Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live

GS1 TANZANIA WAMESAINI MKATABA WA MAKUBALIANO NA TBS

$
0
0
Mkutano ulifanyika katika ofisi ya TIRDO ambayo ni Taasisi tanzu ya Wizara ya Viwanda na biashara, ambapo kulishuhudiwa utiwaji saini wa makubaliano kati ya GS1 Tanzania na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika kushirikiana kufanya kazi pamoja na kujenga mahusiano ambayo ni muhimu haswa kwa wazalishaji wa Tanzania kwani alama ya utambuzi wa bidhaa kwa sasa zinahitajika katika masoko yote ya ndani na nje ya nchi.
TBS imekua ikishirikiana na GS1 Tanzania katika uelimishaji wajasiliamali ambayo mafunzo kadhaa kati ya Taasisi hizi mbili yameshafanyika huko mkoani.
Wazalishaji wa Tanzania wanaotumia Barcode za nje ya nchi wanaaswa kubadilisha na kutumia Barcode(alama za uzalishaji) za hapa nchini kwani itasaidia::
  • Kupunguza matumizi ya fedha za kigeni ambazo zingetumika kulipia huduma hiyo.
  • Kutupa takwimu rasmi za wazalishaji kwani kutumia barcode za nje ya nchi bidhaa inaonekana imetoka kwenye nchi nyingine na sio Tanzania.
  • Kuwepo kwa utambulisho kwa bidhaa za Tanzania kwani nambari tatu za mwanzo za Barcode zinaonyesha bidhaa zinatoka nchi gani, ambapo kwa bidhaa za Tanzania utambulisho wetu ni 620.
  • Mwisho ni suala zima la uzalendo, tujivunie cha kwetu.
Kuna wazalishaji wa Tanzania 13 tu ambao wamechukua alama za uzalishaji (barcode), sio tu wameonesha uzalendo bali wameendana na matakwa ya masoko yaliyo rasmi ya ndani na nje ya nchi. Huduma hii kama umekamilisha matakwa yote unaipata ndani ya siku moja tu.
GS1 Tanzania inahudumia nchi zaidi ya tano ambazo hazina huduma hii nazo ni Rwanda, Burundi, Uganda, Zambia, Malawi na Mozambique.
GSM 1 Tz-30
Mwenyekiti wa bodi GS1 Tanzania Dr. Gedion Mazara alifungua kikao kwa kuelezea kuhusu alama za utambulisho (barcode) na umuhimu wake.
GSM 1 Tz-38
Mkurugenzi mkuu wa GS1 Tanzania pia aliongelea ni jinsi gani wazalishaji wakipata na kutumia barcode/alama za uzalishaji itasaidia sana nchi
GSM 1 Tz-47
Mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Uhamishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo.


KATIBU WA CHADEMA MKOA WA DAR ES SALAAM AZUNGUMZA MIKAKATI MBALIMBALI YA CHAMA CHAO.

$
0
0
 Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar  es salaam, Henry Kileo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo  juu ya mikakati mbalimbali ya chama hicho kulia ni Makamu  Mwenyekiti wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es salaam, Benard Mwakyembe.
Makamu  Mwenyekiti wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es salaam, Benard Mwakyembe  akizungumza na waandishi wa habari juu wananchi wanavyokosa habari wakati bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kuto kuonyesha matangazo ya chama chao
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

MILIONI 967 ZANUSURU KAYA MASIKINI WILAYANI MUFINDI KWA KIPINDI CHA MIEZI 08

$
0
0
Zaidi ya shilingi milioni 967 zimetolewa kwa kaya masikini zipatazo elfu 07   Wilayani Mufindi, ikiwa ni kipindi cha miezi 08 tangu kuasisiwa kwa mpango wa miaka 03 wenye lengo la kuzinusuru kaya masikini, unaoratibiwa na mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF wilani humo.

 Afisa habari na mawasiliano wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi, Ndimmyake Mpokigwa Mwakapiso, amesema, kuanzi kipindi cha mwezi Oktoba mwaka jana hadi mwezi huu. kiasi cha shilingi milioni 967  laki tisa tisini na sita elfu, zimetolewa kama ruzuku kwa wanufaika elfu 07 miatisa 51 kutoka katika vijiji na mitaa 94.

