Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI WA TAASISI YA TAKUKURU PAMOJA NA HUNDI KIFANI YA SH. BILIONI 6 KUTOKA BUNGE BAADA YA KUBANA MATUMIZI

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameishika Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hundi Kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita kutoka kwa Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson mara baada ya Taasisi ya Bunge kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi yasio na Tija ili fedha hizo zikanunulie madawati kwa ajili ya wanafunzi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kulia, Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah pamoja na wafanyakazi wengine wa Bunge wakiwa wameishika hundi Kifani hiyo yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita. Rais Dkt. Magufuli ameipongeza Taasisi ya Bunge kutokana na hatua hiyo ya kubana matumizi na kuamua fedha zao zitumike katika kununulia madawati kwa ajili ya wanafunzi.


MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA BALOZI WA IRAN HAPA NCHINI. AKABIDHIWA CHETI NA WATU WENYE ULEMAVU

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Iran Nchini Tanzania Mhe. Mehd Aghajafari wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 11,2016, kwenye mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia suala la kukuza Ushirikiano kati ya Nchi mbili hizi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Cheti maalum kutoka kwa Muwakilishi wa Jumuiya ya Watu wenye ulemavu Nchini Bibi Stela Jailos kwa ajili ya kutambua mchango mkubwa wa Serikali ya awamu ya 5 kwa Watu wenye Ulemavu.(Picha na OMR)

SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI ASHIRIKI MKUTANO WA MASPIKA KUTOKA NCHI ZA SADC NCHINI MAURITIUS.

$
0
0
 Spika wa Bunge, Job Ndugai  akisalimiana na Spika wa Bunge la Lesotho Mhe. Nthloi Motsamai katika Mkutano wa Maspika kutoka Nchi Wanachama wa SADC unaendelea Nchini Mauritius. Ndugai ndiye Rais wa Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC Parliamentary Forum)
  Spika wa Bunge, Job Ndugai  akisalimiana na Spika Mstaafu wa Bunge la Zambia,  Amusaa Mwanamwambwa ambaye ni mmoja wa watoa mada katika  Mkutano wa Maspika kutoka Nchi Wanachama wa SADC unaendelea Nchini Mauritius katikati ni Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Umoja huo Dr. Essau Chiviya. Ndugai ndiye Rais wa Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC Parliamentary Forum) 
 Spika wa Bunge, Job Ndugai  akisalimiana na Spika Mstaafu wa Bunge la Zambia , Amusaa Mwanamwambwa ambaye ni mmoja wa watoa mada katika  Mkutano wa Maspika kutoka Nchi Wanachama wa SADC unaendelea Nchini Mauritius katikati ni Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Umoja huo Dr. Essau Chiviya. Mhe. Ndugai ndiye Rais wa Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC Parliamentary Forum) 

DKT. SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KIKAO CHA BARAZA LA MAPINDUZI LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi (BLM) mara baada ya kuwaapisha Viongozi hao hapo jana, kikao kilichofanyika leo kiliwajumuisha Mawaziri pamoja na Naibu Mawaziri wote wa wizara 13 katika ukumbi wa Baraza hilo Ikulu Mjini Unguja.Picha na Ikulu.

EAC-USAID REGIONAL TRADE AND FEED THE FUTURE COORDINATION CONFERENCE OPENS IN ARUSHA

$
0
0
The East African Community (EAC) Secretary General, Amb. Dr. Richard Sezibera, today officially opened a two-day Regional Trade and Feed the Future Coordination Conference organized by the United States Agency for International Development (USAID) and the EAC.

The two day conference, which is taking place at the Kibo Palace Hotel in Arusha, Tanzania is aimed at enhancing collaboration and information sharing among USAID missions and Partners to improve integration, innovation and scaling up of results, will focus on the implementation of policy priorities and sharing lessons learned from across the region and initiatives.

Amb. Dr. Richard Sezibera said that the EAC and US government have built and sustained a mutual and strategic partnership dating back to the EAC’s inception.

"The partnership continues to grow from strength to strength through common development objectives and funding for various programs including trade and investment, agriculture, environment, Health and institutional support," said Dr Sezibera.

"I wish to acknowledge and appreciate the tremendous contribution and investments that USAID has made in advancing regional integration particularly in the EAC Region," he added.

