Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

Dk. Kigwangalla azindua utoaji wa hati za viwanja kwa Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla leo 6 Machi amezindua rasmi utoaji wa viwanja kwa wanawake wa Mkoa wa Dar Es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo pia katika Mkoa wa Dar es Salaam maadhimisho hayo yakianza rasmi hiyo leo hadi hapo kilele 8 Machi katika viwanja vya Biafra.

Ambapo Dk. Kigwangalla ameelezea kuwa, maadhimisho hayo yanatoa fursa ya kuweza kufanya tathimini ya mafanikio ya kuwawezesha wanawake katika Nyanja mbalimbali na changamoto wanazokabiliana nazo.

Aidha, Dk. Kigwangalla katika tukio hilo,ametoa vyeti kadhaa vya umilikaji ardhi kwa wanawake vilivyotolewa na benki ya wanawake Tanzania (TWB. Pia amewaagiza maafisa maendeleo ya Jamii nchini kuhakikisha wanashinda kwenye jamii na kubaini kero na changamoto hasa wanazokumbana nazo wanawake na si kukaa maofisini ilikutoa hali na motisha kwa jamii ambayo asilimia kubwa imesahulika ikiwemo kufika ama kushiriki kwenye matukio kama hayo ya maadhimisho.

Dk. Kigwangalla hakufurahishwa na kitendo cha ushiriki mdogo wa wanawake katika shughuli hiyo huku maafisa wa maendeleo ya kijamii wakiwa ndio wenye jukumu lao na hawajachukua hatua yoyote ya kufanya hivyo katika kuwafikia wananachi na hata kuwaalika katika tukio kama hilo.

D. Kigwangalla ambeye alikuwa mgeni rasmi, pia aliweza kutembelea mabandambalimbali na kupata maelezo ya mabanda hayo ambayo asilimia kubwa yalikuwa ni ya wanawake mmoja mmoja na wale wa kwenye vikundi.
Dk. Kgwangalla akiwa meza kuu na viongozi wengine katika tukio hilo leo 6 Machi katika viwanja vya Biafra. 
Dk. Kigwangalla akihutubia kwenye mkutano huo..

Dk. Kigwangalla akitoa hati kwa moja wa wanawake hati ambazo zimetolewa na benki ya wanawake Tanzania (TWB).


MICHUZI TV: MTANANGE WA YANGA NA AZAM

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AENDELEA NA ZIARA MKOANI SIMIYU

$
0
0






Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akikagua jengo la matibabu ya wazee baada ya kulizindua kwenye hospitali ya Wilaya ya Meatu iliyopo Mwanhuzi akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na watumishi wa serikali katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Metu akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipoingia kwenye uwanja wa Stendi ya Mwanhuzi wilayani Meatu kuhutubia Mkutano wa hadhara Machi 5, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipoingia kwenye uwanja wa Stendi ya Mwanhuzi wilayani Meatu kuhutubia Mkutano wa hadhara Machi 5, 2016.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Erasto Mbwilo.

BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

SERIKALI YAANZISHA MFUMO WA 
MALIPO KWA WATUMISHI WA UMMA


SERIKALI imeanzisha mfumo wa Kielektroniki wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao unalenga kuondoa tatizo la madai ya malimbikizo ya stahili zao.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana (Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa sekta mbalimbali  katika wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu alisema mfumo huo ujulikanao kama LAWSON, unatumika kwenye ajira za watumishi wote nchini, wa Serikali Kuu na wale wa Serikali za Mitaa  
Waziri Mkuu alisema mfumo huo unasaidia kutunza, kutuma na kuhuisha  taarifa za watumishi kwa wakati na kwa ufanisi tangu mtu anapoajiriwa hadi inapofikia wakati wa kupandishwa madaraja na hadi anapostaafu.


Kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo, maafisa utumishi walipaswa kukusanya taarifa za watumishi wote walioajiriwa na kuzipeleka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ili zikathibitishwe kabla ya kuzipeleka HAZINA kwa maandalizi ya mishahara. 
Akitolea mfano wa kada ya ualimu, Waziri Mkuu alisema ajira za walimu zilikuwa zinaanzia Idara ya Utumishi wa Walimu  (TSD)  lakini anapaswa aende kuripoti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  (DED) ambaye ni mwajiri wake chini ya TAMISEMI. "Hii ilileta ugumu wa malipo ya kupanda madaraja, uhamisho ama likizo kwa sababu mwajiri anakuwa hajatenga hizo fedha."
"Sasa hivi tuna Tume ya Utumishi wa Walimu  (TSC) ambayo iko chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. Kwa hiyo ni rahisi wao kukaa pamoja na kuamua tuwapandishe daraja walimu 10 na wote hao wakalipwa bula bila kuchelewa," alisema.
Alisema mfumo huo umeanza kutumika tangu mwaka 2012 na ulianza kwa ajira mpya za wakimu na hadi sasa umethibitisha kuwa inawezekana kumlipa mtumishi mshahara wake hata kama ameajiriwa ndani ya mwezi huohuo.
"Kama mtumishi anaripoti kwenye kituo kipya hata iwe wilaya ya wapi ili mradi amefika na barua zake zote na ziko sahihi mtu huyu ataingiziwa taarifa zake na wakati huohuo taarifa zitaonekanaOfisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na pia zitapokelewa kwa maafisa wanaoshughikia mishahara kule HAZINA."
Alisema changamoto pekee waliyokutana nayo wakati mfumo huo umeanza ilikuwa ni kutoingizwa taarifa za wale ambao wameripoti baada ya tarehe 10 ya mwezi husika. "Hii ni kwa sababu matayarisho ya mishahara yanakuwa yameshaanza. Kwa hiyo wengi walishauriwa kuripoti kati ya tarehe 25 hadi tarehe 9 ya mwezi uliofuata na wote hawa hawakupata matatizo ya kucheleweshewa mshahara," alisema.
Akifafanua kuhusu upandishaji madaraja ya watumishi, Waziri Mkuu alisema  Serikali imeondoa utaratibu wa mtumishi kulazimika kuandika barua ya kukiri kupandishwa daraja/cheo ndipo aanze kupata stahili zake mpya. "Hii imeondoa ucheleweshaji wa kufanyika marekebisho ya mshahara  na pili imeondoa tofauti za mishahara kwa watumishi wenye ngazi moja (sifa sawa za kitaaluma, tarehe moja ya kuajiriwa) ambao walikuwa wakilipwa tofauti kwa sababu mmoja aliwahi kuandika barua ya kukiri na mwingine alichelewa kuandika barua hiyo hiyo " alisema

AKATISHA ZIARA KUTOKANA NA MSIBA
Wakati huohuo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amelazimika kukatisha ziara ya mkoa wa Simiyu ambayo ilikuwa imalizike kesho kutokana na msiba wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambayo alipangiwa kuitembelea leo.
Mkurugenzi huyo Bw. Traceas Kagenzi alifariki dunia usiku wa kuamkia jana kutokana na shinikizo la damu. Atasafirishwa kwenda Muleba  kwa mazishi.

Akitoa salamu za rambirambi kwenye ibada ya kumuombea marehemu Kagenzi iliyofanyika nyumbani kwake Maswa mjini, Waziri Mkuu alisema ameshtushwa na msiba huo uliotokea ghafla na kwamba Taifa limempoteza mtumishi mahiri ambaye bado Taifa lilikuwa likimtegemea.

"Nimeshtushwa sana na taarifa za msiba huu. Nimeambiwa hadi juzi usiku alikuwa akishirikiana na Mkuu wa Wilaya hii kuandika taarifa ya ziara ya wilaya hii. Kwa niaba ya Serikali, ninawapa pole sana wafiwa na Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi," alisema.


"Nimelazimika kukatisha ziara ya mkoa 
huu kwa sababu huyu ni mtumishi mwenzetu" alisema Waziri Mkuu.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, MACHI 6, 2016.


DKT. SHEIN AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI YA MZEE HAMID AMEIR MUASISI WA MAPINDUZI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine na wananchi wakibeba jeneza la Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya kuswaliwa leo wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitia udongo katika kaburi la Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya kufariki jana katika hospitali ya Mnazi Mmoja na kuzikwa leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine na wananchi wakiitikia dua iliyoombwa baada ya kuzikwa Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja.

Kampuni ya mitindo yapata mwekezaji

$
0
0
KAMPUNI ya inayojishugulisha na masuala ya mitindo nchini Blackfox Modeling Agency imeahidi kuwaendeleza vijana zaidi katika fani hiyo baada ya kupata mwekezaji mpya kutokea nchini Uingereza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa utiaji wa saini wa mkataba wa makubaliano na mwekezaji huyo, mmiliki wa Blackfox Aj Mynah alisema kuwa hatua hiyo itafungua milango ya wanamitindo wa Tanzania nje ya nchi.Alisema kuwa mkataba huo unalenga kuiongezea nguvu zaidi kampuni ya BlackFox katika harakati zake za kuiendeleza fani ya mitindo nchini na kuifanya kuwa ya kimataifa zaidi.

