Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1166 | 1167 | (Page 1168) | 1169 | 1170 | .... | 3282 | newer

  0 0


  0 0


  Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa baraka kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 uliofanyika katika hoteli ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza wakishuhudia uzinduzi wa nembo mpya ya mashindano ya Miss Tanzania 2016 yaliyobeba kauli mbiu ya "Mrembo na Mazingira Safi"

  Kutoka kushoto ni Miss Tanzania 1998, Basila Mwanukuzi, Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu, Miss Tanzania 2008, Nasreen Kareem pamoja na Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima wakipozi katika picha ya pamoja kwenye uzinduzi wa Msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016.

  Pichani juu na chini ni wadau wa tasnia ya urembo na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa Msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016.Kwa picha zaidi bofya link hii

  0 0  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi. Irina Bokova.

  SHAKESPERE mwandishi maarufu kutoka Uingereza aliyefariki yapata miaka 400 iliyopita, aliandika katika tamthilia yake inayojulikana kama “A Midsummer Night's Dream” kuwa, “Jicho la mshairi, hutazama kwa umakini na undani, kutoka mbinguni hadi duniani, na duniani hadi mbinguni. Na kama vitu vya kufikirika vusivyofahika vinavyoumbika katika mawazo, ndivyo kalamu ya mshairi inavyogeuza mawazo hayo kuwa katika maumbo yasiyoweza kudhaniwa”.

  Kwa kuwatambua na kuwaheshimu wanaume na wanawake, ambao chombo chao pekee ni uhuru wa kujieleza, watu wanaofikiria na kuchukua hatua, UNESCO inatambua thamani ya ushairi kama ishara ya ubunifu wa mwanadamu. Kwa kutoa umbo na maneno kwa mambo ambayo katika hali ya kawaida hayakuwa nayo, kama vile uzuri usiopimika unaotuzunguka na mateso na taabu kubwa za dunia, mashairi yanachangia upanuzi wa ubinadamu wetu, kwa kusaidia kuongeza nguvu za ubinadamu wetu, mshikamano na kujitambua.

  Sauti zinazobeba ushairi husaidia kukuza upana na utofauti wa lugha na uhuru wa kujieleza. Sauti hizi hushiriki katika jitihada za kimataifa kuelekea elimu ya kisanii na usambazaji wa utamaduni. Wakati mwingine, neno la kwanza la shairi latosha kabisa kurejesha kujiamini pale mtu anapokuwa anakabiliwa na upinzani na kupelekea kuiona tena njia ya matumaini pale unapopambana na unyama. 

  Katika zama hizi za teknolojia na uharaka wa maisha ya kisasa, ushairi hufunya nafasi kwa ajili ya uhuru na kuvinjari, hali iliyo ndani ya utu wa mwanadamu. Kutoka Arirang za huko Korea hadi Pirekua za Mexico, nyimbo za Hudhud za jamii ya watu wa Ifugao, Alardah za Saudi Arabia, Koroghlu za jamii ya watu wa Turkmenistan na maeneo ya Iran na Afghanistan, na Aitysh za watu wa Kyrgyz, kila utamaduni una aina ya sanaa yake ya ushairi inaoutumia kupeleka na kusambaza maarifa, maadili ya kijamii na kiutamaduni na kumbukumbu za pamoja, ambayo huimarisha kuheshimiana, mshikamano wa kijamii na kutafuta amani.

  Leo hii, nawapongeza washairi, wasanii, waghani, na wale wote ambao sauti zao, bila ya wao wenyewe kujulikana, wamejitoa, kwa na kupitia ushairi, kutoa masomo katika hali ya taswira au ya uwazi, katika bustani au katika mitaa. Ninatoa wito kwa nchi wanachama wote wa UNESCO kuunga mkono juhudi hizi za ushairi, ambao una uwezo wa kutukusanya pamoja, bila kujali asili au imani, kwa lile lililo hasa katika kiini cha ubinadamu

