Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110006 articles
Browse latest View live

DK.KIGWANGALLA AFUNGA MOCHWARI YA HOSPITALI YA TUMBI, AIPA MASAA 72

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa siku tatu kwa uongozi wa Hospitali y teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi kufunga chumba cha kuhifadhi maiti (Mochwari) baada ya kubaini matatizo mbalimbali baada ya kufanya ziara katika hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla alibaini mambo mbalimbali kutoenda sawa ikiwemo suala la utendaji mbovu ambapo alitoa agizo la kumtaka Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha wanaosimamia Hospitali hiyo kutoa maelezo ndani ya masaa 24 kama anafaa kubaki ama la!.

Aidha, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, hali aliyoikuta katika chumba cha kuhifadhia maiti ni mbaya hivyo ilikuondoa matatizo amelazimika kuifunga kwa muda huo wa siku tatu ilikufanyia marekebisho kwa baadhi ya mambo ndani ya chumba hicho cha mochwari hospitalini hapo.

Awali vyombo vya habari vilitoa taarifa mbalimbali juu ya Mochwari hiyo ikiwemo badhi ya maiti kuhifadhiwa nje na kuatarisha afya za wananchi.
tumbi99
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa na uongozi wa Hospitali hiyo akiwemo Mganga Mkuu wa Hospitali, Dk. Peter Datani (kulia) akitembelea katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi wakati wa ziara hiyo mapema jana Machi 10.2016.
tumbi hjjh
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua Mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

JUKWAA LA KATIBA TANZANIA WAMTEMBELEA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi Jukwaa la Katiba Tanzania Bw. Deus M. Kibamba akiwatambulisha wajumbe wa Jukwaa hilo kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe walipofanya nae kikao kuhusu mwelekeo mpya wa mchakato wa utungaji wa Katiba Tanzania. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ghorofa ya nane jijini Dar Es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi Jukwaa la Katiba Tanzania Bw. Deus M. Kibamba akimuelezea Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe umuhimu wa kumalizia suala la Katiba Mpya ambayo ni muhimu katika Taifa la Tanzania. Maelezo hayo yametolewa na Mwenyekiti huyo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ghorofa ya nane jijini Dar Es Salaam.

EAC SECRETARY GENERAL ADDRESSES ASSEMBLY

$
0
0
EAC Secretary General, Amb Dr Richard Sezibera yesterday delivered a moving Speech as the Assembly completed week one of its deliberations.

The EAC Secretary General's speech gave a score-card of deliverables during his tenure at the helm before an attentive House.   The Secretary General cited five key areas in the broad vision and remarked that under his five year tour of duty, the bloc had witnessed significant achievements.

On the Customs Union, Amb Dr Sezibera remarked that sustained campaigns to ensure realisation of the Single Customs Territory (SCT) had duly paid off. 

"Today, should one visit the Port of Dar es Salaam right here, you will witness revenue officials from the rest of the Partner States clearing goods", he said.  

The time within which it takes to clear goods has reduced tremendously.  At the central corridor it now takes 3 days, down from the 18 days while in the northern corridor, there is significant reduction from 21 days to 5 days," Amb Dr Sezibera said. 

He remarked that there was sustained pressure to rid the region of Non-Tariff barriers and such, were paying off while the port clearance times were also reduced from three weeks to under ten days.

DC.MAKONDA AWAPA WIKI MBILI WATENDAJI WA KINONDONI KUSHUGHULIKIA UCHAKAVU WA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

$
0
0
Mashimo wa Barabara eneo la soko la Mapinduzi kama panavyoonekana katikaka picha, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda leo jijini Dar es Salaam alipotembelea na kuagiza patengenezwe haraka iwezekanavyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiangalia ubovu wa barabara ya Mwanachamala 'A' hadi Makumbusho jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amefanya ziara ya kukagua barabara ya Mwanayama 'A' hadi Makumbusho ambayo imeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Akizungumza baada ya kukagua barabara hizo amewapa watendaji wa manispaa ya Kinondoni wiki mbili kushughulikia tatizo hilo kutokana na adha ya magari yanayotumia barabara hiyo.

Amesema kuwa kuharibika kwa barabara nyingi katika manispaa hiyo ni kutokana na kujenga chini ya kiwango.