Akibainisha baadhi ya mafanikio waliyoyapata wanufaika wa mpango huo, amesema kupitia ruzuku wanayoipata baadhi yao wameweza kuanzisha biashara na shughuli za kijasiliamali, kununua pembejeo za kilimo ambazo huzitumia katika mashamba yao, kununua chakula, kusomesha watoto, kununua bati kwa kila awamu wanayopokea fedha ili kujenga makazi ya kudumu huku kaya Zaidi ya elfu 03 zikijiunga na mifuko ya bima ya afya.

Aidha, pamoja na mafanikio yaliyofikiwa, baadhi ya changamoto zinazojitokeza miongoni mwa wanufaika  ni pamoja na kuzitumia fedha hizo kwenye ulevi, baadhi ya akinamama kutokuwa wawazi kwa kaya zao mara baada ya kupokea fedha huku baadhi ya wanaume wakiwanyang’anya wake zao fedha wanazopokea kwa matumizi ya kaya na kwenda kuzitumia kwa matumizi mengine ya anasa Jambo ambalo ni kinyume na malengo.

Mpango huu wa Kiserikali  ulianza rasmi mwaka 2015 chini ya uratibu wa  mfuko wa maendeleo ya jamii nchini TASAF kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Mufindi, ukiwa na shabaha ya kuzinusuru kaya masikini zaidi zlizokuwa zikiishi katika dibwi la umasikini wa kupindukia Wilayani humo.

TAARIFA YA MABASI YAENDAYO KASI HAPO KESHO JIJINI DAR

$
0
0
MABASI YATAANZA SAFARI SAA KUMI NA MBILI KASORO ROBO KUTOKEA DEPOT YA JANGWANI KWA MPANGILIO UFUATAO.
1. RUTI YA KIMARA- KIVUKONI  Mabasi Sita (6). Kati ya mabasi Hayo sita wakati wa Kutoka Jangwani matatu yataenda Kimara na Matatu Kivukoni.

2. RUTI YA KIMARA - KARIAKOO Mabasi Sita (6). Kati ya hayo Matatu yataelekea Kariakoo na Matatu Kimara.

3. RUTI YA UBUNGO - KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi Manne yataelekea Ubungo na Manne Kivukoni.

4. RUTI YA UBUNGO - KARIAKOO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi manne Yataenda Ubungo na Manne yataenda Kariakoo.
5. RUTI YA UBUNGO - MOROCCO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Manne yataenda Ubungo Manne yataenda Morocco.

6. RUTI YA MOROCCO - KARIAKOO Mabasi sita (6). Kati ya hayo mabasi Matatu Morocco na Matatu Kariakoo.

7. RUTI YA MOROCCO - KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya Hayo Mabasi Manne yataenda Moroco na mabasi manne Kivukoni.

DESPATCH PLAN SAA KUMI NA MBILI KAMILI.

1. Kimara Terminal Mabasi Sita (6)

2. Ubungo Terminal Mabasi kumi na mbili (12)
3. Morocco Termial Mabasi kumi na moja (11)

4. Kariakoo Terminal Mabasi kumi  (10)

5. Kivukoni Terminal Mabasi kumi na moja (11)

JUMLA.NI MABASI HAMSINI (50)

NAOMBA KUWASILISHA

Naibu Waziri Jafo Awataka Watendaji kutembelea maeneo yao ya kazi

$
0
0
Na Rebecca Kwandu

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa na utaratibu wa kutembelea maeneo yao ya kazi mara kwa mara ili kujionea hali halisi na kutatua kero zilizopo.

Akizungumza na walimu wa shule ya msingi Nzuguni B. wakati wa ziara aliyoifanya kutembelea shule  hiyo na shule ya sekondari Nzuguni A., Mhe. Jafo alisema watumishi hawawezi kufanya kazi kwa ubora iwapo watakuwa hawatembelei na kukagua maeneo yao ya kazi.

