Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1182 | 1183 | (Page 1184) | 1185 | 1186 | .... | 3283 | newer

  0 0


  0 0

  Karibuni Lala Land, ulimwengu wa maajabu, ambapo utajifunza na kucheza na Akili! Imba namba! Cheza herufi! Cheka, chora, na jifunze Kiingereza na Akili.

   Akili and Me ni kipindi kipya cha elimu burudani kinachotengenezwa na Ubongo Media, watengenezaji wa Ubongo Kids. Watoto wa miaka mitatu hadi sita watafurahia kuungana na Akili kwenye ulimwengu wake wa maajabu, Lala Land! Watajifunza namba, herufi, kuchora na Kiingereza. Elimika na burudika kupitia “Akili and Me” TBC1 saa 3 asubuhi j1 & j2 pamoja na Ubongo Kids, jumatau - alhamisi saa 8:30 mchana, na ijumaa saa 9 mchana.

  0 0

  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kujiwekea malengo katika utendaji kazi wao ili waweze kutimiza malengo makubwa ya sekta ya elimu.

  Profesa Ndalichako aliyasema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo kutoka Makao Makuu katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee ikiwa ni mara ya kwanza kukutana nao tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi lengo likiwa ni kuwasikiliza lakini pia kujadiliana nao namna bora zaidi ya kuboresha utendaji kazi katika wizara hiyo.

  Waziri Ndalichako aliwataka wafanyakazi kufanya kazi kujituma, kutoa huduma bora kwa wakati kwa kuwa ni watumishi wa umma na maana ya mtumishi wa umma ni kuwa na wajibu wa kuwatumikia wananchi ili wapate haki yao kwa wakati kwani haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyoptea.

  Amewataka watumishi hao kuipende kazi yao, kwa maana mtumishi anayependa kazi yake uifahamu kwa undani wake na inakuwa rahisi kuwatyumika wananchi bila ya kuwa na wasiwasi na kujiamini zaidi .“kila mfanyakazi ni lazima kujivika joho la Wizara kwa maana ya kuijua Wizara vizuri, misingi yake, dira pamoja na sera zinazotuongoza katika utendaji kazi wetu ili tuweze kufikia malengo ya kuinua ubora wa elimu” alisisitza Ndalichako.

  Akizungumza kwa niaba ya watumishi Omary Mkali alimshukuru Waziri kwa kukutana na watumishi na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri ili kuweze kufikia lengo kwa pamoja la kuinua ubora wa Elimu nchini. 
  1.       : waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiongea na wafanyakazi wa Wizara.
     wafanyakazi wa Wizara ya Elimu Sayansi Teknolojia na Ufundi wakimsikiliza Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Maimuna Tarishi akimkaribisha Waziri wa Elimu kuongea na wafanyakazi.
   waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiingia katika ukumbi wa Karimjee kuongea na wafanyakazi wa Wizara.
   


  0 0

   Mkurugenzi wa Trickster, Sonobe Atsushi akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na uzinduzi wa shindano la kibiashara ambali litakuwa katika nchi tano za Afrika.
  Meneja Mradi kutoka kampuni ya Afrika New Business Development Department(DMM)  Bw.Alex Kapungu  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Trickster, Sonobe Atsushi.


  KAMPUNI ya Kijapani inayofanya shughuli zake nchini (Tricster)  imeandaa shindano la wazo la biashara  litakalozishirikisha  nchi tano  za Afrika zikiwemo Kenya,Rwanda,Zambia,Zimbabwe na Tanzania mwenyeji wa  mashindano hayo kwa mwaka 2016.


  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Mradi kutoka kampuni ya Afrika New Business Development Department(DMM)  Bw.Alex Kapungu ambao ndio  wadhamini wa shindano hilo ameeleza kuwa lengo la shindano hilo ni  kusaidia kuboresha ujasiriamali katika bara la Afrika.


  “Shindano hili linafanyika kwa mara ya kwanza na hivyo ni fursa nzuri kwa wajasiriamali na wale wanaotaka kuwa wajasiriamali kushiriki na baadaye kufanikisha wazo hilo kiutendaji kwa kuwa biashara halisi”alisema Bw.Alex.


  Aidha ameongeza kuwa vigezo vya kushiriki shindano hilo ni mshiriki awe amefikisha miaka 18 na kuendelea, awe anajua kuongea na kuandika lugha ya kiingereza na kuwa na hati ya kusafiria.


