Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1209 | 1210 | (Page 1211) | 1212 | 1213 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekabidhi kituo cha Uchunguzi na Matibabu kwa Hospitali ya Rufaa Dodoma kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kupata huduma bora za matibabu.

  Kituo hicho kimekabidhiwa leo mkoani Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Benard Konga kikiwa na lengo la kuwapa wananchi huduma bora za matibabu na kuweka wataalamu wenye uzoefu ili iwe ni sehemu ya kujifunzia kwa wataalamu wa kada mbalimbali za udaktari.

  “Kituo hiki kimejengwa kisasa kwa kuwekewa mfumo wa kisasa wa miito ya manesi (Nurse Call System), jengo la jenereta na transfoma kwa ajili ya kuwa na umeme wa uhakika masaa yote, mifumo ya kisasa ya vipooza hewa, sehemu ya mapokezi, sehemu ya kutolea dawa, sehemu ya dharura, maabara, vyumba vya uchunguzi, vyumba vya Madaktari, chumba cha upasuaji, chumba cha wagonjwa mahututi, kliniki mbalimbali,sehemu za kulaza wagonjwazenye jumla ya vitanda 34 pamoja na Jengo la mgahawa kwa ajili ya huduma ya chakula”alisema Konga.

  Konga ameongeza kuwa kuna baadhi ya shughuli za ujenzi zinaendelea kukamilishwa lakini haziwezi kuzuia kuanza kufanya kazi kwa kituo hicho kwa sababu huduma hizo zinapatikana katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ambayo inasimamia kituo hiko.

  Aidha, Konga amezitaja baadhi ya shughuli za ujenzi zinazoendelea zikiwemo jengo la kuhifadhia maiti, ujenzi wa sehemu ya kufulia nguo pamoja na sehemu ya kuchomea taka ambazo amekiri kuwa hazitachukua mda mrefu kukamilika kwakua fedha za ujenzi huo zilishatengwa.

  Amefafanua kuwa Mfuko huu una mpango wa kuimarisha huduma kwa kujenga vituo kamahivi katika kila Kanda na kwa mwaka wa fedha 2016/2017 mfuko umepanga kujenga kituo kama hiki mkoani Kigoma.Mradi wa ujenzi wa Kituo hicho ulianza mwezi Oktoba, 2009 ambapo ujenzi wa jengo umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 6.Jumla ya shilingi Bilioni 2 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya vifaa tiba na samani.

  0 0  0 0

  Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza


  0 0

  Vyombo vya habari vya asilia, hususan magazeti,  vinakufa. Hivi sasa vvyombo hivyo vinajikongoja kutokana na  mauzo hafifu  na mdororo wa mapato kutoka matangazo na kupunguza wafanyakazi. 
  Ila wakati idadi ya wasomaji wa habari mtandaoni ikizidi kukua, wanaoperuzi mtandaoni  humo hawatumii muda mwingi kwenye magazeti tando, utafiti wa Pew Research Centre unaeleza. 

  Katika utafiti wake wa hali ya vyombo vya habari 2015 ("State of the News Media 2015,”) imeonesha kwamba katika vyombo vya habari vya karatasi (print media), Digitali na TV, imeonesha Dhahiri kwamba magazeti yanaelekea kuzimu. 
  Utafiti huo umetolea mfano magazeti makubwa ambapo wasomaji wake wa mtandaoni wamewashinda kwa mbali kwa idadi ya wasomaji wa makaratasini, ambapo gazeti kubwa sana la New York Times la Marekani limetangaza kuwa nakala zake zipatazo 650,000 kwa wiki zimepitwa kwa mbali sana na wa mitandaoni .
   Hivi sasa kuna mjadala mitandaoni endapo kama Tanzania iko ama itafika huko. Mabishano ni makali ambapo wa makaratasini wanashikilia msimamo wao kuwa nchini hapa tasni ya habari mtandaoni bado ni changa sana kuweza kutishia amani ya magazeti. 
  Upande wa digitali unajibu kwamba endapo kama kuna wahariri viburi wanaobeza kasi ya mitandao, basi wakae mkao wa kulala njaa muda si mrefu ujao, maana ni wachache wanaoendelea kupata habari kwa njia asili ya magazeti. 
  Upande wa digitali umeyasifia magazeti ya Global Publishers na la Mwananchi  anbayo ni dhahiri yana wahariri wanaokwenda na wakati na wanaojua nini wanachokifanya kwa kuanza na mapema kuogelea bahari ya maendeleo ya tasnia kwa vitendo kwa kuwa na vitengo vya mtandao vinavyopelekesha mbio magazeti yanayobeza technolojia hio kwa kubuni. 
  "Ni kweli kwamba Tanzania ni bado sana kiteknolojia na miundombinu kiasi cha habari za mtandaoni zikatishia uhai wa habari za makaratasini, lakini si uwongo kwamba ukizingatia uharaka na gharama pamoja na kwenda na wakati muda si mrefu print media itakwenda na maji", amesema blogger mmoja ambaye pia ni mwanahabari kwenye moja ya magazeti makubwa nchini.