The Secretary General disclosed that in 2015, the EAC concluded a Cooperation Agreement on Trade Facilitation, Sanitary and Phytosanitary Measures (SPS), and Technical Barriers to Trade (TBT), adding that the implementation of the agreement would strengthen the capacities and enhance competitiveness of the EAC Partner States in areas of trade and agricultural development.

On his part, the USAID/Kenya and East Africa/Regional Economic Integration Office Director, Mr. Matthew Rees, hailed the efforts that the Community has made in implementing policy priorities, adding that this has promoted prosperity in the region.

Present at the conference were USAID mission staff, representatives from other US Government Agencies (USDA), implementing partners as well as officials from the Partner States.
The EAC Secretary General, Amb. Dr. Richard Sezibera make his remarks during the official opening session as Mr. Matthew Rees, USAID/Kenya and East Africa/Regional Economic Integration Office Director looks on.
USAID/Kenya and East Africa/Regional Economic Integration Office Director, Mr. Matthew Rees welcomes Dr Sezibera to the high table.

Airtel yaleta 'Jipimie Yatosha Yako' kutoa uhuru zaidi vifurushi vya Yatosha

$
0
0
Airtel Tanzania ili kutoa uhuru zaidi kwa wateja wake imetangaza kifurushi kipya kupitia huduma yake ya vifurushi vya  Airtel Yatosha kijulikanancho kama Airtel Jipimie Yatosha Yako itakayowapa wateja wake faida kubwa na uwezo wa kuweza kupanga na kuunda kifurushi wanachokitaka kutokana na chaguo na mahitaji yake .

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Airtel Bi, Anethy Muga  alisema "Jiunge sasa na Airtel ufurahie Uhuru huu mpya, Tumezindua " Airtel Jipimie Yatosha Yako " kwa ajili ya kuwapatia wateja wetu uhuru wa kuchagua na  kupanga matumizi yao na papo hapo kuunda kifurushi  kitakachoweza kukidhi mahitaji yao  ya kiuchumi na kijamii.

Airtel Jipimie Yatosha Yako "ni moja ya kifurushi cha kibunifu zaidi ambacho na kinapatikana kwa wateja wetu wote hapa nchini ambapo unaweza kupata kifurushi hiki upendavyo wewe yaani kwa siku, wiki, na  hata mwezi.

“Airte daima tunafanyia bidhaa zetu zote utafiti  na kuziunda kwa mujibu wa kile wateja wetu wanataka ili kuleta unafuu na ubora zaidi, kwa mara ya kwanza nchini Tanzania wateja wa simu za mkononi wa Airtel wataweza kuamua kununua vifurushi vya gharama nafuu na watakavyo vya hadi shilingi  500 huku wakijipimia muda wa maongezi tu, au changanya na MB zaidi au unajichaguali Muda wa maongezi na SMS au kujipimia vyote yaani Muda wa maongezi Zaidi, MB zaidi na SMS Zaidi, uhuru ni wako kujipimia utakavyo” na sasa ndio wakati wa kujiunga na Airte.

Airtel inaamini ubunifu wa huduma ya “Jipimie Yatosha Yako" itakuwa suluhisho la mawasiliano kwa wengi na msaada kwa wale ambao walitaka kifurushi kutokana na hitaji lake. Sasa wateja wa Airtel wanauwezo wa kutengeneza Yatosha yao wao wenyewe  na kutimiza mahitaji yao .

Kujiunga na kifurushi cha Yatosha na kufurahia Jipimie Yatosha Yako, wateja wanatakiwa kupiga  namba *149*99# na kuchagua namba 5 ‘Jipimie Yatosha Yako’ na kutengeneza kifurushi cha chaguo lake.

Huduma mpya ya uhuru wa kujipimia Vifurushi vya Yatosha imezinduliwa na kusindikizwa na wasanii wa  kundi la Navy kenzo linaloundwa na Nahreel na Haika ambao wataitambulisha sehemu mbalimbali nchini
“Sisi tuko tayari kama kawaida kuja kujipimia yatosha kila mahali, sasa na nyie kuweni tayari kukamatia chini Yatosha yako inayokutosha" alisema Nahreel wa Navy Kenzo.

