Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1148 | 1149 | (Page 1150) | 1151 | 1152 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (pili kulia) akiwasilia katika uwanja wa Ndege wa Arusha tayari kushiriki kikao cha Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Mabunge Wanachama wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa Region) Jijini Arusha
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifungua kikao cha 70 cha Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Mabunge Wanachama wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa Region) kilichofanyika Jijini Arusha jana.
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kikao cha 70 cha Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Mabunge Wanachama wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa Region) kilichofanyika Jijini Arusha jana. Kikao hicho kinahudhuriwa na Maspika kutoka Uganda, Mauritius, Siera Leone, na Wabunge wanaowakilisha Mabunge yao barani Afrika katika Umoja huo.

  0 0

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa umoja huo Seleman Kirungi na kusho ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) Dkt. Ernesta Mosha.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (mwenye miwani) akisikiliza maelezo kuhusu mwandishi wa Fasihi Hayati Sheikh Amri Abeid Kaluta kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni _Sehemu ya Lugha Bibi. Shani Kitogo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) leo jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amezindua vitambulisho vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wakitoka nyumbani kwenda kazini.

  Katika hatua nyingine Makonda ameziomba sekta mbalimbali nchini kushiriki katika kutoa mawazo yao ya maendeleo ili taifa lizonge mbele badala ya kuwa watizamaji.

  Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam jana mbele ya wazazi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Turiani wakati akizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu wa wilaya yake kupanda daladala bure kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia  walimu hao.

  "Nawaomba watanzania na sekta mbalimbali kuwa na mawazo ya maendeleo ambayo yatawekwa mezani na kuyafanyia kazi jambo litakalo msaidia Rais wetu Dk.John Magufuli katika kuliinua taifa kiuchumi badala ya kumuachia kila kitu akifanye yeye" alisema Makonda.

  Makonda alitoa mwito kwa makondakta wa daladala kutoa ushirikiano kwa walimu hao kesho wakati watakapoanza kupanda magari yao huku wakijua walimu ndio waliowafundisha na kufikia hatua hiyo ya kazi walizonazo.

  Ofisa Elimu wa Sekondari wa Wilaya hiyo, Rogers Shemwelekwa aliwaomba wananchi hao na walimu kuendelea kuunga mkono jitihada za Makonda za kuwaletea maendeleo na kumuombea kwa mungu badala ya kumbeza kwani kazi hizo anazozifanya ni kwa ajili ya wananchi.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akimvika kitambulisho Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani, Beatrice Mhina Dar es Salaam leo asubuhi, baada ya kuvizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wa kwenda kazini kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia walimu hao.
  DC Makonda akimfika kitambulisho Mwalimu Gideon Mwenenyi.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wananchi na walimu wakati wa uzinduzi wa vitambulisho hivyo.