  0 0

  Na Eliphace Marwa MAELEZO

  Jeshi la polisi Mkoa wa kipolisi Ilala limewahakikishia usalama wananchi wa Mkoa wa kipolisi Ilala  na kuachana na taarifa za uvumi kuhusu hali ya usalama katika mkoa huo wa kipolisi.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya  amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga ipasavyo kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote na kutoa tahadhari kwa wahalifu kuwa makini kwani jeshi lake limejidhatiti ipasavyo.

  “Niwahakishie wananchi kuwa hali ya ulinzi iko vizuri na jeshi la polisi Mkoa wa Ilala limejipanga vizuri hivyo wananchi wawe na amani kwani tunafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha hali ya amani na utulivu inakuwepo wakati wote”, alisema Kamanda Mkondya.

  Aidha kuhusiana na malalamiko ya wananchi wa Buguruni kuhusiana na kuwepo kwa kundi la vibaka na waporaji kamanda Mkondya amesema kuwa Jeshi lake linaendelea na operesheni ya kukamata wahalifu usiku na mchana ili kuhakikisha Mkoa wa kipolisi wa Ilala unakuwa salama ambapo mpaka sasa jeshi hilo linawashikilia baadhi ya wahalifu waliokuwa vinara wa uporaji eneo la Buguruni Chama.

  “Mpaka sasa tunawashikilia vijana kadhaa ambao walikuwa ni kero katika eneo la Buguruni chama na maeneo mengine ya Mkoa wa Ilala”, aliongeza Kamanda Mkondya.

  Kwa upande wake Afisa habari wa Manispaa ya Ilala Bw. David Langa amesema kuwa Manispaa yake kwa kushiriana na Jeshi la Polisi wako katika mkakati wa kuanza operesheni ya kuwaondoa wapiga debe ambao wamekuwa wakishtumiwa na wananchi kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika sehemu mbalimbali za Manispaa ya Ilala.

  Aidha Kamanda Mkondya amewataka wakazi wa Ilala kutoa taarifa za kihalifu kwa jeshi lake ili kuweza  kuifanya Ilala kuwa salama na kutimiza dhana ya ulinzi shirikishi.

  0 0

  Na John Gagarini, Kibaha.

  JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Frowin Peter Mbwale (miaka 26, pichani chini) mkazi wa Kawe Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuwa ua kwa kuwachinja mkewe Oliver Erasto (23) na mtoto wake Emanuel Frowin (3) kutokana na wivu wa mapenzi.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Bonaventura Mushongi alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 10:30 usiku eneo la Zinga kata ya Dunda Tarafa ya Mwambao wilayani Bagamoyo.
  Mushongi alisema kuwa katika hali isiyo kuwa ya kawaida juzi siku ya tukio mtuhumiwa akiwa na mwenzake alijulikana kwa jina la Rajabu Juma (20) Mkazi wa Makongo Jijini Dar es Salaam waliwaua watu hao kwenye vichaka vilivyopo kwenye eneo hilo la Kaole.
  “Muda huo mtuhumiwa akiwa na mwenzake alimhadaa mke wake kuwa waende kwenye nyumba yao ambayo inaendelea kujengwa kwa lengo la kuitazama ambapo mke wake alikubali na kumbeba na mtoto wao na kwenda huko ambako aliwachinja shingoni,” alisema Kamanda Mushongi.

  Alisema kuwa mtuhumiwa kumbe lengo lake halikuwa kuangalia ujenzi wa nyumba yao huko Kaole kumbe alikuwa na lengo lingine la kufanya unyama huo ambao aliutekeleza akiwa na rafiki yake huyo ambaye walishirikiana kumchinja mke na mtoto wake.
  “Chanzo cha mauaji hayo ni mtuhumiwa huyo alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa ana uhusiano na mwanaume mwingine aitwaye Hamza mkazi wa Kawe Jijini Dar es Salaam na kusababisha mauaji hayo ya kusikitisha ambayo yamewaumiza watu wengi,” alisema Mushongi.
  Alibainisha kuwa miili ya marehemu hao ilikutwa ikiwa imechinjwa na watu hao umbali wa mita 100 kutoka barabara ya magari itokayo Kaole kwenda eneo la Mbegani.
  Aidha alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa majira ya saa 3:30 usiku baada ya wananchi Zinga kuwatilia mashaka walipokuwa wakijaribu kutaka kutoroka na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika, miili ya marehemu imehifadhiw akwenye Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo kusubiri ndugu kwa ajili ya mazishi.