“Kama inavyofahamika kuwa fani hii ya mitindo nchini sio kongwe sana ikilinganishwa na nchi nyingine hivyo basi makubaliano haya yanalenga kuifikisha kampuni ya Blackfox kuwa ya kimataifa zaidi inayoweza kusaidia mamilioni ya vijana sio tu hapa nchini bali hata nje ya Tanzania” alisema Aj.

Aliongeza kuwa kampuni hiyo inalenga kufungua milango nchi nyingine za Afrika Mashariki, Afrika na hata kwenda katika nchi za Ulaya na Amerika.Alisema kuwa kampuni hiyo imewandaa vijana wengi kuingia katika fani ya mitindo na kujiajili kama wanamitindo, matangazo na mengineo mengi.Alisema kuwa chini ya mkataba huo wanamitindo wa hapa nchini wataweza kwenda kufanya kazi katika nchi za Ulaya na kwengineko.

Kwa upande wake mwekezaji huyo David Johansson alisema kuwa ameamua kuingia mkataba na Balck fox kutokana na fursa zilizopo hapa nchini kupitia fani hiyo.Alisema kuwa Tanzania inao wadada na wakaka ambao wanaweza kutangaza matangazo mbalimbali ya kimataifa na hata kufanya kazi nyingine zinazoendana na fani hiyo.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Blackfox Models Aj Mynah akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kumpata muwekezaji ambae atawezesha kufungua ofisi itakayokuwa na sehemu ya kupigia picha na kufungua ofisi kwenye nchi nyingine mwaka ujao,katika mkutano uliofanyika leo jijini Daer es Salaam kushoto ni mwekezaji huyo David Johansson.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Blackfox Models Aj Mynah na mwekezaji huyo David Johansson wakisani mkataba katika mkutano uliofanyika leo jijini Daer es Salaam.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Blackfox Models Aj Mynah akimkabidhi tishet mwekezaji huyo David Johansson leo jijini Daer es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Blackfox Models Aj Mynah na mwekezaji huyo David Johansson wakiwa katika picha ya pamoja na Models leo jijini Daer es Salaam.

TAASISI YA WIPA YAJA NA SULUHISHO UWAJIBIKAJI KATI KUPUNGUZA MIGOGORO KATI YA SERIKALI NA WANANCHI

$
0
0
Na Chalila Kibuda,
Globu ya Jamii 
 SERIKALI imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa kutowajibika ipasavyo kwenye matatizo yao kutokana na kutokuwepo kwa kiunganishi cha moja kwa moja kati ya wawakilishi na wanaowakilishwa. 
Hayo amesema leo Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Fikra ya Uwajibikaji Nchini (WIPA), Ludovick Utouh wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kutokana na kiunganishi nchi nyingi zimeingia katika migogoro kati ya wananchi na serikali zao yanayosababishwa na maamuzi ambayo yanaathiri maisha yao. 
Amesema kuwa kuwa taasisi hiyo imeanzishwa kwa ajili ya masuala ya uwajibikaji na utawala bora kwa kufungua mlango utakaochochea na kuongeza uelewa mpana wa dhana ya uwajibikaji na utawala bora nchini. 
“Kuwezesha Wananchi Kushiriki Kikamilifu Kwenye Masuala ya Uwajibikaji na Utawala Bora Katika Usimamizi wa Rasilimali za Umma” amesema Utouh 
 Amesema uhamasishaji wa wananchi kwenye ushiriki katika masuala ya uwajibikaji na utawala bora ni jambo la msingi katika kuhakikisha maendeleo yaliyopatikana katika utekelezaji wa dhana hii yanakuwa endelevu. 
 Aidha amesema jitihada za kuimarisha uwajibikaji nchini zilitaachiwa Bunge na taasisi za usimamizi za serikali peke yao, uwezekano wa kufanikisha utekelezaji huu utakuwa ni mdogo kwa sababu suala la uwajibikaji linahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali ili kuleta tija kwa taifa. 
 Ludovick Utouh Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) – Mstaafu kwa kushirikiana na aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Mafuta nchini (TPDC),Yonna Killagane waliona hitaji la kuanzisha Taasisi-Fikra ya Usimamizi isiyo ya kiserikali itakayomilikiwa na wananchi wenyewe ambayo itahusika na uchambuzi wa mfumo na masuala ya uwajibikaji na utawala bora nchini. 
 Amesema wameandaa mkutano wa kwanza wa kimataifa utakaohusu uwajibikaji katika sekta ya gesi asilia na mafuta kwa kuzingatia umuhimu wa sekta hii kwenye maendeleo ya nchi utakaofanyika kuanzia Aprili 11 hadi 12 Aprili 2016 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere 
 Amesema wazungumzaji katika mkutano huo ni nchi ambao ni pamoja na, Al Kassim Mtaalam wa mafuta na gesi kutoka Norway, Prof. Patrick Lumumba kutoka Kenya, Bw. Lai Yahya kutoka Nigeria; kwa upande wa Tanzania ni pamoja na Mtendaji Mkuu wa TWAWEZA, Aidan Eyakuze, Dk Abel Kinyondo kutoka REPOA na Prof. Honest Ngowi wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wajibu,  Ludovick  Utouh akizungumza na wadishi wa habari jijini Dar ers Salaam jana.Kushoto ni Afisa mahusiano Hassan Kisena. 

