi wa huduma ya Mtandao wa kasi wa 4G wa Vodacom Tanzania kesho jioni katika ukumbi wa Mlimani City ,Pamoja na Tamasha la Vodacom Kichuo Zaidi litakalofanyika  katika Chuo Kikuu cha UDOM Mkoa wa Dodoma Mei 12 mwaka huu.  Kushoto ni  Theo Kgosinkwe wakundi hilo na Meneja wa mwanamuziki Nasibu Abdul”.Diamond platinumz “ Sallam Sharaff.
 Mwanamuziki wa kundi la Mafikizolo kutoka Nchini afrika Kusini,NhlanhalaNciza (kulia) na mwenzake Theo Kgosinkwe, wakihojiwa na waandishi  wa habari mara baada ya kuwasili kwenye  Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere   jijini Dar es Salaam leo jioni kwa ajili ya kutumbuiza katika hafla ya Uzinduzi wa huduma ya Mtandao wa kasi wa 4G wa Vodacom Tanzania,Pamoja na Tamasha la Vodacom Kichuo Zaidi litakalofanyika katika Chuo kikuu cha  UDOM Mkoa wa Dodoma Mei 12 mwaka huu. Wapili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.



KIKAO CHA SAA TANO NZIMA KUJADILI MUSTAKABAL NA MUUNGANO WA WATANZANIA UINGEREZA

0
0
Habari na Picha za Freddy Macha, London 1- Nembo ya muda ya Jumuiya - pic by F Macha 2016 Nembo iliyopendekezwa...

Jumamosi Mchana 7 Aprili ilikuwa siku ya jua kali Uingereza. Wananchi wengi walijazana bustanini au sehemu za starehe wakiota jua na kula barafu za sukari yaani "Ice Cream." Magari yalipiga honi, wenyeji waliheushwa na ujoto ujoto huu adimu mazingira ya Ulaya. Ndani ya ofisi ya Ubalozi wa Tanzania London, kundi la Watanzania wanane lilikaa mchana wote likijadili (kwa ari na mori) maslahi ya wananchi wenzao Uingereza.
2- Kikao kikiwa motomoto- pic by F Macha 2016 Chini ya uenyekiti wa Bi Mariam Kilumanga Kikosi Kazi (Task Force – UK, juu pichani) kilichoundwa na Balozi wa zamani Uingereza Mhe Peter Kallaghe, kabla hajamaliza wakati wake hakikulegeza kamba. Mazungumzo makali yaliangalia kuhusu katiba mpya yrnyr kurasa 16. Itafanyiwa marekebisho kusimamia Jumuiya Mpya ya Watanzania Uingereza. Moja ya matumaini yake ni kuunganisha na kuendeleza maisha ya wananchi wetu nje ili kuwafaidi wao na walioko nyumbani. Hebu tazama picha na video uone taswira ilivyokuwa...

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NEWS ALERT: NAULI ZA MABASI YAENDAYO HARAKA KUANZA KUTOZWA MEI 16

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea kituo cha Mabasi yaendayo haraka cha Kamata Kariakoo leo, amesema kuwa kuanzia jumatatu Mei 16, 2016 ndio nauli za mabasi ya mwendo wa haraka zitaanza kutozwa. Pia awaasa watumiaji wa barabara hasa watembea kwa miguu, baiskeli na maguta wasitumie barabara hizo ili kuepusha usumbufu kwa madereva wa mabasi ya mwendo wa haraka. Amesema ameamua kuongeza muda wa kuanza kutoza nauli hizo kwa watumiaji wa mabasi hayo kwaajili ya kuelimisha wananchi namna ya kukata tiketi na jinsi ya kuzitumia wakati wanapoingia kwenye kituo kwaajili ya kusubiri magari.

MIVARF YAONGEZA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI ENDELEVU CHATO

0
0
Programu ya uboreshaji wa miundombinu ya masoko, uongezaji thamani mazao na huduma za kifedha vijijini (MIVARF) imefanikiwa kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi  endelevu wilayani Chato  kwa kuziwezesha kaya za vijiji hivyo kujiongezea kipato, kuboresha miundo mbinu ya masoko na kuongeza ya thamani ya zao la mpunga.

Programu hiyo imeweza kuwajengea uwezo wazalishaji wadogo na kuwaunganisha na masoko na Taasisi za kifedha, kutoa mafunzo ya uongezaji wa thamani wa mazao pamoja na ukarabati wa barabara za vijiji hivyo zinazoanzia mashambani pia na ukarabati wa ghala la kuhifadhi mazao na ujenzi wa soko la mchele.

