Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live

NGOMA AZIPENDAZO ANKA: Bolingo Ya Telephone


TAHADHARI YA UGONJWA WA KIMETA NA MAGONJWA MENGINE YATOKANAYO NA WANYAMA

MAJALIWA: MTU AKIHARIBU KAZI ASITARAJIE UHAMISHO.

0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa(Pichani) amesema watumishi wa umma wako huru kuhamia kokote wapendako lakini wahakikishe wanaenda huko wakiwa safi na kamwe mtu asiharibu kazi kazi akitarajia kuwa atahamishiwa sehemu nyingine.

"Serikali hii haina utumishi kwa mtu aliyeharibu kazi,usije ukaharibu hapa Itilima ukadhani utaenda Bunda kuendelea na kazi. Serikali ya awamu hii haina nafasi na  watumishi wa aina hiyo," amesema.

Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo (Ijumaa, Machi 4, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Itilima kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambao ameuzindua leo hii wilayani Itilima, mkoani Simiyu.

"Watumishi wenzangu huu ni wakati wa kubadilika na kuona mwelekeo wa Serikali hii ya awamu ya tano ukoje. Jukumu letu ni kuwatumikia Watanzania wote bila kujali itikadi zao, rangi wala dini zao," alisisitiza.

Waziri Mkuu aliwahakikishia watumishi hao kwamba Serikali inatambua changamoto walizonazo kutokana na upya wa wilaya hiyo na mkoa huo na akawaahidi kuwa itaboresha mazingira yenu. "Msiwaadhibu wananchi kwa kisingizio cha mazingira magumu ya kazi zenu, tunajua mnayo madai ya nauli, posho za mafunzo, kupandishwa madaraja na malimbikizo ya likizo," alisema huku akishangiliwa.

Alisema Serikali itayalipa madeni hayo japo haitamaliza yote kwa wakati mmoja ila ana uhakika wa kukamilisha walau kwa asilimia 80.

Mapema, akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa wilaya hiyo, Bibi Georgina Bundala alisema wilaya hiyo iliyoanzishwa Machi 2012 na kupata Halmashauri Julai 2013 haina kituo cha polisi cha wilaya, haina gereza, Ofisi za TAKUKURU, mahakama ya wilaya wala benki.

Alisema wilaya hiyo haina hospitali ya wilaya ila akabainisha kuwa wamekwishatenga eneo la ekari 30 kwa ajili ya ujenzi huo. "Pia tumekwishapima viwanja 123 na eneo la kujenga  taasisi lenye ekari 143.8 limefanyiwa uthamini na fidia kukamilika," alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, MACHI 4, 2016.

BARCA YAVUNJA RECORD HISPANIA

0
0
Na Bakari Issa Madjeshi

Klabu ya Soka ya Barcelona ya nchini Uhispania imefanikiwa kuvunja ‘record’ iliyowekwa kwa takliban miaka 27 ya Ligi Kuu Soka nchini humo,baada ya kucheza michezo 35 bila ya kufungwa.

Barca imevunja record hiyo baada ya hapo jana kupata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Rayo Vallecano katika mchezo wa Ligi Kuu maarufu kama La Liga.

Katika mchezo huo, Lionel Messi  alifanikiwa kufunga mabao 3 peke yake(hat-trick) ikiwa ni ya 35,na kufikisha mabao 33 katika msimu wa Ligi,huku mabao mengine ya Klabu hiyo yakifungwa na Ivan Rakitic pamoja na Arda Turan.

Washambuliaji wa Rayo,Diego Llorente and Manuel Iturra  walishindwa kutamba katika mchezo huo mbele ya Barca,wakati bao lao la pekee likifungwa na Manucho.
Kwa matokeo hayo,Barca inafikisha points 69,huku Atletico Madrid ikiwa na points 61 wakati Real Madrid ya Zinedine Zidane ina points 57.

CHAMUITA NAYO YACHOMOZA TAMASHA LA PASAKA

0
0
CHAMA cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kimeeleza kwamba Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka iliyo chini ya Kampuni ya Msama Promotions inatekeleza neno la Mungu na si huduma kama inavyodhaniwa na jamii.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chamuita, Addo November ndio maana mwaka huu wamelihamishia tamasha hilo mikoa ya Kanda ya Ziwa na kuachana na Dar es Salaam kama ilivyozoeleka.

