Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 119 | 120 | (Page 121) | 122 | 123 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Warembo wa Redd's Miss Mzizima 2013 wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya mazoezi yao ya kila siku kujiandaa kuwania taji hilo hapo Mei 17,2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar es Salaam.Warembo hawa wamejipanga kisawasawa huku kila mmoja akionyesha hali ya kuibuka kidedea siku hiyo. 
  Mwalimu wa Warembo wa Redd's Miss Mzizima 2013,Aneth John akitoa somo kwa Warembo wake mara baada ya kumaliza mazoezi ya awaki katika kambi yao iliopo katika Hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar.

  0 0
 • 05/01/13--20:00: ngoma azipendazo ankal

 • 'Binti Kiziwi' ya Z Anto si ya kawaida

  0 0

  Kumbe mambo ya vyama vya siasa kuwa na matawi ughaibuni hayakuanza leo. picha hii iliyopigwa jijini London May 9,  1959 inathibitisha hilo. 
  0 0


   Bunduki aina ya Shortgun Mossberg ikiwa na risasi sita ambayo ilikutwa kwenye begi la dereva huyo wa Boda boda aliyekamatwa na polisi tarehe 28.04.2013.

  Habari na picha na Rashid Nchimbi 
  wa Jeshi la Polisi Arusha
  ---
  Jeshi la Polisi Mkoani hapa limemkamata mtu mmoja aitwaye Ally Rashid Salimu (23) Mwendesha pikipiki za abiria maarufu kwa jina la “Boda Boda” mkazi wa kata ya Sombetini jijini hapa akiwa na bunduki aina ya shortgun Mossberg yenye namba T292166 ikiwa na risasi sita.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana saa 5:30 asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Sabas alisema kwamba, tukio hilo lilitokea juzi tarehe 28.04.2013 muda wa saa 3:00 asubuhi katika maeneo ya Shamsi yaliyopo jijini hapa.

   Alisema siku ya tukio dereva huyo wa pikipiki akiwa katika eneo hilo alikuwa anaendesha pikipiki aina ya Skymark yenye namba za usajili T. 615 BZL huku akiwa amebeba begi lilionekana kutuna sana, ndipo askari waliokuwa doria katika eneo hilo walimtilia shaka na kisha kumfuatilia na kufanikiwa kumsimamisha.

   “Mara baada ya kumsimamisha askari hao walipekua begi hilo na kukuta silaha hiyo ikiwa na risasi sita na kisha kumfikisha mtuhumiwa huyo katika kituo kikuu cha polisi cha hapa Arusha mjini”. Alifafanua Kamanda Sabas.

  Kamanda Sabas alisema upelelezi juu ya tukio hilo bado unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani pindi utakapokamilika.

   Tukio hilo la ukamataji wa bunduki hiyo limekuja wiki tatu tu baada ya jeshi hilo kukamata bastola moja pamoja na risasi 41 kutoka kwa watuhumiwa waliokuwa wanahusishwa na matukio ya kumjeruhi Sister Mary Shobana na kisha kumnyang’anya fedha taslimu Tsh 30,000,000/= (Milioni thelathini) eneo la Notre Dame Njiro lililopo jijini hapa, fedha ambazo alitoka kuchukua benki ya Exim tawi la Shoprite.  0 0
 • 05/01/13--22:55: Yanga bingwa 2013

 •  Nizar Khalfan akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Coastal Union ya Tanga.
   Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima akimtoka beki wa Coastal Union ya Tanga, Philip  Mugenzi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zimetoka sare ya 1-1.
  Mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao wakati ikipambana na Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara. Yanga tayari imetwaa ubingwa huo baada ya kufikisha pointi 57 ambazo hakuna timu yoyote inayoweza kuzifikia.
  Picha na  Francis Dande

  0 0

  Mshambuliaji wa timu ya DHL, Regan Kimaro akimtoka beki wa timu ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Gasper Tumbeza (kulia) katika mchezo wa tamasha la michezo la Mei  Mosi kwa Makampuni lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. 

