Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 118 | 119 | (Page 120) | 121 | 122 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Waziri wa Mazingira Dk. Terezya Huvisa ambaye ni Rais wa Mawaziri wa Mazingira Barani Afrika akiipongeza Hoteli ya DoubleTree by Hilton kwa kuona umuhimu wa elimu kwa kukabidhi taa mia mbili kwa Shule za Msingi zilizopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma , Shule zilizopewa msaada huo ni Shule ya msingi Mletele, Mwanamonga, Liumbu na Namang'ula , Taa hizi zinazotumia Nishati ya jua pia ni rafiki wa mazingira. " Taa hizi zitawasaidia kuepeuka kutumia vibatari na mishumaa muda wa kujisomea kwa sababu ni hatari kwani vimekuwa vikisababisha majanga ya kuungua kwa watoto wengi nchini ".
  Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joesph Joseph Mkirikiti alie kaa katikati na kutoka kulia kwake ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli za DoubletTree by Hilton Tanzania Bw. Judd Helman na alie kaa kushoto ni mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata wakati wa hafula ya kukabidhi msaada wa taa zinazotumia nishati ya jua.
  Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph mkirikiti akiteta jambo na mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata (kushoto) juu ya matumizi ya taa zinazotumia nishati ya Jua ambazo pia ni rafiki wa mazingira kwa Wanafunzi wa darasa la Saba. Kulia ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli za DoubletTree by Hilton Tanzania Bw. Judd Helman.
  Toka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata akiwa ameshikilia taa na wakatikati ni mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph mkirikiti akiwa ameshikilia taa na wa mwisho ni Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw. Judd helman.
  Mkurugenzi wa kanda ya Africa mashariki wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw. Judd helman akimkabidhi moja ya taa inayotumia nishati ya Jua mwanafunzi wa Shule ya Msingi Liumbu iliyopo ndani ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma .
  Waziri wa Mazingira Dk. Terezya Huvisa ambaye ni Rais wa Mawaziri wa Mazingira Barani Afrika hapa ni umati wa wanafunzi (Viongozi wa leo) kila mmoja akitaka ampe mkono wa pongezi baada ya kumalizikla hafla ya kukabidhi taa za nishati ya jua kwa shule nne za manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
  Wanafunzi toka katika shule nne za msingi Mletele, Mwanamonga, Liumbu na Namang'ula na wakifatilia kwa makini hutuba iliyokuwa ikitolewa kabla ya kukabidhiwa taa zinazotumia Nishati ya jua ambazo zimetolewa na Hoteli ya DoubleTree by Hilton.
  Wanafunzi hao wameishukuru Hoteli hiyo na kusema taa hizo zitawasaidia kujisomea hata kipindi ambacho Umeme umekatika majumbani hivyo kuongeza uwezo wao kielimu na kupunguza matumizi ya kununua mafuta ya taa kwa ajili ya kusomea
  Naye Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata amesema
  "tumeamua kufanya kampeni hii ambayo ni endelevu tutakuwa tukigawa taa 200 za mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira vile vile tunaomba wahisani wengine nao wajitokeze".
  Picha na habari kwa hisani ya www.demashonews.blogspot.com

  0 0

  Maelfu ya Wakazi wa Mji wa Mbeya wakisalimiana kwa shauku na Rais Dkt.Jakaya  Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songwe mjini Mbeya tayari kuongoza sherehe za Mei mosi zinazofanyika mkoani humo leo. Picha na Freddy Maro

  0 0
 • 04/30/13--23:46: KUMBUKUMBU
 • NI MIAKA MITANO SASA TOKA ALIPOTUACHA KIJANA WETU MPENDWA BENEDICT JOHN MWANDIKA ALIYEFARIKI DUNIA HAPO TAREHE 01 MAY 2008. ANAKUMBUKWA NA BABA YAKE NA NDUGU ZAKE WENGINE WENGI.

  TUNAMUOMBEA KWA MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI AMIN.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea kushtushwa na kusikitishwa kwake na taarifa za kifo cha aliyekuwa Mweka Hazina wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kiongozi wa miaka mingi wa wafanyakazi na Waziri wa muda mrefu wa Serikali, Mheshimiwa Alfred Tandau ambaye ameaga dunia jioni ya siku ya  Jumanne, Aprili 30, 2013.