  0 0

   Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa pili kushoto), akimkabidhi kijana Joram Deus (wa pili kulia), mmoja wa vijana wanaojishughulisha na uvuvi wa samaki katika ziwa victoria, msaada wa   msaada wa vifaa mbali mbali vya  uvuvi na mashua yenye injini mpya kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kisiwani kwao Iramba, Kagera mwishoni mwa wiki hii. Wanaoshuhudia ni ndugu wa vijana hao na wanakijiji wa eneo hilo.
   Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kushoto), akimkabidhi kijana Joram Deus (kulia), mmoja wa vijana wanaojishughulisha na uvuvi wa samaki katika ziwa victoria, msaada wa msaada wa vifaa mbali mbali vya  uvuvi na mashua yenye injini mpya kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kisiwani kwao Iramba, Kagera mwishoni mwa wiki hii. Wanaoshuhudia ni ndugu wa vijana hao na wanakijiji wa eneo hilo.
   Kijana Joram Deus anayejishughulisha na uvivu wa samaki, akiangalia vifaa mbali mbali walivyokabidhiwa na Airtel Tanzania, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika  kisiwani kwao Iramba, Kagera mwishoni mwa wiki hii. Wanaoshuhudia ni ndugu wa vijana hao na wanakijiji wa eneo hilo.

  Airtel FURSA yawafikia vijana kisiwa cha Iramba, Kagera
  ·        Yatoa msaada wa zaidi ya Shs milioni 22 kuwawezesha vijana hao.

  Kagera, Jumapili  20 Machi  2016Wiki hii Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa umeweza kuwafikia vijana wa kisiwa cha Iramba Mlumo mkoa wa Kagera wanaojishughulisha na uvuvi kisiwani hapo kwa kumuwezesha vijana Joram Deus na wenzie wawili vifaa bora vya uvuvi vyenye dhamani ya shilingi milioni 22, hatua inayotajwa kufungua mustakabali mpya wa maendeleo katika kisiwa hicho.

  Akiongea wakati wa hafla fupi ya makabidhiano katika kisiwa cha Iramba, Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki alisema, kuwezeshwa kwa vijana hawa kupitia Airtel Fursa ni ukombozi wa kiuchumi kwa familia zao na wakazi wa Iramba.

  Airtel Fursa inatekeleza  wajibu wake katika kurudisha sehemu ya faida  kwa jamii ili kukidhi matakwa ya kiuchumi ama kijamii katika eneo husika hasa kwa vijana, na kuunga mkono jitihada za serikali katika kubadilisha maisha ya wananchi.

  Nae mwenyekiti kijiji cha Iramba Mlumo, Novatus Bernado alisema “sekta ya uvuvi ni miongoni mwa sekta za kiuchumi nchini Tanzania, sekta hii ilitazamiwa kukua kwa asilimia 5.3 hadi kufikia mwaka 2015, huku ajira rasmi na zisizo rasmi zikitengenezwa hususani kwa wakazi wanaozunguka maeneo ya vyanzo vya maji kama vile Ziwa, mto ama bahari.

  “Wakazi wa Muleba uvuvi ndio shughuli zetu kuu kiuchumi, changamoto ya zana bora kwa shughuli hiyo ndiyo iliyomfanya kijana wetu Joram kuitikia wito wa kushiriki katika mpango wa Airtel Fursa ili apate kuwezeshwa kuendesha uvuvi wenye tija na kufungua milango zaidi ya kiuchumi na biashara kisiwani hapa.Tunawashukuru sana Airtel kwa kuweza kutuwezesha kwani imegusa uchumi wa kaya husika na pengine ikawa chachu ya ukuaji wa sekta ya uvuvi katika mwalo huu”

  Akipokea  vifaa hivyo  Joram  ameishukuru Airtel Fursa kwa kuweza kubadilisha mtazamo wa biashara yao ya uvuvi, na kuwakumbusha vijana wengine kwamba vijana watoe fikira kwamba wengi wanaamini maisha mazuri na fursa za kiuchumi zinapatikana mjini tu ila wajue pale watakapo nyoosha mkono ndipo watakaposhikwa mkono na kuonyeshwa njia.

  “Airtel fursa imefungua milango kwa sisi vijana na kutuwezesha kuyafikia malengo yetu yenye kukidhi mahitaji yetu na jamii inayotuzunguka.

  Mpango huu ni wa kitaifa vijana wanapewa wito wa kuendelea kushiriki katika kuainisha fursa zao kupitia Airtel Fursa ili kuwezesha na kuyafikia malengo yao.