Makonda amesema fedha zinatolewa kwa ajili ya ujenzi lakini baadhi ya watendaji wanajenga chini ya kiwango na kuwapa adhabu wananchi wanatumia barabara hiyo ikiwemo na gari za kubeba.

Aidha amesema kuwa watahakikisha barabara zinafanyiwa maboresho katika urahishaji wa usafiri katika Manispaa ya Kinondoni.

DUKA LA KAMERA LA KAMPUNI YA JUMBO LAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
 Meneja mauzo kampuni ya Jumbo Camera House Ltd, Mathias Luoga akizungumza na wadau mbalimbali wa Kamera pamoja na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa duka la kampuni ya Jumbo Camera House Ltd linalouza kamera za picha za mnato, picha za mjongeo, mabegi na vitu mbalimbali vya kamera, duka lililopo jengo la Benjamini Mkapa Tower Posta jijini Dar es Salaam.
 Muonekano wa duka la kampuni ya Jumbo Camera House Ltd linalouza
linalouza kamera za picha za mnato, picha za mjongeo, mabegi na vitu mbalimbali vya kamera.
Mgeni Rasmi, Lita Paulsen (wakwanza kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Jumbo Camera House Ltd wakigonganisha glasi za shampeni katika uzinduzi wa duka la kamera lililopo katika jengo la Benjamini Mkapa Tower Posta jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii. 

TATOA KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA 12 MANISPAA YA TEMEKE.

$
0
0
Mwenyekiti wa wa chama cha wamiliki wa malori Tanzania (TATOA), Angelina Ngalula akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na ujenzi wa madarasa 12 katika manispaa ya Temeke.
Sehemu ya Bodi ya TATOA  na watendaji wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akizungumza na bodi ya TATOA jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
CHAMA cha Wamiliki wa Malori nchini (TATOA) kinatarajia kujenga madarasa 12 katika shule msingi maji matitu ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Rais Dk.John Pombe Magufuli ya kuhakikisha shule zinaboreshwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki amesema kuwa wanatambua mchango wao na kuwa watakuwa wamesaidia jitihada za serikali katika kupunguza changamoto za madarasa.

Amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unakabiliwa na changamoto ya madarasa na madawati hivyo kunahitaji wadau kujitokeza kusaidia maeneo hayo.

Mwenyekiti wa TATOA, Angelina Ngalula amesema kuwa wameunga mkono jitihada za serikali kwa upande wa elimu hivyo wanawajibu wa kufanya hivyo katika kutatua changamoto ya vyumba vya madarasa.

Amesema kwa kuanzia wanaanza na madarasa 12 lakini wataendelea kuwasiliana na wanachama zaidi katika kuongeza au kujenga shule nzima ili watoto wasome shule na kuja kuweza kutumikia sekta ya usafirishaji.

Angelina amesema kuwa bodi yao iko imara katika kwenda na suala la shule za msingi ili watoto wapate elimu bora kutokana na mkakati wa Rais kutoa kipaumbele ya elimu ya nchini.

POLISI WAFYATUA MABOMU YA MACHOZI MBELE YA BENKI YA CRDB, TAWI LA MBAGALA-RANGI TATU KUFUATIA UBISHI WA WATEJA KUTUMIA SIMU NDANI YA BENKI

$
0
0


NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
POLISI wamelazimika kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliojikusanya mbele ya Benki ya CRDB tawi la Mbagala-Rangi Tatu, baada ya mtu mmoja aliyekuwa akiongea na simu ndani ya benki hiyo kukaidi maagizo ya polisi ya kuacha kufanya hivyo mapema leo mchana Machi 11, 2016.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, watu watatu mmoja akiongea na simu na wengine wawili waki-chat, ndani ya benki hiyo, waliagizwa na mlizni wa benki kuacha kufanya hivyo lakini wakakaidi.
Baada ya mlizni kuona hivyo alitoa taarifa kituocha polisi Mbagala-Maturubai, nahapo polisi wakiwa ndani ya gari lao maarufu kama Defender, waliwasili kwenye eneo hilo na kuamuru watu hao ambao wanaelezwa kuwa wateja, kutoka ndani ya benki hiyo.
Hata hivyo palitokea mabishanobaadaya mmoja wao kukaidi amri ya polisi na kuanza kupigana nao.
Kuona hivyo wtu walianza kujaa na polisi bila kufanyaajizi wakafyatua mabomuya machozi kutawanya watu na kuwadhibiti “wateja’hao wabishi na hatimaye kufanikiwa kuondoka nao.
Hali hiyo ilizua tafrani hadi watu wakadhani kuwa palikuwepo na tukio la ujambazi kwani ni mwezi uliopita umbali wa mita chache kutoka kwenye benki hiyo, palitokea tukio baya ya uvamizi wa benkiya Access ambapo watus aba waliauawa wakiwemo polisi.