TIZA YA JOTO LA ASUBUHI JUMANNE APRIL 12

BREAKING NYUZZZZZ....: RAIS DKT. MAGUFULI AMWACHISHA KAZI MKUU WA MKOA WA SHINYANGA MAMA ANNE KILANGO MALECELA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, mchana huu ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mama Anna Kilango Malecella, kwa kubaini kuwa alimwambia uwongo kuwa Mkoa wake hauna wafanyakazi hewa wakati kumbe wapo wengi tu.

Rais Magufuli amesema kwamba hakuamini kwamba kuna mkoa ambao hauna wafanyakazi hewa, hivyo akatuma kikosi kazi ambacho hadi usiku wa kuamkia leo kimebaini kuweko na wafanyakazi hewa 45 mkoani Shinyanya.

Rais Magufuli, ambaye alikuwa anaongea baada ya kupokea Ripoti ya TAKUKURU  toka kwa Mkurugenzi wake Mkuu  Valentino Mlowola,  amesema kasikitishwa sana na kauli ya Mama Malecela ambaye bila shaka alikuwa amepata ushauri mbaya toka kwa watendaji wake. 

Amesema idadi hiyo ya wafanyakazi hewa mkoani Shinyanga huenda ikaongezeka zaidi kwani wilaya mbili zilikuwa bado zinaendela kuhakikiwa.
Rais Magufuli amesema pia kwamba hadi jana jumla ya wafanyakazi hewa zaidi ya 5, 507 wamebainika nchi nzima, wengi wao wakitoka katika halmashauri.

Hivyo Rais pia ametengua uteuzi wa  Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul R. Dachi kwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa.
Mama Anna Kilango Malecela, ambaye katika awamu ya nne alikuwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi na Mbunge wa Same Mashairiki, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kuachishwa kazi. Wakuu wa mikoa waliapishwa mwezi uliopita.

Katika siku hiyo Rais aliwapa wakurugenzi wa halmashauri siku 15 wawatoe katika Orodha ya Malipo ya Mshahara (Pay Roll) wafanyakazi hewa wote katika halmashauri zote nchini, na kuwataka wakuu wa Mikoa hao wasimamie zoezi hilo kwa ukamilifu. 

Vile vile Rais Magufuli alionya kuwa halmashauri yoyote baada ya muda huo itakayokuwa na mfanyakazi hewa, mkurugenzi wake atakuwa amejifuta kazi mwenyewe.Vilevile Rais amewaagiza mawaziri wote kuwaeleza watendaji wao wawaondoe wafanyakazi hewa wote ndani ya kipindi hicho cha siku 15 na kubainisha kuwa watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo watafukuzwa kazi kwani sheria ni msumeno.

BASILLA MWANUKUZI FOUNDATION YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR

Waandishi wa habari waaswa kujiendeleza kuelimu

$
0
0
Waandishi wa habari wameaswa kujiendeleza kielimu katika fani ya uandishi wa habari na taaluma nyingine ili waweze kukabiliana na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.
 
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mhadhiri Chuo Kikuu Huria Dr. Hamza Kondo alipokuwa akizindua kitabu chake kiitwacho Watchdog Journalism in Tanzania a Sustainable Struggle ambapo kwa Kiswahili ni “Uandishi Habari Huru Tanzania ni mapambano endelevu”.
 
Dr Kondo amesema lengo la kitabu hicho ni kuwaelimisha na kuwaasa waandishi wa habari na wataaluma ya habari kuzidi kuithamini taaluma hiyo licha ya changamoto zinazowakabili.Amesema kitabu hicho kinazungumzia uhalisia wa uhuru wa habari nchini, hivyo kinafaa kufundishia taaluma ya habari katika vyuo vikuu na vyuo vya kati nchini.
 
Aidha, Mhadhiri huyo ameongeza kuwa ili fani ya taaluma ya habari iheshimike ni lazima iwe na bodi ya wataalamu waliobobea ambayo itaundwa na wasomi wa taaluma husika ili kusimamia maadili ya taaluma hiyo na kuchukua hatua kwa wanataaluma watakaokiuka maadili.
 
Mbali na hayo Dr Kondo ametoa zawadi ya vitabu kwa baadhi ya vyombo vya habari nchini likiwemo gazeti la Jamuhuri, gazeti la majira, gazeti la Habari Leo, gazeti la Mwananchi na gazeti la Nipashe.
 