Akiongea wakati timu ya ufuatiliaji na tathmini ya MIVARF ilipotembelea wilaya hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari alieleza kuwa wananchi 3,961  kutoka katika vijiji 12 vya kata tatu za Nyamirembe, Kigongo na Ichwankima tayari wamenufaika na utekelezaji wa Programu hiyo.
Baadhi ya wakazi wa wilayani chato wakifuatilia maelezo ya mtaalamu wa ufuatiliaji na Tathmini kutoka MIVARF, Wangael Wilfred (hayupo pichani) wilayani hapo wakati wa ufuatiliaji utekelezaji wa Programu hiyo katika wilaya hiyo.

“Programu hii imeweza kukarabati barabara zenye urefu wa kilomita 28.1 za vijijini zinazo anzia mashambani kwa gharama ya  Tsh. 1,118,235,000. Kukarabatiwa kwa barabara hizi kumepunguza gharama za kusafirisha mazao kutoka  mashambani na nyumbani hadi kwa wanunuzi kutoka Tsh 2,000 kwa gunia moja hadi Tsh1,000 kwa gunia moja.” Alisema Hari.

Hari alifafanua kuwa Programu hiyo imeweza kukarabati ghala la kuhifadhi mazao katika kijiji cha Nyamirembe ambapo ghala hilo litasaidia wakulima kuendesha mfumo wa stakabadhi ya mazao gharani suala ambalo litasaidia kukabiliana na kudorora kwa bei ya zao la mpunga hasa wakati wa mavuno.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi; Joel Hari akifafanua jambo kwa mtaalamu wa ufuatiliaji na Tathmini kutoka MIVARF, Wangael Wilfred alipofika ofisini kwake wakati wa ufuatiliaji utekelezaji wa Programu hiyo katika wilaya hiyo.

Mmoja wa wakulima wa zao la mpunga katika kata ya Kigongo, Ngavune John alifafanua kuwa kutokana na uwezo wa kilimo cha kisasa waliojengewa na MIVARF kupitia SIDO Kagera  tayari mavuno yameongezeka kutoka gunia 5 kwa ekari moja hadi gunia 25 kwa ekari moja kwa msimu wa mwaka jana  na wameunganishwa na masoko ya uhakika.

Mratibu wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wilayani humo SIDO Kagera,… alibainisha kuwa vikundi vya uzalishaji wa mpunga wilayani humo vimeunganishwa na taasisi za kifaedha kwa ajili ya kupata mikopo ya kilimo na kujiwekea akiba.

Naye mtaalumu wa Ufuatiliaji na tathmini kutoka MIVARF, Wangael Wilfred alibainisha kuwa  Programu hiyo inalenga kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa wakulima wadogo wadogo, wajasiriamali wadogo wadogo vijijini na Asasi ndogondogo za kifedha zinazotoa huduma vijijini ili kuweza kufanikisha azma ya serikali ya kupunguza umasikini na kuogeza kasi ya ukuaji wa uchumi endelevu kwa kuziwezesha kaya za vijijini kujiogeza  kipato na usalama wa chakula.
Sehemu ya ghala la kuhifadhi mazao liliokarabatiwa na MIVARF katika kijiji cha Nyamirembe wilayani Chato.
Sehemu ya soko la mchele linalojengwa na MIVARF katika kijiji cha Nyamirembe wilayani chato.

JUMLA YA SILAHA 36 ZAZUILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA

0
0
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo.
Na Woinde Shizza,Arusha
Kufuatia zoezi la kuhakiki silaha linaloendelea hapa nchini jeshi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuhakiki jumla ya silaha 2640 na jumla ya silaha 36 zilizosalimishwa zimefutiwa leseni za umiliki kutokana na sababu mbalimbali .

Akiongelea swala hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa silaha silaha hizo zimebaki chini ya uangalizi wa jeshi la polisi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo na baadhi ya wamiliki kupitisha umri wa kumiliki silaha ,wengine wakiwa wagonjwa pamoja na wengine kukosa sifa ya kumiliki silaha hizo.

Alisema kuwa umri wa kumiliki silaha mwisho ni miaka 70 ambapo kuna baadhi ya wananchi ambao walikuwa wanamiliki silaha hizo tayari wameshafikia ukomo wa umri wa kumiliki silaha hizo kisheria.

Aidha alisema pia kuna baadhi ya watu ambao walikuwa wanamiliki silaha zaidi ya moja bila sababu yeyote nao wamenyang’anywa huku wengine wakiwa wamechukuwa silaha hizo bila kujua matumizi halali ya umiliki wa silaha hizo.