'ZUNGU LA UNGA' LADAKWA SAUZI NA MADAWA YA KULEVYA NDANI YA TENKI YA MAFUTA YA GARI

$
0
0
Dereva na mtuhumiwa raia wa Msumbi akiwa chini ya ulinzi
 Sehemu ya 'mzigo' huo
 Askari polisi akichana tenki la mafuta la gari hilo

Madawa ya kulevya aina ya heroin yanayokadiriwa kuwa na thamani ya Rand za Afrika Kusinu milioni 50 yamekamatwa yakisafirishwa ndani ya tenki la mafuta la gari lililokuwa likielekea Gauteng kutokea Msumbiji.




Habari zinasema hilo limetokea baada ya kikosi cha askari polisi wa mbwa cha Whiteriver walifanikiwa kukamata madawa hayo baada ya kusimamisha gari aina ya Toyota Prado lenye kutia mashaka katika geti la kulipia ushuru wa barabara eneo la Nkomazi huko Mpumalanga siku ya Jumapili iliyopita.


Baada ya upekuzi mbwa wa polisi alipata harufu katika moja ya matenki ya gari hilo na kubweka kuwa mna 'mzigo', ndipo baada ya kufungua tenki hilo na kulichana wakakuta 'unga' huo umefichwa ndani ya tenki hilo ukiwa umefungashwa kwenye vifuko vya plastiki, alisema msemaji wa Polisi Sajini Gerald Sedive.
"Madawa ya kulevya yenye thamani ya R50 milioni yalikutwa kwenye tenki la mafuta. Gari lilikuwa likitokea Msumbiji", alisema, na kuongezea kwamba dereva wa gari hilo raia wa Msumbiji ametiwa mbaroni na hatua za kisheria zitachukua mkondo wake.

VIROBA FEKI TANI 3 VYATEKETEZWA WILAYANI ROMBO MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
 Sehemu ya viroba feki tani 3 ambavyo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Amos Makalla, Mkuu wa wilaya Rombo Mhe  Lembris Kipuyo na mbunge wa Rombo Mhe. Joseph Selasini wameshiriki kuteketeza pamoja na bidhaa mbali mbali zilizoisha muda wake ambazo zimekuwa zikiingizwa kupitia njia za panya. Mhe Makalla  ameagiza msako mkali ufanyike ili kuokoa maisha ya wananchi Zoezi la uteketezaji limefanyika kijiji cha Ubetu wilaya ya Rombo
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Amos Makalla na mbunge wa Rombo Mhe. Joseph Selasini wakiwasili kijiji cha Ubetu kushiriki kuteketeza viroba feki tani 3 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Amos Makalla, Mkuu wa wilaya Rombo Mhe  Lembris Kipuyo na mbunge wa Rombo Mhe. Joseph Selasini wakishiriki kuteketeza viroba feki na bidhaa mbalimbali zilizosha muda wake katika kijiji cha Ubetu

JUMA KASEJA AREJEA KIKOSINI MBEYA CITY BAADA YA MAPUMZIKO YA UZAZI

$
0
0
Golikipa mahili wa Mbeya City Fc ya Mbeya, Juma Kaseja  Juma  (pichani) amerejea kikosini kutoa mapumziko ya majuma mawili aliyopewa na kocha  Kinnah Phiri kufuatia  mkewe Bi Nasra Nassor kujifungua watoto mapacha hivi karibuni.
Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa  mbeyacityfc.com  Kaseja amesema kuwa amefurahi kusafiri na hatimaye kurudi salama kwenye timu yake huku pia akitoa shukurani zake za dhati wa wale wote ambao wamekuwa karibu nae yeye kama mchezaji na pia familia yake tangu alipojiunga na City.
“Nashukuru mungu nimefika hapa salama baada ya safari yangu, pia namshukuru kwa kile alichonijaalia, nimerudi kikosini nikiwa na ari kubwa zaidi  ili kuituikia timu yangu kwa nguvu zote  katika kutafuta mafanikio hasa kwenye kipindi hiki  ambacho ligi inaelekea mwishoni, hakika tunapita kwenye kipindi kigumu lakini  umoja wetu utatufanya kuvuka hapa” alisema.
Akiendelea zaidi Kaseja  aliyewahi kucheza kwa mafanikio kwenye timu za Moro United, Simba, na Yanga aliweka wazi kuwa anaimani kuwa na kocha Kinnah Phiri kuwa ataijenga upya City na kuifanya kuwa timu itakayotisha zaidi kwenye msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

