Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1198 | 1199 | (Page 1200) | 1201 | 1202 | .... | 3284 | newer

  0 0

  H.E. Ali Hassan Mwinyi, Former President of the United Republic of Tanzania, over the weekend  presented Amb. Dr Richard Sezibera, the EAC Secretary General, with the final observation report from the recently concluded General Elections held in 18th February 2016, in the Republic of Uganda. The ceremony took place at the  residence  of the  Former President  in Dar es salaam, Tanzania.

  “I was very happy to observe the patience and orderliness with which the people of Uganda conducted her General Elections," said H.E. Ali Hassan Mwinyi. “These and many other things that have also been highlighted in the report, can be used as benchmarks for which other countries can borrow good practices from,” he added.

  While receiving the Report, the Secretary General thanked the Former  President for his leadership and commitment to the EAC Elections Observers Mission, adding that, “the cooperation between the EAC and other stakeholders led to sustainable peace in the country."
  The report consists of recommendations to streamline and improve the electoral process for future  in the Republic of Uganda. The EAC Observer Mission Report will be submitted to, among others, the Electoral Commission of Uganda, through the EAC Council of Ministers for consideration and implementation.
   Hon Peter Mathuki, EALA MP, H.E. Ali Hassan Mwinyi and Dr Richard Sezibera display EAC Observer Mission  Report

  0 0

  Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akikagua matengenezo ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi tarehe 25-04-2016
  Mkuu wa wilaya Kinondoni Ally Salum Hapi wa kwanza kulia hakipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ujenzi wa barabara ya Ali Hassani Mwinyi Halipo tembelea leo kuona maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo
  Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akiwa na wafanyakazi wa MS ESTIM CONSTRUCTION CO.LTD
  Mkuu wa wilaya Mhe.Ally Hapi akiongea na msimamizi wa ujenzi.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi kushoto akiwa na meneja wa Tanroad katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi  tarehe 25 Aprili 2016

  0 0
  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa wiki mbili kwa mkandarasi ESTIM Construction anayejenga barabara ya Bagamoyo, Sehemu ya Morroco-Mwenge kilomita 4.3 kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo.

  Akizungumza mara baada ya kukagua barabara hiyo, Prof. Mbarawa amesema baada ya wiki mbili barabara hiyo itafunguliwa kwa ajili ya matumizi ili kupunguza msongamano wa magari yanayoingia na kutoka katikati ya  jijini.

  “Hakikisheni barabara hii inakamilika ndani ya wiki mbili, ili msongamano wa magari yanatoingia na kutoka katika ya jiji upungue, na hivyo kuiunganisha vizuri barabara hii na ile ya Mwenge-Tegeta”. Amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Aidha amewataka waananchi na madereva wanaotumia barabara hiyo kulinda mazingira kwa kuepuka vitendo vyakumwaga mafuta kwenye barabara hiyo na kutupa takataka zinazosababisha mifereji iliyo pembezoni mwa barabara kuzipa na kuharibu barabara hiyo.

  “Nawataka watumiaji wa barabara, kuzingatia matumizi sahihi ya barabara, tunawekeza fedha nyingi katika ujenzi wa barabara mijini ili kuondoa msongamano hivyo zingatieni matumizi sahihi ya barabara ili zidumu kwa muda mrefu”. Amesema Prof. Mbarawa.

  Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale amemhakikishia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwa ili kupunguza msongamano ujenzi wa barabara hiyo umelazimika kuweka sehemu maalum za watembea kwa miguu kutokana na wingi wa watumiaji wa barabara hiyo katika sehemu hiyo na kupanua maingilio ya barabara ili kurahisisha magari kutoka na kuingia katika barabara hiyo.

  Eng. Mfugale amesema zaidi ya magari 15,000 yanakadiriwa kuwa yatapita katika barabara itakapokamilika na hivyo kupunguza msongamano mkubwa uliokuwepo katika eneo hilo.