  0 0

  Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.
  SERIKALI inaendelea kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli ili kuchangia upatikanaji wa fedha za kusaidia kuimarisha na kuendeleza miradi ya maendeleo nchini. 

  Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imekuwa miongoni mwa taasisi za Serikali ambayo imeanza kukusanya ada zote zitokanazo na huduma inazotoa kwa njia ya kielekroniki kwa wadau wake kufanya malipo kwa njia ya simu au benki kabala ya kupata huduma wanayohitaji.

  Hayo yamebainishwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harisson Mwakyembe alipokuwa akiwasilisha mpango wa makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

  “Tayari wilaya 114 kati ya 139 zinakusanya maduhuli kwa njia ya kielekroniki na kwamba ifikapo Juni, 2016 wilaya zote Tanzania Bara zitakuwa zinatumia njia ya kielekroniki kukusanya maduhuli” alisema Dkt. Mwakyembe.

  Katika kuongeza mapato, Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa upo mkakati wa kuongeza kiwango cha usajili wa vizazi na vifo nchini, ambapo RITA imeanzisha kampeni ya usajili inayoambatana na uboreshaji wa mfumo wa usajili kwa kuweka mfumo wa kompyuta kila wilaya ambapo kampeni hizo zilifanyika.

  Wilaya ambazo kampeni hizo zimefanyika ni Arusha na Arumeru ambapo jumla ya watu 49,548 wamesajiliwa na kupewa vyeti vyao vya kuzaliwa.

  Zoezi hilo la usajili linaendelea katika wilaya ya Kahama na baadaye litaendelea katika wilaya 16 nchini ambazo ni Bariadi, Chato, Dodoma, Igunga, Kilombero, Kilosa, Lushoto, Maswa, Mbinga, Misungwi, Mtwara, Muleba, Nzega, Shinyanga, Sumbawanga na Tunduru.

  Waziri Mwakyembe alibainisha kuwa Wizara hiyo kupitia RITA imekusudia kusajili zaidi ya watu 500,000 katika maeneo hayo na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.

  Kwa mujibu wa utafiti wa afya uliofanyika 2010, asilimia 16 ya watoto wenye umri wa miaka mitano ndio wenye usajili na vyeti vya kuzaliwa Tanzania Bara ikilinganishwa na Tanzania Zanzibar ambapo usajili ulikuwa ni asilimia 79.

  Ili kukabiliana na hali hiyo, RITA kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) wamebaini mradi wa kusajili watoto chini ya umri wa miaka mitano uliofanyiwa majaribio wilaya ya Temeke mwaka 2012 na kuzinduliwa rasmi mwaka 2014 mkoani Mbeya.

  Kampeni hiyo imeonesha mafanikio na tija kwa taifa ambapo usajili umeongezeka na kufikia asilimia 58 ambapo awali mkoa wa Mbeya usajili ulikuwa asilimia 8.7.

  Kampeni hiyo ni endelevu kwa nchi nzima ambapo mikoa itakayoanza kufanya usajili ni Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Iringa, Njombe, Tabora, Kagera na Dodoma.

  0 0

   Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinatoa taarifa potofu kuhusu mchakato wa  Mwenyekiti wa sasa wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete kukabidhi kijiti cha uongozi wa CCM kwa Rais John Pombe Magufuli kama ilivyo mila na desturi ya Chama Cha Mapinduzi. Yamekuwepo madai eti Mwenyekiti amekataa au anachelewesha kukabidhi kijiti.

  Habari hiyo sio kweli kabisa na ni kinyume chake, kwani Dkt. Kikwete amekuwa akisisitiza kukabidhi madaraka mapema iwezekanavyo. Kwa ajili hiyo kwenye kikao cha Mei 3, 2016 alikataa kusiongezwe agenda nyingine ambazo zitalazimisha Mkutano Mkuu Maalum kuchelewa kufanyika kwa sababu ya kukamilisha maandalizi ya agenda hizo. Alisisitiza agenda iwe moja tu.

