Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1171 | 1172 | (Page 1173) | 1174 | 1175 | .... | 3348 | newer

  0 0


  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la wawakilishi Dr.Shein aapishwa kuongoza kipindi cha 2 huku akiahidi mabadiliko makubwa. https://youtu.be/JMpvDsQsTcQ

  Hatimaye zoezi la kubomoa jengo la ghorofa 16 lilijengwa kinyume cha sheria lililoko Manispaa ya Ilala lakamilika kabla ya wakati huku likikamilika bila madhara yeyote.https://youtu.be/javHgG-rBBI  

  Rais John Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia ikulu jijini Dar es salaam. https://youtu.be/plB-sT1WS54  

  Wakazi wa kijiji cha Msimbati viliko visima vya gesi mkoani Mtwara wazuia kwa muda msafara wa kamati ya bunge ya nishati na madini wakilalamikia kutonufaika na uwepo wa gesi uliopo kwenye maeneo yao. https://youtu.be/bVaQVnj5v7c  

  Waziri wa mali asili na utalii Jumanne Maghembe atumbua majipu kadhaa kwa tuhuma za kuisababishia serikali hasara. https://youtu.be/bqdvb0ajXeY  

  Rais wa Zanzibar aapishwa hii leo kutumikia kipindi kingine cha miaka 5 huku akiahidi kufanya kazi kwa maslahi ya wananchi wote. https://youtu.be/_O2FqStivBQ  

  Askofu mkuu wa jimbo kuu Katoliki jijini Mwanza awapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kumaliza salama uchaguzi wa marudio wa Zanzibar huku akiwasihi kuondoa tofauti zao. https://youtu.be/G7YkHrGv0Mc

  Jeshi la polisi Mkoani Kilimanjaro linawashikilia raia wawili wa Uholanzi kwa tuhuma za kutaka kusafirisha tumbili 61 kwenda nchini Armenia.  https://youtu.be/JS9KiKxeJ_k  

  Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF washauriwa kubuni njia mbadala katika kusaidia kaya maskini badala ya kuendelea na mfumo uliopo hivi sasa wa uhawilishaji wa fedha.https://youtu.be/b0JTqhgt2LI  

  Timu ya Azam Fc imeingia kambini kujiandaa na michezo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa huku ikibainisha matumaini ya kutwaa ubingwa. http://simu.tv/kFrJ33S  

  Baada ya Taifa Stars kuibuka na ushindi dhidi ya Chad wadau mbalimbali watoa maoni yao juu ya mwenendo na molari ya timu hiyo. http://simu.tv/MvIYBaC  

  Klabu ya Leicester City imeanza kuchanja mbunga kimataifa baada ya kupangiwa kutifuana na vilabu vikubwa ikiwemo Barcelona na PSG. http://simu.tv/NJpLODo


  0 0


  0 0

  Mkurugenzi na Muasisi wa Shule Direct, Faraja Kotta Nyalandu akitoa hotuba wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo mpya wa kujifunza kupitia simu za mkononi mahususi kwa wanafunzi wa Sekondari ufahamikao kama MAKINI SMS. Kupitia mfumo huo, wanafunzi wa Sekondari wanaweza kujipima kupitia maswali; kupata masomo yaliyofupishwa kwa matumizi ya meseji (SMS); kumuuliza mwalimu mtaalamu wa masomo mbalimbali ‘Ticha Kidevu’; kutumia Wikipedia na kutumia ‘search’ kutafuta na kupata mada wanayohitaji moja kwa moja. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni, Jijini Dar es salaam.
  Sasa ni uzinduzi wa MAKINI SMS.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano, Iku Lazaro na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Shule Direct. Fatma Said, wakifurahia jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo mpya wa kujifunza kupitia simu za mkononi mahususi kwa wanafunzi wa Sekondari ufahamikao kama MAKINI SMS, uliofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam.


