Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1169 | 1170 | (Page 1171) | 1172 | 1173 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Bi.Neli Msuya akizungumza na viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji zilizojengwa chini ya mradi wa Maji Yetu uliofadhiliwa na Serikali ya Ubelgiji uliogharimu shilingi Bilioni 14.5 alipokutana nao leo jijini Dar es salaam.
  Mshauri wa Ufundi wa DAWASA BTC  Mhandisi Praygod Mawalla akitoa elimu kwa viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji katika jiji la Dar es salaam namna ya kuifanya miradi wanayoisimamia ijiendeshe na kuwa endelevu kwa manufaa ya wananchi.
  Mshauri wa Ufundi wa DAWASA BTC  Manjolo Kambili akitoa akitoa ufafanuzi kuhusu Programu ya za utoaji wa mafunzo kwa watumiaji wa Maji katika maeneo yenye miradi hiyo wakati wa mkutano na viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji za jiji la Dar es salaam.


  0 0

  Na Editha Karlo wa blog ya jamii, Kigoma. 

  MKUU wa Wilaya ya Uvinza,Mrisho Gambo amewataka Wananchi wa Tarafa ya nguruka kuchangia Mfuko wa afya ya jamii (CHF) ili kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua wao na familia zao.

  Hayo ameyasema  katika Mkutano wa hadhara wa kuzindua kampeni ya uhamasishaji wa  kuchangia mfuko CHF katika kata ya Nguruka  uliofanyika leo kwenye viwanja vya shule ya msingi Nguruka.

  Gambo alisema kuwa katika hospitali ya Nguruka kuna changamoto kubwa ya upungufu wa dawa kutokana na hali hiyo aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia mfuko huo iliwaweze kuwa na uhakika wa  kupata dawa na matibabu matibabu mengine katika hospital yao.

  "Ninawaomba ndugu  zangu changieni CHF ili muwe na uhakika wa matibabu mnapo umwa tambueni ugonjwa unapokuja huwa hauna taarifa unaweza kuumwa na mfukoni huna pesa lakini kama umechangia CHF utakuwa na uhakika wa matibabu"alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

  Alisema uongozi wa Wilaya ya uvinza una mpango wa kukiboresha kituo cha afya cha Nguruka  kutokana na ahadi ya Muheshimiwa Rais wakati wa kampeni kukifanya kituo hicho kuwa Hospitali ya Wilaya na maandalizi yanaendelea.

  Naye Mkurugenzi wa mifuko ya jamii(CHF) kutoka makao makuu ya bima ya afya (NHIF) Eugen Mikongoti aliwataka wananchi kuchangia mfuko huo kwa wingi kwakuwa serekali nayo uwachangia kiasi kile kile walichochangia wao ambayo huitwa tele kwa tele.

  Mikongoti alisema endapo wananchi watachangia kwa wingi na hudumaza afya  zitaboreshwa zaidi kituoni hapo. "Nataka niwaambie hivi sisi wote ni wagonjwa watarajiwa, hakuna anayejua atagua lini tunachotakiwa ni kujiandaa kwa kujiunga na CHF ili tuwe na uhakika wa matibabu tutakapi ugua"alisema Mikongoti

  Kwa upande wake Meneja wa bima ya afya Mkoa wa Kigoma Elias Odhiambo alisema kuwa hali ya uchangiaji wa mfuko wa afya ya jamii kwa kata ya nguruka hairidhishi hivyo kushindwa kufikia malengo ya huduma za afya.

  Alisema kata ya Nguruka ina jumla ya kaya 6000 lakini kaya 756 ndiyo zimejiunga na kuchangia CHF.

  "Kutokana na uhamasishaji wa kujiunga na CHF tuliofanya leo hapa jumla ya kaya 868 zimejiunga na mfuko huo hapa hapa, kwakweli ni jambo zuri sana tuendelee kujiunga kwaajili ya uhakika wa matibabu pale tunapougua.
  Mkuu wa Wilaya ya uvinza Mrisho Gambo akiwahamasisha wananchi wa kata ya Nguruka kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF) kwenye uzinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Nguruka
  Mkurugenzi wa mifuko ya jamii kutoka makao makuu ya bima ya afya Eugen Mikongoti akiwahamasisha wananchi wa Nguruka kujiunga na mfuko huo.
  Mkurugenzi wa mifuko ya jamii Eugin Mikongoti(mwenye koti jeusi) akiteta jambo na Meneja wa mfuko wa bima ya afya wa Mkoa wa Kigoma Elias Odhiambo wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wananchi kujiunga na CHF kata ya Nguruka.
  Baadhi ya umati wa wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kuhamasisha kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF kata ya Nguruka.


