Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WATOTO CHINI YA MIAKA 5 KUNUFAIKA NA UPIMAJI WA AFYA BURE KUTOKA KWA BANGO SANGHO

$
0
0
Bango Sangho
Mwenyekiti wa Umoja wa Jamii ya watu kutoka India, Bengali waliopo Tanzania (Bango Sangho), Kunal Banerjee akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inayotayotaraji kufanyika katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mmoja wa madaktari watakaoendesha zoezi la upimaji afya kwa watoto hao Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki ya Al Hilal ya jijini Dar es Salaam.

Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) unataraji kutoa huduma ya upimaji wa afya bure kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano, upimaji utakaofanyika Jumapili ya Machi, 13 katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam.

Akizungumzia huduma hiyo, Mwenyekiti wa Bango Sangho, Kunal Banerjee amesema huduma hiyo itawawezesha wazazi kutambua magonjwa yanayowakabili watoto wao bila kulipa malipo yoyote kwa kutambua umuhimu wa afya ya watoto kwa maendeleo ya taifa.Alisema kupitia huduma hiyo madaktari watawapima watoto walio na umri chini ya miaka mitano afya ya kinywa, uzito, ukaguzi na ushauri wa lishe hivyo kuwataka wazazi kuwapeleka watoto wao ili waweze kupata huduma bure.
Ali Mzige
Mmoja wa madaktari watakaoendesha zoezi la upimaji afya kwa watoto hao Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki ya Al Hilal ya jijini Dar es Salaam akifafanua jambo kuhusiana na umuhimu wa kupima afya za watoto katika mkutano na waandishi wa habari.“Tunataka kusaidia marafiki zetu wa Tanzania na katika kuendelea hilo tutatoa huduma ya bure kwa watoto kupima afya zao na tunataka wazazi wawalete watoto ili wapime afya,” alisema Banerjee.

Nae Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki Al Hilal alisema Bango Sangho kimekuwa chama ambacho kikisaidia jamii ya Tanzania katika sekta ya afya na wamekuwa wakitoa huduma ya kupima watoto bure walio na umri chini ya miaka mitano kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Alisema ripoti ya afya Tanzania inaonyesha kuwa kuna watoto 81 wamekuwa wakipoteza maisha kati ya watoto 1,000 walio na umri chini ya miaka mitano kutokana na sababu mbalimbali ambapo wamekuwa hawapati huduma na kupitia huduma hiyo ya kuwapima bure watoto walio na magonjwa wataweza kutambulika.

“Tutafanya huduma ya kupima bure watoto walio chini ya miaka mitano na tutakaobaini wanamatatizo maalum ya kiafya tutawapa rufaa ili wakapate huduma ya matibabu,” alisema Dkt. Mzige.

Huduma hiyo ya kupima watoto walio na umri chini ya miaka mitano ilifanyika pia mwaka jana na watoto 289 walipimwa afya zao huku baadhi walikutwa na matatizo ikiwemo maambukizi ya mfumo wa njia ya mkojo UTI, Utapiamlo, kukatwa vimeo na wengine wakionekana kuwa na afya duni.
Husna Abdallah
Mtaalamu wa afya ya uzazi kutoka Kliniki ya Al Hilal, Bi. Husna Abdallah akitoa msisitizo kwa akina mama kuzingatia kanuni za afya ya uzazi wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
Zawadi Chogongwe
Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Zawadi Chogongwe (kulia) akiuliza swali kwa wataalamu wa afya wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inayotayotaraji kufanyika katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