  Dhamira ya kufanyika Mkutano Mkuu maalum mwezi Juni, 2016 iko pale pale. Kilichoelezwa kwenye kikao ni kutaka kukamilisha utaratibu wa kupata fedha za kugharamia mkutano huo. Taratibu zikikamilika tarehe itapangwa. Mipango ya kutafuta pesa inaendelea na ikikamilika tarehe itatangazwa.
  Tunawataka wana-CCM wasihamanike wala kubabaishwa na taarifa za upotoshaji zinazofanywa na watu wenye nia mbaya na CCM. Hawa ni wale wale ambao wamekuwa wakiiombea mabaya CCM bila ya mafanikio.
  Pia tunapenda kukanusha madai ati kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwatahadharisha Wajumbe wa Kamati Kuu kuhusu ukimya wa Ndugu Edward Lowassa. Hakuna wakati wowote kauli kama hiyo aliitoa. Ni uzushi mtupu. Jina la Ndugu Lowassa halikutajwa kabisa.

  Aidha, tunapenda kukanusha madai ya kufanyika mkutano baina ya Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa CCM kuhusu uchaguzi wa Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM. Hapajawahi kufanyika mkutano wa aina hiyo siku yoyote na mahali popote. Hivyo madai ya kuwepo kwa tofauti baina ya Viongozi wakuu kuhusu nani achaguliwe kuwa Katibu wa Wabunge wa CCM hayana msingi wowote. 
  Kamati Kuu iliteua Wabunge wanne kugombea na kuwaachia Wabunge wa CCM kuamua. Kuhusisha Viongozi na hasa kuzua kuwepo kutokuelewana ni jambo la kusikitisha. Ni taarifa ya uongo yenye nia ovu kwa CCM na Viongozi wake.
  Tunapenda kuwatahadharisha waandishi wa habari kuandika habari za ukweli. Waache kuzua mambo yenye kupandikiza chuki na mgawanyiko usiostahili kuwepo ndani ya CCM na kuyaeneza kwa watu. Waheshimu maadili ya kazi zao.
  Napenda kuwahakikishia na kusisitiza kuwa hakuna mgogoro wa kukabidhi kijiti cha uenyekiti katika CCM na wala hautakuwepo.

  Imetolewa na;
    
  Ndugu Christopher Ole Sendeka   
                    MSEMAJI WA CCM                  

  MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,

  05/05/2016

  0 0

  SERIKALI imekanusha madai ya kutoa maelekezo kwa Uongozi wa vyuo vya elimu ya juu ya kuwanyanyasa wanafunzi wa vyuo hivyo wanaojihusisha na masuala ya siasa na badala yake imewataka wafuate kanuni na taratibu zilizowekwa sehemu husika.

  Hata hivyo imesema itaendelea kuwahudumia Watanzania wote ikiwemo kutoa elimu kuanzia ngazi awali hadi elimu ya juu bila kujali ya itikadi za dini wala vyama vyao vya siasa.Waziri Mkuu,Kassm Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 5, 2016) wakati akijibu swali la papo kwa papo la Mheshimiwa Ester Matiko (Viti maalum Chadema) aliyetaka kujua kama Serikali imetoa maelekezo kwa uongozi wa vyuo vikuu kunyanyasa wanafunzi wanaojihusisha na masuala ya siasa.

  “Nakanusha si kweli kwamba kuna maelekezo kwenye vyuo vyote vya elimu ya juu na pia hakuna unyanyasaji wowote wa vyuo na Watanzania wote wanao uhuru wa kujiunga na vyama vyote wanavyovitaka, lakini kila eneo limeweka utaratibu wake hivyo wafuate taratibu na sheria katika sehemu husika,” alisema.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imeondoa tozo ya asilimia 15 ya eneo la manunuzi ya vifungashio katika zao la korosho ili kumfanya mkulima kupata tija zaidi.Akijibu swali la papo kwa papo la Mheshimiwa Katani Katani (Tandahimba-CUF) aliyetaka kujua ni lini tozo hiyo itaondolewa, Waziri Mkuu Majaliwa amesema tayari tozo hiyo imeshaondolewa na gharama hizo kwa sasa zipo katika mfuko wa wakfu ulioundwa na wadau wa zao hilo na unachangiwa na asilimia 65 ya tozo za korosho zinazouzwa nje.

  Amesema mfuko huo wa wakfu unatakiwa kusimamia upatikanaji wa masoko ya zao la korosho, kununua pembejeo, kusimamia uboreshaji na upanuzi wa mashamba na kugharamia tatifi mbalimbali kwa ajili ya kupata ubora wa zao hilo.Akijibu kuhusu suala la madai ya wakulima ambao korosho zao zimepotea ghallani, amesema mfumo wa uuzwaji wa zao hilo wa stakabadhi ghalani ni wa kiushirika na unasimamiwa na Mrajisi ni vema wakulima wakadai haki yao katika mikutano ya ushirika wao na kama hawaridhiki na majibu waende mahakamani ili kupata haki yao.