  0 0


  Wataalamu wa ujenzi wa daraja la Kigamboni wakisalimiana na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.
  Barabara za kuingilia darajani upande wa Kurasini.
  Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo akionyesha njia za kuingia na kutoka darajani
  Barabara ya kuingilia darajani upande wa kushoto na barabara ya kutokea mjini upande wa kulia. 
  Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara  (wa tatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa wahandisi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni wakati wa ziara yake ya kutembelea daraja la Kigamboni. 

  0 0

  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amewasili Dubai akitokea Tunisia kushiriki Mkutano wa 8 wa Nchi Majirani wa Libya na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mheshimiwa Reem Ebrahim  Al-Hashimy alipomtembelea katika ofisi yake jijini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
  Amefanya mazungumzo hayo leo yenye lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa wa Libya. Mkutano huo ni muendelezo wa utekelezaji wa hadidu za rejea za AU zinazomtaka Mwakilishi Maalum kukutana na wadau wote wa Libya kwa  lengo la kutafuta majawabu ya kudumu ya mgogoro huo. Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ni moja ya nchi zinazoshiriki katika utafutaji wa utatuzo wa mgogoro huo na mwanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab Legue).
  Katika mazungumzo hayo, Mwakilishi Maalum wa AU amemuelezea  Waziri Reem mtazamo na dhamira ya AU katika kutafuta suluhisho la kudumu la mgogoro wa Libya. Amemjulisha jitihada ambazo amechukua toka kuteuliwa kwake kushika nafasi hiyo ikiwemo kukutana na viongozi wa Serikali ya Muafaka wa Kitaifa ya Libya,wadau wa siasa wa ndani ya Libya na wadau  wengine wa siasa wa ndani na nje ya Libya. Amemuelezea pia utayari wa AU kushirikiana na UAE na wadau wengine ili kuwa na sauti moja ya kushawishi pande zote za mgogoro wa Libya kuheshimu na kutekeleza Makubaliano ya Kisiasa ya Libya (Libya Political Agreement) yaliyosainiwa tarehe 17 Desemba, 2015 huko Shkirat, Morocco.  Makubaliano hayo yanahusisha pamoja na mambo mengine Bunge kuidhinisha muundo wa Baraza la Mawaziri na kuhamishia shughuli za Serikali makao makuu ya nchi hiyo jijini Tripoli.
  Kwa upande wake, Waziri Reem amempongeza Rais Mstaafu Kikwete kwa kuteuliwa kwake kuwa Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro huo. Amemuelezea Rais Mstaafu Kikwete kuwa ni kiongozi mwenye uzoefu mkubwa wa uongozi na utatuzi wa migogoro barani Afrika. Amemueleza kuwa UAE ingependa kuona mgogoro huo unapatiwa ufumbuzi haraka ili kurejesha hali ya usalama na kuwaondolea madhila wananchi wa Libya hususan wanawake na watoto. Amemhakikishia ushirikiano wake binafsi na wa Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu katika kufanikisha wajibu wake huo.
  Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika (AU) katika Utatuzi wa Mgogoro wa Libya amekutana na Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mheshimiwa Reem Ebrahim  Al-Hashimy alipomtembelea katika ofisi yake jijini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
   Mwakilishi Maalum wa AU kwa Libya Dkt Jakaya Kikwete akizungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Mheshimiwa Nabeer Al-Arabi jijini Tunis
   Mwakilishi Maalum wa AU kwa Libya katika mazungumzo na Makamu Mwenyekiti (Makamu wa Rais) wa Baraza la Utawala la Libya Mhe. Mousa El-Kouni jijini Tunis
   Mwakilishi Maalum wa AU kwa Libya Dkt. Jakaya Kikwete katika mazungumzo na Naibu wa Kwanza wa Spika wa Bunge la Libya Mhe. Emhemed Shoaib jijini Tunis
   Mwakilishi Maalum wa AU kwa Libya Dkt. Kikwete akiagana na Mwenyekiti (Rais) wa Barza la Utawala la Libya Mheshimiwa Fayez Al-Sarraj  baada y akufanya nae mazungumzo jijini Tunis
  Mwakilishi Maalum wa AU kwa Libya Dkt.  Jakaya Kikwete akatika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ofisi ya Uwakilishi ya AU kwa Libya alipotembelea ofisi zake za muda jijini Tunis