Na Beatrice Lyimo - MAELEZO

 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA MFUMO WA KIELEKRONIKI WA BENKI YA NMB WA KUKUSANYA MAPATO YA SERIKALI

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – Kassim Majaliwa na Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker wakifunua bango la NMB kuashiria uzinduzi rasmi wa mfumo wa kielektroniki wa NMB wa ukusanyaji mapato ya serikali kupitia halmashauri. Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti mpya wa ALAT – Gulamhafeez Mukadam, Mkamu Mwenyekiti wa ALAT – Stephen Mhapa na Abdulmajid Nsekela – Afisa Mkuu wa wateja wadogo wa NMB. 


Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – Kassim Majaliwa na Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker wakiangalia bango lililozinduliwa na Mh Waziri Mkuu kwaajili ya mfumo mpya wa ukusanyaji mapato ya halmashauri kwa njia ya kielektroniki kupitia NMB. Kondi mbalimbali ndani ya halmashauri zitakuwa zinalipwa kupitia NMB Mobile, Matawi ya NMB na NMB Wakala. Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti mpya wa ALAT – Gulamhafeez Mukadam, Mkamu Mwenyekiti wa ALAT – Stephen Mhapa na Abdulmajid Nsekela – Afisa Mkuu wa wateja wadogo wa NMB.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – Kassim Majaliwa akimpongeza Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker kwa hatua iliyofikiwa na benki hiyo ya kuanza rasmi ukusanyaji wa mapato ya halmashauri kwa njia ya kielektroniki kupitia NMB. Kondi mbalimbali ndani ya halmashauri zitakuwa zinalipwa kupitia NMB Mobile, Matawi ya NMB na NMB Wakala. Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti mpya wa ALAT – Gulamhafeez Mukadam, Mkamu Mwenyekiti wa ALAT – Stephen Mhapa na Abdulmajid Nsekela – Afisa Mkuu wa wateja wadogo wa NMB.

WAZIRI MAKAMBA ATEMBELEWA NA BALOZI WA IRELAND

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwa na balozi wa Ireland Bi. Fionnuala Gilsenan aliyemtembelea Ofisini kwake leo mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.

Timu ya Uchukuzi SC IKIJONOA VIKALI KWA MASHINDANO YA MEI MOSI

$
0
0
 Wachezaji wa timu ya netiboli ya Uchukuzi Sports Club, Grace Mwasote (kushoto mwenye mpira) akizuiwa na Johari William wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Bandari, Kurasini mwishoni mwa wiki. Timu hiyo inajiandaa kwa mashindano ya Mei Mosi yatakayofanyika mjini Dodoma.
 Grace Mwasote akiwa na mpira akiangalia jinsi ya kuwatoka wachezaji wenzake wa timu ya netiboli ya Uchukuzi Sports Club. Wengine pichani ni Johari William (kushoto) na Maimuna Ayelo.
 Matalena Mhagama mfungaji mkongwe pia wa timu  ya Taifa ya netiboli(kushoto), akizuiwa na Sharifa Mustafa (kulia) huku Mary Kajigili (kushoto nyuma),akiangalia.
Maimuna Ayelo (kushoto) akidaka mpira huku Subira Jumanne akijiandaa kumzuia katika mazoezi ya timu ya netiboli ya Uchukuzi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bandari Kurasini, wakijiandaa na mashindano ya Mei Mosi.Imetolewa na kitengo cha Sheria na Mahusiano - TAA

MBUNGE WA KALIUA, TABORA MHE. SAKAYA ATOA WITO KWA SERIKALI KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA WATU NCHINI

SIGNING CEREMONY OF THE TREATY OF ACCESSION OF THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN INTO THE EAST AFRICAN COMMUNITY

$
0
0


SIGNING CEREMONY OF THE TREATY OF ACCESSION OF THE REPUBLIC OF

SOUTH SUDAN INTO THE EAST AFRICAN COMMUNITY.
East African Community Headquarters, Arusha, Tanzania: April 12, 2016: His Excellencies Presidents Salva Kiir Mayardit of the Republic of South Sudan and Dr. John Pombe Joseph Magufuli, of the United Republic of Tanzania and the Chairperson of the East African Community Heads of State Summit are scheduled to sign the Treaty of Accession of the Republic of South Sudan into the East African Community (EAC) on Friday 15th April 2016 in Dar es Salaam, Tanzania.