  Amesema kwa sasa Serikali itahamishia nguvu zake katika kusimamia mazao mengine ya pamba, tumbaku na kahawa kama walivyofanya kwenye zao la korosho ili wakulima wa mazao hayo nao wapate tija.

  Akijibu swali la Mheshimiwa Joseph Kekunda (Sikonge-CCM) aliyetaka kujua Serikali inampango gani wa kutatua migogoro ya wakulima na wakulima ,Waziri Mkuu amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha inakomesha migogoro hiyo ambazo ni pamoja na kupima maeneo na kuweka mipango bora ya matumizi ya ardhi.

  Pia kuweka mipaka katika maeneo mapya na kutumia ranchi zilizopo kwa ajili ya wafugaji wakubwa na kwamba itatenga maeneo ya kilimo na kuyabainisha kwa wananchi ili kuepuka muingiliano uliopo hivi sasa.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  05 Mei, 2016.

  0 0

  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Jacob Boniface akizungumza, wakati akitoa taarifa ya kusimamishwa kazi kwa Mwanasheria Mkuu wa Manispaa Bw. Burton Mahenge na Mthamini wa Manispaa Bw. Richard Chidaga.

  Kikao cha Kamati ya fedha na Uongozi cha tarehe 29/4/2016, kiliagiza kuwa yaorodheshwe mashauri yote ambayo hayakusimamiwa vizuri na Mwanasheria wa Manispaa Bw. Burton Mahenge, na hivyo kuisababishia Manispaa kupata hasara, kupoteza Mali, na kuchelewa kupata manufaa katika mali zake.

  Kufuatia makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo, Baraza la Madiwani la tarehe 4/05/2016, limeamua kuwasimamisha kazi Mwanasheria Mkuu wa Manispaa Bw. Burton Mahenge na Mthamini wa Manispaa Bw. Richard Chidaga.

  Makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo ni: 

  1. Miradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa, Manispaa ilipaswa kupata shilingi Milioni 900 kwa mwaka kwa uwekezaji huo. Lakini kutokana na mgogoro wa kimkataba Mapato hayajawahi kulipwa hivyo kupoteza shilingi Bilioni 4.5 mpaka sasa. 

  2. Mgogoro wa wapangaji wa Nyumba za Magomeni Kota, Manispaa  iliandaa mpango wa kuendeleza eneo la Magomeni Kota, hivyo kuwaondoa wapangaji hao na kubomoa Nyumba hizo longer, wapangaji walifungua shauri la kupinga kuondolewa katika Nyumba na kutoa madai ya kujengewa nyumba ama kulipwa fedha za fidia kutokana na Usimamizi hafifu wa shauri hili Mahakama liamuru Manispaa kukaa na kumalizana na wapangaji nje ya mahakama. 

  Halmashauri ikatengeneza mkataba wa kuwalipa wapangaji kiasi cha shilingi 1,080,000/= kwa kila mpangaji kama kodi ya mwaka na kumpatia kila mpangaji kiwanja. Hivyo Manispaa inatakiwa kulipa shilingi 3,271,520,000/= kugharamia fidia hiyo kwa mchanganuo wa shilingi 695,520,000/= pango la mwaka na 2,576,000,000/= fidia ya viwanja 644.

  3.Uwekezaji eneo la Coco Beach Oysterbay, Manispaa iliingia mkataba na Q - Consult Limited, Kampuni hiyo ilishindwa kutekelezwa mradi kwa wakati na Manispaa ikavunja Mkataba huo. Q-Consult Limited ilifungua shauri ambalo halikusimamiwa vizuri na kwa sababu ya kutofika kwenye kesi, Manispaa ilipoteza kesi hiyo. Halmashauri iliagiza kukata kwa rufaa lakini haikuwa na hatua zozote zilizochukuliwa na hivyo Manispaa inaweza kupoteza haki yake. Iliagizwa na Serikali Mwanasheria Mkuu baada ya tamko la Rais Mhe. John Pombe Magufuli kutangaza nia ya kutoachia eneo hilo mpaka sasa Mwanasheria alikuwa hajakata rufaa. 