  0 0

  Wanafunzi wa Feza Boys High School kutoka jijini Dar es Salaam wakipata picha ya pamoja walipokua Virginia International University iliyopo jimbo la Virginia siku ya Alhamisi March 24, 2016, wanafunzi hao wapo kwa ziara maalum ya kuangalia uwezekano wa kujiunga na chuo hicho katika masomo ya juu.
   Makamu Rais wa Chuo hicho Dr. Suleyman Bahceci (kulia) akiwaeleza wanafunzi hao taratibu za kufuata kwa ajili ya kujiunga na VIU
  Kushoto ni Alex Luketa Mtanzania anayefanyakazi chuoni hapo kwa ajili ya kusajili wanafunzi kutoka Afrika Mashariki akiwa pamoja na wanafunzi wa Feza Boys High School wakimsikiliza Makamu Rais wa chuo (hayupo pichani) alipokua akielezea wanafunzi hao utaratibu wa kujiunga na masomo VIU.

  0 0

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .


  VYOMBO vya ulinzi na usalama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) vimefanikiwa kuwanasa wafanyabiashara wawili ndugu, raia wa Uholanzi wakiwa katika harakati ya kusafirisha wanyama Hai 61,aina ya Tumbili kuelekea nchini  Armenia.


  Wanyama hao wakiwa kwenye makasha sita tofauti ya kuhifadhia wanyama walikuwa wasafirishwe kwa ndege maalumu ya mizigo yenye namba EW/364G iliyosajiliwa nchini Belarus kupitia kampuni ya Arusha Freight Limited ya jijini Arusha.


  Raia hao wa Uholanzi waliokamatwa juzi majira ya saa 1:30 jioni katika uwanja wa ndege wa KIA wametambulika majina yao kuwa ni Arten Vardanian (52) aliyekuwa na hati ya kusafiria yenye namba NWF8CKJR8  na Edward Vardanian (46) aliyekuwa na hati ya kusafiria namba NY969P96.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa akiwa ofisini kwake muda mfupi kabla ya kuzungumza na wanahabari.


  Meneja usalama uwanja wa ndege KIA,Kisusi Justine aliliambia Tanzania Daima mbali na kukamatwa kwa raia hao wa kigeni pia walifanikiwa kumshikilia Mtanzania ,Idd Misanya anayedaiwa kuwauzia wanyama hao.


  “Wahusika hawa wawili walifika eneo la Cargo ambako walikuwa katika harakati za kusafirisha wanyama hao ndipo tulipowashikilia kwa sababu taratibu za kusafirisha wanyama Hai zilikiukwa”alisema Justine.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara akisalimiana na Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF, Yacoub Kidula.
  Wataalamu wa ujenzi wa daraja la Kigamboni wakisalimiana na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.
  Barabara za kuingilia darajani upande wa Kurasini.
  Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo akionyesha njia za kuingia na kutoka darajani.


  0 0

  NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

  WATU wanaosumbuliwa na maradhi ya Moyo mkoani Kigoma, watapata faraja kubwa mapema Aprili 4 hadi 9, 2016, kufuatia uwepo wa huduma za uchunguzi wa maradhi hayo utakaofanywa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo, Dkt. Stephan P. Masatu, kutoka jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam, Dkt. Masatu alisema, huduma zote za magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na vipimo vya ECG na ECHO zitatolewa kuanzia asubuhi kwenye hospitali ya kibinafsi ya Upendo iliyo jirani na soko kuu la mkoani Kigoma.

  Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa iliyo pembezoni mwa nchi na zinakabiliwa na upungufu wa wataalamu wa kushughulikia magonjwa kama ya Moyo na kutokana na uchache wa wataalamu hao, itakuwa ni nafasi nzuri kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na vitongoji vyake, kujitokeza ili kuhudumiwa ambapo kliniki hiyo itadumu kwa muda wa siku sita mfululizo.
  Dkt. Masatu akitumia mashine ya kupima ECHO, mmoja wa wagonjwa wa moyo.

  DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo, Dkt. Stephan P. Masatu

  0 0


   The 4th High-Level Dialogue of the EAC Partnership Fund was held on Wednesday, March 25, 2016 in Dar es Salaam Tanzania. The dialogue  was attended by Heads of Diplomatic missions accredited to the EAC and also members the EAC Partnership Fund.

  The dialogue  was co-chaired by the Norwegian Ambassador, H.E. Hanne Kaarstad and the EAC Secretary General Amb.  Dr Richard Sezibera.

  Addressing the Heads of Diplomatic missions, the Secretary General of the East African Community Amb. Dr Richard Sezibera expressed his appreciation for the support he has received from the development partners and noted that for the EAC Partnership Fund was more than monetary support. “The Partnership Fund is a forum for dialogue, creates avenues for discussing key integration issues and mobilizing political support for EAC regional integration”, added Dr Sezibera.

  The EAC Secretary General noted the positive growth of the fund since 2011, and called on Development Partners to honour their pledges through actualizing pending disbursements which currently stand at 24% for the financial year 2015/16.

  Dr. Sezibera underscored the importance of the basket fund to the EAC, noting the significant support the Partnership Fund has given to the EAC including: financial support to the Implementation of the Customs Union and Common Market Protocols; Private Sector development; finalization of the One-Stop Border Post regulations; negotiations and finalization of the EAC Monetary Union Protocol; institutional strengthening  including the EAC Institutional Review; enhancing public awareness of the EAC; and development of EAC Vision 2050 among many other projects that have been completed or currently ongoing.

  The Secretary General further disclosed to the Heads of the Diplomatic missions that the use of Video-Conferencing facilities at EAC has significantly reduced the need for physical meetings by one third, resulting in huge cost savings.

  The EAC Chief called upon Trademark East Africa to join the Partnership Fund in order to better synchronize prioritization of EAC integration projects. Dr. Sezibera urged the Development Partners to provide technical and financial support to South Sudan being a young country joining the EAC. 

  In her welcome remarks, Amb. Kaarstad, on behalf of the Development Partners thanked the outgoing EAC Secretary General for the constructive cooperation and tirelessly promoting the work of the EAC as established in the Treaty and protocols.

  “The large turnout this afternoon is a testament to a strong and continued interest in the EAC’s role and in the regional integration processes”, said Amb Kaarstad.

  Amb. Kaarstad further emphasized, “the accomplishments of the Secretary General span all pillars of the EAC integration. The benefits of easier movement of people, goods, services and capital are the results. The EAC has under Dr Sezibera progressed in eliminating Non-Tariff Barriers, harmonizing common and external tariffs as well as standards and quality”.

  Amb. Kaarstad noted that although the Development Partners account for 43% of final budget at the EAC, a small portion of this goes through the Partnership Fund.

  0 0

  Mkurugenzi  wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna wa Polisi Diwani Athumani amesema hadi kufikia sasa zaidi ya watu 150  wamejitokeza  kuhakiki wa  silaha zao, katika hatua ya  kutii agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul  Makonda.

