Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Mbunge wa Jimbo hilo James Ole Millya Aongoza HARAMBEE ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Ormet

$
0
0
 Diwani wa kata ya Naberera Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Haiyo Yamati Mamasita (kushoto) na Mbunge wa Jimbo hilo James Ole Millya (katikati) wakiwasili uwanjani kwa ajili ya wakiendesha harambee ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Ormet, ambapo sh29 milioni zilipatikana.
 Diwani wa kata ya Naberera Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Haiyo Yamati Mamasita (kulia) na Mbunge wa Jimbo hilo James Ole Millya wakiendesha harambee ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Ormet, ambapo sh29 milioni zilipatikana.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya akisalimianana wakazi wa eneo la Ormet, Kijiji cha Namalulu, alipowasili kwa jaili ya kuendesha harambee ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, vyoo na nyumba za walimu wa shule ya msingi Ormet, ambapo sh29 milioni zilipatikana.

MAKALA MAALUM YA WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO MIKOANI

DK.SHEIN AHUDHURIA MAZISHI YA MAREHEMU ABDALLA MOHAMD MSHINDO (MWENYEKITI CCM)

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzipia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia)akijumuika na Viongizi na Waislamu katika kumswalia aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo katika msikiti wa Khinani,Wilaya ya Magharibi 'A'Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo.
Maelfu ya wananchi na waislamu waliobeba jeneza la Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo katika mazishi yake yaliyofanyika leo kijiji cha Kihinani Wilaya ya Magharibi 'A'Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzipia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto)akitia udongo katika kaburi la Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba katika mazishi yaliyofanyika leo Kihinani Wilaya ya Magharibi 'A',Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATI YA WATANZANIA NA WARUSI 28 APRILI 2016, JNICC, DAR ES SALAAM

$
0
0
Tunayo furaha kubwa kuwakaribisha kwenye Kongamano la Uwekezaji kati ya Watanzania na Warusi litakalofanyika siku ya Ijumaa tarehe 28 Aprili 2016 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Kongamano hili limeandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kikishirikiana na Russian Export Club, Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi na Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania; kwa usimamizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania, Wizara ya Biashara na Viwanda ya Urusi na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi 2016 linatarajia kuwaleta pamoja kundi la wawakilishi wa Serikali ya Urusi, wenye viwanda na wafanyabiashara wakubwa kwa lengo kushirikiana na kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji baina ya nchi hizi mbili. Kupitia mahusiano haya ya ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Urusi kutaongeza zaidi ushiriki wa makampuni ya Kirusi katika kufanya biashara na uwekezaji hapa nchini.

Ujumbe wa wafanyabiashara wa Kirusi unatarajiwa kufikia watu 60 ukiongozwa na Mheshimiwa Denis Manturov, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Serikali ya Shirikisho ya Urusi. Ujumbe huu pia utajumuisha viongozi wengine wa serikali, Wakuu wa makampuni na wawakilishi wa vyombo vya habari kutoka Urusi. Kongamano hili litajikita zaidi katika ushirikiano wa kiuchumi katika sekta za nishati, usafirishaji, miundombinu, mafuta & gesi, madini, huduma za fedha, kilimo na viwanda.

Wakati wa Kongamano hili, yatafanyika majadiliano ya moja kwa moja na mikutano ya Biashara-kwa-Bisahara (B2B), mikutano ya Serikali na Wafanyabiashara (B2G) na Serikali na Serikali (G2G). Wafanyabiashara wa kutoka Urusi watapata pia fursa ya kutembelea maeneo ya viwanda ya EPZA ili kujionea uzoefu wa moja kwa moja kuhusu sekta ya viwanda hapa nchini.

Ushirikiano baina ya Tanzania na Urusi katika nyanja za Uwekezaji na Biashara unaonesha kuwa mzuri kwa miaka ya hivi karibuni ingawa bado ni mdogo ukilinganisha na fursa zilizopo. Hivyo basi, kwa kupitia Kongamano hili, tutatoa nafasi ya kufungua na kujionea fursa lukuki zilizopo za kiuwekezaji na kibiashara baina ya nchi hizi mbili, pamoja na kukuza utalii.


Tunawakaribisha sana Wafanyabisahara wa Tanzania!
Imetolewa na: Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
Tarehe: 26 Aprili 2016.

Warning/Tahadhari: Heavy rain and strong winds/Mvua kubwa na upper mkali from/kuanzia tarehe 26-04-2016 to/...

KUTOKA MAKTABA: ALIYEKUWA RAIS WA TANZANIA DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIZINDUA MTAMBO WA KUHAKIKI TAKWIMU ZA MAWASILIANO

$
0
0
 February 27, 2014: Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System)  katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa  Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.
 Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe  kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam.

Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya  Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) aliouzindua February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. 

