Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1192 | 1193 | (Page 1194) | 1195 | 1196 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Na Chalila Kibuda, 
  Globu ya Jamii.
  SERIKALI imesema kuanzisha kambi za kufanya operesheni kwa watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa itasaidia kuokoa maisha ya  watoto hao kutokana na wazazi wao kushindwa kumudu gharama za oparesheni hizo.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati makababidhiano ya magari kwa ajili ya kambi hizo, Mwakilishi wa Waziri wa Afya na Maendeleo jamii jinsia, Watoto , Mkuu  wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa Mfuko wa GSM wametambua matatizo ya watoto hao na kuamua kutoa sehemu yao katika kuhakikisha watoto hao wanafanyiwa oparesheni.
  Makonda amesema kambi hizo wazazi watapeleka watoto tu ambayo ndio gharama yab kufanya watoto wao wafanyiwe oparesheni ya matatizo yao.
  Amesema kuwa watu walikuwa wanafikiria ndani ya bajeti tu bila kuangalia wadau wana uwezo gani na kusababisha mambo kurudi nyuma kwa GMS wameonyesha  njia katika kufanya ufadhili wa operesheni hiyo.
  ‘’Naamini watoto hao watakuwa kuwa watumishi wenye maadili kutokana na matatizo waliopata na watu wengine wakahangaikia hivyo hawawezi kuwa mafisadi kwa kujua atachochukua kuna watu wanahitaji’’amesema Makonda.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk.Othman Kiloloma amesema kuwa daktari wenye utaalamu huo ni daktari tisa tu kati ya hao nane  ni Hospitali ya Taifa Muhimbili na mmoja Hospitali ya Bungando.

  Dk.Kiloloma amesema kufanya operesheni ya mtoto mmoja ni sh. Laki saba hadi milioni moja ambapo baadhi wanashindwa kumudu hivyo ufadhili wa GSM utafanya kuweka kambi na kutoa huduma hiyo bure kwa watoto pamoja na kutoa elimu kwa baadhi ya daktari juu ya operesheni ya watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa.

  Afisa  Mawasiliano wa GSM , AKhalfan Kiwamba amesema kuwa wanatambua matatizo ya watoto hao na kuamua kufanya ufadhili ili waweze kufanyiwa oparesheni  hiyo.
  Amesema kambi hizo awamu ya kwanza itakuwa Mkoa wa Mwanza Aprili 27 hadi 30, Shinyanga  Mei 2 hadi 4,  Singida Mei 6 hadi 8, Dodoma  10  hadi 13, Morogoro Mei 15  hadi 17 .
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa kambi ya upasuaji ya watoto wa wenye vichwa vikubwa na watoto wenye matatizo ya mgongo wazi ambapo Mfuko wa GMS kushirikiana na Taasisi ya Mifupa (MOI) katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili wataanza kambi hiyo katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma na Mkurugenzi wa tiba MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Samwel Swai.
   Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kambi ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na watoto wenye Migongo wazi. Kulia ni kuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.
  Afisa Uhusiano wa Mfuko wa GSM, Khalfan Kiwamba akizumgumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na GSM kutoa mchango wake kwa kusaidia watoto wenye matatizo ya Mgongo wazi na watoto wenye vichwa vikubwa. Kusoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mfuko wa GSM leo katika hospitali ya Muhimbili kwenye kitengo cha MOI jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  0 0

  TAARIFA KWA UMMA

  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na matamshi yaliyotolewa na Leonard Swai, Wakili wa TAKUKURU aliyenukuliwa kwenye vyombo vya Habari tarehe 15/4/2016 kuhusiana na hali ya Rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Wakili huyo alinukuliwa akisema kuwa Kuna Rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu” baada ya kutolewa hukumu ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Bw. William Mhando ambaye alionekana hana hatia.
  Wakili Leonard Swai si msemaji Rasmi wa Taasisi hivyo matamshi aliyoyatoa si msimamo wa TAKUKURU kuhusu Mahakama. Tunaiomba Idara ya Mahakama na jamii kwa ujumla itambue kuwa matamshi hayo aliyoyatoa ni maoni yake binafsi.

  TAKUKURU ina jukumu la kisheria la Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Mahakama ni muhimili wa Serikali unaotoa haki. Tunaamini kila Taasisi itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo ya Sheria zilizopo.

  TAKUKURU inaheshimu uhuru na mamlaka ya Mahakama na itaendelea kufanya hivyo katika utekelezaji wa majukumu yake.


  IMETOLEWA NA

  OFISI YA AFISA UHUSIANO, 
  TAKUKURU MAKAO MAKUU

  20 April, 2016


  0 0

   Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Sunday Manara akizungumza na vyombo vya habari juu ya uamuzi wa klabu yake hiyo, kumfungia kwa mechi tano beki wao wa kulia, Hassan Ramadhan Kessy kwa rafu mbaya aliyomchezea mshambuliaji wa Toto Africans, Edward Christopher, katika mchezo ambao Simba ililala bao 1-0 kwenye  uwanja wa Taifa, baada ya mchezaji huyo kutolewa nje kwa kadi nyekundu na kudaiwa kuigharimu klabu hiyo kwa kukosa pointi tatu muhimu

  Uongozi wa klabu ya Simba umemsimamisha beki wao wa kulia, Hassan Ramadhan Kessy kwa rafu mbaya aliyomchezea mshambuliaji wa Toto Africans, Edward Christopher.