BREAKING NYUZZZZ.....: BALOZI KIJAZI ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI, BALOZI SEFUE KUPANGIWA KAZI NYINGINE

$
0
0

Katibu Mkuu Kiongozi mpya,
Balozi John William Kijazi.

BABA WA KAMBO- WIMBO ULIOMPA WAKATI MGUMU KAMANDA RAS MAKUNJA NA KIKOSI CHA NGOMA AFRICA BAND

$
0
0
Hakuna kazi isiyokuwa na ugumu,watunzi na waimbaji wa muziki nao wanakumbana na ugumu katika kazi zao,mmoja wao kati ya wanamuziki wanaopata misuko suko kazini ni mwanamuziki nguli Ebrahim Makunja almaarufu Kamanda Ras Makunja mkuu wa kikosi cha Ngoma Africa band aka FFU wenye maskani yao kule Ujerumani.

Mwanamuziki mtanzania Kamanda Ras Makunja, mtunzi,mshairi na mwimbaji aliyepindia akili kazi yake, ametunga na kuimba nyimbo nyingi zenye utamu na uchungu,lakini katika nyimbo zote wimbo wa "Baba wa Kambo" ni wimbo uliompa wakati mgumu sana,mara tatu kutafutwa na bakora na wazee walioguswa na wimbo huo, akiwamo mtu mzima Malumba Kassongo alishawahi mara mbili kuvamia kambi ya bendi hiyo kwa bakora na kudai kuwa kamanda Ras Makunja lazima atiwe adabu kwani mdomo wake si mzuri, mzee huyo amedai mtunzi wa nyimbo hiyo "Baba wa Kambo" amekuwa akiyachunguza maisha ya mzee huyo.

pamoja na makubaliano mbele ya wapatanishi kuwa nyimbo hiyo isiende hewani lakini bendi hiyo imekiuka makubaliano na kurusha hewani tena song hilo "Baba wa Kambo" jiburudishe na song hilo chini.

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: Safari Sound Band - Mama lea mtoto wangu

MAMA JANET MAGUFULI,AKIKABIDHIWA CHAKULA NA PANELI ZA SOLA KATIKA KITUO CHA WAZEE BUKUMBI MWANZA

$
0
0
WAZEE na walemavu wa viungo wanaoishi katika mazingira magumu katika kambi ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi mkoani hapa, wamekumbukwa kwa kusaidiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Milioni 54.

Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo ilifanyika jana mbele ya mke wa Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli katika kambi hiyo yenye watu wenye mahitaji mbalimbali ya kijamii.

Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alivitaja vifaa vilivyotolewa kuwa ni Mchele tani 6, Unga wa mahindi 6, Maharagwe tani 3, Sukari tani 2 na nusu na mafuta ya kula lita 1000.

Dk. Kimei alitaja vifaa vingine vilivyotolewa katika kambi hiyo ya wazee kuwa ni pamoja na umeme wa jua na kudai kwamba hatawataishia hapo wataendelea kutoa misaada ikiwemo kukarabati majengo ya makazi hayo.