  0 0
 • 03/21/16--01:21: Article 13
 • luf
  Digital Pastor ni filamu kali ya Kitanzania ambayo itakua mtaani nchi nzima kuanzia Tar. 7 mwezi Machi jumatatu , ni DIGITAL PASTOR haijawahi tokea sanamu kuongea mti kuongea yote hayo yamo kwenye DIGITAL PASTOR imetengenezwa na kampuni ya kutengeneza filamu ya Lufedha Film Co humo wamo washiriki kama Beni Branco. mchekeshaji maarufu Senga. Salehe Lufedha. Modesti Bafite. nawengine wengi filamu hiyo ya DIGITAL PASTOR.

  0 0

  Uongozi wa Al Masjid Qubbah na Madrasat Rahman ya Tabata Segerea Mwisho,Dar-es-salam inatoa shukurani kubwa sana kwa wale wote waliudhuria na kuchangia kwa kila hali kufanikisha shughuli ya Mawlid ya Mtume Muhammad (S.W.A) yaliyofanyika jumamosi 19 Machi 2016 katika viwanja vya madrasat Rahman Segerea mwisho,jiji Dar-es-salaam ambapo shughuli hiyo ilifana sana kuanzia saa 4 asubuhi kulianza na shughuli ya mawlid upande wa wanawake hadi saa 10 alhasir,ambapo wanafunzi wa kike kutoka madrasa mbali mbali na akimama warishiki,ilipofika saa 2 usiku baada ya swala ya insha ndio kukaanza mawlid ya jumla ambapo wageni, madrasa na wanazuoni mbali mbali walijumuika katika Mawlid hayo ya mtume Muhammad (S.W.A) shughuli iliyojaa baraka tele ilimalizika jumapili asubuhi.

  Madrasa Rahaman Segerea mwisho inawashukuru pia wanahabari na mitandao yote ya kijamii kwani mchango wenu ni mkubwa ni mungu pekee atakaye walipa INSHAALLAH. WABILLAH TAUFIQIH mawasiliano Simu 0777 000036, au 0712 840 960

  www.facebook.com/profile.php?id=100006405199429
  Baadhi ya waumini wa dini ya kiislam wakiwa katika shughuli ya Mawlid, Segerea mwisho, Jijini Dar es salaam.
  wakina mama na wasichana wa kiislam wakiwa kwenye Mawlidi katika viwanja vya madrasa rahman, Segerea mwisho Jijini Dar.
  Wakinamama walianza shughuli ya Mawlid mapema katika viwanja vya madrasa rahman Segerea mwisho, Jijini Dar.

  0 0


  0 0

  Sasa wateja wa NMB na wasio wateja wa NMB wanaweza kufanya malipo ya tiketi za kusafiria za Fastjet kupitia matawi ya NMB yaliyopo nchi nzima au kwa kupitia NMB Mobile. Njia hizi za malipo zitawarahisishia wateja zaidi ya milioni mbili wa benki ya NMB na zaidi ya wateja laki mbili wa kampuni ya ndege ya Fastjet kununua tiketi zao za kusafiria kwa urahisi zaidi. Kwa wale wateja wa NMB, wanaweza kukamilisha manunuzi ya tiketi kwa kutumia NMB mobile au kupitia zaidi ya matawi 170 ya NMB yaliyopo nchi nzima.

  Akiongea na waandishi wa habari, Mtendaji Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker alisema,"Tunayo furaha kushirikiana na fastjet ambayo ni kampuni kubwa ya ndege na yenye gharama nafuu nchini hivyo tunaamini kwamba ushirikiano huu utasaidia kuleta huduma zetu karibu zaidi na watu kupitia mtandao na matawi yetu nchini”.

  Kulipia tiketi ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kufanya maandalizi y safari kupitia tovuti ya fastjet au vituo vyao vya mauzo ambapo utapata namba ya kumbukumbu yenye tarakimu nane. Ukishapata hii namba ya kumbukumbu, kwa wateja wa NMB unaweza kulipia kwa kupitia NMB mobile Piga *150*66# kisha chagua Malipo ya Bili halafu chagua Fastjet.