JUMUIYA YA KIMATAIFA YAKARIBISHA UTEUZI WA MKAPA YATAKA APEWE USHIRIKIANO

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, New York
Jumuiya  ya Kimataifa  imezitaka pande zinazopinga  Nchi  Burundi, kumpatia ushirikiano wa  kutosha ,Rais  Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ameteuliwa na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kuratibu   majadiliano ya kutafuta  ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa   unaoendelea nchi humo.
Pamoja na  pande zinazopingana kutakiwa kufanya hivyo kwa moyo mmoja,  pia     Taasisi za Kimataifa na Kikanda  ukiwamo Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, pamoja na wadau wengine wametakiwa pia kumuunga mkono na kutoa ushirikiano kwa Rais Mstaafu  Benjamin Mkapa.
Wito huo umetolewa siku ya Jumatano, hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  wakati  Wajumbe wa    Burundi Configuration walipokutana katika kikao chao  na kujadili hali ya kisiasa na kiusalama inavyoendelea nchi Burundi kufuatia ziara  iliyofanywa na  Mwakilisji wa Kidumu wa……  Balozi Jurg Lauber ambaye ni   Mwenyekiti wa   Burundi  Configuration.
“Tunakaribia  uteuzi wa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa kuwa  mratibu wa mazungumzo  ya  kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi. Tunatoa wito kwa pande zinazopingana nchi  humo, serikali na  vyama vya kiasa kumpatia ushirikiano bila ya mashari yoyote” akasema Mwakilishi wa Marekani.
Naye Mwakilishi  wa Kudumu wa  Ubeligiji, Balozi Benedicte Frankinet. Pamoja na kueleza kwamba   ujumbe wake   unawasiwasi kuhusu  taarifa za kuendelea kwa matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu na mbinyo kwa vyombo vya habari na uhuru wa watu  kutembea.
Amesema .“ Rais Mstaafu wa Tanzania , Benjamin Mkapa, anauzoefu mkubwa na wa hali ya juu katika   uratibu na  utafutaji ufumbuzi wa  migogoro ya kisiasa, ujumbe wangu unakaribisha uteuzi wake, hapana shaka ataratibu  na kusimamia  majadiliano jumuishi  yatakayohusisha wadau wote wanaopingana  nchini Burundi wakiwamo pia wajumbe wa asasi zisizo za kiserikali”.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa  Kudumu wa  Netherland,  Balozi Karel Van Oosterom,  amesema ujumbe wake pia  unakaribisha uteuzi wa  Rais Mkapa, na kwamba pande zinazopinga nchini Burundi zinatakiwa kuitumia  fursa ya  uteuzi wa Mkapa kurejea katika  meza  ya majadiliano  ambayo  yatakuwa  jumuishi na  huku akizisihi pande hizo kutotoa masharti ya aina yoyote ile.
Naye   Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda,  pamoja na  kukaribisha  uteuzi wa Rais Mstaafu Mkapa ambaye amesema ana uzoefu mkubwa na wanaimani naye,  alimshukuru pia, Rais  John Pombe  Magufuli  kwa  kumteua Mkapa.
Karibu wajumbe wote waliochangia majadiliano kuhusu  hali ya  Burundi walikaribisha na kupongeza uteuzi wa Mkapa  huku, Mjumbe wa Nigeria pamoja  naye kuunga mkono uteuzi wa Mkapa.  Alisisitiza pia kwamba Majadiliano jumuishi ya kutafuta ufumbuzi wa  kudumu nchini  Burundi  yanapashwa kumilikiwa na Warundi wenyewe.
Akatahadharisha kwa kusema kwamba,   mashinikizo kutoka nje ya Burundi  hayana nafasi  katika  mchakato huo na kwamba hali  hiyo ikiruhusiwa inaweza  siyo tu kuathiri majadiliano hayo lakini pia  itakuwa ni kuwaingilia wananchi wa Burundi.
Mwakilishi wa  Kudumu wa Tanzania,  Balozi Tuvako Manongi akichangia  majadiliano hayo, yeye ametaka ushughulikiaji wa  hali tete ya kisiasa na kiusalama uende sambamba na  uondoajji wa vikwazo  vya kiuchumi   kwa Serikali ya Burundi.
“  Hakuna  matinki ya kutia msisitizo wa  kuitaka serikali ya  Burundi kutekeleza mambo kadha wa kadhaa yakiwamo ya  ukiukwaji wa haki za binadamu, pasi kuzungumzia hali  mbaya  ya uchumi na kijamii  inayoikabili Burundi na watu  wake. Akasema Balozi
Nakusisitiza . “Tunapojadili hali ya  usalama tujadili  basi na uondoaji wa  vikwazo vya  kiuchumi kwa sababu mambo haya yanakwenda kwa  pamoja.  Njia sahihi ya kusaidia mchakato  wa  kutafuta amani ya  kudumu nchini Burundi ni kwa   sisi sote   tulio katika meza hii  kufanya kazi  kwa  pamoja  na  katika  namna  inayoeleweka”.
Vile vile Balozi Manongi ambaye Tanzania ni  mjumbe wa Burundi Configuration ambayo ni sehemu ya Kamisheni ya Ujenzi wa Amani ( Peace Building Commission)  amesisisiza  wananchi wa Burundi kumiliki   mchakato wa majadiliano kuhusu mustakabali wa nchi yao.
Hoja ya  kuondolewa kwa vikwazo vya  kiuchumi, Warundi kumiliki majadiliano yao, pia  imeungwa mkono  na  mjumbe wa China ambaye  amesema Haki za binadamu  zinahusu pia haki ya kupata maendeleo na kwamba Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kuisadia Burundi kiuchumi ili wananchi wapate  maendeleo ambayo ni haki yao.