  Katika salamu zake kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Abdulrahaman Kinana, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM amesema:

  “Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mzee Alfred Tandau ambaye nimejulishwa kuwa amepoteza maisha jioni ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) mjini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa kwa matibabu ya kansa ya tumbo.”

  “Nilimfahamu Mzee Alfred Tandau kwa miaka mingi. Alikuwa kiongozi hodari na mwaminifu ambaye katika nafasi zote alizozishikilia katika utumishi wake wa umma alithibitisha uadilifu na uzalendo wa kiwango cha juu,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

  “Katika uongozi wa Chama cha Wafanyakazi cha NUTA na baadaye JUWATA, Mzee Tandau alijipembenua kama mtetezi halisi na mkweli wa maslahi ya wafanyakazi. Katika Serikali ambako alitumia kwa miaka mingi kama Waziri alikuwa mwaminifu na mtii kwa Serikali yake, kwa viongozi wake na kwa wananchi aliowatumikia. Katika nafasi yake ya Mweka Hazina wa CCM aliendeleza sifa hizo hizo alizokuwa nazo tokea nyuma. Tutakosa sana busara na ushauri wake.”

  Ameelezea Rais Kikwete: “Nakutumia wewe Katibu Mkuu wa CCM, Mheshimiwa Kinana salamu zangu za dhati za rambirambi kuomboleza msiba huu. Aidha, kupitia kwako nawatumia rambirambi viongozi na wanachama wote wa CCM kwa kumpoteza kiongozi na mwanachama mwenzao.”

  Amesisitiza: “Aidha, kupitia kwako, naomba unifikishie salamu nyingi za pole kwa familia kwa kuondokewa na kiongozi na mhimili wake. Wajulishe kuwa niko nao katika kuomboleza kifo cha kaka yetu na kiongozi mwenzetu na naelewa machungu yao katika kipindi hiki. Napenda wajue kuwa naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya marehemu. Amina.”  

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  IKULU,
  DAR ES SALAAM

  0 0


  Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania-TRL unapenda, kupitia taarifa hii, kukanusha taarifa zilizochapishwa katika majarida ya Kulikoni la tarehe Aprili 26 – Mei 2 na Fahamu la tarehe 26, April, 2013 kuwa mchakato wa ununuzi wa Vichwa 13 vya treni ulikuwa na utata.

  Ukweli ni kwamba Zabuni ya ununuzi wa vichwa vya treni 13 ilitangazwa kwenye magazeti mbalimbali tarehe 9 na 10 Novemba, 2012. Kabla ya siku ya kufungua zabuni hii ambayo ilikuwa ni tarehe 1 Februari, 2013, TRL ilipokea barua kutoka PPRA iliyopokelewa tarehe 31 Januari, 2013 ambayo iliambatanisha barua ya malalamiko kutoka kwa Kampuni moja ikilalamika kuwa TRL ilikuwa imekiuka Sheria ya Manunuzi kwa kuweka vipengele kwenye zabuni ambavyo viliiengua kampuni hiyo isiweze kushiriki kwenye zabuni.

  Baada ya kupokea barua ya PPRA, TRL ilitathmini hoja ya mlalamikaji kwa kupitia Sheria aliyoitaja pamoja na nyaraka mbalimbali zilizokuwepo. Baada ya tathmini hii TRL ilbaini mambo yafuatayo:

  a)      Mlalamikaji hakuwa miongoni mwa makampuni yaliyokuwa yamenunua nyaraka za zabuni.

  b)      Mlalamikaji alijikita kwenye suala la aina tano tofauti za injini zilizopendekezwa na TRL kutumika kwenye vichwa hivyo vya treni bila kuzingatia kuwa zabuni hii haikuwa ya ununuzi wa injini bali vichwa vya treni. Katika zabuni hii TRL haikuweka masharti yoyote yanayozuia kampuni yoyote duniani kutengeneza vichwa hivyo vya treni.

  c)      Katika barua yake ya malalamiko alieleza kuwa kabla ya kuandika barua kwenda PPRA alikuwa ametuma barua nyingine kwenda TRL akiomba aina ya injini inayotengezwa na kampuni anayoiwakilisha itajwe kama moja ya injini ambazo zingeweza kufungwa kwenye vichwa vya treni ambavyo vingenunuliwa na TRL. Hata hivyo barua aliyoitaja haikuwa imepokelewa na TRL.

  d)      TRL ilijiridhisha kuwa haikuwa imekiuka Sheria ya Manunuzi.

