Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1190 | 1191 | (Page 1192) | 1193 | 1194 | .... | 3285 | newer

  0 0

  19 April (tonight!!) - 'I Shot Bi Kidude / Kifo cha Bi Kidude', is a feature length documentary by Andy Jones, commemorating the third anniversary of the legendary taarab singer Bi Kidude's passing.  May she rest in power! The film explores the strange circumstances surrounded the last year of her life, and reveals the complicated truth behind some of the well-known controversies. 

  The film showed over the weekend in Zanzibar, and has already garnered some interesting press so far. Read the following stories for more info about the film!

  -  27 April – Lute Mwakisopile's exhibition 'Life Goes On' at Oasis Cafe will be up until 27 April. We hope you will stop by to see his colorful mixed media works that center on city life in Dar es Salaam. Lute will be followed by an exhibition of Mohamed Jafry, curated by Nafasi artist Gadi Ramadhani. The exhibition, titled 'Jana na Leo' will be up til 11 May.

  - 28 April - Jan Van Esch and Ebony Verbond's 'In Wonderland' will open at Alliance Francaise. Their work will invite you to venture into new and fantastical realities -- you don't want to miss it!

  -  30 April - we will present a special edition of Chap Chap in partnership with CEFA for the final event of the "Art Against Poverty" project. "Meet the Artists" will give audiences the chance to see the culmination of 24 months of creativity from more than 100 artists from Dar es Salaam and Nairobi. The artists include musicians, dancers, acrobats, clowns, and visual artists. Their portraits will be exhibited in an installation called "Dreams and Selfies." The event starts at 17.00 and is free and open to the public. For more information, you can email cefatanzania@gmail.com and info@nafasiartspace.org

  0 0
 • 04/19/16--04:00: BEI YA MADAFU LEO.

 • 0 0

  Mkurugenzi huduma na elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Richard Kayombo (Kushoto) akizumgumza na waandishi wa habari (hapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana kukusanya mapato kupitia tasinia ya mziki na filamu kwa kuhakikisha  bidhaa za filamu na mziki zenye stemu za kodi ndizo zinazoingizwa sokoni ili kulinda kazui za wasanii wa hapa nchini.
  Katibu Mtendaji wa bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo (wa pili kutoka kulia) akizungumza na waandisho wa ha bari jijini Dar es Salaam leo, amewaomba wadau wa sanaa na wote wanaosambaza na kuuza kazi za Filamu na Mziki hapa nchini ambazo hazijabandikwa stempu halali za kodi kuacha mara moja na kufuata utaratibu wa kupata stempu hizo katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ili wawe halali kuuza bidhaa hizo.
  anayefuata ni Mkurugenzi huduma na elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Richard Kayombo.
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imefungia maduka ambayo yalikuwa yakiuza kanda za muziki na Filamu bila kulipa kodi pamoja na kukosesha msanii kupata haki yake kutokana na kazi zao.

  Akizungumza leo  na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Richard Kayombo amesema katika operesheni walioifanya hivi karibuni kwa kushirikiana na kampuni ya Majembe wameweza kukamata CD na DVD ambazo hazina stempu za kodi na kusababisha wasanii kukosa haki yao kwa kazi walizotweta jasho.

  Amesema katika operesheni hiyo wameweza kukamata CD na DVD za nje zinazoingizwa nchini ambazo,zimekuwa zikilalamikiwa kwa kusababisha kazi za ndani kukosa soko.

  Kayombo amesema katika operesheni hiyo wameweza kukamata CD na DVD 656,579 zenye thamani zaidi ya sh.bilioni moja ambazo zilikuwa zikisambazwa bila kufuata taratibu na sheria na kati ya hizo 650,101 ni za kutoka nje ya nchi huku kazi ndani zikiwa 6,478 ikiwa na kodi iliyokadriwa ni zaidi ya sh.milioni 31 na gharama za stempu ni zaidi ya sh. Milioni 11.

  Maduka waliouafungia ni kutokana na kushindwa kutoa ushirikiano kwa TRA kufanya kazi yake ya kutafuta kodi ambayo ni Kilimanjaro House Music, 1 Shop near Kilimanjaro Music, Siku Hazifanani DVD Move, Lum Mult Technology & General Supplies ,Fetty  Big Star maduka hayo yanapatikana Kariakoo, GM Video Centre Banana Ukonga pamoja na Unknown Mbagala.

