Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1168 | 1169 | (Page 1170) | 1171 | 1172 | .... | 3283 | newer

  0 0
  0 0

  Na Lilian Lundo-MAELEZO

  Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNFPA) limekabidhi simu za kufundishia huduma ya uzazi salama kwa vyuo vya Afya pamoja na taasisi zinajihusisha na masuala ya afya ya mama na mtoto ili kuboresha huduma kwa akina mama wajawazito na watoto wanaozaliwa.

  Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam Machi 21, 2016 baina ya shirika la UNFPA na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

  Akikabidhi vifaa hivyo Mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Natalia Kanem alisema wanashirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukuza na kuboresha elimu juu ya uzazi salama na kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

  “Dhumuni la matumizi ya simu za kufundishia uzazi salama ni kutoa elimu kwa wauguzi na wakunga walioko vijijini na maeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi ili kuwasaidia kupata elimu ya uzazi salama na kupunguza vifo vya mama na mtoto,” alisema Natalia.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowele ambaye alimwakilisha Mganga Mkuu wa Serikali alisema kuwa simu hizo zitarahisisha ufundishaji kwa wauguzi na wakunga kwani zitawawezesha kujifunza masuala yote yanayohusu uzazi salama bila kuondoka kwenye vituo vyao vya kazi.

  Dkt. Gowele aliongeza kwa kusema kuwa, simu hizo zitakuwa na mafunzo ya uuguzi ambayo yako katika mitaala ya vyuo vya uuguzi na mtumiaji wa simu hiyo anaweza kuuliza swali lolote linalohusu uzazi salama akapata majibu kwa njia ya sauti, picha na maandishi.

  Aidha, simu hizo zinachajiwa kwa kutumia umeme wa mwanga jua, umeme wa wakawaida na inatumia betri pia, hivyo inaweza kutumika hata maeneo ambayo bado hayajafikiwa na umeme.

  Kwa upande wake Mtaalamu wa Afya ya Mama na Mtoto wa UNFPA Felister Bwana alisema kuwa, simu hizo zimegawiwa kama majaribio kwa baadhi ya vyuo vya Afya na na taasisi zinazojihusisha na uzazi salama, endapo teknolojia hiyo italeta mafanikio yanayotarajiwa simu hizo zitagawanywa kwa vyuo vyote vya uuguzi na hospitali nchini.

  Vyuo na taasisi ambavyo vimepokea vifaa hivyo ni pamoja na Chuo cha Afya Kilosa, Bugando, Newala, Nachingwea, Bagamoyo, Geita, Kahama, Maswa, Sengerema, KCMC, Zanzibar, Ifakara pamoja na taasisi ya TAMA na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

  Kwa mujibu ya sensa ya mwaka 2010, jumla ya vifo 454 vimekuwa vikitokea  katika kila vizazi hai 100,000 kwa mwaka, idadi hiyo imepungua na kufikia vifo 432 kwa kila vizazi hai 100,000 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.
  Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle akipokea simu ya kufundishia uzazi salama kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la UNFPA Natalia Kanem (katikati) huku wakishuhudiwa na Geeta Lal kutoka makao makuu ya UNFPA.
  Mwalimu wa Uuguzi Asha Ally Khamis (wa pili kulia) kutoka Chuo cha Afya Mbweni Zanzibar akipokea simu ya kufundishia uzazi salama kutoka kwa Natalia Kanem, wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini na Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Otilia Gowelle, kulia ni Nayanesh Bhandutia kutoka makao makuu ya UNFPA. 
  Mkuu wa Chuo cha Uuguzi Newala Tecla Ungele (wa kwanza kulia) akipokea seti ya simu ya kufundishia uzazi salama kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Otilia Gowelle , wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Natalia Kanem

   


  0 0

  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM )umesema ushindi alioupata mgombea wa CCM Rais Dk Ali Mohamed Shein kwamba ni kielelezo cha kuimarika kwa msingi ya demokrasia Zanzibar na kukubalika kwa mgombea huyo kwa wapiga kura na wananchi wa Zanzibar . 


  Umesema ushindi huo sasa umehitimisha mvutano na maneno yaliyokuwepo ambayo yalikuwa yakienezwa kwa makusudi ,  kupotoshwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani visiwani humu. 


  Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka ameeleza hayo Afisi kuu ya UVCCM Kikwajuni wakati akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kumaliza kwa maandano makubwa yaliyoandaliwa na UVCCM kusherehekea ushindi wa CCM uliotangazwa  na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar  Jecha Salim Jecha kulitangaza jina la Dk shein mshindi wa uchaguzi huo. 


