Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110108 articles
Browse latest View live

MAJI TAKA BARABARA YA KUELEKEA UWANJA WA NDEGE WA ZAMANI JIJINI MBEYA


SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aapisha makatibu wakuu

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dkt.Abduhamid Yahya Mzee kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Salum Maulid Salum kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd, Joseph Abdalla Meza kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dkt.Juma Malik Akili kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.

Rais Magufuli afungua daraja la Kigamboni, amsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar Wilson Kabwe.

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe huku viongozi wengine wakiushikilia kuashiria uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016PICHA NA IKULU.
 
Rais Dkt John Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam, Willison Kabwe wakati akizindua daraja la Kigamboni leo baada ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Paul Makonda kufichua maovu yake juu ya kuongeza mikataba ya uzabuni kwa miezi Kumi katika kituo Kikuu cha mabasi cha Ubungo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Aprili, 2016 amefungua rasmi Daraja la Kigamboni linalounganisha usafiri wa barabara kati Kigamboni na Kurasini Jiji la Dar es salaam na amependekeza Daraja hilo liitwe Daraja la Nyerere (Nyerere Bridge).
Sherehe za ufunguzi wa daraja hilo kubwa na la kipekee kwa Afrika Mashariki na Kati zimefanyika kando ya daraja hilo upande wa Kigamboni na kuhudhuriwa na viongozi na wageni mbalimbali wakiwemo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Edwin Ngonyani, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) Mheshimiwa Antony Mavunde, Wabunge na Mameya wa Jiji na Dar es salaam.

Ujenzi wa daraja hilo umehusisha nguzo mbili za pembezoni na mihimili miwili inayoshikilia nyaya 36, na daraja zima lina urefu wa meta 680, upana wa mita 32, njia sita za magari, njia mbili za watembea kwa miguu na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 2.5.
Daraja hilo limejengwa kwa fedha za ndani na kugharimu jumla ya shilingi Bilioni 254.12 ambapo kati ya fedha hizo asilimia 60 zimetolewa na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), na asilimia 40 zimetolewa na Serikali ya Tanzania.

Kujengwa kwa Daraja hili kutaondoa kero ya msongamano wa magari na usafiri kwa wakazi wa Kigamboni na wakazi wa katikati ya Jiji la Dar es salaam ambao walilazimika kutumia kivuko (Ferry) ili kukatiza eneo la mkondo wa bahari ya Hindi ama kutumia barabara ya kuzunguka kupitia Kongowe lenye urefu wa kilometa 52.

Daraja hilo limefanyiwa majaribio kwa kutumia Malori 44 yenye uzito wa tani 30 na limethibitika kuwa na uwezo wa kubeba jumla ya tani 1,320 na hivyo linatarajiwa kusaidia usafirishaji wa mizigo ya kutoka na kuingia katika bandari ya Dar es salaam.
Akizungumza katika sherehe hizo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza vyombo husika vianze mchakato wa daraja hilo kupewa jina la "Daraja la Nyerere" (Nyerere Bridge) ikiwa ni kuuenzi mchango mkubwa wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefanya kazi kubwa ya kuijenga Tanzania.
Aidha, Rais Magufuli amewapongeza wadau wote waliohusika kufanikisha ujenzi wa Daraja hilo likiwemo Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na wakandalasi kutoka China, na ametaka watanzania wajivunie daraja hilo kubwa na lililojenga heshima kubwa kwa nchi.

Pia Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa vyombo vya habari vya Tanzania kuitangaza vyema Tanzania na kuwa na uzalendo wa kweli kwa nchi yao badala ya kubeza kazi nzuri zinazofanywa ndani ya nchi kwa manufaa ya watanzania.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Bw. Wilson Kabwe na kuagiza vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili za kusaini mikataba iliyosababisha serikali kupoteza mapato.
Dkt. Magufuli ametangaza uamuzi huo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa daraja la Kigamboni, baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Paul Makonda kumueleza kuwa amebaini upotevu wa shilingi Bilioni 3 uliotokana na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Bw. Wilson Kabwe kusaini mikataba ya ukusanyaji mapato ya Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo kwa kutumia sheria iliyopitwa na wakati, na pia ukusanyaji wa tozo za uegeshaji wa magari ndani ya Jiji.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
19 Aprili, 2016

ABIRIA WA RWANDAIR SASA KUINGIA NCHINI RWANDA BILA KITABU CHA YELLOW FEVER

$
0
0
Shirika la ndege la RwandAir linapenda kuwatangazia wasafiri wake wanaoelekea nchini Rwanda kuwa hawatahitajika kuwa na chanjo ya vitabu vya njano (Yellow Fever) pindi waelekeapo nchini humo.

Meneja mkazi Shirika la ndege la RwandAir nchini Tanzania, Ibrahim Bukenya amesema chanjo ya Yellow Fever itahitajika kwa wasafiri wanaotoka kwenye nchi zilizo na tatizo la Yellow Fever pekee kuelekea nchini Rwanda.
Ameendelea kuwashukuru wateja na wasafiri  wote wa RwandAir na kuwaomba kusafiri nao tena na tena na tena bila kuchoka.

