Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1156 | 1157 | (Page 1158) | 1159 | 1160 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa Milamba kwenye mkutano wa kuwashukuru na kuwapa taarifa za mambo ambayo ameshafanya mpaka sasa.
  Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Yahaya Nawanda akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mulogo/ Mnazi Mmoja na kuwataka wanakijiji hao kushirikiana ili kufanikisha maendeleo katika kijiji hicho.
  Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na wazee wa kijiji cha wa Milamba mara baada ya kumaliza kwenye mkutano wa kuwashukuru na kuwapa taarifa ya mambo ya kimaendeleo ambayo ameshaanza kuyafanyia kazi.
  Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nambahu.

  0 0

   Naibu waziri wa maji na umwagiliaji mhandisi Izack Kamwele akikagua chanzo kikuu cha maji safi na salama cha mradi wa kuongeza upatikanaji wa maji katika mji wa kigoma kilichopo eneo la katonga.
  Baadhi ya vibarua katika mradi huo wakifukia mabomba ya kupitisha maji yanayotoka kwenye chanzo katika eneo la Katonga
  Naibu waziri na Mhandisi Izack Kamwela akiongea na waandishi baada ya kukagua mradi wa maji Kigoma

  Na, Editha Karlo,wa blog ya jamii Kigoma
  NAIBU Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwela amewabana wakandarasi wa mradi wa maji wa kuongeza uwezo wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa Mkoa wa Kigoma kwa kushindwa kumaliza mradi kwa muda muafaka uliokuwa ndani ya mkataba.

  Akiongea na wakandarasi hao katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa kayika kwenye ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea mradi huo alisema kuwa mradi huo ulitakiwa kuisha mwaka jana mwezi wa kumi na mbili laki mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 46 tu.

  "Huu mradi ulitakiwa uishe ndani ya miezi 24 kwa mujibu wa mkataba lakini sasa hivi ni miezi 34 mpo nje ya mkataba nataka kujua tatizo ni nini? hii siyo kasi ya awamu ya tano"Alisema Mhandisi Kamwele.

  Aliongeza kwa kusema kuwa sasa hivi kila wiki mkandarasi anatakiwa kukaguliwa na akishindwa kukamilisha kazi  mkataba wake utavunjwa, na kama hawezi kukamilisha kazi kwa wakati atafute wakandarasi wenzake wamsaidie tena wakandarasi hao wawe daraja la kwanza. 

  Alisema kuwa mradi huo unatakiwa kukamilika mwezi wa kumi na mbili mwaka huu na usipo kamilika wahusika watawajibishwa kwani watakuwa wameipatia serekali hasara kubwa.

  Naye Mhandisi mshauri wa mradi huo Michael Mwamkinga alisema kuwa mradi huo ulitakiwa uwe umekamilika march 2015 lakini mpaka sasa ni asilimia 46 tu za mradi huo ndo zimekamilika.

  Alisema  sababu zilizopelekea mradi huo kushindwa kukamilila kwa wakati ni mkandarasi aliyepewa tenda hiyo ambaye ni SPEECON alikopa fedha kutoka  Equity Bank na kushindwa kulipa mkopo huo atimaye bank imeamua kumfirisi.

  Mwamkinga alisema kuwa mpaka sasa  asilimia 98 za mradi huo upo chini ya bank hiyo ambapo mradi huo unagharimu zaidi ya euro bilioni 16 chini ya ufadhiri wa European union(umoja wa nchi za ulaya).

  Alisema kuwa baada ya miezi miwili mradi huo utakuwa umekamilika kwa asilimia 70.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali mstaafu Issa Machibya alisema kuwa hali ya upatikanaji wa maji  safi na salama katika mji wa Kigoma umeongezeka kutoka asilimia 56 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 68  mpaka sasa kwasababu ya mradi wa uboreshaji wa maji safi na salama vijijini.

  Machibya alisema kuwa changamoto ziluzopo Kigoma katika sekta ya maji ni upotevu wa maji,ukosefu wa mitambo ya kusafirishia maji, upungufu wa wataalam wa maji kwa Wilaya zote na ukosefu wa pesa za kuboreshea miradi ya maji vijijini.


  0 0

  Bendi maarufu Inafrika band aka Wazee wa Indege wanatarajiwa kuruka wakati wowote ule kuelekea nchini marekani kushiriki katika maoyesho makubwa ya kimataifa ya Festival of nations ,yatakayo fanyika katika Dollywood Theme Park,bendi hii kutoka Tanzania ndio bendi pekee iliyoteuliwa kuliwakilisha bara la Afrika katika maonyesho hayo ya kimataifa.

  Inafrika band itakuwepo nchini marekani katika ziara ya kikazi kwa muda wa miezi mitatu kuzikonga nyoyo za washabiki wa kimataifa nchini marekani.

  Kuchaguliwa kwa Inafrika band kushiriki maonyesho hayo makubwa kunatokana na mvuto wa muziki wa bendi hiyo kukubalika zaidi kimataifa.
  Muziki ambao una maadili ya kitanzania ambako nje ya mipaka umewateka
  washabiki wengi wa kimataifa. 
    