RAIS MAGUFULI AUNGANA NA RAIS KENYATTA KUOMBOLEZA KIFO CHA MAMA LUCY KIBAKI

$
0
0
Marehemu Lucy Kibaki akiwa na Mumewe Rais Mstaafu wa Kenya Mzee Mwai Kibaki siku ya ndoa yao mwaka 1962.

Marehemu Lucy Kibaki enzi za uhai wake

KUTOKA MAKTABA; MSETO FC YA MOROGORO TIMU YA KWANZA KUNYAKUWA UBINGWA NJE YA DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Daniel Mbega
TANGU mwaka 1965 ilipoanza Ligi ya soka ya Taifa Tanzania, ubingwa umekuwa wa timu za Dar es Salaam kutokana na timu za mkoa huo kuutwaa kila mwaka. Hii ni kutokana na uwezo wa kimchezo wa timu hizo, hususan Simba na Yanga.
Lakini ubingwa wa Muungano, ligi ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 1982 ikizihusisha timu mbili zilizoshiriki Ligi ya Bara na mbili kutoka Ligi ya Zanzibar, umewahi kutwaliwa na klabu za nje ya mkoa wa Dar es Salaam mara tisa katika miaka ya 1984, 1985, 1986, 1988, 1989, 1990, 1992, 1998 na 1999, wakati ule wa Tanzania Bara umetwaliwa nje ya Dar es Salaam mara tano katika miaka ya 1975, 1986, 1988, 1999 na 2000 tangu ligi hiyo ianze mwaka 1965.
Mseto FC ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kuupeleka ubingwa wa taifa nje ya Dar es Salaam mwaka 1975 ikifuatiwa na Tukuyu Stars mwaka 1986, Coastal Union ya Tanga 1988, na Mtibwa Sugar ya Morogoro 1999 na 2000.
Timu zilizotwaa ubingwa wa Muungano kutoka mikoa mingini ni KMKM ya Zanzibar mwaka 1984, Maji Maji ya Songea mwaka 1985, 1986 na 1998, African Sports ya Tanga 1988, Malindi ya Zanzibar 1989 na 1992, Pamba ya Mwanza 1990, na Prisons ya Mbeya 1999.
Mwaka 1975 Mseto, ambayo ilikuwa bingwa wa mkoa wa Morogoro, iliwashangaza mashabiki wengi wa soka nchini Tanzania ilipofanikiwa kuwa timu ya kwanza kuupeleka ubingwa wa Tanzania mikoani na kuvunja utawala wa timu za Dar es Salaam zilizokuwa zikiumiliki ubingwa huo kwa kuachiana (Sunderland ‘Simba’ 1965, 1966 na 1973, Cosmopolitans 1967, Young Africans ‘Yanga’ 1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974).
Mashabiki wa soka wa Morogoro waliokuwa kwenye uwanja wa Taifa Jumamosi Agosti 2, 1975 usiku wakati Mseto ilipotwaa ubingwa kwa kuifunga Nyota FC ya Mtwara kwa mabao 3-1 katika mchezo wa fainali ya kuwania kombe hilo lililokuwa likiitwa Karume Cup, waliingia kichaa kwa kushangilia baada ya mechi huku wakiongozwa na Katibu wa TANU wa mkoa wao, A. Lyander.
Katika mechi hiyo Mseto ilijipatia mabao mawili kupitia kwa Shiwa Lyambiko na moja kupitia kwa Omar Hussein, wakati ambao Said Dogoa ndiye aliyefunga bao pekee la Nyota kwa njia ya penati. Mseto iliingia fainali kwa kuitoa Usalama (Polisi) ya Dar es Salaam kwa mikwaju ya penati 5-3.
Kombe la ubingwa lilikabidhiwa kwao na Kamanda wa Vijana wa TANU, Rajabu Diwani. Kwa ushindi huo Mseto ilijipatia nafasi ya kuiwakilishaTanzania katika mashindano ya Klabu Bingwa ya Soka Afrika Mashariki na Kati pamoja na Klabu Bingwa Afrika.
Katika kipindi hicho Mseto ilikuwa na wachezaji wazuri kama Said Gedegela, Charles Boniface Mkwasa, Hamadan, Vincent Mkude, Ramadhan Matola, Aluu Ally, Shiwa Lyambiko, Hassan Shilingi, Omar Hussein, Spencer na Jumanne Hassan ‘Masimenti’ waliocheza fainali. Mwingine alikuwa Miraji Salum ambaye alikuwa na timu ya taifa, Taifa Stars, wakati huo.
Kufuatia mafanikio hayo kwenye ligi ya taifa, Mseto ilijikuta ikiporwa wachezaji wengi wakiwemo Abdallah Hussein aliyekwenda Coastal Union ya Tanga, Jumanne Hassan aliyekwenda Simba, Charles Boniface Mkwasa na Miraji Salum waliokwenda Yanga na Vincent Mkude aliyekwenda Tumbaku pia ya Morogoro.
Hata hivyo, nayo iliwapata wachezaji kadhaa nyota akiwemo golikipa Patrick Nyaga aliyetoka Yanga baada ya kukataa kucheza chini ya kocha Tambwe Leya kufuatia mgogoro mkubwa ulioleta mgawanyiko mwaka 1976.
Baada ya ushindi wao wa mwaka 1975, Mseto ilifanya sherehe kubwa kuanzia Novemba 7 hadi 9 ikishirikisha maonyesho ya muziki wa dansi, taarab, mauled na mechi za soka ambapo zilialikwa timu mbalimbali zikiwemo Simba na Cosmopolitans kutoka Dar es Salaam
Yanga, ambayo ndiyo ilikuwa imevuliwa ubingwa mwaka huo, haikualikwa.
Enzi hizo Mseto ilikuwa chini ya kocha Mohammed Hussein Hassan ‘Msomali’ na baadaye ikaongezewa nguvu na kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Bernard ‘bernt’ Trauttmann ilipokuwa ikijiandaa kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa.

