Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110108 articles
Browse latest View live

BASATA LAONYA KUMBI, LAPIGA MARUFUKU DISKO TOTO

$
0
0

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini linawakumbusha wamiliki na waendeshaji wa kumbi za burudani kufuata sheria, kanuni na taratibu walizopewa kwenye vibali vyao vya uendeshaji wa kumbi.

Wanaelekezwa kuhakikisha wanakuwa na vibali halali vya uendeshaji wa kumbi zao, kuzingatia muda wa utumizi wa kumbi, kuepuka kelele zinazosumbua kwenye maeneo maalum hasa makazi ya watu na kuhakikisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu na mali zao.

Aidha, BASATA linawakumbusha wamiliki wote wa kumbi za sherehe na burudani kwamba ni marufuku kukusanya watoto katika kumbi zao kupitia kile kinachoitwa ‘Disko Toto’ katika msimu huu wa Sikukuu ya Pasaka ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.

Uzoefu unaonesha kwamba, nyakati za sikukuu kama hizi wamiliki wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kuendekeza faida katika biashara zao kiasi cha kuandaa madisko ya watoto hali mbayo imekuwa ikisababisha maafa ambayo yangeepukika kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.

Aidha, baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa kumbi kwa msingi huohuo wa kuendekeza faida pasi na kujali maelekezo ya vibali vyao wamekuwa wakijaza watu kupita viwango vya madaraja waliyopangiwa na BASATA. 

BASATA kama mtoaji wa vibali vya kumbi za sherehe na burudani linasisistiza kwamba halitafumbia macho ukumbi wowote utakaokiuka maelekezo haya sambamba na kuruhusu maonesho machafu yenye kudhalilisha utu wa binadamu hasa yale yanayoonesha maungo ya ndani. Hatua kali na za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maagizo haya.

BASATA linawatakia wasanii na wadau wote wa Sanaa Pasaka njema na yenye furaha tele. 


SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI



Godfrey L. Mngereza 

KATIBU MTENDAJI, BASATA.

NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JNIA

$
0
0
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha (katikati), akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) wakati Waziri huyo alipotembelea Uwanja huo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno.
Mkuu wa Ofisi ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Abuu Mvano (kulia), akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), alipotembelea Idara za Wizara hiyo zilizopo katika Uwanja huo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani waliopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Waandishi wa Habari wakati wa ziara yake aliyoifanya kutembelea Idara za Wizara hiyo zilizomo katika Uwanja huo.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kuendelea kuwezesha miradi ya Umeme

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na watendaji kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Mwakilishi wa Shirika hilo nchini, Emmanuel Baudran (katikati) na kushoto ni Dennis Munuve kutoka Shirika hilo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ( wa kwanza kulia) akiwa katika kikao na watendaji kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake.

Na Teresia Mhagama,

Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) limesema kuwa limeshatoa jumla ya Euro milioni 321 kuanzia mwaka 2009 mpaka sasa ambazo ni sawa na wastani wa Euro milioni 50 kwa mwaka kwa ajili ya shughuli za maendeleo nchini na kwamba mpango wake ni kuongeza kiwango hicho ifikapo mwakani.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Tanzania, Emmanuel Baudran wakati alipofika Wizara ya Nishati na Madini ili kuzungumza masuala mbalimbali na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo pamoja na Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake.

Baudran alieleza kuwa fedha hizo ambazo zimetolewa kupitia mkopo wenye masharti nafuu zimeelekezwa katika Sekta za Maji, Nishati na Miundombinu ya usafirishaji.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

DAWASCO YANASA WAKINA MAMA NTILIE KWA WIZI WA MAJI

$
0
0
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco) limewanasa mama ntilie zaidi ya 6 wakiwa wanatumia huduma ya Maji kinyume cha utaratibu kwa kujiunganishia laini ya Majisafi na kukosa mita wala akaunti kutoka Dawasco kwenye eneo la mtaa wa Kisutu, Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye eneo la tukio Afisa Biashara wa Dawasco, Deogratius Ng’wandu amesema kuwa walibaini wizi huo wa Maji kwenye operesheni yake maalum ambayo inayoendelea kwenye maeneo yote ya Jiji la Dar es salaam na ndipo walipokuta Mama ntilie ambao walikuwa kwenye eneo hilo lilozungushiwa mabati lisilo na jengo ambapo walikuwa wakipika pamoja na kulima mbogamboga kwa kutumia Maji ya Dawasco.