WANDISHI WA HABARI WA ZANZIBAR WATAKIWA KUELIMISHA JAMII JUU YA MARADHI YA KIPINDUPINDU

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya Maafa Zanzibar ndugu Ali Juma Hamad akifungua mafunzo ya waandishi wa habari juu ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu katika Ukumbi wa gereji ya Wizara ya Afya Mombasa Mjini Zanzibar, (kulia) daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt Fadhili Mohd na (kushoto) Mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmay. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza kwa makini Daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt. Fadhili Mohamed alipokuwa akielezea njia za kukabiliana na kipindupindu katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika Ukumbi wa Gereji ya Wizara ya Afya Mombasa Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Rafii Haji Mkame akiwasilisha mada ya wajibu wa waandishi wa habari katika kukabiliana na maradhi ya miripuko katika mafunzo yaliyofanyika Ukumbi wa Gereji ya Wizara ya Afya Mombasa Mjini Zanzibar.
Katibu wa Jumuiya ya Maafisa wa Afya Zanzibar Ahmed Suleiman Said akitoa elimu ya kupambana na maradhi ya kipindupindu kwa wananchi wa shehia ya Shaurimoyo Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Baadhi ya wananchi wa shehia ya Shaurimoyo Mjini Zanzibar wakifuatilia juu ya elimu ya ugonjwa wa Kipindupindu iliyotolewa na Jumuiya ya Maafisa wa Afya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
 

RAIS WA ZANZIBAR AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA VIETNUM

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akipofika kwa mazungumzo na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Ujumbe wake (kushoto) wakiwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Rais wa Vietnam Truong Tan Sang jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akiwa nchini kwa ziara ya Kikazi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akifuatana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(katikati) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(kulia) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Augustin Mahiga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akiagana na mgeni wake Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(katikati) mawair mbali mbali wa Vietnum walioungana na Rais Truong

Rais Magufuli amkaribisha katika dhifa Rais wa Vietnam Ikulu Jijini Dar es Salaam.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali toka Tanzania na Vietnam kwenye halfa ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang akizungumza na viongozi mbalimbali toka Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha  iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akigonga glass na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang ikiwa ni ishara ya ushirikiano kati ya Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Generali Aldof Davis Mwamunyange (Wa pili kulia) akifatilia hotuba za Rais wa Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspecta Generali Ernest Mangu, wa pili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali  Casmir Minja, katikati ni Mkuu wa Usalama Rashid Othman na kushoto ni Kamanda wa Kanda maaalum Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (katikati) akifatilia halfa ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kushoto ni Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la wananchi la Tanzania Luteni Generali Abdulrahman Shimbo.Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO.

SIMU TV: MAPITIO YA MAGAZETI LEO

WAUMINI WA KANISA LA ADVENTISTA LA WASABATO WANATARAJIA AADHIMISHA SIKU YA MATENDO YA HURUMA KWA KUCHANGIA DAMU

$
0
0
Mpango wa Taifa wa Damu salama kwa kushirikiana na waumini wa dhehebu la Sabato wanatarajia endesha zoezi la kuchangia damu kwa hiari katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Mikoa hiyo ni Dar-es-salaam, Morogoro, Mbeya, Dodoma, Mwanza, Kilimanjaro,Arusha, Kigoma, Tabora, Mara,na Iringa, lengo likiwa ni kukusanya chupa 2000.

Siku ya matendo ya huruma hufanyika jumamosi ya tatu ya mwezi wa tatu kila mwaka, ambapo waumini hushiriki katika huduma mbalimbali za jami.

Imetolewa na Idara ya Masoko na Uhusiano Mpango wa Taifa wa Damu Salama Tanzania

KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI CHA MKOA WA LINDI CHAFANYIKA

$
0
0

 Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Jordan Rugimbana akisoma hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Ushauri mkoa.
 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri mkoa wa Lindi.
 Wajumbe wa Kikao cha Ushauri cha mkoa wa Lindi.
 Mbunge wa Jimbo la Lindi mjini Mhe. Hassan Kaunje akichangia maoni yake kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri  ya mkoa wa Lindi.
Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Jennifer Mgendi alipania Tamasha la Pasaka

$
0
0
MWIMBAJI na Msanii mahiri wa Filamu Tanzania, Jennifer Mgendi  amelipania Tamasha la Pasaka linalotarajia kuanza Machi 26-28 katika mikoa ya Geita, Mwanza na Kahama.

Kwa mujibu wa Mgendi hivi sasa analisubiri kwa amu tamasha hilo ambalo lina malengo ya kusifu na kuabudu kupitia nyimbo mbalimbali za Injili sambamba na viongozi wa dini mbalimbali.

Mgendi alisema analisubiri kwa hamu Tamasha la Pasaka ambalo litafanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambako hivi sasa waimbaji wengine pia wanaendelea na mazoezi kuelekea tamasha hilo. 
 
Mgendi alitumia fursa hiyo kuwaomba mashabiki wake wa mikoa hiyo hasa wa nyimbo za Injili na Filamu  kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ili kupokea baraka za bwana kupitia uimbaji.

Aidha Mgendi alisema katika tamasha hilo aakuwa na albamu nyingine mpya inayokwenda kwa jina lka Nyuma ya Mlima  ambako alisisitiza kuwaomba mashabiki wa muziki wa Injili kujitokeza kuipata albamu hiyo.
Anazitaja nyimbo zilizoko kwenye albamu hiyo ni pamoja na Nyuma ya Mlima, Naomba Uzima, Bwana ni Ebenezer, Nawashukuru adui na Nitafika lini Remix.

