Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATUA MTWARA KWA ZIARA YA SIKU MOJA

0
0
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mtwara baada ya kuwasil kwenye uwanja wa ndege ea Mtwara kwa ziara ya siku moja mkoani humo leo Februari 27, 2016. Kulia ni Mkuu wa mkoa huo Mhe. Halima Denengo (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tovuti ya Proin Promotions yavamiwa, Kurudi hewani mara baada ya tatizo kushughulikiwa

0
0
Tunasikitika kuutangazia umma wa watanzania na wadau wetu kwa ujumla kuwa tovuti yetu ya www.proinpromotions.co.tz imevamiwa na watu wanaojiita Classic Flame kwa kitaalamu kunaitwa Hacked.
Timu nzima ya Proin Promotions Ltd inapenda kuwataarifu kuwa wadau wetu kuwa tunalifanyia kazi na kuhakikisha tunaongeza ulinzi katika tovuti yetu na kuirudisha hewani. Tunatarajia baada ya kuirudisha hewani itakuwa imara zaidi na zaidi na tunaamini hii ni changamoto tu katika sekta ya teknolojia.
Tunawaahidi kuwa tovuti yetu itarudi hewani mara baada ya wataalamu wetu kulishughulikia hilo tatizo kwani ni tatizo ndogo.

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

0
0

SIMU.TV:  MKuu wa wilaya ya Lindi amemtaka mkurugenzi wa manispaa hiyo kuhakikisha watumishi wa halmashauri wanashiriki katika zoezi la usafi wa wilaya;https://youtu.be/EFdPVJML0cE
 SIMU.TV:  Utoroshaji wa korosho pamoja na ucheleweshaji wa malipo kwa wakulima mkoani Mtwara wazua mapya mkoani humo;  Utoroshaji wa korosho pamoja na ucheleweshaji wa malipo kwa wakulima mkoani Mtwara wazua mapya mkoani humo.
 SIMU.TV:  Bondia Francis Cheka  na bondia raia wa Serbia Gearad Ajetovic kutunishinana misuli leo katika uwanja wa leaders Club Dar es Salaam;https://youtu.be/A7s1UFbZUeo
 SIMU.TV:  Mswis Gianni Infantino atwaa taji la urais wa shirikisho la kandanda duniani FIFA akimrithi Sepp Blatter aliyejiuzuru mwaka jana; https://youtu.be/jfgAPKt24Ws
 SIMU.TV:  Jifunze mengi kutoka kwa Kamshina wa haki za binadamu kutoka visiwani Zanzibar akikuelimisha mengi kuhusu haki za watotohttps://youtu.be/LmbcOMMkWmA
 SIMU.TV:  Fahamu mambo mengi kutoka kwa makocha wakikujuza kuhusu masuala ya michezo ususani maendeleo ya mchezo wa kuogelea https://youtu.be/QvAXrxn7jcE

BENKI YA NMB MBEYA YAZINDUA KITUO CHA BIASHARA (NMB BUSINESS CENTER)