“Tumekuta wakina Mama ntilie wakiwa wakitumia huduma ya Maji ambayo yameunganishiwa kinyume cha utaratibu ambapo yalikuwa hayana mita wala akaunti namba na Maji hayo yamekuwa yakitumika kupikia  kufanya usafi pamoja na kulima  mboga mboga ila wanadai hawamfahamu mwenye eneo hivyo tumewapeleka Polisi kwa hatua zaidi za kisheria” , alisema Ng’wandu.

Kwa upande wa mwenyekiti wa serikali ya mtaa Kisutu, Subira Ngeseyani ameomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwataja wezi wa Maji kwenye mita yao kama alivyoagiza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda ambapo aliagiza wenyeviti wa Serikali za mtaa jijini Dar es Salaam kushirikiana na Dawasco pamoja wananchi kubaini wezi wa Maji wanaofanya wateja halali kukosa huduma ya Maji.

“Wananchi wote ni jukumu letu kushirikiana na Dawasco kuwabaini wezi wa Maji kwenye mitaa yetu kama Mkuu wa Mkoa alivyoagiza ilikufanya wale wateja halali wanaostahili huduma ya Maji kupata kwani ni haki yao hivyo wote tushirikiane tuondoe tatizo la wizi wa Maji Jijini Dar es salaam”,Ngeseyani.

Kwa upande wa Mama ntilie hao Bi Aziza Hassan amekiri kuwa walikuwa wanatumia huduma ya Maji hayo kwenye eneo hilo ila walikuwa hawaelewi  kuwa yameunganishwa kinyume cha utaratibu na mmiliki wa eneo  pia kutokana na hali ngumu ya kimaisha walishindwa kuulizia kwani walijua gharama zakuunganishiwa kihalali ni kubwa.

“Kweli tumekuwa tukitumia huduma ya Maji kwenye eneo hili kwa shughuli zetu ila hatukuwa tukielewa kama yameunganishwa kinyume cha utaratibu hata hivyo kutokana na hali ngumu ya maisha tusingeweza kujiunganishia huduma ya Maji kwani ni gharama”, alisema bi Aziza.

Hata hivyo Dawasco imeendelea kuwasihi wakazi wa Jiji la Dar es salaam kuwafichua wezi wa Maji kwenye maeneo yao kama alivyoagiza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na pia watu wote ambao wamejiunganishia kinyume na utaratibu wajisalimishe na kutambulika kabla hawajakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

TUME YA UCHAGUZI YAKAMILISHA IDADI YA WABUNGE WA VITI MAALUMU WA TATU.

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva akizungumza na waandishi wa habari na kutangaza Majina ya wabunge wa wa viti maalumu katika ukumbi wa tume ya uchaguzi jijini Dar es Salaam, kuhusiana na tume hiyo kukamilisha idadi ya wabunge watatu wa viti maalumu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wawili na wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mmoja. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Givenes Aswile akiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo.
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva akitangaza majina ya wabunge wa viti maalumu watatu kuwa ni  Ritha Kabati (CCM), Oliver Semunguruka (CCM) pamoja na Lucy Owenya (Chadema). kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Emmanuel Kavishe.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva jijini Dar es Salaam leo wakati akitangaza majina ya wabunge wa viti maalumu
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
IDADI ya wabunge wa Viti Maalum watatu imekamilika baada ya uchaguzi majimbo yote  kufanyika ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata viti maalum viwili na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mmoja.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu ,Damian Lubuva amesema kuwa  uchaguzi umekamilika katika majimbo nane kwa kuwa na majimbo ya Tanzania Bara saba na Zanzibar Moja ambalo ni Jimbo la kijito Upele.

Viti vya wabunge wa viti maalum wanatokana na kura za jumla za wabunge wote na kuweza kupatikana viti hivyo.

Waliopatikana katika mchanganuo wa viti maalum ni, Ritha Kabati (CCM), Oliver Semunguruka (CCM) pamoja na Lucy Owenya (Chadema).

Lubuva amesema kuwa kufikia hapo ndipo uchaguzi umekamilika kutokana na viti hiyo kupatikana na kufanya kuwa viti maalumu 113 katika mgawanyo wa viti hivyo ni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Viti  66,  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  viti 35 pamoja na Chama cha Wananchi (CUF)  viti 10.

Amesema kuwa kutokana na chaguzi zinazoendelea NEC ndiwe iwe sehemu ya usimamizi wa chaguzi zote.

Idadi kura za wabunge CCM katika uchaguzi ambazo zilibaki kutokana wagombea kufariki na kuarishwa kumeongeza viti maalum viwili.

Benki ya Exim yaboresha huduma yake ya utumaji wa pesa kimataifa.