  Baada ya tathmini hii TRL ilipeleka maelezo yake PPRA kwa barua ya tarehe 4 Februari, 2013.

  Ifahamike kwamba taratibu za Rufaa katika Sheria ya Manunuzi ziko wazi. Kama mlalamikaji huyu angekuwa na nia ya kweli kutaka kupata haki yake angefuata utaratibu wa Rufaa ambao umeainishwa katika Sheria hiyo hiyo ya Manunuzi badala ya kutumia vyombo vya habari.

  Uamuzi wa mlalamikaji kutofuata taratibu za kisheria na kuamua kupeleka tuhuma kwenye vyombo vya habari unaonekana ni uamuzi wa kupakana matope ambao hauna tija kwa mlalamikaji, TRL na jamii kwa ujumla.

  Aidha tunatoa rai kwa vyombo vya habari kutokubali kuandika habari kabla ya kuzifanyia utafiti kwani kwa kufanya hivyo jamii ya Watanzania inapotoshwa kwa kiasi kikubwa sana.

  -Mwisho-

  Imetolewa na Afisi ya Uhusiano 
  kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,

  Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu

  Dar es Salaam

  Aprili 30, 2013


  0 0

   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiongozana na balozi wa Canada nchini Tanzania Alexandre Leveque, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Migombani.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na balozi wa Canada nchini Tanzania Alexandre Leveque, ofisini kwake Migombani.
  Picha na Salmin Said, OMKR

  Na Hassan Hamad
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameihakikishia Canada kuwa Zanzibar ina maeneo mazuri ya kuwekeza na kuwaomba wawekezaji wa nchi hiyo kuja kuwekeza katika Nyanja tofauti zikiwemo ujenzi wa hoteli kubwa za kitalii, kumbi za mikutano na uvuvi wa bahari kuu.
  Amesema Zanzibar ina mahitaji makubwa ya uwekezaji katika maeneo hayo, na kwamba hatua hiyo itasaidia kukuza uchumi wa taifa na kunyanyua kipato cha wananchi.
  Akizungumza na balozi wa Canada nchini Tanzania balozi Alexandre Leveque ofisini kwake Migombani, Maalim Seif amesema serikali imelenga kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ili kuwawezesha wawekezaji wa ndani na nje kuja kuwekeza miradi mbali mbali ya kiuchumi.
  Aidha Maalim Seif ameiomba nchi hiyo kuangalia uwezekano wa kuleta wataalamu wa Afya na walimu wa sayansi, ili kupunguza tatizo la wataalamu hao nchini.
  Amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana katika sekta hizo, lakini bado zina upungufu wa wataalamu wakiwemo madaktari wenye sifa, pamoja walimu wa masomo ya sayansi.
  Amesifu mchango wa nchi hiyo hasa katika sekta za afya na elimu na kutaka isichoke kutoa misaada yake katika kusaidia kunyanyua uchumi wa Zanzibar.
  Kwa upande wake balozi Alexandre amesema Canada imekuwa ikihamasisha wawekezaji binafsi, na kuahidi kuwahamisha kuja kuwekeza Zanzibar.
  Kuhusu upatikanaji wa wataalamu wa Afya na walimu wa Sayansi, balozi huyo amesema atawasiliana na mamlaka zinazohusika, ili kupata wataalamu wakiwemo wa kujitolea, watakaoweza kuja kufanya kazi  katika maeneo hayo.
  Amesema Canada inajivunia uhusiano wa muda mrefu uliopo kati yake ya Zanzibar, na kwamba uhusiano huo utaendelezwa kwa maslahi ya pande hizo mbili.
  0 0


  0 0
 • 05/01/13--02:21: kumbukumbu

 • MAREHEMU PIUS WILFRED SHANGALI.