“ Kumekuwa na uzembe kwa Wakuu wa Idara kutokusikiliza matatizo ya chini, kutowatembelea watumishi waliopo chini yetu inawasababishia kukosa mahali pa kusemea shida zao na kuchanganyikiwa. Ni vizuri kuwa na utaratibu wa kuwatembelea watumishi tunaowaongoza ili kujua shida zao na kuzitatua. Alisisitiza Mhe. Jafo.

Aidha, aliwataka walimu wa shule za msingi Nzuguni B na Shule ya sekondari Nzuguni A kuweka utaratibu wa kuweka malengo na kujipima kuona walichokifanya ili kupata matokeo tarajiwa.

Wakati huo huo, Naibu  Waziri wa Nchi Jafo ametoa Mabati 164 ili kuchangia ujenzi wa Madarasa ya shule ya msingi Nzuguni B iliyopo kata ya Nzuguni katika halmashauri ya Mji wa Dodoma.

Mhe. Jafo alitoa Mabati hayo baada ya kufanya ziara ya kutembelea shule hiyo ili kujionea hali halisi ya maendeleo yake ikiwa ni moja ya taratibu alizojiwekea za kutembelea maeneo mbalimbali yanayohudumiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI ili kujionea changamoto mbalimbali zilizopo katika utoaji wa huduma na kuzitafutia ufumbuzi.

Katika ziara hiyo Mhe. Jafo alikuta Idadi  kubwa ya watoto walioandikishwa kujiunga na darasa la kwanza hali iliyopelekea kukosekana kwa vyumba vya kutosha kwa ajili ya kujifunzia wanafunzi ambapo kwa kutatua kero hiyo, shule hiyo imeanza ujenzi wa vyumba vya madarasa na kwa upande wake alichangia bati 164 ili kuwezesha madarasa hayo kukamilika.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kutembelea shule ya msingi Nzuguni B. Kulia kwake ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Mstahiki Jaffari Mwanyemba aliyeongozana na Mhe. Naibu waziri katika ziara hiyo.

Mafanikio ya ziara ya wafanyabiashara wa Oman nchini

$
0
0
Na: Immaculate Makilika – MAELEZO.

Tanzania na Oman zimesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya Tanzania Chambers of Commerce na Oman Chambers of Commerce ili kuanzisha Kampuni ya Oman Tanzania Investment (OTIC) kwa lengo la kutafuta fursa za uwekezaji zilizoko Tanzania na Oman.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Bibi. Mindi Kasiga amesema kuwa mkataba huo ni matokeo ya ziara ya siku tatu ya Waziri Viwanda na biashara wa Oman , Dkt. Ally Mohamed Al Sunaidy, pamoja na ujumbe wa wafanyabiashara 108 na maafisa wa Serikali ya Oman iliyofanyika nchini mwezi Aprili mwaka huu.

Amesema lengo la ziara hiyo lilikua kuwawezesha wafanyabishara wa Oman na Tanzania kushiriki kongamamo la biashara la uwekezaji lililowawezesha wafanya bishara hao kubaini fursa za uwekezaji zilizoko nchini Tanzania na Oman.

Amesema tayari Serikali ya Oman imeonesha nia ya kuwekeza katika kiwanda cha Sukari cha Kagera kilichopo mjini Morogoro ambacho kitazalisha tani laki nne za sukari itakayouzwa hapa nchini huku Tanzania ikitarajia kuzalisha spiriti na hamira itakayouzwa nchini Oman pamoja na nchi za Mashariki ya kati.‘’ Wafanyabishara wetu na wale wa Oman kupitia makubaliano haya watanufaika na fursa za uwekezaji kwa kupata mikopo mbalimbali na tayari mtaji wa Dola za Marekani milioni 25 zitatumika kwa wawekezaji hao’’ Amesema Bibi. Kasiga.

Aidha,amesema Wafanyabiashara kutoka Oman tayari wameonesha nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo madini, viwanda na biashara, kilimo, utalii pamoja na ujenzi wa nyumba za kisasa katika miji ya Dar es Salaam na Zanzibar.Ameongeza kuwa uwekezaji utaongeza ajira akitoa mfano wa kiwanda cha Sukari cha Kagera kitakachozalisha ajira 500 pamoja na kuongeza wigo wa soko.