  Alisema ushindi alioupata Dk shein kwa kupata jumla ya kura  299982sawa na asilimia 91.4 kumeidhihirisha dunia jinsi ya kukubalika kwa kiongozi huyo katika aina ya utawala na uongozi wake.  "Ameonyesha umahiri, upeo na uwezo mkubwa  katika kuongoza serikali ya umoja wa kitaifa kwa miaka mitano iliopita; amekuwa mstahamilivu na nguzo muhimu ili jamii isiendelee kugawanyika "alisema shaka 


  Kaimu Katibu Mkuu alisema aina ya uongozi wa Rais Dk Shein ni wa kipekee na kwamba kama angekuwa si mtawala mwenye maarifa mapana na uvumilivu wa kisiasa serikali hiyo anaamini ingevunjika mapema.  Shaka alisema serikai za mseto za Zimbabwe na Kenya ziliweza kuyumba  na kwamba hazikudumu kutokana na baadhi ya viongozi wake kukosa kuaminiana, kuvumiliana na kustahamiiiana .


  "Ushindi huu ni pigo jipya kwa chama cha CUF ambacho kimesusia uchaguzi wa marudio bila sababu za msingi, ushindi wa Dk shein  naamini utaleta mageuzi makubwa ya kiuchumi  na kuishangaza dunia katika maendeleo ya demokrasia "alisems Shaka .Aidha alisema anatarajia serikali mpya ijayo haitakuwa na viongozi wababaishaji na badala yake watateuliwa wazalendo, wachapa kazi na watu wenye uchungu wa kiyatetea Mapinduzi bila kushiriki usaliti. 


  Hata hivyo Shaka alisema anaamini kuwa chini ya uongozi wa kipindi cha pili cha utawala Dk Shein na sera makini za ccm ,ataendelea kusimamia uadilifu serikalini,  kujenga umoja wa kitaifa nchini  pamoja na kuwatumikia wananchi ipasavyo na kudumisha huduma za jamii . "UVCCM tuna matumaini makubwa na na Dk shein katika awamu mpya ya ushindi wake; ataunda baraza la mawaziri makini, na hatutosita kumpongeza kila atakapofanya vizuri  pia hatutakaa kimya pale tutakapoona mambo  hayaendi ipasavyo "alisema .


  Shaka anewahimiza vijana mahali popote walipo kumuunga mkono Dk shein na kuisaidia serikali yake ili iweze kupiga hatua za kimaendeleo na kwamba hatawaangusha katika uongozi wake.

  "Tunahitaji kutoka mahali tulipo na kufika tunakotarajia, tungependa kuona uwajibikaji mpya,utendaji wenye kubeba dhamira na utekelezaji wa malengo na sera hivyo ni wazi kuwa   wapatikane watu wenye uwezo na upeo ya kukwamua nchi mahali ilipo sasa" 

  0 0

  TWAWEZA, IBM NA BITES & BYTES WAANDAA MKUTANO WA KITEKNOLOJIA MACHI 29 NA 30 MWAKA HUU.

  Mwanzilishi wa Bites& Bytes, Lilian Madeje (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na shindano la kiteknologia litakalofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam Machi 29 na 30 mwaka huu. Kulia ni Mkuu wa Utafiti Twaweza, Elivis Mushi.
  NBV wa benki ya CBA Group, Eric Luyangi(Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kutoka kushoto ni Risha Chande, mwanzilishi wa Bites &Bytes, Lilian Madeje na wamwisho kulia ni
  Mkuu wa Utafiti Twaweza, Elivis Mushi.

  ASASI isiyo ya kiraia ya Twaweza na Kampuni ya IBM ikishirikiana na Bites &Bytes imeandaa mkutano mkubwa wa Kiteknolojia na uvumbuzi unaoitwa Bites &Bytes ambao utafanyika Machi 29 na 30 mwaka huu katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

  Hayo yamesemwa na mwanzilishi wa Bites &Bytes, Lilian Madeje wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  Liliani amesema kuwa lengo mkutano huo ni kuhamasisha uendelezaji wa mawazo mpya pamoja na uvumbuzi wa mawazo mapya ya kibiashara ili aanzishaji wapya wa mawazo waweze kuwapa mwanya wa kubadilishana mawazo na wadau wengine ili waweze kushirikiana kwa pamoja.

  Pia Liliani amesema kuwa washiriki 16 wa mechanguliwa kushiriki katika shindano hilo la ubunifu wa biashara ambapo washiriki hao watashindania kuwania kitika cha shilingi milioni tano(5,000,000).

  Nae NBV wa benki ya CBA Group, Eric Luyangi amesema kuwa katika shindano hilo la Software Developers wanalenga kuleta suluhisho la kuwezesha kufikisha takwimu na tafiti mbalimbali za Twaweza kwa kutumia mitandao tofauti tofauti.

  0 0

  Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika wa Usuluhishi wa Mgogoro wa Libya amewasili jana jijini Tunis nchini Tunisia kushiriki Mkutano wa 8 wa Nchi Jirani ya Libya. Mkutano huo ulioitishwa na Serikali ya Tunisia ni muendelezo wa jitihada za nchi jirani kusaidia kuleta hali ya amani na usalama nchini Libya. Rais Mstaafy amewasili Tunis akitokea Salalah nchini Oman aliposhiriki katika Mkutano wa Kamati ya Bunge la Kuandika Katiba ya Libya.

