Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1145 | 1146 | (Page 1147) | 1148 | 1149 | .... | 3272 | newer

  0 0

    Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom nchini, Balozi Mwanaidi Maajar akihutubia katika  uzinduzi wa Mradi wa Moyo awamu ya Pili unaofadhiliwa na mtandao wa simu nchini Vodacom katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika wilayani Sengerema mkoani Mwanza juzi.
  Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akihutubia katika  uzinduzi wa Mradi wa Moyo awamu ya Pili unaofadhiliwa na mtandao wa simu nchini Vodacom katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika wilayani Sengerema mkoani Mwanza juzi.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Hamis Kigwangalla akihutubia wakati wa hafla ya  uzinduzi wa Mradi wa Moyo awamu ya Pili unaofadhiliwa na Vodacom Foundation iliyofanyika wilayani Sengerema mkoani Mwanza juzi.
   Mkazi wa Sengerema mkoani Mwanza, Lawrencia John akimuonyesha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Hamis Kigwangalla,Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Foundation, Balozi Mwanaid Sinare Maajar, Mkurugenzi wa Vodacom nchini, Ian Ferrao(kulia) mtoto wake Mwalu John aliyejifungua baada ya kupata msaada wa mradi wa Moyo unaofadhiliwa na Vodacom Foundation jana katika uzinduzi wa Mradi huo awamu ya pili mkoani humo.
  Kaimu Mkurugenzi wa USAID nchini, Bethany Haberer akisoma hotuba  wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Moyo awamu ya Pili unaofadhiliwa na Vodacom Foundation iliyofanyika wilayani Sengerema mkoani Mwanza juzi.

  NAIBU Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangala amezindua mradi wa kutokomeza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga nchini,Mradi huo umezinduliwa jana wilayani Sengerema mkoani Mwanza ambapo unafadhiliwa na taasisi ya Vodacom Foundation kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa ya USAID,Path Finder na Touch Foundation.
  Mradi huu ambao unajulikana kama”MOYO”awamu ya pili umelenga kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha sekta ya afya nchini na adhma ya kutokomeza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga nchini.

  Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika mjini Sengerema Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangala amesema kuwa mradi huu unaenda sambamba na malengo ya serikali ambayo imejipanga kuhakikisha matukio ya vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga vinavyojitokeza wakati wa kujifungua kutokana na ukosefu wa huduma za matibabu vinatokomezwa.

  “Katika kukabiliana na tatizo hili ambalo limetukutanisha  hapa siku ya leo na kuboresha huduma za matibabu nchini,serikali inatarajia kujenga wodi za akina mama wajawazito katika vituo vyote vya Afya nchini vilivyopo vijijini na mijini hivyo nawapongeza kwa kuiunga mkono serikali na natoa wito kwa wananchi wote kuelewa jitihada hizi na kuvitumia vituo hivi na huduma hizi ili kufanikisha lengo lililokusudiwa”.Alisema Dk. Hamis Kigwangala.

  Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao amesema tangu mradi wa MOYO awamu ya kwanza ulianza kutekelezwa mwaka 2009 na umefanikiwa kuandikisha wanawake zaidi ya elfu 16,000 katika vituo vya afya, na kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na Watoto zaidi ya 450.
  Alisema zipo baadhi ya changamoto kadhaa za baadhi ya akina mama wajawazito kutojifungua katika vituo vya Afya, ambapo licha ya changamoto hizo  mradi huo umewezesha mafunzo  kwa wahudumu wa Afya wa ngazi ya Jamii wanaopita kila kaya kutoa elimu, ili kubadili mitazamo hasi ya baadhi ya akina mama kutofika kwenye vituo vya afya kupatiwa huduma za uzazi.

  “Kupitia mradi huu ambao pia umelenga kurejesha fadhila kwa wateja wetu tutagharamia usafiri wa akina mama wajawazito kupitia huduma ya M-Pesa kama ambavyo ilikuwa kwenye awamu ya kwanza ya mradi ili waweze kufika kwenye vituo vya afya kupata matibabu haraka pindi patakapohitajika msaada “,Alisema.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Foundation, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar, amesema pamoja na mafanikio  ya kiafya  yaliyopatikana kwa kukabiliana na ugonjwa wa Fistula na huduma ya ujumbe mfupi wa maneno ya kuelimisha akina mama masuala ya uzazi kupitia mradi wa WAZAZI NIPENDENI kusaidia akina mama wengi, vilevile zoezi hilo limekuwa likiviwezesha vikundi vya kuweka na kukopa vya Wanawake na kuwapatia mafunzo ya kuwawezesha kijikwamua  kiuchumi.

  “Kupitia matumizi ya teknolojia ya huduma za simu za mkononi, kampuni imeweza kuboresha maisha ya wananchi.Nawapongeza wadau wote ambao tumekuwa tukishirikiana nao hasa Shirika la Msaada la watu wa Marekani (USAID).

  Mkazi wa Sengerema Mwanza Lawrencia John, ambaye ni mmoja wa wanawake walionufaika  aliupongeza mradi huu na kusema ulimsaidia alipokuwa kwenye hali ya uchungu wakati wa kujifungua mtoto wake wa kwanza. Alipopiga simu aliweza kusaidiwa mara moja na amejifungua salama kabisa na anatoa wito kwa wadau wengine waweze kujitokeza kunufaika na huduma hii.