Kwa upande wake, Janet Magufuli, alisema kuwa katika kipindi kichache alichozunguka katika kambi 17 nchini alikuta kambi hizo zinakabiliwa na changamoto nyingine ikiwemo ya maladhi.

Alisema kuwa hali hiyo ilisababisha kuanza kutafuta wadau mbalimbali ikiwemo benki hiyo ambayo ilichukua jukumu hilo la kuwasaidia watu hao, wanaokabiliwa na changamoto nyingi.

Kambi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1974 kwa sasa ina zaidi ya Wazee 100, kwa muda mrefu sasa watu hao wamekuwa ni omba omba katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza.

Vitu hivi endapo kama havita chuchukuliwa hatua na kuwasaidia yanaweza kuwasababishia magonjwa mbalimbali, sasa nilazima wadau wengine wajitokeze kusaidia kambi hizi, alisema mama Magufuli.
Mke wa Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli (wa pili kulia) akikabidhiwa sehemu ya misaada mbalimbali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, kwa ajili ya kusaidia kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
Mke wa Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli, akiwahutubia wananchi wakati wa hafla ya kukabidhi misaada kwenye kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza. 

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

MFANYABIASHARA WA UTALII ARUSHA ATOA MISAADA YA KIJAMII HOSPITALI MKOA WA ARUSHA

$
0
0
Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet Mfuko akimkabidhi shuka mganga mkuu mfawidhi wa hospital ya mt.Meru dr.Jackline Urio alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa jana.
Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet Mfuko akimuombea mgonjwa Frida Shayo alipotembelea hospitali ya mt.Meru alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa jana. 


Mkurugenzi Viola Mfuko anamlisha keki Habibya Fadhili alipotembelea hospital ya mt.Meru alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa jana.

INTRODUCING Heri Muziki - Na Gode (Yemi Alade Cover)

Zuriels First Film Workshop for Youths - NAMIBIA

$
0
0
Sponsored by Hilton Hotel, Air Namibia and Bank Windhoek, world renowned Girl Education Advocate and the World's Youngest Film Maker - 13 year old Zuriel Oduwole conducted her first ever Film Workshop for youths in Windhoek - Namibia. She spent the day telling her film making story to 25 youths chosen from 255 delegates, who applied from Facebook and Newspaper applications, and teaching them basic film making skills, among other documentary processes.

The highlight of the event was showing a sneak preview of her next film due later in 2016 and shot across 5 countries during the 2014 FIFA World Cup - Brazil, Ethiopia, Nigeria, Mauritius and the US. Zuriels last film "A Promising Africa" released in November 2014 at age 12 showed first across 2 cinema chains in Nigeria, before going on to screen in Ghana, South Africa, London - England and Tokyo - Japan.
She hopes to travel across the continent for more of her education programs, in the future.

VIUMBE WA BAHARINI AINA YA KASA WAKO HATARINI KUPOTEA.

$
0
0
Picha ni mnyama aina ya kasa ambaye anapatikana katika hifadhi ya taifa ya saadani iliopo mkoani Pwani 

Na Woinde Shizza Pwani.
VIUMBE wa baharini aina ya kasa wametajwa kuwa miongoni mwa viumbe wanaoishi katika mazingira hatarishi huku wakitajwa kuwa wako hatarini kupotea duniani kutokana na shughuli za binadamu na mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yamesemwa na mtaalamu wa kasa katika hifadhi ya taifa ya Saadan iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani,Hamis Abdallah wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea katika hifadhi hiyo kujifunza vivutio mbalimbali vinavyopatikana ndani ya hifadhi hiyo.


Akiongea na waandishi wa habari jana mtaalamu huyo alisema ya kwamba baadhi ya wavuvi wamekuwa wakihatarisha maisha ya viumbe hao wanaopatikana kandokando ya bahari ya Hindi inayopakana na hifadhi hiyo kutokana na kuwavua hovyo .

Alisema kwamba kasa huzaliana nchi kavu na ndiyo maana amekuwa akijijengea baadhi ya maadui ambapo aliwataja kuwa ni papa,kenge ambao wamekuwa wakishambulia mayai yao na kutishia uhai wa viumbe hao.

“Kasa wanaishi katika mazingira magumu sana kwa kuwa wanaishi katika kina kifupi cha maji na hivyo baadhi ya wavuvi huwavua hovyo lakini pia wana tabia ya kuzaliana nchi kavu na sio majini”alisema mtaalamu huyo.