BUNGE SPORTS CLUB NA BARAZA LA WAWAKILISHI HAKUNA MBABE,ZATOKA SARE YA BAO 1-1

$
0
0
DSC_2099Kapteni mpya wa timu ya Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, Mh. Sixtus Mapunda akitoa maelezo kwa kikosi hicho cha Bunge muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wao huo dhidi ya timu ya Baraza la Wawakilishi mchezo uliochezwa katika uwanja wa Amaan, Zanzibar.
DSC_2282
Mchezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi ambaye pia analiwakilisha Jimbo la Tunguu, Mh. Simai Mohamed Said akijadiliana jambo na ,Mwakilishi wa Rahaleo (CCM), Mh. Nasasor Salum Al Jazeera wakati wa mchezo huo maalum dhidi ya timu ya Bunge.
DSC_2162
Wachezaji wakisalimiana kabla ya mechi
DSC_2197
Kikosi cha timu ya Bunge kabla ya mchezo huo kuanza.
DSC_2206
Kikosi cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar kabla ya mchezo huo kuanza.




MAKALA YA SHERIA: MAMBO MANNE MUHIMU KUHUSU UMILIKI WA MALI KWA WANANDOA.

$
0
0
Na  Bashir  Yakub
Baadhi  ya  wasomaji  wameuliza maswali  mengi  kuhusu  habari  ya  umiliki  wa  mali  kwa  wanandoa. Wanataka  kujua  ipi  mali  ya  ndoa  na  ipi  siyo, wanataka kujua   mali  unayokuwa  nayo  kabla  ya  ndoa  inahesabika  vipi  baada  ya  kuingia  nayo  katika ndoa, wanataka  kujua  uuzaji  wa  mali  za  ndoa,  wanataka  kujua  kigezo  kinachozingatiwa  katika  kugawana  mali ndoa  inapovunjika, wanataka  kujua  iwapo   inawezekana kuwa  na umiliki  wa  pekee  wa  mali   wakati  upo  katika  ndoa,  wanataka  kujua  haki  ya mali kwa  ndoa ya  mke  zaidi  ya  mmoja, wanataka  kujua  nani  kati  ya  mume  na  mke  ana  haki  zaidi  ya  mali  na  mengine  mengi.

Haya  yameulizwa  na  watu  tofauti  lakini  kwa  wingi. Hata hivyo mengi  yake  yalikwisha elezwa hapa.  Mengi  yameelezwa  katika  makala  tofauti zilizopita.  Tunaamini  wapo  walioona  na  wengine  hawakuona. Kwasababu  hiyo  hakuna  ubaya  kujibu  tena  maswali  ya  aina  hii  ili   hata ambao  hawakubahatika  kusoma  waweze  kusoma  leo.


1.JE  NDOA  INAPOVUNJIKA NI  KIGEZO  KIPI  HUTUMIKA  KATIKA  KUGAWA  MALI  ZA  WANANDOA.

Iliwahi  kuelezwa  hapa  kuwa  wengi  wanajua kuwa  katika  kugawana  mali  za  ndoa  pale  ndoa  inapovunjika  kigezo  kinachotumika  ni  cha  asilimia. Wanajua  kwamba  sheria  imeeleza  wazi  kuwa  kuna  asilimia  fulani  anatakiwa  kupata  mwanamke  na  asilimia  fulani  mwanaume.

 Hili  si  kweli  kwani  kigezo  kikubwa  kinachotumika  ni  kigezo  cha   nguvu au  juhudi  za  pamoja  katika  upatikanaji  mali( joint  effort) husika. Juhudi  za  pamoja  huangaliwa mchango  wa  kila  mmoja  katika  upatikanaji   au  uendelezaji  wa  mali  husika. 