  0 0

  Kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars), leo kimefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa kuwakabili timu ya Taifa ya Wanawake kutoka Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kesho Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

  Twiga Stars inayonolewa na kocha mzawa mwanamke, Nasra Juma imekamilisha ratiba yake leo asubuhi kwa kufanya mazoezi mepesi katika uwanja wa Karume ofisi za TFF, huku kocha wake Nasra akisema vijana wake wote wapo katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo huo.

  Akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa TFF uliopo Karume, Nasra amesema ana waheshimu Zimbabwe wana timu nzuri, ndani ya miaka minne wameshacheza nao zaidi ya mara nne, mapungu yaliyojitokeza katika michezo iliyopita wamefanyi kazi na hivyo kesho ana imani watafanya vizuri.

  Aidha kocha Nasra, amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kesho Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi kuwapa sapoti Twiga Stars katika mchezo huo utakaonza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

  Naye nahodha wa kikosi hicho Sophia Mwasikili, amesema wachezaji wote wapo katika hali nzuri, wana ana ari na morali ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo wa kesho, na kuwaomba watanzania kuwapa sapoti kwa kujitokeza kwa wingi kuja kuwashangilia uwanjani watakapokuwa wakipeperusha bendera ya Tanzania.

  Wapinzani wa Twiga Stars, timu ya taifa ya Zimbabwe wanawasili leo jioni tayari kwa mchezo huo, huku waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Ethiopia wakiwa tayari wameshawasili leo mchana kwa shirika la ndege la Kenya (KQ).

  0 0

  Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions,Alex Msama ambaye pia ni Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni jijini Mwanza,akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari alipokuwa akizungumza nao Ofisi kwake,Kinondoni jijini Dar leo.

  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka  linalotarajiwa kufanyika jijini Mwanza mnamo Machi 27.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maaandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama,amebainisha kuwa Waziri Nape amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo litaanzia Geita Machi 26 na kumalizia Kahama Machi 28.

  Msama alisema kamati yake inaendelea na maandalizi ya kuelekea tamasha hilo ambalo litashirikisha waimbaji mbalimbali hapa nchini.“Maandalizi kuelekea Tamasha la Pasaka yanaendelea vema, hivyo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wajiandae kupokea ujumbe wa neno la Mungu kupitia viongozi wa dini na waimbaji wa muziki wa Injili,” alisema Msama.

  Msama alisema baadhi ya waimbaji waliothibitisha kushiriki tamasha hilo ambao ni pamoja na Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Christopher Mwahangila, Joshua Mlelwa, Sifael Mwabuka, Jenipher Mgendi, Kwaya ya AIC Makongoro na Kwaya ya Wakorintho Wapili.

  Msama pia alidokeza kuhusiana na suala zima la viingilio,alisema kuwa viingilio hivyo vinaendana na tukio hilo ambalo mbali ya kumuimbia na kumtukuza Mungu pia lina dhamira ya kusaidia jamii yenye uhitaji maalum.

  “Nawaomba wakazi wa mikoa Geita, Mwanza na Shinyanga kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha tamasha hilo,” alisema Msama.

  Msama alisema kupitia viingilio vya tamasha hilo wanatarajia kutoa kipaumbele kwa wakazi wa mikoa itakayopitiwa na tamasha kwa kupatiwa  baiskeli zaidi ya 100 za walemavu, ambazo zitagawiwa mikoa mbalimbali.

  0 0

   Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,  Jenista Mhagama akizungumza na makundi mbalimbali mara baada ya waziri huyo kufanya ziara  mkoani njombe katika eneo la mchuchuma na linganga katika wilaya ya Ludewa.
  Baadhi ya wananchi na viongozi mbalimbali waliofika wilayani Ludewa kumsikiliza Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,  Jenista Mhagama.


  Njombe Mmejiandaaje fursa zilizopo kwenye Migodi ya Liganga na Mchuchuma?, swali hilo limehojiwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,  Jenista Mhagama alipofanya  ziara Mkoani Njombe lengo kuu la ziara hiyo ikiwa ni kuhabarisha kuhusu  fursa za kujiajiri zilizopo kwenye Mkoa huo. Waziri huyo amesema kuwa Mkoa wa Njombe ni moja kati ya Mikoa yenye fursa kubwa ya uwekezaji ambayo fursa hiyo ni migodi ya Makaa ya mawe ya Liganga na Mchuchuma  iliyopo katika Wilaya ya Ludewa ambayo inatarajia kutoa ajira rasmi  zaidi ya Elfu Thelathini.

  akizungumza  na baadhi ya makundi ya Vijana wa Bodaboda, Kundi la Vijana Wafyatua tofali, Walemavu wasiosikia (Viziwi), na Vikundi vya ujasiriamali kwa kina mama (VICOBA) Waziri Mhagama amesema kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu imepewa dhamana ya kushughulikia nguzo tisa za kuwawezesha Wananchi Kiuchumi uliozinduliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu lengo kubwa ikiwa ni ifikapo 2020- 2025 Wananchi wawe wamefika kumiliki uchumi wao  wenyewe.