  0 0

  MBUNGE wa Busanda (CCM) LOLENSIA BUKWIMBA ameeleza furaha yake kwa kamati maandalizi ya Tamasha hilo ambalo halikuwahi kufanyika mkoani humo na imekuwa faraja kwake kama mwakilishi wa wananchi  wa mkoa huo  unaokabiliwa na mauaji kwa walemavu wa ngozi.

  Alisema amefurahishwa  kufanyika kwa tamasha hilo mkoani Geita na mikoa mgine kwani ana imani wakazi wa mkoa huo watahamasika  kuacha mauaji ya Watanzania wasio na hatia ambao ni walemavu wa ngozi na vikongwe ambayo yanaendelea. Mbunge huyo anaelezea furaha yake, ana imani wananchi wa mkoa wa Geita watafurahi kwa sababu mkoa huo umesuswa kwa kuwapelekea matamasha ya namna hiyo na kusikia yanafanyika katika mikoa mingine kama Dar es Salaam na Mwanza.

  “Nimefurahi sana Msama kulileta Tamasha hili litakalopiga vita mauaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi, nina imani wananchi wataweza kuelimika kwa njia moja au nyingine, baada ya hapo inawezekana kabisa likaweza kubadilisha fikra na mtizamo juu ya suala hili na kupunguza kabisa mauaji haya,” anasema Lolensia.

  Alieleza kuwa limekuwa jambo la bahati kwa mkoa huo kufikiwa na tamasha hilo ambalo lina mafanikio makubwa katika kutimiza malengo yanayokusudiwa hivyo anaamini kilichokusudiwa kwa Geita kitafanikiwa kwa kiasi kikubwa.“Tunawakaribisha sana na nichukue nafasi ya pekee kumpongeza Msama kwa uamuzi wake wa kutuletea tamasha hili tunatarajia kupata mambo makubwa pia nina imani wanageita watafurahia mno kwasababu wanapenda mambo hayo ya muziki hasa huu wa Injili,” alisema Lolensia.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mama ROIDA MUHAMA mkazi wa Mkimbizi mjini Iringa, anamuuguza mwanaye aitwaye EBENEZA PEMBE anayesumbuliwa na saratani ya ngozi kwa miaka sita sasa.

  Anaomba msaada wa hali na mali ili aendelee kumtibia mwanaye, Anahitaji kiasi cha fedha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuendelea na matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

  Kwayeyote atakayeguswa tuma mchango wako kwa njia ya M-pesa 0767834377 au Tigo pesa 0717353529 kwa SILVANUS KIGOMBA au 0762 174 573 ROIDA MUHAMA (Mama wa Ebeneza).
  Mtoto EBENEZA PEMBE anayesumbuliwa na Kansa ya Ngozi kwa zaidi ya Miaka 6 anahitaji Msaada wa fedha zitakazo muwezesha kwenda kupatiwa Matibabu katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
  Mtoto EBENEZA PEMBE aliyevaa shati la Bluu akiwa amebebwa na Mama yake Mzazi Bi ROIDA MUHAMA mkazi wa eneo la  MKIMBIZI manispaa ya Iringa, kushoto ni mtoto mwingine wa Bi ROIDA wakiwa katika Picha ya Pamoja.
  ...................
  Nimeguswa na maumivu na mateso anayoyapata mtoto Ebeneza kwa zaidi ya miaka 6 nimejitolea kusaidia kusambaza taarifa za Ugonjwa wake ili kukusanya michango kwaajili ya matibabu yake. 

                       Naomba ushirikiano wenu rafiki zangu na Mungu awabariki sana.

  0 0

  MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA(TRA) yafunga mradi wa miaka minne kati ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Shirika la  maendeleo la Japani (JICA) la Serikali ya Japani  mara baada ya  mradi huo kumaliza muda wake.

   Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurgenzi wa Rasilimali watu Mamlaka ya Matapo Tanzania(TRA), Victor Kimaro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa  Mradi huo umewanoa wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania pamoja na wanafunzi 608 na umeghalimu kiasi cha dola za kimarekani milioni3.5.