November alisema kwa kuwa Msama ameonesha kwamba tamasha hilo ni sehemu ya huduma ametumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa mikoa ya Geita, Mwanza na Wilaya ya Kahama na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi ili kupata ujumbe wa neno la Mungu kutoka kwa waimbaji mbalimbali.

November alisema kampuni ya Msama imejipambanua kwamba kupitia tamasha la mwaka huu kuwasaidia walemavu ambako watakabidhiwa baiskeli zaidi ya 100.

Aidha naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema wanaendelea na mchakato wa kufanikisha ibada hiyo muhimu kupitia waimbaji na viongozi wa dini.

Msama alisema tamasha hilo linatarajia kuanza Machi 26 mkoani Geita, Machi 27 Mwanza na Kahama itakuwa Machi 28 ambako waimbaji mbalimbali wamethibitisha kushiriki katika tamasha hilo.

“Nawaomba wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha msaada kwa wenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu na wajane, hivyo wakazi wa mikoa wajitokeze,” alisema Msama.

Msama alisema viingilio katika tamasha hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na shilingi 2000 kwa watoto ambako waimbaji waliothibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni Rose Muhando, Upendo Nkone, Bonny Mwaitege, Jesca BM, Joshua Mlelwa, Jenipher Mgendi, Faustin Munishi, Kwaya ya Wakorintho Wapili na Kwaya ya AIC Makongoro.

MALALAMIKO YANAYOHUSU UPATIKANAJI WA HAKI KUSHUGHULIKIWA KWA WAKATI.

0
0
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Katiba na Sheria  Bi Farida Khalfan (katikati) akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo Pichani) kuhusu utaratibu wa Wizara katika kupokea na kushughulikia malalamiko yanayohusu upatikanaji wa haki kwa wananchi. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya malalamiko  Grifin Mwakapeje na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Ufatiliaji Haki Bi Mary Mrutu.
 Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya malalamiko kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Grifin Mwakapeje akitoa rai kwa wananchi na wadau wa sekta ya Sheria kuendelea kutumia huduma ambazo zinazotolewa na Wizara hiyo ili kuwezesha kupata haki kwa wakati. 
                Mkurugenzi Msaidizi Ufatiliaji Haki Bi Mary Mrutu kutoka Wizara ya Katiba akifafanua kwa waandishi wa habari (Hawapo Pichani) mamlaka ya Waziri wa Katiba na Sheria katika kuongeza muda wa ukomo wa kufungua mashauri ya madai mahakamani.

Na Frank Mvungi-Maelezo.
SERIKALI imedhamiria kuendelea kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi yanayowasilishwa ili kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wakati.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Malalamiko kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Griffin Mwakapeje wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

aAidha , Mwakapeje amesema Wizara hiyo imekuwa ikipokea malalamiko yanayohusu ucheleweshwaji wa utekelezaji wa amri mbali mbali zinazotolewa na mahakama,ucheleweshaji wa nakala za hukumu na mienendo ya mashauri baada ya kumalizika mahakamani.
Malalamiko mengine yanahusu msongamano wa mahabusu, ucheleweshwaji wa upelelezi,wananchi kubambikiwa kesi,migogoro ya ardhi navitendo vya rushwa.

Akizungumzia wajibu wa  Wizara hiyo Mwakapeje amesema ni kuyaratibu na kuyawasilisha kwenye taasisi husika ili kupata muafaka wa malalamiko hayo kwa wakati.

Hatua nyingine inayochukuliwa na Wizara katika kuwasaidia wananchi kupata haki kwa wakati, ni kutoa msaada wa kisheria unapohitajika kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo ili kuwawezesha wananchi kupata haki kwa wakati.
Katika kushughulikia malalamiko hayo “Serikali inayo dhamira ya dhati yakuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki kwa wakati.” Amesema Mwakapeje.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo Bi Farida Khalfan akizungumzia Mfumo wa kupokea malalamiko amesema kuwa wananchi wanaweza kufika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo mtaa wa Sokoine au kuandika barua ili kuwasilisha malalamiko yao na yatafanyiwa kazi kwa wakati.

Wizara ya Katiba na Sheria ina Dhamana ya Kusimamia masuala ya Katiba na Sheria ambapo inatoa huduma mbali mbali za kisheria kwa wananchi,mashirika na taasisi mbalimbali za umma na binafsi.

SHIRIKA LA UMEME ZANZIBAR (ZEKO) LAKANUSHA SHUTMA ZA KUSITISHA KUTOKUZA UMEME ZANZIBAR.