  Naye Mkurugenzi wa Trickster Bw.Sonobe Atsushi amesema washindi watakaoingia nusu fainali watapata fursa  ya kutembelea nchi ya japani ambapo mshindi wa kwanza atapata fedha taslimu  Dola elfu tano za kimarekani.


  Pia ametoa wito kwa watanzania kujitokeza na kushiriki kwa wingi ili wapate fursa ya kuanzisha biashara kupitia mawazo watakayoyatoa na hivyo kupanua wigo wa biashara.


  0 0
 • 04/12/16--06:28: OMBAOMBA KUTIMULIWA DAR.
 • Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza kuhusiana na kuaza operesheni ya kuwaondoa ombaomba waliokandokando ya barabara, jijini Dar es Salaam leo. 
  Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutoa agizo la kuwaondo watu wanao ombaomba kandokando ya barabara jijini Dar es Salaam.

    Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  SERIKALI ya Mkoa wa Dar es Salaam imesema kuwa katika kuweka jiji safi itaanza na operesheni ya kuondoa ombaomba wanaokaa kandokando ya barabara kwa ajili ya kuomba.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa ombaomba wanakuja Dar es Salaam kwa nauli zao hivyo lazima warudi walikotoka kwa nauli zao.

  Makonda amesema operesheni hiyo inatarajiwa kuanza Aprili 18 mwaka huu ambapo kazi hiyo itafanywa na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam.

  Amesema watu wanaofanya kazi hiyo waanze kuondoka wenyewe kutokana na mikakati waliopanga jinsi ya kutekeleza operesheni hiyo.

  Makonda amesema operesheni ya kuondoa omba omba ni endelevu kutokana na kuwepo kwa uchafu kwa baadhi yao kulala katika majengo  na kufanya uchafu huo.

  Nae Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kuwa operesheni hiyo watatekeleza kuanzia siku hiyo hivyo waanze kuondoka mara moja.

  Amesema agizo la Mwenyekiti wa ulinzi na usalama la Mkuu wa Mkoa kazi kwa jeshi la polisi ni kutekeleza tu  kutokana na jamii hiyo inatoka katika sehemu zenye mamlaka ambapo kuna utaratibu juu ya kuwakimu watu wenye mahitaji maalum.

  0 0

  Na  Raymond Mushumbusi MAELEZO.

  Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanaendesha mafunzo ya wiki mbili kwa Wahandisi na mafundi wa Temesa ili kuwajengea uwezo katika kutumia teknolojia ya umeme wa nishati ya jua.

  Akifungua mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea uwezo wahandisi na mafundi ili kuweza kutumia teknolojia ya umeme wa nishati ya jua ambao umekuwa na tija kubwa hasa kwa sehemu ambazo umeme wa kawaida haujafika.

  “Nishati ya umeme wa jua imeshika kasi kwa sasa na inatumiwa sana katika maeneo ambayo umeme wa kawaida haujafika hivyo basi kwa mafunzo haya wahandisi na mafundi wetu wataweza kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuandaa na kutekeleza miradi itakayosaidia kuondokana na tatizo la umeme nchini.” Alisema Mhandisi Manase.

  Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa mafunzo,Mratibu wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu Dar es Salaam Prof Cathbert Kimambo amesema kwa kushirikiana na Temesa wameamua kutoa mafunzo kwa wataalamu hao juu ya teknolojia ya nishati ya umeme wa jua ili kuwasaidia kuendana na mabadiliko ya teknolojia kwa kuwa na utalaamu na uwezo wa kufanya kazi kulingana na mabadiliko yaliyopo.

  Mmoja wa wahandisi Kutoka Temesa Bi Sara Moses ametoa wito kwa Wahandisi wengine kuwa na utaratibu wa kujifunza na kuongeza utaalamu ili kuwezesha kuendana na mabadiliko Sayansi na Teknolojia katika kuleta ufanisi katika kazi zao.
    kaimu Mtendaji Mkuu Temesa  Mhandisi Manase Ole Kujan (wa pili kushoto) akipata maelezo juu ya ufungaji wa moja ya mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) kutoka kwa Mhandisi Zuhura Semboji mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili kwa wahandisi na mafundi wa Temesa.
    Kaimu Mtendaji Mkuu Temesa Mhandisi Manase Ole Kujan (katikati) akiangalia moja ya kifaa cha kupimia umeme kinachotumika katika mafunzo kwa wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
    Mhandisi Amani Mwanga akitoa maelekezo ya namna ya kufunga moja ya mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya  wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
   Fundi Sanifu kutoka Temesa Mganza Juma (Katikati)akiwa makini kufunga moja ya mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya  wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
  Baadhi ya wahandisi kutoka Temesa wakiwa katika harakati za kuchuna na kuunga nyaja katika moja ya mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya  wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.(Picha Zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO).