WADAU WATAKA SIKU YA MSANII IAZIMISHWE NCHI NZIMA

$
0
0
Wasanii na wadau wa Sanaa wameomba kuwe na juhudi za halmashauri na mikoa yote nchini kuunga mkono maazimisho ya siku ya msanii ambayo yamekuwa yakiadhimishwa kila mwaka hapa nchini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye tathmini ya maazimisho ya Siku ya Msanii maarufu kama Msanii Day iliyofanyika mapema wiki hii ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) zilizoko Ilala Sharif Shamba wadau hao walieleza kusikitishwa na siku hiyo muhimu kuadhimishwa mkoa wa Dar es Salaam pekee huku wasanii wa mikoani wakiachwa nyuma.

“Tanzania ina wasanii wengi, haiwezekani siku hii muhimu kwao iwe inagusa wasanii wachache tu. Tunaamini halmashauri na mikoa ina nafasi kubwa ya kuwaunganisha wasanii nchi nzima na kuunga mkono juhudi za Baraza katika kuadhimisha siku hii” alisema Msanii wa Sanaa za Maonesho Nkwama Ballanga.

Aliongeza kuwa kupitia maafisa Utamaduni shughuli za Sanaa zimekuwa zikiendelea maeneo mbalimbali nchini hivyo lazima kuwe na maelekezo maalum kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ya kuwataka maafisa Utamaduni kuwaunganisha wasanii wote katika kuadhimisha siku hii ambayo imekuwa ikiadhimishwa Dunia nzima huku kila nchi ikiwa na namna yake ya kuadhimisha.

Tunajua wasanii katika halmashauri zetu wanafanya kazi nzuri sana lakini pia wana changamoto nyingi zinazowakabili. Kuunga mkono maadhimisho ya siku yao nchi nzima ni kujenga mfumo wa wao kujipongeza, kujitathimi lakini pia kuonesha kazi zao mbalimbali kulingana na fani zao” aliongeza Ballanga.

Kwa upande wake Msanii Ahmad Dadi wa Kundi la Sanaa za Maonesho la Lumumba alisema kuwa siku ya Msanii ni muhimu katika kutambua na kuthamini mchango wa wasanii mbalimbali nchini hivyo lazima kuwe na juhudi za makusudi za kuifanya yenye kufana na yenye kumgusa kila Msanii nchini.

“Tuna wasanii wakongwe ambao wamefanya kazi kubwa ya kuitangaza nchi. Hii ndiyo fursa ya kuwaonesha wasanii wa kizazi cha sasa hali ya Sanaa ilivyokuwa. Kuwepo kwa majukwaa ya maadhimisho kama haya nchi nzima kutaonesha thamani ya Sanaa nay a wasanii” alisema Dadi.

Siku ya Msanii mwaka huu imepangwa kuazimishwa Oktoba 29 ambapo inatarajiwa kupambwa na shamrashamra mbalimbali

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE KWA MAKOSA MBALIMBALI.

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA. 
   
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA, MTU MMOJA MKAZI WA UYOLE JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MASHAKA RAMADHAN [21] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA KETE 12 ZA DAWA ZIDHANIWAZO ZA KULEVYA.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.04.2016 MAJIRA YA SAA 10:20 ASUBUHI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. UPELELEZI NA UCHUNGUZI ZAIDI UNAENDELEA ILI KUBAINI AINA YA DAWA HIZO.

KATIKA MSAKO WA PILI: JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA MATENKI – KASUMULU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PETER CHANGWA [21] AKIWA NA POMBE HARAMU [GONGO] UJAZO WA LITA 20.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.04.2016 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO ENEO LA FORODHA –KASUMULU, KATA YA NGANA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUWA AKISAFIRISHA POMBE HIYO HARAMU KWENYE BAISKELI YAKE AKITOKEA MALAWI. 

KATIKA TUKIO LA TATU, MTU MMOJA MKAZI WA IGOGWE WILAYA YA RUNGWE MKOANI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LESSA JAPHET [45] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI CHUPA 24 AINA YA CHARGER. 

MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 19.04.2016 MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA HUKO ENEO LA MTAA WA IGOGWE, KATA YA KAWETELE, TARAFA YA TUKUYU MJINI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. 

SERIKALI IMEPIGA MARUFUKU UINGIZAJI NA MATUMIZI YA POMBE HIZO KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. POMBE HIZO NI PAMOJA NA CHARGER, RIDDER, DOUBLE PUNCH, POWER NO.1 NA BWENZI AMBAZO UINGIZWA NCHINI KUTOKA NCHINI JIRANI YA MALAWI.

WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI EMANUEL G. LUKULA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE KALI NA POMBE HARAMU [GONGO] KWANI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UINGIZAJI WA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

KATIKA TUKIO LA NNE, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MHAMIAJI HARAMU RAIA WA NCHINI KONGO AITWAYE JEAN MWELA [21] KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

MHAMIAJI HUYO ALIKAMATWA NA ASKARI WALIOKUWA DORIA MNAMO TAREHE 19.04.2016 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO ENEO LA UZUNGUNI – ROMAN KATOLIKI, KATA NA TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.