  “Kutakuwa na mahitaji mengi sana katika Migodi hiyo ya Liganga na Mchuchuma. Tutahitaji mashine kwa ajili ya kusaga nafaka, tutaitaji vyakula vya aina mbalimbali, tutaitaji kina mama lishe na biashara nyingine ndogo ndogo za kila aina hizo zote ni fursa za kutuwezesha sisi kujiajiri na kukuza kipato chetu.Hivyo ni vizuri kila mtu aweze kuona ni kwa namna gani anaweza kunufaika na fursa hizo zilizopo mbele yake” Alisema waziri huyo.


  Vilevile amesema kuwa ili kuwezesha Wananchi Kiuchumi ipo fursa za kila Halmashauri kutengeneza Madawati ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambapo wateuliwa watapewa mafunzo ambayo yatawasaidia kuwaelimisha na kuwasimamia wananchi ili wananchi waweze kushika uchumi wao wenyewe.


  Aidha amesema kuwa kundi la Madereva bodaboda ni miongoni mwa makundi muhimu yatakayonufaika na dawati hilo.

  Tunatambua kuwa Madereva  bodaboda  wengi wanaondesha pikipiki si wamiliki halali wa pikipiki hizo wengi wao wanafanya kama vibarua na wengi wameshindwa kumiliki bodaboda zao wenyewe kutokana  na kuwepo kwa  masharti magumu ya uchukuaji mikopo jambo ambalo limekuwa ni kikwazo kikubwa kwao.


  Hivyo program hii inalenga kuwafanya Vijana wamiliki Bodaboda zao wenyewe sharti kubwa ya program ikiwa ni Vijana kujiunga na Saccos za Vijana ili waweze kupata Mkopo wenye riba nafuu ikiwa riba  ni asilimia tisa (9%) hadi asilimia kumi(10%) mkopo ukiwa  wa mwaka mzima na baada ya hapo kijana atamiliki bodaboda yake mwenyewe.


  Lakini pia program hii itawanufaisha madereva kwani wataweza kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii na kufanya utaratibu wa kupata matibabu pindi watakapopata ajali wawapo kazini.


  Akiongelea swala la VICOBA kwa kina mama amesema kuwa Serikali imeingia Mkataba na Benki ya Posta ambapo kina mama watapata mikopo kwa riba nafuu ambayo itasaidida wanawake wengi kujiajiri.


  Akitoa Maagizo kwenye ziara hiyo waziri huyo ameziagiza Halmashauri zote mkoani  Njombe kuhakikisha kuwa swala la ajira kwa vijana linakuwa moja kati ya agenda za kudumu kwenye Halmashauri zao, na kila Halmashauri ihakikishe inatenga maeneo kwa shughuli mbalimbali za Vijana. Hii itasaidia azma ya serikali ya kuwafanya vijana kujiajiri iweze kutekelezeka lengo kuu ikiwa ni kutokomeza tatizo la ajira kwa vijana ambalo limekuwa tatizo kwa nchi na duniani kwa ujumla.


  Pia ameziagiza Halmashauri Mkoani Njombe kuhakikisha kuwa zinafungua SACCOS za vijana ambazo zitasaidia upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu na Maafisa Ushirika wakague kama SACCOS hizo zipo hai na zinafanya kazi kwa faida ya Mkoa na Vijana kwa ujumla.


   Nae Mwakilishi wa kikundi cha viziwi kutoka Njombe  alitoa kilio chake kwa  waziri kuwa Halmashauri iteue mwakilishi atakayeshughulikia maswala ya walemavu ili nao waweze kushiriki kikamilifu katika fursa hizi za kuwawezesha vijana kujiajiri  na endapo jambo hili litashindikana itakuwa ni sawa sawa na bure kwani nao wanahitaji kufaidika na fursa zilizopo.


  Waziri huyo pia ameahidi kuhakikisha kuwa atajitahidi kuwasiliana na wahusika ili kuona ni namna gani wataweza kutatua kero mbalimbali wanazokumbana nazo vijana wanaojiajiri katika shughuli mbalimbali likiwemo swala la kuhakikisha kuwa  katika ngazi ya Mikoa taasisi nyingi za maendeleo ziweze kuwa na matawi ili kurahisisha utendaji kazi na kupunguza gharama za watu kufuata hudumu maeneo ya mbali pia Ameahidi huzichukua na kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto zilizowasilishwa na makundi mbalimbali katika ziara hiyo.
  IMETOLEWA NA;

  AFISA HABARI HALMASHAURI YA MJI NJOMBE

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam kwenye kikao cha kwanza cha Bodi hiyo kwa mwaka 2016. Kulia ni Zungu Azzan na Kushoto ni Bw. Edward Otieno Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw.Isaya Mngurumi akichangia jambo kuhusu uboreshaji wa miundombinu ya barabara katika Manispaa yake wakati wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema akichangia jambo wakati wa wakati wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es salaam kwa mwaka 2016.
  Baadhi ya Wabunge wa jiji Dar es salaam wakifuatilia kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es salaam. Kutoka kulia ni Mhe. Bonnah Kalua - Mbunge wa Segerea, Mhe. Faustine Ndugulile - Mbunge wa Kigamboni, Mhe. Zungu Azzan – Mbunge wa Ilala na Mhe. Abdallah Mtolea – Mbunge wa Temeke.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  USAID and Vodafone are partnering to reach more mothers in rural Tanzania with emergency transport services so they can safely deliver their babies. Photo Credit: Vodafone Foundation.