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akutana na mkurugenzi wa radio France Internationale

$
0
0
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akimkaribisha Mkurugenzi wa Radio France Internationale(RFI) Bi.Cecile Megie ofisini kwake alipomtembelea kwa ajili ya kufahamiana na kuboresha mahusiano yaliyopo kwa miaka saba sasa.
 Ujumbe kutoka Radio France International (RFI) wakifurahia jambo wakati wa kikao na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura(Hayupo pichani).

Mkurugenzi wa Radio France Internationale (RFI) Bi.Cecile Megie(kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura kuhusu msaada ambao wameipa shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) ili kusaidia katika kufikisha matangazo yake mbali Zaidi.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Radio France Internationale(RFI) Bi.Cecile Megie ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura(kulia) akimpa zawadi ya kahawa kutoka Tanzania Mkurugenzi wa Radio France Internationale(RFI) Bi.Cecile Megie(kushoto) baada ya mazungumzo mafupi ofisini kwa Naibu Waziri uyo kuhusu kuimarisha mahusiano baina ya nchi izi mbili katika masuala ya Habari kati ya TBC na RFI.

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA BALOZI WA KOREA NCHINI TANZANIA

$
0
0

 Balozi wa Korea nchini Tanzania Bw. Chung IL akibadilishana mawazo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria alipomtembelea leo (10/3/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na Balozi wa Korea nchini Tanzania Bw. Chung IL alipomtembelea leo (10/3/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.
 

Majina ya Waalikwa Kwenye Celebrity Corporate Conference & Cocktail

$
0
0
Kama Usipoona jina lako hapa, basi liko kwenye list ya October,2016 ambapo event hii itafanyika tena. 

WAPI: Hyatt Regency,The Kilimanjaro Marquee
MUDA: Saa Nane Mchana 
MAVAZI: Business ( Jeans na T Shirt havitaruhusiwa)
TIKETI: Kwenye Dawati la Kujiandikisha, Hyatt Regency,The Kilimanjaro
Vyeti vitatolewa kwa washiriki wote.

WAALIKWA KWENYE CELEBRITY CORPORATE CONFERENCE AND COCKTAIL, MARCH 2016.

WAZIRI MWAKYEMBE AKIONGEA NA WATENDAJI WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Wakili Bahame Nyanduga akimuelezea Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe juu ya utendaji kazi waTume hiyo na changamoto mbalimbali wanazozikabili . Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri leo  jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na watendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, yaliyofanyika ofisini kwake leo jijini Dar Es Salaam.

SERIKALI YA KIFALME YA NORWAY KUSAIDIA UKUSANYAJI WA KODI NCHINI.

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone Skogen akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mapango wa ukusanyaji kodi nchini kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji.

SERIKALI ya Kifalme ya Norway imetoa kiasi cha Dola za kimarekani shilingi Milioni 5 kwa Serikali ya Tanzania kwa kuwaunga mkono Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Serikali ya awamu ya tano katika jitihada zake katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato nchini.

Makubaliano hayo ya ufunguzi wa kuchangia mapato yamefanyika leo jijini Dar es salaam kati ya Naibu Waziri wa mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone Skogen pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji.

Akizungumza katika ufunguzi huo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone Skogen amesema kuwa lengo la mpango huo ni kuimarisha na kuongeza kodi ya mapato ya ndani kwa  kuhakikisha kwamba mianya ya wakwepaji kodi inazuiwa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amesema kuwa Serikali imeendelea kuimarisha na kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa ulipaji kodi bila kushurutishwa ili kuondokana bajeti  tegemezi kutoka nje.

“Lengo la kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa  ulipaji kodi bila kushurutishwa na kuzuia mianya yote ya ukwepaji kulipa kodi  ni kuondokana na utegemezi wa bajeti na kuanza kujitegemea hivyo hatuwezi kufika huko bila kuimarisha ukusanyaji wa  mapato nchini” alisisitiza Naibu Waziri huyo.

Naye Kaimu Kamishna Mkuu TRA Bw. Alphayo Kidata ameishukuru Serikali ya Kifalme ya Norway kwa kuimarisha uwezo wa wataalamu nchini kwa kuwawezesha mbinu mbalimbali za kukagua mahesabu katika makampuni makubwa nchini.
 
Awali Serikali ya Kifalme ya Norway ilitoa zaidi ya Dola za kimarekani million 3 katika mpango huo wa kuimarisha ukusanyaji wa mapato nchini.

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA KONGAMANO LA TATU LA KISUKARI AFRIKA,.