  0 0

  Bank M Tanzania plc, has recorded a robust performance in the first quarter of the current year. In what has become customary for the Bank, it posted a record growth in balance sheet as well as profitability.

  The nine year old Corporate and Investment Bank registered a pre-tax profit of TZS 7.4Bln during the first three months of the current year compared to TZS 6.13Bln for the same period last year. 

  According to the just released financial statements of the Bank for the first quarter ending on 31st March 2016, a large part of the profit has come from interest income which amounted to TZS 22.11 Bln, an increase of 32% over the corresponding period last year. Non- interest income was reported at TZS 6.6 Bln also recorded a strong growth of 15% against the income realised for the corresponding period in the previous financial year. 

  The financials are also indicative of the prudent lending practices adopted by the Bank as is evident from the NPLs (non-performing loans) remaining below the rate of 3% which stands well below the industry average.
  Bank M's CEO (Designate) Ms. Jacqueline Woiso talking to the reporters while announcing the bank's quarter one financials during the press conference held at in Dsm today. With her is the Bank M's Head of Products Mr. Johnbrighton Ngowi.
  Total assets grew to TZS 889.11Bln as at the 31st March June 2016, registering an annualized growth of 22% over the December 2015 level while deposits grew to TZS 746.49Bln at the same period, recording an annualized growth of 19% over the December 2015 level. 

  Commenting on the performance of the Bank for the first quarter of this year, Jacqueline Woiso, the CEO Designate of the Bank said that the performance was exceptionally good despite the various market challenges.  “The results for the first quarter are quite encouraging as we start this year and we believe that the forthcoming quarters of this year will be even better” she said.

  Additionally Ms. Woiso said that plans are underway to increase the bank’s core capital through a Private Placement and Initial Public Offer, these instruments will provide additional capital to the tune of TZS 50Bln. The capital growth plans are scheduled for the second and third quarter of the current year and subject to approvals by the regulatory authorities. 

  In terms of product development, Bank M is in the process of rolling out two products in the market i.e. Money. Moja Kwa Moja which will enable Bank M clients to upload their outward clearing cheques from the convenience of their offices rather than operating through the traditional ways where a client will be required to physically deposit the cheques at the bank prior clearance.

  The other product in the pipeline is Cash Management which will assist the bank’s clients in faster realisation of their accounts receivables, processing of payments and overall liquidity management though a centralised portal.

  0 0

   Balozi Haule akizungumza kwenye hafla ya kuhitimisha ziara ya Maafisa wa JWTZ.

  Maafisa na wanafunzi 29 kutoka Chuo cha Kamandi na Unadhimu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Duluti, Arusha, wamemaliza ziara ya mafunzo ya wiki moja nchini Kenya mwishoni mwa juma lililopita, iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF).

  Kundi hilo lililoongozwa na Naibu Kamanda na Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha JWTZ, Kanali Celestine Msola, lilitembelea taasisi mbalimbali za serikali na Jeshi la Kenya pamoja na taasisi binafsi. Mafunzo yao yalihusu masuala ya Jamii na Uchumi, Utawala bora, Mfumo wa Kisiasa, Ulinzi na Usalama, na Maendeleo ya Teknolojia ya Kivita.

  Akizungumza katika hafla fupi mwishoni mwa ziara hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule, alimshukuru Mkuu wa Jeshi la Kenya, Jenerali Samson Mwathethe, na watendaji wake, kwa ukarimu waliowafanyia Maafisa wa JWTZ. 