$
0
0


Benki ya Exim Tanzania imeboresha huduma yake ya utumaji na upokeaji wa pesa kimataifa kwa kuharakisha ukamilishaji wa miamala hiyo ambapo kwa sasa wateja wake watatumia saa nne badala ya muda wa  saa 12 uliokuwa ukitumika hapo awali.

“Exim tumekuwa tukipambana kila siku kuhakikisha tunatoa huduma bora, za haraka na kwa usalama zaidi ili kuwaunganisha wateja wetu na fursa za kimataifa. Kwenye hili  tunatoa hakikisho kwa wateja wetu kwamba iwapo kutatokea ucheleweshaji zaidi ya muda wa masaa manne basi tutalazimika kuwarejeshea gharama zao walizolipa kwa ajili ya  huduma,’’ alisema Bw  Tumaini Mwakafwaga ambaye ni mkuu wa kitengo cha operesheni za Benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.

Hata hivyo alibainisha kuwa hakikisho hilo la muda wa masaa manne (guarantee) litahusu wateja wenye maombi (miamala) yasiyokuwa na utata,  wenye nyaraka onyeshi (supporting documents) pamoja na wale wenye kiasi cha kutosha kwenye akaunti zao.

“Lakini pia kuna mazingira ambayo yanaweza kufanya tukashindwa kumrejeshea mteja gharama zake (refund) ikiwemo pale ambapo mfumo wetu wa kuendesha miamala utakuwa umekwama kutokana na sababu  zilizo nje ya uwezo wetu yakiwemo majanga ya asili,’’ aliongeza Mwakafwaga.

Alisema watumiaji wa huduma hiyo watakuwa wakipokea taarifa kuhusu mwenendo mzima wa miamala yao kwa kuwa itakuwa ikifuatiliwa kwa ukaribu kila hatua inayopitia.

“Kiukweli timu yetu inayohusika na kuchakata (processing) miamala hii inauelewa wa kutosha pamoja na uwezo mkubwa wa kutimiza majukumu yao kwa haraka kuanzia muda ambao mteja anaanza kutumia huduma hii hadi hatua ya mwisho. Mameneja na wasaidizi wao wapo tayari kuhakikisha kila kitu kinaenda kwa wakati na kwa usahihi,’’ alisisitiza.

MANYARA YAPITISHA BAJETI YAKE

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera

Na Woinde Shizza,manyara

Mkoa wa Manyara unatarajia kutumia sh202.1 bilioni kwa ajili ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017, ambapo mishahara itakuwa ni sh5.5 bilioni, matumizi ya kawaida sh2.1 bilioni na sh2.7 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Katika mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 mkoa umekadiriwa kukusanya mapato ya ndani ya sh18 bilioni ambapo sh17.9 bilioni ni kwa ajili ya serikali za mitaa na sh192 milioni ni za sekretarieti ya mkoa.

Akisoma mpango wa bajeti ya mkoa huo juzi, Katibu Tawala wa mkoa huo Eliakim Maswi alisema kijiografia Manyara yenye kilomita za mraba 50,921 ni kubwa kuliko baadhi ya mikoa, hivyo inahitaji gharama kubwa za uendeshaji.

Maswi alisema katika mpango huo wa bajeti, Babati mjini wanatarajia kutumia sh25 bilioni, Babati vijijini sh37 bilioni, Hanang’ sh33 bilioni, Kiteto sh30 bilioni, Mbulu vijijini sh38 bilioni, Mbulu mjini sh6 bilioni na Simanjiro sh19 bilioni. “Pia tunakabiliwa na changamoto ya kuchelewa au kutopatikana kwa fedha za ruzuku za matumizi ya kawaida na ruzuku ya miradi ya maendeleo, ufinyu wa bajeti wa kuboresha na kujenga miundombinu ya zahanati na shule,” alisema.

Alisema umbali kutoka makao makuu ya halmashauri ya wilaya hadi makao makuu ya mkoa ambapo ni lazima upitie wilaya nyingine kama Kondoa, Monduli na Arusha ili ufike mkoani wakati wa kufuata huduma mkoani pia ni kikwazo.

Hata hivyo, mkuu wa mkoa huo Dk Joel Bendera alizitaka halmashauri zote saba kuhakikisha zinachangia bajeti zao kwa asilimia 60 ya mapato ya vyanzo vya ndani kama serikali kuu ilivyoagiza ili kutekeleza miradi ya maendeleo yao.