  Bendi hiyo yenye makao jiji Dar-es-salaam imejikuta haina muda wa kupumzika kutoka na wingi Tour za kimataifa kwa muda wa miaka 10 sasa.
  Ni kama wiki mbili tu bendi hiyo imerudi kutoka safari ya nchi 19 za bara la ulaya. Tunawatakia kila la heri Inafrika Band aka Wazee wa Indege katika kutuwakilisha huko Marekani. Bendi hiyo ilikuwapo Dollywood ,Marekani mwaka 2014 na kuwanasa washabiki wengi na muziki wao wa kitanzania
  watupie jicho hapa.


  0 0

   Viongozi wa Kitaifa waliohudhuria mazishi ya  Marehemu Mzee Ibrahim Amaan wakikamilisha hitma ya kumuombea kiongozi huyo Mwanamapinduzi ya Zanzibar huko Kijijini kwake Nymanzi Wilaya ya Magharibi “B”.
   Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakisubiri ibada ya sala ya Maiti kwa ajili ya kumuombea Dua zee Ibrahim Amaan kwenye Msikiti wa Ijumaa aliokuwa mioingoni mwa watu waliouanzisha Kijijini kwake Nyamanzi.
  Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiongozwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Ngwali walimsalia Mzee Ibrahim kwenye msikiti wa Kijiji hicho.
  Picha na – OMPR – ZNZ.
                                     
  MWANAMAPINDUZI ya Zanzibar ya Mwaka 1964 ambae pia ni mwanzilishi wa Chama cha Mapinduzi Mzee Ibrahim Aman aliyefariki Dunia jana mchana amezikwa leo Kijijini kwake Nyamanzi Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi.

  Mzee Ibrahim aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya baridi pamoja na Uzee alilazwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja akipatiwa matibabu kutokana na afya yake.

  Mamia ya Wananchi, waumini wa dini  pamoja na Viongozi wa Kitaifa walihudhuria mazishi hayo yaliyojumuisha pia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu wa SMT  Dr. Mohammed Gharib Bilal.

  Mzee Ibrahim Amaan alizaliwa mwaka 1930 katika Kijiji cha Nyamazi na alipofikia umri wa kusoma Wazazi wake wakampelekea kupata elimu ya Quran iliyoambatana na ile ya Dunia katika ngazi ya Msingi.

  Wakati wa ujana wake marehemu Mzee Ibrahim Amaan alijishughulisha na kazi za ukulima na uvuvi ili kujipatia kipato kilichomuezesha kuanza kujitegemea katika maisha yake ya kawaida.

  Mwaka 1957 Mzee Ibrahim alijiunga na Chama cha Afro Shirazy Party ambapo  kutokana na uzalendo pamoja na umakini wake alifanikiwa kuwa muanzilishi wa Umoja wa Vijana wa ASP  Mkoa wa Kusini Unguja.

  Katika Uhai wake marehemu Mzee Ibrahim aliwahi kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri ya Chama cha Afro Shirazy Party na kushiriki kuuangusha Utawala wa kisultani Mwaka 1964 na baadaye kujiunga na Jeshi la Ukombozi la Unguja akifikia cheo cha Kanal.

  Akisoma Risala ya wakfu wa Marehemu Mzee Ibrahim Makungu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Ikulu na Utawala Bora Dr. Miwinyihaji Makame alisema Chama cha Mapinduzi, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zimepokea kwa masikitiko kifo cha Mwanamapinduzi huyo aliyejitolea muda wake wa maisha kulitumikia Taifa hili.

  Dr. Mwinyihaji alisema Ushujaa wa Mzee Ibrahim ulimpelekea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein kumtunukia Nishani ya Ushujaa wa Mapinduzi kwenye sherehe hizo za mwaka 2014.

  Alisema Mzee Ibrahim miongoni mwa majukumu yake  kwa Taifa aliwahi pia kuwa Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Katibu wa  CCM Idara ya Umma Afisi kuu ya CCM Kisiwandui pamoja na Mwenyekiti wa kazi za njia na nnguvu za umeme.

  Dr. Mwinyihaji alifafanua zaidi kwamba Mzee Ibrahim alikuwa Mjumbe wa Baraza la Wazee la Chama cha Mapinduzi wadhifa ambao aliendelea nao hadi mauti yalipomfika.

  Mzee Ibrahim  Amaan aliyezaliwa mwaka 1930 na kufikisha umri wa Miaka 86 ameacha kizuka Mmoja na Watoto Thalathini.
  Yarabi aiweke roho ya Marehemu Mzee Ibrahim Amaan mahali pema Peponi amin.

  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  12/3/2016.