Na  juhudi  za  pamoja  sio  tu pesa  au  mali  bali  pia  hata  kazi  za  nyumbani  nazo  ni  sehemu  ya  juhudi  za  pamoja  katika  kupatikana  kwa  mali.

Kwa hivyo  juhudi  ya kila  mmoja  itapimwa  na  mali  zitagawanywa. Mahakama  ndio  chombo  chenye  mamlaka  na  kazi hiyo.


KUSOMA  ZAIDI  NENDA sheriayakub.blogspot.com

RAIS DKT. MAGUFULI AVUNJA BODI YA TCRA NA KUMSIMAMISHA MKURUGENZI WAKE MKUU

$
0
0


Dkt. Ally Yahaya Simba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), na kusababisha nchi kupoteza mapato ya takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Rais Magufuli amechukua hatua hiyo leo tarehe 26 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Tarehe 22 Machi, 2013 Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu ambapo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), hali ambayo imesababisha serikali kukosa mapato yanayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Pamoja na kuivunja bodi ya TCRA inayoongozwa na Profesa Haji Semboja na Kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba, Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kumteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo mara moja.

Aidha, Rais Magufuli amewataka Waziri Prof. Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi, na nchi ipate mapato yanayostahili kukusanywa.

“Waziri hakikisha unachukua hatua mara moja, nataka tukusanye mapato yote ya serikali yanayostahili na sitasita kuchukua hatua  dhidi ya yoyote atakayekwamisha jambo hili” Amesisitiza Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongoza kikao cha kazi na watendaji wa serikali wakiwemo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi, pamoja na ma-Katibu wakuu Wizara ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora, Katibu Mkuu Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, Naibu Katibu Mkuu Fedha na Mipango Mhe Dottoa James, Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Alphayo Kidata, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na watendaji wengine. PICHA NA IKULU

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili Rais Zanzibar Mh. Mohamed Abood awataka wazanzibari kuenzi na kulinda masuala ya muungano; https://youtu.be/EkOCxug-_6I  

Jumuiya ya wanataaluma wa chuo kikuu cha Dodoma wafanya kongamano la kuenzi muungano na kutaka wananchi wapewe elimu juu ya muungano;https://youtu.be/WH18ruW0ZIw  

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais mazingira January Makamba awataka wananchi kutumia njia sahihi na za kisheria katika kuzungumzia na kutatua kero za muungano; https://youtu.be/hgTDl8JbX18  

Msikilize mchambuzi wa mambo ya kisiasa Sinza Godigodi akizungumzia kwa ufupi muungano wa Tanganyika na Zanzibar; https://youtu.be/clCCYhxlq_c  

Upanuzi wa barabara ya Makongoro hadi uwanja wa ndege wa Mwanza waanza ili kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kupunguza tatizo la foleni jijini humo;https://youtu.be/vXkq5DVge5w  

Rais Magufuli amtumia salamu za rambirambi Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kufuatia kifo cha aliyekuwa mke wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Mwai Kibaki;https://youtu.be/8vzeMBquDPo  

Timu za Yanga na Azam zinatarajiwa kushuka dimbani kuendelea kumalizia Viporo vyao hapo kesho jijini Dar es salaam; https://youtu.be/N0ZEfm66S1c

Chama cha soka mkoani Ruvuma FARU chajipanga kuongeza timu nyingine ligi kuu kutoka mkoani humo timu ya JKT Mlale; https://youtu.be/UrWUt98Pjp4   

Ligi ya mabingwa barani Ulaya kuendelea tena hii leo kwa kuzikutanisha timu za Manchester city ya Uingereza na Real Madrid ya Hispania;https://youtu.be/MRoi6uf4_PU  

Wanariadha nchini watakiwa kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiweka fiti kwa afya zao na mashindano ya kimataifa; https://youtu.be/BP_SXMr3je4

Rais amevunja bodi ya mamlaka ya mawasiliano TCRA na kumsimamisha mkurugenzi wa mamlaka hiyo kwa kusababisha serikali hasara ya mabilioni ya fedha.https://youtu.be/4pHZx2E_Z0M

Baadhi ya wananchi mkoani Dar es Salaam wameunga mkono hatua ya Rais Magufuli kusitisha shamrashamra za muungano na kuelekeza fedha za shughuli hiyo kujenga barabara ya uwanja wa ndege jijini Mwanza. https://youtu.be/X1mAiQAvidY

Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dodoma amesema kero zinazojitokeza kuhusu muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar zinatokana na kukosekana na utashi wa viongozi wanaosimamia muungano. https://youtu.be/b6sJ2nce0HU

Rais Dr. John Pombe Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa zaidi ya elfu tatu kama sheria inavyomtaka huku msamaha huo ukiwahusu wafungwa wagonjwa, wazee na wanaonyonyesha.  https://youtu.be/jxUlIgEdoZ4