  Kwa wateja wasio wa NMB, wanaweza kutembelea tawi lolote la NMB ili kufanya malipo. Ukishafanya malipo, utapata SMS ya uthibitisho wa malipo pamoja na ticket itakayotumwa kwenye barua pepe ambayo utakua umeisajili wakati wa kupanga safari. Hakikisha una namba yako ya kumbukumbu wakati wote ili ikuwezeshe kufanya malipo popote ulipo.
  Mtendaji Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker na Meneja Mkuu wa Fastjet nchini Bw. John Corse wakieka saini mkataba ambao utawanufaisha wateja wa NMB na ambao sio wateja wa NMB kuweza kulipia tiketi za usafiri wa ndege kupitia NMB Mobile na matawi ya benki yaliyopo nchi nzima.
  Kaimu Afisa Mkuu wa wateja wadogo na kati NMB (kulia), Bw. Abdulmajid Nsekela akifurahia pamoja na Mtendaji Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker na Meneja Mkuu wa FastJet Bw. John Corse baada ya kukamilisha hafla ya makubaliano hayo iliyofanyika katika hoteli ya Courtyard Protea jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na Kati wa NMB, Bw. Abdulmajid Nsekela akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jinsi gani wateja wa NMB na ambao sio wateja wanaweza kununua tiketi kwa kupitia NMB mobile na matawi ya NMB.

  0 0

  Meneja wa Mpango wa uchangiaji wa Hiari PSPF Bi. Mwanjaa Sembe kushoto akimkabidhi vitambulisho vya wanachama wa Mfuko huo Bi. Lightess Thobia kulia ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ASHATA katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Afisa Uendeshaji kutoka Mfuko wa Uchangiaji kwa Hiari PSPF Bw. Delphine Richard wa pili kutoka kulia akimuelekeza jambo Mkurugenzi wa taasisi ya ASHATA Bi. Lightess Thobia katika hafla ya makabidhiano ya vitambulisho vya wanachama iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Afisa Uendeshaji kutoka Mfuko wa Uchangiaji kwa Hiari PSPF Bw. Delphine Richard akiwaelimisha wajasiriamali umuhimu wa kujiunga na mfuko huo kwa hiari.

  0 0


  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Jaji Aloysius Mujulizi (Kushoto aliyesimama) akifungua warsha ya siku moja baina ya Tume na Wadau kujadili mapendekezo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura ya 410 ya Mwaka 2011, iiliyofanyika katika ukumbi wa Tume Dra es Salaam.
    Baadhi ya wadau wakifuatilia vipengele vya sheria wakati wa kupitia mapendekezo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma.
  Sekretarieti ya Tume ikiwa makini kufuatilia hoja zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kupitia mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma.
  (Picha zote na Munir Shemweta, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania).

  0 0

  RAIS na afisa mkuu wa shirika la ndege la Etihad, bwana James Hogan alitoa hotuba ya ufunguzi mbele ya zaidi ya wajumbe 1,200 waliohudhuria kongamano kuu la masuala ya huduma ya mizigo lilofanyika katika kituo cha maoneyesho cha Abu Dhabi kuanzia tarehe 10 hadi 13 Machi.

  Bwana Hogan aliongelea kiundani juu ya mabadiliko katika sekta ya mizigo na jinsi gani muungano wa washirika wa shirika la ndege la Etihad umeongeza nguvu katika utendaji kazi wa kitengo hicho cha mizigo. Kwa kuunganisha ndege za mizigo na mitandao yake, kitengo cha mizigo cha Etihad kinatambulika kama kitengo namba tano (5) kwa ukubwa duniani kikishirikiana kwa ukaribu wa dhati na kitengo cha mizigo cha shirika la ndege la Jet, kitengo cha mizigo cha shirirka la ndege la berlin, Serbia, Alitalia, na kitengo cha mizigo cha shirika la ndege la Seychelles.

  Kitengo cha mizigo cha shirika la ndege la Etihad hutengeneza zaidi ya dola bilioni 1 za kimarekani kama mapato ya mwaka na kukifanya kuwa  moja ya kitengo cha mizigo chenye mafanikio zaidi duniani.  Kilifanikiwa kuhudumia asilimia 88 ya mizigo yote iliyoingia, iliyotoka na iliyosafirishwa  katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi mwaka 2015, mwaka ambao kitengo hicho kilibeba tani 529,090 za mizigo na barua, jumla ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 4 ya mwaka 2014.

  Kwa sasa kitengo cha mizigo cha Etihad kwa kutumia ndege nne aina ya boeing 777F, tatu aina ya boeing 747s, na nne aina ya airbus A330s. ndege iliyoongezwa aina ya  boeing 777 inatazamiwa kuwasili ndani ya mwezi huu uku nyingine aina ya airbus A330 ikiwa imepangwa kuwasili mwaka 2017.

