Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1144 | 1145 | (Page 1146) | 1147 | 1148 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Mhe. William Lukuvi akiangalia maendeleo ya kazi ya ubomoaji wa jengo la ghorofa kumi na sita (16) ambapo ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ambapo kwa sasa zimebaki ghorofa sita (6) tu.
  Mafundi wakiendelea na Ubomoaji wa jengo la ghorofa kumi na sita (16) ambapo kwa sasa zimebaki ghorofa sita (6) tu.

  0 0

  Mhasibu wa Wizara ya Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Godfrey Osmund akimweleza Naibu waziri wa wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura jinsi atakavyozikatia risiti fedha ambazo wadau wa michezo wamezitoa kwa ajili ya kuichangia Timu ya Taifa ya wanawake ya Mpira wa miguu ya Twiga Stars.
  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi leo Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund shilingi milioni mbili zilizotolewa na Mohammed Dewji kwaajili ya kuisaidia timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Hadi sasa wadau wa michezo wameshaichangia timu hiyo shilingi milioni 17.Picha na Anna Nkinda

  0 0

  RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Gianni Infantino kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) mwishoni mwa wiki nchini Uswisi.

  Katika barua hiyo, Malinzi amesema TFF ina imani na ahadi zake za kuendeleza mpira wa miguu, na kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ataendelea kushirikiana naye katika kila jambo katika nafasi yake hiyo na kumtakia kila la kheri na mafanikiko mema.

  0 0


  RATIBA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU DADA JESSIE CHIUME KWA SAFARI YAKE YA MILELE TANZANIA.

  Ratiba kamili ya kuaga mwili wa mpendwa Da Jessie ni kama ifuatavyo.

  1. Kuanzia Jumatatu tutaendelea kujumuika nyumbani kwa marehemu, 44 Fleetwood Ave, Mt. Vernon, NY, 10552

  2. Jumatano, Machi 2, 2016


  Flynn Memorial Home,
  1652 Central Park Avenue,
  Yonkers, NY 10710.


  Heshima za mwisho (Viewing): 4pm-7pm


  Ibada (Service): 7pm-8pm

  Baada ya shughuli kumalizika, tutatoa tangazo la wapi pa kukusanyika usiku huo kwa wale ambao watataka kujumuika na wafiwa.

  Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuondoka New York kwenda Dar es Salaam, Tanzania asubuhi ya Alhamisi Machi 3, 2016.

  Na mazishi yatafanyika sikuya jumamosi ya ter, 5, 2016 katika makaburi ya Kinondoni Dar-Es-Salaam.

  Mwenyezi Mungu akipenda Da Jessie atapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele siku ya weekendi mara baada ya kuwasili Dar es Salaam siku ya Ijumaa, Machi 4. Taarifa zaidi zitafuata.

  Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mpendwa wetu Da Jessie Wayasa Mgeni Chiume mahala pema Peponi. Ameen.

  Link ya kutoa rambirambi ni:


  Kwa taarifa zaidi:
  Michael Chiume: # 646-662-6999
  Chris Litunwa: #614-592-6231
  Nathan Chiume:# 646-552-6347
  Hajji Khamis:# 347-623-8965

  0 0

  DIWANI wa kata ya Mangaka Halima Mchoma akikabidhi vitabu kwa mmoja wa walimu wakuu wa shule za msingi nne za kata ya Mangaka hii leo kwenye viwanja vya shule ya msingi Mangaka.

  ---------------------
  Na Clarence Chilumba, Masasi.

  DIWANI wa kata ya Mangaka jimbo la Nanyumbu mkoani Mtwara, Halima Mchoma amenunua vitabu 488 vya masomo ya sayansi na stadi za kazi vyenye thamani ya shilingi milioni 1,157,000/= kwa wanafunzi wa darasa la nne wa shule za msingi za kata hiyo.

  Shule zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na shule ya msingi Mangaka,Nahawara,Ndwika 2 naMtokora ambazo zote ni kutoka katika kata ya Mangaka Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara.