  0 0


  0 0
  0 0

  Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema amesikitishwa na matokeo ya Kidato cha Nne katika jimbo lake na kusisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za haraka ili kukomesha hali hiyo.
  Aliyasema hayo hivi karibuni katika kijiji cha Murangi, Mkoani Mara kwenye hafla ya kukabidhi gari la kisasa la wagonjwa la Kituo cha Afya cha Murangi.
  Alisema shule za Serikali jimboni humo zimetia aibu kwani matokeo yao hayaridhishi na sio ya kujivunia na huku akisisitiza hatua za haraka zinahitajika ili kubaini chanzo cha tatizo hilo la wanafunzi wengi kufanya vibaya kwenye mitihani yao.
  Kufuatia hali hiyo, Profesa Muhongo aliagiza wasaidizi wake watano ambao waliajiriwa mapema mwaka huu maalum kwa kafuatilia shughuli za jimbo kutembelea shule zilizopo kwenye maeneo yao na kuzungumza na wakuu wa shule hizo na kumpatia taarifa.
  Aliagiza wakutane na wakuu wa shule zote zilizomo jimboni humo na kila mkuu wa shule aeleze sababu za kuwa na matokeo mabaya ya mitihani iliyopita ya kidato cha nne.
  “Hawa vijana nimewaajiri kufuatilia shughuli za jimbo na kwa kawaida kila wiki wananiletea taarifa za masuala mbalimbali ya kimaendeleo ambayo ninatekeleza ili kuelewa kuhusu utekelezaji wake,” alisema.
  Alisema binafsi anaelelewa baadhi ya sababu zinazochangia wanafunzi kufanya vibaya lakini ametoa agizo hilo la kupata maelezo ya wakuu wa shule ili kujiridhisha zaidi.
  Mbali na hilo, Profesa Muhongo aliwalaumu madiwani jimboni humo kwa kushindwa kufuatilia suala la elimu. “Madiwani hii ni kazi yenu, haiwezekani tumepata matokeo mabaya na hadi leo hii hamjaitisha kikao kujadili.”
  Aliagiza kwamba taarifa husika ikamilike ndani ya mwezi mmoja na baada ya kupatiwa taarifa hiyo alisema ataitisha mkutano maalum wa elimu ili kuijadili.
  Alisema endapo kutathibitika kuna wanaosababisha hali hiyo ya matokeo mabaya kwa namna yoyote ile watu hao itabidi wapewe adhabu.
  Alisema inawezekana baadhi ya wazazi pia kwa namna moja ama nyingine wanachangia vijana kupata matokeo mabaya. “Hadi sasa kwa taarifa nilionayo kuna vijana 224 wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza lakini hadi hivi sasa hawajajiunga; na madiwani mpo tu mnatazama bila kuchukua hatua na mnaona ni kawaida,”
  Aliagiza kupatiwa majina ya wazazi wote waliogoma kuruhusu watoto wao kuendelea na masomo na vilevile yapelekwe kwa Mkuu wa Wilaya. “Nataka hili lifanyike ndani ya wiki moja na watoto wote wawe wameenda shule.”
  Vilevile Profesa Muhongo alisema suala alilogundua ni kwamba wanafunzi wengi hawana mazoea ya kujisomea vitabu ili kuongeza uelewa baada ya kutoka shule.
  Alisisitiza umuhimu wa kusoma vitabu badala ya kukariri madaftari ya darasani. “Unakuta motto anatoka shule halafu anasoma daftari aliloandika darasani badala ya vitabu. Ndiyo maana nimewaletea vitabu ili kuwa na uelewa mpana zaidi.”
  Alisema awamu ya kwanza alipeleka vitabu 7,110 vya Sekondari na vitabu 12,800 vya msingi na awamu inayofuata vitabu vitakavyoingia vitakua zaidi ya 25,000 vingi vikiwa ni vya sayansi, hesabu na kiingereza.
  Mbali na hilo, Profesa Muhongo alihoji utendaji wa Halmashauri na kueleza kutoridhishwa na utendaji wake na hivyo aliagiza kufuatiliwa kwa karibu kwa Afisa Elimu wa Halmashauri hiyo.
  “Inashangaza Halmashauri nao wanalalamika sasa kazi yao nini?; Afisa Elimu hafai, tutamfuatilia kwa karibu,” alisema.
  Profesa Muhongo vilevile aliagiza madiwani wote jimboni humo kuacha kuingilia shughuli za watendaji hususan kwenye suala la ukusanyaji wa kodi.
  “Hakuna diwani kukusanya kodi, nyie ni wa kupokea taarifa kujadili na kufanya tathmini; ni utendaji wa hovyo diwani kujihusisha na ukusanyaji kodi. Mliomba udiwani kuleta maendeleo na siyo kutumbua maisha,” alisisitiza.
  Hafla hiyo ya makabidhiano ilihudhuriwa na wananchi mbalimbali wa jimboni humo, wataalamu wa afya wa kituo cha Murangi, wadau wa maendeleo na watendaji wa Halmashauri husika.
   Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maagizo kwa wasaidizi wa Ofisi zake tano za Jimbo.
  Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akifurahia jambo na Mzee Joseph Nyangaga mkazi wa kijiji cha Makojo mara baada ya kumaliza mkutano wake na wananchi wa jimbo la Musoma Vijijini.

  0 0

   Mshambuliaji wa Timu ya Azam, Kipre Tchetche akiwatoka Mabeki wa Timu ya Yanga, Mbuyu Twite na Vicent Bossou, wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliopigwa Jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam. Hadi kipenga cha mwisho kikilizwa na Mwamuzi, Kennedy Mapunda, timu zote zilikuwa zimefungana Bao 2-2 na kuzifanya timu hizo zikiondoka uwanjani hapo zikiwa na Pointi sawa ila Yanga ikiongoza Ligi kwa uwingi wa Magoli ya kufunga.
   Beki wa Yanga, Juma Abdul akiondosha hatari iliyokuwa ikielekezwa langoni kwao na Mchezaji wa Azam, Farid Mussa.
   Mshambuliaji wa Azam, John Bocco akiangalia namna ya kumtoka Beki wa Yanga.
   Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akionyesha umahiri wake wa kumtoka beki wa Azam, Said Morad huku akiwa kadhibitiwa kweli kweli.
   Chukua huyooo....
   Mchezaji wa Azam, Shomari Kapombe akiruka daruga la Beki wa Yanga, Vicent Bossou, wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliopigwa Jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam. Hadi mwisho wa mchezi, Azam 2 - 2 Yanga.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufiwa na kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
  Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufiwa na kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimfariji Mjane wa Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete na wanafamilia, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye kaburi la Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani. Mzee Selemani Kikwete alikuwa kaka mkubwa wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
  Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.