Katika hatua amesema kuwa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa itawapeleka watumishi 105 wa ngazi mbalimbali katika Balozi 35 zilizo katika nchi mbalimbali duniani na kuwarudisha nyumbani watumishi 79.Bibi Mindi, ametaja sababu za kurudishwa kwa watumishi hao kuwa ni pamoja kuisha kwa muda wao wa kuhudumu nje ya nchi ambao ni miaka minne(tour on duty) pamoja, kustaafu na sababu mbalimbali.Amezitaja Kada za watumishi wanaorudishwa nchini kuwa ni mabalozi, wahasibu, makatibu muhktasi na maofisa wa ngazi mbalimbali.

Hata hivyo, hadi kufikia sasa tayari mabalozi watatu wamerudishwa nchini ambao ni Balozi Peter Kalaghe aliyekuwa Uingereza, Balozi James Msekela aliyekuwa Italia na Balozi Batilda Burian aliyekuwa Japan kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa Januari 25, 2016 kuitaka wizara hiyo kuwarudisha nchini mabalozi waliomaliza muda wao wa kuhudumu ili wapangiwe kazi nyingine.

DIWANI KATA YA KIWALANI ACHAGULIWA KUWA NAIBU MEYA WA JIJI LA DAR

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWASILI MKOANI ARUSHA KUFUNGUA MKUTANO WA NANE WA MAWAZIRI WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua vikundi mbalimbali vya ngoma alipowasili Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro kwa ajili ya kufungua Mkutano wa nane wa kikao cha kawaida kuhusu matumizi ya silaha ndogondogo katika nchi za maziwa makuu na pembe ya Afrika unaotarajiwa kuanza kesho April 22, 2016 Mkoani Arusha Picha na OMR.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua vikundi mbalimbali vya ngoma alipowasili Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro kwa ajili ya kufungua Mkutano wa nane wa kikao cha kawaida kuhusu matumizi ya silaha ndogondogo katika nchi za maziwa makuu na pembe ya Afrika unaotarajiwa kuanza kesho April 22, 2016 Mkoani Arusha Picha na OMR.



CHAIRMAN OF UBA GROUP PLC, TONY ELUMELU HONOURED WITH LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD IN ABIDJAN

$
0
0
Tony Elumelu
At the 5th edition of the annual forum, CGECI Academy 2016, the Ivorian National Council of Employers, General Confederation of Enterprises of Côte d'Ivoire (CGECI) presented African businessman and investor, Tony Elumelu, with its 2016 CGECI Lifetime Achievement Award on April 21, 2016 in Abidjan, Côte d’Ivoire. The formal presentation was to honour Mr. Elumelu on his leadership and key role as an African business champion. The event was attended by over three thousand delegates across Africa including top government officials, business leaders, established and aspiring entrepreneurs.

Addressing guests present at the event, Chairman of African investments company, Heirs Holdings, UBA Plc and Transcorp Plc, Mr. Tony Elumelu delivered a keynote speech where he advocated for the collaboration of the private and public sectors to create value in the global competitive business landscape. He said, “SMEs are the backbone of any economy anywhere in the world. And when governments ignore the private sector and fail to attend to their obligations to create and sustain enabling environments for businesses to thrive and flourish, the consequences are stark - low GDP growth, mass unemployment, ethnic strife and possibly, even food and health crises and in some cases, violent conflict”.

Mr. Elumelu also addressed entrepreneurs, urging them to seek opportunities to accelerate their business success — including through The Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship Programme (TEEP). “We are champions of African development because we are Africapitalists. Through Africapitalism, I seek to evangelize what works for successful business investments and inspire other entrepreneurs like yourselves; to also make the promotion of national and regional development a strategic priority for your businesses”, he said.

TEEP is his 10-year, $100 million commitment, to identify and empower 10,000 African entrepreneurs, create one million jobs and add $10 billion in revenues to Africa’s economy. So far, seventeen (17) entrepreneurs from Côte d'Ivoire have received grants and training from the programme.