  Katika mchezo huo ambao Simba ililala bao 1-0 kwenye  uwanja wa Taifa,  Kessy alitolewa nje na kudaiwa kuigharimu klabu hiyo kwa kukosa pointi tatu muhimu.
  Pamoja na uongozi wa Simba kumchukulia hatua Kessy na kukosa mechi zote zilizobakia katika msimu huu, klabu hiyo pia imeshindwa kumchukulia hatua za kinidhamu kipa kutoka Ivory Coast, Vicent Agban ambaye aliamua kumzaba makofi mchezaji huyo aliyejiunga na Simba akitokea klabu ya Mtibwa Sugar.
  Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara alisema kuwa hawana ushahidi wa tukio hilo amalo linadaiwa kutokea katika vyumba vya kubadilishia nguo mara baada ya mchezo huo kumalizika.
  Pamoja na kushuhudiwa na baadhi ya wachezaji na Kessy kutoa taarifa polisi kwa ajili ya kupata matibabu, Manara, mratibu wa klabu hiyo, Abbas na kocha Jackson Mayanja walikanusha taarifa hizo.
  Manara alisema kuwa Kessy alifanya rafu ya ‘kuua’ na klabu yenye heshima kubwa kama Simba imeamua kuchukua hatua kali ili kuwapa fundisho wachezaji wa aina ya Kessy ambao wanataka kufanya hivyo.

  “TFF itamfungia mechi tatu kwani alipata kadi nyekundu ya moja kwa moja (straight red card),  tumeona adhabu hiyo ya kikanuni haitoshi kwetu, tumeamua kumfungia mechi nyingine na kama msimu utaruhusu, atarejea kucheza,” alisema Manara kwa kejeli huku akijua kuwa Simba imebakiza mechi tano tu kumaliza ligi.
  Manara alisema kuwa Simba inahitaji wachezaji wenye nidhamu na weledi na siyo kuwa na wachezaji wa aina ya Kessy ambaye katika mchezo huo alionekana akilaumiwa hata na wachezaji wenzake.

  Kocha wa klabu hiyo, Jackson Mayanja aliunga mkono adhabu hiyo na kusema ilikuwa mbaya sana. Mayanja ambaye aliwaomba radhi  mashabiki wa Simba kwa matokeo mabaya, alisema kuwa rafu ya Kessy haikuwa na sababu kwani alikuwa na mpira peke yake na kumsubiri Christoher na kupiga mpira huku akimpandishia mguu kichwani.
  “Kwa kweli nimeshangazwa sana, sikuwepo uwanjani kwani nami nilikuwa nimeonewa na mwamyuzi, niliangalia kupitia televisheni na kusikitika,” alisema Mayanja.
  Mganda huyo ameshauri kikosi kisibomolewe hata kama Simba itakosa taji msimu huu, ili kiboreshwe na msimu ujao kirejee na nguvu mpya.

  Kuhusu kiungo Abdi Banda, kocha huyo amesema mchezaji huyo hajafukuzwa bali amejiondoa mwenyewe kwenye timu baada ya kususa.

  0 0

   Watuhumiwa wa Tukio la Ujambazi, wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi mara baada ya kukamatwa mchana huu katika eneo la Kariakoo, Jijini Dar es salaam.

  Sehemu ya Umati wa watu wakishuhudia tukio la kukamatwa kwa Watuhumiwa hao wa tukio la Ujambazi.
  Taarifa kamili itakujia baadae kidogo.

  0 0

  Simu.tv: Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC chazindua matokeo ya utafiti wa ripoti ya haki za binadamu Tanzania kwa mwaka 2015.https://youtu.be/ilFiU7xeTic

  Simu.tv: Waziri wa habari, utamaduni, utalii na michezo alitaka shirika la utangazaji Zanzibar ZBC kusitisha matangazo ya mfumo wa analojia na kubaki katika mfumo wa digitali pekee. https://youtu.be/bt8q6Wh-Xi8

  Simu.tv: Jamii visiwani Zanzibar yaaswa kuchukua tahadhari ya kutoishi maeneo hatarishi ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza. https://youtu.be/zG7DE8v29ak  

  Simu.tv: Baada ya Azam kushindwa kusonga mbele, kocha wa timu hiyo na nahodha wake wamesema walijitahidi lakini mchezo haukua bahati yaohttps://youtu.be/2f63QySNOHo  

  Simu.tv: Serikali imeyataka makampuni yanayozalisha bidhaa hapa nchini kusajili nembo za bidhaa zao ili kuweza kupata takwimu sahihi ya bidhaa za Tanzania.https://youtu.be/Cm-hhAHYKdE    

  Simu.tv: Gari dogo aina ya noah limetumbukia bahari ya hindi leo alfajiri na kusababisha vifo vya watu wawili. https://youtu.be/39Bxg1HzEf4  

  Simu.tv: Taasisi ya GSM imejitolea kusaidia upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgogo wazi kwa kuwafuata kule walipo. https://youtu.be/m5aoA6vmAuI  

  Simu.tv: Taasisi ya Habibu imejitolea vifaa vya ofisi makao makuu ya polisi wilaya ya Mwanga pamoja na msaada wa mabenchi katika kituo cha afya.https://youtu.be/V0MCx4cUSE8  

