Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Maalim Seif awasili Zanzibar leo hii

$
0
0
 
 Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad, amewasili Zanzibar alasiri YA LEO akitokea nchini India na Oman. Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege alilakiwa na viongozi kadhaa wa CUF na baadaye kuelekea kwenye makaazi yake, Mbweni.
  

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA ITILIMA MKOANI SIMIYU

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Maabara katika shule ya Sekondari ya Budalabugija wilayani Itilima akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 4, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Machi 4, 2016. (P:icha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua bwawa la umwagiliaji na maji ya kunywa la kijiji cha Mkoma na Mwalushu wilayani Itilima akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu, Machi 4, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwsalimia wananchi baada ya kukagua bwawa la maji ya kunywa na umwagiliaji la vijiji vya Mkomana Mwalushu wilayani Itilima Machi 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwsalimia wananchi baada ya kukagua bwawa la maji ya kunywa na umwagiliaji la vijiji vya Mkomana Mwalushu wilayani Itilima Machi 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Askofu wa Jimbo la Shinyanga, Liberatus Sangu wakati alipoitembelea shule ya Sekondari ya Mwamapalala wilayni Itirima akiwa katika zira ya mkoa wa Simiyu Machi 4, 2016. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)

SUMATRA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI MADEREVA NA MAKONDAKTA WOTE WATAKAOWATOZA ABIRIA NAULI KUBWA TOFAUTI NA ZILIZOPANGWA

$
0
0

Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi Usafiri wa Majini na Nchi Kavu  (SUMATRA) Mkoa wa Kilimanjaro  kuwafikisha mahakamani madereva wote na makondakta wanaowatoza abiria nauli kubwa tofauti na zilizopangwa na ofisi hiyo.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Afisa Mfawidhi Bw.Tadei Mwita alipokuwa akijibu kero ya mkazi wa mkoa huo kwa njia ya simu iliyotolewa na Gazeti  la Mwananchi Machi 04, mwaka huu,iliyozungumzia  daladala zinazofanya safari zake kati ya Moshi Mjini - Himo kuwatoza nauli ya shillingi 1000 abiria wanaoshuka maeneo ya Kiboriloni, Sango Pumuani na Kawawa road tofauti na nauli iliyopangwa na SUMATRA katika vituo hivyo.  

“Kuanzia wiki ijayo wadau wote  watakao kuja kuomba leseni kwa ajili ya usafirishaji wa abiria ndani ya mkoa huu watahitajika kuonyesha nauli watakazo toza abiria katika vituo vya katikati kabla ya kufika kituo cha mwisho cha safari zao,”alisema Bw.Mwita.

 Bw.Mwita alisema hivi sasa SUMATRA Mkoa wa Kilimanjaro  imeanzisha utaratibu wa kuwataka wadau wote wanaotarajia kuanza kutoa huduma za usafiri wa daladala mkoani hapo kuonyesha nauli watakazo toza katika  vituo vya katikati kabla ya kufika kituo cha mwisho.

 Hata  hivyo Afisa huyo aliwashauri wakazi wa maeneo kama kiboriloni kwa sasa kupanda daladala za Kiboriloni kwa kuwa zipo nyingi ili kuepuka usumbufu unaojitokeza.

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: EMBE DODO

Jamii Media yafungua kesi Mahakama Kuu kupinga vifungu vya Sheria ya Makosa ya Mtandao