  “Baada ya Mheshimiwa Rais John Pombe  Magufuli  kufanya uhakiki wa silaha zake  hivi karibuni, watu zaidi ya 150 wakiwemo viongozi mbalimbali waliopo Serikalini, Viongozi wastaafu, Mabalozi wa nchi mbalimbali, wafanyabiashara na  wabunge wamejitokeza  kuhakiki  silaha zao, na wengine wameonesha nia ya kufanya hivyo,  hata hivyo tusingependa kutaja majina yao kwa sababu za kiusalama” amesema Kamishna wa Polisi Athumani

  Athumani amesema kuwa, lengo la kufanya uhakiki wa silaha ni pamoja na kuboresha hali ya usalama na kuwajua watumiaji, kuwatambua tena wamiliki wa silaha pamoja na kuwa wanawatambua isipokuwa  zinaweza kutokea sababu mbalimbali zitakazofanya wasiendelee kumiliki silaha hizo ikiwemo vifo na ulemavu na  kusema kuwa  wangependa kufahamu taarifa za namna hiyo, ameongeza kuwa  zoezi hili sasa ni la nchi nzima si kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee kama ilivyokuwa hapo awali.

  Aidha, wakazi wa  mkoa wa Dar es Salaam wanaweza  kuhakiki silaha zao katika vituo vya  Osterbay Polisi, Temeke Chang’ombe Polisi na Ilala central Polisi, ambapo wanatakiwa kwenda na  kitabu(firearm  licence book), picha ndogo nne za mhusika,  pamoja na  anwani sahihi ya mahali anapoishi mhusika.

  Vilevile, amewataka viongozi mbalimbali na wananchi wanaomiliki silaha kujitokeza kwa ajili ya kufanya uhakiki wa silaha zao huku akisisitiza kwa wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam, wanaweza kuonana na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro na kwa wakazi wa Mikoani waonanae na makamanda wa polisi wa Mikoa yao kwa ajili ya kupewa msaada na maelekezo zaidi ya taratibu  za kufuata ili waweze kufanya uhakiki wa  silaha zao.

  0 0

  Kampuni ya simu tanzania ttcl, imetoa msaada wa vyakula na vinywaji kwa vituo vitatu vya watoto yatima na wenye mahitaji maalumu ili kuwawezesha kusherehekea sikukuu ya pasaka. Msaada huo umetolewa kwa vituo vya friends of don bosco cha kimara suka ,kituo cha honoratha cha temeke na kituo cha green pastures cha bunju vyote vya jijini dar es salaam.

  Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya afisa mtendaji mkuu wa ttcl dr kamugisha kazaura, meneja uhusiano wa TTCL bw nicodemus thomas mushi amesema, ttcl inawathamini watoto wanaoishi katika mazingira magumu na mara zote imekuwa ikijitahidi kuwasaidia ili kuwapunguzia magumu wanayopitia na kuwapa tumaini la maisha.

  Msaada huu ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wetu wa kusaidia jamii. Takribani watoto 300 wa vituo hivi watanufaika.. Watoto hawa ni wetu, ni sehemu muhimu ya jamii yetu, ni tegemeo la nguvu kazi ya taifa letu siku zijazo. Kwa kuwaonesha upendo, tunawatia moyo na kuamsha ari ya kujituma katika masomo ili waweze kutimiza ndoto zao na baada ya masomo waweze kujitegemea na kuwa raia wema wa nchi yetu, amesema bw mushi.

  Misaada iliyotolewa ni mbuzi 3, kilo 300 za mchele, kilo 300 za unga wa sembe, kilo 150 za maharage, ndoo kubwa 6 za mafuta ya kula, katoni 60 za vinywaji( maji, juisi na soda) na viungo mbali mbali vya chakula.

  Akipokea msaada huo kwa niaba ya watoto na walezi wa vituo vilivyosaidiwa, mkuu wa kituo cha green pastures mchungaji douglas kiseu amesema, msaada wa ttcl ni faraja kubwa kwao kwani unawawezesha watoto kufurahia sikukuu kama wenzao walio na wazazi na walezi, na kuwapa fursa ya kutulia, kuelekeza mawazo na juhudi zao katika masomo na mafundisho ya stadi mbali mbali zinazotolewa vituoni humo.