Imesainiwa na:
[EMANUEL G.LUKULA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Namba ya Simu: 0658 376 006 – Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.

MASHINDANO YA CHESS KUANZA 23 APRIL MWAKA HUU.

$
0
0
 Mwenyekiti wa  Chama cha mchezo wa Chess Tanzania (TCA) Bw. Geofrey Mwanyika akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu mashindano ya mtu mmoja mmoja ya ukanda wa Afrika 4.2 yajulikanayo kama (2016 Africa Zone 4.2 Individual Chess Championship). Yatayofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam.
Katibu wa Chama cha Mchezo wa Chess Tanzania (TCA) Bw. Nurdin Hassuji ambaye pia ni Bingwa wa Taifa wa mchezo huo akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu mashindano ya mtu mmoja mmoja ya ukanda wa Afrika 4.2 yajulikanayo kama (2016 Africa Zone 4.2 Individual Chess Championship), kulia ni Mwenyekiti wa  Chama hicho Bw. Geofrey Mwanyika. Picha zote na Ally Daud- BMT.

Na Ally Daud- BMT

MASHINDANO ya mchezo wa chessi yanayojulikana kama mashindano ya mtu mmoja mmoja ya ukanda wa Afrika 4.2 (2016 Africa Zone 4.2 Individual Chess Championship) yanatarajiwa kuanza  tarehe 23 mwezi huu mpaka tarehe 30 April mwaka huu  hapa jijini Dar es salaam.


Akizungumza hayo mbele ya waandishi wa habari Mwenyekiti wa chama cha mchezo huo nchini (TCA) Bw. Geofrey Mwanyika amesema kuwa michuano hiyo iyafanyika katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es salaam Tanzania ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo.


Aidha Bw. Mwanyika ameinisha nchi ambazo zimeleta washiriki wake ni Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Djibout, Eritrea,Somalia,Ethiopia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania  “Jumla ya washiriki 32 watachuana katika mashindano hayo ambayo yamegawanyika katika makundi mawili ya Wanaume na Wanawake na kati ya nchi hizo ambazo zinashiriki Sudan na Seychells hazijathibitisha kushiriki”. Aliongeza Bw. Mwanyika.

Kwa upande wa Katibu wa TCA  Bw. Nurdin Hassuji ambaye pia ni Bingwa wa Taifa wa mchezo huo amesema kuwa zawadi za washindi ni Dola 4500  za Kimarekani ambazo zitagawanywa kwa watakaoshinda.


Aidha Bw. Hassuji amewataka wadau wa Michezo  na waandishi wa habari kujitokeza siku hiyo ili kuipa sapoti timu yao na kuutangaza mchezo ujulikane na kupendwa zaidi nchini.


Mbali  na hayo Bw. Hassuji amesema kuwa mchezo huo wameupa kipaumbele na kwenda kuufundisha mashuleni kwa sababu inawasaidia wanafunzi kuweza kufikiri kwa haraka zaidi na kufanya mwanafunzi awe mwepesi kwenye kupambanua mambo.

RC.MAKONDA AENDELEA KUKOMAA NA WATUMISHI HEWA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na watumishi hewa waliopo katika Manispaa za Mkoa wa  Dar es Salaam. Amesema kuwa mchakato wa kuwatafuta watumishi hewa wengine unaendelea katika manispaa za mkoa wake.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kazi ya kutafuta watumishi hewa katika manispaa za jiji la Dar es Salaam bado linaendelea baada kubaini njia chafu wanazotumia watumishi hewa hao.

Akizungumza leo na waandishi habari ,Makonda amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ni kioo kwa nchi hivyo jitihada zinaendelea ya kutafuta na kazi hiyo itafanywa sekta kwa sekta.

Amesema kuwa Wakuu wa Wilaya katika jiji la Dar es Salaam hakuna kufanya kazi yeyote mpaka wamelize kutafuta watumishi hewa kwa kutumia malipo ya watumishi kutoka taasisi za fedha
(Pay Row).

Makonda amesema idadi ya watumishi hewa 71 aliowasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –Tamisemi, Georgre Simbachawene  ni ndogo katika  jiji la Dar es Salaam hivyo kazi lazima iwe endelevu.

Amesema kuwa watumishi Hewa hawawezi wakawa wanalipwa mshahara huku wanaofanya kazi kwa moyo mmoja wanajisikia  vibaya hivyo ni lazima watafutwe na wachukuliwe hatua na vyombo vya dola.

Mkuu Mkoa amesema kuwa kati ya watumishi hewa 71 ni watumishi 34 hewa wamefunguliwa mashitaka katika mahakama mbalimbali kutokana kuchukua fedha wasioifanyia kazi.

VODACOM TANZANIA FOUNDATION KUWEZESHA WANAWAKE 1000 KUTIBIWA SARATANI.