  0 0

  Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Kanga Meternity Trust (KMT) Dkt. Mohd Hafidh akitoa maelezo ya taasisi hiyo inavyofanya kazi zake kuhakikisha Mama wajawazito wanapata huduma bora wanapokwenda kujifungua hospitali Kuu ya Mnazimmoja katika hafla ya kuwasilishwa Utafiti wa Mradi wa PartoMa iliyofanyika Hoteli ya Tembo, Forodhani Mjini Zanzibar.
  Madaktari bingwa wa Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Naufal Kassim (kushoto), Dkt. Zaki (kati) na Mwenyekiti wa KMT Dkt. Mohd Hafidh wakijadiliana jambo wakati wa hafla ya kuwasilishwa utafiti uliofanywa na Dkt. Anna Maaloe (hayupo pichani) kuhusu wadi za wazazi za Hospitali ya Mnazimmoja.
  Mtafiti kutoka Mradi wa PartoMa Dkt. Anna Maaloe akiwasilisha utafiti wake juu ya huduma za wodi za wazazi za Hospitali kuu ya Mnazimmoja katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Tembo Forodhani Mjini Zanzibar.
  Mwenyekiti wa Baraza la wauguzi na wakunga Dkt. Amina Abdulkadir akitoa mchango wake wakati wa kuwasilishwa utafiti wa huduma za wodi za wazazi za Hospitali kuu ya Mnazimmoja. Picha na Makam Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  Dkt. Ali Salum kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospitali kuu ya Mnazimmoja akimkabidhi cheti na zawadi Metroni Mkuu wa Hospitali hiyo kwa kushiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Mradi wa PartoMa katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Tembo.
  Wauguzi wa wodi ya wazazi katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja wakimpa zawadi ya mlango na kasha Dkt. Anna Maaloe kwa kazi nzuri aliyosimamia ya utafiti wa wodi za wazazi katika Hospitali ya Mnazimmoja. Picha na Makam Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  ………………………………………………………
  Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar 

  Mradi wa PartoMa unaoshirikisha Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini Denmark na Hospitali Kuu ya Mnazimmoja wenye lengo la kuongeza ufanisi na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa wodi za wazazi katika hospitali ya Mnazimmoja umeanza kuleta mafanikio makubwa.

  Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mradi wa PartoMa kwa kushirikiana na Taasisi isiyo ya kiserikali Kanga Martenity Trust (KMT) iliyopo Hospitali ya Mnazimmoja umeonyesha vifo vinavyotokana na uzazi na vifo vya watoto wanaozaliwa vimepungua tokea kuanza kwa mradi huo mwaka mmoja uliopita.

  Akiwasilisha utafiti uliofanywa na mradi wa PartoMa ambao uliwashirikisha madaktari, wakunga na wasaidizi wakunga katika wodi za wazazi, Dkt. Anna Maaloe amesema bado ni mapema kuthibitisha kuwa mafanikio hayo yanatokana moja kwa moja na kuwepo mradi huo lakini ufanisi na utaalamu wa wafanyakazi kwenye wodi za wazazi Hospitali ya Mnazimmoja umeongezeka.

  Amesema Hospitali za rufaa, kama ya Mnazimmoja zinawajibu mkubwa wa kuwa na mafunzo ya mara kwa mara kwa wafanyakazi waliopo na wanaotegemewa siku za mbele na kuweka miongozo bora ili kuokoa maisha ya mzazi na mtoto pamoja na wagonjwa wa kawaida.

  “Kwa kuliona hilo mradi wa PartoMa umekuwa ukiandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo madaktari na watendaji wa wodi za wazazi Hospitali Mnazimmoja siku moja kwa miezi mitatu baada ya saa za kazi na kuweka miongozo ambapo wafanyakazi wengi wamekuwa wakishiriki,” aliongeza Dkt. Anna.

  Katika utafiti huo Dkt. Anna amesema imebainika kuwa wafanyakazi wengi wa Hospitali ya Mnazimmoja wamehamasika kuongeza elimu na ufanisi na hiyo inasaidia katika kuokoa maisha ya wananchi.

  Hata hivyo amesema bado kunachangamoto katika kutoa huduma bora zaidi katika Hospitali ya Mnazimmoja ikiwemo uhaba wa wafanyakazi katika wodi za wazazi ukilinganisha na ongezeko kubwa la wazazi wanaotumia Hospitali hiyo.

  Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Hoteli ya Tembo Forodhani, Mwenyekiti wa KMT Dkt. Mohammed Hafidh amesema utafiti huo ambao ni wa kwanza kufanywa na kuwashirikisha watafiti wa wazalendo Hospitali ya Mnazimmoja utasaidia kuwa na taarifa sahihi na za uhakika kwa maendeleo ya Hospitali hiyo.

  Amesema lengo la utafiti huo ni kuwasaidia mama wajawazito kujifungua salama na kwa heshma na kuzuia vifo vya mama na mtoto ambavyo vinaweza kuzuilika.

  Nae Dkt. Naufal Kassim amekiri kuwepo mtafartoMa na ameshauri madaktari kujipanga kufanya tafiti zaidi za afya na kuyatumia matokeo ya tafiti zilizopo kwa ukamilifu.

  Katika hafla hiyo Dkt. Ali Salum kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja aliwakabidhi vyeti madaktari, wakunga na wasaidizi wakunga walioshiriki mafunzo ya kuwajngea uwezo baada ya saa za kazi bila malipo katika hospitali hiyo.