  On March 2, representatives of the Government of Tanzania, U.S. Agency for International Development (USAID), the Vodafone Foundation, and other partners gathered in Sengerema to celebrate a pioneering new toll-free emergency line and ambulance taxi service that could help save at least 2,700 lives of pregnant mothers and babies in rural Tanzania each year.

  In the country’s most remote regions, high-risk pregnant women have limited transport options to access critical hospital services that often make the difference between life and death for both mothers and babies. In response, USAID and the Vodafone Foundation have partnered to launch a service in Sengerema and Shinyanga districts that could help save around 225 women’s and babies’ lives each month.

  Similar to the 911 emergency line in the United States, this program connects pregnant mothers with a network of 100 taxi drivers who respond to emergency calls and take the women on a three-hour journey to reach the nearest hospital. Once women arrive safely at a hospital, the emergency taxi drivers are paid using Vodafone’s mobile payment service, M-Pesa. A trial of the taxi service late last year in a small area of Sengerema saved the lives of over 300 women and babies.

  Previously, there was no way for pregnant women with serious complications (many of whom are teenagers) to get to a hospital in Sengerema and Shinyanga. Only about 10 ambulances service these expansive regions that are home to two million people, and the unmet need for emergency transport is one reason maternal and infant mortality rates there are among the highest in the world.

  The new ambulance service is part of a broader program implemented by NGO partners Pathfinder International and Touch Foundation that has built a network of 250 community health workers in Sengerema and Shinyanga who have been taught Tanzania’s newborn and child health curriculum.

  More than 200 additional health workers have received training in life-saving emergency obstetric and newborn care and hospital facilities have seen improvements such as the construction of two new theaters for Caesarean sections and installation of solar suitcases that enable hospitals to conduct night deliveries. A mobile application, which lists more than 10,000 pregnant women and identifies those who are high risk cases, has also been developed for the community health workers.

  Vodafone Foundation Director Andrew Dunnett said, “Our maternal health program is another example of the transformative power of technology. This pioneering new service will provide a much-needed lifeline for thousands of high-risk pregnant women in Tanzania without access to emergency healthcare.”

  “We can all be proud of the progress that is in evidence today, yet much work remains to be done,” said USAID/Tanzania Acting Health Office Director Bethany Haberer. “Having achieved remarkable healthcare results in Sengerema, we need to consider the elements of this program that can be replicated, taken to scale, and sustained - all with increased support from the Government of Tanzania."

  Tanzanian Deputy Minister of Health Dr. Hamisi Kigwangalla said, “Maternity is not only a biological process, but a social one that should be a source of joy for families. Let me assure you that the Government of Tanzania will be at the forefront of collaboration and support of all stakeholders who are helping to improve the country's health sector.”

  0 0

   Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh Mwigulu Nchemba akizungumza mbele ya wakazi wa kata ya Kidodi,kijiji cha Tungu-Mikumi (hawapo pichani),kwenye mkutano wa kusikiliza na kutoa majibu kuhusu wakulima wa Miwa,pichani shoto ni Mbunge wa Mikumi, Mh Joseph Haule
   Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Mbunge wa Mikumi, Mh Joseph Haule katika Mkutano wa kusikiliza na kutoa majibu kuhusu wakulima wa miwa uliofanyika katika kata ya Kidodi,kijiji cha Tungu-Mikumi .
  Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Mikumi, Mh Joseph Haule wakifurahia jambo kwa pamoja katika katika Mkutano wa kusikiliza na kutoa majibu kuhusu wakulima wa miwa uliofanyika katika kata ya Kidodi,kijiji cha Tungu-Mikumi .

  0 0


  Mbunge wa Busega Dkt Raphael Chegeni (kushoto) na Mbunge wa zamni wa jimbo hilo, Dkt Titus Kamani ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Simiyu walipotaza rasmi kuzika tofauti zao na kushirikiana kuleta maendeleo kwenye jimbo hilo. Pichani viongozi hao walipowadhihirishia wananchi kuwa hawana chuki wala ugomvi tena na kuwa uchaguzi umekwisha, katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kwenye kijiji cha Lamadi wilayni Busega Machi 2, 2016.

  ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Busega,Dk Titus Kamani amekubali utendaji kazi wa Mbunge wa sasa wa Jimbo hilo,Dk Raphael Chegeni,akidai kwamba wananchi hawakukosea kumchagua.

  Dk Kamani aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji mdogo wa Lamadi Wilayani Busega ambao pia Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa alikuwepo .Dk Kamani,amekiri kwamba Dk Chegeni ni mchapakazi na wananchi wa jimbo hilo hawakukosea kumchagua na kwamba anamuunga mkono katika hatua zote anazofanya za kuleta maendeleo jimboni hapo.