  Ni Miaka 5 sasa tangu ulipotutoka ghafla alasiri ya tarehe 30/4/ 2008 huko nchini  Ujerumani.  Hakika ilikuwa ngumu sana kukubaliana na  taarifa za kifo chako kwani ni wiki 2 kabla ya taarifa hizo ulikuja kutusalimia hapa nyumbani Tanzania, Laiti tungejua ulikuwa umekuja kutuaga na hatutaonana tena. Mpendwa na kiongozi wa familia yetu, tunaamini umepumzika kwa amani, japo hatuko nawe kimwili lakini imekuwa vigumu mno kukusahau kulingana na umuhimu na nafasi uliyokuwa nayo kwenye familia yetu.


  Unakumbukwa na Wazazi wako Mr & Mrs W. Shangali,dada na wadogo zako Suzy,Jane,Theophil,John,Christer na Bertha.  Umetuachia fumbo zito lakini kwa yote tunamshukuru Mungu kwani umetuachia mengi ya kuiga, Hekima zako, upendo, upole, uvumilivu vimebaki mioyoni mwetu na tutavienzi daima.


  Tunaamini kukutana paradiso ya milele. upumzike kwa amani kaka Pius.

  Jina la Bwana libarikiwe . Amen.


  0 0


  Ndugu zangu,
  Februari 6 mwaka huu nilipata bahati ya kukutana na kuongea na wake wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini. Ilikuwa ni nyumbani kwa Balozi wa Sudan.

  Kwenye mazungumzo yangu ( Pichani) niliongelea umuhimu wa Jumuiya hiyo ya wake wa Mabalozi kuendelea kuchangia elimu ya wasichana waliokatishwa masomo.
  Kwamba ni haki kupata elimu na pia kumpa msichana nafasi ya pili katika maisha.

  Nikakumbushia historia ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Jamii kwa kutolea mfano nchi ya Sweden. Kwamba kwa hapa nchini Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi vimetokana na urafiki wa kati ya Rais wa kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere na Waziri Mkuu wa Sweden aliyeuawa, Olof Palme.

  Kwamba ni kutokana na ziara ya Julius Nyerere Sweden iliyopelekea avione Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi vya huko na kuamua kuiga mfano huo. Hapa nchini Vyuo hivyo vilianzishwa katikati ya miaka ya 70. Idadi ya vyuo hivyo kwa sasa ni 53.

  Niakaelezea pia umuhimu wa elimu na namna binadamu tunavyopata maarifa. Kwamba tunapata maarifa kutokana na milango mitatu; Uzoefu ( Fronesis) Shule ( Episteme) na Vipaji ( Tekne). Nilifafanua hayo kwa kutolea mifano hai.

  Na kwamba , wasichana hao wanaokatishwa masomo yao wengine kwa kubakwa na walimu wao nao wana uzoefu ambao, ukichanganywa na elimu ya darasani na vipaji vyao, wanaweza kwenda mbele kimaisha na kutoa mchango katika ujenzi wa nchi yao.

  Juzi, kupitia Shirika la Karibu Tanzania Association, wake hao wa Mabalozi wametoa mchango wa takribani shilingi milioni 4 kusaidia miradi ya kujitegemea ikiwamo ufugaji wa kuku wa kienyeji na bustani inayofanywa na wasichana hao kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi vya Njombe, Ilula na Ulembwe.

  Tunawashukuru kwa mchango huo, na kubwa kabisa, ni kwa wao kufikisha ujumbe, kuwa kuna umuhimu kwa wasichana waliokatishwa masomo kwa sababu ya uja uzito kupewa nafasi ya pili maishani.

  MAGGID MJENGWA  0 0

   Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe.  Ali Ahmed saleh akikata keki na mgeni rasmi katika sherehe hii Mheshimiwa Ahmed bin Mohamed bin Salim Al Futaisi, Waziri  wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Oman 
  Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe.  Ali Ahmed saleh akihutubia.
  Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Dkt Hamisi Kigwangwalla


  Bungeni, Dodoma, Mei 1, 2013.