  Pia amesema mradi huo wa Shirika la  Maendeleo la Japani (JICA) wa Serikali ya Japani umesaidia kuboresha mafunzo kwa  wafanyakazi na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).

  Mwisho wa Mradi huo ni mwamzo wa kuanzisha mradi mwingine wa mafunzo na kuboresha ukusanyaji wa mapato hapa nchini.

  Mradi uliokuwa unaitwa  'PROJECT FOR ENHANCEMENT OF TAXATION TRAINING IN TANZANIA.'
   Kaimu Mkurgenzi wa Rasilimali watu Mamlaka ya Matapo Tanzania(TRA), Victor Kimaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusina na kufunga mkataba wa miaka minne kati ya Tanzania na Japani mkataba ambao ulikua unatoa mafunzo ya kukusanya Kodi hapa nchini kwa wanafunzi wa chuo cha kodi (TRA) pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA). Kushoto ni  Msimamizi wa Mradi wa Shirika la  maendeleo la Japani (JICA), Toshio Nagase.
  Msimamizi wa Mradi wa Shirika la  maendeleo la Japani (JICA), Toshio Nagase akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. kulia ni Kaimu Mkurgenzi wa Rasilimali watu Mamlaka ya Matapo Tanzania(TRA), Victor Kimaro.
   Mkuu wa Chuo cha Kodi (TRA), Isaya Jairo(Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kufunga mkataba wa mradi wa miaka minne ambao ulikuwa unatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na wanafunzi wa chuo cha kodi. Kulia ni Kaimu Mkurgenzi wa Rasilimali watu Mamlaka ya Matapo Tanzania(TRA), Victor Kimaro.
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akitoa salamu zake wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa wa Dodoma baina yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe Mhe. Chiku Gallawa (hayupo pichani) Machi 22,2016.
   Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akitoa salamu zake wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa wa Dodoma baina yake na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (hayupo pichani) Machi 22,2016.
   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (wa kwanza kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa huo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Chiku Gallawa (wa tatu kushoto) Machi 22,2016.

  0 0

     Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
   
  MPANGO wa Kunusuru Kaya Masikini Tanzania  (TASAF III) umetoa zaidi ya shilingi Milioni 137.8 kwa kaya masikini 3627 katika vijiji 57 wilayani Serengeti mkoani Mara.
   
  Hayo yamesemwa na Mratibu wa TASAF Wilaya ya Serengeti Bi Nancy Nzota alipokuwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Gesarya, Kata ya Rung’abure  kuhusu malipo ya kaya hizo kuwa yamefikia awamu ya tano.
   
  Alisema malipo ya fedha hizo yameyotolewa katika kipindi cha utekelezaji wa mpango huo kwa mwezi Machi hadi Aprili 2016.
   
  “Fedha hizi mnazopewa ni mbegu na mnapaswa kuzitumia kukidhi mahitaji muhimu yakiwemo ya elimu, afya na kuanzisha shughuli za uzalishaji” alisema Bi Nancy.
   
  Bi Nancy aliongeza kuwa, watendaji wa vijiji wanatakiwa kubaini kaya zinazotumia fedha hizo kinyume na matakwa ya mpango huo ambapo amewataka watendaji watakaogunduliwa waondolewe katika uwakilishi wa kaya na mchakato wa kubadili wasimamizi/wawakilishi wapya wa kaya zao ufanyike kwa utaratibu maalumu.
   
  Aliwaonya wanufaika wa mpango huo kutokutumia fedha hizo kwa shughuli zinazokinzana na mpango huo kwani kufanya hivyo hakutawatoa wananchi katika hali ya umasikini.
   
  Alisema kuwa elimu hasa ya ujasiriamali ilishatolewa kwa wanufaika katika kila kijiji juu ya kuanzisha shughuli za ufugaji, kilimo na biashara ndogo ndogo.
   
  Aliongeza kuwa pia elimu hiyo huendelea kutolewa mara kwa kwa mara na wawezeshaji wa mpango wa TASAF ambao hutoa elimu hiyo kwa wananchi katika kila awamu ya malipo.
   