  Bwana Hogan alizungumzia jinsi gani Kanda ya Mashariki inaendelea kufanya vizuri katika viwango vya ukuaji wa kimataifa kwenye sekta ya mizigo na ina jukumu muhimu katika mtiririko wa biashara na bidhaa duniani, pamoja na umuhimu wake wa kijiografia kuimarika kutokana na wadau kuhama masoko ya zamani yaliojazana na kuanzisha masoko mapya katika vituo vya biashara huko Mashariki ya Kati, Asia, Amerika ya Kusini na Afrika.

  Alisema: "Kitovu chetu cha Abu Dhabi ni njia panda ya dunia chenye kitengo kikubwa cha kushugulikia mizigo, Shirika la ndege la Etihad  limejiweka nafasi nzuri kunufaika na ongezeko la abiria, ongezeko la mizigo na bidhaa zinazosafirishwa baina ya masoko makubwa na yale mapya”

  Etihad Cargo inatoa huduma ya kubeba mizigo kawaida ndani ya ndege pamoja na kwenye buti la ndege huduma hizi zikifikia mtandao wa abiria pamoja na vituo vya mizigo tu.

  "Kitengo cha mizigo cha Etihad kimekuwa biashara inayoingiza mapato ya mabilioni na inawakilisha sehemu kubwa ya biashara yetu kwa kujidhatiti kutoa huduma maalumu kwa wateja pamoja na bidhaa zenye ubunifu zenye kutoa ushindani mkubwa na kuvutia wateja wetu. Kwa kufanya kazi na washirika wetu, tutaendelea kuongeza faida ya kila kituo cha mizigo kwa kuchanganya rasilimali, mitandao na uwezo kwa manufaa ya wateja wetu wote "alisema Bw Hogan.

  Ushirikiano na watendaji wengine wa mizigo, zikiwemo Atlas Air na Avianca, hutoa msaada mkubwa kwa kituo kikuu, na kitengo kinaendelea fursa za ushirikiano na vitengo vingine vya waendeshaji mizigo. Shirika kwa hivi sasa linafanya kazi katika vituo 14 vinavyojihusisha na mizigo tu ikiwa ni pamoja na Bogotá, Brazzaville, Chittagong, Djibouti, Dubai World Kati, Eldoret, Guangzhou, Hanoi, Houston, Sharjah na Tbilisi.

  0 0

   Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Joel Balisidya (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni 1/- kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko (wa pili kushoto) baada ya kuibuka Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara,mwezi Desemba mwaka jana.Kulia ni Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh na Kocha Msaidizi, Juma Mwambusi.


                                                       Na Mwandishi wetu
  WADHAMINI Wakuu wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Kampuni ya mawasiliano ya simu Vodacom Tanzania, wamekabidhi kitita cha Shilingi milioni moja  kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko baada ya kuibuka Mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi Desemba  mwaka jana.
  Mzimbabwe huyo alikabidhiwa kitita hicho jana na Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Joel Balisidya wakati timu hiyo ikifanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kujiandaa na mechi yao ya leo  dhidi ya APR ya Rwanda katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

  Katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo hiyo Kamusoko alimshinda mchezaji mwenzake wa Yanga, mshambuliaji Amiss Tambwe, raia wa Burundi.

  Kamusoko aliisadia timu yake ya Yanga kupata ushindi katika michezo iliyochezwa mwezi Desemba kwa kushiriki dakika zote katika mechi tatu zilizochezwa mwezi huo.

  Akizungumza baada ya kukabidhiwa kitita hicho wakati  mahojiano aliyofanya na Vodacom Tanzania, Kamusoko aliishukuru kampuni hiyo kwa kudhamini Ligi Kuu  hiyo akisema kwamba imemuwezesha kuonesha kipaji chake.

    Mbali na kuishukuru kampuni hiyo,  Kamusoko pa aliwashukuru  mashabiki wa timu yake kwa kuendelea kuwasapoti wachezaji na amesema anawapenda na anawaamini sana.

  "Ninaimani kila timu inapocheza na Yanga inatamani kutufunga, hivyo ninawaomba mashabiki wawe wavumilivu, lakini tunawahakikishia ushindi kila tunapocheza kwenye uwanja huu” alisema Kamusoko.