“Nitakuwa mkali katika kuhakikisha hilo linatekelezeka hivyo kila halmashauri ihakikishe inakusanya mapato yao na kufikia asilimia 60 kwani mimi ndiye ninayekwenda kuomba kupitishwa kwa bajeti yetu,” alisema Dk Bendera.

TAIFA STARS KUWASILI DAR LEO.

$
0
0
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kinatarajiwa kuwasili leo saa 8 usiku katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. JK Nyerere kikitokea nchini Chad kilipokuwa na mchezo dhidi ya wenyeji jana jioni.
Msafara wa Taifa Stars unaongozwa na mkuu wa msafara ambaye pia ni Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ravia Idarus Faina utaondoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa N’Djamena saa 8 mchana kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia, kabla ya kuunganisha ndege saa 4 usiku tayari kwa safari ya kurejea nyumbani Tanzania.
Stars inarejea nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya wenyeji Chad, bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta katika mchezo uliochezwa uwanja wa Omnisport Idriss Mahaymat Ouya jijini N’Djamena katika mchezo wa kundi G kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017.
Mara baada ya kuwasili jijini Dar es salaam, kikosi cha Taifa Stars kitaingia moja kwa kwa moja kambini katika hoteli ya Urban Rose iliyopo eneo la Kisutu kujiandaa na mchezo wa marudano utakaochezwa siku ya Jumatatu ya Pasaka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

VODACOM TANZANIA NA SAMSUNG ZAWALETEA GALAX S7 NA S7 EDGE ZISIZOINGIZA MAJI.

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(wapili kushoto)akionesha simu ya kisasa aina ya Galax S7 kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa simu hizo aina ya Galax S7 na S7 Edge ambazo haziingizi maji ulifanyika Makao Makuu ya Kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Samsung Tanzania,Kutoka kushoto Meneja wa bidhaa wa Samsung,Rayton Kwembe,Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Charles na Meneja masoko wa Samsung,Tulisindo Mwachula.
Meneja wa bidhaa wa Samsung,Rayton Kwembe(kushoto)akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)jinsi ya unavyoweza kuitumia simu ya aina ya Galax S7 na S7 Edge katika matumizi mengine, wakati wa uzinduzi wa simu hizo ambazo haziingizi maji ulifanyika Makao Makuu ya Vodacom Tanzania Mlimani City jijini Dar es Salaam,Katikati Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu na Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Charles.
Meneja wa bidhaa wa Samsung,Rayton Kwembe(kushoto) Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu, Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Charles, Meneja masoko wa Samsung,Tulisindo Mwachula,wakionesha simu aina ya Galax S7 na S7 Edge kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa simu hizo ambazo haziingizi maji ulifanyika Makao Makuu ya Vodacom Tanzania Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Meneja wa bidhaa wa Samsung,Rayton Kwembe(kushoto) na Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Charles(kulia)wakimshuhudia Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu,akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)simu ya kisasa aina ya Galax S7 wakati wa uzinduzi wa simu za aina hiyo na S7 Edge ambazo haziingizi maji ulifanyika Makao Makuu ya Kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Samsung Tanzania.

TUKIWA kampuni inayoongoza kwa mawasiliano hapa nchini leo tunautangazia Umma kwa kuzindua mauzo ya simu za kisasa kabisa ulimwenguni na ambazo haziingizi maji, Galax S7 na S7 Edge kwa kushirikiana na kampuni ya Samsung.

Simu hizi mbili ambazo tumezizindua leo na kuanzia sasa zitakuwa zinapatikana katika maduka yote ya Vodacom pamoja na ya Samsung kote nchini.Tukiunga mkono jitihada zinazofanywa na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)kwa wananchi kutokuuziwa simu zisizokidhi kiwango cha ubora wa simu yaani(Simu feki)

“Samsung Galaxy S7 na Galaxy S7 Edge zitakuwa zikitolewa kupitia maduka yetu yote huku zikiambatanishwa na Power-Bank ya BURE; ambapo vilevile, kwa wanunuaji 50 wa kwanza wataweza kujipatia Bluetooth Earphones za Galaxy za bure kabisa,” Alisema Matina Nkurlu, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania.

Nkurlu alibainisha kwamba,Simu hizi mbili zimekuja zikiwa na maboresho mahsusi yanayolenga kukidhi mahitaji ya vijana wa kisasa hususani katika msimu huu wa sikukuu ya Pasaka, ambapo watumiaji wataweza kufurahia na internet ya kasi na haraka zaidi kupitia mtandao wa Vodacom.

TANZIA

UINGEREZA KUSAIDIA UFIKIWAJI WA HAKI NCHINI.