  Vitabu alivyovinunua diwani huyo ni pamoja na vitabu 388 vya somo la sayansi, vitabu 100 vya somo la stadi za kazi pamoja na boksi nne za peni zenye peni 400 ambazo watapewa walimu wa shule za msingi katani humo.

  Diwani huyo ameamua kununua vitabu hivyo pamoja na peni kwa walimu wote wa kata hiyo kwa fedha zake za mfukoni kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya kutoa elimu bila malipo.

  Akizungumza leo wakati wa kukabidhi msaada huo kwa walimu wakuu wa shule hizo katika viwanja vya shule ya msingi Mangaka alisema ameamua kununua vitabu vingi vya sayansi kutokana na ugunduzi wa gesi mkoani humo ambao wengi wa wataalamu wanaohitajika ni wale waliosoma masomo ya sayansi.

  Alisema kutokana na kero ya upungufu wa vitabu kwenye kata hiyo waliyokuwa wanailalamikia walimu ndicho kilichomsukuma kuamua kununua vitabu hivyo ambapo kwa sasa kila mtoto wa darasa la nne atatumia kitabu kimoja kama inavyotakiwa kitaalamu.

  Mchoma alisema kwa vitabu vya awamu ya kwanza alivyonunua vina thamani ya sh.1.2 milioni na kwamba lengo lake kwa sasa ni kutatua changamoto zilizopo kwenye shule hizo ikiwemo upungufu wa madawati,matundu ya vyoo,vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za walimu.

  “Nimeguswa na tatizo la wanafunzi wa kata yangu kutumia kitabu kimoja zaidi ya wanafunzi wawili…ndio maana nimeamua kununua vitabu hivi ambavyo kwa sasa naamini kila mwanafunzi anayesoma darasa la nne kwenye kata hii atatumia kitabu chake na nitafanya hivi kwa kipindi chote cha uongozi wangu ndani ya miaka mitano,”alisema Mchoma.

  Alisema pia amefanya uamuzi huo baada ya kuguswa na namna walimu wa kata hiyo wanavyojituma katika kufundisha kunakopelekea shule za kata hiyo kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani mbalimbali ikiwemo yale ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka 2015.

  Kwa upande wake ofisa elimu taaluma wa shule za msingi wilayani Nanyumbu Stephen Urassa alimpongeza diwani huyo kwa namna alivyoonesha njia na kwamba msaada huo umekuja wakati muafaka ambao wanafunzi wa darasa la nne wanajiandaa kufanya mitihani ya majaribio.

  “Nimekuwa Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu tangu mwaka 2008…lakini sijawahi kuona kiongozi yeyote wa kisiasa akitoa msaada wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za msingi hivyo hii inaonesha ni kwa namna gani wananchi wa kata ya Mangaka hawakufanya makosa kukuchagua”.alisema Urassa.

  Naye mratibu Elimu kata wa kata ya Mangaka Fidelis Hokororo alisema kata hiyo ina jumla ya wanafunzi 253 wa darasa la nne ambapo kutokana na msaada huo kwa sasa kila mwanafunzi wa darasa la nne atakuwa anatumia kitabu kimoja cha sayansi huku vitabu 135 vikiwa zidifu.