  Amesema katika operesheni hiyo wameweza kukakamata mitambo  47 ya kudurufu kazi za wasanii  CD na DVD, Komputa nne na UPS moja na wafanyabiashara wenye mitambo hiyo ni, Peter Zakaria Mkude mkazi (Mabibo), Ismail Seif (kigogo), Auguster Company (Kariakoo), Hillary Proches (Sinza),Babu Juma Kundawi (Mwanayamala), Ignus Peter Mushi (Mwananyamala).

  0 0
 • 04/19/16--05:07: MATUKIO YA BUNGENI LEO.
 •   Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongozwa na Mpambe wa Bunge kuingia kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma  kuongoza kikao cha kwanza cha  mkutano wa tatu wa Bunge   Aprili 19, 2016.
    Spika wa Bunge Job Ndugai   (kulia) akimwapisha  Ritta Kabati kuwa mbunge kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma  Aprili 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)


  Spika wa Bunge, Job Ndugai akimwapisha Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mstaafu,  Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge kwenye ukumbi wa Bunge  Mjini Dodoma Aprili 10, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Bumbuli na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, January Makamba, bungeni mjini Dodoma Aprili 19, 2016.
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  STATE HOUSE ZANZIBAR.
  OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

  PRESS RELEASE

  Zanzibar                                                             19.4.2016.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa juhudi za makusudi sambamba na mashirikiano ya pamoja zinahitajika katika kupambana na maradhi ya kipindupindu ambayo yameonesha kushika kasi hivi sasa hapa nchini.


  Dk. Shein aliyasema hayo katika mazungumzo kati yake na uongozi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa Tanzania, ukiongozwa na Mwakilishi wa Shirika hilo Dk. Chatora Rufaro pamoja na viongozi wengine wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) wanaofanya kazi zao hapa nchini.


  Katika mazungumzo hayo Dk. Shein aliyapongeza mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) yanayofanya kazi zake hapa nchini likiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO), pamoja na UNICEF katika juhudi zao za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar hasa katika mapambano ya maradhi ya kipindupindu yalioibuka hivi sasa.


  Dk. Shein alisema kuwa ujio wa Mwakilishi huyo wa (WHO) hapa nchini katika kipindi hichi ni muhimu sana na utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya katika kusaidia mapambano ya maradhi hayo.


  Alisema kuwa iwapo juhudi za makusudi zitachukuliwa na kila mmoja akafanya wajibu wake ipasavyo sambamba na kuwa na mwamko katika kuchukua tahadhari kuhusu kujikinga na maradhi ya kipindupindu hatua hiyo itasaidia katika kupambana na maradhi hayo ambayo hatimae yatapungua ama kuondoka kabisa.


  Dk. Shein alisema kuwa maradhi hayo yana historia hapa Zanzibar na yaliwahi kuibuka katika miaka ya nyuma lakini baada ya juhudi kubwa za kuyatokomeza kuchukuliwa na Serikali kwa mashirikiano na wananchi pamoja na washirika wa maendeleo yalichukua muda kuibuka tena kutokana na juhudi za pamoja zilizochukuliwa wakati huo.


  Aidha, Dk. Shein alieleza haja ya kudumisha usafi hasa katika maeneo yote ya visiwa vya Zanzibar yakiwemo maeneo ya Manispaa ya mji wa Zanzibar ambayo hali ya usafi wa mji huo haiko vizuri hali ambayo inachangia kuibuka kwa maradhi hayo.


  Akieleza umuhimu wa kutumia dawa za kutia kwenye maji yaani vidonge vya “water guard” Dk. Shein alisema kuwa mbali ya hatua hiyo watendaji wa Wizara ya Afya nao wanajukumu kubwa katika kutekeleza majukumu yao na kusisitiza ulazimu wa kutumia maadili yao ya kazi katika kuwasidia wananchi.