$
0
0
Wakina mama wanaotibiwa ugonjwa wa kansa ya kizazi katika hospitali ya Ocean road wakifurahia jambo na Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza(kulia) baada ya kutangaza mfumo wa kusaidia matibabu kwa kina mama hao ulioshirikisha taasisi za T-MARC Tanzania,Pink Ribbon Red Ribbon na Vodacom Foundation ambayo imetoa kiasi cha Dola za Marekani 87,400 kwa ajili ya kuwawezesha akina mama waishio vijijini wanaosumbuliwa na Kansa ya kizazi kuweza kusafiri kutoka maeneo wanayoishi hadi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa awali pamoja na matibabu ya ugonjwa huo katika hospitali ya Ocean Road(ORCI).
Baadhi ya akina mama wanaotibiwa ugonjwa wa kansa ya kizazi katika hospitali ya Ocean road, wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliohusu taasisi zisizo za kiserikali za T-MARC Tanzania,Pink Ribbon Red Ribbon na Vodacom Foundation wakitangaza mfumo wa kusaidia matibabu kwa wakina mama hao ulioshirikisha taasisi hizo ambapo Vodacom Foundation imetoa kiasi cha Dola za Marekani 87,400 kwa ajili ya kuwawezesha wakina mama waishio vijijini wanaosumbuliwa na Kansa ya kizazi kuweza kusafiri kutoka maeneo wanayoishi hadi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa awali pamoja na matibabu ya ugonjwa huo katika hospitali ya Ocean Road(ORCI).

SARATANI ni moja ya ugonjwa ambao umekuwa ukiongezeka kwa kasi nchini katika miaka ya karibuni ambapo umekuwa ukisababisha watu wengi kupoteza maisha huku wahanga wengi wa ugonjwa huo wakiwa hawajui wafanye nini zaidi ya kuishi kwa hofu , wengi wakiwa hawajui dalili zake na wanaozijua wakiwa wanaamini kuwa hauna tiba.

Ugonjwa wa Saratani umekuwa ukiwashambulia binadamu kupitia aina mbalimbali za viungo vyao na matibabu yake yamekuwa yakitofautiana kadri ya ugonjwa unavyokuja.

Kwa hapa nchini Saratani ya Shingo ya kizazi ambayo imekuwa ikiwashambulia wanawake ni tishio kubwa na imekuwa ikisababisha vifo vingi.Tafiti za karibuni zinabainisha kuwa kati ya wanawake wahanga wa ugonjwa wa Saratani nchini,asilimia 55 hadi 65 wanasumbuliwa na saratani ya shingo ya kizazi na inakadiriwa kuwa kati ya wanawake 7,515 wanaobainika kuwa na ugonjwa huu kwa mwaka idadi yao kubwa yaani 6,009 hupoteza maisha.

Changamoto nyingine kwa wanawake wahanga wa ugonjwa huu inayopelekea wachelewe kupata matibabu imebainishwa kuwa ni kuwa na maisha duni ambapo wengi wao wanakuwa hawana uwezo wa kusafiri hadi kwenye hospitali kubwa zinazofanya uchunguzi na matibabu , matokeo yake wengi huishia kubaki majumbani kwao hususani maeneo ya vijijini hadi wanapofikwa na mauti ya kifo.Zaidi ya asilimia 95 ya wanawake wahanga wa Saratani ya Shingo ya kizazi nchini wanakabiliwa na tatizo hili.

Katika kupunguza vifo vya akina mama kutokana na Saratani ya Shingo ya kizazi, taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali ya T-Mark na Pink Ribbon Red Ribbon yameamua kulivalia njuga tatizo hili kwa kuanzisha mradi unaotoa elimu kwa akina mama kujua dalili za ugonjwa huo na kuwawezesha kusafiri bure kutoka makwao hadi jijini Dar es Salaam ilipo hospitali inayotoa matibabu ya Saratani ya Ocean Road na Bugando ili wakatibiwe.

Kupitia huduma ya M-Pesa wanawake waliofanyiwa uchunguzi na kubainika kuwa na dalili ya Saratani ya shingo ya kizazi huweza kupata fedha za nauli kutoka kwa washirika wa Vodacom Foundation katika utekelezaji wa mradi huu ambapo huweza kufika kwenye hospitali kwa ajili ya matibabu.Katika kipindi cha miaka 5 mradi huu umelenga kuwafikia wanawake zaidi ya 1,000 ambao watapatiwa nauli kutibiwa katika hospitali 2 za Bugando na Ocean Road.

RAIS WA ZANZIBAR, DKT. SHEIN ATEMBELEA KAMBI YA KIPINDUPINDU

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Daktari dhamana wa Kituo cha Maradhi ya Kipindupindu Ramadhan Mikidadi Suleiman leo asubuhi alipotembelea kituoni hapo Chumbuni karakana Wilaya ya Magharibi Unguja,wengine ni Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo(wa pili kushoto) na naibu Waziri wa Wizara hiyo Harusi Said Suleiman na Katibu Mkuu Dkt.Juma Malik Akili (katikati).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka Mkurugenzi kinga Wizara ya Afya Dk.Mohamed Dahoma (katikati) wakati alipotembelea Kituo cha Maradhi ya Kipindupindu hapo Chumbuni karakana Wilaya ya Magharibi Unguja leo asubuhi,wengine ni Daktari dhamana wa Kituo cha Maradhi ya Kipindupindu Ramadhan Mikidadi Suleiman (kushoto)Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt.Jama Adam Taib(wa pili kushoto).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akimsikiliza Mwanamama Siti Akida Makame mkaazi wa Ziwa Maboga aliyeruhusiwa kurudi nyumbani katika kituo cha Maradhi ya Kipindupindu hapo Chumbuni Karakana Wilaya ya Magharibi Unguja,baada ya kuugua maradhi hayo wakati Rais alipotembelea Kituo hicho leo asubuhi.