  Simu.tv: Halmashauri ya manispaa ya Ilala Imewasimisha kazi wahandisi waliokua wakisimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo baada ya kujengwa chini ya kiwango. https://youtu.be/Ynm4eKErpfY  

  Simu.tv: Shirika la hifadhi za taifa TANAPA limejipanga kuanzisha kampeni ya ufanyaji usafi katika mlima Kilimanjaro. https://youtu.be/7WcQpog7RX0
     
  Simu.tv: Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi limeipongeza kampuni ya START OIL Kwa juhudi zake za kuwezesha vijana kutoka mikoa ya Lind na Mtwara.https://youtu.be/HhhbpSQZn_k  

  Simu.tv: Wafanyakazi wa kujitolea 43 kutoka Marekani wameapishwa ili kwenda kufundisha shule za sekondari vijijini. https://youtu.be/S74vHMgNHOY

  Simu.tv: Watu wawili wafariki dunia jijini Dar es salaam leo baada ya gari walilokua wakisafiria kuserereka kutoka katika Panton na kuingia Baharini;https://youtu.be/6LgIwjyE7g8

  Simu.tv: Rais Magufuli amteua Mhandisi Paskasi Muragili kuwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya ustawishaji makao makuu Dodoma; https://youtu.be/YN2xXImmhLc

  Simu.tv: Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala wataka vyombo vya usalama na TAKUKURU kuhakikisha ndani ya siku 28 kukamilisha uchunguzi wa ufisadi soko la Mwanjelwa; https://youtu.be/hTh4_gGylJ0

  Simu.tv: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aongoza mamilia ya wananchi mkoani Dodoma katika mazishi ya Askofu; https://youtu.be/t5SFVleGHLE

  Simu.tv: Wabunge wa Bunge la Afrika watembelea soko la samaki la Ferry na kuwahamasisha wafanyabiashara kutumia fursa zilizopo afrika mashariki;https://youtu.be/FDZaGhOELLc

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Askofu Mkuu wa Jimbo la Dodoma , Beatus Kinyaiya katika mazishi ya Askofu Mstaafu wa Dodoma Mathias Isuja yaliyofanyika kwenye kanisa kuu la Mtakatifu Paul wa Msalaba Mjini Dodoma Aprili 20, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Askofu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mathias Isuja katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa   Kuu la Mtakatifu Paul wa Msalaba Aprili 20, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mathias Isuja  katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa  Kuu la Mtakatifu Paul wa Msalaba,  Aprili  20, 2016.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya waumini na wakazi wa mkoa wa Dodoma katika mazishi ya Mhashamu Askofu Mstaafu, Mathias Isuja wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.

  Amesema kifo hicho ni pigo kwa watu wote na si kwa kanisa pekee kwa sababu walimtegemea kulisaidia Taifa kiroho na kimaendeleo.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 20, 2016) wakati akizungumza na waumini na wakazi wa mkoa huo na mikoa jirani kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiaskofu la Mtume Paulo wa Msalaba mjini Dodoma.

  Askofu Isuja ambaye alizaliwa Agosti 14, 1929 alikuwa Askofu wa kwanza mzalendo katika Jimbo la Kanisa Katoliki la Dodoma. Alistaafu kazi ya uaskofu mwaka 2004 kwa mujibu wa sheria ya kanisa. Alifariki Aprili 13, mwaka huu.

  Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kumuenzi Askofu Isuja kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati wa uhai wake na kuyaendeleza yote aliyoyaanzisha kwenye maeneo aliyowahi kuyatumikia.

  “Tumepoteza mtu makini, sisi ni mashahidi wa mchango mkubwa wa marehemu siyo tu katika kutoa huduma za kiroho, bali pia huduma za kijamii zilizolenga kuleta maendeleo kwa wananchi katika jimbo hili la Dodoma na katika taifa kwa ujumla,” amesema.

  Mapema, akitoa mahubiri wakati wa ibada hiyo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Judathadeus Ruwa’ichi alisema waumini wa kanisa hilo wa mkoa wa Dodoma na Tanzania nzima wanapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha marefu aliyomjalia Askofu Isuja.

  “Tunapaswa kumshukuru kwa maisha marefu ambayo Mungu alimzawadia baba yetu Isuja. Katika Zaburi ya 90 tunasoma kuwa mwanadamu ana miaka ya matazamio ambayo ni 70, lakini yeye alipewa miaka ya matazamio 70 na akazawadiwa nyongeza ya miaka 10 na kisha miaka mingine sita na nusu,” alisema.

  Alisema zawadi nyigine ambayo Mungu aliwapatia waumini hao ni ya imani ambayo Baba Askofu Isuja aliipokea, aliifundisha na aliishi na akawataka waendelee kumshukuru Mungu kwa hilo. “Miaka 56 ya utumishi wake kama padre na askofu ni zawadi kwa Dodoma na Tanzania na siyo kwake yeye binafsi,” alisema.

  Ibada hiyo ya mazishi ilihudhuriwa na Maaskofu Wakuu na Maaskofu wa kawaida 28 kutoka majimbo ya Dodoma, Mwanza, Mbeya, Njombe, Mpanda, Iringa, Songea, Tabora, Morogoro na Mahenge. Mengine ni Musoma, Rulenge, Mbinga, Moshi, Same, Kahama, Sumbawanga, Shinyanga, Mtwara na Lindi. Majimbo mengine ni Bukoba, Tanga, Singida, Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha, Kondoa na Kayanga.
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980.
  DODOMA.