  Akigusia suala zima la elimu kwa jamii, Dk. Shein aliitaka Wizara ya Afya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi mara kwa mara kupitia vyombo vya habari juu ya athari, kinga na maambukizi ya maradhi hayo.


  Dk. Shein alisema kuwa mripuko wa maradhi hayo katika kipindi hichi ni changamoto kubwa kwa Wizara ya Afya na kueleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea na juhudi zake za kuzisaidia sekta zote katika kupambana na maradhi hayo.


  “Maradhi ya kipindupindu ni rahisi kupambana nayo iwapo kila mmoja atatimiza wajibu wake na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kuacha kutumia maji yasiyo salama ambayo ni moja ya chanzo kikubwa cha kupata maradhi haya….. kama tulivyofanikiwa kupambana na Malaria nalo hili linawezekana”,alisema Dk. Shein.


  Nae Mwakilishi wa (WHO) nchini Tanzania Dk. Rufaro Chatora alimueleza Dk. Shein azma ya Shirika hilo katika kuisaidia Zanzibar kwenye vita ya kupambana na maradhi hayo hapa nchini na kusisitiza umuhimu wa kuwepo mashirikiano na uratibu wa pamoja kati ya taasisi za Serikali, taasisi za kiraia na watu binafsi katika kutekeleza wajibu wao juu ya kukabiliana na kipindupindu.

  Mwakilishi huyo alieleza kuwa tokea mwezi wa Septemba mwaka jana yalipoibuka maradhi hayo hapa Zanzibar wamekuwa wakifanya kazi kwa pamoja na Wizara ya Afya na kuahidi ushirikiano zaidi katika kupambana na tatizo hilo huku akisisitiza haja kwa vyombo vya habari kusaidia juhudi hizo.
  Aidha, Mwakilishi huyo wa (WHO) amesema kuwa Shirika hilo kwa kushirikiana na mashirika mengine ya Kimataifa litaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukabiliana na maradhi hayo ili kuhakikisha yanamalizika.


  Sambamba na hayo, kiongozi huyo alieleza kuwa chanzo kikubwa cha maradhi hayo ni maji hivyo kuna kila sababu ya kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kutumia maji yalio safi na salama ikiwa ni pamoja na kutumia ‘water guard’ pamoja na kuimarisha usafi katika maeneo yote.


  Akizitaja tahadhari juu ya maradhi hayo, Dk. Chatora alisema ni pamoja na kuweka mazingira safi, kufuata masharti ya afya, kuchemsha maji ya kunywa ama kutumia maji yaliyotiwa dawa ya kuulia bektiria wanaosababisha maradhi ya kipindupindu.


  Pia, Mwakilishi huyo alieleza haja kwa wananchi kuwapeleka mapema katika vituo vya afya watu wanaobainika na dalili za maradhi ya kipindupindu kwa vile imeonekana wagonjwa wengi wanapopelekwa vituoni afya zao zinakuwa mbaya na hatimae matibabu yanakuwa magumu.


  Mapema aliekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Mohammed Saleh Jidawi alieleza mashirikiano na uhusiano mwema uliopo kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo (WHO) jinsi linavyotoa ushirikiano wake katika vita ya kupambana na maradi hayo.

  Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.


  Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

   E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais Dkt. Magufuli akimpongeza Mathias Meinrad Chikawe mara baada ya kumuapisha kuwa  Balozi Mpya wa Tanzania nchini Japani.
  Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuamuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais Dkt. Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  PICHA NA IKULU.

  0 0  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifungua mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkazi Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda Bibi. Mary Kawar akizungumza na vijana (hawapo pichani) wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na shirikila hilo leo jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akitoa mada wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam.

  Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo.

  0 0

  Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akizungumza kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) juu ya droo hiyo pamoja na ofa mbalimbali zinazoendelea kutolewa kwa wateja wa DSTV. 

  Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionyesha majina ya washindi kwenye 'sreen' kubwa (Haipo pichani) wakati wa tukio hilo.
  Droo hiyo ya JISHINDIE NA DSTV ikienndelea huku maafisa wa MultiChoice Tanzania na Mwakilishi wa Mchezo wa kubahatisha Tanzania pamoja na wanahabari wakishuhudia tukio hilo mapema leo Aprili 19.2016, Makao makuu ya kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam.
   (Picha zote na Andrew Chale.)

  KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania inayosambaza vifaa vya ving’amuzi vya DSTV hapa nchini mapema leo Aprili 19.2016 imechezesha droo maalum na kuwapata washindi wa “JISHINDIE NA DSTV” katika tukio lililofanyika Makao makuu ya kampuni hiyo Oysterbay, barabara ya Ali Hasan Mwinyi, Jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini.


  Awali katika droo hiyo, Meneja wa Huduma kwa wateja, Bi Hilda Nakajumo alieleza kuwa, droo hiyo ilianza tokea mwezi wa kwanza ambapo wateja walitakiwa kuwa na malipo kwenye ving’amuzi vyao vya DSTV bila kukatika kuanzia hiyo Januari hadi mwezi Machi.

  Wateja ambao hawajakatiwa ving’amuzi vyao katika promosheni hiyo ya JISHINDIE NA DSTV, waliotangazwa leo ambaoo ni wateja waliojiunga mwezi wa kwanza na kuweza kulipia DSTV zao bila kukatiwa matangazo kwa muda wa miezi mitatu wameweza kujishindia zawadi ya safari ya kwenda Zanzibar wakiwa wao na familia zao.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafnyakazi, WCF, Masha Mshomba, akizungumza wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, na kufanyika makao makuu ya Mfuko, barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam Aprili 19, 2016. 
   
  Lengo la semina hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kwa viongozi hao juu ya shughuli za Mfuko na faida ya wafanyakazi kupatiwa fidia endapo patatokea madhara awapo kazini. Wengine pichani ni mgeni rasmi, Pendo Z.Berege, (Mwakilishi wa Msajili wa vyama vya afanyakazi na waajiri, na Peter J. Mbelwa kutoka Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii, (SSRA).

  NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

  MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, umeendesha semina ya siku moja kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kuwalipia michango ya mwezi.

  Semina hiyo iliyofanyika makao makuu ya Mfuko, barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Aprili 19, 2016, ilifunguliwa na mwakilishi wa Msajili wa vyama vya wafanyakazi na waajiri, Bi.Pendo Z.Berege.Katika hotuba yake, Bi. Berege alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatwapo na majanga wakiwa kazini.

  Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi ni taasisi ya serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi No. 20 ya mwaka 2008.Akiwakaribisha wana semina kwenye semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Msomba alisema, Mfuko umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi kwa wafanyakazi na kwa kutambua kuwa viongozi wa wafanyakazi ndio wadau wakuu wa Mfuko huo, semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini pia wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.

  Akitoa mada juu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, alisema, Mfuko huo upo kisheria ili kutoa fidia kwa wafanyakazi waumiapo kazini.
  Naye Bi.Amina Likungwala kutoka WCF, amesema katika mada yake ya Wajibu wa Vyama vya Wafanyakazi ambapo alisema, ni wajibu wa vyama kutoa elimu kwa wanachama wao ambao ni wafanyakazi lakini pia kuwaeleza waajiri umuhimu wa kutoa michango kwa wakati 

  Mshiriki akisoma kijitabu chenye maelezo ya kina kinachofafanua majibu ya maswali ya mara kwa mara ambayo wadau wanataka kujua kuhusu WCF.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, SSRA, Bi.Irene Isaka, akitoa hotuba ya kufunga semina hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba.
  Mzee Mchafu Chakoma, mwakilishi wa viongozi wa wafanyakazi akitoa neno la shukrani.
   

  0 0

  Na Grace Michael

  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya umetoa msaada wa saruji tani tatu katika shule ya Sekondari ya Kilangalanga iliyopo mkoani Pwani kwa lengo la kujengea ukuta na kuimarisha hali ya usalama shuleni hapo.

  Akikabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Rehani Athumani alisema kuwa Mfuko unatoa kipaumbele kikubwa katika suala la elimu kutokana na kuwa na umuhimu mkubwa katika suala la afya.

  “Jamii ikiwa na elimu au ikielimika hata baadhi ya magonjwa yataondoka yenyewe...hivyo Menejimenti imeona ni vyema ikawaunga mkono katika suala hili ili hawa watoto wawe kwenye mikono salama na mazingira safi ya kusomea,” alisema Rehani.