TANAPA KUZINDUA KAMPENI YA USAFI MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Pascal Shelutete akizungumza na wanahabari jijini Arusha (hawapo pichani) kuhusiana na Kampeni ya siku Kumi ya Usafi wa Mlima Kilimanjaro inayotarajiwa kuanza kesho. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania, Cyril Ako.

Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kesho tarehe 21.04.2016 litazindua Kampeni Maalum ya siku 10 ya usafi wa Mlima Kilimanjaro. Uzinduzi huo Utafanywa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Mecky Sadik.

Kazi hii ya kusafisha Mlima Kilimanjaro itafanywa na watumishi wa hifadhi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa utalii zaidi ya 200, wakiwemo mawakala wa utalii (tour operators), waongoza wageni (guides), wapagazi (porters) na wapishi (cooks) wanaowahudumia watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro.

Usafi huu utahusisha maeneo mbalimbali ya hifadhi kama vile njia za kupandia mlimani, maeneo ya kupiga kambi, maeneo ya mabanda, na maeneo ya kupumzikia wageni (picnic sites).

Kampeni hii ni muendelezo wa utaratibu wa kawaida wa hifadhi unaofanyika kila wakati kuhakikisha maeneo ya hifadhi hasa yanayotumika na wageni yanakuwa katika viwango vya kimataifa vya utoaji huduma kwa wageni. Huu ni utaratibu wenye lengo la kuwahamasisha wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa wanauweka Mlima Kilimanjaro katika hali ya usafi muda wote.

Mlima Kilimanjaro unachangia zaidi ya Shilingi Bilioni 60 ambazo ni sawa na asilimia 34 kwa mwaka katika mapato ya TANAPA. Aidha, Mlima Kilimanjaro hutoa ajira zaidi ya laki tatu(300,000) kwa mwaka kwa Watanzania wanaofanya shughuli za utalii mlimani.

DENMARK YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MUZIKI KWA TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBA)

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa,na Michezo Leah Kihimbi akizindua mradi wa vyombo vya muziki kati ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) na Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Watu wa Denmark (CKU), uzinduzi huo ulifanyika katika Chuo cha Sanaa mjini Bagamoyo mkoani Pwani jana.
Msimamizi wa program wa Kituo cha Utamaduni na Maendeleo Denmark (CKU) hapa Nchini,Mandolin Kahindi akielezea utekelezaji wa mpango wa utamaduni na ubunifu Tanzania inayotekelezwa na kituo hicho kwa ushirikiano na ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.
Wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakitoa burudani.

KITUO cha Utamaduni na Maendeleo cha Denmark (CKU), kimetoa msaada wa vifaa vya muziki katika Tasisi ya sanaa na utamaduni Bagamoyo (TASUBA) vyenye thamani ya shilingi milioni 80 za kitanzania.

Mbali na kununua vifaa vya muziki,sehemu ya fedha hizo pia zitatumika katika matengenezo na usimamizi wa vifaa hivyo kwa kipindi cha mwaka mmoja wa mradi huo.

Akizungumza jana wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Msimamizi wa program CKU hapa Nchini,Mandolin Kahindi anasema kuwa ni moja fursa ya kuendeleza utamaduni na maendeleo ya kiuchumi.

Alisema kuwa msaada huo ni utekelezaji wa mpango wa utamaduni na ubunifu Tanzania inayotekelezwa na kituo hicho kwa ushirikiano na ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.


"Unajua mpango wa kuanza kutoa msaada Tasuba ulianza mwaka 2014 baada ya CKU kukitembelea chuo hicho na kuelezwa kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa vifaa vya muziki vya kufundishia na kujifunzia"alisema.

Alifafanua kuwa mpango huu wa kusaidia uliazinduliwa rasmi juni mwaka jana ililenga kutengeneza fursa za kiuchumi kupitia jukwaa la sanaa na ubunifu ambapo watanzania watajipambanua kupitia kushiriki shughuli mbalimbali za kitamaduni na kujipatia kipato.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Kutoka Wizara ya Habari ,utamaduni,sanaa,na michezo Leah Kihimbi alisema kuwa amefurahi kupata msaada huo katika chuo cha sanaa lengo likiwa ni kuendeleza vipaji hapa nchini.

"Katika chuo hiki ni kweli kulikuwa na uhaba wa vifaa vya kufundishia lakini sasa tumepokea msaada kutoka katika Danish Centre for Culture and Development(CKU) kuweza kuwasaidia wanafunzi katika chuo hiki.

Aliongeza na kusema kuwa ni jambo la kuigwa kwa tasisi nyingine lengo ni kuweza kusaidia vyuo mbalimbali hapa nchini.