Hatahivyo,alisisistiza ya kwamba kutokana na tishio la kutoweka kwa viumbe hao hifadhi ya taifa ya Saadan imechukua hatua za haraka kuhakikisha wanachukua eneo kubwa la bahari ili kuwahifadhi viumbe hao sanjari na kutunza mazingira katika eneo hilo.

Alisema kuwa hifadhi yao kupitia kitengo cha ujirani mwema kimekuwa kikishirikiana na jamii inayoizunguka hifadhi hiyo kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kuhusu kutunza mazingira kwa lengo la kutoathiri mabadiliko ya tabia nchi kwa maslahi ya viumbe hao.

“Tushirikiane kutunza mazingira ili kuhifadhi hawa viumbe wa baharini kwa kuwa wana faida kubwa sana kwa taifa endapo tutaendelea kuwatunza kasa hawa”alisisitiza Abdallah

Hatahivyo,mtaalamu huyo alifafanua kuhusu sheria za utunzaji wa viumbe wanaoishi baharini na kusema kwamba sheria nambari 9 kifungu cha 12 inayohusu utunzaji wa mazingira ya baharini ina sema iwapo mwananchi atahusika na uharibifu wa viumbe walio hatarini kutoweka atahukumiwa kifungo cha miaka mitatu hadi mine.

WAZAZI WAOMBA SEREKALI KUCHUNGUZA KWANINI WATOTO WAO WANAFELI SANA WILAYANI KARATU.

$
0
0
Na Woinde Shizza,Karatu.
WAZAZI wa vijiji vya Kata ya Barai iliyoko Wilayani Karatu Mkoani 
Arusha wameiomba Serikali ya awamu yaa tano kuchunguza sababu za watoto wao kufanya vibaya katika mitahani ya kuhitimu darasa la saba. 

Wazazi hao wametoa kilio hicho kufuatia ufauulu duni wa mara kwa mara kwa watoto wanaohitimu darasa la saba ambapo wanafunzi hao wamekuwa wanahitimu wakiwa hawajui kusoma wala kuandika na kushika nafasi za mwisho kitaifa katika mtihani wa darasa la saba jambo ambaalo wanaliona kama kuwapotezea muda watoto hao ambapo wazazi hao wakiwa wanawaitaji kuwachungisha mifugo. 

Aidha Kata hii ya Barai yenye shule 12 za msingi ambapo kati ya shule hizo shule sita zimefanya vibaya kitaifa na zimeshikilia nafasi za mwisho kabisa kitaifa ambapo alisema shule sita izo zipo katika nafasi za shule kumi zilizofanya vibaya kitaifa katika mtiani wa darasa la saba kwa mwaka jana. 

Mwandishi wa habari hii alitembelea shule tatu za Kata hiyo kujua sababu zinazosababisha kutafaulu kabisa kwa wanafunzi ambapo taarifa zinaonyesha kuwa kuwa shuke hizo zina walimu sita pekee ikiwa na maana kila shule yenye madarasa saba ina walimu wawili 

Wakizungumzia sababu za shule hizo kufanya vibaya mmoja wa mwalimu wa shule ya msingi Gidamilanda Paul Hando alisema kuwa ni pamoja na umbali mrefu ambao wanafunzi wanalazimika kutembea wakija mashuleni ambapo wanatembea zaidi ya kilimeta 24 kwenda shuleni ,pamoja na 
wanafunzi kutumia muda mwingi kuchunga mifugo badala ya kujisomea pindi wanapotoka mashuleni. 

Aidha alibainisha kuwa mbali na tatizo la umbali mrefu pia wanafunzi wamkuwa wakisumbuliwa na tatizo la njaa kwani shule hizo zimekuwa hasipikii wanafunzi mashuleni mchana kutokana na kutokuwa na bajeti hiyo.

Kwa upande wake mmoja wanafunzi hao ambao alijitambulisha kwa jina la Gilony Gitonyi alisema kuwa wamekuwa wanashindwa kusoma kutokana na njaa pamoja na kukosa mda wa kujisomea pindi wanaporudi nyumbani kwani muda mwingi wamekuwa wakiutumia kwa ajili kuchunga mifugo pindi wanaporudi majumbani.

