Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1154 | 1155 | (Page 1156) | 1157 | 1158 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Mkuu wa Magereza Mkoani Kagera, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Omar Mtiga(wa pili kushoto) akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa tatu kulia) nyumba mbili za Askari wa Jeshi la Magereza ambazo tayari zimekamilika katika eneo linakojengwa Gereza la Wilaya ya Biharamulo(wa pili kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Shaaban Ntarambe.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(suti nyeusi) akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Chato wakiaangalia moja ya Bweni la kulala Wafungwa/Mahabusu ambalo tayari limekamilika katika eneo linakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato Mkoani Geita. Kukamilika kwa Gereza hilo kutasaidia kutatua tatizo la Msongamano wa Wafungwa na Mahabusu katika Magereza ya Biharamulo na Gereza Muleba.
  Mkuu wa Gereza la Biharamulo, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Gidion Kakulu akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza maeneo mbalimbali ya Gereza hilo katika ziara yake ya Kikazi leo Machi 10, 2016. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo ambao wameambatana na Kamishna Jenerali wa Magereza katika ziara yake ya kikazi.
  Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP John Casmir Minja akisalimiana na Mkuu wa Gereza Kuu Butimba, Mwanza Kamishna Msaidizi wa Magereza, Jaili Mwamugunda alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera ambapo leo Machi 10, 2016 ametembelea eneo kunakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato lililopo Mkoani Geita pamoja na Gereza la Wilaya ya Biharamulo(wengine) ni Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Ofisi ya Magereza Mkoani Mwanza.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akifurahia jambo pamoja na Luteni Jenerali Mstaafu Samuel Ndomba walipokutana katika Kivuko cha Busisi kabla ya kuendelea na safari kuekelea Mkoani Kagera(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Mwanza, Goleha Masunzu.

  0 0

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang leo mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakiwa katika mazungumzo yaliyohusishwa na baadhi ya ujumbe toka nchi ya Vietnam na Tanzania leo mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza mara baada ya kuzindua mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara ulioendana na mkutano mkuu wa Taasisi hiyo na uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye akizungumza katika uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara ulioendana na mkutano mkuu wa kumi na sita (16) wa Taasisi hiyo na uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na mwenyekiti mtendaji wa IPP LTD Dkt. Reginald Mengi akizungumza katika uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara ulioendana na mkutano mkuu wa kumi na sita (16) wa Taasisi hiyo na uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), wakifuatilia uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara ulioendana na mkutano mkuu wa Taasisi hiyo na uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  0 0


  0 0

  Na Avila Kakingo , Globu ya Jamii.
   KITABU cha HOW TANZANIA CAN MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  (Jinsi gani Tanzania kuweza kujikwamua na umasiki) kimezinduliwa jijini Dar es Salaam leo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi (akimwakilisha waziri mkuu Kassimu Majaliwa), Kitabu hicho kimetungwa na wahadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa hisani ya Ofisi ya waziri mkuu.

  akizungumza katika uzinduzi wa kitabu hicho Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi amesema kuwa
  kitabu hicho kicholenga kwenye mada  ya  "Tanzania Move from Poverty to Prosperity", hasa kwa kipindi hiki, ikizingatiwa kwamba Serikali ya awamu ya tano ipo katika vita ya kupambana na adui umaskini ili tuweze kufikia malengo ya millennia ya mwaka 2025. 

   "Chapisho hili la kitabu (How Can Tanzania Move from Poverty to Prosperity) limetolewa wakati sahihi kwa taifa letu Tanzaniani chapisho la aina yake toka Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam linaloonesha kiu ya wataalamu, wanataaluma na wale wanaotekeleza Sera  kutaka taifa letu lijikomboa kutoka kwenye dimbwi la umaskini na kufikia ustawi katika Nyanja za kiuchumi, kijamii, na kisiasa." Amesema Dkt. Possi.

  Kwa upande wa Mhadhir wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally amesema kuwa dhima ya kitabu cha (How Can Tanzania Move from Poverty to Prosperity) inalenga uchumi wa watu kwa watu wenyewe.