  “Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na wananchi wangu uchaguzi ulishakwisha na sasa nimeamini mmepata mbunge makini na mchapakazi ,nimetambua sasa kuwa sikustahili kupingana naye ,nitashirikiana naye katika kazi wana busega ni wamoja na wanaCCM tunajenga nyumba moja hatuna haja ya kutokubaliana ikiwa tunaona aliyechaguliwa anafanya kazi nzuri,”alisema Dk Kamani.

  Alisema wananchi wa Busega wanampenda Dk Chegeni na CCM kwa ujumla hivyo ni wajibu wa viongozi wengine kumuunga mkono ili kusaidia wananchi wa jimbo hilo na mkoa wa Simiyu kwa ujumla.“Huyu bwana kweli mchapakazi,nilikosea njia kupingana naye sasa namkubali rasmi naona muda mfupi tangu aingie madarakani Busega imeanza kubadilika na mambo yanaenda,wanabusega Chegeni ni Jembe,tufanyeni kazi hakuna uchaguzi hapa umshakwisha,”alisema Dk Kamani.

  Kwa upande wake Dk Chegeni alieleza kuwa tofauti zao zilishakwisha na sasa wanafanya kazi ila amefurahi kuona kwamba Dk Kamani ametambua utendaji wake na kuahidi kuendelea kufanya kazi ya kuwatumikia wanabusega.

  0 0

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO.

  Watanzania na wadau wa haki za wanawake nchini wameshauriwa kuunga mkono haki sawa na ushiriki kwa wanawake katika fursa za uongozi wa kisiasa na kiuchumi na kupima mafanikio yaliyofikiwa na kuweka mipango yenye matokeo makubwa. 

  Akitoa taarifa juu ya siku ya wanawake Duniani, Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Wanawake Bi Sihaba Nkinga amesema kuwa siku ya wanawake Duniani husisitiza kujenga mshikamano wa wanawake wote duniani, kuhamasisha jamii kutafakari kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku hiyo ya kila mwaka.

  Amesisitiza kuwa wananchi wametakiwa pia kubainisha shuhuda za wanawake waliotoa mchango uliotukuka katika kuwezesha maendeleo ya wanawake na taifa kwa ujumla na Tafakuri hii hufanywa kwa kuelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali na asasi mbalimbali yakiwemo Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kuwaendeleza wanawake na kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali ya Serikali yenye lengo la kudumisha Amani, Usawa na Maendeleo kwa wanawake kwa ujumla.

  “Kuanzia mwaka 2005 Serikali ilipitisha uamuzi kuwa, maadhimisho haya yafanyike Kitaifa kila baada ya miaka mitano ili kutoa muda wa utekelezaji wa maazimio na kupima mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitano”Alisema Bi Sihaba.

  Sihaba Nkinga amewashauri wanahabari wote kuelimisha jamii kuhusu kauli mbiu ya Siku ya Wanawake kwa mwaka 2016 inayosema “50 – 50 Ifikapo 2030; Tuongeze Jitihada”, ambapo Kauli mbiu hii inasisitiza kuwa na mikakati thabiti yenye mwelekeo wa kufikia Agenda ya 2030 yenye malengo ya kufikia asilimia 50 kwa 50 ya ushiriki wa wanawake na wasichana katika nyanja zote za maendeleo.

  Aidha Bi Sihaba Nkinga amemtaka kila Mtanzania aweze kutambua jukumu alilonalo katika kufikia lengo la ushiriki sawa wa wanawake na wasichana katika Uchumi; Afya, Elimu, Ajira, Sheria na Siasa ifikapo mwaka 2030.

  Kwa mwaka 2016, katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani,mikoa yote nchini itazingatia hali na mazingira ya mikoa husika na kwa mkoa wa Dar es Salaam siku hii itaadhimishwa katika Manispaa ya Kinondoni. Wizara inatoa wito kwa mikoa yote kuhamasisha wananchi na wadau wote kushiriki maadhimisho ya siku hii adhimu na kuzingatia ujumbe wa kauli mbiu ya mwaka 2016.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati), akiwa na viongozi wa Mtandao wa Kingdom Leadership Tanzania Network na Viongozi wa Dini wa Mataifa mbalimbali Duniani, wakati wa uzinduzi wa mpango wa Sala maalum ya kuliombea Taifa utakaofanyika kila mwaka, uzinduzi huo umezinduliwa leo March 03, 2016 katika Hoteli ya Hayyat jijini Dar es salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua mkutano wa tisa wa siku mbili kwa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki pamoja na Wabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaojadili kuhusu kupitia kanuni, Sheria na Itifaki zilizotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki juu ya Chaguzi zinazofanyika ndani ya Nchi hizo. Mkutano huo umefunguliwa leo katika ukumbi wa LAPF Makumbusho jijini Dar es salaam
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mtandao wa Kitaifa wa Kingdom Leadership Tanzania Network na Viongozi wa Dini wa Mataifa mbalimbali Duniani baada ya uzinduzi wa Mpango wa Sala Maalum ya kuliombea Taifa uliofanyika leo March 03,2016 katika Hoteli ya Hayyat Dar es salaam.
  (Picha na OMR)

  0 0

  Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
  Serikali imeongeza wigo wa utoaji wa kibali cha uchangiaji wa elimu msingi bila malipo hadi kwa Wakuu wa Mikoa baada ya kujiridhisha kuwa taratibu zilizowekwa zimefuatwa kikamilifu.
   
