Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1167 | 1168 | (Page 1169) | 1170 | 1171 | .... | 3270 | newer

  0 0

  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amezungumza na wadau wa mziki wa Dansi  leo jijini Dar es Salaam na kusikiliza changamoto mbalimbali za wadau hao wa muziki huo wa Dance.
  Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na wanamziki wa Dansi leo alipokutana nao katika ukumbi wa vijana Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mungereza.
  Mkurugenzi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mungereza akizungumza na wakongwe wa muziki wa Dansi leo katika ukumbi wa Vijana Kinondoni jijini Dar es Salaam.  Kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
   Mkurugenzi wa bendi ya Muziki wa Dance nchini African Starz (Twanga Pepeta), Asha Baraka akizungumza katika mkutano wa wanamziki wa Dansi  na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye 
   Wakongwe wa mziki wa Dansi wakimsikiliza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Nape Nnauye leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Al-Hassan Michuzi.


  0 0
 • 03/21/16--10:29: OBAMA TOUCHES DOWN IN CUBA
 • 0 0


  Mfanyakazi wa kujitegemea wa  Deutsche Welle nchini Tanzania, Salma Said, alizuiliwa kwa muda wa siku mbili na watu waliomteka nyara katika eneo moja lisilojulikana. Kwa mujibu wa polisi, hatimaye aliachiwa huru jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili ya Machi 20. 

  Mwandishi huyo alitekwa nyara Ijumaa ya Machi 18 katika Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam akitokea Zanzibar, ambako alikuwa aripoti  juu ya  uchaguzi wa marudio uliofanyika Jumapili ya Machi 20,  lakini kutokana na taarifa alizozipata kwamba usalama wake uko hatarini na baada ya kuzungumza na Idara ya Matangazo ya Afrika ya Deutsche Welle mjini Bonn, alishauriwa aondoke visiwani Zanzibar na akaelekea jijini Dar es Salaam. Kulingana na familia yake, Salma hakufika jijini humo. 

  Kwa mujibu wa polisi jijini Dar es Salaam, sababu za kutekwa nyara kwake, mahala alipokuwa akizuiliwa au ni kina nani waliofanya  kitendo hicho, ni mambo ambayo bado yanachunguzwa. Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro aliiambia DW kwamba: "Tumo katika kuchunguza na tutatoa taarifa kuhusiana na tukio hilo na nani walihusika hapo baadaye." 
  Mkurugenzi Mkuu wa  Deutsche Welle, Peter Limbourg, alisema baada ya kupokea taarifa ya kuachiwa huru Salma Said kwamba: "Fikra zetu ziko pamoja  naye na tuna furaha kwamba mwenzetu yuko huru. Heshima ya wafanyakazi wetu  ni muhimu zaidi, hasa katika nchi ambako uhuru wa vyombo vya habari na wa kutoa maoni unaekewa vipingamizi. Tunataraji kwamba uchunguzi juu ya kisa hiki utakamilika na kuwekwa wazi." 

  Salma Said ni mwandishi na ripota maarufu. Mwandishi huyu wa habari mwenye umri wa miaka 45 amekuwa akifanya kazi kama mwandishi wa kujitegemea  wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle tokea mwaka 2000. Pia huyaandikia magazeti kadhaa ya ndani nchini Tanzania na mitandao kadhaa ya kijamii. Aliwahi kushambuliwa mnamo miaka ya nyuma. Mwaka 2012, alishambuliwa na kikundi cha watu alipokuwa akitoka kuripoti juu ya mkutano  wa hadhara wa  chama cha upinzani mjini Unguja. 