  0 0


  0 0  AIR CARGO TO DAR £4.00 INCLUSIVE CLEARANCE

  AIR CARGO TO DAR £2.00 EXCLUSIVE CLARANCE


  SEA CARGO TO DAR £2.00 INCLUSIVE CLERANACE


  4X4 CARS TO DAR/MBS £850

  SALOON CARS TO DAR/MBS  £720


  40' CONTAINER TO DAR/MBS £1,700

  20' CONTAINERS TO DAR/MBS £1,100


  WE ARE HERE TO MAKE CHANGES ON SHIPPING INDUSTRY


  QUALITY SERVICES AT AFFORDABLE RATES


  CALL US TODAY AT +44 1708524200  
  MOBILE +44 7913376799  UNIT 2 HARBOUR HOUSE, COLDHARBOUR LANE, RAINHAM. RM13 9YB


  0 0

  Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Makete Mh.Noramn Sigalla wakati alipowasili kwenye shamba la Kitulo ambalo ni moja ya Mashamba makubwa ya kufuga Ng'ombe wa kisasa aina ya Mitamba.
  Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo kutoka kwa meneja wa shamba la kitulo kuhusiana na uzalishaji wa Ng'ombe aina ya mitamba.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Makete Ndg.Mh.Mwigulu Nchemba akiwa kwenye shamba la kitulo akipewa maelezo mbalimbali yanayohusiana na kuyumba kwa ufugaji wa ng'ombe kwenye shamba hilo.
  Huwa ni mfano wa Ng'ombe wa kisasa aina ya Mitamba wanaopatikana shamba la kitulo wenye uwezo wa kutoa maziwa lita 15 hadi 20 wanapokamuliwa mara moja kwa kila mmoja.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Abdulaziz Ahmeid, Lindi.

  Kilio cha wakazi wa kata ya kitumbikwera na Msinjahili katika Halmashauri ya manispaa ya lindi cha kukosa usafiri wa uhakika kimepata ufumbuzi baada ya kupatiwa boti na Halmashauri hiyo aina ya faiba ambayo hadi Uzinduzi Imegharimu shilingi Milioni 44 zilizotokana na mapato ya Manispaa hiyo.
  Akisoma taarifa fupi kabla ya uzinduzi wa boti hilo mkurugenzi wa manispaa ya lindi ndugu Jomaary Mrisho Satura alisema lengo kubwa la Halmashauri hiyo kununua boti ni moja ya Njia ya kurahisisha Utoaji wa Huduma kwa jamii zilizo katika kata zilizo Upande wa pili wa bahari ya Hindi katika manispaa hivyo kwa kutambua kero hiyo wameona umuhimu wa kuwapatia usafiri wa uhakika.
  "maeneo yale wapo wanafunzi watumishi mbalimbali ambao wanahitaji huduma hii lakini pia kuna zahanati ambapo kunawakati mwingine kunakuwa na wagonjwa wanaopewa Rufaa ambao wanatakiwa kufikishwa hospital ya rufaa ya Sokoine kwa haraka zaidi isitoshe itasaidia watumishi na wanafunzi kuwahi"alimalizia Satura.
  Kwa upande wake diwani wa kata hiyo ndugu Frank Magali ameishukuru Halmashauri na baraza la Madiwani kwa kupitisha Ununuzi wa boti hiyo licha ya kutoa huduma pia ni moja ya chanzo kizuri cha mapato kwa manispaa yetu huku Tukisubiri Utekelezaji wa Ahadi ya Mhe Rais kutununulia pantoni ili kuharakisha maendeleo na hii inawapa faraja kuona tozo na kodi mbalimbali za Halmashauri zinarudi kwa wananchi kwa kuwahudumia....Alimalizia Magali.
  Akizindua boti hiyo mkuu wa wilaya ya lindi,Yahya Nawanda alisema kuwa boti hiyo ni kwa ajili ya wakazi wa lindi na hasa wa manspaa na kuonyesha Umuhimu wa utoaji wa huduma na kusaidia Jamii,Nawanda ametoa Fursa kwa wanafunzi,Akina mama wajawazito,wagonjwa wenye Mahitaji maalum pamoja na watumishi wa serikali watakuwa wanavuka bure kwa kutumia Boti hiyo.
  Nae bi zahara selemani Ambae ni Diwani wa Kata ya Mikumbi katika manispaa hiyo alisema ni faraja kuona Halmashauri imetambua changamoto inayowakabili Wakazi wa maeneo hayo na kuwapatia boti kwa sababu usafiri kwa kuwa ni muhimu sana ukizingatia hii ni bahari na vinatakiwa vyombo vya usafiri Vinavyomilikiwa na Halmshauri kwa ajili ya kusaidia huduma muhimu kwa wakati wote.
  Boti iliyonunuliwa na Manispaa ya Lindi kwa ajili ya Utoaji huduma na kuongeza mapato ya halmashauri.
  Muundo wa ndani wa boti hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 40.
  Wanafunzi wakiteta na mkuu wa wilaya wakati akifanya uzinduzi wa boti hiyo ikiwemo kumshukuru kwa kuagiza wanafunzi wapande Boti hiyo Bila malipo.
  Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe. Yahya Nawanda akishuka kutoka katika boti hio baada ya kuizindua ili kutoa  huduma za usafiri. Boti hiyo imenunuliwa kwa mapato ya ndani ya Halmshauri.