   Mshambuliaji wa timu ya NSSF, akiwa katika harakati za kufunga wakati wa tamasha la michezo la Mei Mosi kwa Makampuni.
  Kikosi kamili cha timu ya NSSF kilichoshiriki tamasha la michezo la Mei Mosi kwa Makampuni na kufanyika katika viwanja vya Leaders Club jijijni Dar es Salaam.

  0 0

  Bondia Fransic Cheka (kushoto) akipambana na Bondia mwenzake,Thomas Mashali wakati wa mpambano wao uliofanyika jana ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam. Cheka alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya kumi.
  Bondia Fransic Cheka (kushoto) akimshambulia kwa makonde ya nguvu Thomas Mshali wakati wa mpambano wao uliofanyika jana ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam. Cheka alishinda kwa KNOCKOUT raundi ya kumi.
  Bondia Thomas Mashali (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Cheka katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam jana.  Shomari kimbau akiwa na Cheka baada ya kumvisha ubingwa wa IBF Africa aliokuwa akiutetea
  Kutoka kushoto ni Kocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa Rajabu Mhamila 'Super D' mdau ambaye ajajulikana jina Mtayalishaji wa mpambano kati ya Fransic Cheka Vs Thomasi Mashali,Adamu Tanaka 'Tunaluza' na MC wa mpambano huo COOL.Picha na Super D Blog

  0 0

  MWENYEKITI wa Jumuia ya kusafirisha mahujaji ya Ahludaawa akichangia katika mkutano wa kuimarisha huduma za usafiri kwa mahujaji ulioandaliwa na Kampuni ya ndege ya Yemenia uliofanyika katika Hoteli ya Tembo mjini Zanzibar.
  MWENYEKITI wa Jumuia ya kusafirisha mahujaji ya Tawheed ,Tahir Ally akichangia katika mkutano wa kuimarisha huduma za usafiri kwa mahujaji ulioandaliwa na Kampuni ya ndege ya Yemenia uliofanyika katika Hoteli ya Tembo mjini Zanzibar.
  MENEJA mauzo na masoko wa Kampuni ya Ndege ya Yemenia , Zeenat Manji Kassam akifafanua jambo kwa Viongozi wa taasisi mbali mbali za usafirishaji wa mahujaji Tanzania. Katikati Mwenyekiti wa taasisi hizo Tanzania , Ustadh Khalid Mohammed Mrisho na Katibu wa Bodi ya mahujaji Zanzibar, Dk.Slim Mohammed Mgeni. Mkutano huo wa kuimarisha huduma za usafiri kwa mahujaji ulifanyika katika Hoteli ya Tembo mjini Zanzibar leo.
  MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Taasisi za Hijja Zanzibar (UTAHIZA), Khamis Yussuf akitoa mchango wake katika mkutano wa kuimarisha huduma za usafiri kwa mahujaji ulioandaliwa na Kampuni ya ndege ya Yemenia uliofanyika katika Hoteli ya Tembo mjini Zanzibar.Picha na Haroub Hussein

  0 0


  0 0

  By Ambassador Alfonso E. Lenhardt

  One of the benchmarks of a democratic society is the existence of a vibrant, free, and independent media. In every democratic nation, citizens must be able to debate current issues freely, vigorously, and peacefully. That is the true fabric of a democracy, and it cannot exist without the press freedom so essential to sustain it. That is why the United States of America has made the promotion of freedom of the press a top foreign policy priority, which President Obama's administration has further underscored.

  For democracy to flourish, the media must practice unimpeded its role of informing citizens based on fact-based reporting so that they in turn can form their own opinions and assessments. The opposite of that is tyranny, which distinguishes nations that do not trust their citizens to express their own judgments either at the ballot box or the privacy of their own homes.