  Pia amesema kuwa kitabu hicho kimegusia suala la maliasili na umhimu wake kwenye mageuzi wa uchumi wa viwanda Tanzania, uvuvi, madini, misitu kilimo na nguvu kazi ya gharama nafuu pia kimetaja umhimu wa Diplomasia ya kiuchumi, mifumo ya kitaifa ya Sayansi na tecknologia, ubunifu usalama wa raia na mali zao. 
   
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi akizungumza katika uzinduzi wa kitabu cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  (Jinsi gani Tanzania kuweza kujikwamua na umasiki) kilichotungwa na wahadhili kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kitabu hicho kimezinduliwa katika ofisi za waziri mkuu jijini Dar es Salaam leo.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu  cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  katika ofisi ya waziri mkuu jijini  Dar es Salaam leo akiwa na wahadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam..
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi akiwa na baadhi ya wahadhiri, watunzi wa kitabu na waalikwa wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya uzinduzi wa kitabu  cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  katika ofisi ya waziri mkuu jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii. 
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Naibu Gavana wa BOT Dkt. Natu Mwamba akiwasili makao makuu ya Benki Kuu ya Tanzania alikofanya ziara ya kushtukiza leo Machi 10, 2016 .


  0 0

  Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tang San akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Simu za mikononi kutoka nchini Vietnam ya Halotel inayofanya kazi hapa nchini Tanzania. Kampuni hiyo inatoa huduma ya simu Vijijini kwa gharama nafuu.  Rais Truong Tang San anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku nne hapo kesho na kuelekea nchini Msumbiji kwa ajili ya ziara nchini humo.
  Viongozi mbalimbali walioambatana na Rais Truong Tang San, wakiwa pamoja na Balozi wa Vietnam, Mhe. Vothanh Nam (katikati) wakisikiliza kwa makini mazungumzo aliyokuwa yakiendelea kati ya Rais Tang San (hayupo pichani) na viongozi wa Kampuni ya simu ya Halotel
  Rais Truong Tang San akizindua Sanamu ya kiongozi wa zamani wa Vietnam iliyopo kwenye Kampuni ya Simu ya Halotel.
  Viongozi wa Halotel na Viongozi walioambatana na Rais Tang San (hayupo pichani) wakishangilia wakati uzinduzi ukiendelea   
  Rais Truong Tang San akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya simu ya Halotel.
                                                     Picha na Reginald Philip 

  0 0

  Rais Dkt Magufuli akizungumza na Uongozi wa juuu wa Benki Kuu

  0 0
 • 03/10/16--20:00: NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: SEYA

 • 0 0

  Leo tarehe 11 Machi 2016 umefikisha mwaka mmoja tangu umetangulia kwa Baba yetu aliye mbinguni.
  Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa baraka na upendeleo wa kuwa sehemu ya maisha yako hapa duniani.
  Tunaendelea kukumbuka kwa upendo wako, ukarimu, ucheshi na ufundishaji wako.
  Daima mioyoni mwetu unakumbukwa na mkeo, watoto wako, wakwe zako, wajukuu wako,  wanafunzi wako, ndugu, jamaa na marafiki. 
  Pumzika kwa Amani Mzee Makilagi. Raha ya Milele Uwape Eh Bwana, na mwanga wa milele uwaangazie. 
  Amina


  0 0

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar waliopo Mtaa wa Magogoni Mjini Dar es salaam ambapo Ofisi
  hiyo kwa sasa iko chini ya uratibu wa Ofisi yake.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimjuilia hali Mbunge Mstaafu wa lililokuwa Jimbo la Rahaleo Wilaya ya Mjini Kanal Mstaa Saleh Ali Fara aliyelazwa Hospitali ya Jeshi
  Lugalo Jijini Dar es saam akipatiwa huduma za matibabu akizumbuliwa na maradhi ya Mgongo.
  Balozi Seif akibadilishana mawazo na Madaktari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ } Lugalo Hospitali Mjini Dar es salaa baada ya kumjulia hali Mbunge mstaafu wa Mlandege Kanal Mstaafu Saleh Ali Fara.
  Picha na- OMPR – ZNZ.