  0 0
  0 0  SIMU.TV: Timu ya Yanga yaibuka kidedea ugenini baada ya kuifunga magoli mawili kwa moja timu ya APR kutoka nchini Rwanda: https://youtu.be/6hFcn55brp8

  SIMU.TV:Watu watatu wapoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi katika mgodi wa JW mkoani Manyara;  https://youtu.be/F1FpwMfPpXc
  SIMU.TV:Ofisi ya bunge yatoa ufafanuzi juu ya kukamatwa kwa mbunge Ester Bulaya na kusafirishwa kwenda Dar es Salaam;https://youtu.be/JF0j0I14OWs 
  SIMU.TV:Serikali yakamata ng’ombe zaidi ya 300 waliokuwa wakitoroshwa kutoka Mvomero bila kuwa na kibali;https://youtu.be/sXQUFrQ5ReU
  SIMU.TV:Wananchi wa Urambo Tabora wamemuomba waziri Isack Kamwelwe kuwawajibisha watendaji walioshindwa kujenga mradi wa maji licha ya kuwachangisha wananchi; https://youtu.be/2gr4nFyxiUE
  SIMU.TV: Katibu mkuu wizara ya maji na umwagiliaji aitaka DAWASA kuepuka gharama za kuagiza wataalam kutoka nje ya nchi;https://youtu.be/w0VGZelbHbc
  SIMU.TV :Rais Magufuli amtumia salamu za rambirambi rais Shein kufuatia kifo cha moja ya wanamapinduzi aliyefariki jana visiwani Zanzibar;https://youtu.be/AanlXwIQhJM  
  SIMU.TV:  Vituo binafsi vya afya vimetakiwa kutoa huduma bora za afya ya uzazi ili kuunga jitihada za serikali kutokomeza vifo vya mama wajawazito na watoto; https://youtu.be/Q1WFNBnrir4 
  SIMU.TV:  Mh.Angela Kairuki ametoa wito kwa waajiri na wananchi kutunza nyaraka muhimu za ajira ili kuwaondolea usumbufu wakati wa kustaafu; https://youtu.be/KDwEJAORGYM 
  SIMU.TV:  Wana tamutamu Mtibwa Sugar waibuka na ushindi dhidi ya JKT Ruvu  baada ya kuwacharaza goli mbili kwa moja;https://youtu.be/37KIld6CDBM
  SIMU.TV:  Udanganyifu wa umri katika michuano ya vijana ya ligi ya mchezo wa kikapu NBA yawa changamoto kwa waendesha mashindano hayo;https://youtu.be/Y9Y2RmqUCwE 
  SIMU.TV:  Somo la hisabati limetaja kuwa moja ya masomo muhimu katika msingi wa wanafunzi kuanzia shule za msingi hadi sekondari. https://youtu.be/vbFH4mz6J1E  
  SIMU.TV:  Jamii imetakiwa kutambua kuwa zama za enzi zimekwisha katika kumkandamiza mwanamke.   https://youtu.be/QhHFKiJ5qu4 
  SIMU.TV:  Jumla ya nyumba 7 za wananchi wa mkoa wa Kaskazini Pemba zimeteketea vibaya kwa moto usiku wa kuamkia leo.https://youtu.be/35E20rZdamM
  SIMU.TV:   Serikali ya Tanzania imesema kuwa ujio wa Rais wa Vietnam utaongeza wigo wa kibiashara katika nchi zote mbili.https://youtu.be/nIorLFKFYYs
  SIMU.TV:  Watu watatu wanahofiwa kupoteza maisha baada ya kupata ajali ya kufunikwa na kifusi katika mgodi mkoani Manyara :https://youtu.be/s_2dcDTUmkE 
  SIMU.TV:  Serikali imeyafunika mashimo  yanayosadikiwa kuwa na dhahabu mkoani Geita, baada ya watu watano kupoteza maisha katika mashimo hayo: https://youtu.be/z1nD57YwQUg
  SIMU.TV:  DAWASCO  wamtumbua majipu mkazi wa manispaa ya Ilala baada ya kujiunganishia maji kinyemela kutoka katika bomba kubwa la DAWASCO: https://youtu.be/Keh-TSHsuP8 
  SIMU.TV:  Timu ya Yanga yaibuka kidedea ugenini baada ya kuifunga magoli mawili kwa moja  timu ya APR kutoka nchini Rwanda:https://youtu.be/6hFcn55brp8

  0 0

  Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Jijini Mwanza, Joseph Stanford, maarufu kwa jina la Rich4D akiwaonyesha wanahabari Jijini Mwanza (hawapo pichani) ramani ya Mkoa wa Dar es salaam aliyoitumia kutambua maeneo ya Mkoa huo.