  Akiwa jijini Tunis, Rais Mstaafu Kikwete amefanya mazungumzo jana na Waziri wa Masuala ya Maghreb, Arab na Afrika wa Algeria Mheshimiwa Abdelkader Messaleh aliyemtembelea hotelini kwake. Katika mazungumzo yao, Waziri Messaleh alimpongeza Rais Mstaafu Kikwete kwa kuteuliwa na Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika kusuluhisha mgogoro wa Libya. Alimuelezea hali ya usalama na kisisa ya Libya na mtizamo wa nchi yake juu ya namna bora ya utatuzi wa mgogoro huo.
  Alimhakikishia Rais Mstaafu ushirikiano wa Serikali ya Algeria katika jukumu lake alilokabidhiwa na Umoja wa Afrika.

  Kwa upande wake, Rais Mstaafu Kikwete alimshukuru Waziri Abdelkader Messaleh kwa maelezo aliyompatia na ushirikiano aliomuahidi. Alimuelezea matumaini yake ya kupatikana kwa suluhu ya mgogoro huo madhali nchi jirani na Libya na Umoja wa Afrika zitashirikiana na wadau wote kuhakikisha mgogoro huo unatatulika. Alisisitiza kuwa hatimaye suluhu ya kudumu ya mgogoro wa Libya uko mikononi mwa wananchi wa Libya wenyewe.

  Katika ziara yake nchini Tunisia, mbali na kuhudhuria Mkutano wa 8 wa Nchi Jirani na Libya, Rais Mstaafu Kikwete anatarajiwa pia kukutana na Waziri Mkuu Mteule na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Libya (Presidency Council) Mheshimiwa Fayez Al-Sarraj, wadau wengine wa Libya pamoja na kutembelea Ofisi ya Ujumbe wa Umoja wa Afrika kwa Libya iliyoko jijini Tunis. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete anatarajiwa kurejea nchini tarehe 25 Machi, 2016.
  Mwakilishi Maalum wa AU wa Mgogoro wa Libya akizungumza na Waziri wa Masuala ya Maghreb, Arab na Afrika Mheshimiwa Abdelkader Messahel.
  Mwakilishi Maalum wa AU wa mgogoro wa Libya akiagana na Waziri Abdelkadir Messahel wa Algeria baada ya mazungumzo yao.

  0 0


  0 0

  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lina sikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali January Claudio Kisanko (mstaafu) kilichotokea tarehe 21Machi 2016.

  Meja Jenerali January Kisanko (mstaafu) alizaliwa mwaka 1945 katika kijiji cha Mkima, Tarafa ya Lyangalile, Wilaya ya Sumbawanga. Alipata Elimu ya Msingi Mkoani Rukwa na baadaye elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya wavulana Agakhan ambayo kwa sasa ni shule ya Sekondari Tambaza, hadi alipohitimu kidato cha Sita mwaka 1966.

   Marehemu Meja Jenerali January Claudio Kisanko (Mstaafu) alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 31 Mei, 1967 na kutunukiwa Kamisheni tarehe 24 Julai, 1969.Marehemu alilitumikia Jeshi kwa muda wa miaka 35 na mwezi 1 hadi alipostaafu utumishi Jeshini tarehe 30 Juni 2002.

   Katika utumishi wake marehemu alishika Madaraka mbalimbali Ikiwemo Kamanda wa patuni Nachingwea 1969 hadi 1970, Kamishina wa Mipango na Sera katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa 2001, madaraka ambayo alikuwa nayo hadi alipostaafu tarehe 30 Juni 2002.

  Marehemu Meja Jenerali January Kisanko (Mstaafu) alifariki dunia tarehe 21 Machi, 2016 katika Hospitali ya TMJ Dar es salaam. Ameacha Mke na Watoto. Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 28 Machi, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na mazishi yatafanyika katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, saa 10:00 jioni.

  MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
  MEJA JENERALI JANUARY KISANKO (MSTAAFU)
  AMINA

  Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
  S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
  Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638

  0 0


  0 0


  0 0


  0 0
 • 03/22/16--21:00: UNFINISHED HOUSE FOR SALE
 • The plot on which the house exists is located at Tegeta - Mivumoni via Madale road, Five kilometers (5 kms) from Wazo Cement Factory over a gravel road all time accessible by any means of transport.
  The plot is Eight hundred square meters (800m2) in size, with lots of space left for car park, garden and even a servant quarter. The building comprises of 4 bedrooms of which 2 are self contained, spacious lounge, dinning, kitchen, public toilet and bathroom, 2 verandas. It has reached roofing stage.