  Akishukuru kwa niaba ya wenzake, mtoto elizabeth mapunda amesema, jamii inao wajibu mkubwa wa kuwasaidia wahitaji ili kutimiza maagizo ya mwenyezi mungu yanayowataka wenye uwezo kuwa msaada kwa wanaopungukiwa. Watoto wote wenye mahitaji tunamshukuru rais john pombe magufuli na mama janeth magufuli kwa kuonesha mfano mwema wa kutujali na kuwa mstari wa mbele kutusaidia na tunaziomba taasisi za umma na binafsi kuunga mkono juhudi hizo kama ttcl inavyofanya mara kwa mara.
  Mchungaji Douglas Kiseu wa Kituo cha Green Pasture akipokea msaada wa vyakula kwa ajili ya sikukuu ya pasaka kutoka kwa Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Thomas Mushi.
  Mwakilishi wa Kituo cha Honoratha cha Temeke akipokea msaada wa vyakula kwa ajili ya pasaka kutoka kwa Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Thomas Mushi.
  Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Thomas Mushi akizungumza na vyombo vya habari katika hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa vituo vitatu (3) vya jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya kuwafanikisha kusherehekea sikukuu ya Pasaka.

  0 0


  0 0
 • 03/25/16--06:20: Taarifa ya msiba
 • Sky background. Sky and clouds background.Sky.
  Zebedayo Maingu Mafuru enzi za uhai wake.

  Ndugu Asheri Mafuru, anasikitika kutangaza kifo cha ZEBEDAYO MAINGU MAFURU wa KIBAMBA DAR ES SALAAM, KILICHOTOKEA KIBAMBA DAR ES SALAM ALFAJIRI YA TAR. 23/03/2016. 

   Habari ziwafikie MAMA MZAZI RAHEL BISWALO WA KIBARA BUNDA, BABA MDOGO WA MAREHEMU GALIGWA MAFURU WA MRANGI MUSOMA, ONESMO NYABUGIKA WA MGANGO MUSOMA, NDUGU JAMAA NA MARAFIKI POPOTE WALIPO.

   MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU KIBAMBA JIJINI DAR ES SALAAM. MAZISHI YATAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU JUMAMOSI TAREHE 26/03/2016. BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

  0 0


  0 0
  0 0

   Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa Machi 25, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa na waumini wengine katika Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa Machi 25, 2016
   Msalaba ukipelekwa altereni kuanza ibada ambayo imehudhuriwa pia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa katika Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa Machi 25, 2016 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akijiandaa kuubusu Msalaba wakati wa Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa Machi 25, 2016

   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akibusu Msalaba wakati wa Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa Machi 25, 2016
   Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akibusu Msalaba wakati wa Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa Machi 25, 2016
  Sehemu ya waumini katika Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa Machi 25, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na watu wenye ulemavu baada ya  Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa Machi 25, 2016. Picha na IKULU

  0 0

  Familia ya mwenyekiti wa CCM-NY inapenda kuwakaribisha watanzania wote kwenye kisomo cha marehemu mpendwa baba yao mkubwa kitakachofanyika Jumamosi hii (3/26/16) kuanzia saa kumi na moja jioni (5:00PM). Mahali kisomo kitakapo fanyika ni: 

  2505 Third avenue, Bronx, NY 10451. 

  Tafadhali jisikie huru kifika na kitu chochote kile utakachojaaliwa. Natanguliza shukrani nyingi kwenu nyote.
  Kwa taarifa zaidi unaweza kuwasiliana NA
  SEIF AKIDA-917-557-3195
  SALIMU AKIDA-646-807-5838
  GASTON MKAPA-646-358-2367

older | 1 | .... | 1171 | 1172 | (Page 1173) | 1174 | 1175 | .... | 3348 | newer