  Imetolewa na: 
  Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle
  Bonn
  Ujerumani

  0 0  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watotoimepokea kwa masikitiko makubwa tukio la kunajisiwa kwa watoto watatu wa kike wenye umri kati ya miaka minane hadi tisa, wanafunzi wa darasa la tatu wa Shule ya Msingi Msaranga Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro. 
  Tukio hili la kunajisi watoto ni ukiukwaji mkubwa wa haki za mtoto ambao huchangia kudumaza na kurudisha nyuma usitawi na maendeleo yamMtoto na ni kinyume cha Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009. 
  Wizara imesikitishwa na taarifa kuwa, kuna baadhi ya wanajamii wanaowafanyia ukatili watoto wa kike kwa kuwashurutisha kuwa na mahusiano na watoto hao katika umri mdogo, kitendo ambacho kwa kiasi kikubwa kinarudisha nyuma jitihada za Serikali kuhakikisha kuwa jamii zetu zinakuwa mahala salama kwa watoto kuishi.  
  Wizara inalaani vikali unyanyasaji waliofanyiwa watoto hao kwani katika umri huo mdogo hawakustahili kufanyiwa ukatili huo. Aidha, wazazi na walezi tutambue kuwa tunaowajibu mkubwa wa kufuatilia mienendo ya watoto wetu mara kwa mara ili kuwanusuru na matukio ya ukatili.  
  Wizara inatoa pongezi kwa wananchi, Jeshi la Polisi, wanahabari na wadau wote ambao wameonesha ushirikiano katika kufuatilia na  kuripoti tukio hili.  Aidha, Wizara inalipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro kwa kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja anayehusishwa na tukio hili baya la kunajisi watoto hao. Tunahimiza Polisi katika mkoa wa Kilimanjaro kumsaka mtuhumiwa wa pili na kumjumuisha katika shauri hili. 
  Maagizo yanatolewa kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha anatoa huduma stahiki ya vipimo na tiba kuokoa afya za watoto hao. Aidha, Afisa Ustawi wa Jamii na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Kilimanjaro wahakikishe wanafuatilia shauri la watoto hawa kwa karibu, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya afya za watoto hao; na kutoa ushauri nasaha kwa watoto, wazazi na walezi wa familia za watoto hao ili kuwawezesha watoto hao kuendelea na masomo yao kikamilifu, na kutoa taarifa kwa Wizara mara kwa mara.


  Imetolewa na: 
  Erasto Ching’oro

  Msemaji wa Wizara


                                                              Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto


  0 0


  Tanzanian former international model Tausi Likokola who just returned from a trip from Europe has been in and out of the country to promote her beauty and lifestyle products launched through her company now based here in Tanzania  named Tausi Dreams LTD. 

  Tausi is still based in the US but is now back in Tanzania to continue working on a number of projects as well as marketing her latest launched products; perfume named 'Tausi Dreams ' as well as high quality human hair extensions named 'Tausi Beautiful You Hair'. 


  Tausi who raised in high fashion world internationally on the 90's worked with  fashion houses such as Gucci, Christian Dior, Issey Miyake, Tommy Hilfger, Escada etc. Tausi also covered numerous fashion magazines and inspired many current Tanzanian models and others around the globe. Tausi uses her name to help her own people in Tanzania in education, HIV/AIDS awareness, society areas of need,  and positively contributed to Tourism in her country of birth Tanzania as well as business sector and natural resources. Tausi is currently planning to host a few charitable activities through her non for profit organization 'Tausi and Friends For Life.
  Tausi will start this coming Saturday March 26th 2016 to film a reality TV series inspired by her book "The African Princess" and the shows will be a model search that will be mentoring inspired models using experiences Tausi gained during her years in the fashion Industry.