  Aidha aliwataka wanafunzi wa shule hiyo kuhakikisha wanasoma kwa juhudi zote ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano ambayo imetoa kipaumbele kikubwa katika suala la elimu.

  “Nawaombeni sana tumieni muda wenu kwa kusoma vizuri na sio kufanya mambo ambayo yatawapotezea muda, Rais wetu wa Awamu ya Tano anapenda kila mmoja awe na elimu bora hivyo tumieni hii fursa ili mje kuiongoza nchi badae,” aliwahamasisha wanafunzi hao.

  Kwa upande wa Mjumbe wa Bodi wa shule hiyo Mbwana Chombiga akizungumzia msaada huo alisema kuwa kitendo kilichofanywa na NHIF ni cha kupigiwa mfano kwa kuwa shule hiyo imehangaika kwa kipindi kirefu bila kupata msaada.

  “Ndugu zangu kwa kweli sisi hatuna neno la kusema zaidi ya kuwashukuru tu...mnaona hata wanafunzi wana furaha kweli maana wanaona sasa mazingira yao yatakuwa bora, tunawashukuru sana na tunasema tutashirikiana nanyi katika elimu ya wananchi kujiunga na huduma za Mfuko,” alisema Bw. Chombiga.

  Katika hatua nyingine Mfuko ulikubali ombi la shule hiyo la kuwa mlezi wa shule.
  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Rehani Athumani akiwasalimia wanafunzi wa shule ya Sekondari Kilangalala Mkoani Pwani.
  Sehemu ya Msaada wa Saruji tani tatu ukikabidhiwa kwa shule hiyo kwa lengo la kusaidia ujenzi wa uzio
  Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma Grace Michael akigawa vipeperushi vyenye ujumbe wa huduma ya Toto Afya Kadi kwa wanafunzi hao.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule, ametembelewa na Viongozi wa ujumbe kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Dar es Salaam, ambao uko nchini Kenya kwa ziara ya mafunzo ya wiki moja. Ujumbe huo unaongozwa na Kamanda wa Chuo cha Ulinzi, Meja Jenerali Yacoub Mohamed, na unajumuisha Maafisa na Washiriki wa Kozi 12.
  Makundi mengine matatu kutoka chuo hicho kilichoko Kunduchi yako kwenye ziara kama hii nchini Afrika Kusini, Botswana na Namibia.
   Balozi Haule (kulia) katika mazungumzo na Vingozi waliomtembelea. Wapili kulia ni Meja Jenerali Mohamed na Kushoto ni Mwambata wa Kijeshi Ubalozini, Luteni Kanali Fabian Machemba.
   Meja Jenerali Mohamed akimkabidhi Balozi Jarida lililochapishwa na Chuo cha Ulinzi kwa heshima ya Rais Mstaafu, Mhe. Jakaya Kikwete.
  Picha ya Pamoja, Luteni Kanali Maulid Surumbu, Bw. Johnson Nyingi, Mwakilishi wa Jeshi la Kenya, Kanali Sebestian Likaunye, Meja Jenerali Mohamed, Balozi Haule, Luteni Kanali Machemba na Kamishina Msaidizi wa Magereza Phaustine Kasike.

  0 0

  Idhaa ya Kiswahili ya DW imeanzisha huduma mpya: Mukhtasari wa habari ndani ya sekunde 100. Mbali na kukuletea matangazo ya redio ya kila siku kwa ajili ya Afrika Mashariki na eneo la Maziwa Makuu, Jumatatu hadi Ijumaa DW itakupatia video fupi zenye habari. 
  Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Andrea Schmidt, ana furaha kwamba yeye na timu yake ya waandishi wa habari kutoka nchi tano tofauti wanaanzisha huduma hii mpya itakayoitwa Papo kwa Papo na itakayokuwa jicho la kuutazama ulimwengu. 
  Kupitia video zetu utaweza kupata habari muhimu za kimataifa za kila siku.

  “Papo kwa Papo” itapatikana katika chaneli ya YouTube ya DW Kiswahili, Facebook na toleo fupi la sekunde 60 litarushwa kupitia WhatsApp.