Since its initiation in 2012 by the Ivorian National council of Employers, the annual economic forum, CGECI Academy, has provided a platform to raise awareness among African entrepreneurs about existing sources of capital and investors available to help grow and develop their businesses. The forum seeks to change the paradigm of access to finance in Côte d’Ivoire, creating a platform for sharing experiences and expertise. 

Furthermore, it aims to present the Ivorian private sector to regional and international partners and highlight the achievements and the opportunities within it. Other activities during the event include the announcement of the yearly business plan competition and a segment dedicated to sharing the experiences and testimonials of entrepreneurs.

The ceremony was attended by the Prime Minister of Côte d’Ivoire, Daniel Kablan Duncan, and the Prime Minister of Mauritius, Sir Anerood Jugnauth, among other business leaders and senior government officials.

RAIS DKT. MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA KUWASHUKURU WENYEVITI, MAKATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WA MIKOA NA WILAYA ZA TANZANIA BARA NA VISIWANI.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA KUWASHUKURU WENYEVITI, MAKATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WA MIKOA NA WILAYA ZA TANZANIA BARA NA VISIWANI.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wenyeviti, Makatibu wa Chama cha Mapinduzi wa mikoa na Wilaya za Tanzania bara na Visiwani Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wenyeviti wa CCM wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi kumshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akitoa hotuba yake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wenyeviti wa CCM wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi kumshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akitoa hotuba yake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza kwa makini taarifa zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Wenyeviti na Makatibu wa CCM kutoka mikoa mbalimbali nchini. Kulia kwake ni makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti CCM Taifa Philip Mangula na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Mohamed Sinani Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka mikoa mbalimbali nchini mara baada ya kumaliza kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

JOTO LA ASUBUHI LA 93.7 EFM IJUMAA APRILI 22, 2016 KUANZIA SAA 12 ASUBUHI

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

NICO NJOHOLE NA RENATUS NJOHOLE KUONGOZA SIMBA UGHAIBUNI, MPAMBANO WA WATANI WA JADI DALLAS

$
0
0
Kikosi cha Yanga ughaibuni
Kikosi cha Simba ughaibuni

Wanandugu wawili Nicodemus Njohole na Renatus Njohole ambao kwenye nyakati tofauti waliwahi kuchezea timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, wamethibitisha kuichezea timu ya Simba ughaibuni kwenye mpambano wa watani wa jadi utakaofanyika siku ya Jumamosi April 30, 2016 jijini Dallas, Texas nchini Marekani.

Hii itakua ni mara ya tatu kwa mpambano huu wa Simba na Yanga kuchezwa nje ya DC. Kama ilivyozoeleka watani hawa wa jadi mara nyingi mechi zao hufanyikia Washington, DC, na mara zote Yanga inaibuka mshindi.
Majimbo mengi ambako mpambano huu ulishawahi fanyika ni Columbus, Ohio na Houston, Texas.
Vijimambo ingiongea na Renatus Njohole kutokea nchini Switzerland na kuthibitisha kuiongoza Simba yeye na kaka yake Nico Njohole kwenye mpambano utakaochezwa Dallas katika kiwanja cha Hufthines Recreation Center ambacho anuani yake ni 200 N Piano Road, Richardson, TX 75081. Nicodemus yeye anaishi London, Uingereza.
Mapambano huu utakua wa wazi kwa mashabiki na wachezaji kujumuika pamoja na kuandika historia ambako kwa mara ya kwanza utaandika historia mpya ya kuchezwa na wachezaji wawili waliowahi kuichezea Club ya Simba. Michezo mingine iyakayokuwepo ni mpirsa wa kikapu na mpira wa wavu ikienda sambamba na nyama choma.
Mechi hii inayosubiliwa kwa hamu ni sehemu ya burudani itakayokuwepo kwenye kongamano la DICOTA ambalo mwaka huu linafanyika Dallas, Texas kuanzia April 28, mpaka May 1, 2016. Mashabiki na wachezaji wa pande zote wameanza kutupiana vijembe huku mashabiki wa Simba wakifurahia ujio wa Renatus Njohole na kaka yake Nico kuja kutia nguvu timu hiyo ambayo mechi nyingi za Simba na Yanga ughaibuni huishia kupata kipigo kutoka kwa mahasimu wao.
Timu ya Simba ughaibuni ina historia nzuri inapocheza nje ya DC, mara zote imeibuka mshindi.
Huu utakua mpambano wa pili wa Simba na Yanga kugombea kombe la DICOTA mara ya kwanza timu hizi zilikutana kwenye kongamano la DICOTA lililofanyika Washington, DC mwaka 2011 na kongamano hilo Rais mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete ndiye aliyekua mgeni rasmi kwenye kongamano hilo..