0
0
Meneja Mkuu Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali Mbarouk alipokuwa akizungumza na wandishi wa Habari kuhusu uvumi ulionea kwamba litasitisha  huduma ya kuuza umeme kwa siku kadhaa katika Mkutano uliofanyika Ofisi za ZECO ziliopo Bulioni Mjini Zanzibar.

Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar .
Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) limekanusha uvumi ulionea kwamba litasitisha  huduma ya kuuza umeme kwa siku kadhaa na kusababisha ghofu kwa wateja  na kupelekea msongamano katika vituo vya kununulia umeme vya Shirika hilo katika siku za karibuni.

Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Makadara, Meneja Mkuu wa ZECO ndugu Hassan Ali Mbarouk amesema kuongezeka kwa wateja katika vituo vya kuuzia umeme vya Shirika hilo kumesababishwa kukosekana huduma hiyo kwa kutumia simu za mkononi za Zantel kwa Easy pesa.

Ndugu Mbarouk amesema huduma ya kununua umeme katika vituo vyote vya ZECO itaendelea kama kawaida kwa siku zote na hakutakuwa na kuzimika wala kusita kuuza umeme katika vituo hivyo.

Hata hivyo amesema huduma ya kununua umeme  kwa kutumia  simu za mkononi kwa njia ya easy pesa itaendelea kukosekana  na amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati huu ambapo ZECO na Zantel  wanaendelea kulitafutia ufumbuzi tatizo lililojitokeza.

Amesema kukosekana  huduma hiyo  kwa njia ya easy pesa imesababishwa na mfumo  huo  kupata matatizo kuanzia tarehe 20 mwezi uliopita.
Amewahakikisha watumiaji wa umeme kwamba tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi katika kipindi kifupi kijacho kwani mkataba wa mwanzo wa miaka miwili wa ZECO na Zantel utakapo malizika  mkataba mpya utatoa fursa kwa mashirika mengine ya simu kuingia mkataba wa kuuza umeme.

Akizungumzia zoezi linaloendelea la kubadilisha mita za zamani na kuweka mita za Tukuza, Menaja Mkuu amesema  Shirika limepanga itakapofika  mwishoni mwa mwaka 2017  wateja wote wa umeme watakuwa wanatumia mita za  Tukuza.

Amesema pamoja na mafanikio makubwa waliyopata ya kubadilisha mita za zamani wanawasi wasi kwa baadhi ya wateja wasiowaaminifu kuzihujumu mita za Tukuza na kulikosesha fedha shirika kwani mita hizo zinachukua muda mkubwa kukaguliwa baada ya kuwekwa tafauti na mita za zamani ambazo hukaguliwa kila mwezi.

Meneja Biashara wa Shirika la umeme Zanzibar ndugu Thabit Salum Khamis amewaeleza waandishi wa habari kuwa usambazaji umeme katika visiwa vya Unguja na Pemba umefikia asilimia 86 lakini watumiaji umeme ni chini ya asilima 50.

Ndugu Thabit amewataka wananchi kubadili mfumo wa maisha kwa kutumia  zaidi  umeme kwani ni rahisi  kwa matumizi ya nyumbani ikilinganishwa na nishati ya kuni na mkaa.       
        

TAARIFA YA MSIBA WA WAZIRI WA ZAMANI WA MAMBO YA NJE

0
0
Tumepokea taarifa ya msiba wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Da es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa miaka ya 1983-1995 na kuwa Balozi nchini Zambia Balozi Joseph Rwegasira. 

Amefariki dunia katika Kitengo cha Moi Hospitali Taifa ya Muhimbili. Msiba uko nyumbani kwake Msasani; utaagwa katika kanisa Katoliki St. Peters tarehe 6/3/16 na utasafirishwa tarehe 7/3/16 kuelekea Bukoba kwa maziko.

Tunamuomba Mwenyezi ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. 

Amin.

Tanzania: Oil down, Opportunities are up

0
0
The oil price has been falling since  June 2014. And it continues to hit new bottom every day. 

Recent global oil price drop   sign several years of $ 100 per barrel which has led to massive oil production coming online  and supply exceed demand. The low demand is the result of the slowdown in  China’s  economic  activities .And rapid increase in a number of shale wells in the US thanks to  technology’s improvement.

 The price slump  hurt exporting countries but for Tanzania as an importer, it  brings prosperity.

In the positive sense, 
Cheap price  minimizes the living costs. And  Tanzanians are more likely to use  kerosene, diesel and cooking  gas in place of firewood and charcoal that are popular with low-income earners. 