MANISPAA YA KINONDONI YAINGIA MKATABA WA UJENZI WA BARABARAZA MANISPAA YA KINONDONI NA KAMPUNI YA MS/H.P GAUFF INGENIEURE GMBH&CO,KG-JBG

$
0
0
 Meya wa Halmashauri  Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  juu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kusaini Mkataba na Kampuni ya MS/H.P GAUFF INGENIEURE GMBH&CO,KG-JBG kwa ajili ya Ujenzi wa  Barabara za Halmashauri ya Kindondoni kwa kiwango cha lami  ambazo zitapunguza  msongamano pamoja na ujenzi wa mifereji ya kusafirishia maji ,leo  jijini Dar es Salaam.kushoto ni Meneja wa Tawi la Gauff Consultants, Thorsten  Seitz
 Meneja wa Tawi la Gauff Consultants, Thorsten  Seitz, akizugumza na kuishukuru  Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwakumpa kampuni yake Zabuni  hiyo leo  jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meya wa Halmashauri  Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagulumjuli.
 Mkataba kisaniwa.
Meya wa Halmashauri  Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob wa (kushoto) akimkabidhi mkataba Meneja wa Tawi la Gauff Consultants, Thorsten  Seitz.
(Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya Jamii).

WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI KUTOKA TANZANIA WATEMBELEA SOKO LA SAMAKI FERRY

$
0
0

Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki (EALA), kutoka Tanzania, Mh.Abdullah Mwinyi, (katikati-wapili kulia), akipewa maelezo na meneja wa soko la samaki Ferry, Bw.Solomon Mushi, kuhusu biashara ya samaki sokoni hapo leo Aprili 20, 2016.

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

WABUNGE wa bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania, wameendelea na ziara za kutembelea shughuli za kiuchumi za wananchi na leo Aprili 20, 2016 walikuwa kwenye soko la samaki la kimataifa ferry jijini Dar es Salaam.

Wabunge hao wakongozwa na mwenyekiti wao, Mh. Makongoro Nyerere, Wamewaeleza viongozi wa wavuvi, wakaanga samaki na wapaa samaki fursa zilizopo kwenye ushirikiano wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki ambapo kwa sasa lina jumla ya nchi wanachama sita, Sudan Kusini ikiwa ndio mwanachama wa hivi karibuni kabisa.

Wabunge hao pia wametembelea na kujionea shughuli zihusianazo na samaki kwenye soko hilo. Pia walipata fursa ya kusikiliza maoni mbalimbali ya wadau hao katika soko la samaki Ferry. Soko lasamaki Ferry ni moja ya maeneo yanayotoa ajira kwa vijana wengi hapa jijini Dar es Salaam, ambao ukiacha wavuvi wao hufanya kazi ya kupaa samaki, kushusha samaki kutoka kwenye mitumbwi na kukaanga samaki. Pia kuna akina mama na baba wanaotoa huduma za chakula.
Mh. Mwinyi, akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana mawazo baina ya wabunge hao nawashika dau kwenye soko hilo, wengine kutoka kushoto ni Meneja wa soko hilo, Bw. Mushi, Mwenyekiti wa bodi ya soko ambaye pia ni diwani wa kata ya Kivukoni jijini Dar es Salaam, Mh.Masaba, Mwenyekiti wa wabunge wa EALA-Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, na Mh. Nderaikindo Kessy
Mvuvi akieleza maoni yake mbele ya wabunge hao.
Shughuli za samaki zikiendelea kwenye moja ya mabanda ya soko hilo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Forty-Three American Peace Corps Volunteers Sworn In

$
0
0
U.S. Peace Corps Volunteers dancing to a Tanzanian traditional song moments before being sworn into their two years of service by U.S. Embassy Dar es Salaam’s Chargé d’Affaires, a.i., Virginia M. Blaser. The ceremony was held at the U.S. Embassy in Dar es Salaam on April 20, 2016.

U.S. Embassy Dar es Salaam’s Chargé d’Affaires, a.i., Virginia M. Blaser swore in 43 Peace Corps Volunteers today into to their two years of service to Tanzania.  The Volunteers will serve two years in Tanzania and will be stationed in 19 districts, including:  Iringa, Mufindi, Kondoa, Mbinga, Masasi, Ludewa, Lushoto, Songea, Hanang, Makete, Singida Rural, Same, Njombe, Manyoni, Shinyanga, Njombe, Makambako, Wanging’ombe, and Mbeya.

Also in attendance at the ceremony at U.S. Embassy Dar es Salaam were Deputy Permanent Secretary for Health Deogratius Mtasiwa from the President’s Office, Peace Corps Country Director Elizabeth O’Malley, the new Volunteers’ district supervisors who will work with them over the next two years, and former Peace Corps Volunteers from around the world.

Ms. Blaser told the new Volunteers:  “What will define you, what will set you apart in the minds of the Tanzanians with whom you will live and work over the next two years, is your commitment to friendship, and your desire to forge a peace that cuts across national boundaries and interests.”