JAJI MKUU AWATAKA WATUMISHI WA MAHAKAMA MKOA WA MBEYA KUFANYA KAZI YA UTOAJI HAKI KWA UADILIFU.

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman  akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman  amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli za Mahakama katika Kanda ya Mbeya. 

Ziara ya Mhe. Jaji Mkuu katika kanda hii imelenga kujionea hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha Watumishi wa Mahakama kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuboresha huduma ya utoaji haki nchini. 

Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu aliambatana na Maafisa na Watendaji kadhaa wa Mahakama kutoka Makao makuu ili kujionea hali ya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kubainisha na kufanyia kazi changamoto ambazo watumishi wanakumbana nazo katika utendaji kazi wa kila siku. 
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, (katikati) akipata taarifa fupi ya utendaji kazi wa Mahakama Kanda ya Mbeya kutoka kwa Mhe. Noel. P. Chocha, Jaji Mfawidhi Kanda ya Mbeya (aliyesimama), mara baada ya kuwasili katika kikao kilichohusisha Mahakimu Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya.

Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye alipata nafasi ya kukagua na kuongea na Watumishi wa ngazi mbalimbali za Mahakama katika mkoa huo.

Katika kikao alichofanya na Watumishi wa Mahakama mkoani humo ikiwa ni pamoja na Wahe. Majaji na Mahakimu, Mhe. Jaji Mkuu alisisitiza mara zote juu ya utendaji kazi kwa kujituma ili kubadili taswira ya Mahakama kwa wananchi ambao ndio wadau muhimu wa Mahakama.
Akiongea na Watumishi wa Mahakama wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Jaji Mkuu alieleza kufurahishwa na kasi ya usikilizaji na umalizwaji wa mashauri katika Mahakama za Mwanzo mkoani humo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman akizungumza na  Mahakimu Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya alipokutana nao na kuwaasa kuendelea kutenda Haki kwa wakati ili kuweza kupunguza na kumaliza mashauri yanayowasilishwa mahakamani.

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WATATU KUTOKA NCHI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Balozi wa Vatican hapa nchini anayemaliza muda wake nchini Francisco Montecillo.
  Balozi wa Algeria hapa nchini Belabed Saada akikabidhi ujumbe uliotoka kwa Rais wa Algeria kuja kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa Canada hapa nchini Alexandre Leveque wapili kutoka kulia pamoja na waakilishi wengine wa Serikali pamoja na Ubalozi wa Canada.
PICHA NA IKULU.

MUOGELEAJI WA TANZANIA HILAL HILAL ATWAA MEDALI YA SHABA DUBAI.

$
0
0
 Muogeleaji nyota wa kiume wa Tanzania, Hilal Hilal (wa kwanza kulia) akiwa kwenye jukwaa mara baada ya kupokea medali yake ya Shaba katika mashindano ya Kanda ya Nne ya Cana. 
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kinanchoshiriki katika mashindano ya Cana Kanda  ya nne. kutoka kulia ni Amani Doggart, Catherine Mason, Hilal Hilal na Smriti Gokarn.

Na Mwandishi wetu
Muogeleaji wa Tanzania, Hilal Hilal ametwaa medali ya Shaba katika mashindano ya kuogea ya Cana Kanda ya Nne yanayoendelea nchini Mauritius.