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence M. Melo (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufungua kesi Mahakama Kuu Dar es Salaam kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinavunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao ya kijamii. Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence M. Melo (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufungua kesi Mahakama Kuu Dar es Salaam kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinavunjwa kwa kinachosemekana ni haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao ya kijamii.Baadhi ya wanasheria wa Jamii Media wakieleza kwa wanahabari dhumuni la kufungua kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao. Baadhi ya wanasheria wa Jamii Media wakieleza kwa wanahabari dhumuni la kufungua kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kusema  vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao.]Baadhi ya wanasheria wa Jamii Media wakieleza kwa wanahabari dhumuni la kufungua kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao. Baadhi ya wanasheria wa Jamii Media wakieleza kwa wanahabari dhumuni la kufungua kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kudai kuwa  vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao.
--------------------------------------------------
  KAMPUNI ya Jamii Media, waendeshaji wa mitandao ya JamiiForums.com na FikraPevu.com wametinga Mahakamani kufungua kesi ya kikatiba wakipinga baadhi ya vifungu vya sheria ya makosa ya mtandao kwa kile kuingilia Uhuru wa Maoni na Kujieleza wa wananchi. Jamii Media imefungua kesi hiyo Mahakama Kuu leo jijini Dar es Salaam, kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao ili kulinda maslahi ya umma kwa kuzingatia vifungu 26(2) na 30(3) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence M. Melo mara baada ya kesi hiyo kufunguliwa mahakamani, alisema kampuni hiyo imelazimika kufungua kesi hiyo baada ya kushinikizwa mara kadhaa na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za baadhi ya wateja wao.

 Alisema takribani miezi mitatu iliyopita, Jeshi la Polisi limekuwa likiushinikiza mtandao huo kwa njia ya barua kutoa taarifa za baadhi ya wateja wake wanaoonekana kutoa taarifa zile ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaibua ufisadi mkubwa na ukwepaji wa kodi. 

 Aliongeza kuwa JamiiForums katika kuhakikisha inasimamia usiri (privacy) wa wateja wao, wamekuwa wakihoji mashinikizo hayo yanazingatia sheria gani na kutaka kujua ni vifungu gani vya sheria ambavyo wadau wa mtandao huo wamevivunja lakini wamekuwa hawapewi maelezo yanayoridhisha zaidi ya kuelezwa kuwa hatua zaidi zitachukuliwa kama hautatolewa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi. 

 "...Baada ya kupata mashinikizo takribani manne yanayoashiria kuwa haki ya watanzania watumiao mtandao wa intaneti na hasa watumiaji wa mtandao wa JamiiForums, Jamii Media imeshauriana na Wanasheria wake na kuona ni wakati sasa wa Kuilinda haki ya wananchi kupata taarifa na kulindwa kwa Uhuru wao wa Maoni na Kujieleza inayolindwa kwa mujibu wa Katiba ya Nchi ibaraya 18 ambapo imefungua Shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Kesi namba 9 ya mwaka 2016); kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinapelekea kuvunjwa kwa haki za msingi za watanzania watumiao mitandao ili kulinda maslahi ya umma kwa kuzingatia vifungu 26(2) na 30(3) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano," alisema Melo. Alibahinisha kuwa mtandao wa JamiiForums utaendelea na shughuli zake kama kawaida na utaendelea kuwahakikishia watumiaji wake kuwa mahala salama pa kutolea madukuduku yao na hata kuisaidia Serikali kuonyesha nyufa zilipo kwa maslahi mapana ya Taifa (wakizingatia mwongozo wa ushiriki wa mijadala anuai). 

 Alisema JamiiForums itaendelea kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika jitihada zake za kupambana na ufisadi kwa kutoa uwanja/fursa salama na rahisi kwa wananchi kuweza kuyaainisha yale wanayoyabaini kuwa yanachelewesha maendeleo ya Taifa lao. 

 Mtandao wa JamiiForums ni mtandao mkubwa wa Kiswahili kwa Afrika Mashariki na Duniani ukiwa na wasomaji wasiopungua Milioni 4 kwa mwezi ambapo kwa mwaka 2016, mtandao huu unatimiza rasmi miaka 10 tangu uanzishwe. Mtandao huu unasifika kwa kutoa fursa ya kipekee kwa watumiaji wake kutoa yaliyo mioyoni mwao huku wengine wakijifunza mbinu kadha wa kadha za kijasiriamali, afya, elimu na hata kuibuka wanasiasa wapya waliofundwa na wana JamiiForums. "Pamoja na kuendelea kutoa huduma hata katika nyakati ngumu, mtandao wa JamiiForums unakumbana mara kwa mara na changamotonyingi zinazopelekea waanzilishi na waendeshaji wake kuwa katika misukosuko mara kwa mara." Anasema Melo.