  Aliwapongeza Maafisa hao kwa nidhamu ya hali ya juu waliyoonyesha muda wote, akisema wameacha sifa nzuri ya JWTZ na Tanzania kwa ujumla.
  Mwakilishi wa KDF, ambaye pia ni Kamanda wa Chuo cha Teknolojia cha Ulinzi, Kanali Oscar Muleyi, alisema Maafisa wa Jeshi la Kenya wameshafanya ziara ya mafunzo nchini Tanzania na walikarimiwa vizuri sana.
  Balozi Haule (Katikati) akimpongeza Mwambata wa Kijeshi Ubalozini Nairobi, Luteni Kanali Fabian Machemba. Kulia ni Kanali Msola.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga (kulia) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Pavel Rezac, na kisha kufanya nae mazungumzo yaliyojikita katika kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Czech. 
  Waziri Mahiga (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Sudani Kusini Mhe. Mariano Deng Ngor (wa tatu kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Balozi Samwel Shelukindo (wa kwanza kushoto), Afisa Ubalozi wa Sudani Kusini nchini (wa pili kutoka kulia) na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Eric Ngilangwa (wa kwanza kulia). 
  Picha na Reginald Philip.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  TIMU ya Mpira wa Pete ya Wanawake wa Idara ya Uhamiaji imebuka mshindi wa tatu katika mashindano ya Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Uganda.

  Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kaimu Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli  amesema kuwa washindi wa tatu ni mwanzo wa kujipanga mashindano mengine katika kuibuka kuwa washindi wa kwanza.

  Amesema kuwa watatoa ushirikiano kwa wanamichezo katika wa idara hiyo kuendeleza vpaji wa vya watumishi katika sekta ya michezo.

  Nahodha wa Timu hiyo, Juliana Mwakalemela amesema kuwa katika mashindano hayo idara ya uhamiaji ndio pekee walioshiriki mashindano hayo.

  Juliana amesema kuwa kikombe cha mshindi waa tatu ni nyota njema katika kujiandaa mashindano mengine na kuweza kuibuka washindi.

  0 0

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanaendesha mafunzo ya wiki mbili kwa Wahandisi na mafundi wa Temesa ili kuwajengea uwezo katika kutumia teknolojia ya umeme wa nishati ya jua.

  Akifungua mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea uwezo wahandisi na mafundi ili kuweza kutumia teknolojia ya umeme wa nishati ya jua ambao umekuwa na tija kubwa hasa kwa sehemu ambazo umeme wa kawaida haujafika.

  “Nishati ya umeme wa jua imeshika kasi kwa sasa na inatumiwa sana katika maeneo ambayo umeme wa kawaida haujafika hivyo basi kwa mafunzo haya wahandisi na mafundi wetu wataweza kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuandaa na kutekeleza miradi itakayosaidia kuondokana na tatizo la umeme nchini.” Alisema Mhandisi Manase.

  Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa mafunzo,Mratibu wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu Dar es Salaam Prof Cathbert Kimambo amesema kwa kushirikiana na Temesa wameamua kutoa mafunzo kwa wataalamu hao juu ya teknolojia ya nishati ya umeme wa jua ili kuwasaidia kuendana na mabadiliko ya teknolojia kwa kuwa na utalaamu na uwezo wa kufanya kazi kulingana na mabadiliko yaliyopo.

  Mmoja wa wahandisi Kutoka Temesa Bi Sara Moses ametoa wito kwa Wahandisi wengine kuwa na utaratibu wa kujifunza na kuongeza utaalamu ili kuwezesha kuendana na mabadiliko Sayansi na Teknolojia katika kuleta ufanisi katika kazi zao.
  Fundi Sanifu kutoka Temesa Mganza Juma (Katikati)akiwa makini kufunga moja ya mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
  Baadhi ya wahandisi kutoka Temesa wakiwa katika harakati za kuchuna na kuunga nyaja katika moja ya mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
  Kaimu Mtendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Mhandisi Manase Ole Kujan (wa pili kushoto) akipata maelekeo juu ya ufungaji wa moja ya mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) kutoka kwa Mhandisi Zuhura Semboji mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili kwa wahandisi na mafundi wa Temesa.
  Mhandisi Amani Mwanga akitoa maelekezo ya namna ya kufunga moja ya mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limewapongeza viongozi, mashabiki, wachezaji wa vilabu na timu za Taifa kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ya kimataifa iliyochezwa mpaka sasa.

  Katika kipindi cha mwezi mmoja, Tanzania imeshiriki katika michuano mbalimbali ya kirafiki, mashindano ngazi za vilabu, timu za taifa ikiwemo ya Wanawake (Twiga Stars), Vijana (Serengeti Boys) na Taifa Stars.

  Katika michezo kumi iliyochezwa mfululizo mpaka sasa, timu za  Tanzania hazijapoteza mchezo hata mmoja mpaka sasa, ikiwa ni kwa vilabu pamoja na timu za taifa za Wanawake, Vijana na Taifa Stars.