  Takribani shilingi bilioni 4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo na hivyo kuiunganisha barabara ya Mwenge-Morroco na ile ya Mwenge-Tegeta.

  Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), kufanya tafiti na kuangalia fursa zitakazoiwezesha kupata mapato kutokana na kazi inazozifanya.

  Amesema iwapo Mamlaka hiyo itafanya kazi kwa uadilifu na uaminifu itaongeza idadi ya watu inaowahudumia kwa mwaka nchini na hivyo kusaidia wadau mbalimbali wa sekta za Kilimo, Ujenzi, Afya, Uvuvi kufanya kazi kwa faida.

  Prof. Mbarawa amekagua vitengo cha takwimu za hali ya hewa, hali ya hewa ya kilimo na Utabiri na kusisitiza kuwa ni wakati wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa teknolojia ya kisasa ili kuhudumia wadau wengi kwa wakati mmoja.

  “Hakikisheni taarifa zenu zinawafikia watu wengi hususan wale wanaozihitaji taarifa hizi kwa kutekeleza shughuli zao kiuchumi”. Amesema Prof. Mbarawa.

  Naye Mkurungenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa Mamlaka hiyo inafanya utabiri  kwa usahihi wa asilimia 80 na ni miongoni mwa Mamlaka inayofanya vizuri katika huduma za utabiri barani Afrika.

  “Taarifa zetu ni sahihi na kila baada ya dakika 15 tunatoa taarifa zinazoonyesha hali ya hewa nchini”. Amesema Dkt. Kijazi.

  Dkt. Kijazi amesema mamlaka hiyo imejipanga kuongeza uelewa wa watumiaji wa hali ya hewa hapa nchini ili kuwezesha wadau wa hali ya hewa kunufaika kikamilifu na utabiri unaotolewa na Mamlaka hiyo.


  Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, 
  Uchukuzi na Mawasiliano, 
  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng. Patric Mfugale kuhusu kukamilika kwa upanuzi wa barabara ya Morocco-Mwenge KM 4.3.

   Mafundi wa kampuni ya Estim Construction wakiendelea na Ujenzi wa barabara ya Mwenge –Morocco KM 4.3 ambayo ni sehemu ya Barabara ya Morocco –Mwenge-Tegeta.

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS akimuonyesha Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano kazi ya ujenzi wa mifereji pembezoni mwa Barabara ya Morocco-Mwenge inavyoendelea. 


  0 0


  0 0  0 0
 • 04/25/16--23:00: yale yaleeeee....
 • Serikali/NSSF wafunge CCTV camera wahalifu wakamatwe watolewe picha magezitini wapate kuona aibu. Faini ya fedha haitoshi watu wana jeuri ya pesa. Tukiacha hivi mwisho taka zitarushwa baharini hapo itakuwa janga, madhara yake makubwa - MDAU WA MAZINGIRA

  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongoza kikao cha kazi na watendaji wa serikali wakiwemo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi, pamoja na ma-Katibu wakuu Wizara ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora, Katibu Mkuu Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, Naibu Katibu Mkuu Fedha na Mipango Mhe Dottoa James, Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Alphayo Kidata, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola pamoja na uongozzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na watendaji wengine. PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Rabi Hume.
  Kwa kuhakikisha jamii inakuwa katika hali ya usalama wa kiafya, Taasii ya Fazel Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Afya na Madawa (TAHMEF) wametoa huduma ya upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi wa Kigogo, Dar es Salaam.


  Zoezi hilo lilifanyika Aprili, 23 katika Msikiti wa Al Ghadir uliopo Kigogo Post na jumla ya 352 wanawake wakiwa 150 na wanaumme 202 walipimwa Malaria, Kisukari, Shinikizo la Damu na Upungufu wa Damu mwilini.

  Kati ya watu hao, watu 38 wameonekana kuwa na Shinikizo la Damu, 36 Upungufu wa Damu, 8 Kisukari na mmoja Maralia ambapo walipata nafasi ya kupatiwa dawa na ushauri kutoka kwa madaktari mbalimbali.