  Mpango huu ulizinduliwa mkoani Dodoma, Agosti 2012 na Rais mstaafu, Dk Jakaya Kikwete, ambapo kwa Wilaya ya Serengeti malipo kwa kaya masikini lilianza rasmi Julai 2015 na limeonesha kuanza kuzinufaisha kaya hizo.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
   
  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) imesema suala la Shirika la Usafiri Mkoa  Dar es Salaam (UDA) wameliweka pembeni kutokana na baadhi ya wajumbe kubadilishwa katika kamati hiyo ikiwa ni pamoja na unyeti wa suala hilo kwa masilahi mapana ya wananchi wa jiji la Dar es Salaam.
   
  Akizungumza leo Kaimu Makamu Mwenyekiti wa LAAC , Abdallah Chikota amesema kuwa wajumbe wapya lazima wasome taarifa  ya shirika hilo , ili waje na ushauri ambao utasaidia kumaliza suala hilo.
   
  Amesema kuwa kamati itafanya kila jitihada za kukutana na jiji katika kuweza kushughulikia masuala mawili ambayo  ni UDA pamoja na Kiwanda cha Nyama yamekuwa yakileta matatizo kwa wananchi ya sitofahamu.
   
  Aidha amesema kuwa suala hilo kuwa suala la wa UDA linatakiwa kila taarifa kutoka wadau mbalimbali ziweze kupitiwa katika kuweza kuepuka kufunguliwa kesi zisizo kuwa msingi.
   
  Chikota ametaka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam irudishe ardhi ya kiwanda cha Nyama (Tanganyika Packers) katika mamlaka yake huku huku wakisubiri hatima ya kiwanda hicho.
   
  Waziri wa nchi ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amesema kuwa wanakubaliana na kamati kutokana na unyeti   wa  suala la Uda  kwa masilahi mapana kwa wananchi.
   
  Simbachawene amesema wamechoshwa na suala la uda na Kiwanda cha nyama na kuahidi akipata muda atakutana na wadau ili kuondokana mlolongo wa kesi zitakazotokana na ufumbuzi wa UDA  na ufumkwa minajili ya kulinda masilahi ya wananchi wa jiji la Dar es Salaam.
   
  Nae, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema kuwa yeye ni mgeni hivyo anahitaji kupata muda wa kusoma taarifa mbalimbali juu ya hoja ya UDA pamoja na suala la kiwanda cha Nyama.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(Kulia) akionesha kitabu cha sera ya wazee ambayo inatarajiwa kuandikiwa mswaada wa kuwa sheria na kupelekwa Bungeni kushoto ni Katibu Mkuu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Sihaba Nkinga.
   2 Mwenyekiti wa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali akizungumza katika kikao cha wazee wa mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy mwalimu(Kushoto).

  Baadhi ya wazee wa mkoa wa Dar es Salaam wakifatilia kikao chao na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kilichofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.


  Na Raymond Mushumbusi- MAELEZO
  SERIKALI imejipanga kuipa nguvu Sera ya wazee nchini kuwa Sheria itakayowasaidia wazee kujikwamua katika changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa sasa.

  Waziri Ummy amesema wazee wanakumbwa na changamoto nyingi katika maisha yao ya kila siku nakusema kuwa azma ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wazee wanapata mahitaji yao muhimu ambayo ni huduma ya afya,haki ya kuwezeshwa kiuchumi na uwakilishi katika vyombo vya maamuzi.

  “Mimi mwenyewe nalichukua jukumu hili la kufanikisha kuandikwa kwa mswaada wa Sheria ya wazee nchini na kuipeleka katika Bungeni mwezi Septemba ili tuwe na Sheria itakayowezesha kuwabana watu ambao watakaidi kutekeleza masuala yahusio wazee” Alisema Mhe.Ummy.

  Naye mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Mzee Hemed Mkali akiwasilisha mada katika kikao hicho amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwajali na kuwapa kipaumbele wazee kwa kuwapa wizara ambayo itawasaidia kutatua changamoto zinazowakabili na wanaimani na Waziri husika na watashirikiana naye ili kufanya wazee wa Tanzania waishi katika maisha mazuri.

  Aidha Waziri Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote nchini katika Hospitali zilizopo chini yao kuanzisha na kuboresha madirisha kwa ajili ya wazee na kuongeza kuwa huduma kwa wazee ni bure kuanzia kumwona Daktari, Vipimo mpaka madawa na kuhamasiha wazee kuungwa kwenye Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) ambao unatoa huduma za afya katika maeneo mengi zaidi.