$
0
0
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ugonjwa wa Kisukari (Tanzania Diabets Association), Profesa Andrea Swai akizungumza na waandishi wa habari jinini Dar es Salaam leo kuhusiana na maradhi ya ugonjwa wa kisukari pamoja na chanzo cha ugonjwa huo ambao sio wa kuambukizwa.
Mwathirika wa ugonjwa wa Kisukari, Ramadhan Mongi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kufuata sheria za ulaji ili kuepukana na ugonjwa wa kisukari ambao ni ugonjwa unaosababishwa na ulaji mbaya wa chakula pamoja na kutokufanya mazoezi.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ugonjwa wa Kisukari (Tanzania Diabets Association), Profesa Andrea Swai katikati, kulia ni Mwathirika wa ugonjwa wa Kisukari, Ramadhan Mongi na Mratibu wa Mpango wa kitaifa wa kisukari Tanzania, John Gadna wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na ugonjwa wa Kisukari.

TANZANIA inatazamia kuwa mwenyeji wa kongamano kubwa la tatu la kisayansi la Magonjwa yasiyoambukiza ikiwa ni pamoja na Kisukari, Kongamano ambalo litaanza Machi 14 na linatazamiwa kuendela hadi tarehe 16 March, 2016 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Convention Centrem, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari juzi, Mwenyekiti wa Chama cha kisukari Tanzania Profesor, Andrew Swai, amesema ni furaha kubwa na heshima kwa Tanzania kuwa wenyeji wa Kongamano hilo ambalo litawakaribisha wageni kutoka nchi nyingine za Afrika ya Mashariki na kusini kushiriki katika majadiliano na uchunguzi huo na Kisayansi.

Amesema kongamano hilo ambao litahusisha Nchi za Afrika Mashariki na kusini kujadili mbinu mbalimbali za namna ya kuudhibiti ungonjwa huo, limeandaliwa na East African Diabetes study Group (EADSG) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Aidha Profesor Andrew Swai amesema kuwa Kongamano hilo litafuatiwa na mkutano Maalum wa wadau wa kisukari duniani utakaofanyika, Machi 17 hadi 18 2016 katika ukumbi huo huo wa Kimataifa wa Julius Nyerere Convention Centre jijini Dar Es Salaam, Tanzania.

Mkutano huo ulioandaliwa na Mfuko wa kusaidia Kisukari Duniani (NCD Symposium),kutoka Denmark kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto nchini Tanzania, pamoja na Shirika la Afya Duniani Ofisi za Mikoa kwa Afrika pamoja na Shirikisho la Kisukari duniani utajadili mambo mbali kuhusu namna ya kusaidia wagonjwa waishio na Kisukari kwa kuwa gharama zake ni kubwa mno.

Mikutano hiyo miwili inalenga kutatua tatizo kubwa la Kisukari linalooendela kukua barani Afrika kwa sasa ambalo limeonekana kukua mara tatu zaidi ndani ya miaka mitano iliyopita.

Profesa Swai amesema kuwa, mbali na mjadala wa uchunguzi wa kisayansi, Mambo mengine yatakayo jadiliwa ni pamoja na
• Kuongezeka kwa ugonjwa wa kisukari katika nchi zinazoendelea, na lengo hasa juu Africa na namna ya kutatua matatizo yatokanayo.
• Kujadili kuhusu mzigo wa kijamii na kiuchumi unaotokana na watu wenye ugonjwa wa kisukari , familia zao na jamii kwa ujumla.
• Umuhimu wa kutafuta ufumbuzi wa Ugonjwa huu.
• Taarifa za uchunguzi za wataalam ngazi za mkoa.
Aidha utafiti uliotolewa hivi karibuni umeonyesha kuwa katika kila sekunde sita mtu mmoja hufa kutokana na ugonjwa wa kisukari ( vifo zaidi ya milioni 5.0 hutokea duniani)
- Mmoja katika watu wazima 11 ana ugonjwa wa kisukari ( watu milioni 415 duniani kote wanaishina Kisukari)
- Moja katika vizazi saba, huadhirika na ugonjwa wa kisukari katika kipindi cha ujauzito na kujifungua.
- Robo tatu (75%) ya watu wenye ugonjwa wa kisukari wanaishi katika nchi chini na kipato cha kati.
- Zaidi ya watu wazima wengi wanakufa kutokana na ugonjwa wa kisukari kuliko kutokana na VVU / UKIMWI, kifua kikuu na hata malaria.
- Wastani wa milioni 14.2 watu wazima wenye umri kati ya 20-79 wana ugonjwa wa kisukari katika Kanda ya Afrika.

- Afrika inaongoza kwa wagonjwa wa kisukari ambao haujatambuliwa, kutokana na kutocheki afya zao; zaidi ya 66.7 % ya watu wenye ugonjwa wa kisukari hawajui kuwa wana ugonjwa wa kisukari.

- Mtu na kisukari aina ya 2 (Type 2 Diabetes) anaweza kuishi kwa miaka kadhaa bila kuonyesha dalili yoyote, madhara yanayoweza kujitokeza ni pamoja na ugonjwa wa figo, moyo kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa jicho na kusababisha upofu na matatizo ya mguu na kusababisha ulema.

- Mataifa ya Afrika kwa idadi kubwa ya watu wenye ugonjwa wa kisukari ni pamoja na Afrika Kusini (2.3 milioni ), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (1.8 milioni ), Nigeria ( milioni 1.6 ) na Ethiopia (1.3 milioni).