  4.Mradi wa Ujenzi wa maduka Makumbusho (Eastern Capital Ltd) Mkataba juu ya uendeshaji wa stendi haina manufaa kwa Halmashauri ,KMC inapata 1% ya makusanyo kwa mwaka sawa na Shilingi Milioni 4 tu kwa mwaka, wakati kabla ya uwekezaji, local standy Halmashauri ilikuwa ikipata Milioni 12 kwa mwezi.

  5. Kubomolewa kwa ofisi ya Kata ya Msasani, mwananchi ajulikanaye kwa jina la Chacha aliingilia eneo la ofisi ya kata ya Msasani na baadae kuishtaki Manispaa. Usimamizi dhaifu wa shauri hilo kuisababishia mahakama kutoa amri ya kubomoa ofisi ya Kata, Manispaa imekata rufaa na sasa ni muda mrefu shauri halisikilizwi na hakuna ufuatiliaji unaendeleaje. Hata hivyo kwa makusudi Bw. Chacha aliamua kuuza Kiwanda hili kwa Lake Oil CO. Limited wakati shauri halijaisha.Manispaa imekosa manufaa mengi kwa kuchelewa kukamilika kwa shauri hilo, yangu upande wa pili ulikataa Jaji, tuna zaidi ya mwaka hatujapangiwa Jaji mwingine na hatujafuatilia kama Halmashauri.

  6. Ujenzi wa Nyumba za makazi (Apartment) Hill Road Oysterbay, mradi inafanyika kwa ubia na mwekezaji Texas Enterprise Company Ltd, mkataba uliingiwa mwaka 2009, na mradi umesimama kwa muda mrefu sasa.Pamefanyika mabadiliko katika mkataba na mkataba umefanyiwa marekebisho bila idhini ya Halmashauri. Manispaa inakosa manufaa ya mali yake kwa sababu ya kuchelewa kwa mradi. Lakini pia uendeshaji mpya wa sasa hauna makubaliano wa Financial proposal na Investment capital. 

  7. Ujenzi wa Nyumba za makazi (Apartment s) Kiwanda no. 314 Toure Drive.
  Mradi huu unatekelezwa kwa ubia na Kampuni ya Lake Oil Limited mkataba uliingiwa 2009.

  Mabadiliko yamefanyika katika Mkataba bila idhini ya Halmashauri na kuisababishia mradi kuchelewa kukamilika, Manispaa inakosa manufaa ya mali yake kwa kuchelewa kukamilika mradi.

  Halmashauri bado inaendelea kufuatilia miradi mwingine ambayo umeingia na haina manufaa kwa Halmashauri.

  0 0

  Fundi Mitambo wa Redio Bomba Fm 104.0 iliyopo Jijini Mbeya Jina lake Limehifadhiwa alileta tafrani Mchana wa Leo mara baada ya kupanda juu ya  mtambo wa Redio hiyo, na kutishia kujitupa chini kwa madai ya kuhitaji kulipwa mshahara wake kutoka kwa muajiri wake wa kituo hicho cha Redio kilichopo maeneo ya Block "T" Jijini Mbeya.
  Fundi Mitambo wa Redio Bomba Fm (jina kapuni) akiwa juu ya Mnara wa Redio hiyo huku akisikika kusema "Mpaka Kieleweke leo nataka Pesa Zangu..."
  Mpaka Kieleweke...
  Baadhi ya wakazi na Wananchi wa Jiji la Mbeya wakishuhudia tukio hilo...
                                      PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.
                                                      PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0


    TIB imefanya mabadiliko ya kitaasisi ili kuweza kuwa kituo cha huduma zote za kifedha kwa kushughulikia mahitaji ya wawekezaji wa ndani wote kwa lengo la kusukuma maendeleo ya uchumi wa taifa.Mwanza, 5, May-2016: Benki ya Rasilimali nchini (TIB) imesema imekusudia kuwawezesha kifedha wakandarasi wa ndani ili waweze kutekeleza vema majukumu yao ya ujenzi wa miradi ya barabara na mingineyo.

  Akizungumza wakati wa mkutano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB) uliofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Mikopo wa Benki ya TIB, Theresia Soka amesema mikopo inayotolewa na benki yake kw wakandarasi wazawa nchini haihitaji mhusika kuweka dhamana benki. 

  ‘Benki ya Rasilimali imemua kurahisisha taratibu zake za kutoa mikopo kwa wakandarasi wa ndani, na tunachohitaji kwa mkandarasi anayetaka tumpe mkopo wa fedha atuletee vielelezo tu vinavyomtambulisha kuwa yeye ni mkandarasi na amesajiliwa kisheria’ alisema Bi Soka. 