READ MORE HERE

MBALI NA DIAMOND PLATNUMZ & NEYO WAFUATAO NI WAKALI AMBAO MPAKA SASA WAMESHATAMBULISHWA KUWAKO NDANI YA JEMBEKA FESTIVAL 21/05/2016 CCM KIRUMBA MWANZA

$
0
0






LIST BADO INAENDELEA.............

Uchukuzi SC yaanza michuano ya Mei Mosi kwa kishindi, yaichapa Ukaguzi bao 3-1

$
0
0
 Kikosi cha Uchukuzi SC kabla ya mechi na Ukaguzi.
 Mchezaji wa timu ya Uchukuzi SC, Abubakar Mwamachi (mwenye namba 22 mgongoni) akifunga kwa kichwa bao la kwanza. Uchukuzi iliishinda Ukaguzi kwa magoli 3-1.
 Mkuu wa benchi la ufundi la timu ya soka ya  Uchukuzi SC, Kenneth Mwaisabula (kulia) akiongea na mmoja wa wachezaji wa timu ya Ukaguzi, mara baada ya mchezo wao kumalizika. Uchukuzi walishinda kwa magoli 3-1.

TIMU ya soka ya Uchukuzi SC imeng’ara kwa kuifunga Ukaguzi mabao 3-1 katika mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Uchukuzi SC ambayo chini ya benchi la ufundi mahiri linaloongozwa na Kenneth Mwaisabula ‘Mzazi’ ambaye ni Mkuu wa benchi hilo,  huku Elutery Muholeli ni kocha na Robert Damian ni meneja wa timu hiyo, waliwapeleka puta wapinzani wao na kuandika bao la kwanza lililofungwa kwa kichwa na Kado Nyoni, baada ya kuwahi mpira wa kona safi iliyochongwa na Omar Said ‘Chidi’ katika dakika ya 34.

Hatahivyo, Ukaguzi walisawazisha katika dakika ya 50 kupitia kwa Ben Chezue aliyepiga mpira wa adhabu ndogo uliokwenda moja kwa moja golini. Chezue aliingia dakika 49 kuchukua nafasi  ya Deo Masanja aliyekuwa ameumia.

Uchukuzi SC iliongeza bao katika dakika ya 72 lililofungwa Issac Ibrahim aliyeachia shuti kali, lililomshinda kipa wa Ukaguzi, Shomari Dumba.

Nahodha wa Uchukuzi SC, Francis Charles alipigilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao la tatu katika dakika ya 90 kwa njia ya penati baada ya Bilal Mleli kushika mpira katika eneo la hatari.

Uchukuzi SC iliyokuwa ikicheza kwa kuonana, awali timu Uchukuzi SC ilikosa magoli kibao ya wazi, baada ya wachezaji wake Abubakar Mwamonchi katika dakika ya 25 kupiga mpira uliopita pembeni kidogo ya goli, huku Francis alishindwa kuunganisha krosi ya Masoud Juma katika dakika ya 30, tena Francis aliyeisumbua ngome ya Ukaguzi katika dakika ya 58 alipaisha mpira akiwa karibu na kipa.

Akizungumza mara baada ya mechi, kocha Muholeli alisema Ukaguzi ni moja ya timu ngumu, lakini aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kutoka na ushindi mnono, ambao umesaidia kusafisha njia.

“Hapa tumekuja kushindana na kila mechi kwetu tunaiita ni fainali, hivyo timu zote zilizokuja hapa ni nzuri, ila tunataka tushinde mechi zote ili tujiweke pazuri kushinda na kutwaa kombe hili, kwani tumeshafika fainali mara nne,” alisema Muholeli.

Naye Mwenyekiti wa Uchukuzi SC, Mohamed Ally alisema wamekuja Dodoma kuchukua ubingwa na anauhakika wa timu yake itafanya vyema kutokana na nidhamu ya mazoezi wanayofanya kila.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Kituo cha Jemolojia Kuboreshwa Zaidi