Alitaja aina ya silaha ya silaha mbalimbali ambazo tayari zimekaguliwa na kukabidhiwa kwa wamiliki kuwa ni bastola 1434,Raifo 540 pamoja na Shortigun 666.

Alisema kuwa jeshi la polisi bado linaendelea kuhakiki silaha hizo hivyo wananchi wote ambao wanamiliki silaha wajitokeze na silaha zao kwa ajili ya kuhakikiwa kwani zoezi likiisha wataanza upekuzi wa silaha zote ambazo hazijahakikiwa na mtu akikutwa nayo akiwa ajahakiki ataokana ametenda kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria .

Mkumbo pia aliwasihi watu wote ambao wanataka kumiliki silaha kwenda kupata mafunzo kwanza kabla ya kukabidhiwa silaha na ambaye amesahamu matumizi ya silaha basi arudi kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi juu ya matumizi sahihi ya silaha.

Serikali kuwaunga mkono Wananchi wa Busiri katika uchimbaji madini.

0
0
Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI imewaunga mkono Wachimbaji Wadogo wa Madini wa Busiri kwa kuwatafutia maeneo ya uchimbaji wa madini, ambapo Wizara ya Nishati na Madini imetenga eneo lenye ukubwa wa hekta 11,031 lililokuwa chini ya Leseni za Utafutaji namba PL 3220/2005 ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Bw. Daudi Mbaga pamoja na PL 5853/2009 iliyokuwa ikimilikiwa na na Meru Minerals Resources Limited ambazo zilizoisha muda wake.

Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Medard Kalemani wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi kuhusu mikakati ya Serikali ya kuwaunga mkono Wachimbaji wadogo wadogo wa Busiri.

Mhe. Kalemani ameeleza kuwa, hadi mwishoni mwa mwezi Machi, 2016, Wizara yake imegawa kwa wananchi wa Busiri leseni 81 za Uchimbaji Mdogo wa Madini (PMLs) katika eneo hilo, sawa na takribani hekta 810 kati ya hekta 11,031 za eneo lililoachwa kwa ajili ya Wachimbaji Wadogo.

“Wizara imegawa leseni nyingine 30 za uchimbaji mdogo (PMLs) katika eneo lililopo katika kijiji cha Kuntakama takribani kilomita moja eneo la uchimbaji mdogo wa madini la Busiri”, alisema, Mhe. Kalemani.

Ameongeza kuwa, mkakati mwingine wa Serikali ni kuendelea kulitumia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kutoa huduma ya ugani kwa wachimbaji madini wadogo wa kijiji cha Busiri na wengine wote nchini ikiwemo kutoa ruzuku kupitia Mfuko wa Wachimbaji Wadogo.

“STAMICO pia itaendelea kuwapa elimu wachimbaji wadogo na kuwahamasisha kuunda Vikundi vya Uchimbaji ili waweze kusaidiwa kwa pamoja”, alisema Mhe. Kalemani.

Aidha, Serikali imekuwa ikiwatembelea wachimbaji madini wa eneo tajwa mara kwa mara kwa kutumia Maafisa na Wataalamu wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi-Bukoba.

Amefafanua kuwa, tarehe 11 Machi, 2016 Afisa Madini Mkazi wa Bukoba alifika na kufanya mkutano na kikundi cha Busiri Mining Co-operative Society Limited chenye Leseni Na. PML 001712WLZ.

“Ili kutekeleza ombi la sasa la Mheshimiwa Mbunge, Wizara yangu itamtuma Afisa Madini wa Kanda ili awatembelee tena na kuwaelimisha juu ya fursa zilizopo za kuendeleza wachimbaji wadogo ili uchimbaji uwe wenye tija na kutoa ajira na kuondoa umaskini kupitia uchimbaji wa madini”, aliongeza, Mhe. Kalemani.

KAMPUNI YA PIZZA HUT YAZINDUA MGAHAWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

0
0


Balozi wa Marekani hapa nchini, Mark Childress katikati akikata utepe kuzindua Mgahawa wa Pizza Hut jijini Dar es Salaam.
 Mgahawa wa Pizza Hut upo katika maeneo ya Mkuki Mall Kariakoo.
  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Pizza Hut Afrika, Randall BlackFord akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusherekea ufunguzi wa Mgahawa wa Pizza hut ambao ni wa miamoja duniani kwa kupeleka pizza kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro. Amesema kuwa huduma ya kupeleka izza katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kitatimiza rekodi ya dunia ya Gines kwa kutoa piza katika urefu wa juu kabisa.