Hilal ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa katika mchezo huo, amemaliza katika nafasi ya tatu katika staili ya butterfly kwa kutumia muda wa sekunde 26.70 katika mashindano hayo magumu yaliyoshirikisha nchi za Uganda, Kenya, Rwanda Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Somalia, Sudani Kusini na Sudan.

Muhimbili Yatoa ufafanuzi kuhusu matibabu ya wagonjwa wa Selimundu (Sickle Cell).

$
0
0
Na Magreth Kinabo- Maelezo.

 Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) umetoa ufafanuzi kuhusu  matibabu ya wagonjwa wa Selimundu(Sickle cell) ambapo umesema kwamba  hudumma hiyo haijasitishwa kama ilivyoelezwa  na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

 Ufafanuzi huo, umetolewa leo na   Mkuu wa   Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Aminiel  Eligaesha  kuupitia taarifa kwa vyombo vya habari ,ambapo amesema uongozi wa  hospitali hiyo haina mpango wa kusitisha huduma hiyo.

“Watu wanaoeneza uvumi huo kuwa  huduma hii imesitishwa  wana maslahi yao binafsi kuhusu tiba ya wagonjwa hawa,”   alisema Eligaisha.

 Aliongeza kwamba ni kweli huduma hiyo imekuwa ikitolewa  kwa kipindi cha miaka kumi, hivyo kulikuwa na mradi uliokuwa ukifadhili matibabu  ya pamoja na utafiti wagonjwa wa Selimundu, ambao muda wake umeisha 31 Machi,  mwaka huu  kwa sababu ya utafiti ulihitaji wagonjwa wote kuja muhimbili kwa ajili ya utafiti na tiba.

 Mkuu huyo alisema  hivyo basi  hali hii ilisababisha wanaohitaji  huduma ya selimundu kufuata matibabu hospitalini hapo, licha ya kwamba  mahitahi yao hayakuhitaji wataalamu wa MNH.

“ Tunaomba jamii ikumbuke kabla ya mradi huo, hospitali hiyo  ilikuwa inatibu wagnjwa  hao waliokuwa  wanapata rufaa, hivyo baada ya mradi huo kuisha hospitali hiyo  imewaagiza wagonjwa hao kufuata mfumo wa kawaida kama ilivyo kwa wagonjwa wengine. Hii ina maana kwamba wagonjwa hao wasiohitaji  wataalamu   wetu wattaendelea  na huduma  katika hospitali  zilizo karibu nao na watakao onwa na  Muhimbili  ni wale watakaopata rufaa kutokana na matatizo yao,” alisisitiza.

 Aidha Eligaesha  alisema wagonjwa hao  wanaohitaji huduma yao watapata huduma za matibabu kwa mujibu wa taratibu  na kanuni zilizopo bila ya ubaguzi.

WAZIRI MKUU: TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA LAPUNGUA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana nchini kimepungua kwa asilimia 2.5 na kwamba Serikali itaendeleza juhudi za kuvutia uwekezaji ili kupunguza zaidi kiwango hicho.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Aprili 22, 2016) wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapatona matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma.

“Utafiti wa hali ya ajira nchini wa mwaka 2014 umeonesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kimepungua kutoka asilimia 11.7 mwaka 2006 hadi asilimia 10.3 mwaka 2014. Aidha, ukosefu wa ajira  kwa vijana umepungua kutoka asilimia 14.2 mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 mwaka 2014,” amesema. 

Waziri Mkuu amesema moja ya changamoto zinazosababisha ukosefu wa ajira ni vijana kutojengewa maarifa na ujuzi wa kuajiriwa na kuajirika. Hivyo, Serikali itaendelea kutekeleza Programu ya Miaka Mitano ya Kukuza Ujuzi Nchini (2015/2016 – 2019/2020).

“Programu hiyo inalenga kuongeza idadi ya watu wenye kiwango cha juu cha ujuzi kutoka asilimia tatu ya sasa hadi asilimia 12 inayotakiwa kuendesha uchumi wa viwanda. Vilevile, kupunguza idadi ya watu wenye kiwango cha ujuzi wa chini kutoka asilimia 75 ya sasa hadi asilimia 54,” amesema.