  Tausi withdrew from working actively in the fashion industry to raise a family of her own. Her life journey has taken her from Africa, Europe, Asia, Australia and current in the USA where she calls home. Tausi has published four books and is using her internationally gained experience to work with young girls globally to empower them to full potential. Tausi published books are tittled; 'The Art of Beauty and Health', The African Princess', T'he Touch of an Angel'& 'Beautiful You'. 
  Later last year Tausi was a guest of honor at her former school Jangwani form six graduation where they asked her to help with a new printing machine after the school used an old model for over 10 years. Tausi will be re-visiting her school this coming Wednesday 23rd at 10am to donate digital printer as well as to speak to the students. Press is invited 10am sharp. Tausi is a firm believer in investing in education and young women in the society to bring about a difference. On other like event before her recent travel to Europe Tausi visited Sega girls secondary  school in Morogoro where she also mentored young girls

  0 0


  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dares salaam kuzungumza na wawakilishi wa Mawakala wa Forodha na Bandari leo Machi 21, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipekuwa baadhi ya nyaraka zinazoonyesha jinsi wizi wa fedha za serikali  uliofanywa kwenye  bandari ya Dar es salaam  ukihusisha mabenki wakati akizungumza na  Mawakala wa Forodha na Bandari kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo.
  Baadhi ya Mawakala wa Forodha na Bandari wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salam leo Machi 21, 2016.
  Kamishna  wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Alphayo Kidata akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizozuka katika mkutano na Waziri Mkuu
   (Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu).
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  WAZIRI MKUU AMUAGIZA CAG KUKAGUA BANDARI, CRDB
  ·         Amtaka Mkurugenzi wa Bandari aandae dispatch zote tangu 2014

  ·         Naibu Waziri Ujenzi aagiza kampuni za forodha zifunguliwe


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali aende Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili akague taarifa za mapato ambazo zilikuwa zikilipwa na mawakala wa forodha na bandari kupitia benki ya CRDB lakini hazionekani kwenye mifumo ya benki.

  Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumatatu, Machi 17, 2016) wakati akizungumza na mamia ya mawakala wa forodha na bandari waliohudhuria mkutano aliouitisha ili kusikiliza kero zinazowapata katika utendaji kazi wao.

  Akizungumza na mawakala hao kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alisema kuna dalili za kutupiana lawama baina TPA na CRDB kuhusu malipo yaliyikuwa yakifanyika benki halafu fedha hazionekana na wakala anaidaiwa kuwa hajalipia mzigo wakati alishaulipia.
  “Kimsingi bado liko tatizo baina ya Mamlaka ya Bandari pamoja na Benki ya CRDB. Naona kila mmoja hapa anamkana mwenzake. Nitamtuma CAG ili akafanye ukaguzi wa kina ili tujue ni nani kati yao amehusika na upotevu wa fedha,” alisema huku akishangiliwa na mawakala hao.
  Alimwagiza pia Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Eng. Aloyce Matei aandae dispatch zote walizotumia kupokelea malipo za kuanzia mwaka 2015 na ikibidi aandae za kuanzia mwaka 2014 ili CAG anapozopitia aweze kupata picha halisi.
  Vilevile, Waziri Mkuu alimwagiza Eng. Matei kuhakikisha wananunua mashine ya photocopy ili iwekwe kwenye chumba cha kupokelea stakabadhi za malipo ya benki (bank pay in slip) ili mteja anapoleta nakala ya benki aweze kutolewa photocopy na kubakia na nakala ya malipo aliyofanya,