  Over sixty years after the Universal Declaration of Human Rights proclaimed the right of every person “to seek, receive and impart information and ideas through any media and regardless of frontiers,” that right remains in peril in far too many countries. We must reflect on the fact that journalism remains a dangerous profession in some nations today, be it from political censorship or threats from criminal gangs and terrorists. We pay special tribute to those journalists who have sacrificed their lives, freedom or personal well-being in pursuit of truth and justice. We also honor the role of a free press throughout the world in creating sustainable democracies and prosperous societies. This further underscores the fact that freedom of the press is necessary to promote economic development through good governance, transparency, and a strong civic sector.

  Journalism is one of the noblest professions, and one practiced admirably by every day heroes - Tanzanian journalists, bloggers, and citizen journalists - who richly contribute to public debate. As they go about their daily duties, they can count on the unequivocal and strong support of the United States. Among many partnership programs with the media, we are especially proud of our ongoing outreach with journalism university students through film screening and information programs that encourage the next generation of journalists to embrace with pride their future profession and contributions towards building a brighter future of prosperity for Tanzania and all its citizens.

  On this World Press Freedom Day, the United States of America salutes Tanzanian journalists for their contributions to civic dialogue and dedication to their profession, and we reaffirm our commitment to support their goals and aspirations towards strengthening Tanzania's democracy through their fair, accurate and timely reporting.

  0 0


     Ney, Mauture, Roma, Madee, na Fid Q kupamba jukwaa la Airtel yatosha BURE.

  Katika mfululizo wa matamasha ya Airtel Yatosha yanayoendelea mikoa mbalimbali nchini , Kampuni  ya Airtel  mwishoni mwa wiki hii itatoa burudani pamoja na utambulisho wa huduma ya Airtel Yatosha kwa wakazi wa temeke , jijini Dar es salaam katika viwanja vya Mbagala Zakhem siku ya Jumamosi na Jumapili ya tarehe 4 na 5 mwenzi May 2013.

  Tamasha la Airtel yatosha litapambwa na waimbaji mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wakiwemo , Sir Juma Nature akiwa na kundi la wanaume halisi, Madii akiwa na kundi zima la tiptop connection,  pamoja na wakali wa hipop  Fid Q , Roma Mkatoliki na Ney wa mitego.

  Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando amesema, tumefanya matamsha ya Airtel yatosha katika mikoa mbalimbali nchini lengo hasa likiwa ni kutoa elimu kuhusu huduma zetu ikiwemo Airtel yatosha na kuwaunganisha watanzania katika mtandao wa mawasiliano bora na bei nafuu wa Airtel,

  Na mwishoni mwa wiki hii tunawafikia wateja na wakazi mkoa wa Dar es salaamawa na kuwapa  nafasi ya kusajili namba zao, kujiunga na huduma ya Airtel yatosha,  Airtel Money na  internet ya kasi ya 3.75G, kupata elimu kuhusu huduma na ofa mbalimbali za Airtel na kuunganishwa na mtandao wa Airtel kwa wale wateja wapya.

  Kiingilio ni  BURE, Njoo na kitambulisho chako upate kuunganishwa na huduma zetu na kupata burudani kutoka kwa wasanii mahiri wa kizazi kipya Aliongeza Mmbando.

  Kujiunga na huduma ya Airtel Yatosha mteja anatakia kupiga *149*99#  na kuunganisha moja kwa moja kwenye orodha ya huduma hii na kuchagua kifurushi anachokipenda na kuweza kujipatia dakika za maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet.

  0 0

  Habari Ankal,

  Leo katika pita pita zangu za kila siku,nilibahatika kupita barabara ya Msasani ambapo ni karibu kabisa na kituo cha Daladala cha Tido na kukutana na kitu ambacho sikuweza kuamini baada ya kuona kwa macho yangu ya kawaida,kwani niliona lori (semtrela) likipiga utani moja matata na kupelekea sisi wengine wenye mikoko ya mikopo,kusimama ili kusubiria mtaalam huyo apige hiyo yutani yake.hapa ndipo nilipoanza kujiuliza lile swali la kuwa,magari makubwa ya namna hii kwanini yanaruhusiwa kuingia maeneo ya katikati ya mji nyakati za mchana??Wadau namba mnisaidie katika hil.