  JUMATANO, APRILI 20, 2016.

  0 0

  Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Kikosi cha Maji, wakiwa katika boti, wakati wa zoezi la kutafuta miili ya watu waliozama baharini asubuhi ya leo, baada ya gari aina ya Toyota Hiace kuteleza kutoka kwenye Pantoni kabla ya kutumbikia na kuzama baharini. Imedaiwa kuwa gari hiyo ilikuwa na watu wawili, dereva mwanaume na abiria mwanamke. Waokoaji walifanikiwa kuopoa mwili wa dereva kwanza na baadaye wakaupata mwili wa mwingine mnamo majira ya saa tatu asubuhi ya leo. Mwanamke huyo inasemakana alikuwa anarejea nyumbani akitoka katika msiba wa ndugu yake uliotokea siku 9 zilizopita.
  Mwili wa Mmoja wa watu hao ukitolewa mara baada ya kupatikana majini, juhudi za kuutafuta mwili zilifanikiwa masaa mawili badae.
   Zoezi la Upoaji likiendelea.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela alimuwakilisha Mkuu wa mkoa katika mazishi mke wa Mkuu wa mkoa mstaafu Mh Erasto Mbwillo; Afisa Elimu Mbeya Vijijini Mama Margareth Mgimwa Mbwilo. Msiba huo uliondeshwa na Makamu Mkuu wa Chuo Padri Dr Mgimwa pia uliudhuriwa na Jaji Mkuu Chande Othman; Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bwana Katanga; Mkuu wa Mkoa Simiyu Bwana Anthony Mtaka, Wakuu wa wilaya Makete- Mh Daud Yassin, Rungwe Mh Zainab Mbiro na Songea Mh Mpesya pamoja na viongozi wengine wengi wakiwemo wastaafu wakiongozwa na Mkuu wa mkoa mstaafu Mh Abbas Kandoro
    Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimfariji Mkuu wa mkoa mstaafu Mh Erasto Mbwillo
   Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman akimpa pole  Mkuu wa mkoa mstaafu Mh Erasto Mbwillo
   Waombolezaji msibani 
  Makamu Mkuu wa Chuo Padri Dr Mgimwa akiendesha misa

  0 0

  UNIVERSAL AUCTION CENTRE Kwa idhini waliyopewa na Ubalozi wa Marekani watauza kwa mnada wa hadhara fanicha za ofisi na nyumbani  tarehe 23  April, 2016 Jumamosi saa 4:00 asubuhi. Mnada utafanyika Golden Resort Sinza,  Lion Street. (nyuma ya Lion Hotel Sinza, Dar es salaam) 
  MALI ZITAKAZOUZWA:Sofa sets, Sofa bed, Chest drawer, China base, Hatch, Dressers, Coffee table, Book case, Dining table/chairs, Meza za ofisi, Bamboo chairs, Carpet,  Vitanda, Magodoro, Fridge, Freezer, Majiko,  Washer, Dryer, Air condition split unit na vingine vingi. 
  Mali zote zinaweza kukaguliwa Golden Resort Sinza,Lion Street tarehe 20 mpaka 22 April,  2016 kuanzia saa 4.00 asubuhi mpaka saa 11.00 jioni.  MASHARTI YA MNADA:

  1. Mnunuzi   atatakiwa kulipa malipo yote pale pale kwa keshia (cashier).

   Mali zote zitauzwa kama zilivyo bila dhamana.

  1. Mnunuzi atawajibika kulipa ushuru na kodi zingine zote.

   Mali zote zilizouzwa zitatakiwa kuondolewa baada ya kulipa malipo yote pamoja na kodi. 
  Kwa maelezo zaidi waone:

  UNIVERSAL AUCTION CENTRE

  PLOT NO. 5 “E” LION STREET SINZA

  CELL NO:  0754 284 926, 0757 284 926                        
  E-mail: universalauction@hotmail.com

  DAR ES SALAAM.

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Habari  Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan Omar kushoto akikabithiwa nyaraka  na Katibu Mkuu Mstaafu Ali Mwinyikai katika makabidhiano ya Ofisi yaliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo  Kikwajuni Mjini Unguja.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari  Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan Omar kushoto na Katibu Mkuu Mstaafu Ali Mwinyikai wakitiliana saini katika makabidhiano ya Ofisi yaliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari  Utalii Utamaduni na Michezo  Kikwajuni Mjini Unguja.
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Amina Ameri Issa kulia akikabidhiwa nyaraka na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu Issa Mlingoti katika makabidhiano ya Ofisi yaliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari  Utalii Utamaduni  na Michezo  Kikwajuni Mjini Unguja
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari  Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan Omar akitoa nasaha zake kwa Wakurugenzi na Watendaji mbali mbali waliohudhuria katika makabidhiano ya Ofisi yaliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari  Utalii Utamaduni  na Michezo  Kikwajuni Mjini Unguja
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan Omar mwenye koti na tai akiwa katika Picha ya pamoja na Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo Amina Ameri Issa pamoja na Wakurugenzi na Watendaji wa Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Kikwajuni Mjini Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  BENKI ya Exim Tanzania imeshiriki kikamilifu kwenye mbio za tisa za Ngorongoro ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa kupitia mbio hizo katika kukabiliana na ugonjwa wa malaria hapa nchini.