  Waziri Mkuu alisema Serikali inatambua bandari ni eneo nyeti katika kuinua uchumi na mapato ya nchi lakini pia ni eneo muhimu katika kutengeneza ajira. “Ninapenda niwahakikishie kuwa bado tutaendelea kukagua bandari hadi pawe safi. Hii bandari ni yenu na mtafanya kazi kama kawaida,” alisema. 
  Mapema, akizumgumza kwa niaba ya mawakala hao, Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha nchini (TAFFA), Bw. Stephen Ngatunga alieleza matatizo mbalimbali ambayo wao kama mawakala wa forodha wamekuwa wakikumbana nayo kuanzia ulipaji, utoaji wa mizigo na kuitaka Serikali iongeze nguvu katika kuikabilia sekta hiyo. 
  Alizikosoa baadhi ya sheria ambazo zinaruhusu wamiliki wa bandari kavu kumiliki pia makampuni ya uwakala wa forodha, sheria kadhaa zinazochangia kukwamisha utoaji wa mizigo bandarini, ukaguzi hafifu wa kwenye scanner na uwepo wa vituo vinane vya mizani kuanzia Dar es Salaam hadi Tunduma ambavyo vimegeuka kuwa kero kwa wasafirishaji wa mizigo kwenda nchi jirani. 
  Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani amesema Serikali imeamua kuyafungulia makampuni zaidi ya 150 ambayo yalikuwa yamefungiwa kufanya kazi za uwakala wa forodha kutokana na madai ya kuhusishwa na ukwepaji wa kodi. 
  “Hapa tumegundua kuwa wote siyo wasafi iwe ni mawakala, benki ama bandari. Mkurugenzi wa Bandari, kuanzia leo watu hawa waruhusiwe waanze kufanya biashara lakini nyaraka za nyuma zisiguswe hadi CAG atakapokamilisha uchunguzi wake,” alisema kuibua kelele za shangwe kwenye ukumbi huo.
    
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM

  JUMATATU, MACHI 21, 2016.  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kwa makini zoezi la uhakiki wa silaha zake lililokuwa likifanywa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Neema Laizer Ikulu jijini Dar es salaam. Mhe. Rais amekuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam Paul Makonda.
  Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi Silaha aina ya Bastola Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi silaha aina ya shortgun Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiiweka silaha yake vizuri mara baada ya kuhakikiwa Ikulu jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa mtu kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam la kuhakiki silaha, ambapo bunduki zake mbili aina ya Shortgun na Pistol zimehakikiwa nyumbani kwake Ikulu Jijini Dar es salaam.

  Uhakiki huo umefanywa na maafisa wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro.


  Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Rais Magufuli amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Jeshi la Polisi kwa kuendesha zoezi la uhakiki wa Silaha, na ametoa wito kwa watu wote wanaomiliki silaha nchi nzima kuhakikisha zinahakikiwa.Dkt. Magufuli pia amelitaka Jeshi la Polisi kuongeza juhudi za kukabiliana na watu wanaojihusisha na vitendo vya uharifu ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo.

  "Ni aibu kumuona askari polisi mwenye silaha ananyang'anywa silaha, ni aibu, na nasema hiyo ni aibu, mpaka jambazi akunyang'anye silaha na wewe una silaha?"Amehoji Rais Magufuli.Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro, amemshukuru Rais Magufuli kwa kuunga mkono zoezi hilo na amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa mafanikio.

  Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ametaka pande zinazogombea kiti cha Umeya katika Jiji la Dar es salaam, kukamilisha mchakato wa kumpata Meya katika uchaguzi uliopangwa kufanyika kesho tarehe 22 Machi, 2016 badala ya kuendelea kurumbana.


  Dkt. Magufuli amesema upande wowote uwe tayari kupokea matokeo ya uchaguzi huo, ili Meya apatikane na Jiji liweze kuendelea na mipango yake ya kuwahudumia wananchi bila vikwazo.


  "Mahali tunapostahili kushinda kama tumeshinda tushinde kweli, lakini mahali tunaposhindwa napo tukubali kushindwa, na hiyo ndio demokrasia ya kweli"ameongeza Rais Magufuli


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dar es salaam


  21 Machi, 2016  0 0

  Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager leo imefanya mazoezi katika uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya ulipo katika jiji la D’jamena ikiwa ni maandalizi ya mchezo dhidi ya wenyeji Chad siku ya Jumatano.

  Taifa Stars imefanya mazoezi kuanzia majira ya saa 9 alasiri, ikiwa ni sawa na muda utakaochezwa mchezo siku ya Jumatano sawa na saa 11 kwa saa za nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki.