  Kikao hiki cha wazee wa mkoa wa Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto dhumuni kubwa ni kwa wazee ni kuomba kukutana na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli  kujadili mshtakabali wa maendeleo ya wazee nchini.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigela akitoa taarifa ya hali ya miundombinu katika mkoa wa Tanga kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ofisini kwake.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa pili kulia) akimwonesha moja ya nyaraka Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (wa pili kushoto) kabla ya kusaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa tatu kulia) pembeni ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa.


  0 0

  Na Zuena Msuya

  Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amepokea ripoti maalumu ya kumaliza mgogoro wa wananchi wa Nyamongo na mgodi wa wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia North Mara uliodumu kwa miaka 6 sasa.

  Akizungumza mjini Tarime Mkoani Mara baada ya kupokea ripoti hiyo Prof. Muhongo ameshauri wananchi wa Tarime kuwa watulivu wakati akiendelea kuisoma ripoti hiyo na kutolea majibu mambo yalioyo andikwa katika riporti hiyo.

  Profesa Muhongo alisema anaimani mambo yote yalioandikwa katika ripoti hiyo ni mawazo ya wananchi waliohojiwa na  atashangaa endapo kuna mtu atajitokeza  kuikataa.

  Kwa upande wake mkuu wa Wilaya Tarime,Glorious Luoga alisema ripoti hiyo itatoa majibu stahiki kwa wanaohitaji kulipwa na hata wasiostahili hivyo wananchi wakae tayari kupokea utekelezaji wa ripoti baada ya kusoma na kupitishwa na Waziri.

  Naye Mbunge wa Tarime vijijini John Heche alisema kuwa anaimani na ripoti hiyo kuwa itatenda haki kwa wananchi wake wa Nyamongo ili kutimiza  ahadi ya Rais aliyoitoa wakati akiomba kura kuwa hatamaliza kabisa tatizo la Nyamongo lililodumu kwa muda mrefu.

  Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhandisi John Nayopa alisema kamati hiyo imepokea malalamiko zaidi ya 4400 ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi,malalamiko ambayo yalilenga masuala ya fidia ya ardhi,athari za shughuli za mgodi hasa upande wa mazingira,uvamizi wa mgodi,sakata la tegesha na Askari kutuhumiwa na kunyanyasa na kutesa wananchi.

  Kamati hiyo iliundwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mwezi mmoja uliopita ina wajumbe 27,19 wataaalamu wa Serikali, na Wenyeviti wa vitongoji 80.
  Mwenyeki wa kamati John Nayopa akimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo,Taarifa ya kamati ya kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa Nyamongo na Kampuni ya mgodi wa dhahabu ya Acacia North Mara.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo,akionesha taarifa aliyokabidhiwa na Kamati hiyo ambapo ameahidi kuisoma na kuitolea majibu yanayostahili ndani ya kipindi cha wiki tatu tangu Machi 23,2016 alipokabidhiwa taarifa hiyo.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, akizungumza jambo mara baada ya kupokea Taarifa ya utekelezaji kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa North Mara katika eneo la Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara na Mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia wa North Mara.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo akimjulia hali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Ibrahim Matovu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) anapo endelea kupatiwa huduma, Dar es Salaam leo, ambapo anatarajiwa kuruhusiwa kutokana na haliyake kuendelea vizuri. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA )
   Diwani wa Kata ya Kilomo, Bagamoyo, Hassan Usinga (Wembe) akimjulia hali Afisa Maendeleo ya Jamii ya Bagamoyo Julius Mwanganda mara alipofika katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) anapopatiwa matibabu kutokana na ajali mbaya iliyotokea mkoani  humo hivi karibuni
   Diwani wa Kata ya Maboga iliyopo wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa, Vemi Chambala akimsimulia   Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo (aliyefunga mikono) wakati alipofika katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI)  Muhimbili, kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya Bagamoyo  ambapo wanapata matibabu kutokana na ajali mbaya iliyotokea mkoani humo
   Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo, akimjulia hali Afisa Maendeleo ya Jamii ya Bagamoyo Julius Mwanganda

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ileje Rosemary Staki pamoja na Wakuu wa Wilaya kutoka Wilaya mbalimbali wakiongozana na vijana wa Scauti waliobeba mashada kuelekea kanisani tayari kwa ibada.
  Vijana wa Scauti wakiwa wamebeba jeneza lililohifadhi mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Marehemu Bi. Sarah Dumba mara baada ya kuwasili nje ya viwanja vya kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mkoani Njombe.
  Baadhi ya Wananchi waliohudhuria kwenye ibada ya kumuaga Marehemu Sarah Dumba.
  Wanafamilia wa Marehemu Sarah Dumba wakionesha sura za huzuni na Majonzi baada ya kuondokewa na mpendwa wao.
  Viongozi wa dini wakiongozwa na Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mkoa wa Njombe Askofu Isaya Japhet Malenge wakiombea dua mwili wa marehemu.