Kongamano la Biashara Tanzania na Vietnam kufanyika March 9, 2016 ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre, jijini Dar es salaam

Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Azindua Tawi la Bank Of Africa Mlandege Zanzibar.

$
0
0
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf mwenye mkasi akijiandaa kukata utepe kuashiria kulizindua Tawi la Bank Of Africa Zanzibar lilioko katika barabara ya Mlandege.kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Balozi Mwanaidi Maajar. 
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bank Of Africa wakishiriki katika kukata utepe kulizindua rasmin Tawi la Bank Of Africa Zanzibar, uzinduzi huo umefanyika Zanzibar. 
Wageni Waalikwa na Wajumbe wa Bodi na Maofisa wa Bank Of Africa wakishangilia Uzinduzi huo wa Tawi lao la Banki Zanzibar.
Wajumbe wa Bank Of Africa wakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Nchini Tanzania Bwa. Ammish Owusu-Amoah, katikati wakizungumza wakimsubiri Mgeni rasmin Waziri wa Fedha Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bodi ya Bank Of Africa Tanzania Balozi Mwanaidi Maajar akisalimiana na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee alipowasili katika viwanja vya Bank hiyo hapo mlandege kwa ajili ya Uzinduzi wa Bank hiyo.
Waziri wa Fedha Zanzibar akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Bank Of Africa alipowasili katika eneo hilo. akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya BOA, Balozi Mwanaidi Maajar.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WABUNGE WA MABUNGE YA AFRIKA MASHARIKI (EALA) WAKAMILISHA SEMINA YOA YA SIKU MBILI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Mwakilishi kutoka Burundi akichangia mada wakati wa kipindi cha kutoa maoni toka nchi wanachama wa Bunge la Afrika Mashariki ambapo jana 04 Machi, 2016 Wabunge hao wamehitimisha Semina yao ya siku mbili iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi kutoka Rwanda akichangia mada wakati wa kipindi cha kutoa maoni toka nchi wanachama wa Bunge la Afrika Mashariki ambapo jana 04 Machi, 2016 Wabunge hao wamehitimisha Semina yao ya siku mbili iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.




Mwakilishi kutoka Tanzania akichangia mada wakati wa kipindi cha kutoa maoni toka nchi wanachama wa Bunge la Afrika Mashariki ambapo jana 04 Machi, 2016 Wabunge hao wamehitimisha Semina yao ya siku mbili iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi kutoka Uganda akichangia mada wakati wa kipindi cha kutoa maoni toka nchi wanachama wa Bunge la Afrika Mashariki ambapo jana 04 Machi, 2016 Wabunge hao wamehitimisha Semina yao ya siku mbili iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. 


Muhongo akabidhi gari la wagonjwa la kisasa jimboni kwake

$
0
0
Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akifungua mlango wa gari la wagonjwa kabla ya kulikabidhi rasmi.
Daktari Bingwa wa huduma za dharura na Majanga, Dkt. Christopher Mnzava (kulia) akizungumza jambo wakati wa hafla ya kukabidhi gari la wagonjwa la Kituo cha Afya cha Murangi. Kushoto ni Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akimkabidhi nyaraka za gari la wagonjwa la Kituo cha Afya cha Murangi, Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Dkt. Naomi Nyanchara.

WANAWAWAKE KUMILIKI ARDHI BADO NI NDOTO MAKETE MKOANI NJOMBE

$
0
0
Hii  ni Ofisi ya afisa Mtendaji Kata ya Iwawa, Kituo cha wakulima

Na Blogs za Mikoa Tanzania
Mila potofu zinazokandamiza wanawake zimeripotiwa kuendelea kushamiri katika baadhi ya mambo baada ya kutembelea katika maeneo tofauti tofauti ya wilaya ya Makete mkoani Njombe na kuzungumza na wakazi wa wilaya hiyo

Katika kijiji cha Iwawa wilaya ya Makete mkoani Njombe mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Jane Sanga amesema wanawake wengi wilayani hapo hawamiliki ardhi kutokana na mila potofu kuwa wamiliki wa ardhi ni wanaume pekee.