Akizungumzia swala hilo mbunge wa jimbo la karatu Willy Qambalo alisema kuwa kwa upande wake anaona suluhisho la kutatua tatizo hilo ni pamoja na kujenga mabweni ilikuweza kuwasadia wanafunzi kupata elimu ili kila mwanafunzi asome apoapo shuleni ili kuweza kujipatia muda wa kujisomea. 

"unajua kujengwa kwa haya mabweni pia itasiadia kuwapata wanafunzi kirahisi ambao muda wamekuwa wakiacha masomo na kwenda kuchunga mifugo jambo ambalo linapingwa vikali na wazazi wa vijiji hivyo na pia wanafunzi hao watapata muda mrefu wa kujisomea na swala wao kupata njaa litapungua kwani kutakuwa na chakula shuleni kwa ajili yao"alisema Qakambalo

Aidha Tafiti zinaonyesha walimu ,wenye utovu wa nidhamu watoro na walevi katika maeneo ya mijini ndio hupelekwa katika shule hizzo zilizoko maeneo ya porini kama adhabu kwao.Swali la kujiuliza je mwalimu huyu atakuwa na nia ya kuwafundisha wanafunzi?Kupelekwa kwa mwalimu huyu kama adhabu badala ya eyey kuridhia Kujua kusomaa na kandika kwa wanafunzi hawa itakuwa ni ndoto.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMPA POLE RAIS MSTAAFU.

$
0
0
Waziri Mkuu Majaliwa na mkewe Mary wakimpa pole  Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mkewe Salma (kushoto) wakati walipokwenda nyumbani kwao jijini  Dar es salaam kuhani msiba wa kaka yake Rais Mstaafu Marehemu  Selemani Mrisho Kikwete leo.
 (Picha n ofisi ya Waziri Mkuu).

MAJALIWA AKABIDHI ZAWADI YA LAPTOP KWA MSHINDI WA TATU WA MASHINDANO YA INSHA AFRIKA YA MASHARIKI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Said Jabir wa Shule ya Mbekenyera  wilayani Ruangwa,  zawadi ya Laptop baada ya kuwa   mshindi wa tatu katika mashindano ya uandishi wa Insha kwa nchi za Jumuiya ya  Afrika ya Mashariki. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 7, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Said Jabir zawadi ya Laptop baada ya kuwa mshindi wa tatu katika mashindano ya uandishi wa Insha kwa nchi za Jumuiya ya  Afrika ya Mashariki. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam leo Kushoto ni  Shannel Nchimbi, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mbekenyera wilayani Ruangwa alikosoma mwananfunzi huo,  (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema shule za sekondari za kata zina fursa ya kufanya vizuri kama zilivyo shule nyingine licha ya kuwa watu wengi wamekuwa wakizidharau.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Machi 7, 2016) wakati akikabidhi zawadi ya kompyuta mpakato (laptop) kwa mwanafunzi aliyeshinda shindano la kuandika insha katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC ). Kompyuta hiyo ina thamani ya sh. 1,992,000/-.


Mwanafunzi huyo, Jabir Mandando (20),  amehitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Mbekenyera iliyoko wilayani Ruangwa mkoani Lindi. Amepata ufaulu wa daraja la pili na sasa anasubiri matokeo ya kujiunga na kidato cha tano. Lakini aliandika insha hiyo mwaka jana wakati akiwa kidato cha nne.

"Huyu ni mtoto wa kijijini tu. Anatoka kijiji cha Namilema wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi. Shule ya Mbekenyera aliyosoma ni shule ya kata. Ameweza kushinda tuzo na kushika nafasi ya tatu katika shindano lililoshirikisha shule nyingi za Jumuiya ya Afrika Mashariki."

"Jabir ameweza kuchomoza kitaifa kwa kushiriki shindano la kimataifa. Nimeamua kumpa zawadi ya laptop pamoja na begi lake ili aweze kujisomea  zaidi na kupata elimu ya masuala mbalimbali kwa kutumia kompyuta hii. Pia nataka iwe ni chachu kwa vijana wengine kushiriki mashindano kama haya," alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu pia alikabidhi Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Shanael Nchimbi fedha taslimu sh. 500,000/- zikiwa ni zawadi kwa ajili ya shule hiyo. mwalimu Nchimbi alimsindikiza mwanafunzi huyo Arusha kupokea zawadi hizo kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliomalizika Arusha wiki iliyopita.

Kwa upande wake, kijana Jabir alisema anashukuru sana kwa zawadi aliyopewa na kuahidi kuwa atajitahidi kusoma kwa bidii masomo ya kidato cha tano na sita ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa daktari.