  Akiongelea maandalizi ya mchezo huo, Kocha Mkuu wa Taif Stars Charles Boniface Mkwasa amesema anashukuru vijana wake waliotangulia wamefika salama, hakuna majeruhi na wote wameweza kufanya mazoezi aliyoyapangilia.

  “Hapa D’jamena hali ya hewa ni joto kali tofauti na nyumbani, kwa hizi siku mbili tutakazofanya mazoezi hapa, naimani vijana wataweza kuzoea hali ya hewa na kufanya vizuri katika mchezo wa Jumatano” alisema Mkwasa.

  Mkwasa amesema wachezaji wake wametoka katika vilabu vyao ambavyo vilikua na michezo mwishoni mwa wiki, wote bado wako fit kikubwa wanafanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo.

  “Hatujapata muda mrefu wa kufanya mazoezi kwa pamoja, wachezaji walikua na majukumu katika vilabu vyao, nashukuru wote wamewasili wakiwa salama na kesho wataungana na wachezaji wenzao wanaokuja katika kundi la pili kwa ajili ya mazoezi ya mwisho na mchezo wenyewe” aliongeza Mkwasa.

  0 0


  0 0

  Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa ya kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Njombe na aliewahi kuwa Mtangazaji wa Radio Tanzania RTD, Dada Sara Dumba, kilichotokea ghafla usiku huu, huko Njombe.

  Hakika ni taarifa ya kusikitisha sana na ni pigo kubwa kwa familia yake na tasnia nzima ya habari. 

  Mungu aiweke Roho ya Marehemu Sara Dumba, mahaha pema peponi

  Amin.

  Pichani ni miaka kadhaa iliyopita, nikiwa na Mh. Betty Mkwasa ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero na Marehemu Sara Dumba ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe.

  0 0


  0 0

  Vipindi vya redio vya Shuga vitaanza kuunguruma tena kupitia redio mbalimbali nchini kuanzia wiki ya pili ya mwezi wa nne mwaka huu. Vipindi hivyo vinalenga kuwaelimisha vijana kuhusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI, usawa wa jinsia, kufanya maamuzi sahihi, matumizi sahihi ya kondomu na kuepukana na msongo rika.

  Mfulilizo huu wa mchezo wa redio wa Shuga unawalenga zaidi vijana hususan wasichana, kwa kuangalia mtazamo wao, matarajio yao, changamoto wanazopitia ili kutimiza malengo yao na jinsi wanavyopambana na maisha yao ya kila siku. 

  Mchezo wa redio wa Shuga ulianzishwa mnamo mwaka 2014 kwa ushirikiano kati ya MTV, HIV and AIDS Free Generation, Shirika la TACAIDS pamoja na UNICEF. Baada ya mafanikio makubwa msimu wa kwanza, TACAIDS na UNICEF pamoja na wadau wengine waliamua kupanua wigo wa program hii kwa kuandaa vipindi zaidi ili kuimarisha tabia chanya zilizojengwa katika msimu wa kwanza wa vipindi vya Shuga.

  Katika kuboresha utoaji elimu kuhusiana na mahudhui ya vipindi, mashirika ya UNICEF pamoja na TACAIDS kwa kushirikiana na kampuni ya True Vision Production wanaendesha mafunzo elekezi kwa vituo vya radio za jamii, mameneja wa radio shiriki, watangazaji na waandishi wa habari pamoja na kwa waratibu wa UKIMWI ngazi za Halmashauri na Mkoa, ambapo warsha hii inafanyika mkoani Iringa.

  Radio zitakazoshiriki katika urushaji wa vipindi vya Shuga msimu wa pili ni Clouds FM, Nuru FM – Iringa, Kitulo FM – Makete, Kyela FM – Kyela pamoja na Furaha FM, Hope FM, Qibla Ten FM za Iringa.
  Mratibu wa Ukimwi kutoka Tume ya Kudhibiti ukimwi mkoa wa Njombe – TACAIDS Abubakari Magege akiongea na washiriki wa kipindi cha redio cha shuga katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini.