"Kwa hapa Makete wanawake unaowaona wanamiliki ardhi kwa kiasi kikubwa unakuta ni mjane anaimiliki baada ya kufiwa na mumewe au unakuta mwanamke huyo ana uwezo wa kifedha na ameamua kukunua kipande chake cha ardhi na anakimiliki mwenyewe, hapo hakuna anayemuingilia, na hata wale wajane bado utakuta wanasumbuliwa na ndugu wa marehemu mumewe, kwa hiyo bado hali ni ngumu" amesema Jane
Hiki ni kipande kidogo sana ambacho analima Bi. Jane(Hayupo Pichani)

Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Grace Mbilinyi ambaye amekutwa na mwandishi wetu akiandaa shamba kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula katika msimu ujao, amesema anamiliki shamba aliloachiwa na marehemu mumewe, licha ya kuendelea kusumbuliwa na ndugu wa marehemu wakidai kuwa mwanamke hataweza kuendeleza ardhi aliyoachiwa na mumewe

"Kwa kweli ni shida lakini Tutafanyaje sasa, mimi ni mama  wa nyumbani ambaye sana sana najishughulisha na ujasiriamali na kilimo kama hivi, kwa sasa ninamiliki hili shamba nililoachiwa na mume wangu kwa ajili ya kilimo, lakini vijimaneno vya ndugu vipo lakini bado sikati tamaa maana uwezo wa kumiliki ninao, na nitaiendeleza kwa kilimo" amesema Bi Grace

James Sigala ni mkazi wa Makete ambaye amekiri kuwepo kwa mila hizo zinazokandamiza wanawake hasa katika umiliki wa ardhi na kusema ingawa elimu inaendelea kutolewa na wanaharakati lakini bado kuna haja ya kuendelea kuitoa ili jamii ibadilike na kuamini kuwa hata wanawake wanaweza kimilikishwa ardhi kama wanaume
Afisa mtendaji kata ya Iwawa Bw. Festo Msigwa akiongea na mwandishi wa Blogs za Mikoa

Blog za Mikoa kupitia Njombe yetu  haikuishia hapo imebisha hodi katika ofisi za kata ya Iwawa iliyoko katika mji mdogo wa Iwawa (Makete Mjini) na kukutana na afisa Mtendaji Bw. Festo Msigwa ambaye amekiri kuwa bado umilikishwaji au umiliki wa ardhi kwa wanawake ni mdogo kutokana na mila potofu 

Amesema katika kata yake zipo kesi za ardhi zinazoletwa katika ofisi yake zikiwemo za wanawake wajane kupokonywa umiliki wa ardhi kutoka kwa ndugu wa mume wake kwa madai kuwa yeye kama mwanamke hawezi kumiliki wala kuiendeleza jambo ambalo limepingwa na kulaaniwa vikali na mtendaji huyo

"Wanawake wanaweza kwanza katika shughuli za shambani wao ndio wachakarikaji kuliko sisi wanaume, fikiria kwa mfano hawa wajane wanaokuja kwenye kesi za ardhi katika baraza la ardhi hapa, unakuta wakati wa uhai wa waume zao wao ndio walikuwa walimaji wazuri na watunzaji wakubwa wa mashamba, sasa kama aliweza toka mwanzoni iweje sasa washindwe" amesema Msigwa

Machi 8 mwaka huu ni kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kwa wilaya ya Makete maadhimisho yatafanyika katika kata ya Iwawa katika mji mdogo wa Iwawa

Shule ya sekondari Mgutwa kupanda miti 1,500 ili kutunza mazingira na kupiga vita jangwa na ukame

$
0
0
ILI kukabiliana na ukame, kupiga vita jangwa na utunzaji wa mazingira, shule ya sekondari Mgutwa iliyopo Kata ya Shambarai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ina mpango wa kupanda zaidi ya miti 1,500 kwenye eneo hilo.