  Property is legally owned by one person with Purchase (Ownership) documents witnessed and approved by Local Government. Most of the neighbouring plots are surveyed.
  The area is quite ideal for residencial and commercial use with facilities like Electricity and Tap water accessible. Neighbouring landmarks are residencial houses, St. Patrick secondary school, vocational training college, Mivumoni dispensary and TAG church.
  For more details; Call, Sms or WhatsApp: +255715902270 or Email: philipbenedict88@yahoo.com

  0 0

  Mlezi wa kituo hicho cha Iringa Sober Hous Bw Godwin Msillu kushoto akiwa na baadhi ya vijana waliokuwa watumiaji wa dawa za kulevya ambao wanaishi kituoni hapo .
  Shadrack John ambae ni anaishi kituo cha Iringa Sober House aliyetoka mkoa wa Arusha akijisomea Biblia baada ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya .

  Na MatukiodaimaBlog.

  KAMANDA wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa  Iringa Bw Salim Asas ameunga mkono kwa vitendo mapambano ya vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini yaliyoanzishwa na Rais Dr John Magufuli kwa kusaidia uanzishwaji wa kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya mkoani hapa.

  Bw Asas ambae wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu alipata kuweka bayana mkakati wake wa kusaidia vijana walioathiriwa na matumizi ya madawa ya kulevya ameungana na kituo cha Iringa Sober House kilichopo Semtema katika Manispaa ya Iringa kuwasaidia vijana hao ambao afya zao zimeathiriwa na madawa ya kulevya kwa kuwakusana na kuwapatia tiba.

  Akizungumza na mtandao wa matukiodaima leo Dr Alli Ngalla ambae ni Mkurugenzi wa NGOs ya Foundation for ellevition of drug eddiction anda sufferings (FADAS) wameanzisha kituo cha kutoa huduma kwa waathirika wa madawa ya kulevya cha Iringa Sober House ambacho kimeanza kufanya kazi chini ya ufadhili mkubwa wa Bw Asas .

  Alisema kuwa kituo kituo hicho toka kimefunguliwa kina zaidi ya mwezi mmoja ambapo jumla ya wategemezi 7 ambao wanahudumiwa katika kituo hicho pamoja na wasimamizi watatu ambao pia walikuwa ni watumiaji wa dawa za kulevya ambao kwa sasa waliacha .

  " Kwa kweli kuendelea kwa kituo hiki kumechangiwa kwa karibu na Salim Asas ambae amekuwa bega kwa bega kuona vijana walioathirika na madawa ya kulevya wanasaidiwa na anachofanya salim pia ni kumuunga mkono Rais Dr Magufuli ambae ametangaza vita dhidi ya madawa ya kulevya ......hivyo bado tunaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia mapambano haya ya kunusuru afya za vijana wetu "alisema Dr Ngalla 

  Kuwa lengo la kituo kuweza kuwahudumia waathirika wa madawa ya kulevya kutoka mikoa mbali mbali nchini hasa wamelenga kuwafikia vijana wa mkoa wa Mbeya, Njombe , Ruvuma na Iringa japo tafiti zinaonyesha mkoa wa Mbeya ndio unaongoza kwa matumizi ya madawa ya kulevya .Msimamizi wa kituo hicho Bw Godwin Msillu alisema kuwa mkakati wa kuanzisha kituo hicho ulitokana na mkakati wa NGOS ya FADAS ambao walikuja na mpango wa kuanzisha kituo hicho .

  Alisema kuwa kati ya waathirika wa dawa za kulevya ambao wapo kituoni hapo baadhi yao ni kutoka mkoa wa Arusha na kuwa kumekuwepo na mafanikio makubwa kwa walengwa hao afya zao kuanza kuimarika na hivyo  kuwataka vijana wengine walioathirika na dawa za kulevya kutosita kufika kituoni hapo ili kusaidiwa zaidi.

  Akizungumza kwa niaba ya wenzake walioathirika na madawa ya kulevya Bw Shadrack John alisema kuwa amepata kufika mkoani Arusha kuja kupatiwa huduma hiyo na kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri zaidi.

  Huku kijana Ibrahim Abdu alisema kuwa amekuwa akitumia madawa hayo kwa zaidi ya miaka 10 sasa kabla ya kuamua kuacha na kujiunga na kituo hicho hivyo kupongeza jitihada za Asas kuunga mkono kituo hicho huku akiwataka vijana wenzake kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya .


  0 0

  Faith Shayo - Unesco, Tanzania

  Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda (hayupo pichani) kufungua rasmi mafunzo ya Tehama kwa walimu nchini.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

  MAFUNZO kwa walimu watakaotumia teknolojia ya mawasiliano na habari (Tehama) kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu yamefunguliwa katika maabara za Chuo Kikuu Huria jijini Dar es salaam.