At their 17th Ordinary Summit held on 2nd March, 2016 in Arusha, Tanzania, the EAC Heads of State received the report of the Council of Ministers on the negotiations for the admission of the Republic of South Sudan into the Community and decided to admit the Republic of South Sudan as a new member.

The Summit then designated the Chairperson, His Excellency President Dr. John Pombe Joseph Magufuli of The United Republic of Tanzania, to sign the Treaty of Accession with the Republic of South Sudan.

WASHTAKIWA WA TUMBILI WASOTEA DHAMANA

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

HATMA ya dhamana kwa washtakiwa saba wa makosa ya uhujumu uchumi wakiwamo wafanyabiashara raia wa Uholanzi waliokamatwa Machi 23 mwaka huu wakijaribu kusafirisha wanyama hai 61 aina ya Tumbili sasa kujulikana Alhamisi (Aprili 14).

Uamuzi huo umetolewa jana na Jaji wa mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Moshi ,Aishiel Sumari wakati akitoa uamuzi mdogo juu ya hoja zilizotolewa na upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Majura Magafu dhidi ya upande wa Jamhuri kuhusu maombi ya dhamana kwa washtakiwa.
 
Hoja za upande wa utetezi zilitokana na upande wa Jamhuri kuwasilisha mahakamani hapo hati zuio la dhamana kwa washtakiwa wote saba iliyotoka kwa mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP).

Maombi matatu ya dhamana yaliwasilishwa mahakamani hapo ambayo ni ombi la tatu la raia wa Uholanzi ,Artem Vardanian ,Eduard Vardanyan na Idd Misanya ,ombi nne la ,Nyangabo Musika,Martina Nyakanga na Very Anthon huku ombi la tano lilikuwa ni la aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa idara ya wanyamapori nchini Dkt Charles Mulokozi.

Baada ya maombi hayo kuwasilishwa upande wa utetezi uliridhia kuunganishwa kwa maombi hayo ili kuokoa muda wa mahakama katika kusikiliza shauri hilo baada ya maombi hayo kufanana.Akitoa uamuzi huo Jaji Sumari aliuelekeza upande wa jamhuri kupitia kwa wanasheria wa Serikali Wankyo Simon na Robart Rogart kutumia siku ya leo (Jumanne) kuwasilisha hoja kinzani na kwamba upande wa utetezi utawasilisha maombi yao kesho (Jumatano) baada ya kujibiwa na upande wa pili.
Baadhi ya Washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi ya usafirishaji wa wanyama Hai 61 aina ya Tumbili wakiongozwa na asakari Polisi walipokuwa wakiwasili katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Moshi.
Washtakiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili raia wa Uholanzi ,Artem Vardanian na ndugu yake Eduard Vardanyan wakisindikizwa na askari Polisi kuingia mahakamani,Nyuma yao ni mshtakiwa mwingine Idd Misanya . Washtakiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili raia wa Uholanzi ,Artem Vardanian na ndugu yake Eduard Vardanyan wakiwa katika viunga vya mahakama kuu kanda ya Moshi ,kulia ni aliyekua Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt Charles Mulokozi. 

BEI YA MADAFU LEO.

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA UJUMBE WA KAMATI YA FEDHA YA BUNGE LA FINLAND.

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano na Mazingira) January Makamba akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wabunge la Finland. Wabunge hao wa Kamati ya Fedha wamefanya mazungumzo na Waziri Makamba hii leo Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli, Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Finland Nchini Tanzania Bw  Mart Akhtsary (kushoto) akitambulisha ujumbe wake.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba hii leo amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Kamati ya Fedha ya Bunge la Finland. 

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Luthuli Dar es Salaam, wabunge hao wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada inazofanya za kulinda na kuhifadhi mazingira.

Awali, akiwakaribisha wabunge hao Waziri Makamba amesema Tanzania inajivunia uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Finland na kuwashukuru  wabunge hao kwa kufanya ziara hiyo ya kikazi nchini Tanzania.

Waziri Makamba amesema Serikali ya awamu ya Tano imejikita zaidi katika kuimarisha Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ikiwa ni pamoja na kuandaa Mkakati Mkubwa wa Kitaifa wa kupanda miti nchi nzima hususan maeneo kame ili kunusuru nchi na athari za mabadiliko ya Tabianchi.