However, it  reduces  transportation costs. Less costly  foods.  And low living costs for average Tanzanians.

Most importantly, production costs decrease. Many people available globally at low  costs than ever. Pipelines firms are in need of work. Major construction organizations  have little tasks.So the project should get low investment  costs than similar projects from 2-3 years in the past. 

In the context of low price, upstream activities are decreased and there’ll be easy availability of  drilling rigs  and other supporting activities with cheap costs.

In the negative side.
Undermine investment: Exploration  and production companies cut  costs range. So, going into the new finding works won’t be of interest in their strategy. And they’ll  be wanting to postpone important investment project, which will take years to show valuable earnings.  If the project has a risk, It might be better to get the same cash in a known project field, than try to create in a new, unknown field  with lots of business risks.

 However, some exploration and production companies  such as BG and Swala energy claim that the drop in costs is a short-term issue and won't considerably impact their  investment plan in Tanzania. 

Australia based  oil and gas exploration firm  (Swala energy) lately stated that it’ll continue with its exploration projects across Tanzania in 2016 despite the fall in oil price. Also low-level prices are damaging Tanzanian  Graduates who strategy career in oil and gas sector. Sadly,  Tanzanians  get laid off as the  oil firm’s strategies  to deal with a price drop.

Conclusion
The price has fallen dramatically and some supply  will go off-line finishing the gap until the price improves again. But the time of that process is incredibly uncertain and is expected  to persist in 2016 and maybe beyond. But for policymakers in Tanzania, the fall in oil price provides a period to execute economic plan and structural changes as well as finance social program.

Hussein Boffu
Graduate In Petroleum Geoscience
Hussein.Boffu@tanzaniapetroleum.com
0655 37 65 43

UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA (UWT) YAKABIDHIWA GARI MBILI ZENYE THAMANI YA SH MILIONI 22 NA MBUNGE WA VITI MAALUMU FAHARIA SHOMARI KHAMIS.

0
0
 Mbunge wa viti maalum, Faharia Khamis Shomari  akizungumza na Wajumbe wa Umoja wa WanawakeTanzania (UWT) katika ukumbi wa CCM Mkoa pichani hawapo kwenye sherehe ya makabiziano ya magari hayo yalio fanyika katika Ukumbi wa CCM Mkoa Amani Zanzibar.
 Mhe: Faharia  Shomari Khamis akimkabidhi funguo Mgeni Rasmi katika sherehe za Makabidhiano Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai kwaajili ya kuwakabidhi wahusika.
Magari aina ya Noha waliokabidhiwa Umoja wa Wanawake UWT Tanzania.(PICHA NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR).

ENEO KOROFI LA FUKWE ZA COCO LAANZA KUFYEKWA.

ONESHO LA ARDHI NA MAENDELEO YA JAMII LAFUNGULIWA RASMI MAKUMBUSHO YA TAIFA

0
0
Mgeni Rasmi kwa niaba ya Balozi wa Sweden Bw Jorgen Erickson na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula wakikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa onesho la Ardhi na Maendeleo ya Jamii, kwenye Ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula akitoa ufafanuzi juu ya onesho la Ardhi na Maendeleo ya Jamii na kuipongeza Serikali kupitia Wizara ya Ardhi na Makazi kwa kusimamia vyema matumizi ya ardhi, kwenye Ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
mtafiti mzamivu katika taaluma ya mazingira na matumizi bora ya ardhi kutoka Sweden Bi. Emma Li Johansson akitoa maelezo mafupi juu ya utafiti alioufanya Kilombero Mkoani Morogoro juu ya Matumizi ya Ardhi ambapo matokeo yake ndio onesho lililofunguliwa leo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI ALHAMISI MACHI 3

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA SHULE YA SEKONDARI TAMBAZA MWAKA 1990 WATOA MSAADA WA VITABU VYA SAYANSI SHULENI HAPO LEO

0
0
Wanafunzi waliomaliza kidato cha sita Shule ya Tambaza mwaka 1990 (Class of 99), leo wamekabidhi msaada wa vitabu vya sayansi shuleni hapo kama mchango wao kwa shule yao ya zamani

Akiongea na waandishi wa habari Mratibu wa Class of 99, Marsha Makatta Yambi amesema lengo ni kuhakikisha dhana ya Elimu bure inatekelezwa kwa kila mwenye kuguswa na matatizo ya Elimu kusaidia kwa kadri ya uwezo wake. Marsha amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto za maisha yao