  Mbio hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita wilayani Karatu chini ya ushiriki wa Waziri wa Maliasiri na Utalii Prof. Jumanne Maghembe, aliyekuwa mgeni rasmi zinalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa malaria sambamba na kusaidia elimu ya awali kwa jamii wa Wamasai waishio jirani na kivutio hicho.

  Mbali na kushiriki katika udhamini wa mbio hizo baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo walijumuika na washiriki wengine katika mbio za kilometa 5 zilizohusisha kundi la washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali (corporate challenge category). Watoto pia walipewa fursa ya kukimbia mbio fupi za kilometa 2.5, wakati shindano refu lilikua la kilometa 21 tokea Ngorongoro hadi Karatu.

  “Ni wazi kwamba taasisi za kifedha tukiwemo Benki ya Exim ustawi wetu unategemea sana uwepo wa jamii yenye afya na ndio maana tumekuwa mstari wa mbele kushiriki mbio hizi kwa maana ya kuhamasisha michezo lakini pia kuunga mkono malengo yake yaani kuikabili malaria na kusaidia elimu,’’ alisema mwakilishi wa benki hiyo Bw. Emmanuel Mwamkinga, meneja wa benki ya Exim tawi la Karatu.

  Aliongeza kuwa benki hiyo itaendelea kushiriki katika kusaidia michezo na matukio mbalimbali hasa yale yenye kuleta tija kwa jamii hususani kwenye sekta ya afya, elimu na mazingira.

  Katika mbio hizo zilizoanzia katika lango la kuingilia na kutokea Hifadhi ya Ngorongoro na kuishia kwenye uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu ilishuhudiwa mwanaridha Ismail Juma akivunja rekodi ya mbio hizo kwa kutumia saa 1:02:48 na kuipiga kikumbo ile ya awali ya saa 1:03:00 iliyowekwa miaka ya nyuma.
   Waziri wa Maliasili na Utalii prof Jumanne Maghembe akimpongeza meneja wa benki ya Exim tawi la Karatu Emanuel Aaron kwa kupata tuzo ya ushiriki wa mashindano ya Ngorongoro marathon yaliyofanyika wilayani Karatu mkoani Arusha.
   Meneja wa Benki ya Exim tawi la Karatu Emanuel Aaron akipokea tuzo kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya ZARA Zainab Ansell,kwa  ajili ya ushiriki wa mashindano ya Ngorongoro marathon  yaliyo fanyika wilayani Karatu mkoani Arusha.

    Waziri wa maliasili na utalii prof Jumanne Maghembe katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya Exim mara baada ya kutembelea banda siku ya mashindano ya Ngorongoro marathon yaliyofanyika wilayani Karatu mkoani Arusha..
  Afisa masoko wa Exim benki wa kwanza (kushoto),meneja mauzo Zaitun Mussa (katikati) na Meneja wa tawi la Karatu Emanuel Aaron wakiwa na tuzo yao waliyo ipokea siku ya Ngorongoro Marathon yaliyofanyika wilayani Karatu,Arusha
   
   

  0 0
 • 04/21/16--02:45: YALIYOJIRI BUNGEN

 • 0 0

  Mwathirika ambaye pia ni mwenye matatizo ya goti tangu vita vya Kagera, Matern Ndimbo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  WAATHIRIKA wa vita vya Kagera vilivyoanza mwaka1978 hadi 1979 kati ya Tanzania na Uganda wameiomba serikali kuwakumbuka kwani walipata ulemavu walipokuwa vitani. 

  Hayo yamesemwa na mwathirika wa vita vya Kagera, Matern Ndimbo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa walioathirika katika vita vya Kagera ambao bado wapo hai mpaka sasa wanaomba kukumbukwa na serikali ya awamu ya Tano.

  Ndimbo ameiomba serikali kuwaangalia kwa jicho la pekee kwani ndio waliopigana vita vya Kagera ambavyo vilikuwa kati ya Tanzania na Uganda na kupata ulemavu.

  Amesema kuwa kupata ulemabu isiwe sababu ya kuishi maisha ya kuhangaika kwani kipindi cha vita walikuwa msaada mkubwa kwa nchi.

  Pia ameiomba serikali kwa siku ile ya Julai 25 ya kila mwaka ambapo huadhimishwa siku ya mashujaa ameomba serikali iwakumbuke kwa kuwajengea nyumba za kuisha na familia zao kwani kwa uongozi wa awamu ya tano unaweza kuwa msaada kwao.

  "Mashujaa hai ndio wa kumbukwa sana kwani bado  tunaweza kusimulia ilikuwaje, ikiwa na mashujaa waliofariki  ni mhimu kuwakumbuka nao kwakuwa walipigania nchi yetu". Amesema Ndimbo.

  0 0
 • 04/21/16--04:16: BEI YA MADAFU LEO.