  0 0

  Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Dodoma siku ya Jumanne na Jumatano, Machi 22-23, 2016. 

  Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 97 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.


  PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.  Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na  Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.
  RC wa Dodoma, Jordan Rugimbana, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3

  Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana, na uzinduzi ulihudhuriwa pia na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Dodoma ambaye amehamishiwa mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.  Watu takribani 180 walihudhuria.  Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Dodoma, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe  wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye Halmashauri. 

  Mkoa wa Dodoma una Halmashauri  nane, ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, na Halmashauri ya Mji wa Kondoa.
  Dk. Conrad Mbuya wa PS3 akitoa mada wakati wa uzinduzi wa mradi mkoani Dodoma.

  PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID.  Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni:  Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute. 


  Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.

  Mkurugenzi wa Mradi wa PS3, Dk. Emmanuel Malangalila, akitoa mada kwenye uzunduzi wa mradi wa PS3 mkoani Dodoma

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0
 • 03/23/16--16:32: THE LEGENDS FAMILY TOUR 2016
 • THE LAST WEEKEND OF THE MONTH PARTY Ndio Hii Hapa, Ijumaa Hii Tunakutana Club Rouge Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel Na Jumamosi Tunakutana Mzalendo Pub Millenium Tower Kijitonyama.

  WATU 50 WA KWANZA KUFIKA WATAKABIDHIWA NON STOP CD MPYA YA MWEZI HUU

  0 0

  Zuriel lends her voice to raising the standard of tertiary Education in Africa, starting with Nigeria, at a Foundation event at the Waldorf Astoria in New York.

  0 0

  Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager leo imeibuka na ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya wenyeji Chad katika mchezo uliomalizika jioni hii katika uwanja wa Omnisport Idriss Mahamat Ouya uliopo jijini N’Djamena.

  Kikosi cha Stars kilicheza vizuri kwa maelewano kwa lengo la kusaka bao la mapema, safu ya ushambuliaji ilikuwa mwiba kwa walinzi wa Chad katika dakika 30 za kipindi cha kwanza na kukosa nafasi zaidi ya nne za wazi kupitia kwa Ulimwengu, Farid, Samatta na Kazimoto.

  Nahodha Mbwana Samatta ambaye leo alikua akikiongoza kikosi cha Taifa Stars kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa katika nafasi hiyo, aliipatia Tanzania bao la kwanza dakika ya 30 akimalizia pasi ya Farid Mussa aliyewataoka walinzi wa Chad kabla ya kumpasia mfungaji.

  Mara baada ya bao hilo wenyeji walikuja juu kusaka bao la kusawazisha, lakini ukuta wa Stars uliokuwa chini ya Kelvin Yondani, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi na mlinda mlango Aishi Manula walikua imara kuokoa michomo hiyo.

  Kipindi cha pili Stars ilianza kwa kufanya mabadiliko, Mwinyi Kazimoto aliyeumia alimpisha John Bocco na kuongeza nguvu katika sehemu ya ushambuliaji, na kuwapa wakati mgumu walinzi wa Chad.

  Dakika ya 73, David Mwantika aliingia kuchukua nafasi ya Farid Mussa, huku Ibrahim Ajibu akiingia dakika ya 80 kuchukua nafasi ya Thomas Ulimwengu, mabadiliko ambayo yaliongeza nguvu kwa stars na kujilinda mpaka mwisho wa mchezo.

  Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Chad 0 –1 Tanzania.
  Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa mara baada ya mchezo wa leo amewapongeza wachezaji wake kwa kupambana ugenini na kuibuka na ushindi huo japo mazingira ya joto yalikuwa tatizo kwa vijana wake katika muda wote wa mchezo.

  Mkwasa amesema leo vijana wake wamecheza dakika 90 za kipindi cha kwanza na kuweza kupata ushindo, hivyo akili yao sasa ni katika mchezo wa marudiano utakaocheza Jumatatu ya Pasaka jijini Dar es salaa, ambapo amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kuja kuwapa sapoti.