BENKI YA CRDB WAELIMISHA WATEJA WAKE KUTUMIA INTANETI BENKI.

0
0
 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Vijana, Pales Fungo akizungumza na wafanyakazi wa Benki ya CRDB wa matawi matatu tofauti jijini Dar es Salaam wakati wa kuwapa mafunzo ya benki kwa njia ya Mtandao(Internet Banking.)

Kutoka kushoto ni Msimamizi wa benki ya CRDB kwa njia ya mtandao(Internet Banking), Sarah Nzowa, Meneja wa benki ya CRDB tawi la Water Front,Donath Shirima na Meneja wa njia mbadala wa Benki ya CRDB, Hamis Mhini  wakimsikiliza Meneja wa maswala ya mtandao(Internet Banking) wa Benki ya CRDB, Mangire Kibanda.Meneja wa maswala ya mtandao(Internet Banking) wa Benki ya CRDB, Mangire Kibanda (aliye simama) kifafanua jinsi ya kutumia mtandao wa intaneti  yaani (Internet Banking) jijini Dar es Salaam.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

RAIS AMETEUA WAKURUGENZI WA BODI YA SHIRIKA LA MAKUMBUSHO YA TAIFA,TAFORI NA TTB.

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII.
UTEUZI WA WENYEVITI NA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA LA MAKUMBUSHO YA TAIFA, TAASISI YA UTAFITI WA MISITU TANZANIA (TAFORI) NA BODI YA UTALII TANZANIA (TTB).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Makumbusho ya Taifa, Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Katika uteuzi huo Mhe. Rais amemteua Bi. Anna Abdallah (Mbunge Mstaafu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Makumbusho ya Taifa, Dkt. Felician Kilahama (Mbobezi katika fani ya Misitu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Kufuatia uteuzi huo wa Mhe. Rais, Waziri wa Maliasili na Utalii kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Shirika la Makumbusho ya Taifa Sura ya 281 kifungu cha 4(2) kikisomwa pamoja na Jedwali aya ya (1a) amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi hiyo; 

1.Dkt. Amina Amer Issa, Mkurugenzi wa Makumbusho, Nyaraka na Mambo ya Kale Zanzibar.
2.Dkt. Ali S. Mcharazo, Mkurugenzi wa Tanzania Library Services, Dar es Salaam.
3.Prof. Godius Kahyala, Dean, College of Arts and Social Sciences, University of Dar es Salaam.
4. Prof. Thomas J. Lyimo, Dean, Faculty of Science University of Dar es Salaam.
5.Dkt. Oswald Masebo, Mhadhiri, Mkuu wa Idara ya Historia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
6.Bw. Lota Melamari, Consult, Management of Natural Resources and      Environment and Coordinator of Tanga Botanical Gardens, Arusha.
7.Dkt. Anna M. Kishe, Mtaalam wa lugha za Kiswahili na Kiingereza na      Mhadhiri katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dar es Salaam.
8.Bw. Donatius M. Kamamba, Mkurugenzi wa Mambo ya Kale, Wizara ya Maliasili na Utalii.

Aidha, kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) Sura ya 277 kifungu cha 6(2) kikisomwa pamoja na Jedwali la 2 (1)(a), Mhe. Waziri amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi hiyo; 

1.Prof. Salim Maliondo, Profesa wa Biologia ya Misitu  Chuo  Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
2.Dkt. Susana Augustino, Mhadhiri Mwandamizi matumizi ya mazao ya misitu, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
3.Bw. Deusdedit Bwoyo, Kaimu Mkuruenzi Msaidizi, Maendeleo ya Misitu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dar es Salaam.
4.   Prof. Dismas L. Mwaseba, Director of SUA Centre for Sustainable Rural Development (SCSRD), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
5.Bw. Charles Maguta Kajege, Business Consulatant (Finance), Dar es Salaam.
6.Dkt. Lemayon Melyoki Mkurugenzi, Shule ya Ujasiriamali, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
7.Dkt. Tuli S. Msuya, Katibu Tawala, Mfuko wa Misitu Tanzania, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dar es Salaam.
8. Dkt. Emma Liwenga, Mtafiti Mwandamizi, Taasisi ya Tathmini ya Maliasili (IRA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
9.Dkt. Lawrence Mbwambo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Morogoro.