  Aidha kwa mafanikio hayo, Fazel Foundation inawashukuru wote walioshiriki katika huduma hiyo akiwepo Dkt. Mohammed Alloo, Dkt. Sibtain Moledina, Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL Group), Salama Pharmaceuticals na Clinicheck Labs, Imam wa msikiti wa Al Ghadir Sheikh Jalala, Msikiti wa Al Ghadir, Diwani wa Kigogo, Bw. Manyama, Team ya Volunteers na Hawza ya Imam Sadiq kwa ushiriki wao katika zoezi hilo.
  Boniventure Pius akimpima Imam wa Msikiti wa Al Ghadir, Sheikh Jalala wakati wa uzinduzi wa upimaji afya bure kwa wakazi wa Kigogo. Aliyesimama kulia ni Mwanzilishi wa Fazel Foundation, Dkt. Sajjad Fazel.
  Mary Kalleku akimpima mmoja wa wananchi waliofika katika kituo kilichokuwa kikitumika kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo, Dar es Salaam.
  Mwanzilishi wa Taasisi ya Fazel, Dkt. Sajjad Fazel akisalimiana na Diwani wa Kigogo, Bw. Manyama wakati wa funguzi wa huduma ya upimaji wa afya bure kwa wakazi wa Kigogo. Katikati ni Imam wa Msikiti wa Al Ghadir , Sheikh Jalala. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe Dkt. Abdallah Possi akiwasilisha hoja za masuala ya Watu wenye Ulemavu wakati wa Mkutano wa Bunge wa kujadili Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/17 kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde tarehe 25 Aprili, 2016.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akiwasilisha hoja zinazohusu masuala ya Kazi na Ajira wakati wa mkutano wa Bunge wa Kujadili Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/17 Bungeni Dodoma tarehe 25 Aprili, 2016.

  Serikali imeahidi kuboresha Makazi ya watu wenye ulemavu na wenye mahitaji maalum ili kutatua changamoto wanazokabiliana nazo katika maisha yao ya kila siku.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt Abdallah Possi wakati akichangia hoja katika Mkutano wa Bunge wa kujadili Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/17 Bungeni mjini Dodoma.

  Naibu Waziri aliwaeleza Wabunge umuhimu wa Serikali kuboresha makazi ya Watu wenye Ulemavu na wenye mahitaji maalum kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya watu wenye Ulemavu namba 9 ya mwaka 2010 inayoeleza haki za watu wenye Ulemavu kuboreshewa maeneo muhimu ikiwemo elimu, ajira, fursa sawa na miundombinu.

  “Dhamira ya Serikali ni kuhakikiasha Watu wenye Ulemavu wanashiriki katika shughuli mbalimbali kwa kuwawekea mazingira rafiki yanayowasiaida kutekeleza majukumu yao kulingana na hali zao” Alisema Mhe.Possi.

  Aidha, Serikali imefanya jitihada za awali kwa kuyatembelea makazi ya watu wenye ulemavu yakiwemo makazi ya Nunge yaliyopo wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es salaam, Sarame Mkoani Manyara, Kituo cha Wagonjwa wa Ukoma cha Msufini mkoani Tanga pamoja na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na kubaini umuhimu wa kuyaangalia maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto za uvamizi wa makazi ya watu wenye mahitaji maalum.

  “Makazi ya watu wenye ulemavu na wale mahitaji maalum yana changamoto nyingi ikiwemo uchakavu wa majengo, kukosa vifaa, uhaba wa wahudumu, changamoto za kifedha na uvamizi wa mara kwa mara” Alisema Naibu Waziri.

  Naibu Waziri Possi alisisitiza kuwa hadi sasa Wizara hiyo imeshakubaliana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuangalia hatua za kuzuia uvamizi katika Makazi ya Watu wenye Ulemavu na wenye Mahitaji maalum ili kuimarisha usalama wao.