  Mwakilishi wa UNICEF Alice Ijumba akijibu maswali ya washiriki wa kipindi cha redio cha shuga katika uzinduzi rasmi wa msimu wa pili wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini.


  0 0


  Na Sebastian Emmanuel jr. Mafinga.


  Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Rose Tweve ameendelea kukutana na makundi mbalimbali katika mkoa huo, mwishoni mwa wiki hili amekutana na wajasiliamali wanawake katika makundi mawili tofauti. Kundi la kwanza alilokutana nalo ni lile la umoja wa wanawake wa ccm Iringa mjini, waliounda vicoba kwa ajili ya kukopeshana na kuendeleza miradi kadhaa ya kijasiliamali.


  Aidha wanawake hao wakati wakisoma risala kwa mbunge huyo wamesema kuwa wanakabiliana na changamoto kadhaa hasa ukosefu wa mtaji utakao wafanya waendeleze vicoba hivyo ambavyo imekuwa kimbilio la makundi mbalimbali mijini na vijijini.

   Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (CCM), Rose Tweve


  Pia wanawake wao wamemwomba mbunge huyo kuhakikisha kuwa wanawake wa mkoa wa Iringa wanakuwa mfano wa kuigwa katika kuanzisha, kukilinda na kukitetea chama chao hicho cha vicoba kwa kuwa vinaonesha nia ya kuwasaidia kujikimu kimaisha, mpaka sasa wameanza kutafuta wataalamu wa kufundisha namna ya kufuga kuku ili wapate elimu sahihi na kasha kuanza kutekeleza mladi huo.


  Kwa upande wake mbunge huyo kijana ametoa milioni moja taslimu kama mkopo usiokuwa na riba ili uweze kuwasaidia kuendeleza mtaji wao pia akatumia fursa hiyo kuwaomba mkopo huo wauzungushe katika miradi mbalimbali kama ya ufugaji kuku n.k. pia ameonesha nia ya kuwasaidia wanawake hao na kuwaahidi kuwa wakiwa na uaminifu wa kulinda mtaji wao hata kama ni mdogo atahakikisha kuwa vicoba hiyo inakuwa ya mfano wa kuigwa mkoani Iringa. 


  Mbunge huyo amewaomba wanawake wote wa mkoa wa Iringa wasikate tamaa badala yake wapende kujifunza na kutaka kupata nafasi ambayo itawapeleka kwenye mwanga wa  mafanikio. Amesema kuwa hata yeye amekuwa akithubutu kujituma kwa bidii ili aweze kufikia lengo la kuwasaidia wanawake wote bila kujali itikadi, kabila wala dini zao.

   Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Rose Tweve akiwana baadhi ya wananchama wa chama ch mapinduzi.


  Aidha kundi jingine la pili ni lilela wanawake wanaoishi na ulevu Mjini Iringa, wametumia fursa hiyo kuongea na mbunge huyo na kumweleza changamoto wanazokumbana nazo, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mtu wa kuwasaidia kwa mda mrefu kulingana na changamoto zinazo wakabili na kuonesha imani kwa mbunge huyo kuwa sasa wanamatumaini mapya kuwa wamepata mtu muafaka wa kuwasaidia.


  Wanawake hao wanaoishi na ulemavu wameomba pia kupatiwa mtaji ili uweze kuwasaidia katika umoja wao wa kazi za mikono ikiwa ni ususi wa shanga za kimasai, mikoba ya kimasai na mikoba ya kisasa kwa kutumia shanga mbalimbali za asili, ambapo mbunge huyo licha ya kuwapa kiasi cha pesa kwa ajili ya kuendeleza mtaji wao pia amewaomba waanzishe mladi wa utengenezaji wa batiki utakao wanufaisha kwa kiwango kikubwa kwani unaonesha kuwa na soko la uhakika.