  Mdau wa Ukweli wa Globu ya Jamii

  0 0

  Katika mfululizo wa matamasha ya Airtel Yatosha yanayoendelea mikoa mbalimbali nchini , Kampuni ya Airtel mwishoni mwa wiki hii itatoa burudani pamoja na utambulisho wa huduma ya Airtel Yatosha kwa wakazi wa temeke , jijini Dar es salaam katika viwanja vya Mbagala Zakhem siku ya Jumamosi na Jumapili ya tarehe 4 na 5 mwenzi May 2013.

  Tamasha la Airtel yatosha litapambwa na waimbaji mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wakiwemo , Sir Juma Nature akiwa na kundi la wanaume halisi, Madii akiwa na kundi zima la tiptop connection, pamoja na wakali wa hipop Fid Q , Roma Mkatoliki na Ney wa mitego.

  Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando amesema, tumefanya matamsha ya Airtel yatosha katika mikoa mbalimbali nchini lengo hasa likiwa ni kutoa elimu kuhusu huduma zetu ikiwemo Airtel yatosha na kuwaunganisha watanzania katika mtandao wa mawasiliano bora na bei nafuu wa Airtel,


  Na mwishoni mwa wiki hii tunawafikia wateja na wakazi mkoa wa Dar es salaamawa na kuwapa nafasi ya kusajili namba zao, kujiunga na huduma ya Airtel yatosha, Airtel Money na internet ya kasi ya 3.75G, kupata elimu kuhusu huduma na ofa mbalimbali za Airtel na kuunganishwa na mtandao wa Airtel kwa wale wateja wapya.


  Kiingilio ni BURE, Njoo na kitambulisho chako upate kuunganishwa na huduma zetu na kupata burudani kutoka kwa wasanii mahiri wa kizazi kipya Aliongeza Mmbando.

  Kujiunga na huduma ya Airtel Yatosha mteja anatakia kupiga *149*99# na kuunganisha moja kwa moja kwenye orodha ya huduma hii na kuchagua kifurushi anachokipenda na kuweza kujipatia dakika za maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet.

  0 0

  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo ya kifo cha Waziri wa zamani wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Alfred Tandau, nyubani kwa marehemu,Magomeni jijini Dar es salaam, Mei 2,2013.
  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumzana na mtoto wa kwanza wa Waziri wa Kwanza wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Julius Tandau wakati alipokwenda kuhani msiba wa Waziri huyo wa zamani aliyefariki dunia hivi karibuni, nyumbani kwa marehemu, Magomeni jijini Dar es salaam Mei 2, 2013. (Picha na Ofis ya Waziri Mkuu)

  0 0
 • 05/02/13--03:40: bei ya Madafu leo

 • 0 0
  0 0
 • 05/02/13--18:11: Article 23


 • 0 0
 • 05/02/13--19:58: Article 22

 • 0 0
 • 05/02/13--20:00: ngoma azipendazo ankal

 • Ngoma ya 'Dar mpaka Moro' ya Chege ni noma!!

  0 0

  Aliyekuwa katibu mkuu wa chama tawla cha TANU enzi hizo Bw. Oscar Kambona akirejea nchini mwaka 1992 akiwa na binti yake, Neema, baada ya kuishi uhamishoni jijini London, Uingereza, kwa takriban miaka 25 kutokana na vuguvugu la kisiasa la wakati huo. 
  Picha hii, aliyopiga Ankal uwanjani hapo, haikuwa rahisi kuipata. Wanahabari, waliofika hapo saa kumi alfajiri, walizuiwa kuingia ndani kwa ile hofu kwamba Bw Kambona angetiwa mbaroni na kutokea vuruguru. Ankal alipenya na kuwa wa kwanza kuipata taswira hii ambayo hadi sasa ndiyo iliyobaki kuonesha tukio hilo la kihistoria. Bw Kambona hakukamatwa na hakuna vurugu zilizotokea...

older | 1 | .... | 119 | 120 | (Page 121) | 122 | 123 | .... | 3272 | newer