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa NMB Business Center Mkoa wa Mbeya akizungumza na wafanyabiashara katika uzinduzi huo
Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bi Ineke Bussemaker akiwakaribisha wafanyabiashara waliofika katika uzinduzi wa NMB Business Center Jijini Mbeya
Mkuu wa Idara ya Biashara Bw. James Meitaron akimfafanulia jambo Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker. Anaeshuhudia katikati ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi wa benki hiyo Bw. Abdulmajid Nsekela.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kituo cha biashara cha NMB (NMB BUSINESS CENTER) Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker na Afisa Mkuu wa Huduma kwa Wateja Binafsi Bw. Abdulmajid Nsekela katika uzinduzi wa kituo hicho hivi karibuni.
Meneja wa NMB Business Center Jijini Mbeya Bi. Mary Ngalawa akimuonyesha Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker maeneo mbalimbali ya kituo hicho.
Benki ya NMB imezindua kituo cha biashara (NMB BUSSINESS CENTER) mkoani Mbeya kitakachokuwa kikihudumia wateja wafanyabiashara na kuboresha uendeshaji wa biashara kwa wateja wafanyabiashara katika Mkoa huo.
Akiongea katika uzinduzi wa kituo hicho Afisa Mkuu wa wateja binafsi wa NMB Abdulmajid Nsekela amesema kuwa lengo la vituo vya biashara kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini ni kuboresha utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara na hivyo kuchangia katika kuchochea ufanisi wa wafanyabiashara na kukuza uchumi. Hivyo wanataraji kuendelea kuwafikia wafanyabiashara popote walipo kwa huduma bora.
Aidha Afisa huyo wa Wateja Binafsi ameeleza kuwa katika mpango huo wanataraji kufanikisha malengo ya wateja wao ambao ni wafanyabiashara wakubwa, wa kati, wadogo sambamba na wakulima kwa kuboresha biashara ya kilimo.
Pia Bw. Nsekela amefahamisha kuwa pamoja na kufanya shughuli za kibenki, NMB pia inachangia shughuli za kijamii katika kuchangia maendeleo na wanatenga pato lao la mwaka kama mchango wao katika sekta ya afya na elimu ikiwa na lengo la kuiunga mkono Serikali ambapo wanatenga asilimia moja katika pato la mwaka kufanya shughuli hizo. 
Afisa huyo wa NMB amewataka wateja wa kati kuchangamkia fursa hiyo ambayo inawapa nafasi wafanyabiashara kupanda kutoka daraja moja kwenda lingine kulingana na ufanisi wa vituo vya biashara na elimu ya kifedha watakayopatiwa na NMB. 
Kwa upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi wa kituo cha biashara cha NMB mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro amewataka wafanyabiasha na wakazi wa Mkoa huo kutumia fursa za kibenki ambazo zinatolewa ili kufikia malengo yao ya kibiashara.
Mh. Kandoro amefahamisha kuwa kabla ya kuchukua mkopo wanatakiwa kufanya tathmini na kujua biashara gani wanaweza kufanya na kuweza kufanya marejesho ya benki.
Pia Mh. Kandoro aliwataka viongozi wa benki ya NMB kuangalia suala la riba katika mikopo wanayotoa kwa vile wananchi wengi wanaogopa kukopa kutokana na baadhi ya mabenki nchini kutoza riba kubwa jambo linalowawia vigumu wafanyabiasha wadogo kujenga kasumba ya kuhofia mikopo kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi na kupanua wigo wa biashara zao. 
Benki ya NMB pia imejikita kwenye shughuli za kilimo kwa kuwezesha urahisi wa upatikanaji wa pembejeo ambapo hivi karibuni wameanzisha mpango wa kuwapatia wateja wake matrekta kwa gharama nafuu baada ya kuingia mkataba na kampuni ya Jebiz ambao ni wasambazaji wa matrekta.
Benki ya NMB ina matawi 175, Mashin za kutoa pesa (ATM) zaidi ya 600 na Mawakala ambao wanarahisisha shughuli za kibenki zaidi ya 450 pia wamejiunga na mitandao ya simu yanayotoa huduma za kifedha kwa njia ya simu. 
Kwa upande wa mikopo Mkuu wa Kitengo cha Biashara Bw. James Meitaron ameeleza utaratibu mzima wa utoaji wa mikopo kwamba kiwango ambacho wanaanzia kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ni kuanzia Shilingi milioni moja hadi milioni thelathini (milioni 30) mkopo ambao unapatikana ndani ya siku mbili na kuwa benki hiyo imempa mamlaka Meneja wa tawi kufanikisha mikopo ya kiwango hicho.
Kama biashara yako imeanza kukua, kituo cha biashara ambapo kwa Mbeya kipo NMB Mwanjelwa kinatoa mkopo kuanzia milioni 30 hadi bilioni 2.
Meitaron amesema kuwa riba ya mikopo kwa benki hiyo haizidi asilimia 23 kwa mwaka na kadiri unavyolipa mkopo riba inapungua mpaka kufikia asilimia 18 kulingana na mkopo uliokopa.

.VURUGU ZA MACHINGA ZAZUA TAFRANI LEO JIJINI MBEYA

0
0
Baadhi ya Vibanda vya Biashara vya Wafanyabiashara Ndogondogo Maarufu kama Machinga Vikiteketea kwa Moto mara baada ya Wafanya Biashara hao wa Eneo la Sido na Stendi ya Kabwe Jijini Mbeya kuanzisha Vurugu Baada ya Kubomolewa Vibanda vyao vya Biashara katika maeneo waliyokuwa wakifanyia Biashara Zao.
Jitihada za kuzima Moto ulio washwa na Wamachinga wa Kabwe na Sido zikifanyika kutoka kwa Jeshi la Zima Moto Jiji la Mbeya katika Vurugu zilizo Dumu kwa Muda kuanzia Asubuhi ya Leo na kupelekea Wamachinga hao Kuchoma Matairi Barabarani na Baadhi ya Masalia ya Vibanda vyao mara baada ya Kubomolewa Vibanda vyao vya Biashara.
Jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza Ghasia kikiwa Ngangari kuhakikisha hali ya Usalama ina kuwa Shwari na Vurugu kutoendelea...
Baadhi ya wapiga Debe wa Stendi ya Kabwe wakiwa hawana nongwa na Mtu bali wakiendelea kutimiza agizo la Rais Dkt.John Pombe Magufuli kufanya Usafi kila Juma Mosi ya mwisho wa Mwezi na hapo wakiwa Sambamba na Vifaa vyao vya kufanyia Usafi mbele ya Jeshi la Polisi kama waonekanavyo katika Taswira.
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.

Markaz Shaafiyatul Azhariyah - Salasala , Dar es salaam yafunguliwa leo Rasmini.