  Alisema kwa upande wa vitabu vya stadi za kazi ambavyo ni 100 kwa wastani kila wanafunzi watatu watakuwa wanatumia kitabu kimoja na kwamba watatumia baadhi ya vitabu vilivyopo kwenye shule hizo ili kufikia lengo la kila mwanafunzi kutumia kitabu kimoja.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akionyesha usinga na mkuki ambavyo alipewa na wazee wa Kisukuma wa Busega katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Lamadi Machi 2, 2016. Wazee hao pia walimbatiza jina la Massanja.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutanowa hadhara katik kijiji cha Lamadi wilayani Busega Machi 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Lamadi wilayani Busega kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara wenye uwanja wa michezo Machi 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Mbunge wa Busega Dkt Raphael Chegeni (kushoto) na Mbunge wa zamni wa jimbo hilo, Dkt Titus Kamani ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Simiyu wametangaza rasmi kuzika tofauti zao na kushirikiana kuleta maendeleo kwenye jimbo hilo. Pichani viongozi hao wakiwadhihirishia wananchi kuwa hawana chukui wala ugomvi tena na kuwa uchaguzi umekwisha katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kwenye kijiji cha Lamadi wilayni Busega Machi 2, 2016. .
  Mbunge wa Busega Dkt Raphael Chegeni (kushoto) na Mbunge wa zamni wa jimbo hilo, Dkt Titus Kamani ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Simiyu wametangaa rasmi kuzika tofauti zao na kushirikiana kuleta maendeleo kwenye jimbo hilo. Pichani viongozi hao wakiwadhihirishia wananchi kuwa hawana chukui wala ugomvi tena na kuwa uchaguzi umekwisha katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kwenye kijiji cha Lamadi wilayni Busega Machi 2, 2016.

  0 0


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.PICHA NA IKULU.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kando ya Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Mkoani Arusha, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuimarisha mahusiano hususani katika masuala ya kiuchumi.

  Baadhi ya maeneo waliyokubaliana kutilia mkazo katika mahusiano hayo, ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo inayounganisha nchi mbili ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kukuza biashara na kuzalisha ajira kupitia viwanda.Rais Uhuru Kenyatta amesema amefurahishwa sana kuona Rais Magufuli yupo tayari kuhakikisha nchi ya Kenya na Tanzania zinakuwa karibu, na miradi ya maendeleo inaharakishwa.

  "Kwa sababu nia yetu sisi ni kuona maendeleo ambayo yatagusa mwananchi wa kawaida, tumalize umasikini, uchumi ukue, na hivyo hatuwezi kufanya tukiwa tumetengana" Amesisitiza Rais Kenyatta.

  Kwa upande wake Rais John Pombe Magufuli, amesema Tanzania na Kenya zina kila sababu ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara hasa katika ujenzi wa viwanda utakaozalisha ajira kwa kuwa watu wake ni wamoja.

  "Wazee wetu Mzee Kenyatta na Mzee Nyerere walijenga mazingira mazuri ya kuwa na nchi hizi mbili wakati wakipigania uhuru, sasa sisi vijana wao ni wakati wetu kwenda mbele kwa ajili ya maendeleo" amebainisha Rais Magufuli.Dkt. Magufuli amebainisha kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinajenga mahusiano na ushirikiano zinalenga kupata manufaa hayo ya kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wake.

  Ameutaja mradi mmojawapo kuwa ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tanzania kwenda nchini Kenya kupitia Namanga, na akaongeza kuwa Tanzania itakapoongeza uzalishaji wa umeme na kuanza kuvuna gesi, itaiuzia pia Kenya, halikadhalika Kenya nayo itauza bidhaa zake Tanzania.

  Kabla ya kukutana na Rais Kenyatta, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuzidisha mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda ambapo Rais Magufuli amemhakikishia kuwa serikali yake itakamilisha ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard Gauge" ili kurahisha usafirishaji wa bidhaa na watu.

  Rais Kagame amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake bora uliolenga kuimarisha uchumi, ikiwemo kuimarisha bandari ya Dar es salaam ambayo Rwanda inaitegemea na ujenzi wa Reli ya Kati ambayo pia ni tegemeo kubwa kwa uchumi wa Rwanda.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiano, IKULU
  Arusha
  02 Machi, 2016

  0 0

  Wadau mbalimbali wameisifu kazi nzuri iliyofanywa na NiceMedia Production. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati mbalimbali wadau hao wamesema wamebahatika kuona nyimbo zlizofanyika NiceMedia na kusema kuwa zina ubora unaokubalika kimataifa.