  Mafunzo hayo yanayohusisha walimu kutoka Vyuo vya Monduli, Tabora na Morogoro yamelenga kuoanisha ufundishaji na matumizi ya Tehama katika program ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya kuboresha elimu Tanzania kupitia ufadhili wa taifa la China.

  Programu hiyo inayotoa ushirikiano mpya kati ya China na shirika hilo la Umoja wa Mataifa inafanyakazi katika mataifa manane ya kusini mwa jangwa la sahara inatekelezwa kwa lengo la kuwezesha mafanikio kwa malengo ya 2030.Nchi zinaozhusika na mpango huo ni Tanzania Kongo ya Kinshasa (DRC), Congo, Liberia, Uganda, Côte d’Ivoire, Ethiopia na Namibia.
  Mpango huo ambao kwa ujumla wake , awamu ya kwanza na ya pili unachukua miaka minne umelenga kuwezesha vyuo vya walimu kutoa walimu wa kufunza wenzao kwenye stadi za kufundisha kwa kutumia Tehama.

  Mradi huo unaojulikana kama UNESCO-China Funds-in-Trust (CFIT) wenye lengo la kuziba pengo la ubora wa elimu wa kuwawezesha walimu kufundisha kwa kutumia Tehama ulizinduliwa Novemba 22,2012 kwa nchi tatu za kwanza na baadae kuongezwa nchi nyingine tano kufikia nane mwaka 2013.Mpango huo ni wa dola za Marekani milioni 8 kutoka China mahususi kwa mataifa ya Afrika kuboresha elimu kupitia Unesco.
  Prof. Elifas Bisanda
  Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa walimu watakaotumia teknolojia ya mawasiliano na habari (Tehama) kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu yanayoendelea katika maabara za Chuo Kikuu Huria (out) jijini Dar es salaam.  

  Walioketi kutoka kushoto ni Basiliana Caroli Mrimi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo pamoja na Kiongozi wa kitaifa wa timu ya mradi wa CFIT kit, Prof. Ralph Masenge.  0 0
 • 03/23/16--00:41: DONDOO ZA MAGAZETI LEO

 • 0 0


  Na Rhoda James.

  Serikali imesema inakaribisha kampuni mbalimbali kutoka nchini Canada ili kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini lengo likiwa ni kuongeza kiwango cha umeme.

  Wito huo umetolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipokutana na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Alexandre Leveque. “Tunataka kiwango cha umeme nchini kiongezeke mara mbili ya kiwango kilichopo sasa,” alisema Profesa Muhongo.

  Aliongeza kwamba bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam lina matoleo katika maeneo mbalimbali nchini ikiwamo wilayani Mkuranga ambapo linaweza kuzalisha si chini ya megawati 2000. “Tunahitaji mwekezaji makini ambaye ataweza kuwekeza kwenye eneo hilo,” alisema Profesa Muhongo.

  Profesa Muhongo alisema kuwa tayari ameshafanya mazungumzo na makampuni mbalimbali duniani kwa ajili ya kuwekeza kwenye nishati ya umeme na kwamba bado anaendelea kutafuta makampuni makini ya ndani na nje ya nchi ili Tanzania iweze kuwa na nishati ya uhakika.

  Kwa upande wa Sekta ya Madini Profesa Muhongo alisema kuwa Serikali itaendelea kuwawezesha wachimbaji wadogo katika masuala mbalimbali ikiwemo utoaji wa ruzuku na mafunzo ya uchimbaji bora wenye tija.

  Alisisitiza kwamba lengo la Serikali ni kuwakomboa wachimbaji wadogo kuondokana na umasikini na alieleza kuwa wachimbaji hao wakiwezeshwa itachangia ongezeko la ajira.  

  Pia Profesa Muhongo alimuomba Balozi huyo wa Canada kufuatilia suala la kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake ili kuleta ufanisi wenye tija katika sekta za Nishati na Madini.

  Kwa upande wake Balozi Leveque, alisema Canada inavutiwa kuwekeza hasa katika nishati jadidifu ikiwemo umeme wa jua na kwamba atayakaribisha makampuni ya nchini Canada kuwekeza katika uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia.

  Balozi Leveque pia aliishauri Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi na kutoa wito wa usimamizi madhubuti wa Sekta ya Madini ili kuepusha muingiliano wa maeneo ya wachimbaji madini wakubwa wa nje na ndani ya nchi.

  Aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo mbili na kuahidi kuwa Serikali ya Canada itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa masuala mbalimbali yakiwemo kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara na Taasisi zake.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mbele) na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (kushoto kwa Waziri) wakiwa katika kikao cha pamoja na Ubalozi wa Canada na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Taasisi zake.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mbele) akishuhudia Balozi wa Canada nchini Tanzania, Alexandre Leveque akitia saini kitabu cha Wageni mara alipofika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Kansela Siasa, Uchumi, Masuala ya umma kutoka Ubalozi wa Canada nchini,  Theressa de Haan.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati),  Balozi wa Canada nchini Tanzania, Alexandre Leveque (kulia kwa Waziri)  na Kansela Siasa, Uchumi, Masuala ya umma, Theressa de Haan wakiwa wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Alexandre Leveque katika picha ya pamoja ofisini kwake jijini Dar es Salaam.    