Akizungumza na wageni waliotembelea shule hiyo Megan Allen kutoka Marekani na Juliane Friedrich wa Ujerumani, meneja wa shule hiyo Monica Mlemeta, alisema wao ni wana mazingira, hivyo wataendelea kupanda miti mingi zaidi japo eneo hilo waliloligeuza kuwa la kijani tofauti na awali.

Mlemeta alisema shule hiyo ina wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne, ina lengo la kuanzisha kidato cha tano hadi cha sita, ili kuboresha elimu ya eneo hilo la Simanjiro pamoja na kuzidi kutunza mazingira kwa kupanda miti mingi. 

Alisema japokuwa wanatumia gharama kubwa kupanda miti katika eneo hilo kutokana na jiografia iliyopo ikiwemo kutoa udongo sehemu nyingine, watahakikisha wanabadili mandhari ya eneo kwa kuotesha miti zaidi.

Mratibu wa asasi ya Community Education resources foundation, Godfrey Lema walioipatia shule ya Mgutwa miti hiyo 1,500 alisema lengo lao ni kuhakikisha wanatunza mazingira na kuondokana na ukame uliopo katika eneo hilo.

Alisema  kwa kushirikiana na asasi za Nick’s Eco safaris na Moivaro Jitegemee Family wamefanikisha hilo, japo ardhi ya eneo hilo ina mwamba na magadi, uongozi wa shule umelibadili kuwa la kijani, kwa kuendeleza utunzaji mazingira na kuwa mfano wa kuigwa.

“Wageni wetu Megan Allen kutoka Marekani na Juliane Friedrich wa Ujerumani, wamefurahia ukijani uliopo hapa na tutahakikisha tunaendelea kuiunga mkono shule hii, kwani imekuwa mfano bora wa utunzaji mazingira,” alisema Lema.

Alisema elimu ya mazingira inatakiwa kutolewa kwa sehemu kubwa ya jamii ya wananchi wa wilaya ya simanjiro, ili kuhakisha wanapanda miti kwa wingi kwani ndiyo vyanzo vya mvua na kupata kivuli, matunda na hewa safi.
Wageni mbalimbali wakiwemo Megan Allen wa Marekani na Juliane Friedrich wa Ujerumani, walioitembelea shule ya sekondari Mgutwa iliyopo Kata ya Shambarai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiangalia baadhi ya miche ambayo itapandwa kwenye shule hiyo.
Mwalimu wa mazingira wa shule ya sekondari Mgutwa iliyopo Kata ya Shambarai, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Godlove Issa (kushoto) akiwaonyesha wageni walioitembelea shule hiyo, baadhi ya miche inayotarajiwa kupandwa ili kutunza mazingira.
Mwalimu wa mazingira wa shule ya sekondari Mgutwa iliyopo Kata ya Shambarai, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Godlove Issa na raia wa Marekani Megan Allen, wakipanda mti kwenye shule hiyo ili kutunza mazingira.

WWF KUSAIDIA UJENZI WA MAJIKO SANIFU KATIKA SHULE TATU ZA MANISPAA YA MOSHI NA KUWEKA SOLAR KATIKA ZAHANATI YA MSARANGA.

$
0
0
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akiongozana na wa wakuu wa idara katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi walipotembelea shule ya sekondari J.K Nyerere .
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako wakiwa katika jiko la shule hiyo kuangalia namna ambavyo wanaweza kupunguza matumizi ya kuni kupikia.
Matumizi ya kuni ni makubwa katika shule za msingi ambazo zimekuwa zikitumika kupikia hali inayochangia ongezeko la uharibufu wa mazingira kwa kukata miti.
Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akitia saini katika kitabu cha wageni katika shule hiyo ,katikati ni mkuu wa shule hiyo , Parfectius Mushi akimtizama na kulia ni afisa kutoka WWF ,

TFF YAZIJIA JUU KAMPUNI ZA MICHEZO YA KUBAHATISHA

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa mshtuko taarifa za kuwepo makundi ya watu na makampuni wanaochezesha michezo ya kubahatisha inayohusu mashindano mbalimbali yanayoandaliwa na kusimamiwa na TFF (betting).