  0 0
 • 03/06/16--03:22: SHUKRANI
 • DIONICE ANATOLY MFINANGA (1984 – 2016)

  Familia ya Bwana & Bibi Anatoly Henry Mfinanga wa Chanjale, Kisangara, Mwanga Kilimanjaro inapenda kutoa shukrani kwa watu mbalimbali walio fanikisha shughuli nzima ya mazishi ya ndugu yetu mpendwa DIONICE ANATOLY MFINANGA (32) aliye fariki  kwa kuuwawa na majambazi usiku wa kuamkia tarehe 06/02/2016 siku ya jumamosi maeneo ya Survey Dar es Salaam.

  Shukrani zetu ziwafikie ndugu wote upande wa baba na mama hususani shukrani za kipekee ziwandee Baba Hashimu Kiure, Mjomba John Msami na Baba Halifa Katani kwa kutuongoza tangu siku ya tukio tarehe 06/02/2016 nyumbani kwa kaka wa marehemu Ndg. Boniface A. Mfinanga Mbezi kwa Msuguri Dar es Salaam hadi siku ya kusafirisha mwili wa marehemu siku ya jumatatu tarehe 08/02/2016 kwenda nyumbani Chanjale, Kisangara, Mwanga, Kilimanjaro.

  Shukrani ziwaendee pia wanamalezi wote wa Chanjale Seminary katika umoja wao kwa ushirikiano tangu kutoa taarifa ya kifo hadi siku ya mazishi, tunawashukuru Class mate wa marehemu MBA 2015 Mzumbe University kwa ushirikiano wao kupitia wawakilishi wao. Shukrani ziwaendee pia majirani wote wa marehemu wa Kimara Korogwe, wafanyakazi wa Ubalozi wa Afrika Kusini, Tanganyika Arms Ltd, jumuiya ya Mashahidi wa Uganda Rau parokia ya Moshi mjini, Jumuiya ya Mt.

   Petro Parokia ya Mwanga  kwa ushirikiano na michango yao.

  Kadhalika tunapenda kuwashukuru majirani wote mbezi kwa Msuguri nyumbani kwa kaka wa marehemu kwa ushirikiano wao wote wa hali na mali waliouonyesha.

  Tunatoa shukrani zetu pia kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kama mwajiri wa marehemu kwa ushirikiano wa hali na mali walio uonyesha kuanzia siku ya tukio hadi siku ya mazishi.

  Shukrani za kipekee zimuendee Baba Askofu Jacob Venance Koda pamoja na Baba Poroko Samwel J. Lawena Parokia ya Chanjale na team yote ya mapadre kwa kutuongoza katika ibada ya kumsindikiza ndugu yetu Dionice katika nyumba yake ya milele. Shukrani pia ziwaendee majirani wote wa Mwanga na kijijini kwetu Chanjale Kisangara, Mwanga kwa umoja katika kufanikisha shughuli nzima za mazishi.