 • 0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba (kushoto), Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo, Amani Mashaka (katikati), anayefuata ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Jenita Ndone wakiwaongoza wajumbe wa Baraza hilo kuimba wimbo wa mshikamano daima kabla ya Naibu Katibu Mkuu kufungua kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kabla ya kufungua mkutano wa siku moja wa baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Jeshi la Magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Balozi Simba aliwataka watumishi wa wizara yake wafanye kazi kwa bidii ili kuiletea maendeleo wizara hiyo.
   Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Jeshi la Polisi, Arcado Nchinga akichangia mada katika kikao cha Baraza hilo kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe hao katika Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. 
  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

   Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akisalimiana na wawakilishi wa mashirika ya WHO na UNICEF alipowasili katika kambi ya maafa kuona mazingira ya Kambi hiyo iliyopo Skuli ya Sekondari ya Mwanakwerekwe C nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
   Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhi katika kambi ya maafa Mwanakwerekwe C.
  Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  Na Ramadhan Ali-Maelezo Zanzibar.
  MAAFISA wanaoshughulikia wananchi waliohifadhiwa katika kambi ya maafa Mwanakwerekwe C wameshauriwa kutoa elimu ya Afya kwa wananchi hao ili kuwaepusha na maradhi ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

  Naibu Waziri wa Afya Bi. Harusi Said Suleiman ametoa ushauri huo alipoitembelea kambi ya maafa kuona mazingira  na matatizo yanayowakabili katika kambi hiyo akiambatana na wawakilishi wa Mashirika ya WHO na UNICEF waliopo Zanzibar.

  Amesema  kambi inakusanya watu wengi wenye desturi na taratibu za maisha tofauti hivyo suala la kutoa elimu ya Afya itakayosaidia maambukizi ya maradhi ni kitu muhimu .
  Amewata wananchi hao  kufuata taratibu na maelekezo ya maafisa wa kambi hiyo ikiwemo  kunywa maji yaliyotiwa dawa na kukosha mikono baada ya kutoka chooni na kabla ya kula ili wawe walimu wazuri watakaporejea kwenye makaazi yao.

  Afisa Msaidizi wa Kambi ya maafa Makame Khatib Makame amemueleza Naibu Waziri wa Afya kwamba hivi sasa kambi inawatu 420 wakiwemo wanawake 240.

  Amesema huduma zote muhimu zinatolewa ndani ya kambi hiyo na wameanzisha utaratibu wa kuwapeleka  na kuwarejesha watoto wanaosomo katika skuli zao.

  Wananchi wanaohifadhiwa katika kambi ya maafa wameiomba Serikali kuweka utaratibu wa kuwasaidia watakaporejea katika makaazi yao kwa vile wamepoteza vifaa vingi vya matumizi baada ya nyumba zao kujaa maji. 

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Dodoma

  TIMU ya netiboli ya Uchukuzi SC jana ilianza vyema mchezo wake wa kwanza kwa kuwaicharaza CDA ya Dodoma katika mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea mkoani Dodoma.

  Uchukuzi SC inayoundwa na wachezaji wakongwe, akiwemo mfungaji mahiri wa timu ya Bandari na Taifa, Matalena Mhagama waliwapeleka puta wapinzani wao ambapo hadi mapumziko walikuwa mbele kwa magoli 11-6.

  Katika mchezo huo uliokuwa umetawaliwa na rafu za hapa na pale na kulalamikiwa mara kwa mara na wachezaji wa Uchukuzi SC, ulimalizika kwa mfungaji Matalena kufunga magoli 16 na Tatu Kitula akifunga saba, wakati wapinzani wao Tatu Fungo nma Margeth Nicholaus kila mmoja akifunga magoli nane.

  Kocha Mkuu wa Uchukuzi SC, Judith Ilunda alisema wamepata ushindi huo wa kwanza kutokana na kufanya mazoezi ya pamoja ya muda mrefu, pamoja na kwamba wapinzani wao walikuwa ni wazuri na wenye uzoefu mkubwa.

  “Wengi waliocheza na kikosi change ni wakongwe wapo niliocheza nao mimi kwenye mashindano mbalimbali, hivyo wameweza kutumia ukongwe wao lakini tuliwazidi mbinu kutokana na timu yetu kuundwa na chipukizi wengi,” alisema Ilunda.

  Lakini, alilalamikia maamuzi ya waamuzi waliocheza mchezo huo kuwa mengi yamepitwa na wakati kutokana na sheria kubadilika mara kwa mara. “Hawa waamuzi wamekuwa wakichezeshakwa sheria nyingi za zamani na kusababisha mvutano, hivyo wanatakiwa wabadilike kwa kujisomea mara kwa mara ili kuondoa mkanganyiko kwa timu zinazocheza,” alisema Ilunda.

  Hatahivyo, waamuzi Mariam Makisi na Caroline Paulo wote wa Dodoma, kwa nyakati tofauti walisema wamechezesha mchezo huo kwa kanuni na sheria za mchezo huo, lakini wameshangazwa na malalamiko ya kuwa wamechezesha kwa sheria za zamani.

  “Unajua timu za Dar es Salaam siku zote zinajifanya kujua sheria zaidi, na wangeweka wazi ni wapi waamuzi tulipopindisha sheria,” alisema Makisi. Wakatihuohuo, timu ya Tamisemi iliwafunga TPDC kwa magoli 6-1 katika mchezo wa soka uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri.

  Wafungaji wa Tamisemi ni Mwigane Yeya kafunga magoli mawili, wakati waliofunga moja-moja ni Hamis Shedafa, Hamad Majura, Nelson Richard na Phillipo Oden; wakati bao la kufutia machozi la TPDC lilifungwa na Shija Dalushi.