Pia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Bodi ya Utalii Tanzania Sura ya 364 kifungu cha 3(2) kikisomwa pamoja na Jedwali 1(2), Mhe. Waziri amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi hiyo; 

1.Bw. Ibrahim Mussa, Mkurugenzi wa Masoko, TANAPA
2. Balozi Joseph Sokoine Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.
3. Bw. Mark Leveri, Mtaalam wa kutengeneza filamu na matangazo ya       video, Ex. Tanzania Film Company.
4. Bw. Richard Rugimbana, Mtendaji Mkuu Tanzania Confederation of Tourism (TCT).
5. Bibi. Zabein Muhaji Mhita, Mbunge Mstaafu na Mkurugenzi wa Elimu ya  Msingi Mstaafu.
6.Agustine Kungu H. Olal, Kamishna Msaidizi wa Sera na Uchumi, Wizara ya Fedha na Mipango.

Uteuzi wa Wenyeviti na Wajumbe hao ni wa muda wa miaka mitatu kuanzia tarehe 24/04/2016 hadi tarehe 23/04/2019.
IMETOLEWA NA:
Angelina E.A. Madete
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
11 Mei, 2016.

MAKACHERO FEKI WA TAKUKURU KUFUATILIA ZOEZI LA SUKARI.

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
Tangu kuanza kwa zoezi la kufuatilia wafanyabiashara wanaoficha sukari kwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh. Dr John Pombe Magufuli, kumekuwa na wimbi la watu wanaojiita “makachero wa TAKUKURU  kutoka Makao Makuu” nao wakifuatilia sakata la sukari mkoani Kilimanjaro.

Matapeli  hao ambao kwa sasa wapo  wilayani  SIHA, wamekuwa wakiwasumbua   wafanya biashara kwa kudai kuwa  wametumwa kuwashughulikia huku wakiomba kupewa  fedha ili wawasafishe. Kiasi cha fedha ambacho kimekuwa kikiombwa ni kati ya Shilingi 150,000/= hadi 500,000/= kama “gharama ya kuwasafisha kwa Mheshimiwa Rais”

Naomba  wafanya baiashara  Mkoani Kilimanjaro waelewe kwamba, TAKUKURU inao mfumo wa utendaji kazi ambao unajali misingi ya utawala bora na kamwe haihusiki na utapeli wa aina hii. TAKUKURU katika utendaji wake wa kazi, haiwatozi wafanya biashara fedha kama adhabu kwa kuhifadhi sukari kinyume na taratibu. TAKUKURU  inafuatilia, kuhoji na kumtaka mfanyabiashara kuonesha namna  anavyomiliki sukari hiyo kwa kutoa vielelezo husika. Mwisho wa zoezi hili, atakayetoa tamko ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

 Ifahamike kuwa hakuna afisa wa TAKUKURU mpaka sasa aliyetumwa kutoka Makao Makuu kuja mkoani Kilimanjaro kufuatilia zoezi la sukari. Zoezi hili mkoani hapa linaendeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama kama timu moja na wala halifanywi na TAKUKURU pekee .

Ifahamike pia kuwa hakuna zoezi linaloihusisha TAKUKURU litakaloendeshwa mkoani bila ofisi ya mkoa kuwa na taarifa. Kwa misingi hiyo yeyote anayeendesha zoezi hilo nje ya utaratibu nilioufafanua ni tapeli, taarifa zake zitolewe mapema ili akamatwe na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Maofisa wote kutoka ofisi ya TAKUKURU mkoa wanavyo vitambulisho na kama watatiliwa shaka basi ofisi yangu ijulishwe kupitia simu namba   0784 998 804 au 0786 089 805 muda wowote.                                                                 
                                                                 IMETOLEWA NA                                                                   
ALEX J KUHANDA
MKUU WA TAKUKURU  MKOA WA KILIMANJARO
11/5/2106.

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA.

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Uutumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge Iringa Mjini, Mhe. Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari wakiwapungia mkono Wapiga picha (hawapo pichani wakati wakiingia Bungeni kwa ajili ya vikao vinavyoendelea mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akifurahiua jambo pamoja na Wabunge wenzie nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
(Picha zote na Benedict Liwenga, Dodoma)

WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO WAIOMBA SERIKALI KUWAPA MAENEO YANAYOWAFAA.

TANZANIA KUENDELEA KUZINGATIA HAKI ZA BINADAMU- PROF MCHOME.

0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome akiwasilisha Taarifa ya Serikali ya Tanzania ya Mapitio ya Hali ya Hali za Binadamu mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva -Uswisi.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome akipewa mikono ya pongezi mara baada ya Tanzania kuwasilisha Taarifa yake ya Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva -Uswisi.
Ujumbe wa Tanzania  katika picha ya pamoja mara baada ya Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome kuwasilisha Taarifa ya nchi ya Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva -Uswisi.