 Wananchi wa Liwale katika kijiji cha Ngunja licha ya kutofanyika kwa mikutano ya mapato na matumizi ya kijiji hicho wameelezwa kuwa wamekuwa wakikusanya mapato yao na kuyahifadhi kwa mwananchi; https://youtu.be/X1mAiQAvidY

Timu ya taifa taifa stars inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya kenya harambe stars mei 29 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo dhidi ya misri wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika. https://youtu.be/a1VEkqKj9co

Michuano ya mpira wa mikono imehitimisho leo ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemobaaddhi ya timu kutokujitokeza na kubaki timu za majeshi tu kitu kilichofanya michuano hiyo kukosa mvuto.
Wafanyabiashara kutoka Urusi wanatarajiwa kuingia nchini kesho kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji nchini na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi.https://youtu.be/xtsoDCHNGGk

Wafanyabishara na wananchi waishio eneo la Ubungo Extenal wamelalamikia chemba za maji machafu yanayotiririka kutoka mabweni yanayotumiwa na chuo kikuu cha dar es salaam (MABIBO HOSTEL). https://youtu.be/eFGe4KQcnD4

Mtu mmoja amekutwa ameuwawa kwa kupigwa na watu wasiojulikana katika manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. https://youtu.be/iMWhr1BF7fs

Serikali ya awamu ya nne inajivunia kuweka malengo ya kutekelezeka kwenye sekta ya elimu na kutatua changamoto nyingi za elimu. https://youtu.be/YcVZQ4quKnk

Umoja wa waganga na wakunga wa jadi kutoka Geita wilaya ya Nyang’wale wamesema elimu na juhudi waliotoa uongozi wa wilaya hiyo kuwa umepunguza mauaji ya vikongwe na albino. https://youtu.be/-MMuKsFGVgE

Amri ya kuwataka ombaomba kuondoka jijini Dar es Salaam imeonekana kupuuzwa baada ya kuonekana ombaomba wakiendelea kufanya kazi yao katika mitaa mbalimbali. https://youtu.be/qAQbTF4KZbM

JIJI LA DAR ES SALAAM KUCHUNGUZA MALI ZAKE.

$
0
0
 Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuanza kuchunguza mali za jiji la Dar es Salaam, (Katikati) Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es Salam, Halima Mdee na Kulia ni Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es Salam, Saed Kubenea wakiwa katika mkutano wa Meya wa jiji la Dar es Salaam.
Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es Salam, Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na mali zilizopo jiji la Dar es Salaam kuwa zipo chini ya jiji la Dar es Salaam. Kushoto ni  Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita. 
Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es Salam, Saed Kubenea akionyesha baadhi ya nyaraka za siri za jiji la Dar es Salaam ambazo wameanza kuzichambua kwaajili za kutambua mali zilizo chini ya jiji la Dar es Salaam. katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita na Afisa habari wa Ukawa, Gasto Makwembe.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
BARAZA la Madiwani la Jiji la Dar es Salaam limeunda kamati ya kuchunguza mali za jiji hilo kutokana na mali hizo  kugubikwa na mbinu chafu na jiji kushindwa kunufaika mali hizo.

Akizungumza leo na waandishi habari  jijini Dar es Salaam, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema kuwa kamati hiyo lazima ichambue mali hizo na kama ziko kwenye mikataba nazo ziangaliwe jinsi walivyoingia.

Amesema kuwa katika mali hizo ni pamoja na vibanda 130 vilivyo katika Benjamin Mkapa Kariakoo waliopanga vibanda hivyo wanalipa sh.30,000 ambapo kwa kiwango hicho ni kidogo sana kutokana eneo vilipo.

Mwita amesema kuwa mali za jiji zimekuwa hazinufaishi na kufanya mapato  kukusanywa  sh.bilioni 11.7  hivyo  mali zote zikichambuliwa jiji linaweza kukusanya zaidi ya sh.bilioni 20.

 Aidha amesema kuwa UDA ni mali ya jiji kutokana na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa  Hesabu za Serikali (CAG) kuzungumza kuwa shirika la Uda ni mali ya jiji.

Mwita amesema vyanzo vingine ambavyo jiji haipati fedha ni Soko la Kariakoo, DDC  hivyo vikiamgaliwa na kamati iliyoundwa itaonyesha hali  halisi na jinsi jiji watavyonufaika.

USAID WAZINDUA MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA MKOANI MTWARA LEO

$
0
0
Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Mtwara  siku ya Jumatano na Alhamisi, Aprili 27-28, 2016.

Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 97 katika mikoa 13 ya Tanzania bara. 

PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.  Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na  Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.

Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana, na uzinduzi ulihudhuriwa pia na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Dodoma ambaye amehamishiwa mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.  Watu takribani 180 walihudhuria.  Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Dodoma, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe  wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye Halmashauri. 

Mkoa wa Dodoma una Halmashauri  nane, ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, na Halmashauri ya Mji wa Kondoa.

PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID.  Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni:  Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute. 

Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.
MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Ally akizungumza wakati wa Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
 Abdul Kitula ambaye ni mtaalam wa fedha wa mradi wa PS3 akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mradi huo wakati wa uzinduzi hii leo mjini Mtwara.
Mwakilishi wa USAID, Laura Kikuli alikuwepo na kutoa salamu zake katika uzinduzi huo a,mbao ulishirikisha watendaji wa Halamashauri zote za Mkoa wa Mtwara.

WANANCHI ZAIDI YA 100 WA KIJIJI NYEBURU WALIOKUWA NA GIZA WANUFAIKA NA MRADI WA UMEME VIJIIJINI REA

$
0
0
NA VICTOR MASANGU, PWANI MRADI.
WAKAZI zaidi wa 100 katika  kijiji cha  Nyeburu  Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani waliokuwa na tatizo  la upatikanaji wa nishati ya umeme na kuishi  katika giza  kwa kipindi cha muda mrefu kwa sasa wamenufaika baada ya  kuunganishiwa umeme kutokana na  kukamilika kwa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu wa pili.

Baadhi ya wakazi hao  ambao wamenufainika  na mradi huo wakizungumza na na mwandishi wa habari hizi  akiwemo Mguya Mvuti,Tina Emmanuel pamoja na Lamia Suka   wamesema kwamba  hapo awali walikuwa wanapata kero ya umeme na kusababisha kukwamisha shughui mbali mbali za kimaendeleo.

Aidha walisema kwamba kukamilika kwa mradi huo kutaweza kuleta chachu kubwa ya kimaendeleo katika kijiji hicho kwani mwanzoni wananchi hao  walikuwa wanashindwa tutimiza malengo yao waliyojiwekea kutokana na kutokuwa na nishati hiyo ya umeme.

“Kwa kweli sisi kwa upande wetu kama wananchi wa kijiji hiki cha nyeburu hapo awali tulikuwa tunapata shida kubwa sasa nah ii yote ni kutokana tulikuwa tunaishi giza kipindi chote lakini kukamilika kwa maradi huu wa umeme vijijini hata kijiji chetu kitaweza kuapata maendeleo.
 
Kwa upande wake Meneja wa shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani  Martin Madulu alisema kuwa kwa sasa wanatekeleza  agizo lililotolewa na serikali kuhakikisha wanawafikia wateja wao wote hususan wale wa vijijini  kwa lengo kuweza kuwaunganishia umeme kwa bei nafuu.

Aidha Madulu alisema kwamba kwa sasa watahakikisha wanafanya jitihaza za hali na mali katika kuwafikia wateja wao ili waweze kuwa na nishati ya umeme katika maeneo mbai mbali hususan kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya vijijini.

“Lengo letu kubwa kwa sasa tunatakeeza agizo lililotoewa na serikali na tumeshaanza katika maeneo ya Chalinze, Kisarawe na tutaendelea katika sehemu mbali mbali za Mkoa wetu wa Pwani na tunatarajia kufikia vijiji vipatavyo 109 vilivyopo katika Mkoa huu,”alisema Madulu.
  
Naye Mhandisi mkuu wa Miradi ya kupeleka umeme vijijini (REA) Mkoa wa Pwani  Leo Mwakatobe amebainisha kuwa wanakumbana na changamoto nyingi katika utekelezaji wa majukumu yao hasa wakati wanapotaka kupitisha miundomibu katika makazi ya watu.  

MRADI huo wa kusambaza umeme vijijini (REA) awamu ya pili katika Mkoa wa Pwani unatarajia kuvinufaisha vijiji vipatavyo 109,sawa na wateja 11000 ambapo utakamilika mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu kwa gharama ya kiasi cha shilingi bilioni 30.

Shirika la Ndege la RwandAir sasa kufanya safari katika Miji 17 Afrika Mashariki

$
0
0
Shirika la Ndege la RwandAir hapa nchini linapenda kuwatangazia Watanzania wote na wasafiri wa Ndege zake, kuwa wamenza kufanya safari zake za anga katika miji 17 kwa nchi za Afrika Mashariki na kati likiwa na ndege kubwa nane.

 Shirika hilo hivi karibuni, litaongeza ndege nyingine kubwa nne (mbili ni Airbus na mbili Boeing) na kufanya kuwa na jumla ya ndege kumi na mbili. 

Mbali na safari za ndani ya Afrika Mashariki na kati, Ndege hizo mpya pia zitakuwa zikiruka kwenda kwenye miji ya Mumbay (India), Guangzhou (China), Paris (Ufaransa) na London (Uingereza).