  Katika mchezo mwingine wa soka, timu ya Tanesco ilipata ushindi wa chee baada ya wapinzani wa CWT ya Dodoma kushindw kutokea uwanjani.
  Mfungaji wa CDA Dodoma, Tatu Fungo akiuwahi mpira katika mchezo wao wa netiboli wa Kombe la Mei dhidi ya Uchukuzi SC. Uchukuzi walishinda kwa magoli 23-16.
  Mchezaji Mwadawa Hamisi wa Uchukuzi SC (GK) akiangalia mwenzake wa kumrushia baada ya Tatu Fungo wa CDA kufunga bao katika michuano ya Mei Mosi. Uchukuzi walishinda magoli 23-16.
  Mchezaji Matalena Mhagama wa Uchukuzi SC (GS) akijiandaa kupokea mpira kutoka kwa Tatu Kitula aliyezuiwa na Catherine Ukunguala, katika mchezo wa netiboli wa mashindano ya Mei Mosi.

  0 0


  Kaimu Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja akitoa ufafanuzi kwa wahariri wa vyombo vya Habari kuhusu matokeo ya Utafiti wa Watu wenye uwezo wa kufanya Kazi leo jijini Dar es salaam. Matokeo hayo yataiwezesha Serikali kuangalia upya tija ya utendaji kazi katika shughuli zinazofanywa na makundi mbalimbali ili kubaini mchango wake katika kukuza Pato la Taifa.

  Kaimu Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja akitoa ufafanuzi kwa wahariri wa vyombo vya Habari kuhusu matokeo ya Utafiti wa Watu wenye uwezo wa kufanya Kazi. Kushoto kwake ni Hashim Njowele na Saruni Njipay, Watakwimu wa Idara ya Ajira na Bei wa Ofisi hiyo.
  Baadhi ya Wahariri na Waandishi wa Habari waliohudhuria ufafanuzi kwa wahariri wa vyombo vya Habari kuhusu matokeo ya Utafiti wa Watu wenye uwezo wa kufanya 2014 Kazi leo jijini Dar es salaam.

  Na. Aron Msigwa-Dar es salaam. 
  OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema kuwa takwimu za matokeo ya utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa Mwaka 2014 zitatumika kufanya maboresho ya Mipango na Sera mbalimbali za kukuza ajira na kupunguza umasikini nchini.

  Matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa asilimia 70.9 ya muda wa watu wenye umri wa miaka 15 au zaidi kwa siku hutumika kwenye shughuli zisizo za uzalishaji ikilinganishwa na asilimia 18.5 inayotumika kwenye shughuli za kiuchumi. 

  Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam Kaimu Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi hiyo Bi. Ruth Minja amesema kuwa matokeo hayo yataiwezesha Serikali kuangalia upya tija ya utendaji kazi katika shughuli zinazofanywa na makundi mbalimbali ili kubaini mchango wake katika kukuza Pato la Taifa.

  Amesema kwa mujibu wa utafiti huo Tanzania ina nguvu kazi ya Taifa ya watu milioni 22.3 wanaume wakiwa milioni 11 na wanawake wakiwa milioni 11.2 huku idadi ya watanzania walio nje ya nguvu kazi ya Taifa wakifikia milioni 3.4.

  Amefafanua kuwa idadi ya watanzania walio kwenye ajira ni milioni 20 ikilinganishwa na watu milioni 2.2 ambao hawako kwenye ajira huku akibainisha kwamba kiwango cha nguvu kazi iliyo katika uzalishaji wa bidhaa na huduma za kiuchumi na nguvu kazi iliyo tayari kujihusisha na uzalishaji mali kimepungua kutoka asilimia 89.6 mwaka 2006 hadi asilimia 86.7 ya mwaka 2014.

  Kwa mujibu wa utafiti amesema kiwango cha watu wenye umri wa kufanya kazi walio na ajira kwa upande wa wanaume kwa mwaka 2006 kilifikia asilimia 80.8 ikilinganishwa na asilimia 82.1 za mwaka 2014 huku kiwango hicho hicho kwa upande wa wanawake kwa mwaka 2014 kikifikia 73.8 kutoka 77.6 za mwaka 2006.

  “ Kiwango cha watu wenye umri wa kufanya kazi walio na ajira kwa ujumla kimepungua, hii inaonesha kuwa, kiwango cha uchumi kuzalisha ajira kimepungua kidogo kutoka asilimia 79.2 mwaka 2006 hadi asilimia 77.8 mwaka 2014” Amesema.

  Kuhusu masaa ya kufanya kwa watu wenye umri wa miaka 15 na kuendelea Bi. Ruth Minja amesema kuwa kati ya mwaka 2006 hadi 2014 kumekuwa na ongezeko la masaa ambayo watu hufanya kazi kwa makundi yote ya ajira akifafanua kuwa watu wanaofanya kazi kwa malipo na waliojiajiri wamekuwa wakifanya kazi zaidi ya saa 50 kwa wiki kuliko hali nyingine za ajira.

  “ Napenda kuwaeleza kuwa takwimu hizi zitasaidia kuboresha sera ya ajira na programu nyingine ili kuwe na uwiano kati ya saa za watu wanaofanya kazi, uzalishaji na malipo wanayopewa” Amesisitiza.

  Aidha, amefafanua kuwa kwa upande wa ukosefu wa ajira kwa muda mrefu kwa watu wenye umri wa miaka 15 au zaidi kote nchini wananwake wana kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kuliko wanaume kwa miaka yote ya utafiti uliofanywa na Ofisi hiyo toka mwaka 2006 hadi 2014.