  Msingi wa hoja iliyojibiwa na Naibu Waziri imetokana na michango iliyotolewa na wabunge kuhusu masuala ya Watu wenye Ulemavu kuitaka Serikali kuhakikisha inaboresha mazingira ya watu wenye ulemavu.

  Maeneo  yanayoboreshwa na kutekelezwa ni pamoja na kuwaboreshea namna ya wanavyotakiwa kupata elimu bora, kukomesha mauaji ya wenye ualbino, suala la kodi na Makazi ya watu wenye ulemavu na wenye mahitaji maalum wakati wa kuchangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/17.

  0 0  0 0

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,kamishna msaidizi ,Wilbroad Mutafungwa akionesha misokoto ya Bhangi iliyokamatwa baada ya wahusika kufanikiwa kuwakimbia askari Polisi.
  Baadhi ya vitu mbalimbali walivyokamtwa navyo watuhumiwa wa ujambazi.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Wilbroad Mutafungwa akionesha bastola ambayo inadaiwa kutumika katika kufanyia uharifu.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0


  0 0
  0 0

   Mbunge wa Monduli Julius Kalanga akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari Moringe iliyoko wilayani humo  jana wakati wa mahafali ya kidato cha sita

   Sehemu ya wanafunzi wahitimu wakiwa wanasikiliza amgeni rasmi kwa makini
  Mbunge  wa Monduli Mhe.  Julius Kalangaakiwa akigawa cheti kwa mmoja wa wanafunzi aliyemaliza (Picha na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii,Monduli)

  0 0

  Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa kipindi cha mpito cha mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), watumiaji wa vyombo vya usafiri wametakiwa kutotumia njia maalum za mradi huo.
  Mradi huo unatarajiwa kuanza kufanya kazi tarehe 10 Mwezi ujao na kuendeshwa na kampuni  ya UDA Rapid Transit (UDA-RT).
  Msemaji wa Kampuni ya UDA-RT, Bw. Sabri Maburuki amesema jana kuwa “Wananchi waheshimu njia za mabasi hayo kwani itasaidia kuepukana na ajali na wepesi wa kuendesha mradi huo.”
  Kwa sasa madereva wa mabasi ya mradi huo wanafanya mazoezi tayari kwa kuanza kwa mradi huo.
  Alisema pamoja na kupigwa marufuku, bado kuna baadhi ya vyombo vya usafiri kama magari, bodaboda, bajaji na maguta yanapita katika barabara hizo huku mabasi yakiwa yanafanya mazoezi.
  Alisema miundombinu ya mradi huo imejengwa kulingana na mahitaji, hivyo kila chombo cha usafiri kipite na waenda kwa miguu wapite katika njia zilizotengwa.
  Akitoa mfano wa kutoheshimu taratibu alisema tayari mabasi manne ya mradi huo yameshakwanguliwa na vyombo vingine katika kipindi hiki cha mazoezi.
  “Sheria za mabasi haya ni kama treni, yule aliyegongwa au kagonga basi ndiye mwenye kosa,” alisema.
  Alisema tayari mabasi yana madereva waliofuzu, yamekatiwa bima na nauli zinatarajiwa kutangazwa hivi karibuni na Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA).
  Alisema katika kudhibiti ulinzi wa vituo na mabasi, wamefunga kamera kwa ajili ya kubaini watu wenye nia mbaya ya kuhujumu miundombinu hiyo.
  Mradi wa BRT unatarajiwa kupunguza kwa kiwango kikubwa tatizo la usafiri katika jiji la Dar es Salaam linalokadiriwa kuwa na watu milioni tano.
  Msemaji wa Kampuni inayotarajiwa kuendesha mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) katika kipindi cha mpito, UDA-RT, Bw. Sabri Maburuki akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu kuheshimiwa kwa njia za mabasi hayo ili kusaidia kuepukana na ajali na wepesi wa kuendesha mradi huo unaotarajiwa kuanza tarehe 10 mwezi ujao.