$
0
0
Mshauri wa Makosa ya Jinai kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania Bw. Andy Stephens (aliyesimama) akizungumza  katika mkutano aliofanya na Wanasheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu namna nchi yake itakavyoshirikiana na Tanzania katika kuboresha utoaji wa haki nchini hasa katika maeneo ya upelelezi, uendeshaji wa mashtaka na utoaji haki katika Mahakama zetu. Mazungumzo hayo yamefanyika leo (24/3/2016) katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyeweka mkono kichwani) akimsikiliza kwa makini Mshauri wa Makosa ya Jinai kutoka Ubalozi wa Uingereza Bw. Andy Stephens (aliyesimama) alipokuwa akizungumza kwenye kikao na Wanasheria wa Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu nchi ya Uingereza itakavyoshirikiana na Tanzania katika kuboresha utoaji haki nchini hasa kwenye Mahakama za Tanzania. Kikao hicho kimefanyika leo (24/3/2016) katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria.

ALIYEKUWA MHASIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI KATIKA JESHI LA KUZIMA MOTO NA UOKOZI NA WENZAKE WA HUKUMIWA KWA KESI YA UHUHUJUMU UCHUMI

$
0
0
Aliyekuwa Mhasibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani katika jeshi la kuzima moto na uokozi na Bw. Naamini Hendry Sangiwa pamoja na Mkandarasi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiareni Investment Ltd Bw. Webu Manoth Masawe wamehukumiwa leo tarehe 24/3/2016 kwa kesi ya kuhujumu uchumi katika Mahakama ya wilaya ya Ilala. Hukumu hiyo ilisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mhe. Hassan.
Washtakiwa tajwa hapo juu walishtakiwa kwa makosa 7 yakiwemo Matumizi Mabaya ya Madaraka, Kutumia Nyaraka Kumdanganya Mwajiri kinyume na kifungu cha 22 na 31 mtawalia vya Sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11/2007, Kughushi Nyaraka kinyume na Kifungu cha 333, 335 (d) (1) na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, na kuisababishia Serikali hasara kinyume na Aya ya 10(1) ya Jedwali la Kwanza, Kifungu cha 57(1) na 60(1) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200.

Mnamo mwaka 2009 Serikali ilitoa zabuni ya Ujenzi wa uzio wa Chuo cha Zimamoto na Uokozi kilichopo Mbopo Bunju katika Manispaa  ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Kampuni ya Kiareni Investment Ltd (Mzabuni), ilipatiwa zabuni hiyo na kulipwa Kiasi cha Shilingi 81, 963, 360/=. Hata hivyo taratibu za utoaji zabuni hazikufuatwa, na Mzabuni ambaye ni Kampuni ya Kiareni Investment Ltd, alifanya kazi yenye thamani ya kiasi cha Shilingi 13, 784, 652/= tu kati ya fedha yote aliyolipwa. Ili kuwezesha malipo ya Shilingi 81, 963, 360/= kulipwa pasipo kazi kukamilika, Washtakiwa walitoa zabuni kwa Mkandarasi pasipo Mkataba (LPO), na Kughushi Hati ya kuonesha kazi imekamilika (Certificate of Works Completion).

Washitakiwa wote watatu walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mwanzoni mwa mwaka 2014 na kusomewa mashtaka yao Mbele ya Hakimu Mkazi Hassan, ambapo washitakiwa walifunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi No. 06/2014. Upande wa Jamhuri katika Kesi hii uliwakilishwa na Wakili STANLEY HILMAR LUOGA akisaidiana na Wakili EMMANUEL
JACOB, wote waendesha Mashitaka wa TAKUKURU Makao Makuu. Upande wa washtakiwa wote waliwakilishwa na Wakili wa Kujitegemea MDUMA. Upande wa Jamhuri uliita Mashahidi 7 na kupeleka vielelezo 21 ili kuthibitisha kesi dhidi ya washtakiwa. Upande wa washtakiwa hawakuita shahidi hata mmoja walijitetea wenyewe.
Mshitakiwa wa kwanza Dotto Salehe Mgogo, ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Mafunzo wa Wizara ya Mambo ya Ndani katika idara ya Jeshi la Zimamoto na Uokozi alifariki dunia mwaka 2014 baada ya kusomewa mashitaka na hivyo Mashitaka dhidi yake yalifutwa kwa mujibu wa sheria. Kufuatia kifo cha Mshitakiwa wa kwanza,