                                          Press   Release:-

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na mipango ya kuijengea utaratibu madhubuti Ofisi yake iliyopo Mjini Dar es salaam ili iweze kuratibu shughuli zake kwa ufanisi mkubwa zaidi. Balozi Sei alisema hayo wakati akizungumza na watendaji wa Ofisi ya SMZ iliyopo Mtaa wa Magogoni Jijini Dar es salaam baada ya kupokea changamoto zinazowakabili sambamba na kuangalia muelekeo mzuri utakachangia majukumu ya Ofisi hiyo kutekelezwa katika njia ya kitaalamu.

  Alisema Mipango hiyo itawawezesha watendaji wa Ofisi hiyo kuwapa fursa ya kubuni njia sahihi zitakazoiwezesha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutanua mafungamano yake zaidi na Taasizi za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na zile za Kimataifa. Balozi Seif alieleza kwamba malengo ya kuanzishwa kwa Ofisi ya SMZ Dar es salaam ilikuwa ni kuratibu masuala ya uchumi na fedha kati yake na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika dhana nzima ya
  kudumisha Muungano wa Tanzania.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwashauri watendaji hao kuzingatia  mfumo wa utaratibu watakaopewa  na Serikali baada ya kukamilika kwake na kutumia utaalamu sambamba na bidii zao ili lile lengo lililokusudiwa la kuundwa kwa Ofisi hiyo likamilike vizuri. “ Tunachokitarajia kutoka kwenu ni kuona taaluma zenu zinaleta mafanikio katika Nyanja zote za maendeleo iwe, Kilimo, uchumi,Utamduni  na hata ustawi wa wananchi ”. Alisema Balozi Seif.

  Akigusia hali ya Kisiwani Visiwani Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba watendaji hao wa SMZ Dar es salaam kuendelea majukumu yao ya ujenzi wa Taifa bila ya hofu yoyote. Alisema hali ya utulivu, amani na mshikano ndani ya Visiwa vya Unguja na Pemba hivi sasa  inaendelea kama kawaida na kuwaomba waondoe shaka kutokana na baadhi ya taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya Habari na mitandao ya Kijamii vikidai kwamba hali ya kisiasa Zanzibar wakati huu imekuwa tete.

  “ Unashangaa kusikia au kuona kwenye baadhi ya  vyombo vya habari vikiandika na kutangaza kwamba hali ya Zanzibar ni tete wakati wananchi wanaendelea na hrakati zao za kimaisha bila ya bughdha. Sasa hii hali tete inatoka wapi? ”. Aliuliza Balozi Seif. Alisema harakati za kimaisha hasa wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida zinakwenda na ushahidi wa hao ni mmiminiko wa watalii na wageni wanaoingia Zanzibar kila kukicha. 

  Balozi Seif  aliwahakikishia wananchi kwamba hali ya amani itaendelea kuimarishwa na Taasisi za ulinzi kabla na wakati wa marejeo ya uchaguzi Mkuu wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Tarehe 20 mwezi huu.


  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  10/3/2016.

  0 0


  Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk Richard Masika(kushoto)akimwongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen kuwasilimia wafanyakazi wa taasisi hiyo katika ziara yake ,Norway ni moja ya nchi zinazosaidia sekta ya elimu ya ufundi nchini.

  Ujumbe uliongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen kutoka Norway na maafisa kutoka ubalozi wao nchini wakisalimiana na wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi Arusha.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen (kulia)akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhil Nkurlu(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Richard Masika. 
   

  0 0

  MKUU wa Wilaya ya Geita Manzie Mangochie anasema Tamasha la Pasaka ni jambo kubwa sana kwao kwa sababu linafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.

  Mangochie anasema ukubwa na umuhimu wa tamasha hilo ni kutajwa kwa neno la Mungu na waimbaji sambamba na viongozi mbalimbali wa dini wanaofika katika tamasha hilo.Mangochie anasema Mkoa wa Geita una matatizo mengi ambayo yalikuwa yanahitaji kukemewa, lakini mwaka huu Mungu amesikia matakwa ya wakazi wengi wa mikoa hiyo ambayo ilitawaliwa na matukio ya mauaji yakiwemo ya vikongwe na walemavu wa ngozi ‘Albino’.

  “Mikoa hii ya Kanda ya ziwa iligubikwa na shetani ambaye ni mauaji ya Maalbino na Wakongwe ambao walikuwa wakitendewa unyama ambao Mungu alikuwa akichukizwa nao, hivyo kupitia Tamasha la Pasaka neno la Mungu litasaidia kuondosha madhila hayo,” alisema Mangochie.