Pichani Marsha makatta Yambi akimkabidhi makamu mkuu wa shule ya sekondari ya Tambaza vitabu hivyo ambavyo vimegharimu Shilingi Milioni Tatu na Laki Mbili.
Naye makamu wa mkuu wa shule ya Tambaza alishukuru kwa msaada huo ambao anasema ni wa kipekee na kuwaomba wanafunzi wengine waliohitimu shuleni hapo kuiga mfano huo sababu mahitaji ni mengi na serikali peke yake haitaweza kuyatimiliza bila ya msada wa wadau

MKUU WA MAJESHI AONGOZA KUWAAGA MAOFISA MAJENERALI 16 WA JWTZ WALIOSTAAFU.

0
0
Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kwenye gari kushoto) na Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela wakitoa heshima katika hafla ya kuagwa iliyofanyika Viwanja vya Twalipo Mgulani Dar es Salaam leo mchana. Maofisa Majenerali 16 waliostaafu Utumishi Jeshini waliagwa.
Askari wa JWTZ wakifuatia matukio mbalimbali kwenye 
hafla hiyo.
Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba, akikagua gwaride hilo maalumu kwa ajili ya kuagwa.
Na Dotto Mwaibale.
JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ), limewaaga Mameja generali, Luteni na Brigedia Generali 16, akiwemo, aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Luteni Generali Samwel Ndomba.

Tukio la kuwaaga majenerali hao ambao wamestaafu  utumisho wao jeshini limefanyika jijini Dar es Salaam leo katika viwanja Twalipo Mgulani saa tatu hadi saa tatu asubuhi ambapo liliambatana na gwaride maalumu la vikosi mbalimbali vya Anga, nchini kavu, majini pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Hafla hiyo ya kuwaaga Magenerali hao iliongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Davis Mwamunyange ambapo waaga hao ni wa vyeo mbalimbali vya Brigedia Generali waliokuwa nane, Meja Jenerali sita na Luteni wawili na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali na wastaafu wa jeshi hilo.

Majenerali hao kila mmoja alipata fursa ya kukagua gwaride kila alipowasili viwanjani hapo ambapo kati yao ni Luteni Generali walipata heshima ya pekee na kufanyiwa gwaride lililokuwa tofauti na wengine.

Majenerali hao ni Mnadhim Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama JWTZ, Luteni Jenerali Samwel Ndomba ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mkuu wa Utumishi katika jeshi hilo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Wengine ni Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi jeshini, Luteni Jeneral Paul Ignas ambaye pia aliwahi kuwa ni Mkuu wa Mjeshi ya kulinda amani Darfur nchini Sudani.

Kwa upande wa Mameja Jenerali ambao walipewa heshima na kukagua vikosi hivyo ni Mkuu wa Jeshi la Nchi kavu, Meja Jenerali Salum Kijuu, Mkuu wa Utumishi Jeshini, Meja Jenerali Vicent Mlitaba, Mkuu wa Jeshi la Anga, Meja Jenerali Joseph Kapwani, Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu kilichopo Duruti mkoani Arusha Meja Jenerali Ezekiel Kiunga.

Wengine ni Mkuu wa Shirika la Mzinga mkoani Morogoro, Meja Jenerali Chalres Mzanila, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Mhunga.

Na wengine ambao ni Mabrigedia ni Mkuu wa Chuo cha Kijeshi cha Sayansi ya Tiba Lugalo, Brigedia Jenerali Dk.Luhindi Msangi , Mkuu Tawi la Ukaguzi jeshini ambaye pia aliwahi kuwa mkaguzi wa majeshi ya SADC, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga.

Wengine ni Mkuu wa Tawi la Akiba, Brigedia Jenerali Agustino Gailanga ambaye pia aliwahi kuwa mpambe wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Mratibu wa Miradi ya Maendeleo Jeshini, Brigedia Jenerali Mrisho Abdallah , Mkuu wa Kikosi cha Ndege cha usafirishaji, Brigedia  Jenerali Ezra Ndimugwango.

Na wengine ni Kamanda wa Brigedi ya Tembo mkoani Songea, Brigedia Jenerali John Chacha, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa jeshini, Brigedia Jenerali Martini Mwankanye na Mkuu wa Shule ya 'Eflantria' mkoani Arusha, Brigedia Harodi Mzirai.

Akizungumza mara baada ya hafla hiyo Luteni Jenerali mstaafu Ndumba alifurahia hatua hiyoa na kubainisha kuwa kwa sasa wanaenda kuanza maisha mapya.