  0 0

   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula (Mb), akijaribu kutumia  kifaa cha upimaji (Total Station) kinachotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Ardhi mjini  Morogoro  kupima, katika mahafali ya 34 yaliyofanyika chuoni hapo.

   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula (Mb), akipewa maelezo juu ya matumizi ya kifaa cha upimaji (Total Station) na mmoja wa wanafunzi wa chuo cha Ardhi  Morogoro ambaye pia ni mhitimu katika mahafali ya 34 ya chuo hicho.

  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula (Mb), (katikati)   akiwa na viongozi wa chuo cha Ardhi – Morogoro pamoja na wahitimu katika mahafali ya 34 ya chuo hicho, wa pili kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Upimaji na Ramani; Bwn. Justo Lyamuya.


  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Lugimbana akizungumza na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM -UDOMASA), wakati wa mdahalo wa miaka 52 ya Muungano uliofanyika katika Ukumbi wa Chimwaga  uliopo UDOM leo. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo  hicho,  Professa Idrissa Kikula. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Mwenyekiti wa Jmuiya ya Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA),  Mhadhiri Msaidizi, Edson Baradyana akitoa shukurani kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Lukimbana kwa kukubali kufungua kongamano hilo.
   Baadhi ya wanachuo na wanataaluma wakishiriki kwenye kongamano hilo la miaka 52 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

   Jopo la wawezeshaji wa kongamano hilo.

  0 0  Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Ruth Mtoi Simba akikabidhi msaada  wa vifaa tiba kwa  Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ngarenaro  Dkt. Hosea Naaman msaada uliotolewa na Umoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki  maarufu kama (WATJAM)jana jijini Arusha.

  Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Ruth Mtoi Simba akikabidhi msaada  wa vifaa tiba kwa  Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ngarenaro  Hosea Naaman ,msaada uliotolewa na Umoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki  maarufu kama (WATJAM)jana jijini Arusha.

  Na Woinde shizza,Arusha.
  Hospitali ya Ngarenaro iliyoko wilaya ya Arusha mjini mkoa wa Arusha
  inakabiliwa na uhaba wa vifaa tiba pamoja na ukosefu wa miundombinu ya maji katika wodi ya wazazi jambo ambalo linapunguza ufanisi wa
  upatikanaji wa huduma za afya kwa wagonjwa.
  Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo Hosea Naaman  amesema kuwa uchache wa vifaa tiba umekua ukiathiri ari ya wauguzi katika kuwahudumia wagonjwa licha ya juhudi zinazofanywa na serikali bado hospitali hiyo ina mahitaji ya vifaa tiba hasa katika wodi ya wajawazito
  Kufuatia Changamoto hizo Umoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki  maarufu kama (WATJAM) wameitikia wito na kujibu changamoto hizo kwa kutoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali ikiwemo gloves,mashuka,ambavyo vitawezesha upatikanaji wa huduma bora kwa mama na mtoto.
  Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu Ruth Mtoi Simba amesema kuwa
  Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya wameamua kuchangia huduma za kijamii ili kuwasaidia watanzania wenye kipato cha chini kupata huduma bora za afya.
  Mwanachama wa  Umoja huo  Fadhili Mganya na Katibu wake Costantini Mashauri wamesema kuwa umoja huo umelenga kuwasaidia watanzania kutatua changamoto mbalimbali za afya ,kijamii na kiuchumi kwa kushiriki katika kutatua changamoto hizo.
  Umoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki leo wamesheherekea sikukuu ya Muungano kwa kutembelea hospitali ya Ngarenaro na kutoa msaada wa vifaa tiba ili kusaidia kuboresha huduma za afya .


older | 1 | .... | 1198 | 1199 | (Page 1200) | 1201 | 1202 | .... | 3284 | newer