Mshitakiwa wa Pili Bw. Naamini Hendry Sangiwa ambaye alikuwa Mhasibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Katika Jeshi la Zimamoto na Uokozi alikuwa anakabiliwa na makosa manne (4) ambapo makosa mawili ni ya Matumizi Mabaya ya Madaraka, Kughushi na Kuisababishia Serikali Hasara, ametiwa hatiani katika makosa yote mawili ya Matumizi ya Madaraka na kupewa adhabu ya kulipa faini ya Tshs.300, 000 kwa kila kosa la Matumizi Mabaya ya Madaraka kama atashindwa kulipa faini, kwenda jela miezi 6 kwa kila kosa. Katika Kosa la Kughushi Nyaraka, Mshtakiwa ametiwa Hatiani na Kuamriwa kutotenda kosa lolote la jinai kwa muda wa miezi 12.

Mshitakiwa wa tatu ambaye ni Bw. Webu Manoth Masawe, ambaye ni Mkandarasi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiareni Investment Ltd, anakabiliwa na Kosa moja la Kuisababishia Serikali Hasara. Mahakama imemtia hatiani na kumpa adhabu ya kwenda Jela miaka mitatu (3) pamoja na Kuirudishia Serikali kiasi cha Shilingi 67, 913, 748/= ikiwa ni hasara aliyoisababishia Serikali.



IMETOLEWA NA OFISI YA AFISA UHUSIANO 
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA


24 MACHI, 2016

TANZANIA NA SAUDIA ZASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MASUALA YA UCHUMI NA UWEKEZAJI.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akiwa katika mazungumzo  na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia uwekwaji saini wa mkataba kuhusu Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa upande wa Tanzania mkataba ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (kulia) na Serikali ya Saudi Arabia iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Adel Al Jubair.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia kubadilishana hati baada ya uwekwaji saini wa mkataba kuhusu Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa upande wa Tanzania mkataba ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (kulia) na Serikali ya Saudi Arabia iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Adel Al Jubair.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia.  Picha na IKULU

DKT. SHEIN AAPISHWA KUWA RAIS WA ZANZIBAR WA AWAMU YA SABA

$
0
0
Rais Mteule wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiapishwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Omar Othman Makungu katika uwanja wa Amaan Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.]

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA AWAMU YA SABA WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR DKT. ALI MOHAMED SHEIN

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono mamia ya wananchi wa Zanzibar mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amaan kisiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jeneral Devis Mwamunyange wakifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa na Yamoto bendi katika uwanja wa Amaan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakifatilia kwa makini burudani iliyokuwa ikitolewa na Bendi ya muziki ya Yamoto katika uwanja wa Amaan. 


KONSELI MKUU WA UBALOZI MDOGO WA TANZANIA JEDDAH,SAUDI ARABIA, ATEMBELEA ENEO LA KUHIFADHIA MIFUGO LA SALEH BAKHATAB MJINI MECCA

$
0
0
Kufuatia ziara ya Bw. Saleh Saeed Bakhatab Jumanne Machi 22, 2016, katika Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Jeddah, Saudi Arabia, Konseli Mkuu Bw. Suleiman Saleh, nae Jumatano Machi 23, 2016, alimtembelea mfanya biashara huyo mwenye makazi yake katika mji wa Mecca ili kuona aina ya mifugo ambayo anaiagizia kutoka nchi za nje. 
Wakati wa ziara hiyo Bw. Saleh alipokelewa katika mji wa Mecca na Bw. Bakhatab ambaye kwa kiasi kikubwa alifarijika na uharaka wa ziara hiyo ya ufuatiliaji siku moja tu baada ya yeye kutembelea Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Jeddah, Saudi Arabia. 
Bw. Bakhatab ambaye yumo katika maandalizi ya kutembelea Tanzania alimkaguza Konseli Mkuu katika eneo analopokelea mifugo ya aina mbali mbali ikiwemo ya ngamia, ngombe, kondoo na mbuzi . Bw. Bakhatab alimueleza Bw. Saleh aina mbali mbali ya mifugo hiyo na namna anavyoihifadhi na kuipatie lishe stahili ili kukidhi viwango wa soko la Saudi Arabia. Aidha, katika ziara hiyo, Bw. Bakhatab alimuhakikishia Bw. Saleh kwamba anaamini kwamba Tanzania itakuwa moja ya chanzo kikuu cha kampuni yake kununua mifugo ya aina mbali mbali na hivyo kusaidia juhudi za Serikali za kuinua uchumi wake.
Bw. Saleh Saeed Bakhatab anaemiliki kampuni ya SALEH SAEED ESTABLISHMENT FOR CONTRACTING AND CATTLE IMPORTS amejizatiti katika kufanya biashara ya mifugo na Tanzania, amejipanga kusafirisha mifugo hiyo kwa ndege maalum kutoka Tanzania hadi Djibouti ambapo baadae itapakiwa katika meli hadi Jeddah, Saudi Arabia akiijumuisha na mifugo kutoka nchi za Sudan na Somalia.