Tanzania imeahidi kutekeleza ahadi yake kuhusu Haki za Binadamu kama ilivyotajwa katika Katiba ya nchi na kuridhia kwake kwa Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za  Binadamu na kuiomba jumuiya ya kimataifa iunge mkono juhudi zinazofanywa na Tanzania katika kukuza na kulinda haki za binadamu.

Kauli hiyo imetolewa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome alipokuwa akiwasilisha taarifa ya Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu katika Mkutano wa 25 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa unaofanyika nchini Uswis.

Akiwasilisha taarifa hiyo Prof Mchome alisema Tanzania imefanya mambo makubwa nane ndani ya kipindi cha mapatio ya hali ya haki za binadamu ambayo nchi inajivunia kutokana na kufanyika kwake  Aliyataja mambo hayo kuwa ni Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Mchakato wa Mapitio ya Katiba,uwepo wa haki ya kufanya kazi, hifadhi wa jamii na faida za kiuchumi. Mengine ni uwepo wa haki ya faragha na ulinzi binafsi, haki ya afya ambapo mpango wa kitaifa wa kuzuia na kujikinga na malaria2014-2020 ulianzishwa na Zanzibar kutokomeza malaria , uwepo wa haki ya kuwa na mazingira safi na salama na kutimiza matakwa ya kimataifa ya haki za binadamu.

Akiongelea utekelezaji wa mapendekezo 107 ambayo Tanzania iliyachukua kutoka katika kikao kilichopita Prof Mchome alisema kuwa mapendekezo hayo yaligawanywa katika makundi 23 na kusambazwa kwa wadau mbalimbali kwa ajili ya kuyafanyia kazi na baadae yaliingizwa katika Mpango kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu ili kurahisisha utekelezaji wake. 

Taarifa hiyo inaeleza kwamba mapendekezo mengine yaliyotekelezwa Serikali ni pamoja na kuridhia na kutunga sheria kwa ajili ya utekelezaji wa mikatba ya Kimataifa kuhusu haki za binadamu,m  kuimarisha Taasisi inayoshughulikia masuala ya haki za binadamu, haki za wanawake,kutambua watu wenye ulemavu kwa umri, jinsia na maeneo wanayoishi ambao walitambulika kupitia sense ya mwaka 2012.

Mengine ni kutokomeza mauaji ya watu wenye walemavu wa ngozi, kupambana na biashara haramu ya binadamu, kusimamia haki za watoto, watoto wa mitaani, ajira kwa watoto,upatikanaji wa elimu, afya na maji safi na salama, uhuru wa kujieleza na kujumuika , kuboresha hali za magereza, mahusiano na asasi za kiraia na majukumu ya makampuni kwa jamii.

Taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo ya haki za binadamu kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa hutolewa kila baada ya niaka mitano baada ya nchi husika kukubali na kutekeleza mapendekezo hayo na kuangalia namna utekelezaji wake ulivyofanyika.

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE

0
0

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akionyeshwa barabara zinazopishana juu na chini na Meneja wa Ujenzi wa Daraja la Nyerere Mhandisi Karim Mataka wakati alipofanya ziara katika daraja hilo jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Ziara ya Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Nchini Uingereza na Ujio wa Mh. Balozi Mpya Dr. Asha Rose Mtengeti Migiro


VIKUNDI 39 VYA WANAWAKE WILAYANI MOROGORO VYAPATIWA MIKOPO YA SHILINGI MILIONI 23.8

0
0

Na Benedict Liwenga, 
MAELEZO, Dodoma.

Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imeviwezesha Vikundi 39 vya Wanawake pamoja na Vijana vyenye wanachama 295 kupatiwa mikopo ya jumla ya shilingi milioni 23.8 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Wanawake.
Taarifa hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo (Mb) wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, Mhe. Tebweta Omary lililotaka kujua mpango wa Serikali wa kuzibana na kuziamuru Hallmashauri zote ikiwemo ya Morogoro Vijijini kutenga asilimia 5 ya fedha za mapato ya ndani kwa Vijana na asilimia 5 kwa ajili ya akina mama.