BENKI YA CRDB YAIKOPESHA MANISPAA YA TEMEKE BIL.19.6

$
0
0
MANISPAA ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, imepokea mkopo wa sh bilioni 19.6 kwa ajili ya kuwalipa fidia wakazi wa maeneo yatakayobomolewa ili kupisha mpango wa maendeleo na ustawi jiji.

Mkopo huo utakaolipwa kwa miaka sita una lengo la kufanikisha mradi mkubwa wa ujenzi na uboreshaji miundombinu ya jiji uitwao Dar es Salaam Metropolitan Development Project (DMDP).

Akizungumza na ujumbe wa viongozi na madiwani wa wilaya ya Temeke ulioongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei iliyotoa mkopo huo alisema wanaunga mkono hatua za maendeleo zinazochukuliwa na Serikali Kuu na Tamisemi. 

Alisema fedha hizo zitatumika kwenye ujenzi wa mtandao wa barabara za lami wenye urefu wa kilometa 81.63 ujenzi wa masoko ya kisasa, vituo vya mabasi ya kisasa, upimaji wa viwanja 2,000 eneo al Kijichi na kuweka huduma za msingi, ujenzi wa mifereji ya mvua kilometa 22.4, dampo la kisasa eneo la Kisarawe na madaraja yanayounganisha kata mbalimbali.

“Tumetoa mikopo ya maendeleo kama huu kwenye halmashauri za Mwanza, Magu, Kinondoni, Mbeya na Mji wa Bukoba ambapo jumla ya sh trilioni tatu ambazo ni karibu sawa na bajeti ya maendeleo inayotengwa na serikali ambayo ni sh trilioni saba,” alisema Dk. Kimei.

Mjema aliwaonya watendaji wanaohusika na mradi huo kutoongeza majina ya wanaotakiwa kulipwa huku akisisitiza kwamba watakaobainika kuhujumu mradi huo na kutumia isivyostahili mkopo huo, watafukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya kutia saini mkataba wa mkopo wa shs. bilioni 19.6 kwa ajili ya ulipaji fidia kwa wananchi wanaopisha mradi wa uboresha miundombinu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za jijini la Dar es Salaam (DMDP). (Picha ha Francis Dande)
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB akizungumza katika hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumza katika hafla ya kutia saini mkataba wa mkopo wa shs. bilioni 19.6 kwa ajili ya ulipaji fidia kwa wananchi wanaopisha mradi wa uboresha miundombinu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za jijini la Dar es Salaam (DMDP).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAHAKIMU WAMETAKIWA KUTUMIA TAALUMA KATIKA KUAMUA KESI.

$
0
0
 Balozi Mdogo wa Uingereza, Matt Sutherland  akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na Uingereza na Tanzania kufanya kazi kwa pamoja katika mafunzo haya. Historia yenye kufanana katika sheria na taasisi zetu za kisheria inatoa fursa pana kwa nchi hizi kuweza kufanya kazi na kujifunza baina ya kila mmoja. Mafunzo haya yatawezesha kutoa ujuzi wenye thamani kwa wale watendaji wa mstari wa mbele katika kupambana na makosa makubwa nchini Tanzania.leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Shaban Lila.
 Jaji Kiongozi kutoka mahakama kuu ya Tanzania Shaban Lila akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mahakimu watatumia  ujuzi  na elimu walioipata katika kutatua changamoto ya ucheleweshwaji wa kesi na mashauri mbalimbali, leo jijini Dar es Salaam.
 Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Shaban Lila akimpa cheti chamafunzo ya namna ya kushughulikia makosa makubwa Joachim Tiganga katika hoteli ya White Sands, Mbezi Beach, Dar es Salaam.
Balozi Mdogo wa Uingereza, Matt Sutherland na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Shaban Lila wakiwakatika picha ya pamoja na Mahakimu wafawidhi 14 toka mahakama mbalimbali Tanzania ikiwemo; Kisutu, Kigoma, Arusha, Moshi, Mwanza, Sumbawanga, Temeke, Dodoma, Kinondoni na Mbeya wamehudhuria mafunzo hayo.leo jiji Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
MAHAKIMU nchini wametakiwa kuhakikisha wanatumia vyema mafunzo wanayoyapata katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufasaha hasa katika kuamua kesi kubwa kama za ugaidi, madawa ya  kulevya ,ufisadi na utakatishaji wa fedha haramu  ili kuiendeleza nchi.

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Jaji Kiongozi Mahakama kuu ya Tanzania, Shaban Lila  wakati akifunga mafunzo maalumu kwa ajili ya kuongeza ujuzi wa kijaji wa kuhukumu makosa makubwa ya kialifu.