Hayo yamesemwa na Meneja Mkazi wa Shirika hilo hapa nchini, Ibrahim Bukenya. Pia anapenda kuwajurisha kuwa bei zao ni nafuu na hudumu nzuri kuanzi kukata tiketi hadi mwisho wa safari.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA UONGOZI WA BARAZA LA TAWLA NA UONGOZI WA SKAUT LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na uongozi wa Baraza la Wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) wakati Uongozi huo ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 27,2016 kwa lengo la kumpongeza na pamoja na kumuelezea malengo na mikakati ya kiutendaji ya Chama hicho.
Makamu wa Rais Mhe. Samia akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Baraza la TAWLA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Baadhi ya Wawakilishi na Wanachama wa Chama cha SKAUT Nchini wakati ujumbe wa wawakilishi hao ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 27,2016 kwa ajili ya kumuelezea Makamu wa Rais shuhuli zao za kiutendaji hasa katika kutoa mafunzo mbalimbali kwa Mtoto wa kike.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, na Katibu Mkuu Kiongozi Baolozi Peter Kijazi Baada ya kuapishwa Makatibu wa Mikoa leo April 27,2016 Ikulu Dar es salaam. (Picha na OMR).

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kazi kubwa ya Chama Cha Skauti wa Kike nchini hivi sasa ni kuhakikisha kinarejesha heshima ya mwanamke katika jamii.

Samia ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na baadhi ya wanachama wa chama hicho waliofika ofisi kwake Ikulu kwa ajili ya kuelezea shughuli zao katika kusaidia watoto wa kike waweze kujitambua na hatimaye kulitumikia Taifa.

Alisema pamoja na chama hicho kinafundisha kujenga ujasiri na kuwa huru kwa mtoto wa kike lakini kuna haja ya kukumbushana umuhimu wa kuzingatia mila na desturi nzuri zilizopo katika matendo yao ili kurejesha heshima ya mwanamke.

"Sasa hivi utakuta binti kavaa kipanti kinambana hasa, anazunguka barabarani huku na kule, mwenyewe anajiona yuko sawa...hicho ni kinyume kabisa na maadili yetu, mila na desturi zetu za kiafrika tumeziacha kabisa." alisema Makamu wa Rais.

Aidha alisema katika enzi hizi za utandawazi kumekuwa na urushwaji wa mambo yasiyo na maadili katika mitandao jambo ambalo mtoto wa kike anaweza kuutumia uhuru huo kwa kufanya mambo kinyume na mila na desturi.

Alisema pamoja na kwamba Tanzania inapingwa na mataifa makubwa kwa kupitisha sheria ya makosa ya mtandao lakini bado chama hicho kina kazi kubwa ya kusaidia jitihada za serikali katika kulea watoto wa kike kimaadili. 

"Nyinyi Girl Guide mna hiyo kazi ya kusaidia kuwalea watoto wa kike waliojengeka vizuri kimaadili na wanazingatia mila na desturi," alidokeza Samia

Makamu wa Rais alikitaka chama hicho pia kuandaa miradi kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyoo bora mashuleni kulingana na mahitaji ya watoto wa kike na hivyo kuwawezesha kuhudhuria masomo siku zote bila kukosa kama ilivyo kwa wavulana.


Mwenyekiti wa chama hicho, Matilda Balawa alimshukuru Makamu wa Rais kwa kukubali kuwa mwanachama na kupongeza utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AKUTANA NA WAZIRI WA WA VIWANDA NA BIASHARA WA SINGAPORE

$
0
0
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa  Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia kwake) na ujumbe wake, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na Waziri wa Biashara na Viwanda wa  Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia ) na ujumbe wake kabla ya mazungumzo yao , Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

CCM ZANZIBAR YATOA MSAADA WA VIFAA VYA TSH MIL.5 KWA WAHANGA WA MAFURIKO NA KIPINDUPINDU

$
0
0
Katibu wa kamati maalum ya NEC, idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi, Waride Bakar Jabu akimkabidhi misaada Katibu mkuu wa ofisi ya makamo wa pili wa rais, Joseph Abdallah Meza kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa mafuriko waliopo kambi ya mwanakwere "C" Unguja.
Katibu wa kamati maalum ya NEC, idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi, Waride Bakar Jabu akikagua wahanga wa mafuriko katika kambi ya mwanakwere zanzibar.
Kambi ya kipindupindu iliyopo chumbuni Zanzibar.

CHAMA chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewataka wananchi kuendelea kufuata kanuni na taratibu zinazotolewa na  wataalamu wa kiafya ili kujikinga na maambukizi ya maradhi ya kipindupindu yaliyopo nchini.