“Hivi sasa tuko katika hatua za kuainisha maeneo yatakayopandwa miti hiyo kwa kuangalia aina za udongo na miti itakayoweza kuhimili katika maeneo husika” Alisisitiza Makamba.

Waziri Makamba ameiomba Serikali ya Finland kuendelea kushirikiana zaidi na Serikali ya Tanzania ili kufikia malengo endelevu ya Uchumi na maendeleo ya Viwanda bila kuathiri Mazingira.


Naye Balozi wa Finland Nchini Tanzania Bw Mart Akhtsary aliyeambatana na ujumbe wa wabunge kutoka Finland amemhakikishia Waziri Makamba kuendeleza na kudumisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

FAO JIPYA LA WOTE SCHEME LA PPF LITASAIDIA KUKUZA UCHUMI WA WATANZANIA.

$
0
0
Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa akizungumza wakati wa semina hiyo.

Fao jipya la Wote Scheme ambalo ni mfumo wa hiari kwa wanachama ulioanzishwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF utasaidia kuwapa fursa watanzania waliopo kwenye sekta isiyo rasmi kukidhi mahitaji na kutambua mchango na ushiriki wa sekta hizo katika kukuza uchumi.

Fao hilo pia linatoa fursa kwa wafanyakazi waliopo kwenye sekta iliyo rasmi kuwawezesha kunufaika na mfumo huo kwa ajili ya kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa alisema hayo juzi wakati semina kwa askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Zimamoto mkoani Tanga uliokuwa na lengo la kuwapa uelewa juu ya mafao yanayopatikana kupitia mfuko huo.
Washiriki wa semina hiyo Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa.

Alisema kupitia fao hilo mwanachama anafaidika na huduma za Afya ikiwemo kupata kadi ya Afya mahali popote kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) mwaka mzima bure.

Aidha alisema kupitia skimu hiyo mpya ya mfuko huo unachangia na kuwapa uelewa watanzania utamaduni wa kujiwekea akiba ya baadae ili kuweza kukabiliana na ugumu wa maisha wakati wanapokuwa wakifikia umri wa kustaafu.

“Lakini pia sisi kama PPF tunarahisisha uchangiaji kupitia mitandao yote ya simu kwani hii imesaidia kuweza kuepusha changamoto mbalimbali ambazo wanaweza wakukumbana nazo wanachama wetu ambao wamejiunga ma Mfuko huu “Alisema.

Hata hivyo alisema kuwa wanaendelea kutoa mikopo ya elimu na biashara ili kuweza kuwainua wanachama wao kiuchumi sambamba na kujiendeleza kielimu ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha na utandawazi.
“Fao hili lilianzishwa mwezi wa saba mwaka jana ambapo mwanachama anafaidika na huduma za afya (Kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini - NHIF),mikopo mbalimbali na Fao la Uzeeni(Pensheni) "Alisema Meneja huyo.

Semina hiyo ililenga kuwapa uelewa wa mambo mbalimbali kuhusu mfuko huo ikiwemo uandikishaji wanachama,mafao yatolewayo na mfuko huo,Wote Scheme (mfumo wa Hiari),Mikopo ya Saccos na Fao la Elimu.
Picha na Stori kwa Hisani ya blog ya Kijamii ya Tanga Raha

MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU AZINDUA KONGAMANO LA WANAWAKE KATIKA UONGOZI LEO.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mhe. Zakia Meghji alipowasili ukumbi wa Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kuzindua Kongamano la Wanawake katika Uongozi linalojadili kuendeleza Mazingira kuwezesha kuinua Wanawake ambao bado hawajapata fursa kufikia nafasi za Uongozi. Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi limefanyika leo April 12, 2016.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Kongamano la Wanawake katika Uongozi linalojadili kuendeleza Mazingira kuwezesha kuinua Wanawake ambao bado hawajapata fursa kufikia nafasi za Uongozi. Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi limefanyika leo April 12, 2016 katika ukumbi wa Mwalim Nyerere. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake waliohudhuria Kongamano la Wanawake katika Uongozi linalojadili kuendeleza Mazingira kuwezesha kuinua Wanawake ambao bado hawajapata fursa kufikia nafasi za Uongozi. Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi limefanyika leo April 12, 2016 katika ukumbi wa Mwalim Nyerere. 
(Picha na OMR)
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images