Mafunzo yalioandaliwa na serikali ya uingereza  kwa kushirikiana na mahakama  kuu ya uingereza ambapo amesema  mafunzo hayo yatakuwa na msaada zaidi endapo wahusika ambao ni mahakimu watatumia  ujuzi  na elimu walioipata katika kutatua changamoto ya ucheleweshwaji wa kesi na mashauri mbalimbali.

Mafunzo haya ni ya pili kutolewa kwa Mahakama ikiwa ni kufatiwa kwa mafunzo yaliyokwisha kutolewa mnamo Novemba, 2015 kwa Majaji wa Mahakama Kuu.

Ukanda wa Bahari ya India unakabiliwa na ongezeko kubwa la wasafirishaji wa madawa ya kulevya ambao husafirisha viwango vikubwa vya madawa haramu ya kulevya kuyaleta Afrika Mashariki toka nchi za Afghanistan na Pakistani. 

Tangu mwaka 2012 Majeshi ya Kimataisha ya Wanamaji katika ukanda huu yamemudu kudhibiti zaidi ya vyombo vya baharini 44 na kukamata zaidi ya tani 8 za madawa aina ya heroini na tani 30 za madawa aina ya “hashish”.

Ushirikiano katika kazi baina ya Uingereza na Tanzania umefanikisha kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa wasafirishaji wakubwa wa kimataifa wa madawa ya kulevya kote Tanzania na Uingereza Matt Sutherland alieleza na kufafanua kwanini Uingereza inafadhili kazi hizi Tanzania na Uingereza ina mtizamo unaoshabihiana katika kukabiliana na makosa makubwa. 

Tunaona kuongezeka kwa wahalifu wa kimataifa wakitumia mitandao ya kimataifa kusafirisha madawa ya kulevya, mazao haramu ya wanyamapori au kuficha wahalifu. Ni kwa kufanya kazi kwa ushirikiano tu ndipo kunaweza tukahakikisha wahalifu hawana mahala pakujificha.

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA GHAFLA BENKI KUU (BOT) JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa kaongozana na Naibu Gavana wa BOT Dkt Natu Mwamba akiwasili makao makuu ya Benki Kuu ya Tanzania alikofanya ziara ya kushtukiza leo Machi 10, 2016.

VIETNAM KUPANUA WIGO WA KUWEKEZA SEKTA YA MAWASILIANO TANZANIA.

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa (katikati) akizungumza na Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Vietnam Bw.  Nguyen Bac Son (kushoto) kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Vietnam na (kulia) ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwini Ngonyani.

Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Vietnam Bw.  Nguyen Bac Son (kulia) akimuaga mwenyeji wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa wa pili (kushoto) baada ya kufanya mazungumzo ya ushirikiano katika sekta ya Mawasiliano, (kushoto) ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwini Ngonyani.


 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
VIETNAM KUPANUA WIGO WA UWEKEZAJI KWENYE SEKTA YA MAWASILIANO TANZANIA.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Mb) amekutana na Waziri wa Habari na Mawasiliano wa nchi ya Vietnam Bwana Nguyen Bac Son ofisini kwake kwa lengo la kupanua wigo wa uwekezaji kwenye Sekta ya Mawasiliano nchini Tanzania na kushirikiana kwa pamoja kuendeleza Sekta hizo baina ya Tanzania na Vietnman. Kikao hicho ni muendelezo wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang na ujumbe wake nchini Tanzania.


Prof. Mbarawa alisema kuwa Tanzania imekuwa na ushirikiano na Vietnam kupitia Kampuni ya Viettel kwa kuwekeza kwenye miundombinu ya kufikisha huduma za mawasiliano vijiini kwa kutiliana saini Mkataba. Mkataba huo ni wa miaka mitatu kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2014 hadi Novemba, 2017 ikijumuisha ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wenye urefu wa kilomita 20,000 kwenye wilaya zote nchini; kujenga miundombinu ya mawasiliano kwenye vijiji  4,000; kuunganisha Ofisi za Wakuu wa Wilaya; hospitali za Wilaya; Ofisi zote za Posta  za Wilaya; na kupeleka na kutoa huduma za intaneti bila malipo kwenye shule 3 za Sekondari za Serikali katika kila Wilaya nchini kwa kipindi cha miaka mitatu.


Aidha, Prof. Mbarawa aliongeza kuwa tangu Kampuni ya Viettel yenye jina la biashara la Halotel ilipoanza kufanya kazi rasmi mwezi Oktoba mwaka 2015, imeweza kupeleka huduma ya mawasiliano maeneo ya vijijini na hadi hivi sasa ina watumiaji wa simu za mkononi wapatao milioni 1.2 na wananchi walio wengi wanafurahia huduma hiyo tofauti na hali ilivyo kuwa hapo awali kipindi cha miezi sita iliyopita na ikizingatiwa kuwa sehemu nyingine za vijijini hapakuwa na mawasiliano. Pia alisema kuwa, “Serikali ya Tanzania itaendelea kujenga na kuwekeza kwenye Sekta ya Mawasiliano ili kuwavutia wawekezaji na kampuni za simu za mkononi ambapo Serikali ya Tanzania ilitoa ruzuku kiasi cha dola za marekani milioni 30 ili kuziwezesha kampuni hizo kupeleka mawasiliano vijijini na maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara”. Hadi kufikia mwezi Machi, 2016 Halotel imejenga Mkongo wenye urefu wa kilomita 18,000 kati ya kilimota 20,000; na kujenga miundombinu ya mawasiliano kwenye vijijini 1,605 kati ya vijiji 4,000 visivyokuwa na mawasiliano.