  0 0


  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.) , akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Chuo cha Diplomasia wakati wa ziara yake Chuoni hapo. Chuo hicho ni moja ya Taasisi zilizo chini ya Wizara. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Dkt. Mohammed Maundi (katikati) na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Taaluma Chuoni hapo, Dkt. Wetengere Kitojo . Naibu Waziri akiangalia vitabu vilivyopo kwenye Maktaba ya Chuo hicho
  Naibu Waziri akiwaeleza jambo uongozi wa chuo hicho. 

  Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa imejipanga kuhakikisha Chuo cha Diplomasia kinaboresha huduma zake za utoaji elimu na mafunzo ya masuala ya Diplomasia ili kukidhi mahitaji ya Watanzania katika taaluma hiyo.

  Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba alipofanya ziara katika Chuo hicho kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam ambacho ni moja ya Taasisi zilizo chini ya Wizara.

  Mhe.  Kolimba alisema kwamba Chuo cha Diplomasia ambacho kilianzishwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Msumbiji ni miongoni mwa vyuo vilivyojipatia sifa kubwa ndani na nje ya nchi kwa kutoa mafunzo katika masuala ya Diplomasia na hivyo Wizara haina budi kuhakikisha inaendelea kukiboresha ili kuhakikisha kinakidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.

  Mhe. Dkt. Susan alisema kuwa, miongoni mwa masuala yanayotakiwa kufanyiwa kazi katika maboresho hayo ni pamoja na miundombinu ya Chuo kwa maana ya kuongeza majengo, vifaa vya kisasa vya kufundishia, maabara za kisasa za lugha, maktaba na kuongeza Wakufunzi.Aidha, Mhe. Kolimba aliueleza Uongozi wa Chuo hicho kuwa ni vema vipaumbele katika kukiletea chuo maendeleo vikaainishwa ikiwa ni pamoja na kuonyesha mikakati ya kila changamoto ili kupata suluhisho la haraka la changamoto hizo.

  “Ninawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya na tunaahidi kuwa pamoja nanyi wakati wote ili kuhakikisha Chuo chetu kinafikia viwango vinavyostahili” alisema Mhe. Kolimba.Vilevile alieleza kuwa ni vema Chuo kikaimarisha ushirikiano na Vyuo vingine vya ndani na nje kwa kuainisha maeneo muhimu ya ushirikiano yenye faida kwa pande zote. Pia alikitaka Chuo kuwa na mikakati itakayokiwezesha Chuo hicho kuweza kujiendesha kibiashara kama vyuo vingine nchini na kuacha utegemezi mkubwa katika bajeti ya Serikali.

  Awali akimkaribisha Naibu Waziri Chuoni hapo, Mkurugenzi wa Chuo hicho, Balozi Mohammed Maundi alisema kuwa Chuo hicho kinaendelea kuboresha maeneo mbalimbali ya Chuo hicho ikiwemo kuanzishwa kwa Kozi ya Shahada mwaka 2015 na tayari chuo kimepata michoro ya majengo kwa Chuo kipya wanachotarajia kukijenga na sasa kinachohitajika ni fedha ili kukamilisha mpango huo ambao kwa kiasi kikubwa utamaliza changamoto zinazokikabili Chuo.

  Chuo cha Diplomasia (CFR) ni chuo kilichoanzishwa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Msumbiji mwaka 1978. Chuo kimekuwa kikitoa elimu katika ngazi ya Cheti, Diploma, Shahada na Shahada ya Juu. 
   

  0 0

  Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi  Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers  ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation utaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Dodoma kuanzia Jumatatu, tarehe 28 March 2016 kwenye ukumbi wa  LAPF House Mkoani  Dodoma. Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake watakaochaguliwa 30 kutoka mkoani Dodoma na mikoa ya jirani. 

  Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Dodoma wanafikia malengo yao waliojiwekea. Wanawake wakazi wa Mkoa wa Dodoma waliotuma maombi na wanaopenda kunufaika na mradi huo  wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya usaili siku ya Jumamosi tarehe 26 Machi 2016 kuanzia saa tatu (9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi wa  LAPF House Mkoani Dodoma.

  Mafunzo yana lengo la  kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha, muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 

  Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa mikopo bila riba ya bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa  Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
  Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 712 646 322  au +255 718 010 107

  0 0

  Ni kweli ni muhimu sana huyu, kwani juhudi zake  ndizo zinakufanya wewe unafurahia maisha sasa,  una uwezo wa kusafiri umbali mrefu kwa ndege au gari, unatumia internet kuwasiliana na rafiki kujifunza, una jiko la gesi, yote haya ni kwa sababu ya huyu bwana Edwin Laurentine Drake.