  Miongoni mwa mambo mengine, tutakuletea “hashtag” zilizovuma pamoja na katuni za kisiasa kutoka kwa wasanii maarufu Gado na Said Michael.

  Pamoja na hayo, kila Ijumaa DW Kiswahili itakuletea sekunde 100 za matukio muhimu ya kisiasa yaliyotokea katika juma zima.

  ·         Tafadhali kuwa shabiki wetu YouTube: www.youtube.com/kiswahili

  ·         Jiunge nasi katika ukurasa wetu wa Facebook: https://www.facebook.com/dw.kiswahili.

  ·         Pata “Papo kwa Papo” na taarifa zaidi kupitia WhatsApp. 
  Unaweza kujiunga nasi kupitia kiungo hiki: bit.ly/1Q86kjt 
  Kila siku Idhaa ya Kiswahili ya DW inarusha masaa matatu ya matangazo Afrika Mashariki na katika eneo la Maziwa Makuu. Kwa kushirikiana na redio washirika katika eneo zima, DW inawapatia wasikilizaji habari zisizoegemea upande wowote kuhusu yanayojiri duniani kwa ujumla na hasa barani Afrika kupitia masafa ya FM. Ili kutoa mtazamo huu wa kimataifa, timu ya waandshi wa habari kutoka nchi tano inafanya kazi na mtandao mkubwa wa waandishi walioko Afrika na kwengineko.

  Matangazo ya Kiswahili ni miongoni mwa matangazo ya DW yenye wasikilizaji wengi zaidi. DW inajumuisha vipindi vilivyopokea tuzo kama vile Learning by Ear - Noa bongo, jenga maisha yako - na vipindi vinavyojadili afya, haki za binadamu, mazingira, wanawake na maendeleo, vijana na utamaduni na sanaa. 
  www.dw.com/kiswahili

  Waliosimama kutoka kushoto Daniel Gakuba, Iddi Ssessanga, Grace Kabogo, Sudi Mnette, Bruce Amani na alieketi Caro Robi
  Kuangalia video clic link ifuatayo: 

  0 0


  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu akifungua maonesho ya kimataifa ya madini ya Arusha Gem Fair kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda leo katika hoteli ya Mount Meru .

  Kaimu Kamishna wa Madini nchini,Mhandisi Ally Samaje akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo,alisistiza nia ya serikali kupambana na utoroshwaji wa madini nje ya nchi.

  Mwenyekiti wa kamati ya Arusha Gem Fair,Peter Pereira akitoa neno la utanguliza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya madini yanayohudhuriwa na waoneshaji na wanunuzi zaidi ya 400 kutoka sehemu mbalimbali duniani.
  Madini aina ya Tanzanite.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na   Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO hapaTanzania Dr.Chatora Rufaro akiongoza Ujumbe wa mashirika ya Umoja wa Mataifa UN walipofika Ikulu Mjini Zanzibar.


  0 0

  19 April (tonight!!) - 'I Shot Bi Kidude / Kifo cha Bi Kidude', is a feature length documentary by Andy Jones, commemorating the third anniversary of the legendary taarab singer Bi Kidude's passing.  

  May she rest in power! The film explores the strange circumstances surrounded the last year of her life, and reveals the complicated truth behind some of the well-known controversies. 

  The film showed over the weekend in Zanzibar, and has already garnered some interesting press so far. Read the following stories for more info about the film!

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe huku viongozi wengine wakiushikilia kuashiria uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata picha ya kumbukumbu viongozi wengine baada ya  uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiteta jambo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt Ramadhani Dau wakati wa  uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine wakitembea juu ya Daraja la Kigamboni baada ya kulizindua katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.
  PICHA NA IKULU.

  0 0

  The Tanzania Cardiac Society (TCS) in Collaboration with thr Pan Africa Society of Cardiology – Heart Failure Task Force (PASCAR-HF Task Force) Conference 21 - 22 April 2016, at Julius Nyerere international Convention Centre (JNICC), Dar es Salaam, Tanzania. The guest of honour for the opening ceremony will Honourable, Ummy Ally Mwalimu, Minister, Ministry of Health, Social Welfare, Gender Elderly and Children

  Tanzania Cardiac Society, will be re-launched and will holds the First National Conference, the theme of the conference; Solace of Heart Failure in our community “The Comfort in Disappointment or Misery”Tanzania like other sub Saharan countries is facing an epidemiological paradigm shift from communicable diseases to non-communicable particularly cardiovascular diseases being the leading cause of morbidity and mortality in the country.