Katika mazungumzo hayo ya kuendeleza sekta ya Mawasiliano Tanzania, Prof. Mbarawa aliwaalika wawekezaji kutoka Vietnam wa Sekta ya Mawasiliano na kampuni ya Halotel kujiandaa na kuja Tanzania kushiriki mnada wa kununua masafa ya 700MHz ambayo yamepatikana baada ya kuhama kutoka Teknolojia ya Utangazaji ya Analojia na kuhamia Teknolojia ya Utangazaji ya Dijitali.  Pia alisema kuwa Kampuni za Vietnam zinakaribishwa kuanzisha na kuendeleza huduma za mawasiliano za mfumo wa kumpatia mteja huduma tatu kwa pamoja ya sauti; intaneti; na kuangalia televisheni ikijulikana kwa jina la triple player ili Tanzania iweze kwenda sambamba na kasi ya ukuaji wan a maendeleo ya TEHAMA yanayotokea dunia nzima.


Katika kikao hicho, Prof. Mbarawa alimweleza Mhe. Ngoyen Bac Son kuwa Tanzania iko tayari kusaini Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano na Serikali ya Vietnam wa kubadilishana wataalamu kwenye Sekta ya Mawasiliano na kuwapatia mafunzo ili kujenga uwezo wa wataalamu wetu wa Tanzania; na kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo vidogo vya TEHAMA (ICT Small Scale Factories) nchini Tanzania ambapo viwanda hivyo vitazalisha ajira; kurahisisha upatikanaji wa vifaa na huduma za TEHAMA kuendana na mahitaji na mazingira yetu; kuongeza mapato; na kuwahudumia wateja wa nchi za jirani na Tanzania.


Mhe. Ngoyen Bac Son alisema kuwa Serikali ya Vietnam iko tayari kuendeleza ushirikiano baina ya Serikali yao na ya Tanzania ya kuendeleza Sekta ya Mawasiliano;  na sekta ya kukuza Uchumi na Maendeleo ya Tanzania kama alivyozungumza Rais wa Vietnam. Pia aliongeza kuwa, “Serikali ya Vietnam iko tayari kuleta kampuni za kuwekeza Tanzania kwa kuanzisha Kiwanda cha vifaa vya mawasiliano kwa ajili ya kuwapatia watanzania huduma za mawasliano na ni matarajio yetu kuhakikisha kuwa ni kiwanda kikubwa ambacho kitahudumia na wateja wa nchi za jirani na Tanzania”. Aidha, Mhe. Ngoyen Bac Son aliongeza kuwa Serikali ya Vietnam inaridhia kusaini Mktaba wa Ushirikiano baina ya nchi hizo na amewakaribisha wafanyabiashara na kampuni za Tanzania kwenda kuwekeza nchini Vietnam.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

MAKATIBU WAKUU NA NAIBU WAMEWATAKIWA KUFANYA KAZI KWA MUJIBU WA SHERIA NA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA-BALOZI KIJAZI

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
KATIBU Mkuu Kiongozi, Mhadisi  Balozi  John Kijazi amesema makatibu wakuu na manaibu wafanye kazi kwa mujibu sheria na waishi kama viongozi wa umma katika maisha.

Katibu Mkuu Kijazi ameyasema hayo leo wakati wa mafunzo maadili ya viongozi wa Umma kwa Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam,amesema kuwa kama sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma ina matatizo ya utekelezaji wa kisheria kwa viongozi wa umma serikali iko tayari kuyarekebisha.

Amesema mafunzo kwa viongozi wa umma ni muhimu katika kupunguza masuala ya rushwa pamoja na ubadhirifu wa mali za umma.
Aidha amesema kuwa makatibu wakuu na manaibu wafanye kazi kwa kutenda haki kwa waliochini yao  kutokana na maadili ya utumishi  wa umma.

Nae Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada zinazofanyika hivi sasa za kukuza na kuinua kiwango cha uwajibikaji na maadili katika utumishi wa Umma kutokana na maadili ya taifa ni moja ya tunu taifa muhimu inayotambulisha Taifa.

Angellah amesema mafunzo waliopata yawe ni chachu ya kasi ya kujenga na kukuza maadili katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Amesema watendaji wakuu wanatakiwa kuwa mfano bora  na wa kuigwa kwani serikali imechukua hatua mbalimbali ili  kuongeza  mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa na ukosefu wa maadili hususani miongoni mwa viongozi wa umma. 
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images