  0 0


  0 0

  Katika kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake, taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF) imeandaa semina ya kwanza na ya aina yake nchini kwa Wauguzi wa Wodi za Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti)  Machi 21-22, 2016 kwenye hoteli ya Giraffe ocean View jijini Dar es salaam. 

  Doris Mollel Foundation ilizinduliwa Machi 20, 2015. Semina hii imedhaminiwa na Hoteli ya Giraffe Ocean View, Asas dairies, GSM Foundation, Kilimanjaro water na Waziri Angela Kairuki ambaye alizaliwa njiti pia.

  Dhima ya semina hii ni kuwajengea manesi nchini uwezo wa kukabiliana na changamoto za kuwasaidia watoto njiti pamoja na mbinu mbali mbali za kuzuia uzazi wa njiti ambapo  kulingana na takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, takriban watoto 88,128 walizaliwa njiti au wakiwa na uzito mdogo nchini Tanzania mwaka 2014/2015 pekee.

  Pamoja na semina hii, DMF kwa kushirikiana na mashirika wadhamini pia wametoa msaada wa mashine 5 za Oxygen zenye thamani ya Tsh 10.3 zilizotelewa na benki ya Amana pamoja na GSM Foundation.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akipokea mashine tatu maalum kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), zilizotolewa na Kampuni ya GSM Foundation, katika Semina ya kuwajengea uwezo Wauguzi nchini wa kukabiliana na changamoto za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) pamoja na mbinu mbali mbali za kuzuia uzazi wa njiti, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Giraffe ocean View jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa DMF, Dorice Molel ambaye ndie muandaaji wa semina hiyo.

  Asasi na makampuni mbalimbali ambao ni washirika wa DMF wamehudhuria warsha hii kuendelea kujionea changamoto mbali mbali ambazo manesi wanakabiliana nazo ili kwa pamoja kuendelea kuona jinsi ya kuwasadia katika kupunguza tatizo hili. Baadhi ya asasi hizi ni Vodacom Foundation, Bank M, Clouds Media Group,  Amana Bank, NSSF, CBA, NHIF, Kilimanjaro Water, Mashirika ya UNICEF, MAMAYE,  JHIPEGO, USAID, TICA, Ubalozi wa Vietnam, Hassan Maajar Trust. Elizabeth Glasier pediatric aid Foundation, FHI360, Plan International, ubalozi wa Japan.

  Semina hii ambayo imeongozwa na wataalam wa afya kutoka shirika la kijerumani la GIZ kwa kushirikiana na Dk Augustine Massawe kutoka hospitali ya taifa ya muhimbili imehudhuriwa na manesi (Ma-incharge) kutoka wodi za njiti katika hospitali kuu za mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani na imezinduliwa na Mgeni rasmi Mh Paul Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akihutubia katika Semina ya kuwajengea uwezo Wauguzi nchini wa kukabiliana na changamoto za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) pamoja na mbinu mbali mbali za kuzuia uzazi wa njiti, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Giraffe ocean View jijini Dar es salaam.

  Ndani ya mwaka mmoja DMF kwa kushirikiana na wadhamini na washirika mbali mbali imeweza kutoa kufikisha mchango kwenye jamii kwa kuleta  uelewa na mwamko kuhusu tatizo la njiti lakini pia DMF imeweza kufikisha mashine na michango yenye thamani ya Tsh 152,000,000/= (Mia moja na hamsini na mbili milioni) kwenye hospitali 15 nchini pamoja na sekta ya elimu.


  0 0


  0 0

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke walioko masomoni na likizo wametakiwa kurudi mara moja katika vituo vyao vya kazi ili kuhakikiwa.

  Agizo hilo limetolewa hivi karibuni na uongozi wa Halmashauri hiyo ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli la kuhakiki watumishi wote wa umma waliopo kwenye orodha ya malipo ya watumishi wa umma ndani ya siku 15 ili kubaini watumishi hewa wanaoendelea kulipwa mishahara.