   Historia ya sekta ya mafuta na gesi Duniani ilizaliwa   August 27 mwaka 1859 uko Titusville Pennsylvania nchini Marekani, baada ya Edwin Laurentine Drake  ambae alifanya kazi ya ukonda kwnye gari moshi (treni) kwa miaka 8, alipochimba kisima cha kwanza cha mafuta(black gold) na kufanikiwa kuyapata kwenye urefu wa futi 69.5.

  Kabla ya Drake Kuchimba kisima cha kwanza cha mafua katika mji wa  Titusville, Pennsylvania Nchini Marekani, watu wote ulimwnguni walikuwa wakipata mafuta katika sehemu  ambazo mafuta yalikuwa yakitiririka yenyewe toka ardhini bila kuchimbwa. Yani ilikuwa huitajiki kutumia teknolojia yoyote kuchimba mafuta, mafuta yalikuwa yanatiririka toka ardhini kama vile unavyoona chem chem za maji. Njia hii raisi ya upatikanaji wa mauta iilikuwa bado ni changamoto kwani  bado hizo chem chem zilikuwa hazizalishi kiwango kikubwa cha mafuta kukidhi mahitaji.

  WASIFU WA EDWIN KWA UFUPI
  Edwin Laurentine Drake alizaliwa tarehe 29 mwaka 1819, Katika maisha yake Edwin alifanya kazi tofauti ngumu kwa miaka 11, mwaka 1845 alijikuta akizama kwenye dimbwi la kimapenzi na kumuoa mwanadaa Philena Adam ambaye alifariki wakati alipokuwa akijifungua, Mwaka 1849 alipata kazi ya kuwa kondakta wa gari moshi(treni) ambayo aliifanya kazi hiyo kwa miaka 8. Mwaka 1957 Drake alioa tena mke mwingine Laura Dowd. Baadae Drake alilazimika kuacha kazi hiyo ya ukonda kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli.

  DRAKE KUTOKA KWENYE UKONDA HADI KUAJIRIWA KWENYE KAMPUNI YA MAFUTA
  Mwaka 1850 kundi la wanasheria na wakemia wa Marekani walianzisha kampuni ya kwanza ya mafuta duniani iliyoitwa “The Seneca Oil Company” Edwin alifanikiwa kupata kazi kwenye kampuni hiyo Huku kazi yake ya ukonda wa treni ikiwa kama ndio sifa iliyomfanya apate kazi hiyo kutokana na waajiri wa kampuni walikuwa wakitaka mtu ambae ataweza kusafiri vijiji vya mbali vya Pennsylvania kukusanya mafuta kwenye chem chem zilizokuwa zikitiririsha mafuta.Hivyo uzoefu wa Drake kuwa konda ilionekana atainufaisha kampuni kwani huenda akasafiri hadi vijijini eidha bure au kwa gharama nafuu.

  EDWIN AANZA KUCHIMBA KISIMA WATU WAMCHEKA NA KUMUITA MJINGA
  Edwin alipoanza kufanya kazi na kampuni hiyo ya mafuta alifikiri namna ya kuongeza uzalishaji wa mafuta katika chem chem ambazo mafuta yalikuwa yakitiririka bila kuchimbwa (oil seeps). Katika kufikri hilo akapata wazo la kuchimba shimo ili kuweza kupata mafuta. Lakini jitihada zake ziligonga mwamba kwani alikutana na changamoto nyingi mwanzoni na kumpelekea kushindwa. Hata msaidizi wake wa uchimbaji (driller) aliyeitwa  William alianza kukata tama.Kisima(shimo) hicho ambacho Edwin alishindwa kilitwa “Drake’s folly” yani upumbavu wa Drake na baadhi ya watu ambao waliamini hataweza kufanikiwa

  EDWIN ATUMIA UBUNIFU
  Edwin aliamua kubadili na akaamua kutumia mabomba ya  chuma ambayo yaliweza kutoboa mwamba tabaka(sedimentary rock) aina ya shale. Ilikuwa ni august 27 1859 ambapo  alifanikiwa kuyapata mafuta (black gold) katika urefu wa futi 69. Asubuhi yake msimamizi wake alipoenda  site kukagua kazi aliona ajabu sana kuona kisima cha Drake (Drake’s well) kikitoa kiwango kikubwa cha mafuta. Inakadiriwa kisima hicho kilikuwa kina uwezo wa kuzalisha mapipa ya mafuta 20 hadi 40 kwa siku.