   

  Nawasalimu kwa heshima na taadhima.
  Napenda kutumia fursa hii kutoa taarifa kwa wanahabari na umma kwa ujumla kufuatia habari iliyotoka leo mapema asubuhi kwenye gazeti la Sauti ya watu Tanzania Daima, toleo Na.3071 na kuzua mjadala mkubwa na mzito kwenye jamii pamoja na kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na hadhi, heshima na uadilifu wangu kwenye jamii nikiwa kama kiongozi wa umma. Niwape pole wale wote walioguswa na kushughulishwa na jambo hili, haswa familia yangu, ndugu, marafiki na wananchi wa Nzega; ambao siku zote wanaamini sana katika uadilifu wangu na namna ninavyosimamia misingi ya haki, sheria na uzalendo.

  Nimesikitishwa sana na habari  hii hususan kwa kuwa ilichapishwa bila kunipa fursa ya kueleza kwa mapana uhusika wangu. Niwapongeze gazeti la Nipashe kwa kupuuza uzushi huu mara baada ya kunipigia na kueleza upande wangu wa hadithi.

  Kumekuwa na wimbi kubwa la baadhi ya watu kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari za uongo kwa maslahi maovu ya kuwachafua wanasiasa na watu wengine. Watanzania sote tubadilike na tukatae tabia za kutumika vibaya namna hii, maana ni hatari kwa ustawi wa weledi, na kwa umoja na mshkamano wa kitaifa. Ukishaandika jambo ambalo litamchafua mwenziyo, hata kama utamsafisha kiasi gani ni wazi hautokuwa na uhakika kuwa utawafikia wale wale waliosoma zile za jana za kumchafua – hivyo ni jambo la kawaida kabisa kuanza kwanza kwa kuwa na uhakika kabisa na habari kabla ya kuiandika. 

  0 0

  Jonia Bwakea, Afisa Habari wa KNCU, akikabidhi zawadi ya Kahawa inayokaangwa na kufungashwa na KNCU kwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh.Leonidas Gama wakati wa sherehe za siku ya Mei Mosi zilizofanyika ndani uwannja wa Chuo cha Ushirika Moshi.
   Wafanyakazi tawi la TCCCo, kiwanda cha kukoboa Kahawa wakiwa ktk maandamano.
   Wanyama waliokaushwa, kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii. 
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0


  0 0


  Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wanamuziki walioingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa New World Cinema,Mwenge,jijini Dar es Salaam.
  Mdau wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013,Taji Liundi akitoa maelezo ya kina namna mchakato wa Academy ulivyofanyika na mpaka kuwapata washindani walioingia kwenye kinyang'anyiro hicho,wakati wa semina ya siku moja kwa wanamuziki watakaowania tuzo hizo, iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa New World Cinema,Mwenge,jijini Dar es Salaam.
  Kiongozi wa Kundi la TMK Wanaume Family,Said Fella akiuliza swali kwa Wadau wa wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013.
  Mkongwe wa Muziki wa Miondoko ya Mwambao (Taarab) hapa nchini,Khadija Koppa akiuliza swali lake lenye kutaka kufahamu kwamba kwanini Bendi ya TOT haijawahi kuingizwa kwenye kinyang'anyiro cha Tuzo hizo na wakati yeye amekuwa akiingia mara nyingi?
  Sehemu ya washiriki wa Semina hiyo ya siku moja ya wanamuziki walioingia kwenye kinyang'anyiro cha Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013  iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa New World Cinema,Mwenge,jijini Dar es Salaam.

  KUONA PICHA ZAIDI ZA SEMINA HIYO

  0 0

  This is a group founded by KCMC (Kilimanjaro Christian Medical University College)students 3 years ago aimed at helping children who are less fortunate (orphans ,street children etc ) achieve their dreams, have a chance at

  life and a bright future . If you feel you can participate or support us in any way or means (currently based in Moshi, Tanzania), Contact us: email-sal.kcmc@gmail.com


  The Hand Washing Campaign kicked off well at Msamaria Centre and Children of Destiny in moshi this last sunday .we would like to thank all who participated in one way or another

  " Cleaning hands saving. Lives"
  children at msamaria in handwashing training.
  MAMA MSAMARIA shows the children how its done .
  Children at the children of destiny in handwashing training.
  Talking to the children about their handwashing knowledge attitude and practice before the training children of destiny