  ‘Tumeamua kuwawezesha wakandarasi kwa lengo la kusaidia ukuaji wa maendeleo nchini katika sekta hii muhimu ya ujenzi’ alisema Bi Soka. Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa TIB, Bahati Minja, alisema benki hiyo inayomilikiwa na Serikali, imeboresha huduma zake za kibenki ndiyo maana inahitaji kuwawezesha wakandarasi wazawa nchini. 

  ‘Lengo kubwa la Benki ya TIB ni kuhakikisha wakandarasi tunawawezesha kifedha ili wawe na vitendeakazi, yakiwamo magreda’ alisema Bi Soka. Minja aliwaomba wadau hao wa maendeleo kuchangamkia fursa hiyo kwa kuchukuwa mikopo itakayowasaidia katika majukumu yao. 

  Hata hivyo makandarasi waliohudhuria mkutano huo ambao miongoni mwa wafadhili wake ni benki hiyo, waliupongeza uongozi wa Benki ya TIB kwa kuamua kuwawezesha mikopo wakandarasi. Wakandarasi hao walisema uwezeshwaji huo wa mikopo nafuu inayotolewa na benki hiyo, itawasaidia kuendesha kampuni zao za ujenzi. 

  Mkutano huo utafuatiwa na mkutano mwingine utakaofanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Daimond Jubilee kuanzia tarehe 26 hadi 27 mwezi huu wa tano, mwaka huu una kauli mbiu ya ‘Kuwajengea Uwezo Wakandarasi wa Ndani kwa ajili ya Uchumi Endelevu: Changamoto na Mipango ya baadae’. 

  Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB), Bahati Minja (aliyesimama) akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa mkandarasi mkoani Mwanza, kuhusu huduma bora za mikopo zinazotolewa na TIB kwa wakandarasi nchini katika mkutano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi nchini (CRB) uliofanyika jijini Mwanza jana.

  0 0

  Shekhe Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar bin Zuberi akizungumza viongozi wakati wa ufunguzi wa semina elekezi ya viongozi wa Bakwata katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
  Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum akitoa neno wakati wa kumkaribisha , Shekhe Mkuu wa Tanzania ,Mufti Abbakari Ally Bin Zuberi katika semina elekezi ya viongozi wa Bakwata iliyofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya viongozi wa Bakwata wakimskiliza Shekhe Mkuu wa Tanzania , Mufti Abbakari Ally Bin Zuberi (hayupo pichani) wakati wa semina elekezi ya viongozi wa Bakwata iliyofanyika katika ukumbi wa Karimjee ,jijini Dar es Salaam.(picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)

  0 0

  Meneja Mradi wa Shirika l nyumba la Taifa NHC Kawe unaokwenda kwa jina la 711 Injinia Samwel Metil akitoa maelezo kwa Timu ya Menejimenti ya NHC wote(Directors, Regional Managers & Line Managers) wakati walipotembelea miradi ya 711 Kawe , Morocco Square, Victoria Place, Eco Residence na Kibada ambapo ambapo pia watafanya pia kazi katiia miradi hiyo Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kuwafahamisha juu ya maendeleo na changamoto za miradi hiyo. 
  Mmoja wa Mainjinia wa Mradi wa 711 Kawe Bw.Kishor Hirani akimelezea jambo Meneja mradi Injinia Samwel Metil wakati menejimenti ya shirika hilo ilipotembelea katika mradi huo.
  Wakuu wa vitengo mbalimbali na mameneja wa mikoa wakitembelea mradi wa 711 Kawe leo.
   

  0 0

  Mkuu wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Kamishna Msaidizi Juma Yange akitoa maelezo namna kisima cha maji maalumu ya Zimamoto (fire hydrant) kinavyofanya kazi kwa Kamishna Jenerali Thobias ndengenye alipotembelea kituo hicho mapema leo.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akijitambulisha kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Ramadhani Maleta alipotembelea leo uwanja huo wakati akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya kutembelea vituo vya zimamoto na uokoaji nchini.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akitoka kukagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linalojengwa eneo la Tazara Mchicha mapema leo asubuhi alipokuwa akiendelea na ziara yake ya kutembelea vituo vya Zimamoto katika Jiji la Dar es salaam. (Picha na FC Godfrey Peter)

  0 0

  Tasnia ya filamu Tanzania inazidi kukua kwa kasi, si tu nyumbani hata nje ya nchi watanzania wanazidi kungara.

  Safari hii mtoto wa watanzania wenzetu aitwaye Evan Byarushengo amabahatika kupata nafasi ya kushiriki katika filamu ya kimarekani iitwayo THE REAL MVP: The Wanda Durant Story.