  The theme chosen to highlight the plight heart failure in our community as common end point pathway of conundrum of cardiovascular diseases the country is facing.

  Tanzania Cardiac Societyin Collaboration with Pan Africa Society of Cardiology – Heart Failure Task Force (PASCAR-HF Task Force), provide forum to discuss the means of reducing the socioeconomic impact of cardiovascular disease in the country.

  The Conference will comprise of an outstanding Scientific Exhibition/Program, the world’s leading specialists with over 200 Pan African participants expected to attend this premier event. The Tanzania Cardiac Society/ PASCAR-HF Task Force conference offers an exciting opportunity to our local doctors to share knowledge and skills in the field of cardiovascular medicine particularly management of heart failure which would be translated into daily clinical care to reduce the negative impact of cardiovascular diseases in the country. 

  The Registration fee per delegate is Tsh. 218,500/= equivalent to USD 100$ which can be deposited direct to: Stanbic Bank; Account Name; Tanzania Cardiac Society; Account Number.9120000854687 Shillings (TZS) or 9120000854709 Dollar (USD)

   NB: Registration fee paid early before 20th April 2016 will get 20% registration discount. Onsite (during conference) registration no discount

  For Registration please contact Ms Martha Yeronimo, The Event /Exhibition Manager, Tanzania Conference Services Ltd, Email: md@events.co.tz   Tel: +255 754 434 101 /+255713 329923

   Tanzania Cardiac Society is looking forward to work with you on this conference and beyond, for long-term partnership.
    
  Dr Robert Sostenes Mvungi, 
  MD(Dar), Mmed(Wits), FCP(SA), Cert.Cardio(SA)Phys 

  President Tanzania Cardiac Society

  Cell; +255 755 262 519/+255 686 178 590
  0 0

  Msanii wa bongo fleva Saraha ambaye ni raia wa Sweden ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden jijini Stockholm leo na kukutana na kufanya mazungumzo na Balozi Dora Msechu.
  Saraha hivi sasa anatamba kwenye anga za muziki nchini Sweden na nyimbo  ya "Kizunguzungu" ambayo ameimba kwa lugha ya kiswahili.
  Balozi Dora Msechu amempongeza Saraha kwa mafanikio makubwa aliyopata kwa wimbo huo ikiwa ni pamoja na  kuingia fainali ya mashindano makubwa ya kutafuta nyimbo bora hapa Sweden, Melodifestivalen. 
  Mhe. Balozi amemshukuru sana Saraha kwa kuitangaza vyema Tanzania na kusambaza lugha ya kiswahili  nchini Sweden kupitia fani ya muziki.
  Kwa upande wake, Saraha ameeleza kuwa amepata faraja kubwa sana kukaribishwa na Mhe. Balozi  kutembelea Ubalozi wa Tanzania na amefurahi sana kupata fursa ya kuzungumza Kiswahili. 
  Saraha amesema  kuwa ana mapenzi makubwa sana na Tanzania  na ataendelea kutumia lugha ya kiswahili katika kazi zake za usanii hapa Sweden. Amebainisha kuwa  hivi sasa yupo mbioni kutoa nyimbo nyingine kali ya kiswahili hapa Sweden.
  Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dorah Msechu akiongea na mwanamuziki Saraha na meneja wake walipotembelea ubalozini jijini Stockholm leo.
  Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dorah Msechu akipozi na mwanamuziki Saraha alipotembelea ubalozini jijini Stockholm
  Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dorah Msechu na watumishi wa ubalozi wakipozi na mwanamuziki Saraha alipotembelea ubalozini jijini Stockholm. Cheki video yake ya ngoma yake kali ya  "Kizunguzungu" hapa chini.

older | 1 | .... | 1190 | 1191 | (Page 1192) | 1193 | 1194 | .... | 3285 | newer