  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es salaam Msemaji wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu amesema kuwa awali vibali hivyo vilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pekee ikiwa na lengo la kudhibiti michango holela.

  Taarifa hiyo imesisitiza kuwa azma ya Serikali ya kutoa elimu msingi bila malipo haizuii wadau mbalimbali wa elimu kuchangia maendeleo ya elimu kwa hiari ambapo wadau wakiamua kuchangia kwa nia ya kushughulikia kero fulani iliyopo katika shule yao au shule zao baada ya kupata kibali wanaruhusiwa kufanya hivyo.

  Katika kutekeleza dhana ya utoaji wa elimumsingi bila malipo, hadi kufika mwishoni mwa mwezi Januari, 2016 Serikali inatoa elimu hiyo kwa jumla ya wanafunzi 9,771,902.

  Kati ya wanafunzi hao, 8,301,759 ni wa elimu ya msingi na 1,470,143 ni wa sekondari ambao wanapatiwa elimumsingi bila malipo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

  Serikali inasisistiza kuwa viongozi wanahusika katika kusimamia utekelezaji wake ambapo kwa upande wa wazazi au walezi, kamati na Bodi ya shule pamoja na jamii wao nao wanajukumu la kuelewa majukumu yao ipasavyo.

  Aidha, juhudi za makusudi zinapaswa kufanywa na viongozi na watendaji wa elimu ili kuwezesha jamii kufahamu wajibu wao katika utekelezaji wa elimumsingi bila malipo na hatimaye kufikiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.

  Katika kutekeleza wajibu wake, Serikali ya Awamu ya Tano (SAT) kuanzia mwezi Januari, mwaka huu imeanza kutoa elimumsingi bila malipo imetoa waraka wa Elimu Namba 6 wa Mwaka 2015 ambao unaofafanua na kubainisha majukumu ya serikali na wadau mbalimbali katika utekelezaji wa elimu msingi bila malipo.

  0 0

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

  Watumishi wameaswa kuzingatia taratibu za uhamisho na wametakiwa kuwa makini na utapeli pamoja na upotoshaji unaofanywa kupitia mitandao ya kijamii na matangazo mbalimbali yanayowataka  kulipia pesa ili kupata uhamisho.

  Aidha, Serikali imewaonya watu wote wanaoghushi na kutumia vibaya nembo yake pamoja na mihuri kwa lengo la kuwalaghai wananchi na kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.

  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo jijini Dar es salaam, Msemaji wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu amesema kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayepatikana na hatia ya kughushi nyaraka na kujipatia fedha kwa njia isiyo halali baada ya kuwarubuni wananchi.

  Taarifa hiyo ya Serikali inafuatia kuzagaa kwa upotoshaji unasosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na matangazo yanayoeleza kuwa baada ya mtumishi kutuma maombi kwa Katibu Mkuu TAMISEMI na kukubaliwa, Katibu Mkuu atamtuma Afisa wake atakayepeleka majibu ya uhamisho na kumtaka mtumishi aliyeomba uhamisho kumgharimia  anapompelekea uhamisho jambo ambalo siyo kweli. 

  Kwa mujibu wa TAMISEMI, miongoni mwa watu wanaosambaza taarifa za upotoshaji ni Charles Machali ambaye amejipachika cheo cha Afisa Mdhibiti Uhamisho na anapatikana kwa simu Na. ni 0782 803783 na 0674 583941 na barua pepe yake ni charles53gachari@gmail.com.

  Baada ya taratibu za uhamisho kukamilika, Serikali hutangaza majina ya watumishi waliopata uhamisho kupitia tovuti ya Wizara  ambayo ni    www.tamisemi.go.tz

  Taratibu za kawaida za uhamisho zinamtaka mtumishi kupitishia barua kwa kiongozi wake mahali anapofanya kazi na katika mkoa wake ambao ndio una jukumu la kuleta maombi hayo kwa Katibu Mkuu TAMISEMI.

  0 0

  SERIKALI imesema kwa sasa itakuwa ikihudumia wagonjwa wote ndani ya nchi ikiwemo wale wagonjwa Mahututi ambao awali walikuwa wakipelekwa nje ya nchi. Hii ni baada ya kuendelea kuimarisha huduma hizo pamoja na kuwa na wataalam wa kutosha ambaio watapatiwa mafunzo zaidi.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mheshimiwa Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa kuzindua rasmi wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU) iliyopo katika jengo la Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

  Dk.Kigwangalla katika uzinduzi huo, amewapongeza watendaji wote waliofanikisha ikiwemo uongozi uliopita na ule wa sasa, Serikali pamoja na wadau wa sekta hiyo ya afya walioguswa na kuchangia upanuzi wa huduma za tiba ya wagonjwa hao Mahututi ambayo imewezeshwa kuwa na vifaa tiba vya kisasa huku ikiongezwa vitanda kutoka 8 hadi 25 kwa sasa.