  Twiga Stars ilitoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya Zimbabwe mchezo uliochezwa Harare, Yanga ikaifunga APR mjini Kigali 2-1, kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 jijini Dar es salaa, wakati Azam FC ilifunga Bidvest 3-0 Johanesburg na kuendeleza tena ushindi wa 4-3 Azam Complex Chamazi.

  Taifa Stars ikiwa mjini N’Djamena ilibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chad katika mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2017, Serenegti Boys ikiifunga The Pharaohs kutoka Misri katika michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa (2-1), (3-1) michezo iliyochezwa Uwanja wa Taifa na Azam Complex Chamazi.

  Mchezo wa tisa wa kimataifa, Yanga SC ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Ahly katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL), huku Azam FC ikiibuk na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Esperance ya Tunisia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC).

  TFF inawaomba wachezaji, viongozi, wadau na Mashabiki kuendelea kupigana kusaka ushindi katika michezo inayofuata na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ya nchi.

  0 0

  2
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Misitu wa Serikali ya Czech Republic Bw. Dusan Benza akizungumza katika kongamano la wafanyabiashara wa nchi hiyo na watanzania lililofanyika leo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
  Mawaziri wawili Kilimo na Viwanda wa Jamhuri ya Jamhuri ya Czech wakiongozana na wafanyabiashara zaidi ya thelathini wako nchini kwa ajili ya kutafuta na kujionea fursa za uwekezaji nchini Tanzaniam Mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja na Tanzania Investiment Bank (TIB), Ubalozi wa Szech Republic nchini Kenya na Tanzania House Of Business Company Limited (THB).
  Ujumbe huo metembelea wizara ya Kilimo na wizara ya Viwanda na Biashara na kusaini mikataba ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji hapa nchini na nchi ya Szech Republic ili kuunganisha masuala ya kibiasha na uwekezaji na kuwezesha wafanyabiashara wa nchi hizi kuwekeza katika masuala ya biashara, Teknolojia na Kilimo kwa ujumla.
  3
  Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic hapa nchini John Chaggama akizungumza na mmoja wa viongozi wa ujumbe huo huku Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa Czech akisikiliz kwa makini.
  4
  Injinia Michal Basovnik wa kampuni ya Impuls akitoa mada kuhusu shughuli mbalimbali zinazotolewa na kampuni yao ambayo ina tawi pia nchini Zambia.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. Marehemu Christina Lissu Mughwai, alifikwa na umauti mwishoni mwa wiki iliyopita, kutokana na Maradhi ya Kansa yaliyokuwa yakimsumbua.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisaini kitabu cha Maombolezo ya Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. 
   Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, Mh. Tundu Lissu, akisoma wasifu wa Marehemu, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake, leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. 
  Mtoto wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, akitoa taarifa fupi juu ya Mama yake.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimfariji Mtoto wa Christina Lissu Mughwai, mara baada ya kutoa taarifa ya Mama yake.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Aprili, 2016 ameungana na Ndugu, Jamaa na Marafiki kuuaga mwili wa Mbunge Mstaafu wa Mkoa wa Singida Marehemu Christina  Lissu Mughwai katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.

  Christina Lissu Mughwai aliyekuwa Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Singida katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, alifariki dunia tarehe 07 Aprili, 2016 katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es salaam, alikokuwa akipatiwa Matibabu.

  Pamoja na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Viongozi wengine waliohudhuria shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge Mheshimiwa Freeman Mbowe.

  Akitoa salamu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa George Simbachawene amewapa pole familia ya marehemu na kueleza kuwa katika kipindi chake cha ubunge Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai alitoa mkubwa kama mbunge na kama mtaalamu wa Uchumi.

  "Mheshimiwa Rais anatoa pole nyingine kwenu familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina" Amesema Mheshimiwa Simbachawene.
  Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai umesafirishwa leo kwenda kijiji cha Mahambe Mkoani Singida kwa Mazishi.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  12 April, 2016

  0 0

  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva akizunumza mara baada ya kukabidhi Pikipiki aina ya Boxer kwa wanakikundi cha polisi jamii cha mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.