  Mangochie anasema kupitia Tamasha la Pasaka waandaaji watasaidia wakazi wa mikoa hiyo kuachana na kusahau matukio ya kumchukiza Mungu.Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema maandalizi ya kuelekea tamasha hilo yanaendelea vilivyo kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.

  Msama alisema tamasha hilo linatarajia kuanza Machi 26 kwenye ukumbi wa Desire ulioko mkoani Geita, Machi 27 litafanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na Machi 28 litafanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.

  Msama alisema viingilio kwa wakubwa ni shilingi 5000 na watoto shilingi 2000 ambako alitoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati alipokwenda kumjulia hali katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo Machi 11, 2015.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akifanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati alipokwenda kumjulia hali katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo Machi 11, 2015.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya hali ya afya yake.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, mara bade ya kumjulia hali katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo Machi 11, 2015.

  0 0
 • 03/11/16--03:33: TAARIFA YA MSIBA
 • Bi Tertula Mbuya wa Kilema moshi anasikitika kutangaza kifo cha mumewe mpenzi bw Urban Peter Mbuya kilichotokea alfajiri ya tar 11 march 2016 katika hospitali ya taifa ya muhimbili. 

  Mipango ya mazishi inafanyika mbezi beach nyumbani kwa binti yake na mwili wa marehemu unatarajia kusafirishwa kwenda kijijin kwake kilema moshi kwaajili ya mazishi tar 15 march 2016. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

  0 0


  Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu (kulia kwa waziri) akimsikiliza Balozi wa Ujerumani nchini ,Egon Kochanke (Katikati) wakati alipomtembelea ofisini kwake leo.
  Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akimsikiliza Balozi wa Ireland nchini Fionnuala Gilsen Nan(kulia kwa waziri wakati alipomtembelea ofisini kwake leo.Wengine ni baadhi ya maofisa wa ubalozi huo.

  0 0

  Kamishina Jenerali wa Mageraza nchini John Carmir Minja afanya ziara ya kikazi Mkoani Kagera yenye lengo la kutembelea na kukagua Magereza ya Mkoa wa Kagera pamoja na kujionea miradi ya uzalishaji inayosimamiwa na Jeshi hilo.

  Akiwa Mkoani hapa Kamishna Jenerali Minja alifika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella na kufanya naye mazungumzo kuhusu utendaji kazi na ufanisi wa Jeshi la Magereza Mkoani hapa katika kuimarisha ulinzi na usalama.

  Aidha katika mazungumzo hayo walizungumzia changamoto ya msongamano wa Mahabusu katika Gereza la Wilaya ya Muleba ambalo hivi sasa linatumika kuhifadhi Mahabusu wa Wilaya ya Muleba na Wilaya ya Chato Mkoani Geita ambayo haina Gereza la Wilaya.

  Kamishna Jenerali wa Mageraza nchini John Carmir Minja pia alitembelea Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba na kufanya mazungumzo na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo Mhe. Sivangilwa Mwangesi juu ya namna ya kuongeza kasi ya usikilizwaji wa kesi mbalimbali za watuhumiwa ili kuondoa msongamano Magerezani.

  Vilevile Kamishna Jenerali Minja alitembelea Gereza la Wilaya la Bukoba na kuongea na wafungwa na Mahabusu wa Gereza hilo pia na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la zahanati ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilishwa ili liweze kutoa huduma za afya kwa wafungwa na watumishi wa Jeshi hilo pamoja na wananchi wanaoishi jirani na zahanati hiyo.