WAKALA WA MAJENGO TANZANIA YAIPA MKATABA YONO AUCTION MART WA KUKUSANYA MADENI NCHINI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale
WAKALA  wa Majengo Tanzania (TBA), umecharuka kwa kuingia mkataba na Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart & Co. Ltd ili kusaidia kukusanya madeni ya wadaiwa sugu ambao walikopa nyumba.
Wakati huo huo mwakilishi wa kampuni hiyo ya udalali ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scollastica Kevela ametoa siku tatu kwa wadaiwa wote wa TBA kuhakikisha wanalipa fedha hizo kabla ya kufikiwa na kampuni hiyo ambayo Jumatano ya Machi 16 mwaka huu itaanza rasmi kazi ya kuwaondoa katika nyumba za wakala huo watumishi wote wanaodaiwa kwa kufuata sheria kama inavyoelekeza.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa kutiliana saini na kampuni hiyo ya udalali kwa ajili ya kukusanya fedha kutoka kwa wadeni wa wakala huo  Mtendaji Mkuu wa TBA ,  Elius Mwakalinga alisema wamefia hatua hiyo baada ya kuona wadaiwa wao ambao wengi wao ni kutoka sekta za serikali kushindwa kulipa fedha hizo.

"Tumeingia mkataba na Kampuni ya Yono Auction Mart baada ya kushinda zabuni ambayo tulitangaza Februari 23,2016 na sasa kazi yote ya ukusanyaji wa fedha hizo itafanywa na kampuni hiyo" alisema Mwakalinga.
Mwakalinga alisema fedha nyingi za wakala huo zipo mikononi mwa wadaiwa wao ambapo kwa mkoa wa Dar es Salaam na Dodoma ni shilingi.Bilioni 6 na kwa waliokopa ni sh.milioni 800 huku fedha zinazodaiwa kwa ajili ya kutoa ushauri mbalimbali wa ujenzi ni sh.bilioni 6.95.
Mwakilishi wa kampuni  ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scollastica Kevela alisema wametoa siku tatu kwa wadaiwa wote kuhakikisha wanalipa fedha hizo vinginevyo watafikiwa na kampuni hiyo ambayo imepanga rasmi kupita kila nyumba inayodaiwa na kuwa kila muhusika atatakiwa kuilipa kampuni hiyo asilimia tano ya fedha anazodaiwa na TBA.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ,  Arch. Elius Mwakalinga (kushoto), akikabidhiana hati ya mkataba na Mwakilishi wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scollastica Kevela Dar es Salaam leo asubuhi, baada ya kampuni hiyo kushinda zabuni ya kukusanya madeni ya TBA kuanzia leo.
 Taswira meza kuu katika mkutano huo.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) , Arch Elius Mwakalinga (katikati), akizungumza katika mkutano huo kabla ya kutiliana saini na kampuni ya Yono. Kushoto Ofisa wa Idara ya Manunuzi, Mariam Kazoba.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Waziri Mkuu awapongeza Lulu na Richie kwa tuzo walizopata

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea tuzo za wasanii wa filamu nchini walizoshinda nchini Nigeria. Wasanii hao ni Elizabeth Michael na Single Mtambalike. Shughuli hiyo ilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 11, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Wasanii wa filamu Elizabeth Michael na Single Mtambalike baada ya kupokea tuzo za wasanii hao walizoshinda nchini Nigeria. Tukio hilo lilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 11, 2016. (
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Tuzo kutoka kwa Msanii wa filamu Elizabeth Michael ambayo msanii huyo alishinda nchini Nigearia. Tukio hilo lilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 11, 2016.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akipokea tuzo kutoka kwa msanii wa filamu, Single Mtambalike ambayo msanii huyo alishinda nchini Nigeria. Tukio hilo lilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