Alipoulizwa alipataje taarifa ya uwepo wa shindano hilo, Jabir alisema: "Walimu walipata taarifa wakazileta darasani na kutuambia tushiriki kuandika. Walizikusanya na kuchagua tatu bora, ndipo yangu ikashinda."
Amesema insha aliyoiandika ilihusu: "The importance of political stability in the East African Integration."

Alimwonyesha Waziri Mkuu cheti na dola za Marekani 200 ambavyo alipewa zawadi kutokana na ushindi huo. Shule ya Mbekenyera ambayo alikuwa akisoma, pia ilizawadiwa laptop na printer kutokana na ushindi wa kijana Jabir.

Mshindi wa kwanza katika shindano hilo ametoka shule ya Sekondari Mzumbe, mshindi wa pili  alitoka Kenya na wa tatu alitoka shule ya Mbekenyera. 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
JUMATATU, MACHI 7, 2016.

kampuni mpya ya huduma za tiketi za ndege pamoja na Utalii ya SkyPalm Travel yazinduliwa

$
0
0
BALOZI wa Uturuki nchini Yesemin Eralp amezindua kampuni mpya ya huduma za tiketi za ndege pamoja na Utalii ya SkyPalm Travel and Tour Ltd.

Tukio hilo lilitokea jumamosi hii hapa jijini ambapo balozi huyo alitoa wito kwa wawekezaji zaidi kujitokeza kuwekeza kwenye sekta hiyo.

Alisema kuwa Tanzania imekuwa ikifanya vema kwenye sekta ya utalii huku ikiwa na vivutio vingi vya utalii vinavyovutia zaidi na kuwavutia watalii kutokea nchi mbalimbali. Aliongeza kuwa wageni kutokea nchi mbalimbali duniani wanahitaji huduma kutokea kwa kampuni bora zaidi itakayowahudumia kwa ufanisi na umakini.

Kwa upande wake Mkuu wa Biashara wa kampuni hiyo Meysun Buyuksarac alisema kuwa kampuni hiyo imelenga kuimarisha utoaji bora wa huduma za usafiri wa ndege pamoja na utalii nchini.

Alisema kuwa Tanzania inazo fursa nyingi za utalii ambapo zimekuwa zikipelekea wageni wengi kujitokeza kuja nchini kutalii, na hivyo kupekekea wageni kutokea nje ya kuja kwa wingi na wao kama kampuni wamejipanga kutoa huduma bora zaidi ili kukidhi uhitaji.
sky palms launch-153
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Yesemin Eralp akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi kampuni mpya ya huduma za tiketi za ndege pamoja na Utalii ya SkyPalm Travel and Tour Ltd.
sky palms launch-146
Mkuu wa Biashara wa kampuni mpya ya huduma za tiketi za ndege pamoja na Utalii ya SkyPalm Travel and Tour Ltd, Meysun Buyuksarac akizungumza katika hafla hiyo.
sky palms launch-51
sky palms launch-147
Baadhi ya Wageni waalikwa.

Muhongo auagiza mgodi wa MMG kuanza uzalishaji

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Seka na wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa MMG Gold Mine Ltd mara baada ya kuwasili mgodini hapo
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya dhahabu ya MMG Gold Mine Ltd, Harrison Abraham (kulia).
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akikagua mgodi wa dhahabu wa MMG Gold Mine Ltd. Kushoto ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Harrison Abraham (kulia).
Baadhi ya mitambo ya kuchenjulia dhahabu iliyopo katika mgodi huo wa MMG Gold Mine Ltd uliopo katika kijiji cha Seka, wilaya ya Musoma.

Serikali imetoa miezi minne kwa mgodi wa dhahabu wa MMG Gold Ltd uliopo katika kijiji cha Seka wilaya ya Musoma kuanza uzalishaji vinginevyo itafutiwa leseni.

Agizo hilo limetolewa hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipofanya ziara mgodini hapo kwa lengo la kujionea shughuli zinazoendelea katika mgodi huo.

Awali Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Mashariki, Mhandisi Juma Sementa alisema leseni ya mwanzo kutolewa kwa mgodi huo ilikua mwaka 2002 ambapo Kampuni ya awali ilikuwa JMG Exploration Co. Limited ambayo ilifanya utafutaji wa madini kuanzia mwaka 2002 hadi 2005.    

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live


Latest Images