Wito huo umetolewa na Katibu wa Kamati Maalum NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar,   Waride Bakar Jabu katika ziara ya kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa wa  Kipindupindu wa kambi iliyopo Chumbuni Zanzibar, alisema endapo wananchi watafuata kanuni za kiafya itasaidia kutoweka  ugonjwa huo kwa haraka.

Waride alisema CCM itaendelea kutoa misaada ya hali na mali kwa wagonjwa wa kipindupindu ili kusaidia serikali huduma za uendeshaji kwa wagonjwa hao.

“ Tunawaomba wananchi waendelee kuweka mazingira yao katika hali ya usafi sambamba na kutumia maji salama, vyoo kuwa visafi na wagonjwa wenye dalili za maradhi hayo kupelekwa haraka katika kambi za kipindupindu.

SERIKALI YAZUIA UINGIZAJI HOLELA WA MCHELE.

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameviagiza vyombo vya dola viimarishe ulinzi kwenye mipaka ya nchi na hasa katika mwambao wa Bahari ya Hindi ili kuzuia uingizwaji holela wa mchele wa magendo kutoka nje ya nchi.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatano, Aprili 27, 2016) wakati akijibu hoja za wabunge na kuhitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma.

“Napenda kuviagiza vyombo vya dola viendelee kuimarisha ulinzi wa mipaka yetu hasa katika mwambao wa Bahari ya Hindi ili kuzuia uingizwaji holela wa mchele wa magendo kutoka nje ya nchi. Endapo patatokea upungufu wa mchele nchini, Serikali itaangalia uwezekano wa kuruhusu kuagiza mchele kutoka nje,” amesema.

Waziri Mkuu amesema katika kipindi cha miaka sita iliyopita, kumekuwa na ongezeko la asilimia 14 katika uzalishaji wa mpunga hapa nchini na hivyo kufanya kiwango cha uzalishaji kiwe ni kikubwa kuliko mahitaji.

“Takwimu za uzalishaji mpunga zinaonesha kuwepo ongezeko katika kipindi cha miaka sita iliyopita ambacho kiliongezeka kutoka tani 1,699,825 mwaka 2009/2010 hadi kufikia tani 1,936,909 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 14. Katika kipindi chote hicho, kiwango cha uzalishaji wa mpunga kimekuwa kikubwa kuliko mahitaji,” amesema.

“Kutokana na mwenendo huo mzuri wa uzalishaji wa mpunga hapa nchini, Serikali ilisitisha kutoa vibali vya kuagiza mchele kutoka nje ya nchi tangu Machi, 2013. Hatua hii itasaidia wakulima wetu kupata soko la uhakika na bei nzuri, jambo ambalo linawaongezea kipato na pia kuwahamasisha kuongeza uzalishaji zaidi,” amesema.

Akizungumzia kuhusu deni la sh. bilioni 134 ambalo Serikali inadaiwa na Bohari ya Dawa nchini (MSD), Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kulishughulikia deni hilo kwa kumwelekeza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ahakiki deni hilo. “Mpaka sasa CAG amehakiki madai ya jumla ya shilingi bilioni 67 na kazi ya uhakiki inaendelea.”

Akifafanua kuhusu vigezo vilivyutumika kugawanya majimbo mapya ya uchaguzi, Waziri Mkuu alisema mwaka 2015, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea maombi 77 ya kuanzishwa majimbo mapya, ambapo Halmashauri 37 ziliwasilisha maombi ya kugawa majimbo ya uchaguzi na maombi 40 yalitoka katika majimbo yaliyokuwepo yakiomba kugawanywa. Kati ya maombi yaliyowasilishwa, maombi 35 tu ndiyo yalikidhi vigezo na yalistahili kugawanywa.

“Kutokana na ongezeko la Halmashauri mpya ambazo kisheria ni majimbo ya uchaguzi, ongezeko la idadi ya wabunge wanawake wa viti maalum na uwezo wa ukumbi wa Bunge; Tume iliamua kutumia vigezo vitatu tu ili kupata idadi ya majimbo yanayoweza kugawanywa. Vigezo hivyo ni: Wastani wa idadi ya watu (Population Quota), mipaka ya kiutawala na uwezo wa ukumbi wa Bunge,” alisema.

Waziri Mkuu alisema chini ya mchakato huo, Tume ilianzisha majimbo mapya 25  ambapo majimbo 19 yalitokana na ongezeko la Halmashauri mpya; na majimbo sita yalitokana na kigezo cha wastani wa idadi ya watu.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alibainisha kwamba kwa sasa Serikali haina mpango wa kuongeza maeneo mapya ya utawala zikiwemo wilaya na mikoa mipya kwa sababu bado inaendelea kujengea uwezo wa rasilmali watu na vitendea kazi katika maeneo mapya ya utawala yaliyopo hivi sasa.
Bunge limepitisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2016/2017.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATANO, APRILI 27, 2016.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images