   Hiyo ilikuwa baada ya kuwasili Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuonana na Rais John Pombe Magufuli ili kumpongeza kwa kuwajumuisha wasanii katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika baraza lake la Mawaziri. Rich4D alitembea kwa miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es salaam ili kutimiza adhma yake hiyo.
  Msanii Joseph Starnford maarufu kwa jina la Rich4D alitembea kwa miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es salaam ili kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuwajumuisha Wasanii katika Baraza lake la Mawaziri, amesisitiza kuwa shauku yake ni kuonana na rais ili kutimiza adhma yake.
  Zaidi Bonyeza HAPA

  0 0

  Shirika la Majisafi na Majitaka Jijini Dar es Salaam (Dawasco) limebaini wizi mkubwa wa Maji kwenye operesheni yake maalumu ya kubaini watumiaji wa huduma ya Maji ambao hawajaunganishiwa kihalali kwenye mtaa wa Ilala kota karibu na nyumba za Shirika la nyumba la taifa (Nhc) jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza kwenye tukio hilo Meneja wa Dawasco Ilala, mhandisi Ramadhani Mtindasi alieleza kuwa wanatekeleza agizo la Mh. Waziri wa Maji ambapo amewaagiza Dawasco kufunya uchunguzi kwenye Magorofa yote makubwa jijini ambayo wanadai wanatumia Maji ya visima na ndipo walipogundua jengo hilo la ghorofa lenye nyumba ndogo (apartments) 8 likiwa na laini mbili moja ya Maji ya kisima na nyingine ni ya Dawasco ambayo haikuwa na mita wala kusajiliwa na Dawasco .

  “Tumeanza operesheni maalum ya kukagua majengo yote makubwa jijini ambayo wanatumia huduma ya Maji ilikubaini kama ni ya visima au ya Dawasco kama Mh. Waziri wa Maji alivyotuagiza na ndipo tulipogundua jengo moja eneo la Ilala kota likiwa na laini ya Maji ya Dawasco ila halina mita wala hatujamsajili amejiunganishia kiholela”

  “Hivyo tuwewashirikisha serikali za mitaa kubaini mmiliki wa jengo hilo lakini hakuweza kufahamika bali tumepata namba zake za simu na tulipompigia alidai anatumia huduma ya Maji ya kisima tu hivyo tumemuandikia barua afike kwenye ofisi zetu kujisali na alipe faini”, alisema mhandisi Mtindasi.

  Kwa upande wa mjumbe mtaa wa Ilala Kota Bi Habiba Hamisi ameeleza kuwa Majengo mengi makubwa yamekuwa yakijiunganishia huduma ya Maji kiholela na kudai kuwa ni ya kisima kumbe sio hivyo kuwafanya wananchi wengine waotegemea huduma ya Maji ya Dawasco kukosa kutokana na kuwa majengo hayo makubwa yana matumizi makubwa.

  “Majengo mengi makubwa yana laini mbili ya Dawasco na visima ila ukiwauliza wasema wanatumia maji ya visima tu kumbe sio kweli na matumizi yao kwenye majengo hayo ni makubwa hivyo wanasabisha wanaostahili kukosa huduma ya maji hivyo Dawasco wawachukulie hatua kali za kisheria” alisema Bi Hamisi.

  Dawasco imewasihii wamiliki wote wa majengo makubwa ambao wamejiunganishia huduma ya Maji Kiholela kujisalimisha mapema kabla ya hatua kali za kisheria hazijachukuliwa juu yao endapo watakamatwa. 

   Meneja wa Dawasco llala (katikati) Mhandisi Ramadhani Mtindasi pamoja na mjumbe wa mtaa wa Kota Bi. Habiba Hamisi akionyesha bomba la Maji ambalo linaleta Maji kutoka kwenye laini kuu lilo uunganishwa kiholela inayotoka kwenye Bomba kubwa kwenye eneo la Ilala Kota Mchikichini Jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa Dawasco Ilala Mhandisi Ramadhani Mtindasi  akionyesha boza linalotumika kuhifadhi Maji yanayotoka kwenye bomba la Dawasco .

  0 0

  Shirikisho  la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limefanya mkutano wake mkuu katika hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, huku mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza akiwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo utakaomalizika kesho kwa shughuli ya uwekaji jiwe la msingi katika eneo la kukuzia vipaji mjini humo.