  Aidha, Dk. Kigwangalla ametoa shukrani ya kipekee kwa wadau waliojitolea kwa moyo wao kuchangia huduma hiyo ya wagonjwa Mahututi ikiwemo Shirika lisilo la Kiserikali la Gastrenterology Foundation kutoka Ujerumani na wadau wote kwa kuweza kufanikisha huduma hiyo kuweza kupatikana hapa nchini na kupunguza safari za nje ambazo zimekuwa zikiigharimu Nchi fedha nyingi.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru (kushoto) akisoma hotuba maalum juu ya uzinduzi huo wa wadi ya wagonjwa Mahututi (ICU). Anayefuatia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mheshimiwa Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi. Wengine ni wadau waliowezesha kwa wodi hiyo akiwemo Rais wa shirika la Gastrenterology, Prf. Meinhard Classen (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na Bingwa wa Magonjwa ya tumbo kutoka Misri, Prf. Abdel Meguid.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mheshimiwa Dk. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo katika mkutano huoleo wakati alipokuwa mgeni rasmi mapema leo Machi 3.2016.
  Dk. Kigwangalla akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa wadi ya wagonjwa mahututi (ICU) katika jengo la Mwaisela. Wanaoshuhudia ni Rais wa shirika la Gastrenterology, Prf. Meinhard Classen (kulia) na Prf. Museru kushoto.
   (Picha zote na Andrew Chale.)

  0 0

  Kamishna wa oparesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Nsato Marijani, akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam. Kamishna Nsato Marijani amesisitiza wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuupunguza uhalifu na hatimaye nchi iwe ya Amani na utulivu. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Kamati ya Uchumi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ikutane na wafanyabiashara wote ili wajadiliane na kupanga kiwango cha ushuru kinachopaswa kutozwa kwenye mazao ya wilaya hiyo.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Machi 3, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Dutwa, Wilayani Bariadi, mkoani Simiyu.

  Amefikia uamuzi huo baada ya kuona bango lililoshikwa na wananchi wakilalamikia kutozwa ushuru wa sh. 3,000/- kwa gunia moja la mazao badala ya sh. 1,000/- ya zamani.

  "Masuala ya ushuru ni maamuzi baina yenu na Halmashauri yenu lakini hiyo tozo imeongezwa sana kutoka sh. 1,000/- hadi sh. 3,000/-. Ninaiagiza Kamati ya Ucumi ikae na wafanyabiashara wote ili mjadili suala hili na mkubaliane kiwango cha ushuru."

  "Wabunge pia waalikwe kwenye kikao hicho na Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Baraza la Madiwani nalo pia lishiriki kikao hicho. Kama mnataka kupandisha ushuru ni lazima mkubaliane viwango ili Watanzania wafanye biashara wakiwa na mapenzi na nchi yao," alisema huku akishangiliwa.

  Hata hivyo Waziri Mkuu alifafanua kwamba suala la kulipa ushuru ni la muhimu katika kuchangia makusanyo ya kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi. "Ushuru ni lazima ulipwe lakini pia ni lazima muwe mmekubaliana ni kiwango gani mnatoza. Makusanyo yote haya tunayofuatilia kwa sasa ni matokeo ya watu kulipa kodi na ushuru kama huu," alisisitiza.

  Wakati huo huo, Waziri Mkuu amekataza tabia ya maafisa wa kutoza ushuru kudai fedha kabla mwananchi hajauza mifugo wanapoileta mnadani kwani anakuwa amekuja kutafuta fedha.

  Alikuwa akijibu hoja iliyotolewa na mbunge wa viti maalum (CHADEMA), Bi. Gimbi Masabo ambaye alimweleza Waziri Mkuu kwamba kuna tabia ya kutoza sh. 6,000/- kwa kichwa kwa kila ng'ombe anayeswagwa kuingia eneo la mnada bila kujali kama mtu huyo ameuza ng'ombe au hajauza.

  "Hivi unawezaje kumtoza mtu ushuru wakati hajauza chochote au wakati akiwa njiani kuelekea mnadani? Ni bora umtoze mtu baada ya kuuza. Kumbukeni kuwa wananchi wetu wanakuja mnadani ili wauze na kupata fedha ya kurudi nayo nyumbani, sasa nyie mnamtoza kabla hajauza chochote au hata kama hajauza. Acheni hiyo tabia," alisema.

  Alimtaka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Bw. Robert Lweyo aimarishe usimamizi wa minada na kujua idadi ya mifugo ambayo inaingizwa, inayouzwa na ile inayobaki ambayo imeshindikana kuuzwa.

  "Jipange wewe Mwenyekiti na timu yako ya watoza ushuru mfuatilie agizo hili. Mkiwa wavivu ndiyo mnakuja na maamuzi haya ya jumla jumla ya kuanza kutoza ushuru hata mtu akiwa njiani anakuja mnadani kutafuta fedha," alisema Waziri Mkuu.