TFF inauthibitishia umma wa watanzania kuwa Shirikisho halihusiki wala halijawahi kutoa kibali chochote cha kuhusisha mashindano yake na michezo ya kubahatisha.

Kwa kuwa baadhi ya wahusika wa matendo hayo ni makampuni ya nje ya nchi hivyo TFF imechukua hatua zifuatazo:

1.TFF imeandika barua kwenye Shirika la Bahati Nasibu ya Taifa ili kupata mwongozo wa kisera na kisheria kuhusu haki na majukumu ya Shirika hilo  katika kudhibiti na kusimamia  jambo hilo.

2.TFF imeandika barua kwa kitengo cha sheria cha FIFA ili kupata mwongozo na ushauri wa namna ya kudhibiti makampuni ya nje yanayoshiriki mchezo huu.

TFF inawaomba wadau wa mpira wa miguu na washiriki wa michezo ya kubahatisha wajiepushe kushiriki michezo ya kubahatisha inayohushu michezo yote inayoandaliwa na TFF.

ODINGA’S DAUGHTER CLAIM ON OLDUVAI GORGE SITE AS KENYAS’ IS OUTREGIOUS

$
0
0
Six months ago, Rosemary Odinga, the daughter of Raila Odinga (Kenya prominent Politician,former PM and the leader of Kenya leading opposition party ) gave a  misleading presentation at United Nations headquarters in New york city,  claiming Olduvai Gorge archaeological site is located in Kenya. This presentation was troubling at best and disgraceful at worst.

Miss Rosemary’s misleading presentation has simply intensified the anger of many of us (Tanzanians) over this issue and further reinforces what is well known that Kenya is ripping off our tourist industry with its unfair tourism trade practices, mainly by misrepresenting   the geographical facts of Tanzania’s tourist’s attraction sites.

For a long time, Kenya have consistently been advertising deceptive information that Kilimanjaro Mountain and other Tanzanian’s tourist’s attraction sites belong to Kenya. The impact of Kenya’s unfair trade on Tanzanian people’s life is real. Millions of Tanzanians suffered from poverty and currency devaluation resulting from the poor economy which handily depended on tourism (and I don’t blame Kenya for all Tanzania’s economic problems).

I remember back in 1998, I met a doctor who was travelling with his family to Kenya on summer vacation to tour Serengeti, Ngorongoro crater,  and   mount Kilimanjaro. I asked him why he was flying to Kenya instead of flying straight to Tanzania where these sites are actually located. Apparently he was misled by Kenyan tourist agent that Mount Kilimanjaro is in Kenya.

That was in 1998, when smart phones were not around, internet was luxury item, I mean the era of Macintosh and Google was barely known.

In today’s world of abundance of smart phones, social media and Google search and the existence of   Google map; for Miss Rosemary to think she would get away with these old dirty   business deceptions is appalling, and frankly, she should be ashamed of herself. 

To be fair to Miss Rosemary, we still don’t know her intent to mislead the world on the geographical facts; she might have had a bad Geography teacher in College.

Miss Rosemary has eventually apologized, a step in the right direction. I hope this incident will lay the ground work for a fair business practice between two countries. Let us all move forward and work together as neighbors to strengthen our mutual interest of advancing our precious tourism industry.

THE END 3/3/16
MOHAMED MATOPE IS AN OPINION WRITER FOR VAROUS AFRICAN’S BLOGS.

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB TAWI LA WATER FRONT WATOA MSAADA KATIKA TAASISI YASARATANI YA OCEAN ROAD LEO.