  Taifa Stars inatarajiwa kurejea nyumbani kesho usiku kwa usafiri wa shirika la ndege la Ethiopia, ikitoka N’Djamena Chad saa 8 mchana kupitia Addis Ababa na kasha kuwasili uwanja JNIA Nyerere majira ya saa 7 usiku.

  Stars iliwakilishwa na Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mwinyi Haji, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Himid Mao, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/John Bocco, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu/Ibrahim Ajibu, Farid Mussa/David Mwantika.

  Chad: Diara Gerrad, Asselmoun Massam, Nadjim Haroun, Abaya Cesar, Kelvine Nicaise, Ndoumnan Herman, Beadoum Monde/Altama Saana, Mahama Azarack, Djimenan Leger/Aldo Mathew, Ndouassel Ezekliel, Ninga Casimin

  0 0

  Konseli Mkuu wa Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Jeddah, Saudi Arabia, Suleiman Saleh amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa SALEH SAEED ESTABLISHMENT FOR CONTRACTING AND CATTLE IMPORTS, Saleh Said Bakhatab,  ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa mifugo nchini Saudi Arabia, Bw. Saleh alimkaribisha Bw. Bakhatab ofisi kwake Jeddah, ambapo alipata maelezo ya kina kutoka kwa mgeni wake huyo kuhusiana na utayari wake wa kununua na kusafirisha mifugo mbali mbali wakiwemo ng'ombe, kondoo na mbuzi kwa ajili ya soko la Saudi Arabia.

  Bakhatab alibainisha kwamba kwa miaka 25 amekuwa akinunua kondoo, mbuzi na ng'ombe kutoka Sudan, Ethiopia, Somalia, Australia, Romania na Uruguay na utafiti wake umeonyesha kwamba Tanzania ina mifugo yenye ladha nzuri kutokana na aina ya malisho bora, Kwa mantiki hiyo, Bakhatab alimuomba Konseli Mkuu kumuandalia miadi na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye dhamana ya sekta hiyo ili kukamilisha azma yake hiyo.

  Aidha Bakhatab alimweleza Saleh kwamba kuna mambo ya msingi ambayo katika kufanikisha biashara hiyo ni vyema yakaandaliwa ili biashara ifanyike kisasa na kwa ufanisi mkubwa. Mambo hayo ni pamoja na kuandaliwa utaratibu endelevu wa kupatikana kwa mifugo hiyo kulingana na mahitaji ya soko la Saudi Arabia, Pili, kuandaa mazingira elimishi kwa wafanyakazi wa bandari na viwanja vya ndege ili wawe na ufahamu wa kina kuhudumia mifugo inayosafirishwa ambapo alionyesha utayari wake kusaidia katika kuleta video za mafunzo hayo.

  Pia alishauri kuandaliwa eneo mahususi la Karantini kwa mujibu wa taratibu za kiafya za kimataifa ambapo mifugo inahifadhiwa na kupata huduma ya uchunguzi sahihi kabla ya kusafirishwa. Mwisho, Khatab alipendekeza mkutano baina yake na viongozi wa Wizara husika nchini Tanzania ili kuweka mikakati ya haraka ya kufanyika kwa biashara hiyo.

  Kwa upande wake Suleiman Saleh alimhakikishia Bakhatab kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Joseph Magufuli imeanza kazi kwa kasi ya aina yake kwa kujenga mazingira rafiki na yenye ufanisi wa hali ya juu na kumuahidi kwamba atawasiliana na viongozi wa Wizara ya Kilimo na Mifugo ili wampokee atakaposafri kutembelea Tanzania hivi karibuni.
  Konseli Mkuu wa Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jeddah,Saudi Arabia, Suleiman Saleh, akimkaribisha ofisini kwake Mmiliki wa Kampuni ya SALEH SAEED ESTABLISHMENT FOR CONTRACTING AND CATTLE IMPORTS ya Saudi Arabia, Saleh Saeed Bakhatab, tayari kwa mazungumzo.
  Bw. Suleiman Saleh akiendelea na mazungumzo na Bw.Bakhatab.

  0 0


  0 0
 • 03/23/16--23:33: DONDOO ZA MAGAZETI LEO

older | 1 | .... | 1169 | 1170 | (Page 1171) | 1172 | 1173 | .... | 3272 | newer