Mhe. Jafo amesema kuwa, katika mwaka wa fedha wa 2015/16, Serikali imetenga shilingi milioni 175 kwa ajili ya wanawake na vijana kutokana na mapato ya ndani.
Amefafanua kuwa, mkakati wa sasa wa Serikali ni kuimarisha makusanyo ya mapato ili kujenga uwezo wa kutenga fedha zaidi ambapo katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/17 sharti la kupitisha makisio ya bajeti ya kila Halmashauri lilikuwa ni kuonyesha asilimia 10 zilizotengwa kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Wanawake kutokana na mapato ya ndani.
"Halmashauri zote zimeagizwa kuhakikisha fedha hizo zinapelekwa kwenye vikundi husika ikijumuisha walemavu na kusimamia marejesho yake ili vikundi vingine viweze kunufaika.
Kwa upande mwingine, Mhe. Jafo amejibu swali la Mbunge wa Geita Mjini, Mhe. Kanyasu Costantine John ambaye alitaka kujua kwanini Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankimbo imabaki kuwa shule ya Kutwa wakati mazingira yake yanafaa kuwa sekondari ya Bweni ambapo alijibu kuwa shule hiyo ilijengwa chini ya Mradi wa Geita Giold Mining na kupata usajili wa Na. S.1942 mwaka 2006 ikiwa ni shule ya kutwa kwa kidato cha Kwanza hadi cha Nne.
Aidha, amesema kuwa mwaka 2012 shule hiyo iliongezewa kidato cha Tano na Sita hali iliyoifanya shule hiyo kuwa imesajiliwa ya kutwa kwa kidato cha kwanza hadi cha nne na Bweni kwa kidato cha Tano na Sita. "Taratibu zilizotumika ili kuisajili shule kuwa ya bweni ni Halmashauri yenyewe kuwasilisha maombi Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ili kupata kibali", alisema Mhe. Jafo.

Aliongeza kuwa, kabla ya kupata usajili, Kamishna wa Elimu atatuma Timu ya Wataalam katika shule husika kwa ajili ya kuhakiki uwepo wa miundombinu inayohitajika ilio shule iweze kusajiliwa kuwa ya bweni.

UONGOZI INSTITUTE: In Focus with Hon. Justice Augustine Ramadhani

GREEN VOICES WASAIDIA KILIMO CHA UYOGA DAR

0
0
WAKATI Magdalena Bukuku anaibua wazo la kilimo cha uyoga akiwa mafunzoni jijini Madrid, Hispania mapema mwaka huu 2016 hakutegemea kama angeweza kupata mwitikio mkubwa kutoka kwa akinamama wa maeneo ya Boko na Bunju jijini Dar es Salaam anakoishi.

Lakini leo hii, Magdalena, ambaye ni miongoni mwa akinamama 15 wanaotekeleza Mradi wa Green Voices maalum kwa kupaza sauti za wanawake kwa ajili ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi, anafarijika baada ya wazo lake hilo kuzaa matunda.

Tayari wanakikundi cha ‘Tunza Women Group’ cha Bunju wameanza kuvuna kidogo kidogo uyoga ikiwa ni takriban mwezi mmoja tu tangu walipopatiwa mafunzo, huku wale wa Boko wakiwa katika hatua nzuri za kuendeleza shamba lao.

“Ni mradi mzuri, unatumia gharama kidogo huku mavuno yake yakiwa endelevu hasa ukiwa na nia, dhamira na jitihada, hapa Bunju tayari akinamama wameanza kuvuna uyoga, ambao soko lake lipo kubwa,” anaeleza Magdalena.

Magdalena ni mmoja wa akinamama wanaotekeleza kwa vitendo mradi wa Green Voices, ambao unafadhiliwa na taasisi inayojihusisha na maendeleo ya wanawake wa Afrika, ijulikanayo kama Foundation for Women of Africa inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, María Teresa Fernández de la Vega.

Akinamama wengine wanatekeleza miradi mbalimbali ya ujasiriamali unaoendana na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Kigoma, Kilimanjaro, Pwani na Mwanza.Anasema, uyoga ni zao linalohitaji eneo dogo na matumizi kidogo lakini endelevu ya rasilimali maji, hivyo kuwa rafiki mkubwa wa mazingira licha ya umuhimu wake kwa afya ya binadamu.
Bi. Esther Chiombola akionyesha uyoga ambao uko tayari kuvunwa. Uyoga huo unalimwa na kikundi cha Tunza Women Group cha Bunju jijini Dar es Salaam kwa ufadhili wa mradi wa Green Voices (Makala na Picha zimeandaliwa na www.brotherdanny.com).
Bi. Sauda Issa miaka 70 (kushoto) mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam akipokea zawadi ya kitabu maalum kinachozungumzia kilimo cha uyoga kutoka kwa Bi. Esther Chiombola ambaye ni Ofisa Kilimo Msaidizi Mwandamizi wa Manispaa ya Kinondoni.
Mratibu wa vikundi vya kilimo cha uyoga Bunju na Boko, Magdalena Bukuku (katikati) akiteta jambo na mratibu wa green Voices nchini Bi. Secelela Balisidya wakati wa uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na Green Voices. Wengine pichani kutoka kushoto ni Bi. Lucresia Tarimo aliyemwakilisha Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Kinondoni, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilungule Seif Stambuli, na Ofisa Kilimo Kata ya Bunju, Rhoda Mruttu. 
Bi. Sophia Chove, mwenyekiti wa kikundi cha wakulima wa uyoga Bunju, akitoa maelekezo kwa watu mbalimbali kuhusu namna ya uchanganyaji wa vimeng’enyo vya kuoteshea na kukuzia uyoga. 