  Mapema, akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Bw. Ponsiano Nyami alisema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ofisi kwa sababu majengo ya iliyokuwa ofisi ya wilaya hivi sasa yanatumiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa hali iliyowalazimu wahamie kwenye ofisi za Halmashauri.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMISI, MACHI 3, 2016.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akisalimiana  na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Dutwa  akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi3, 2016.Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum , Esther Midimu. 
    Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akikagua ujenzi wa nyumba ya kuishi ya Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi akiwa akika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 3, 2016.
    Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  akiweka jiwe la msingi la Ofisi ya CCM ya wilaya  ya Bariadi akiwa katika  ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dk. Adolf Rutayuga, (Kulia) akisisitiza jambo wakati alipokuwa ikitangaza wa kuzindua Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo, utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree)   Katikati ni Mkurugenzi Udhibiti Ubora Rasmalimali watu , Edmund Kinwasi na Kaimu Mkurugenzi  Idara ya  Ufuatiliaji  Tathimini na Uthibiti wa baraza hilo , Christina Kumwenda. Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Katibu Mkuu wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dk .Adolf Rutayuga,  akipofya kitufe cha komputa  kuashiria Uzinduzi  rasmi wa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo, utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree)  wanaoshuhudia kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi  Idara ya  Ufuatiliaji  ,Tathimini na Uthibiti ,Christina Kumwenda,  Mkurugenzi  udhibiti  ubora  rasmalimali watu Edmund Kinwas, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Vyuo ushauri na Mipango Alfred Kilasi,Mkurugenzi Mafunzo na Upimaji Bakari Issa (kushoto) na  Afisa Mifumo ya Kompyuta wa baraza hilo , Daud Mabena.Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.

   Kaimu Katibu Mkuu wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt .Adolf Rutayuga(Kushoto) akifafanua jambo  kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ( hawapo pichani) kuhusiana na Uzinduzi  wa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree)    wapili kushoto ni   Mkuu wa Kitengo cha Udahili Seremani Majindo, Mkurugenzi wa Mfumo na Upimaji,Bakari Issa  na  Kaimu Mkurugenzi Idara ya vyuo na ushauri na Mipango.Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam 

  BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), limetangaza ufunguzi rasmi wa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo, utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree”).


  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maelekezo na Msaada kwa Taasisi wa NACTE, Dk. Adolf Rutayuga amesema kuwa, kwa mwaka wa masomo wa 2015/16, Baraza liliratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo mbali mbali kwa kozi za astashahada (Cheti) na stashahada (Diploma) kwa mafunzo ya afya na ualimu yaliyoidhinishwa na Baraza. ameongeza kuwa, Baraza pia  lilishirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, kuratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo mbali mbali kwa kozi za shahada ya kwanza kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)).

  “Mifumo hii miwili ilifanyika kwa ufanisi mkubwa na uliwawezesha  waombaji kudahiliwa. Mifumo hii ya udahili imekuwa na mafanikio yafuatayo: Kudhibiti udanganyifu katika udahili uliotokana na baadhi ya waombaji kutumia vyeti vya bandia, kuwapunguzia waombaji gharama za kuomba udahili katika vyuo mbalimbali, kuondoa uwezekano wa mwombaji udahili mmoja kudahiliwa zaidi ya mara moja na kuwanyima waombaji wengine nafasi, kuiwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi za waombaji udahili kwa ajili ya kufanikisha mipango ya elimu nchini, na kuwawezesha waombaji udahili kujiunga na mafunzo kwenye taasisi zinazotambuliwa na Serikali,” alieleza.


  Dk Rutayuga alieleza kuwa, kwa kutambua mafanikio ya udahili wa pamoja  yaliyopatikana,  Serikali ya kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, imeamua kuwa maombi yote ya udahili kwa ajili ya mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (Bachelor Degree) yafanywe kupitia kwenye Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS). 


  Amefafanua kwamba. Baraza linautangazia umma kuwa, kuanzia mwaka wa masomo 2016/2017 udahili wa kozi zote nchini utafanywa kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) unaosimamiwa na NACTE, Vyuo Vikuu  na taasisi za Elimu zote nchini Tanzania zinazotoa mafunzo ya Cheti na Diploma kutodahili wanafunzi nje ya mfumo wa udahili wa Pamoja kuanzia mwaka wa masomo 2016/17.


  “Tunapenda kutoa taarifa pia kuwa, maombi ya kujiunga na kozi za Cheti na Diploma yataanza kupokelewa rasmi kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja kuanzia tarehe 4 Machi 2016, saa sita mchana. Baraza pia litaanza kupokea rasmi maombi ya kujiunga na kozi za Shahada (Degree) kwa wahitimu wenye Diploma kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja kuanzia tarehe 4 Machi 2016, saa sita mchana,” 


  Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kuomba mafunzo kwa kutumia Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS), alisema Baraza linashauri waombaji watembelee tovuti ya Baraza ambayo ni www.nacte.go.tz.

  0 0
 • 03/03/16--12:21: Article 3


 • 0 0
 • 03/03/16--12:22: Article 2


 • 0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwaongoza Marais wa Kenya, Uganda, Makamu wa Rais wa Sudani Kusini pamoja na Burundi kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mitambo itakayotumika katika ujenzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimwagilia mti maji pamoja na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(Nairobi) Gabriel Negata mara baada ya uzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Nchi.


older | 1 | .... | 1145 | 1146 | (Page 1147) | 1148 | 1149 | .... | 3272 | newer