(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com.

UPENDO GOSPEL YAANDAA TAMASHA LA PASAKA LITAKALOFANYIKA MACH 27 VIWANJA VYA LEADER'S.

0
0
Mwenyekiti wa Tamasha Upendo Gospel International, Amarido Charle's akizungumza na waandishi wa habarin (hawapo pichani) juu ya tamasha la pasaka litakalofanyika Machi 27 katika viwanja vya leadar's jijini Dar es Salaam,katika ni Maneja Uendeshaji, Shaweji Steven, Kushoto ni Meneja wa Gospel, Emmanuel Mweta.
02.Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tamasha Upendo Gospel International, Amarido Charle's wakati akitangaza tamasha la pasaka la Machi 27 mwaka huu leo jijini Dar es Salaam
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya jamii)

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
UPENDO Music Festival imeandaa tamasha la Injili litakalofanyika  Machi 27 mwaka huu katika viwanja vya Leader,s jijini Dar es Salaam .
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tamasha Upendo Gospel International, Amarido Charle's amesema  kuwa tamasha hilo litakuwa  na ubora kutokana na walivyoliandaa kwa miaka mingi na sasa imetimia waumini mbalimbali kuungana kuikaribisha pasaka.

Charle's amesema kuwa tamasha litakuwa na vionjo mbalimbali kutoka kwa wasanii wa injili katika wa vikundi mbalimbali bila kujali kanisa analotaka.

Amesema wamekuja katika tamasha kwa muonekano tofauti kwa wasanii kutumia majukwa tamasha hilo kujitangaza na sio kupigiwa simu hali hiyo ndio imesaidia nchi zilizoendelea kuwa na wasanii nyota kutokana na kujitoa katika matamasha.

Tamasha hilo litakuwa na viingilio ikiwa kama sehemu ya uendeshaji wa uwanja na sio kwa ajili ya kujinufaisha kwa kuwa na kiingilio kwa mkubwa sh.5,000 na viti maalum kwa sh.10,000.

Charle's amesema kuwa kuanzia majira saa nne kutakuwa na michezo mbalimbali katika viwanja hivyo nia ikiwa na kutambua na vipaji vingine vya michezo.

WANANCHI WA SEGEREA WATINGA MAHAKAMA YA ARIDHI LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

0
0
Diwani wa Kata ya Tabata, Patric Assenga akizungumza na wananchi wa Segerea ambao walifika katika Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi kusikiliza ombi la kibali cha kufungua kesi ya kupinga ubomoaji wa nyumba za wananchi wa segerea leo jijini Dar es Salaam,kulia ni Naibu Meya wa Ilala, Omary Kumbilamoto.kesi hiyo imearishwa na Jaji Fredrica Mgaya kutokana na wakili wa serikali kupatwa msiba na itasikilizwa tena Machi 8 mwaka huu katika mahakama hiyo.

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na waandishi hawapo pichani mara baada ya kutoka Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi kusikiliza ombi la kibali cha kufungua kesi ya kupinga ubomoaji wa nyumba za wananchi wa segerea leo jijini Dar es Salaam, ,kesi hiyo imearishwa na Jaji Fredrica Mgaya kutokana na wakili serikali kupatwa msiba na itasikilizwa tena Machi 8 mwaka huu katika mahakama hiyo.
Wananchi wa segerea wakiwasilikiliza viongozi wao Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi waliofika kusikiliza ombi la kibali cha kufungua kesi ya kupinga ubomoaji wa nyumba za wananchi wa segerea leo jijini Dar es Salaam,.kesi hiyo imearishwa na Jaji Fredrica Mgaya kutokana na wakili serikali kupatwa msiba na itasikilizwa tena Machi 8 mwaka huu katika mahakama hiyo. 
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya jamii)

DIRA YA DUNIA IJUMAA 04.03.2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

MAREHEMU CELINA AKILIMALI AZIKWA JIJINI DAR

0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Bi. Angel Akilimali (kushoto)akiwa na mtoto wake pamoja na mumewe wakiweka udongo kwenye kaburi la mama yake marehemu Celina Akilimali.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Celina Akilimali mama mzazi wa Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Bi. Angel Akilimali.
 Mwenyekiti wa bodi ya Uhuru Alhaji Adam Kimbisa akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Celina Mfala Akilimali , mama mzazi wa Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM .
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwa kwenye ibada ya kumuombea marehemu Mama Celina Akilimali kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe .

 BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live




Latest Images