  Naye kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi  aliwashukuru Vodacom akisema kwamba  wamemchagua mchezaji ambaye ana vigezo vyote vya kuweza kuwa mchezaji wa Yanga”

  Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amewataka wachezaji wanaoshiriki katika  ligi hiyo kujituma ili nao waweze kujinyakulia kitita kama hicho.

  “Sisi kama wadhamini wa ligi hii  tunaona fahari mchezaji anapojituma uwanjani na kuisaidia timu yake,hivyo niwaombe wachezaji wajitume ili waweze kuzawadiwa,”alisema Nkurlu.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Mamlaka ya Reli Nchini (TRL) imesitisha safari zake kutoka Dar es salaam kwenda Mikoani na kuhamishia huduma hiyo mkoani Dodoma kutokana miundombinu ya reli kuharibiwa na mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini. 

  Mvua hizo zimeharibu miundombinu ya reli ya kati wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Kaimu Mkurugenzi TRL, Masanja Kadogosa amesema kuwa kutokana na kusitishwa kwa huduma hiyo ratiba ya huduma mpya inatarajiwa kuanza kesho Machi 22 kwa wasafiri wanaotarajia kusafiri kutoka Dodoma kwenda Mwanza na Kigoma kuanzia majira ya  saa 11 jioni.

  Amesema gari moshi jipya ya Delux kwa wasafiri wa Kigoma wanatakiwa kukata stakabadhi ya malipo ya safari siku ya Jumanne saa 2:00.

  Kadogosa amesema kuwa jitihada mbalimbali zinaendelea kufuatia mashirikiano kati ya kampuni hodhi ya Rahco pamoja na Shirika la reli nchini ili kuweza kurejesha huduma hiyo kama ilivyokuwa awali.

  Amesema kuwa wasafiri wanaotumia usafiri huo waondowe wasiwasi kutokana na jitihada zinazofanywa za urejeshaji wa huduma ya reli.

  0 0

  Aliekuwa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dkt. Ali Mohammed Shein akikabidhiwa cheti cha Ushindi kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha, mara baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Zanzibar akiwa na kura 299,982.
  Aliekuwa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamed ndiye alieshika nafasi ya pili akiwa na kura 9,734.

   Matokeo kamili kama yalivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), yanaonesha licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia, mgombea wake Maalim Seif Sharif Hamad alipata kura 6,076 kwenye uchaguzi wa marudio uliofanyika Jumapili.

   Kulikuwa na wagombea 14 kwenye karatasi za kura za kumchagua Rais. Majina yao ndiyo haya: 

  1Khamis Iddi LilaACT-W
  2Juma Ali KhatibADA-TADEA
  3Hamad Rashid MohamedADC
  4Said Soud SaidAFP
  5Ali Khatib AliCCK
  6Ali Mohamed SheinCCM
  7Mohammed Massoud RashidCHAUMMA
  8Seif Sharif HamadCUF
  9Taibu Mussa JumaDM
  10Abdalla Kombo KhamisDP
  11Kassim Bakar AlyJAHAZI
  12Seif Ali IddiNRA
  13Issa Mohammed ZongaSAU
  14Hafidh Hassan SuleimanTLP

  0 0
 • 03/21/16--03:52: TAARIFA YA UTEUZI


 • 0 0

  Msafara wa Wabunge wa Mkoa wa Pwani, RAS na Kamati ya TAMISEMI umepata ajali katika eneo la Kerege, Bagamoyo Mkoani Pwani, iliyohusisha Magari mawili yaliyogongwa na Lori. Gari la Mkurugenzi wa Bagamoyo na Gari la TASAF Bagamoyo. Inaelezwa kuwa Madereva wa magari hayo wawili pamoja na Afisa Mipango wamefariki papo hapo na Majeruhi wamekimbizwa Muhimbili hali mbaya.

  Taarifa kamili itawajia baadae kidogo.
   Hivi ndivyo ionekanavyo moja ya gari lililohusika kwenye ajali hiyo.


  0 0

  Tunauza viwanja ambavyo vimepimwa kwa maana vina offer tayari kwa bei ya 15000 kwa square meter moja. Eneo ni Kigamboni kata ya kisarawe 2 mtaa wa Vumilia Ukooni Dar es salaam. Kilometer 3 kutoka barabara kuu inayokwenda Kimbiji kituo ni Dege au ECO village.
  Kwa mawasiliano

older | 1 | .... | 1166 | 1167 | (Page 1168) | 1169 | 1170 | .... | 3282 | newer