   Wametolea mfano baadhi ya nyimbo ambazo wamezitazama kupitia YouTube ikiwa ni pamoja na wimbo Unaozungumzia mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino ulioimbwa na Mrs Elihuruma Chao unaoitwa "Albino hawana hatia" na kusema kwamba umekidhi vigezo vyote vya kimataifa Wameendelea kusema kuwa Wimbo mwingine ambao umeonekana kuwa bora ni huu ulioimbwa na Oculy Pendaely unaoitwa "Najivunia kuwa na Yesu" ambao unabeba album yake ya kwanza iitwayo "Najivunia Kuwa na Yesu". 
   Tazama wimbo huu wa OCULY Pendaely ambao umefanyika katika studio za NiceMedia Production jijini Arusha chini ya producer Elihuruma Chao ambaye ndiye aliyifanya Audio ya wimbo huu pamoja na Shooting ya Albam ya mwimbaji Oculy Pendaeli ya "Najivunia kuwa na Yesu' ikiwa ina nyimbo takriban nane.Ukibahatika kupata albam hii utabarikiwa zaidi. NiceMedia ni studio ambayo inarekodi nyimbo za injili Pekee pamoja na matukio mmbalimbali kama vile Vipindi vya radio na Televishei,Harusi ,Ubarikio nk.

  0 0

  Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Jumatano Machi 2, 2016 kwa kauli moja umemteua Dkt Libérat Mfumukeko (pichani) kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo. 

   Dkt Mfumukeko, ambaye anayetarajiwa kuanza kazi rasmi mwezi ujao, kuchukua nafasi ya Dkt. Richard Sezibera aliyemaliza muda wake baada ya kufanya kazi tokea April 2011, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, akishughulikia fedha na utawala, nafasi aliyoteuliwa mwaka jana. 
   Kabla ya kujiunga na EAC, Dkt. Mfumukeko alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nishati na Madini la Burundi (REGIDESO) na pia alikuwa mwenyekiti wa Kamati Endeshaji ya Nishati ya Afrika Mashariki - East African Power Pool (EAPP). 
   Mkutano huo, ukiendeshwa chini ya Mwenyekiti wake Rais Dkt John Pombe Joseph Mgufuli, pia uliridhia nchi ya Sudani ya Kusini kuingizwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, kungana na Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi na Tanzania.

  0 0  0 0


  0 0

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge amefanya ziara ya kikazi katika mikoa ya Mara na Mwanza leo na jana katika harakati ya kutatua kero ya maji kwa wananchi. Mhe. Lwenge ambaye ana dhamana ya kuinua na kuendeleza Sekta ya Maji na Umwagiliaji, amekagua miradi mbalimbali katika maeneo tofauti huku akizungumza na viongozi, wataalamu, wakandarasi na wananchi kwa nia ya kutafuta suluhisho la kudumu la tatizo ya maji.

  Lengo kubwa la ziara hiyo ni kujua sababu ya kusuasua kwa utekelezaji wa baadhi ya miradi na kusukuma utekelezaji wa miradi inayotekelezwa katika mikoa hiyo ikamilike kwa wakati na kuleta matokeo mazuri kwa wananchi na maendeleo ya taifa kwa ujumla. Katika ziara hiyo Mhe. Lwenge alitembelea miji ya Musoma, Magu, Mwanza na Sengerema.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge, akiwa kwenye Mradi wa Kuzalisha na Kusambaza Majisafi wa Musoma Mjini ambao utekelekezaji wake utagharimu Sh. Bil 45 ambao unategemewa kukamilika Juni, 2016 na unategemewa kutoa huduma ya maji katika Manispaa ya Musoma kwa zaidi ya asilimia 90.
  Mtambo wa Kusafisha na Kutibu Maji ambao ni moja ya sehemu ya Mradi wa Kuzalisha na Kusambaza Majisafi wa Musoma Mjini ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 75 kwa sasa.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa tanki la Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) lenye mita za ujazo 135,000 eneo la Rwamlimi, Halmashauri ya Manispaa ya Musoma ambalo linategemewa kuhudumia wakazi 1,000.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Faraja Nyalandu, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Shule Direct na Aneth Gerana wakikimbia mbio za kilometa 21.1 wakati wa mbio za Kili Marathon. Shule Direct walishiriki mbio hizo kwa ajili ya kuchangisha fedha kuwezesha upatikanaji wa kompyuta zenye matini ya masomo tisa ya Sekondari kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia katika shule za Ufundi Sekondari Moshi na Njombe Sekondari ya viziwi.
  Wakiwa wenye nyuso za furaha, Faraja Nyalandu, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Shule Direct, Aneth Gerana na wengine kutoka Shule Direct na marafiki wa Shule Direct mara baada ya kumalizi mbio za kilometa 21.1 wakati wa Kili Marathon.