Bw. Suleiman Saleh Konseli Mkuu wa Ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Jeddah,Saudi Arabia, akiwa na Bw. Saleh Saeed Bakhatab wakiwa katika eneo lake la kuhifadhia mifugo anayoiagizia kutoka nje katika mji wa Mecca, Saudi Arabia. 

TANZANIA DIASPORA CONFERENCE 2016 IN LONDON

$
0
0
This is to announce the Tanzania Diaspora Conference, which will run from April  30th April-1st May , 2016 in London.
 This   event will create awareness, enable collaboration and enhance learning amongst the diaspora community in the UK and beyond
The weekend is organized by a consortium of Tanzania Diaspora organisations in the UK led by Newdeal  Africa.
 The 2016 Tanzania Diaspora conference will provide a platform to showcase exemplary initiatives in international development and diplomacy by diaspora communities around the world, highlight paths to success for diaspora engagement, and allow for collaboration between the public and private sectors and civil society. It  will also  highlight trade  and  investment  opportunities  in  Tanzania
The purpose  of  this  letter  is  to  kindly  invite  you  as  a  speaker  ,exhibitor  and  sponsor
There are issues right now that  are  relevant  to  our  diaspora  communities  and  how  KCB CAN BRIDGE  THIS  GAP  in  monetary  terms.So  we  have  arranged  a  ‘meet  the  Diaspora   event’  during  this  weekend.
I hope this request will  meet  your  kindest  consideration.
Further details to follow  upon  request.
NEWDEAL AFRICA
LONDON

Why Should You Exhibit?
·         Networking opportunity
·         Increase YOUR sales volume
·         Promote your products/services
·         Partnership OPPORTUNITIES
·         Support the Diaspora
·         Reach a new market segment
·         Inform  the  public  about  your  product/service
 
Who will you meet at the Convention?
 
·         A Distinguished Guest of Honour
·         His Excellency Mr Peter Kallaghe (The former High Commissioner of Tanzania London)
·         High Delegates, Government bodies and officials
·         Tanzanians (The Diaspora) and businesses with interest in Tanzania
·         ENTREPRENEURS looking for opportunities in UK and Africa
·         Use the Convention as a global platform for expansion
·         Many delegates from all over Europe, UK, Africa and Tanzania
·         Diaspora businesses of all sizes based in the UK
INVESTORS for various business including:                                
-Start ups
-Small Medium enterprises
-Micro Organisation
-Macro Organisations
-International TRADERS
- And Many More

MKUU WA MKOA MPYA WA KAGERA AANZA KAZI RASMI KWA KUTOA MAAGIZO YAKE KWA WATENDAJI NA VIONGOZI WA MKOA HUO

$
0
0
Na Faustine Ruta, Bukoba

Mkuu wa Mkoa mpya wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu amekabidhiwa rasmi ofisi na kuanza kutekeleza majukumu yake kama Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Makabidhiano hayo yamefanyika siku ya Jumanne Machi 22, 2016 kati yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella aliyehamishiwa Mkoani Mwanza. 
Katika hafla fupi ya makabidhiano hayo Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu akiongea na wadau mbalimbali wa Mkoa aliwaomba wananchi wote wa Kagera kuonesha ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake aidha aliongelea mikakati yake katika kutekeleza majukumu yake hapa Mkoani.
Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu aliwakumbusha watumishi wa umma katika Mkoa wa Kagera kuifahamu vizuri dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kuwa ni kuwajibika kwa kufanya kazi kwa kasi inayotakiwa, kwa nguvu, maarifa, upendo na uadilifu mkubwa bila kusukumwa na mtu yeyote aidha, kila mtumishi afanye kazi kwa uwezo wake wote. 
“Mtumishi wa umma anatakiwa kufahamu wajibu wake hasa kwa kuwatumikia wananchi ili kusukuma maendeleo yao mbele kwa kufanya kazi kwa kujituma bila kubabaisha, pili kufanya kazi kwa kutenda haki bila kudhurumu wananchi haki zao.” Alitoa ilani Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu. 
Maagizo 
Mkuu wa Mkoa Mpya wa Kagera Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu aligiza kuundwa mara moja mabaraza ya kushughulikia haki za wananchi kama hayapo na kama yapo yaanze kufanya kazi zake mara moja kwa kuwahudumia wananchi ili kupata haki zao. Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wananhimiza wananchi kufanya kazi kila mtu kwa nafasi yake bila kutega. 
Sekta ya Afya, Vituo vyote vya kutolea huduma za afya vinatakiwa kuwa katika hali ya usafi na kutoa huduma stahiki kwa wananchi. Watoa huduma wanatakiwa kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana muda wote kama ambavyo Serikali imekuwa ikiagiza mara kwa mara. 
Ulinzi na Usalaama wa Mkoa, Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu alisema kuwa wale wote ambao wanafanya vitendo vya uvunjifu wa amani hasa kwa kuteka wananchi na vyombo vya usafiri maporini, atahakikisha anasafisha uchafu huo wote kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalaama ili kukomesha tabia hiyo.
Wahamiaji Haramu, Mkuu wa Mkoa Mpya amewaagiza Wakuu wa Wilaya za mpakani kutoa au kugatua madaraka kwa Wenyeviti wa vijiji na Vitongoji ili waweze kufuatilia mienendo ya wageni wanapoingia nchini ili waweze kuwarudisha mara moja walikotoka. Aidha, aliwaagiza Afisa Uhamiaji Mkoa na Jeshi la Polisi kufanya kazi zao kikamilifu ili kuondoa wahamiaji haramu. 