JWTZ LAANDAA SEMINA YA WAKUU WA KAMANDA WA MAJESHI YA NCHI KAVU AFRIKA

0
0
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa kutakuwa na Semina ya wiki moja ya Wakuu wa Kamandi wa majeshi ya Nchi kavu Afrika itakayoendeshwa Mkoani Arusha katika Hoteli ya Mount Meru kuanzia tarehe 13 hadi 19, Mei 2016.

Lengo la Semina hiyo ni kuwakutanisha Wakuu wa kamandi hizo Afrika ili kujadili na kuendeleza ushirikiano katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayolikabili bara la Afrika katika Nyanja ya ulinzi.

Kauli Mbiu ya Semina hiyo ni Ujenzi wa Usalama Afrika kupitia Ushirikiano.

Semina hii hufanyika kila mwaka katika mojawapo ya nchi za Afrika, ili kuwajengea makamanda hao ushirikiano katika kutatua changamoto mbalimbali za kiulinzi zinazotokana na mabadiliko katika Nyanja za kiusalama.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.

SERIKALI KUSHINDANISHA WAWEKEZAJI SEKTA YA NISHATI

0
0
Na Veronica Simba
Serikali imesema ushindani kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika sekta ya nishati, ndiyo njia bora zaidi itakayowezesha kuwapata wawekezaji wenye vigezo vinavyotakiwa.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliyasema hayo jana, Mei 10, alipokutana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO kutoka Japan, Norio Shoji na Ujumbe wake, ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika uzalishaji na usafirishaji wa umeme nchini, kwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwemo gesi asilia na jua.

“Kampuni nyingi zimeonesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya nishati. Serikali inao uhitaji mkubwa wa wawekezaji walio makini, hivyo tunahitaji kuwapata wawekezaji wenye vigezo kwa kutumia ushindani unaozingatia uwazi,” alisisitiza Profesa Muhongo.

Aliongeza kuwa, ili kuwarahisishia wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya nishati nchini, Wizara inaandaa taarifa maalum itakayobainisha maeneo yanayohitaji uwekezaji pamoja na vipaumbele vyake.
“Endapo tutaendesha zoezi la ushindanishaji wawekezaji na wote walioshindanishwa wasipotimiza vigezo vinavyotakiwa, hatulazimiki kumchukua yeyote tu. Tutakachofanya ni kutokumchukua yeyote kati yao na hivyo kuendelea na zoezi hilo baada ya muda tutakaoubainisha, hadi pale tutakapowapata wawekezaji wenye vigezo tunavyovitaka.”

Profesa Muhongo alibainisha kuwa, mchanganyiko wa nishati ambao Serikali imekusudia kuutumia kama vyanzo vya kuzalisha umeme nchini kwa sasa ni pamoja na gesi asilia, maji, upepo, jua, makaa ya mawe, mvuke (maji moto) na tungamotaka.

 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kushoto), akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO kutoka Japan, Norio Shoji (Kulia) pamoja na Ujumbe wake, baada ya kikao baina yao. Kushoto kwa Waziri ni baadhi ya Viongozi na Maofisa wa Wizara na Taasisi zake walioshiriki kikao hicho kilichofanyika Mei 10, mwaka huu Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam. KOYO imeonesha nia kuwekeza katika sekta ya nishati nchini.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo (Kulia), akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO kutoka Japan, Norio Shoji, baada ya kikao baina ya Waziri wa Nishati wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Kampuni husika, kilichofanyika Mei 10 mwaka huu Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam. Kampuni ya KOYO imeonesha nia kuwekeza katika sekta ya nishati nchini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Katikati), akiwa katika kikao na Ujumbe kutoka Kampuni ya KOYO ya Japan (Kushoto). Kulia ni baadhi ya Viongozi na Maofisa wa Wizara na Taasisi zake walioshiriki kikao hicho kilichofanyika Mei 10 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo imeonesha nia kuwekeza katika sekta ya nishati nchini.





Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images