  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiyahiyo  jijini Arusha  Machi 2, 2016.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini ya Kanuni za Madili ya Mfuko wa Sekta Binafsi wakati wa Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya hiyo  jijini Arusha  Machi 2, 2016.
  Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda akijiandaa kuweka saini ya Kanuni za Madili ya Mfuko wa Sekta Binafsi wakati wa Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha  Machi 2, 2016

  Rais Paul Kagame  wa Rwanda akiweka saini ya Kanuni za Madili ya Mfuko wa Sekta Binafsi wakati wa Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha  Machi 2, 2016.
  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiweka saini ya Kanuni za Madili ya Mfuko wa Sekta Binafsi wakati wa Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha  Machi 2, 2016
  Kijana Simon Sahaya Mollel (18) mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Mzumbe ya mjini Morogoro akionesha dola 1500 alizokabidhiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  kama zawadi baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa kuandika Inshawakati wa Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha  Machi 2, 2016.
  Wanafunzi walioshinda mashindano ya Insha ya EAC wakipata selfie na viongozi baada ya Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha  Machi 2, 2016.PICHA NA IKULU

  0 0  0 0
  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Makoye Alex Nkenyenge akizungumza wakati wa kikao baina ya Wizara, TFF na Kampuni ya MaxCom kuhusu matumizi ya mfumo wa Kielektroniki katka ukataji Tiketi kwa ajili ya kuingilia wakati wa mechi mbalimbali jana jijini Dar es Salaam. Mkakati huo ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Waziri Mkuu alilolitoa wakati akiongea na wadau wa michezo hivi karibuni.
  Mwakilishi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Boniphace Wambura (kulia) akichangia hoja wakati wa kikao baina ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, TFF pamoja na Kampuni ya MaxCom ili kujadili kuhusu uanzishwaji wa matumizi ya mfumo wa Kielektroniki katika ukataji Tiketi kwa ajili ya kuingilia wakati wa mechi mbalimbali leo jijini Dar es Salaam. Mkakati huo ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Waziri Mkuu alilolitoa wakati akiongea na wadau wa michezo hivi karibuni.Kushoto ni Afisa Tehama wa wizara hiyo Nuru Bakari.
  Mwakilishi wa Kampuni ya MaxCom Deogratius Lazaro (katikati) akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, TFF pamoja na Kampuni ya MaxCom ili kujadili kuhusu uanzishwaji wa matumizi ya mfumo wa Kielektroniki katika ukataji Tiketi kwa ajili ya kuingilia uwajnjjani wakati wa mechi mbalimbali leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Muhasibu wa TFF Daniel Msangi na kulia ni Mwakilishi mwenza wa MaxCom Erick Charles.
  Mwakilishi wa Kampuni ya MaxCom Erick Charles (wapili kutoka kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, TFF pamoja na Kampuni ya MaxCom ili kujadili kuhusu uanzishwaji wa matumizi ya mfumo wa Kielektroniki katika ukataji Tiketi kwa ajili ya kuingilia uwajnjjani wakati wa mechi mbalimbali leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Ugavi na Ununuzi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Cecilia Kasonga, Mwakilishi wa Kampuni ya MaxCom Deogratius Lazaro na Muhasibu wa TFF Daniel Msangi.
  Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kujjadili namna ya kuanza kwa matumizi ya mfumo wa Elekroniki katika ukataji wa tiketi za kuingilia uwanjani kwenye mechi mbalimbali. Kikao hicho kimejumuisha wajumbe kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo,TFF na Kampuni ya MaxCom ambao ndiyo wataalamu wa kuendesha mfumo huu.
  Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kujjadili namna ya kuanza kwa matumizi ya mfumo wa Elekroniki katika ukataji wa tiketi za kuingilia uwanjani kwenye mechi mbalimbali. Kikao hicho kimejumuisha wajumbe kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo,TFF na Kampuni ya MaxCom ambao ndiyo wataalamu wa kuendesha mfumo huu.