  Amesema kuwa pikipiki hiyo ni ya mwanzo kwaajili ya kuwasaidia vijana wanaojitolea kulinda usalama wa mtaa huo.
   Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva akimkabidhi Kamanda wa Kikosi cha Polisi jamii cha Guard, Moksin Mwalimu pikipiki ya wanakikundi cha Polisi jamii kwaajili ya kuwasaidia katika kazi yao ya ulizi hasa wakati wa usiku.
  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva akimkabidhi ufunguo wa pikipiki ambayo ni msaada mkubwa kwao kwaajili ya ulizi wa mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam.

  Kamanda wa Kikosi cha Polisi jamii cha Guard, Moksin Mwalimu akipanda pikipiki kwaajili ya kuijaribu mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva jijini Dar es Salaam leo.

  MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva ni mfano wa kuigwa na jamii kwani ni kiongozi wa mtaa ambaye amesaidia jamii yake kwa kadiri ya uwezo wake.

  Mwenyekiti huyo ambaye ameweza kusaidia vijana katika mtaa wake leo amewakabidhi pikipiki aina ya boxer vijana  wa kikundi cha Polisi jamii katika mtaa huo jijini Dar es Salaam leo.

  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva amesema kuwa katika kutekeleza maagizo ya Serikali kuu ya kuimalisha ulinzi na usalama wa mitaa kupitia vikundi vya Polisi jamii.

  Ameyasema hayo mara baada ya kuwakabidhi Pikipiki aina ya Boxer  wanakikundi cha Polisi jamii cha mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuimarisha ulinzi wa maeneo yote ya mtaa huo.

  Lubuva ameishukuru serikali kwa kumuunga mkono katika kutekeleza majukumu yake kama kiongozi wa Serikali za Mtaa.

  Pia Lubuva amewaomba wananchi wa maeneo hayo pamoja na makampuni mbalimbali taasisi  mbalimbali za eneo hilo kuweza kusaidia vijana wa polisi jamii ili nao waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwasilisha bajeti ya ofisi yake wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Kupitisha Bajeti uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam Aprili 12, 2016.
  Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya kupitisha bajeti wakifuatilia bajeti ya ofisi hiyo walipokutana kuijadili na kuipitisha bajeti hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam Aprili 12, 2016.
  Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Issa Nchansi akifafanua jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya kupitisha bajeti kilichofanyika tarehe 12 Aprili, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Kupitisha Bajeti Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye ni mbunge wa Rufiji (katikati) akieleza jambo wakati wa kikao hicho walipokutana kujadili Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 12, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  I remember  the optimism with Tanzanians  when  the  Italian Oil company  (AGIP) , broke the news on Natural  gas discovery  In the songo songo field In 1974.

  Many had strong feeling  the new found resources wealth could transform their lives. And brought hope to a future generation.

  It’s  42 years now.  Tanzania’s petroleum resources have become a powerful magnet for foreign investors. And  we hear new gas discoveries  announcement  every now.
  The  question  lingered  in mind is how best to  manage such resources.  And  transform temporary  windfall into general  uplifting of the population.

  Experience  is the great teacher.

  In many African countries, natural resources have fueled violence and war instead of an opportunity for all.

  In Nigeria, for example,  Oil has resulted in violence in the  Niger delta. And despite the Oil wealth, Unemployment remains high. And poverty is still widespread .Surprisingly enough, 93 million Nigerians live in the households that  lack access to electricity.

  Natural resources have played important role in widening the gap between the rich and the poor in many  Africa’s  oil and gas rich countries
  The truth ought to know about  oil and gas
  The closer relationship between   chaos and  petroleum resources has led people to describe  that  oil and gas exploration and extraction projects are a curse.

  But Tanzania gas. Not a curse. Not  blessing. But is just an opportunity. And they can be used for adding value or  can ruin everything.

  In real life, oil and gas do not cause conflicts. But  violence  occurs  when the government is  very weak to withstand political and religious   pressure in peaceful dialogue.

  But petroleum resources  can amplify , accelerate and tearing apart  the already weaken  fabric.
  Tanzania’s gas and oil are simply an opportunity.  Tanzania’s gas means universal electricity.  Clean energy that does not pollute households. More business opportunities.  And more jobs especially amongst young people.

  History teaches us,  Many African citizens doubt  the  system.But to build confidence national oil company must remain sensitive to  citizen’s need as they continue to support  leadership that has signed  a regional contract.

  Most importantly , they must invest in a range of program that benefits, environment, local communities  and society as a whole.