  0 0
 • 05/01/13--12:49: Article 19


 • 0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi Gazeti la Mfanyakazi wakati wa kilele cha Sherehe ya Sikukuu ya Wafanyakazi,Mei mosi zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa michezo wa Sokoine mkoani Mbeya.kushoto ni Kaimu Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Bi.Nortiburga Maskini na kulia ni Katibu mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Ndugu Nicholaus Mgaya(picha na Freddy Maro)

  0 0


   Muwakilishi kutoka benki ya NMB akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya TANESCO,mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika  bonanza la soka la Mei Mosi lililojulikana kwa jina la Sports Bar & Sports Xtra Day,lililoratibiwa na Clouds Media Group na kufanyika kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.Bonaza hilo lilijumuisha makampuni 14 na yote yalichuana vikali kuhakikisha kila mmoja anajitahidi kushinda ili kulinda heshima.Lengo la la bonanza hilo ilikuwa ni kuwaweka pamoja wafanyakazi wa kampuni mbalimbali ili waweze kufahamiana na pia kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwao.
  Pichani kulia ni Meneja wa bia ya Castle Lager (TBL) kabula Nshimo akimkabidhi nahodha wa timu ya Fast Jet kikombe kwa kuibuka washindi wa pili katika bonanza la soka la Mei Mosi lililojulikana kwa jina la Sports Bar & Sports Xtra Day,lililoratibiwa na Clouds Media Group.
   Baadhi ya wachezaji  na washabiki wa timu ya Fast Jet wakishgalia kombe lao mara baada ya kunyakua nafasi ya washindi wa pili.
   Mchezaji wa timu ya Clouds Media Group,Ben Kinyaia akiwatoka wachezaji wa timu ya TBL
   Mchezaji wa timu ya TANESCO akimchomoka mchezaji wa timu ya Fast jet,wakati wa fainali yao iliyowakutanisha pamoja,ambapo timu ya TANESCO waliibuka kinara kwa kuifunga timu hiyo ya Fast Jet goli 1-0,na hatimaye kunyakua kombe la ushindi katika bonanza hilo lililofana kwa kiasi kikubwa.
  Baada ya mpira wa miguu kuisha na kuwapata washindi,pia kulikuwepo na burudani iliyotolewa na bendi ya muziki wa dansi ya Skylight pamoja na wasanii mbalimbali kutoka THT.

  0 0

  NEEMA HERBALIST & NUTRTITIONAL FOODS CLINIC ni wauzaji wa dawa mbalimbali za asili. Tunayo dawa nzuri na ya asili ya KUONDOA KITAMBI. Dawa hii ni ya asili “ pure herbal “, haijachanganywa na kemikali yoyote, haina side effect kwa mtumiaji na inaondoa kitambi ndani ya siku kumi na nne tu. Bei yake ni Shilingi Elfu Arobaini Tu ( Tsh 40,000/=)

  Tunapatikana jijini Dar Es salaam, katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU. Vile vile tunafanya ‘delivery’ kwa wateja wasio weza kufika ofisini kwetu, na kwa wateja wa mikoani tunawatumia kwa njia ya mabasi, wateja waliopo Zanzibar tunawatumia dawa kwa njia ya meli na kwa wateja waliopo nje ya nchi tunawatumia kwa magari, DHL, ama posta kulingana na nchi waliyopo.

  PIA tunayo dawa ya asili iitwayo JIKO ambayo hutibu tatizo la ukosefu na upungufu wa nguvu za kiume.

  Wasiliana Nasi kwa Simu : 0767010756 au 0766538384. 
  Website http://www.neemaherbalist.blogspot.com


  0 0  Bayern Munich will contest a third Champions League final in four years after a 3 - 0 win at the Camp Nou gave them a crushing 7 - 0 aggregate victory over Barcelona, who were without Lionel Messi.

  Robben and Thomas Muller were both on target with Gerard Pique putting through his own net on a miserable night for the Catalan giants.

older | 1 | .... | 118 | 119 | (Page 120) | 121 | 122 | .... | 3270 | newer