  Akizungumza kwa njia ya simu msemaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke Bi Joyce Nsumba amesema zoezi hilo ni muhimu sana kwa watumishi hivyo basi  watumishi wote wa Halmasahuri hiyo waliopo likizo na masomoni wanatakiwa kurudi katika vituo vyao vya kazi ili kuhakikiwa.

  “ Taarifa imeshatoka kwa watumishi wote kuwa wanatakiwa kuhakikiwa na kwa wale waliopo likizo na kwenye masomo wanatakiwa kurudi ili wahakikiwe na kuendelea na likizo na masomo yao kwani mara baada ya uhakiki huu kukamili majina ambayo yatakuwa hayajahakikiwa yatafutwa kwenye orodha ya  watumishi” Alisema Bi Joyce.

  Bi Joyce Nsumba ameongeza kuwa mpaka sasa uhakiki unaendelea  kwa makundi mbalimbali wakiwemo watumishi kutoka Idara ya Afya, Elimu, Fedha na Biashara, Kilimo,Mifugo,Ujenzi,na Maendeleo ya Jamii na mpaka  sasa wameshahakiki zaidi ya watumishi  8,000.

  Zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma nchini limekuja mara baada ya uchunguzi uliofanywa katika mikoa ya Singida na Dodoma katika Halmashauri 14 na kugundulika kwa watumishi hewa 202 wanaolipwa mishahara  na hivyo Mhe. Rais Magufuli kutoa agizo la kuhakiki watumishi wote katika Wizara,mikoa,Wilaya,Idara,Taasisi na Wakala za Serikali ndani ya siku 15.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema daraja la Kigamboni litafunguliwa rasmi Aprili, 16 mwaka huu. Amesema kazi inayoendelea sasa hivi ni kupitisha magari maalum kwa ajili ya kupima ubora wa daraja hilo ili kujiridhisha kabla ya kukabidhiwa rasmi Serikalini.

  Amewataka watumiaji wa daraja hilo kuwa waangalifu, kulinda miundombinu na kuepuka vitendo vya hujuma ili lidumu kwa muda mrefu. “Daraja hili lina urefu wa mita 640, barabara sita, tatu zinapanda na tatu zinashuka, hivyo tunawaomba wananchi watakaovuka kuzingatia usafi na ustaarabu”, amesema Profesa Mbarawa.

  Amebainisha kuwa Serikali itaweka sheria kali kwa wote watakaokiuka matumizi sahihi ya daraja hilo na kusisitiza umuhimu wa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani wanapovuka katika daraja hilo.

  Meneja Msimamizi wa ujenzi wa daraja hilo Eng. Karim Mattaka amesema wataalam wanaendelea na taratibu za kulipima daraja hilo ili kujiridhisha kama linamudu kupitisha uzito uliokusudiwa kabla ya kulikabidhi kwa Serikali mapema mwezi ujao.

  Amesema awamu ya kwanza ya kulipima daraja hilo imekamilika na sasa wanaendelea na awamu ya pili hadi watakapomaliza awamu nne ili kujiridhisha kabla ya kuanza kutumika.

  Takribani shilingi bilioni 216 zimetumika katika ujenzi wa daraja hilo linalotazamiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa abiria na magari katika kivuko cha Magogoni na Kigamboni.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Msimamizi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni Eng. Karim Mattaka alipokagua daraja hilo leo jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja miradi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Eng. John Msemo wakati alipotembelea daraja la Kigamboni kuangalia ujenzi wa daraja la Kigamboni leo jijini Dar es salaam.
  Mwonekano wa lango la kuingilia daraja la Kigamboni kwa upande wa Kigamboni, linavyoonekana pamoja na vyumba vya kukatia tiketi.


older | 1 | .... | 1167 | 1168 | (Page 1169) | 1170 | 1171 | .... | 3270 | newer