Amewaagiza watendaji wakuu wa wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, taasisi za umma, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha kuwa ukuzaji wa ajira  unakuwa ni agenda ya msingi ya kudumu katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumzia kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu hususan watu wenye ualbino, Waziri Mkuu amesema Serikali inafanya jitihada kubwa kukomesha vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwakamata wote wanaojihusisha na vitendo hivyo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

“Ukatili huo umesababisha watu wenye ualbino kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu. Hali hiyo haikubaliki na haivumiliki katika jamii ya Watanzania. Napenda kusisitiza watu wenye ulemavu wana haki ya kuthaminiwa utu wao na kulindwa dhidi ya ukatili na aina yoyote ya ubaguzi,” amesema.

Waziri Mkuu amesema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itaviboresha Vyuo vya Ufundi na Marekebisho (Vocational and Rehabilitation Training Centres) vya watu wenye ulemavu nchini ili kutoa ujuzi unaoendana na mahitaji yao katika soko la ajira ikiwa ni pamoja na kuandaa walimu wa elimu maalum na kutoa vifaa saidizi kwa walimu na wanafunzi wenye ulemavu mashuleni.

Akitoa maelezo kuhusu juhudi za Serikali kuwawezesha wananchi kiuchumi, Waziri Mkuu amesema Serikali imesaidia uanzishwaji wa taasisi mwavuli ya kusimamia VICOBA inayoitwa VICOBA FETA ambayo imeanza kuonyesha matunda mazuri.

“Takwimu zilizotolewa mwezi Februari 2016 na taasisi hiyo zinaonesha kuwa kuna vikundi 100,000 vya VICOBA vyenye wanachama milioni 2.2 na mtaji wa shilingi trilioni 1.2. Ni jambo la kujivunia kwamba asilimia 79 ya wanachama wa VICOBA ni wanawake,” amesema.

Amezitaka Halmashauri zote nchini ziweke orodha sahihi ya vyama vya ushirika wa kuweka na kukopa vilivyosajiliwa kwa kila kijiji na kuchukua hatua za kuwezesha uanzishaji na usajili wa SACCOs zinazokidhi vigezo kulingana na shughuli za uzalishaji katika Halmashauri husika.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, APRILI 22, 2016.

MKURUGENZI Mkuu wa Zamani wa Mamlaka ya Bandari Tanzania na naibu wake wana kesi ya kujibu - Mahakama ya Kisutu

$
0
0
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) Ephraimu Mgawe (Kulia) na Makamu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamadi Koshuma.
-------------------------------------------------------------
MKURUGENZI Mkuu wa Zamani wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe na Naibu Mkurugenzi Mkuu wake,  Hamadi Koshuma wana kesi inayowakabili ya kujibu dhidi ya mashtaka ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka wameonekana wana kesi ya kujibu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hatua hiyo ilifikiwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Mhe. Cyprian Mkeha, anayesikiliza kesi hiyo baada ya kusikiliza ushahidi wa Jamhuri wa mashahidi watano. 
Hakimu huyo lisema baada ya kusikiliza ushahidi wa Jamhuri, kuita mashahidi watano dhidi ya kesi hiyo, mahakama yake imeona wana kesi ya kujibu. 
Hakimu alisema washtakiwa wanatakiwa kupanda kizimbani kujitetea ili kuondoa maswali katika ushahidi ulioacha mashaka dhidi yao. 
Alisema washtakiwa wataanza kujitetea Mei 16, mwaka huu na dhamana zao zinaendelea.
Katika kesi ya msingi, Desemba 5, mwaka 2011, washtakiwa wakiwa watumishi wa umma, katika utendaji wao wakazi kwa makusudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kusaini mkataba wa kibiashara bila kuitisha zabuni.
Ilidaiwa kuwa mkataba huo ulikuwa kati ya TPA na Kampuni ya ujenzi ya Communication and Construction ya China (CCCC), ambao ulikuwa unahusu ujenzi wa gati namba 13 na 14 katika bandari ya Dar es Salaam, bila kuitisha zabuni.
Ilidaiwa kuwa, kitendo hicho kiliipa faida Kampuni  hiyo ya China.
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live




Latest Images