Waziri wa maji aendelea na utumbuaji majipu baada ya leo kuiagiza bodi ya DAWASCO kusimamisha watumishi 9 kwa tuhuma za ufisadi.https://youtu.be/h3UhTNR7KI8
 Serikali ya Vietnam yakubali kuisaidia Tanzania katika kutafuta mbegu bora za mazao, kuongeza thamani ya mazao pamoja na namna ya kutafuta masoko moja kwa moja kwenye soko la dunia. https://youtu.be/hj6jUJpJGGg
 Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema Edward Lowassa amtembelea na kumjulia hali Maalim Seif huku pia akizungumzia uteuzi wa Chadema.https://youtu.be/ihkX8df4Kxc
 Majeruhi watatu waliofukiwa na kifusi katika machimbo ya Nyarugusu mkoani Geita wahamishiwa hospitali ya rufaa ya Bugando baada ya hali zao kuwa mbaya. https://youtu.be/qtzPSdZdVT0
 Jeshi la polisi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere wakamata watuhumiwa 2 waliokuwa wakisafirisha madawa ya kulevya kuelekea nchini Canada. https://youtu.be/jFNx_0_7Elk
 Wafanyakazi wa kiwanda cha uzalishaji wa mbolea cha Minjingu wagoma kufanya kazi kutokana na madai mbalimbali kwa uongozi wa kiwanda hicho.https://youtu.be/1MpubZhiIGM
 Rais wa baraza la habari Tanzania jaji mstaafu Thomas Mihayo awaapisha majaji wateule 9 ambao ni miongoni mwa majaji 10 walioteuliwa kuunda jopo litakalo simamia mchakato na hatimaye kupata washindi wa tuzo za umahiri wa uandishi wa habari kwa mwaka 2015. https://youtu.be/Kw7dgmxMyrY 
Waziri wa maji atumbua majipu, kwa kuagiza kusimamishwa kazi kwa watumishi waandamizi 9 wa DAWASCO kufuatia utendaji usioridhisha.https://youtu.be/TXr1PRq4iZ8
 Wakala wa majengo nchini TBA aingia makataba na kampuni ya udalali ya YONO AUCTION MART kukusanya madeni yanayodaiwa na wakala huo kutoka kwa wapangaji na wanunuzi wa nyumba za serikali.https://youtu.be/TjCWqg3i4aQ
 Ziara ya siku 4 ya Rais wa Vietnam nchini yamalizika hii leo na kuondoka nchini kuelekea nchini Msumbiji kwa Ziara nyingine ya kikazi. https://youtu.be/Efn9Q-PEV7k
 Tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC, yathibisha kupokea karatasi za kupigia kura kutoka nchini Afrika kusini. https://youtu.be/TrSraEcms9E

DIRA YA DUNIA IJUMAA 11.03.2016

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA MWAKA CHAMA CHA WATANZANIA SWEDEN

$
0
0
SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 26/3/2016

SAA 12 JIONI.

SEHEMU: Bergshamraskolan , Hjortstigen 1 Solna

BAADA YA MKUTANO BURUDANI MPAKA ASUBUHI…..!!

VINYWAJI/CHAKULA BEI POA KUTOKA FC-KILIMANJARO!

MGENI RASMI: BALOZI H. E DORA MMARI MSECHU

WOTE MNAKARIBISHWA!


                                  TAFADHALI TUZINGATIE WAKATI!

MATUKIO MBALI MBALI YA ZIARA YA RAIS WA VIETNAM NCHINI TANZANIA

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: Banana Zoro - Zoba

Tanzania katika mkutano wa SADC wa Mawaziri mjini Gaborone, Botswana

$
0
0
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa SADC, wa Mawaziri,Gaborone Botswana. Kutoka Kushoto Dr. Aziz Ponary Mlima, Katibu Mkuu Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dr. Stegomena L. Tax, Katibu Mtendaji wa SADC, Mheshimiwa Dr. Ashantu Kijaji, Naibu Waziri wa Fedha  a Mipango, Bwana Said Magonya, Kamishna wa Madeni ya Nje, (Hazina).

CCM YATAKA WAKURUGENZI MANISPAA YA ILALA, KINONDONI WAWAJIBISHWE KUCHELEWESHA UCHAGUZI WA MEYA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam kimemuomba Waziri Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene kuwawajibisha Wakurugenzi wa Manispaa ya Ilala na Kinondoni kwa kile walichodai ni kuvuruga uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.