  Amesisitiza kuwa ipo haja kwa Serikali na wadau mbalimbali kushughulikia kiwango cha watu wasio na kazi na wale ambao hawako tayari kufanya kazi yoyote ya kiuchumi kutokana na ongezeko lake kuwa kubwa kutokana na athari yake kwa uchumi wa taifa. 

  “ Kiashiria hiki katika utafiti tulioufanya kinabainisha kuwa kiwango cha watu ambao hawakuwa na kazi wala hawakuwa tayari kufanya kazi yoyote ya kiuchumi kimeongezeka kutoka ailimia 10.4 za mwaka 2006 hadi 17.2 za mwaka 2014 “ Amesisitiza.

  Ameeleza kuwa kufuatia kiashiria hicho wanawake wana kiwango kikubwa zaidi kuliko wanaume kwa kuwa wao hujishughulisha na shughuli za nyumbani ambazo sio za kiuchumi zikiwemo za kufua nguo, kupika na malezi ya watoto.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Moovn Tanzania,Godwin Ndugulile akionesha simu jijini Dar es Salaam jinsi Aplikesheni ya Moovn Driver inavyofanya kazi kati ya simu ya Dereva na Abiria. Kulia ni Meneja wa kampuni hiyo,Ibrahim Ligonja.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Moovn Tanzania,Godwin Ndugulile akiangalia Aplikesheni ya Moovn Driver akiangalia simu mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Kulia ni Meneja wa kampuni hiyo,Ibrahim Ligonja na Kushoto niDereva ambaye wanajaribia simu yake kuangalizia Aplikesheni ya Moorn Driver, Masood Mohamed.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  TANZANIA inatarajia kunufaika na teknolojia ya kisasa ya usafirishaji ya  moovn Driver, kwa watu wanaohitaji kupiga simu ya mkononi kuhitaji usafiri.

  Akizungumza  leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo,Godwin Ndugulile amesema  huduma hiyo itawasaidia madereva wa taksi, pikipiki na bajaji nchi kufanya biashara kwa wakati na kukuza kipato chao na nchi kwa kulipa kodi.

  Amesema mtu atahitaji usafiri wa taxi au bodaboda, bajaji kwa nyakati tofauti ataweza kupata huduma hiyo kupitia teknolojia tuliyoibuni na kupelekwa popote katika hali ya usalama.

  Ndugulile amesema kuwa  dereva huyo kwa mfumo huo ataonekana kila sehemu atakapokwenda kupitia tekinolojia hii.

  Amesema watumiaji satelaiti ambapo abiria atakapo kuwa akiiitumia kumtafuta dereva itamuonesha dereva aliyekuwa karibu yake na kuongeza kuwa endapo dereva huyo naye atakuwa akiitumia atapata taarifa kuwa katika eneo Fulani kuna abiria.

  Alisema aplikesheni hiyo inapatikana bure kwa wateja wote ili kuweza kutoa huduma  nafuu kwa vyombo vya usafirishaji mbalimbali kama taxi bodaboda, na bajaji.

  Amesema madereva wataongeza kipato, watarahiaisha biashara, usalama dhidi ya mteja aliyempakia, mawasiliano, ripoti ya mapato na maripo ya kirahisi ya kulipwa kwa njia ya mtandao kupitia teknolojia hiyo.

  Meneja wa kampuni hiyo,Ibrahim Ligonja, amesemaa kabla ya kuanza utaratibu huo waliishirikisha serikali na kuiingizia manufaa ya kupunguza uhalifu, uwezo wa kukusanya kodi sahihi ya mapato ya madereva na kuongeza kipato, kuhakikisha madereva wanafuata sheria na vibali na kurahisisha ajira.

  0 0


  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO.
  JUMLA ya wahalifu 71 wamekamatwa ndani ya siku 7 katika maeneo mbalimbali katika Kata ya Gongo la mboto,Wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam wakiwa na kete za bangi pamoja na madumu ya pombe aina ya  gongo.

  Idadi hiyo imetajwa leo Jijini Dar es salaam na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi, Bw. Lucas Mkongya alipokua akifafanua juu ya malalamiko ya wananchi wa Gongo la Mboto kuhusu uhalifu uliokithiri katika  maeneo hayo pamoja na jitihada wanazozichukua katika kuzuia uhalifu huo.

  “Kweli uhalifu upo na kila siku tunajitahidi kufuatilia maeneo yote ya Gongo la Mboto. ndani ya  siku saba kuanzia Aprili 14 hadi 20 mwaka huu tumekamata jumla ya kete za bangi 640 pamoja na lita 90 za pombe aina ya gongo”alisema Kamishna Msaidizi Mkongya.

  Kamishna Msaidizi Mkongya amesisitiza wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu pia amewaomba wananchi wajitahidi  kuunda ulinzi shirikishi utakaosaidia kulinda maeneo yao  kwa sababu polisi pekee  hawawezi kulinda kila nyumba.
  Aidha, Kamishna Msaidizi Mkongya ametoa rai kwa wazazi kutoa malezi mazuri kwa watoto wao kwa kuwa asilimia kubwa ya wezi wa maeneo hayo ni watoto wao wenyewe.

  Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na walinzi shirikishi wanajitahidi kufanya doria kila siku katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam ili kuhakikisha wahalifu wote wanakamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki.

older | 1 | .... | 1192 | 1193 | (Page 1194) | 1195 | 1196 | .... | 3282 | newer