  But the government  can’t resolve all such challenges on their own. Private sector and stakeholder must shoulder their responsibility
   In essence, It’s all our pleasure, Tanzania succeed. We all benefit when oil and gas   turn into a permanent  human breakthrough. And everybody gets fair deal.

  Hussein Boffu
  Graduate In Petroleum Geoscience
  Hussein.Boffu@gmail.com
  0655 37 65 43

  0 0

   SHIRIKA la Ndege la Etihad limepokea tuzo  ya  uzinduzi bora katika sekta ya usafiri wa ndege kwa mwaka 2016 kutoka kwenye jarida la kimataifa linaloongoza kwa makala za usafiri wa anga. Sherehe za tuzo hizo zilifanyika katika maonyesho ya ndege yaliyofanyika jijini Hamburg, nchini Ujerumani.

  Shirika lilijinyakulia tuzo hiyo kwa kuzingatia viwango vya juu vya teknolojia na maendeleo ya burudani inayotolewa ndani ya ndege (E-BOX) pamoja na mtandao wa mawasiliano (IFEC) zinazopatikana kwenye safari zake za kimataifa. Tuzo hii ni muedelezo wa tuzo ambazo shirika limekuwa linajinyakulia kwa mwaka uliopitia kupitia huduma zake bora za ndani ya ndege zikiwemo, tuzo ya shirika bora la ndege mwaka 2015 kutoka jarida la Inflight, tuzo ya uzinduzi bora mpya kwa shirika la ndege mwaka 2016 kutoka jarida la kimataifa la PAX kwa kanda ya mashariki ya kati, pamoja na tuzo ya shirika lenye huduma bora za burudani ndani ya ndege kutoka jarida la World Travel.

  Shane O'Hare, Makamu wa Rais kitengo cha Masoko wa Shirika la ndege Etihad, alisema: " Tuzo hii, iliyopigiwa kura na wasomaji wa jarida la kimataifa la PAX kwa kipindi cha miezi sita, ni utambuzi tosha juu ya dhamira ya shirika la ndege Etihad  kuhakikisha wageni wetu wanaendelea kufurahia burudani bora ndani ya ndege pamoja na mtandao thabiti wa mawasiliano ndani ya ndege zetu.”

  Shirika la ndege Ethihad linamiliki idadi kubwa ya ndege aina ya Airbus za kisasa pamoja na Boeing kubwa za kubeba abiria/mizigo kwa wingi na ndogo ze abiria/mizigo kidogo.

  Huduma ya Tv zenye kurusha matangazo na vipindi moja kwa moja  hupatikana kwenye ndege kubwa za Shirika la ndege, hii ni kuleta vipindi bora kutoka vituo saba ikiwa ni pamoja na BBC World News, Sport 24 na CNN, zikiwa zinaongoza kwa utazamajia, na CNBC, euronews , Japan NHK World Premium na Sky News Arabia.

  Shirika limetambulisha huduma mpya ya burudani ndani ya ndege ya E-BOX kwa ajili ya burudani binafsi kwa kutumia mfumo wa Panasonic eX3, na ndio shirika la kwanza kufunga huduma hiyo kwenye ndege aina ya Airbus A380. Ndege zote aina ya Airbus A380s na Boeing 787s  zitakuwa zimeunganishwa na mfumo huo wa burudani na vifaa vya Panasonic eX3. Mfumo huu hutoa mamia ya masaa ya burudani ya kutazamwa yenye muonekano mzuri, kwenye TV zenye ukubwa wa kuanzia inchi 11.1 kwa daraja la Uchumi, Inchi 18 kwa daraja la Biashara, Inchi 24 kwa daraja la Kwanza na Inci 32 kwa wanaotumia huduma ya “Makazi”.

  Huduma nyingine za burudani ni pamoja na kuimarishwa kwa ubora wa video, kuimarishwa kwa kioo cha kugusa cha TV, uwezo wa kufanya manunuzi kwenye TV pamoja na michezo ya video, huduma ya ramani na Graphical User Interface (GUI) kwa ajili ya abiria wenye umri mdogo.