  Kamishna Jenerali Minja yupo Mkoani Kagera kwa siku 7 kuanzia tarehe 10 hadi 16 Machi, 2016 ambapo lengo la ziara hiyo ni kutembelea na kukagua Magereza ya Mkoa wa Kagera pamoja na kujionea miradi ya uzalishaji inayosimamiwa na jeshi hilo.
  Kamishna Jenerali wa Magereza John C. Minja( wa pili kushoto) akikagua maeneo mbalimbali ya Gereza Bukoba alipofanya ziara ya kikazi leo Machi 11, 2016 (wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera, SACP. Omari Mtiga (wa pili kulia) ni Mkuu wa Gereza Bukoba, ACP. Benizeth Bisibe.
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella akiongea ofisini kwake na Kamishna Jenerali wa Magereza John C. Minja na ujumbe wake kama inavyoonekana katika picha.
  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba Mhe. Sivangilwa Mwangesi Akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza John C. Minja alipomtembelea ofisini kwake.
  Kamishna Jenerali wa Magereza John C. Minja (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani Kagera mara baada ya kutembelea Gereza la Wilaya ya Bukoba (Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Klabu maarufu ya kuogelea jijini, Dar Swim Club imewapongeza waogeleaji wake kwa kufanya vyema katika mashindano ya taifa ya kuogelea yaliyomalizika hivi karibuni katika bwawa la Hopac.

  Akizungumza jijini jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Inviolata Itatiro alisema kuwa waogeaji wake wameweza kuboresha muda wa kuogelea na kuiwezesha klabu hiyo kutwaa nafasi ya kwanza kwa upande wa wanawake kwa kukusanya jumla ya pointi 1,964.50.

  Inviolata alisema kuwa kwa upande wa wanaume, walikusanya jumla ya pointi 1,086.50 na kushika nafasi ya pili. Alisema kuwa wamefarijika na matokeo hayo kutokana na wao kuwakilishwa na waogeleaji chipukizi katika mashindano hayo.

  “Hii ni faraja kwetu, tumeweka mikakati ya kukuza mchezo wa kuogelea kwa miaka 10, tunawaogeaji wadogo sana lakini wana vipaji vya hali ya juu, lakini kutokana na mfunzo mazuri ya makocha wetu, wameweza kuwashinda waogeleaji wenye umri mkubwa, kwa kweli wanastahili pongezi,”.

  “Wakati tunaanza, hatukutegemea kufikia hatua hii, tuliweza kutwaa medali 94 katika mashindano ya kuogelea ya Taliss na kushika nafasi ya kwanza na kuwa klabu bora, natoa wito kwa wazazi ambao wanataka watoto wao kujua kuogelea na kushindana katika mashindano ya ndani na kimataifa, kujiunga na klabu yetu,” alisema Inviolata.
  Alisema kuwa mafanikio ya klabu yao yametokana na ushirikiano wao na wazazi na wadhamini mbalimbali ambao wamekuwa nguzo kubwa ya kufanikisha mambo kadhaa ya maendeleo ya mchezo wa kuogelea.

  “Tuliweza kufanya semina kwa makocha na waogeleaji wetu chini ya mkufunzi wa kimataifa na muogeleaji nyota wa zamani wa Olimpiki, Penny Heyns wa Afrika Kusini. “Mafunzo yalikuwa ya kisasa na sasa tunajivunia matunda yake, nawashukuru makocha kwa kufanya kazi kubwa,” alisema.

  Alisema kuwa makocha wao, Michael Livingstone, Ferick Kalengela, Radhia Gereza, Kanisi Mabena, Adam Kitururu, Simon Ngoya na Salum Mapunda wamekuwa nguzo kubwa ya kufikia malengo yao.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akisalimiana na Rais wa Vietnam NdgTruong Tan Sang mapema hii leo walipokutana kwaajili ya mazungumzo kuhusu fursa zilizopo katika kilimo,mifugo na uvuvi katika nchi mbili hizi rafikiKatika mazungumzo ya pamoja kati ya Rais wa Vietnam na Mh.Mwigulu Nchemba na ujumbe wake,Pande hizi mbili zimekubaliana kushirikiana kwenye uzalishaji wa mbegu bora za mazao na uzalishaji wa samaki hapa nchini,Mbali zaidi wamekubaliana kufungua fursa zaidi kwa wafanyabiashara wa nchi hizi mbili kuwekeza kwenye kilimo,mifugo na uvuvi.Mauzngumzo yakiendelea kati ya ujumbe kutoka Vietnam na wadau wa kilimo hapa nchini.
  Mh.Mwigulu Nchemba akiagana na Rais wa Vietnam mara baada ya mazungumzo ya pamoja kumalizika.
  Picha/Maelezo na Festo Sanga Jr.

older | 1 | .... | 1154 | 1155 | (Page 1156) | 1157 | 1158 | .... | 3285 | newer