Hayo yalizungumzwa Dar es Salaam jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar e Salaam, Juma Simba 'Gadafi' wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kumekuwa na sintofahamu hadi sasa kuhusiana na uchaguzi huo kutokana na woga wa wakurugenzi hao ambao wameshindwa kujiamini.


" Wakurugenzi hawa ndiyo chanzo cha vurugu katika uchaguzi huu wa meya tumewaomba wakurugenzi hawa watoe tamko na tafsri sahihi ya ushiriki kwa wajumbe wenye sifa ili kuacha kuupotosha umma juu ya uchaguzi huu,"alisema Gadafi.


Gadafi alisema kuwa wakurugenzi hao kwa makusudi na huku wakifahamu wanakiuka sheria waliruhusu baadhi ya maswahiba wao kutoka chama cha upinzani ( Ukawa) ambao walitoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam kuingia kwenye uchaguzi uliovurugika.


Gadafi alisema mwanachama yeyote wa CCM anaruhusiwa kufanya uchaguzi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kupingwa kama taratibu unavyoelekeza.


Alisema hizi kauli zinazotolewa kuwa haiwezekani wajumbe wakatoka nje ya Dar es Salaam na kupiga kula eneo lingine hazina ukweli wowote kwani siku za nyuma ziliwahi kufanyika kwa vyama vingine lakini hakukuwa na kulalamika.


Aidha katika hatua nyingine Simba amesema Meya wa Ukawa walioshinda katika Manispaa za Kinondoni na Ilala wanatakiwa watambue kuwa Halmshauri hizo hazitaendeshwa kwa ilani ya chama chao bali ni ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa asilimia 60 ya bajeti ya maendeleo inaongozwa na chama. 

HOW TO FIND THE RIGHT OIL PRODUCTS SUPPLIER IN TANZANIA

$
0
0
Lubricant Oil,   diesel, petrol,  Grease and kerosene  business are growing at a quick rate in the country.
The problem is this, the market is soaked, with many suppliers  pretends to be  the best in the field.
You can be overwhelmed, frustrated,  and you could be wondering  how  to pick the good  fit  for your  business.
It is shocking that, many people invest in the company that  advertises themselves  as the best in the industry.
Sadly,  they wind up  reaping  less profit. And instead of  prosperity, the business  turns into disappointment and difficulties
To find oil supplier you trust  is an effort. It takes time, energy, perhaps money.
In fact,  before you put your hard-earned money in a particular company, investigate much about them to see If they can influence  your business the right way.
Unless you  arrive  the trusted, and respect company you’ll never reduce risk   and sustain   your company reputation.
The more time you spend in research, the more risk you reduce.
However, in this article, I would not specify the best  oil distributor  in Tanzania. But  I’ll share fundamental viewpoint to offer you  some assistance with landing the right  one.
Do you want to reap the bountifully in this business? Below are the factors to consider in your research.
Quality
Remember that, most  people offer the same lubricant oil, diesel,  and grease as you do.
So how do you  get ahead of them?
By working  with a distributor that deliver quality items.
And serving your customer with top high-quality products. Customers need petroleum products that improve their production as the a whole.
You must  work with the supplier that has a proven record in  offering superb products.
Never be enticed by cheap prices.  No matter how much you price, your products,  the customer will  buy, provided  you deliver quality items  that meet their   needs.
Average is the failure  in business.
If you still offer  your customers with low-quality items, I have three words for you: quit or improve.
Reputation of the company
How other clients talk about the organization you want to work with.
How the supplier is viewed  in the business.
How people think about their items and services.
Research  all insight about the firm before commitment.

Safety records
Safety is the critical issue in choosing the right supplier. Work with a company that put safety first. Imagine what might happen if the safety issues are  overlooked in a truck stacked with diesel, petrol, Lubricants, Grease even motors oil.

Conclusion
In any case, the right supplier  must be open, and transparent  about who they are. Working with best petroleum products companies makes you reap  good  profit from the business.
So start, researching, and use the information  you gather to your advantage. You’ll thanks me in the future  when you start enjoying  the reward of working with the sound supplier.
 Hussein Boffu
Hussein.Boffu@tanzaniapetroleum.com
0655 37 65 43
Viewing all 110006 articles
Browse latest View live


Latest Images