  0 0


  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York 
  Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, ni Mwenyekiti wa Kundi la Nchi za Afrika katika Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa March. Miongoni mwa majukumu ya Mwenyekiti wa Mwenzi ni pamoja na kuitisha , kuratibu na kuendesha mikutano inayowahusisha Wawakilishi wa Kudumu kutoka Nchi 53 wanaoziwakilisha Nchi zao katika Umoja wa Mataifa. 
  Mwenyekiti wa mwezi, pamoja na kuratibu na kuendesha mikutano yenye ajenda mbalimbali pia anawajibika katika kuwasilisha kauli ya nchi za Afrika kupitia ama utoaji wa hotuba au mawasiliano na Wakuu wa Idara mbalimbali ndani ya Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa, akiwamo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pale inapolazimu. 
  Pichani ni baadhi ya Matukio yaliyotokea mwishoni wa wiki wakati wa Mkutano wa Wawakilishi hao wa Nchi za Afrika chini ya uenyekiti wa Tanzania, ambapo walipokea taarifa mbalimbali kutoka kwa watendaji wa Umoja wa Mataifa pamoja na taarifa kutoka kwa Muungano wa Wakuu wa Idara za Takwimu kutoka Afrika waliokuwa wakishiriki katika Mkutano wa 48 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa.
   Balozi Tuvako Manongi akimkabidhi zawadi ya kumuanga  kwa niaba ya  Mabalozi wenzie  aliyekuwa  Mwakilishi wa  Kudumu wa  Liberia katika Umoja wa Mataifa, Balozi Marjon V. Kamara ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje  wa Liberia. 
   Mkurugenzi  Mkuu wa Ofisi  ya Taifa ya Takwimu, Dr. Albina Chuwa  (kushoto) akitoaa taarifa  fupi kwa niaba ya Wakurungezi  Wakuu wa Idara za Takwimu kutoka  Nchi za Afrika kuhusu maazimio na mapendekezo yao  kuhusu viashiria vya ajenda  ya Maendeleo Endelevu.  Kulia kwa Balozi Tuvako Manongi ambaye  Tanzania ni Mwenyekiti wa Mwezi wa  nchi za Kundi la Afrika ( African  Group) Ni Mtakwimu Mkuu kutoka Ivory Coast.
   Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi wa Idara ya Siasa ya Umoja wa Mataifa, Bw. Taye-Brook Zerihoun  naye akiwasilisha taarifa yake kwa Wawakilishi wa Kudumu wa Nchi za Afrika, ambapo pamoja na mambo mengine aliwaomba wawakilishi hao kuunga mkono pendekezo la  Idara yake la kupatiwa fedha ambazo wanataka kuzitumia katika eneo la uratibu na usimamia wa majadiliano  kuhudu dhana  nzima ya uzuiaji wa machafuko ( mediation and  prevention ) pamoja na kuongeza ajira.
   Sehemu ya Mabalozi na Maafisa  kutoka   nchi Wanachamawa Umoja wa Afrika  wakifuatilia mkutano.
  Sehemu ya Mabalozi na Maafisa  kutoka   nchi Wanachamawa Umoja wa Afrika  wakifuatilia mkutano.

  0 0


  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  MGOGORO wa kugombea ardhi ya shamba la Lokolova lenye ukubwa wa ekari 2,470 lililopo kata ya Makuyuni wilaya ya Moshi vijijini umeibuka upya huku wananchi jamii ya wafugaji wakimbebesha lawama mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi hatua yake ya kutangaza kurejeshwa ardhi hiyo kwa chama cha Ushirika wa Wakulima ,wafugaji na uzalishaji mali cha Lokolova.  Mgogoro huo wa zaidi ya miaka 30 sasa ,umeibuka baada ya kundi kubwa la wananchi hao kukusanyika katika eneo hilo wakiwa na mifugo yao pamoja na mabango yenye ujumbe mbalimbali huku wakiimba kuonesha kupinga hatua hiyo ya serikali wakidai itachochea kuibuka kwa mgogoro uliokuwepo.  Februari 19 mwaka huu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Makala akiwa ameongozana na viongozi wengine kutangaza maamuzi ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa kurejesha shamba hilo kwa Ushirika wa Lokolova hatua ambayo imefuta mpango wa awali wa serikali ulioasisiwa na mtangulizi wake (Leonidas Gama) wa kulifanya eneo hilo la ardhi litumike kujenga soko la kimataifa na mji wa viwanda.

  Katika mkutano wake wa hadhara na wanachama wa chama cha ushirika cha Lokolova pamoja na wananchi wa eneo hilo Makala aliweka bayana hatua zilizofikiwa na kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kilichokutana Feb.12 Mwaka huu Mjini Moshi kuwa Serikali imeridhia kurudisha shamba lenye ukubwa wa ekari 2,470 kwa wanaushirika.


  Kiongozi wa wananchi Jamii ya wafugaji washio vijiji vya Lotima na Makuyuni Ismail Sevule alisem katika tamko lao kuwa wanapinga hatua ya mkuu wa mkoa (Makala) kurejesha ardhi hiyo ya Shamba la Lokolova kwa chama cha Ushirika ,Ushirika ambao walida ulikwisha futwa tangu mwaka 2014.


  “Tunatoa tamko la kupinga hatua ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kurejesha ardhi ya eneo la Lokolova kwa chama cha ushirika ,wanaushirika ambao si wa kata ya Makuyuni ,watu hawa waliingia kwa mbinu katika ushirika uliokuwepo ,hata hivyo bado ushirika huu ulifutwa tarehe 1 4 ,mwezi wa tatu mwaka 2014 na kutangazwa katika gazeti la serikali la tarehe 23/5 mwaka 2014 “.alisema Sevule.
  Wananchi jamii ya wafugaji wakiwa wamebeba Mabango yenye ujumbe mbalimbali wakipinga hatua ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi Makala kurejesha ardhi ya Shamba la Lokolova kwa chama cha Ushirika wa Wakulima ,wafugaji na uzalishaji mali cha Lokolova.

  hi hao wakiimba kupinga hatua hiyo.Msemaji wa jamii ya wafugaji Ismail Sevule (mweye kofia ya kijani) akiwa na wananchi.
  Wananchi wakipiga Push Up wakati wa mkusanyiko huo.