  0 0

  Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bi. Suzan Mshakangoto akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu taratibu zinazotakiwa kuzingatiwa na taasisi za Serikali katika kuimarisha matumizi sahihi na salama ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kuendesha mifumo ya Tehama Serikalini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usimizi wa Huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wakala hiyo. 
  Mkurugenzi wa Usimamizi wa Huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bw. Benedict Ndomba akifafanua kuhusu mpango wa Serikali wa kuimarisha mawasiliano katika mifumo ya TEHAMA Serikalini.
  Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo

  Na Beatrice Lyimo – Dar es Salaam
  Wakala ya Serikali mtandao (e-Government Agency) imezishauri Taasisi zote za Umma ,Wizara, Idara zinazojitegemea, Sekreterieti za Mikoa, Wakala na Mamlaka za Serikali ,Bodi, Tume, Mabaraza, Mifuko, Mashirika ya umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufuata miongozo na viwango vilivyotolewa Wakala hiyo katika uanzishaji na usimamizi wa mifumo ya Tehama Serikalini.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bi. Suzan Mshakangoto alipokuwa akitoa maelekezo na ufafanuzi wa taratibu zinazotakiwa kuzingatiwa na taasisi hizo kwa lengo la kuimarisha matumizi sahihi na salama ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kuendesha mifumo ya Tehama Serikalini.

  Bi. Mshakangoto amesema kuwa miongozo na viwango hivyo vinalenga kuziwezesha taasisi za umma kujenga mifumo inayoendana na mahitaji halisi ya taasisi husika na kuepuka mifumo inayojengwa kwa shinikizo la wafanyabiashara, wafadhili au kwa matakwa ya mtu binafsi.

  “ Taasisi zote zikitumia miongozo ya viwango tuliyoweka, Serikali itakuwa na uwezo wa kuepuka urudufu wa mifumo na kupunguza gharama kubwa za uendeshaji kwa kuwa na mifumo endelevu yenye gharama halisi inayofuata viwango vya Usalama katika kulinda taarifa na data za Serikali” Alifafanua Meneja huyo.

  Amezishauri taasisi hizo kuwasilisha maandiko ya mifumo mipya ya TEHAMA na kujaza taarifa za mifumo au miradi ya TEHAMA iliyopo katika mfumo wa kukusanya na kutunza taarifa za miradi ya TEHAMA Serikali ili iweze kuthibitishwa iwapo imefuata miongozo na viwango vilivyowekwa kabla ya kujengwa na kusakinishwa.

  Akitoa ufafanuzi kuhusu wafanyabiashara wanaojihusisha na miradi au utengenezaji wa mifumo ya TEHAMA Serikalini amesema kuwa wanashauriwa kufuata miongozo na viwango hivi ili kujua mahitaji halisi ya Serikali na kuweza kujenga mifumo ya TEHAMA endelevu na inayoleta tija kwa umma.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usimizi wa Huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bw. Benedict Ndomba ameeleza kuwa mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa mifumo yote ya TEHAMA ya Serikali inakuwa na mawasiliano na kubadilishana taarifa mbalimbali.

  Amesema kuwa Serikali imekuwa ikiweka msisitizo wa matumizi ya TEHAMA kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji kwa kuwawezesha wananchi na wadau mbalimbali kupata huduma za Serikali kwa gharama nafuu kwa njia ya Mtandao.

  Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2012.kwa sheria ya Wakala za Serikali Na. 30, Sura ya 245 ya mwaka 1997. Wakala hii ina majukumu na mamlaka ya kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao nchini Tanzania.

older | 1 | .... | 1144 | 1145 | (Page 1146) | 1147 | 1148 | .... | 3278 | newer