  Tuanajua ni watu wengi waliojitolea kwa ajili ya kufanikisha shughuli nzima ya mazishi na msiba kwa ujumla hivyo kwa yeyote ambaye hatukumtaja hapa atuwie radhi ila tunathamini sana kile alichkitoa kwa ajili yetu. Kama familia hatuna la kuwalipa ila Mungu aliyewapa Moyo wa kujitolea awabariki sana.

   Zaidi ya shukrani hizo wote tunajua leo tarehe 6/3/2016 ni mwezi mmoja tangu mpendwa wetu Dionice atutoke ghafla, tumebaki na kumbukumbu ya mapenzi yako ya dhati, wema wako tutaukumbuka daima, tutakukumbuka daima kila tutakapolitaja jina lako, kumbukumbu zetu kwako haziwezi kuelezeka, Daima utabaki kuwa mioyoni mwetu tunakuombea upumzike kwa Amani katika maisha yako haya mapya.

  Utakumbukwa daima na Baba yako Anatoly H.J. Mfinanga Mama yako Esther H. Mfinanga, wajomba, shangazi na mama wote, Mama mkwe, shemeji zako, mkeo Catherine, wanao Anatoly na Primi, Kaka zako Boniface, Bruno na Gift, dada zako Bona,Yukunda, Angela, Dorice, Luciana na Anna ndugu, jamaa na marafiki wote.

  “BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE”

  AMEN.

  0 0

  Na Nuru Mwasampeta

  Imeelezwa kuwa mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wa madini katika eneo la Uwaseke wilayani Iramba mkoa wa Singida na kampuni ya Meek Mines umemalizika baada ya Serikali kutoa ahadi ya kutoa  ufumbuzi ndani ya siku Saba. 

  Hayo yamebainika mwishoni mwa wiki baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Merdard Kalemani kufanya ziara katika eneo hilo lenye mgogoro na kusikiliza malalamiko ya pande zote zinazohusika katika mgogoro huo.

  Ilibainishwa kuwa wachimbaji wadogo wa eneo la Uwaseke mkoani humo waliingia ubia na kampuni ya Meek Mines kwa makubaliano ya kampuni husika kutoa ajira kwa wachimbaji wadogo wa eneo hilo lakini makubaliano hayo hayajafanyiwa kazi  kwa kipindi cha miaka minne sasa na kuwafanya wakazi wa eneo husika kukosa kipato.

  Dkt. Kalemani alisema kuwa Serikali itatoa tamko rasmi ndani ya siku Saba litakalowezesha shughuli za uchimbaji kuendelea na hivyo kuchangia pato la taifa kupitia kodi mbalimbali na mrabaha unaolipwa serikalini.

  “Suala la eneo hili kutofanya  uzalishaji kwa kipindi kirefu kumeipotezea Serikali mapato mengi sana hivyo ni lazima suala hili tulitatue haraka iwezekanavyo,” alisema Dkt. Kalemani.

  Kwa upande wake Kamishna wa Madini kanda ya Kati, Sostheness Massola alisema kuwa amefarijika sana kwa ziara hiyo ya Naibu Waziri ambayo imetoa muongozo wa utatuzi wa mgogoro huo.

  “Naibu Waziri tunashukuru sana kwa kufika katika eneo hili kwani mgogoro huu umekuwa wa kipindi kirefu lakini sasa ufumbuzi utapatikana kwani umeshatoa maagizo yatakayotatua mgogoro huo,” alisema Massola.

  Makubaliano kati ya kampuni ya Meek Mines na Uwaseke yalifanyika mwaka 2012 na sasa wananchi wanaomba mkataba huo  kusitishwa ili waendelee na shughuli zao bila kuihusisha kampuni hiyo kama ilivyokuwa awali. 


  0 0


  0 0

  Benki ya CRDB inajivunia mapinduzi makubwa katika sekta ya fedha nchini, iliyoyafanya katika kipindi cha miaka 20 ya uwepo wake, kwa kufanikisha kuwafikishia huduma za kifedha Watanzania walio wengi na haswa walio vijijini, hivyo CRDB kujikuta imetimiza malengo ya kuanzishwa kwake. 

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dr. Charles Kimei, katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi, katika kutathimini mafanikio ya benki ya CRDB kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya Benki ya CRDB.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dr. Charles Kimei, akifanya mahojiano maalum na Mwandishi wa Habari wa Kujitegemea, aliyejikita katika kuandika habari za kimaendeleo, Pascal Mayalla, kuhusiana na maendeleo yaliyoletwa na CRDB Banki katika kipindi cha miaka 20.