  Matumizi ya ugunduzi wa mafuta ya Edwin Drake yalitia hamasa ubunifu wa wajasiriamali  na wagunduzi wengi duniani ambao walibuni  vitu kama magari vitakavyoweza ktumia mafuta ili kumrahisishia maisha mwanadamu.Leo hii kila mtu anatumia kifaa au vifaa ambavyo viligunduliwa na wajasiriamali wengine baada ya Drake kugundua mafuta.Leo hii una uwezo wa kusafiri mamia na melfu ya maili za umbali kutokana na mafuta, unatumia gesi kupikia nyumbani, unatumia generata na pia mafuta na gesi kwa sasa ndo yanaendesha internet na mawasilano yote duniani.

  TAFAKARI NA JIFUNZE YAFUATAYO KUTOKA KWA EDWIN DRAKE
  Unadhani Ingekuwaje Drake angesikiliza maneno ya watu waliokuwa wakimuona mjinga na kumkatisha tamaa.
  Unadhani  dunia ingekuwaje leo bila magari ndege,internet kama Drake angekuwa ni mtu wa kutaka majibu ya haraka na kama angekuwa mtu wa kuogopa kushindwa.

  Dunia ingekuwaje kama tu baada ya kuajiriwa Drake angekuwa mtu wa kuridhika na mshahara bila kujali kufikiri ni jinsi gani anaweza kuongeza thamani kwenye kampuni, kutatua changamoto za kampuni na kuongeza uzalishaji.

  Hussein Boffu
  Graduate In Petroleum Geoscience
  www.Tanzaniapetroleum.com
  0655 37 65 43

  0 0

  Kampuni ya simu ya Zantel leo imekabidhi vifaa vya kusomea kwa watoto wenye vifaa vya ulemavu wa macho wa shule ya msingi Kisiwandui Unguja vyenye thamani ya shilingi milioni 20. Vifaa hivyo ni mashine ya perkins brailler, index printer, braillon paper pamoja na salte na stylus.

  Msaada huo umekabidhiwa na Mshauri wa Mahusiano ya Umma wa Zantel, Mohamed Mussa kwa mwalimu mkuu wa shule Bi Taifa Ahmed pamoja na Mkurugenzi wa Elimu ya Shule ya Msingi, bwana Ahmed Abulmajid Shaaban.Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mohamed Mussa alisema vifaa hivyo ni sehemu ya mkakati wa  kampuni ya Zantel katika  kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata elimu bora bila kujali tofauti zao.

  ‘Wajibu wetu kama wanajamii ni kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata msaada kama ilivyo kwa watu wengine na pia kuweza kuwaanda  kwa ajili ya kuweza kufikia malengo yao kama walivyo kusudia’ alisema Mussa. Shule ya msingi Kisiwandui ilianzishwa mwaka 1991, na mpaka sasa wanafunzi 199 wamepitia shuleni hapo.
   Mshauri wa Mahusiano ya Umma wa Zantel, Mohamed Mussa akizungumza wakati akikabidhi vifaa vya kusomea kwa watoto wenye ulemavu wa macho wa shule ya msingi Kisiwandui. kwa mwalimu mkuu wa shule Bi Taifa Ahmed pamoja na Mkurugenzi wa Elimu ya Shule ya Msingi, bwana Ahmed Abulmajid Shaaban. 
  Mshauri wa Mahusiano ya Umma wa Zantel, Mohamed Mussa akikabidhi vifaa vya kusomea kwa watoto wenye ulemavu wa macho wa shule ya msingi Kisiwandui kwa Mkurugenzi wa Elimu ya Shule ya Msingi, bwana Ahmed Abulmajid Shaaban. Anayetazama katikati ni mwalimu mkuu wa shule Bi Taifa Ahmed. 
   Mshauri wa Mahusiano ya Umma wa Zantel, Mohamed Mussa akizungumza wakati akikabidhi vifaa vya kusomea kwa watoto wenye ulemavu wa macho wa shule ya msingi Kisiwandui. kwa mwalimu mkuu wa shule Bi Taifa Ahmed pamoja na Mkurugenzi wa Elimu ya Shule ya Msingi, bwana Ahmed Abulmajid Shaaban.  0 0

  Wahariri wa vyombo vya habari za kidini wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara ya kimafunzo mkoani Pwani, ziara hiyo imeandaliwa na TACAIDS .
  Mhariri wa Habari kutoka Radio Maria Bi. Judidh Francis akiongea jambo katika ziara ya wahariri wa vyombo vya habari vya kidini katika kituo cha afya cha utoaji huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze,ziara hiyo imeandaliwa na TACAIDS 
  Mhariri wa Habari kutoka Radio Sauti ya Quran Bw. Sadiki Faki akiongea jambo katika ziara ya wahariri wa vyombo vya habari vya kidini katika kituo cha afya cha utoaji huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze,ziara hiyo imeandaliwa na TACAIDS .
   

older | 1 | .... | 1168 | 1169 | (Page 1170) | 1171 | 1172 | .... | 3283 | newer