$
0
0
KUELEKEA siku ya wanawake duniani  wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Water front jijini Dar es Salaam leo wametoa msaada wa vitu mbalimbali pamoja na fedha katika taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuwasaidia baadhi ya wagonjwa waliopo katika hospitali hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufika katika Taasisi ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road  jijini Dar es Salaam leo kwaajili ya kutoa masaada wa vitu mbalimbali.
Baadhi ya vitu vilivyotolewa na wafanyazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam. 
......................................
Hata hivyo wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam wametoa elimu kwa wafanyakazi na wanakikundi cha  'The Great Ten'wa Kampuni ya Busines Times jijini Dar es Salaam kuhusiana na kufungua Akaunti ya MALKIA katika benki hiyo kwa kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo kilele cha maadhimisho ya siku hiyo ni Machi 8 kwa kila mwaka.
 Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam, Adam Akaro (kulia) na Meneja wa huduma kwa mteja wa benki ya CRDB tawi la water Front jijini Dar es Salaam wakiwa katika kikao na wafanyakazi wa wafanyakazi wa kampuni ya Business Times wanaounda kikundi cha 'The Great Ten'.
Baadhi ya wafanyakazi wa wafanyakazi wa kampuni ya Business Times wanaounda kikundi cha 'The Great Ten'.wakimsikiliza Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam, Adam Akaro (kulia) na Meneja wa huduma kwa mteja wa benki ya CRDB tawi la water Front jijini Dar es Salaam leo.

Hali ya usafi katika soko la Ilala jijini Dar es Salaam imeonekana sio ya kuridhisha kutokana na uchafuzi wa mazingira.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS - MAZINGIRA NA MUUNGANO, JANUARY MAKAMBA AKUTANA NA WANAUWAMITA

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba akiangalia baadhi ya sampuli za mifuko isiyoharibu mazingira ambayo inatengenezwa na Umoja wa Watengeneza mifuko isiyoharibika Tanzania (UWAMITA) Kulia  ni Mwenyekiti wa kikundi hiko Jumanne Mgude.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba, akiongea na Wanakikundi wa Umoja wa Watengeneza Mifuko isiyoharibika Tanzania (UWAMITA) walipomtembelea Ofisini kwake mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo.

MAHAFALI YA NNE YA CHUO CHA ZENITH LEARNING CENTER KWA KUSHIRIKIANA TRAVELPORT.

$
0
0
Mwalimu wa Chuo cha Zenith Learning Center Ali Mussa Mohammed, akizungumza kabla ya kuaza Mahafali ya Nne ya Chuo hicho yaliofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho Majestik Zanzibar jengo la Zanlink,Jumla ya Wahitimu 28 wametunikiwa Vyeti vyao na Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib.
Wahitimu wa Mafunzo hayo wakiwa ukumbi wa Mahafali hayo ya yaliofanyika katikav Ukumbi wa Chuo hicho Majestik Zanzibar jengo la Zanlink 
Mgeni Rasmin wa Hafla hiyo ya Mahafali ya Nne ya Chuo cha Zenith Learning Centr akiwa na Viongozi wa Chuo hicho wakati wa Mahafali hayo yaliofanyika katika Chuo hicho Zanzibar. 
Mgeni Rasmin Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib na Ungozi wa Chuo hicho wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao baada ya kuwakabidhi Vyeti vyao.
 Imetayarishwa na OthmanMapara.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Tamasha la Michezo la Wanawake kuelekea kilele cha siku wa wanawake duniani lafana

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (watatu kulia) akiongoza wanawake kufanya mazoezi wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga (katikati) akifanya mazoezi ya kukimbia wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Michezo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bibi. Zainabu Mbussi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akirusha mpira kuashiria ufunguzi wa mchezo wa mpira wa pete wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam. Anayezuia mpira ni Mjumbe wa Baraza la Michezo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bibi. Zainabu Mbussi.

Tutumie Utamaduni Wetu kujenga Nchi - Mh. Nape

$
0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipiga ngoma alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa Golden Jubelee Towers alipokuja kushiriki katika uzinduzi wa Video mpya ya Mshairi Mrisho Mpoto inayoitwa Sizonje .Wengine Pichani ni Mrisho Mpoto,Dr Mwaka na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bi leah Kihimbi.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye Nape Nnauye akizindua rasmi video ya Sizonje,Kushoto kwake ni Mrisho Mpoto.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiinadi video ya Sizonje kwa wadau mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi huo.Nape aisema video hiyo inawakilisha serikali ya awamu ya tano na utumbuaji wa majipu.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Msichana Butogwa Charles Shija aliyeongoza kitaifa katika mtihani wa kidato cha nne.


Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images