$
0
0
Na Asteria Muhozya, Arusha 
Imeelezwa kuwa, Serikali imeandaa mpango wa kuhakikisha inakiendeleza Kituo Cha Jemolojia Tanzania (TGC) ili kiwe kituo Bora cha utoaji mafunzo ya uongezaji thamani madini nchini. 
 Hayo yameelezwa na Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), Mhandisi Idrisa Yahaya katika Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Vito yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 19 hadi 21, Aprili, 2016. 
Mhandisi Yahaya aliyasema hayo baada ya kuhudhuria semina ya mafunzo kuhusu madini ya Vito na uzoefu yaliyotolewa na Wataalam waliobobea kwenye Sekta hiyo kutoka nchi ya Madagascar wakati wa Maonesho hayo. 
Mhandisi Yahaya alisema kuwa, bado jitihada zinafanywa na Serikali kuwekeza zaidi katika Kituo hicho jambo litakalopelekea kufikia kiwango ambacho nchi ya Madagasca imefikia katika utoaji mafunzo mbalimbali katika sekta hiyo. 
Aliitaja mipango hiyo kuwa ni pamoja na upatikanaji wa wakufunzi kutoka nje ya Tanzania, kukiunganisha Kituo cha TGC na vituo vingine vya kimataifa duniani na ununuzi wa vifaa vya mafunzo. 
“ Bado tunahitaji kuwekeza zaidi katika Chuo chetu ili kuweza kufikia hatua iliyofikia nchi ya Madagasca. Kuna mipango mingi imeandaliwa kwa ajili ya kituo hicho,” alisema Mhandisi Yahaya. 
Kwa upande wake, Mratibu wa Kituo cha TGC, Musa Shanyangi akieleza mipango ya kituo hicho mara baada ya kuhudhuria semina hiyo alisema ni pamoja na kuanzisha kozi ya Jemolijia, usonara, kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma kozi ya lapidary kutoka wanafunzi 18 wa sasa hadi wanafunzi 36
Pia  kuanzisha maabara ya utambuzi wa madini ya vito na kuanzisha makumbusho ya madini ya vito na bidhaa za usonara. 
Akiwasilisha uzoefu wa Chuo cha Jemolojia cha nchini Madagascar (IGM) wakati akitoa mada kuhusu chuo hicho kwa washiriki wa maonesho hayo, Mkurugenzi Mtendaji, Rasolonjatovo Adrianirina alieleza kuhusu mafunzo na huduma mbalimbali zinazohusu Chuo hicho ambacho kinatajwa kuwa Chuo bora kwa utoaji wa mafunzo ya aina mbalimbali katika fani za Jemolojia Afrika. 
Alisema kuwa, mafunzo yanayotolewa na Chuo hicho yapo katika vipindi tofauti kulingana na aina ya mafunzo yanayotolewa na hivyo kuwataka washiriki kuona umuhimu wa kukitumia chuo hicho kupata mafunzo kwa lengo la kuwezesha uongezaji thamani wa madini katika nchi husika. 
Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), cha jijini Arusha, kilianzishwa ikiwa ni moja ya hatua za Serikali za kutimiza malengo yaliyomo katika Sera ya Madini ya Mwaka 2009 yenye lengo la kuongeza mchango wa Sekta ya Madini katika pato la Taifa na ajira kwa Watanzania kupitia Uongezaji thamani madini hapa nchini. 
Aidha, mafunzo yanayotolewa na Kituo hicho ni pamoja na ukataji na ung’arishaji wa madini ya Vito ( Lapidary), utengenezaji wa bidhaa za mapambo, (Jewelry Design and Manufacturing) na uchongaji wa vinyago vya mawe (Stone Carving). 
Uongezaji thamani madini unalenga kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania watakaofanya kazi kwenye vituo vya kuongeza thamani madini huku wengine wakijiajiri na kuongeza mapato ya Serikali, hivyo kuongeza mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa. Kituo cha Jemolojia kilianzishwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.
 Mjiolojia kutoka Idara ya Madini, Asimwe Kafrika akizungumza wakati Semina ya Mafunzo kutoka Chuo cha Jemolojia cha Madagascar iliyotolewa wakati wa Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Vito- Arusha yaliyoanza  jijini Arusha tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016.

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi Dominic Rwekaza (kushoto) akiwa na Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa  Rasilimali Madini (SMMRP), Mhandisi  Idrisa Yahaya na Kiongozi wa Mradi     wa SMMRP wa Benki ya Dunia, Mamadou Barry       wakizungumza mara baada ya kuhudhuria  Semina ya Mafunzo kutoka Chuo cha Jemolojia cha Madagascar iliyotolewa wakati wa Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Vito- Arusha yaliyoanza  jijini Arusha tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016.

 Mkurugenzi Mtendaji, wa Chuo cha Jemolojia  cha Madagascar, Rasolonjatovo Adrianirina  akizungumza na Washiriki wa Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Vito- Arusha yaliyoanza  jijini Arusha tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016.

 Washiriki wa Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Vito- Arusha yaliyoanza  jijini Arusha tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016 wakiwa katika Semina ya Mafunzo kutoka Chuo cha Jemolojia cha Madagascar iliyotolewa wakati wa Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Vito- Arusha yaliyoanza  jijini Arusha tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016.

Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda Kusini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka akizungumza wakati wa Semina ya Mafunzo kutoka Chuo cha Jemolojia cha Madagascar iliyotolewa wakati wa Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Vito- Arusha yaliyoanza  jijini Arusha tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016.

TASWIRA ZA WADAU WALIOSHUHUDIA UZINDUZI WA DARAJA LA NYERERE KIGAMBONI JANA APRILI 19, 2016

$
0
0

 Rais John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Naibu Kamishna wa Uhamiaji George Goda alipowasili Kigamboni na mkewe mama Janeth Magufuli kuzindua daraja la Nyerere na Jumanne Aprili 19, 2016
 Wadau kutoka sehemu mbali mbali wakishuhudia siku hii ya kihistoria
 Viongozi wa taasisi mbalimbali pamoja na wananchi
Rais John Pombe Joseph Magufuliakichukua mkasi kukata utepe  kuzindua daraja la Nyerere huko Kigamboni Jumanne Aprili 19, 2016.
Viewing all 110108 articles
Browse latest View live




Latest Images