  0 0

   Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vicent Mashinji, akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, usiku wa kuamkia leo mara baada ya kuchaguliwa, kwenye Mkutano Mkuu uliokuwa ukifanyika Jijini Mwanza. Dkt. Mashinji anaziba nafasi iliyoachwa wazi na Aliekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Willbload Slaa. 
   Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA wakishangilia baada ya kupatikana bila kwa Katibu Mkuu mpya, Dkt. Vicent Mashinji.
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, Makamu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Mh. Said Issa Mohamed pamoja na Mjumbe wa Mkutano Mkuu, Mh. Edward Lowassa wakifarilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu mpya wa Chama hicho, Dkt. Vicent Mashinji (hayupo pichani).

  0 0

  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katikati akijadiliana jambo na Kaimu Mtendaji mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), Eng. Manase Ole Kujan kulia na mkuu wa wilaya ya Kilombero Lephy Gembe kushoto wakati akikagua kivuko hicho mara baada ya ukarabati.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. MAKAME MBARAWA amesema Serikali imejipanga kuhakikisha ujenzi wa daraja la mto Kilombero unakamilika ifikapo mwezi Novemba mwaka huu ili kumaliza changamoto ya usafiri inakabili wanachi wa wilaya za KILOMBERO na ULANGA mkoani MOROGORO.

  Prof. MBARAWA ametoa kauli hiyo Wilayani KILOMBERO mkoani MOROGORO mara baada ya kukagua maendeleo ya kivuko cha MV- KILOMBERO kilochokuwa kikikarabatiwa kufuatia kuzama mwishoni mwa mwezi Januari ambapo amesema tayari Serikali imemlipa mkandarasi zaidi ya shilingi bilioni kumi na moja ili kuhakikisha ujenzi wa daraja katika mto huo linakamilika kwa wakati.

  Amesema tayari mkandarasi anayejenga daraja hilo kutoka China ameshalipwa shilingi bilioni 11.2 katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ambapo hivi sasa kazi inayoendelea kwa mkandarasi huyo ni kutengeza vifaa maalumu kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo huko nchini China .

  “ Ifikapo novemba mwaka huu tutakuwa tumelipatia ufumbuzi wa kudumu swala la daraja la Kilombero na hivyo mpapita kwa uhakika na kufanya biashara zenu kwa uhakika”, amesema Prof.MBARAWA.

  Aidha Prof. Mbarawa amekagua na kuruhusu kuanza tena kwa shughuli za usafirishaji katika kivuko cha Mv Kilombero ambazo zilikuwa zimesimama kwa takribani kipindi cha mwezi mmoja tangu kivuko hicho kupata ajali mnamo Januari mwaka huu kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo.

  Ukabati wa kivuko hicho umegharimu shilingi milioni 342.5 ambapo Prof.MBARAWA amewataka wananchi kufuata maelekezo ya wasimamizi wa kivuko wakati wa safari zao na kulipa nauli stahili.

  “Lazima mlipe nauli kwa sababu nauli hiyo ndio tunayotumia kuendeshea vivuko na pia mzingatie usalama wenu na kusikiliza maelekezo ya wasimamizi wa kivuko ili kuepuka kadhia “amesisitiza Prof.MBARAWA.

  Ujenzi wa daraja katika mto Kilombero ni sehemu ya mkakati wa Serikali tangu awamu ya kwanza uliolenga kujenga madaraja makubwa ni daraja la mto Rufiji mkoani Pwani, daraja Kirumi mkoani Mara, daraja la Malagarasi mkoani Kigoma na Kigamboni la jijini Dar es salam.

  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akishuka kwenye kivuko cha MV KILOMBERO mara baada ya kukikagua.
  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akishuka kutoka katika kivuko cha Mv Kilombero mara baada ya kukagua utendaji kazi wa Nahodha wa kivuko hicho.
  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa wakazi wa wilaya za Kilombero na Ulanga kuhusu umuhimu wa kulipa nauli ya kivuko na kuzingatia usalama wawapo kwenye kivuko mara baada ya kukikagua kivuko hicho.

  0 0


  0 0

  DIWANI wa Kata ya Vigwaza wilayani Chalinze, Mohsin Bharwani ameokoa maisha ya wanafuzi wa Shule ya Msingi Kidogozero waliokuwa wakikabiliwa na tatizo la kushambuliwa na mamba. Tayari wanafunzi kadhaa wamepoteza maisha kutokana na kushambuliwa na mamba katika Mto Ruvu, wakati wakichota maji. 