Chakula, Kwakuwa Mkoa wa Kagera hauna baa la njaa Mkuu wa Mkoa alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuhamasishwa kutunza chakula hata kama hakuna baa la njaa ili kujihakikishia akiba ya mbeleni bila kuuza chakula chote cha akiba. 
Ukusanyaji wa Mapato ya serikali, Mkuu wa Mkoa aliziagiza taasisi zote za Serikali kuhakikisha zina kusanya mapato kwa njia ya kielekitroniki ili Serikali ipate mapato ambayo yanarudishwa Mkoani kwetu ili yatekeleze miradi ya maendeleo kwa wananchi. 
Mishahara Hewa, Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu aliagiza kwa watendaji wa Serikali kama kuna watumishi hewa waondolewe mara moja kabla ya tarehe 30/03/2016 na baada hapo utafanyika uhakiki kwa kupokea mishahra dirishani kama mwaka 1994 na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria. 
Elimu, viongozi na na watendaji wanatakiwa kutekeleza Sera ya Serikali ya Elimu Bure kwa kukabiliana na changamoto mabalimbali ambazo zimejitokeza mara baada ya kuanzishwa Sera hiyo kama uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa na kufikia Juni 30, 20116 changamoto hizo ziwe zimefanyiwa kazi na kumalizika.
Milioni Hamsini kila Kijiji, Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu alimalizia kwa kuwaagiza viongozi na watumishi wa Serikali hasa ngazi za Serikali za Mitaa kuwaandaa wananchi kwa kuwaelimisha juu ya uibuaji wa miradi ya maendeleo ili Milioni Hamsini zilizohaidiwa katika kampeini ambazo zipo karibu kuletwa ziwanufaishe wananchi katika vikundi na siyo kuzigawana tu. 
Kwa upande mwingine aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliyehamishiwa Mkoani Mwanza Mhe. John Mongella aliwashukuru wananchi wa wote wa Kagera kwa kipindi alichokuwepo Mkoani kwa ushirikiano wao mkubwa na kuwaomba ushirikiano huo wauendeleze kwa Mkuu wa Mkoa Mpya Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu.


Historia Fupi 
Mkuu wa Mkoa mpya Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu amehudumu katika Jeshi la Wananchi Tanzania kwa miaka arobaini (40) na alistaafu Jeshini Januari 30, 2016 akiwa Kamanda wa Majeshi ya nchi kavu. Aidha, Aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera tarehe 13/03/2016 na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli tarehe 15/03/2016. 
Mkuu wa Mkoa mpya Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera wa 22 tangu uhuru mwaka 1961 amabpo Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Kagera alikuwa Marehemu Samwel Ntambala Rwangisa. 

Article 18

Petra Diamonds sells exceptional pink diamond from Tanzania for $15 million

$
0
0
Petra Diamonds Ltd said on Thursday it had recovered and sold an exceptional 32.33 carat pink diamond from the Williamson mine in Tanzania for $15 million.
The company, which owns the historic Finsch and Cullinan mines, said it would retain a 10 percent interest in the polished proceeds.

The diamond was bought by Golden Yellow Diamonds on behalf of diamond manufacturer M.A. Anavi Diamond Group, Petra said. 
Viewing all 110108 articles
Browse latest View live




Latest Images