  Dr Kimei amesema, miongoni mwa mafanikio makubwa ya kujivunia ya Benki ya CRDB, ni kitendo cha benki hiyo kufanikiwa kutimiza malengo, dira na dhima ya benki hiyo, ambayo ni kufikisha huduma za kibenki kwa Watanzania wengi zaidi hadi vijijini, ambapo lengo hili limetizwa kupitia kwa mawakala wa CRDB waitwao Fahari Huduma waliotapakaa nchi kote hadi Vijijini.

  “Katika mambo mengi ambayo CRDB inajivunia katika miaka hii 20, ni kuingiza mfumo mpya wa kimapinduzi wa kutolea huduma kwa wateja wetu wengi zaidi hadi wa hali ya chini ambao wengi wako vijijini, wamekuwa hawafikiwi na huduma za kibenki, hivyo Lengo na azma ya CRDB ya kuwafikia wateja wengi, limetimizwa. 
  Akinamama wa Kibamba, wakielekea kwenye kituo cha Wakala wa Fahari Huduma wa Kibamba, kupata huduma za kifedha, wakala huo, unaomilikiwa na Bw. Frank Mwalinga na mkewe Mainda, wakati wa ziara za kukagua mafanikio ya miaka 20 ya Benki ya CRDB.


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (Mb.) (kulia), akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya kitaifa ya siku 4 ya Rais wa Vietnam nchini, Mhe.Truong Tan Seng kuanzia tarehe 08 hadi 11 Machi, 2016. Ziara hiyo itakuwa ni ziara ya kwanza ya kuja Tanzania pia Afrika. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga naye akisikiliza kwa makini mazungumzo ya Waziri na Waandishi wa Habari.

  Waandishi wa Habari wakimsikiliza kwa makini Balozi Mahiga (hayupo pichani). 


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na Kampuni ya TRUMARK katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es salaam jana March 05,2016.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wajasiriamali wa Vikundi vya Vikoba kutoka katika taasisi mbalimbali kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani yaliyondaliwa na Kampuni ya TRUMARK katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es salaam jana jioni March 05,2016.


  0 0

  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi apokea Msaada kwa Wahanga wa mafuriko Iringa. Msaada huo ni kutoka Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) ambayo imemkabidhi Mhe. Lukuvi Unga kilo 155, Nguo na viatu balo 2, Sukari kilo 25 na Madftari Boksi 2 kwa ajili ya wahanga wa mafuriko jimboni kwake Isimaani.

  Taasisi ya TGGA ni shirika lisilo la Kiserikali na ni chama cha kujitolea kinachojishughulisha na kuwaendeleza Wanawake pamoja na Watoto wa kike katika maswala ya kijamii na kiuchumi kwa kuwapa elimu na mafunzo.
  Mhe. William Lukuvi akipokea msaada wa Wahanga wa mafuriko Isimani Iringa kutoka kwa Bibi Sawidath Mohamed Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) tawi la Dar es salaam akiwa na Bibi Rose Majuva Kamishna wa Makao Makuu ya Taasisi hiyo (wa pili kulia) na Grace Shaba Naibu Katibu Mkuu TGGA.
  Baadhi ya vitu alivyopokea Mhe. Lukuvi kwa ajili ya wahanga hao vikiwa katika gari ambavyo ni Chakula, Nguo , viatu na Madaftari.
  Bibi Sawidath Mohamed Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) tawi la Dar es salaam akimkabidhi Mhe. William Lukuvi msaada wa Wahanga wa mafuriko Isimani Iringa.
  Mhe. William Lukuvi akiwa na viongozi wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) ofisini kwake.

  0 0

   Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Arusha Mhe. Catherine Magige, leo amekabidhi ofisi ya UWT mkoa wa Arusha ambayo amefanyia ukarabati na kuweka vitu vya thamani iliyogharimu shilingi milioni 6 na nusu. 
   Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Arusha Mhe. Catherine Magige akicheza ngoma na viongozi wa UWT mkoa wa Arusha mara baada ya kukabidhi ofisi ya UWT aliyokarabati kwa gaharama ya shilingi milioni 6.5 ,ambapo ofisi imepakwa rangi ,kuwekwa tiles , viti, meza , amakabati pamoja na TV.
  Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Arusha Mhe. Catherine Magige akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wajumbe wa UWT mkoani Arusha.


older | 1 | .... | 1148 | 1149 | (Page 1150) | 1151 | 1152 | .... | 3272 | newer