   Kutokana na hilo, diwani huyo alitekeleza ahadi yake ya kuwanunulia wanafunzi hao mashine za kuvuta maji kutoka katika mto huo hadi shuleni.
  Diwani wa Kata ya Vigwaza wilayani Chalinze, Mohsin Bharwani (kushoto) akimkabidhi na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidogozero, Ali Mwanga, msaada wa vifaa vya mradi wa maji toka Mto Ruvu vyenye thamani ya sh. milioni 5 ili kusaidia wanafuzi wa Shule ya Msingi Kidogozero ,wilayani Chalinze Mkoa wa Pwani jana. Katikati Mwalimu Mkuu wa shule hiyo. Hilda Ngakuka.
  Diwani wa Kata ya Vigwaza wilayani Chalinze, Mohsin Bharwani (katikati) na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidogozero, Ali Mwanga (kushoto) na Mtendaji wa Kata hiyo, Masukuzi Masukuzi, wakisikiliza maoni ya wananchi baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mradi maji toka Mto Ruvu vyenye thamani ya sh. milioni 5 kwa ajili ya kusaidia wanafuzi wa Shule ya Msingi Kidogozero iliyopo wilayani Chalinze Mkoa wa Pwani jana.
  Diwani wa Kata ya Vigwaza wilayani Chalinze, Mohsin Bharwani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwazoka, wilayani Chalinze Mkoa wa Pwani jana alipowatembelea kusikiliza kero zao.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia mashimo ya choo vya shule yanayojengwa kwa nguvu ya wananchi wa shule ya Msingi Nahukahuka.
  Mzee Chitende mbunge wa zamani wa Jimbo la Mtama ambaye sasa ni Mshauri wa Mhe. Nape Nnauye akihutubia umati wa watu waliojitokeza kwenye mkutano wa Mbunge na Wananchi.
  Wananchi wa kijiji cha Nahukahuka wakimsikiliza Mbunge wao Mhe. Nape Nnauye akiwasomea vijiji vitakavyopata umeme wa Mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu.
  Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa kata ya Nahukahuka kwenye mkutano wa kuwashukuru na kuwapa taarifa za mambo ambayo ameshafanya mpaka sasa.
   

  0 0

  Three years has passed since that sad day,When one we loved was called away.

  God took him home. It was His will, 
  But in our hearts he liveth still.

  Your wife Agatha Ibrahim John, your parents Mr & Mrs John Keraryo, brothers, sisters, nephews and nieces, inlaws and friends can’t forget your fond memories of kindness, friendship and amazing sense of humor. 

  You were a wonderful leader on others and inspirational to every one of us. 

  We still remember that sad final moment when you left us with disbelief and tearful eyes. We have leant to remember you with smiles not tears as we believe we will see each other once again; When God call us we hope to be right by your side and reunite.

  “Whosoever believeth in Christ shall never perish, but have eternal life”.(John 3:16)
  There's a face that is haunting as ever
  There's a voice that we're longing to hear.
  There's a smile we'll remember forever,
  Though we try to forget every fear.
  There's a sad but sweet remembrance,
  There's a memory fond and true,
  There's a token of affection dear
  And heartache still for you.

  Continue to Rest In Eternal Peace our dear Brother,
                   AMEN

  0 0

  Waungwana kila uchwao kwenye jiji hili na viunga vyake sambamba na maeneo mengi ya nchi, kuna neno wa ‘kimataifa’ hulisikia likiimbwa.

  Waimbaji wakuu wa neno hilo ni mashabiki wa Yanga wakiongozwa na mpiga zumari wao aliyeacha kazi yake na kujigeuza muimbaji.

  Kinyume chake hilo neno klabu ya Simba huitwa wa ‘mchangani’ au wa ‘matopeni’. Wengi wananilaumu kuwa kwa nini huwa sijibu neno lolote la ajabu kwa Yanga. Jibu langu ni jepesi tu, lazima tujitofautishe msemaji wa klabu na mropokaji wa klabu.

  Mimi hupenda kuzungumzia issues sio porojo au lugha za uchochoroni. Haiwezekani nikawa kiongozi kisha nikaongea lugha za mashabiki ‘maandazi’.

  Kwa hiyo mtaniwia radhi wapenzi wa mpira kwa kutokuwa muimbaji wa ngonjera za uchochoroni. Mara zote nitabaki msemaji wa klabu kubwa nchini na ntaongea facts kwa kadri zilivyo.

  Wadau zisomeni sifa za kimataifa kwa klabu ya Simba nje ya nchi halafu zifananisheni na timu nyingine nchini.

  Walau kama zitafikia nusu tunawaruhusu watafute tusi jipya. Ombi langu kwenu isambazeni taarifa hii katak kila mtandao wa kijamii kisha waseme wao wanaojiita wa kimataifa.

  Simba ndiyo timu ya kwanza nchini kupanda ndege na hii ilikuwa mwaka 1963 tena wakati huo taifa la Tanzania halikuwa limeundwa, ilikwenda Ethiopia kwa mwaliko wa rais wa taifa hilo Haile Selassie
  Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa jezi na hii ilikuwa 1938 ilipocheza na kombaini ya mabaharia wa meli zilizotia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam.

  Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa viatu nchini na hii ilikuwa1949 ilipocheza na kombaini ya jeshi la majini Navy ya Afrika Kusini.
  Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa na basi lake yenyewe na hili lilinuliwa mwaka1968.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

older | 1 | .... | 1156 | 1157 | (Page 1158) | 1159 | 1160 | .... | 3284 | newer