  Filamu hii inajaribu kuonyesha jinsi mama wa mchezaji nyota wa mpira wa kikapu Kevin Durant alivyohangaika kuwakuza watoto wake mpaka kufikia kuwa mastaa.

  Evan anaigiza kama Kevin Durant akiwa mtoto wa miaka 7. Waigizaji wakuu wa filamu hii ni pamoja na Cassandra Freeman anayeigiza kama mama Evan; Pauletta Washington (mke wake Denzel Washington) ambaye anaigiza kama bibi yake Evan na wengine wengi.
  Juu, katika clip mojawapo Evan akifanya mazoezi ya kucheza mpira wa kikapu. Nyuma ni director wa filamu George Nelson na wasaidizi wake.
  Juu, Evan akiwa anaongea na bibi yake (Pauletta) na mtoto anayeigiza kama kaka yake Kevin aitwaye Tony.
  Juu Evan(aliyechuchumaa) akipitia script mbele ya wenzake.
  Evan na mwenzake mwishoni walipata bahati ya kuonana na mama yake Kevin ambaye stori ya filamu inamuigiza.

  0 0

  Kwa mara ya kwanza MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI CAG profesa MUSSA JUMA ASSAD amezungumzia ripoti yake katika kipindi cha Mizani ya Wiki AZAM TV ambapo amesema kwa hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaajibisha watumishi walioshindwa kutekeleza majukumu yao anaamini mapendekezo yalipo katika ripoti yake yatachukuliwa hatua stahiki ili kuwawajibisha viongozi walioisabiashia serikali hasara ya mabilioni ya mafedha .usikose kuangalia kipindi hiki jumapili saa mbili na nusu hapa AZAM TWO ndani ya mizani ya wiki na JAMALY HASHIM.

  0 0

  Msanii Wa Bongo Fleva Snura Mushi (Snura) amewaomba radhi watanzania kwaujumla pamoja na vyombo vya serikali vinavyosimamia sekta ya sanaa kwa kutokufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika uendeshaji wa sanaa.

  Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, radhi hiyo imekuja mara baada ya Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo jana kufungia video ya wimbo wa msanii huyo wa Chura ikiwa ni pamoja na kutoonyeshwa kwenye Televisheni pamoja na kupigwa kwenye redio. Amesema kuwa tayari  video ya wimbo huo ameshatoa kwenye mtandao wa kijamii wa Youtube.
  Msanii Wa Bongo Fleva, Snura Mushi (Snura) awaomba radhi watanzania kwa kufanya video isiyo na maadili ya kitanzania ya wimbo wake wa Chura ameomba radhi watanzania mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja wa msanii Wa Bongo Fleva, Snura Mushi (Snura), Hemed Kavu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuwaomba radhi wa tanzania kwa video ya wimbo wa Msanii Snura na wimbo wake wa Chura.

  Kulia ni Msanii Wa Bongo Fleva, Snura Mushi (Snura) na Kushoto ni meneja wa msanii huyo, Hemed Kavu.
  Snura amesema kuwa yupo tayari kufanya upya video ya Wimbo wake wa chura ambayo itafuata maadili ya kitanzania kwani tayari ameshachukua vibali vya kufanya upya video ya wimbo huo.

  0 0


  0 0

  Mwamuzi Joseph Odartei Lamptey, Jumamosi Mei 7, 2016 anatarajiwa kuwa mwamzi wa kati katika mchezo wa kimataifa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaozikutanisha timu za Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na GD Sagrada Esperanca ya Angola, Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 
  Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, Lamptey kutoka jiji la Accra, Ghana atasaidiwa na raia wenzake wa nchi hiyo kuchezesha mchezo huo Na. 99. Mwamuzi Msaidizi Na. 1 (line 1) ni David Laryea wakati Mwamuzi Msaidizi Na. 2 (line 2) ni Malik Alidu Salifu. 
  Mwamuzi Msaidizi mezani (Fourth Official) ni Cecil Amately Fleischer huku Kamishna wa mchezo huo, akiwa ni Asfaw Luleseged Begashaw wa Ethiopia. 
  Viingilio na upatikanaji wa tiketi utatangazwa kesho Ijumaa Mei 6, 2016 na uongozi wa klabu ya Young African mara baada ya mkutano kati ya makocha wa timu zote mbili. Mkutano wa makocha hao utafanyika saa 5.00 mchana kwenye Ukumbi wa mikutano wa TFF.

older | 1 | .... | 1209 | 1210 | (Page 1211) | 1212 | 1213 | .... | 3278 | newer