  Shirika la ndege Etihad linaendelea kuleta bidhaa mpya zenye ubunifu ili kufikia malengo yake ya kubadilisha sekta ya usafiri wa anga. Tayari shirika linatoa huduma ya “Makazi” kwenye ndege zake aina ya Airbus A380, ina wahudumu binafsi waliobobea na kupata mafunzo kutoka hoteli ya Savoy yenye sifa kubwa Jijini London, wapishi wakuu kwenye daraja la Kwanza, mameneja wa vyakula na vinywaji kwenye daraja la Biashara, na wahudumu wa watoto waliohitimu kutoka chuo cha mfunzo cha Norland. Mkusanyika wa kumbi za mapumziko zinapatikana dunia nzima zikitoa huduma na vyakula kama vinavyopatikana kwenye hoteli kubwa duniani. Uwekezaji wa shirika la ndege Etihad kwenye burudani na mtandao wa mawasiliano kwenye ndege ni sehemu kubwa ya mipango yao katika kufikia mainduzi katika sekta ya usafiri wa anga.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Vishale Tanzania (TADA), Subira Waziri akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani leo jijini Dar es salaam kuhusu kuanza kwa mashindano ya Afrika mashariki  huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo kulia ni  Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bi. Redempta  Mwebesa.
   Makamu Mwenyekiti wa  Chama cha Mchezo wa Vishale Tanzania( TADA), Redempta  Mwebesa  (katikati) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani leo jijini Dar es salaam kuhusu kuanza kwa mashindano ya Afrika mashariki , wa kwanza kulia ni Katibu mkuu wa chama hicho Bi. Subira Waziri na wa kwanza kushoto ni Afisa Habari wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi Najaha Bakari.
  Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini mkutano ulioandaliwa na viongozi wa Chama cha Mchezo wa Vishale Tanzania( TADA) hawapo pichani kuzungumzia kuhusu kuanza kwa mashindano ya Afrika mashariki  yanayotarajiwa kuanza  April 29 mwaka huu.
  Picha na BMT.

  Na Mwandishi wetu- BMT
  MASHINDANO ya wazi ya Kitaifa na Kimataifa ya Shirikisho la Mchezo wa Vishale Afrika Mashariki yanatarajiwa kufanyika April 29 mpaka Mei Mosi jijini Dar es salaam, Tanzania ikiwa kama mwenyeji wa mashindano hayo.

  Mashindano hayo yanatarajiwa kujumuisha nchi za ukanda wa Afrika mashariki zikiwemo Tanzania kama mwenyeji, Kenya, Uganda, Burundi na Ruanda  huku Kenya ikiwa bingwa mtetezi wa michuano hiyo.

  Akizungumza hayo leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Vishale Tanzania (TADA) Bi. Subira Waziri amesema kuwa  Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazoshiriki michuano hiyo ikiwa na mategemeo makubwa ya ushindi.

  “Tuna matarajio ya kuibuka washindi katika michuano hiyo kutokana na kujiandaa vya kutosha kwa upande wa mazoezi ukizingatia kuwa tuna utayari na uzoefu wa mchezo huo” alisema Waziri.

  Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa TADA Bi. Redempta Mwebesi amesema kuwa licha ya mashindano hayo kuanza mwezi huu pia wana ukosefu wa Vifaa vya Michezo pamoja na gharama za kuweka kambi ili kujifua zaidi.

  Aidha Bi. Mwebesi ameongeza kuwa wana ukosefu wa pesa taslimu na vikombe vya kuwapa washindi kwa kuwa wanategemea viingilio kutoka kwa washiriki wa mashindano hayo.

  “Tunaomba wadhamini na wadau wa michezo wajitokeze kutusaidia kudhamini michuano hii  kwa kutupa vifaa na gharama za kukaa kambini ili tuweze kujifua zaidi na kurudisha heshima tuliyoipata mwaka 2014 kwa kuibuka washindi wa michuano hii” aliongeza Bi. Mwebesa.


  Pia Bi. Mwebesa ameongeza kuwa wana mikakati ya kuanzisha na kukuza mchezo huo kuanzia mashuleni , vijijini na Tanzania kwa ujumla ili kuweza kupanua na kuongeza ushindani wa mchezo huo nchini.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa Bw. Serge Prammertz wakati Bw. Serge alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 13,2016 kwa ajili ya kujitambulisha.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa Bw. Serge Prammertz wakati Bw. Serge alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 13,2016 kwa ajili ya kujitambulisha.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa Bw. Serge Prammertz wakati Bw. Serge alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 13,2016 kwa ajili ya kujitambulisha. (Picha na OMR)   . 

older | 1 | .... | 1182 | 1183 | (Page 1184) | 1185 | 1186 | .... | 3283 | newer