0
0

Kituo cha Markaz Shaafiyatul Azhariyah leo kumefunguliwa rasmini kwa ufunguzi wa Msikiti , Kisima na Madrasa maeneo ya Salasala jijini Dar es salaam.
Kwa Niaba ya Uongozi wa kituo tunatoa Shukran za dhati kwa wote walio shiriki kwa hali na mali katika Ujenzi wa sehemu ya kituo hiki.
Shukran ziwaendee Blogs za Kijamii zote  kwa kurusha habari zetu na kuwafika watu mbalimbali.
Linalo fuata sasa ni Usajili maalum wa vijana ambao watakuwa ni mwanzo Katika project hii kutoka mikoa Mbalimbali.
Ombi kwa kila mpenda kheri safari yetu ndio imeanza tushirikiane kwa pamoja katika kufanya ya kheir.

Kwa mawasiliano zaidi.au Michango Tafadhali Wasiliana , 0715800772,0673800772,
face book :- Kijana wa Kiislam Dsm .


                                                  Shukran Jazakum llahu khairan.

Na Mratibu Msimamizi wa PROJECT
 GHALIB NASSOR MONERO.
Ufunguzi rasmi wa kituo cha Markaz Shaafiyatul Azhariyah leo maeneo ya Salasala jijini Dar es salaam.


 Jengo la madrasa
 Msikiti
 Mapacha wawili Ustaadh Hassan na Hussein wakimkabidhi Risala Mgeni katika Shughuli ya ufunguzi Sheikh Othman Kaporo.
 Ndani ya msikiti
Kinamama wakati wa ufunguzi huo

JOB VACANCIES AT DUWASA-DODOMA

0
0

Dodoma Urban Water Supply and Sanitation Authority (DUWASA) was established under section 3(I) of Cap. 272 of 1997 as repealed by section 60 of Water Supply and Sanitation Act No. 12 of 2009. DUWASA is charged with the overall responsibility of operations and management of water supply and sanitation services in Dodoma urban within the Municipality. Applications are invited from suitably qualified, dynamic, experienced and performance driven Tanzanians, male and female, to fill the following positions:


JOB TITLE:  Commercial Manager


REPORTS TO: Managing Director



JOB PURPOSE: To maintain customer records and follow up customer bills to ensure customers who get water, are correctly billed and pay for the water they have consumed at the right time.


wazee wa Mji mdogo wa Mirerani wazawadiwa magunia 100 ya mahindi

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona, (kulia) akiwazawadia wazee wa Mji mdogo wa Mirerani sh50,000  baada ya kuzungumza nao na kuwakabidhi msaada wa magunia 100 ya mahindi yaliyotolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Hussein Gonga.
 Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona, akigawa kwa wazee wa mji mdogo wa Mirerani, moja kati ya magunia 100 ya mahindi ya msaada yaliyotolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Hussein Gonga, kwenye ofisi za Sawata.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona, akizungumza na wazee wa mji mdogo wa Mirerani na kuwagawia msaada wa magunia 100 ya mahindi ya msaada yaliyotolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Hussein Gonga, kwenye ofisi za Sawata.

MAGONJWA YA MIFUGO ,MAJANGA YA MOTO NI CHANGAMOTO KUBWA INAYOIKABILI HIFADHI YA MKOMAZI

0
0


Waandishi wa habari wakimuangalia mnyama aina ya kobe  ndani ya hifadhi ya Mkomazi wilayani Same Mkoani Kilimanjaro

Na Woinde Shizza, Same

Vita dhidi ya magonjwa ya mifugo, majanga ya moto, ongezeko la watu pamoja na ukame  ni changamoto kubwa inayoikabili hifadhi ya taifa ya Mkomazi iliyopo wilayani same Mkoani Kilimanjaro ambapo imesababisha baadhi ya wanyama ambao ni vivutio vikubwa katika hifadhi hiyo kutoweka  .



Hayo yamebainishwa na afisa utalii mwandamizi  wa hifadhi ya mkomazi   Bw. Pellagy Marandu wakati akiongea na waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo kujionea vivutio ambavyo vinapatikana ndani ya hifadhi hiyo.



Alisema changamoto hizo zimekuwa zinaletwa na wafugaji ,wakulima ambao wamekuwa wanaleta wanyama ndani ya hifadhi ambapo alibainisha kuwa wanyama wengine wanaweza wakawa na magonjwa ya kuambukiza hivyo wanapoingia ndani ya hifadhi wanaweza kuambukiza wanyama walioko hifadhini hali ambayo inaweza kusababisha janga kubwa kwa hifadhi.


“Kwa upande mwingine wakulima wamekuwa wakileta madhara wakati wa kuandaa mashamba yao kwa ajili ya kilimo ambapo wamekuwa wakiaribu mazingira kwa kuchoma moto mabaki ya mazao ambayo walipanda msimu uliopita “alisema Marandu.

Aidha ilikukabiliana na changamoto hizo wamekuwa wakifanya doria kwa kushirikiana na wananchi wanaozunguka hifadhi ambao ni ujirani mwema ambapo wamekuwa wakiweza kufichua wale wote ambao wanaingiza mifugo ndani ya hifadhi kinyume cha sheria ambao wamekuwa wakipigwa faini huku wengine wakifikishwa mahakamani.

Kwa upande wake mkuu  wa hifadhi ya Mkomazi Donat Simon Mnyagatwa Alisema kuwa mbali na kuwepo na changamoto hiyo ya kuingiza mifugo ndani ya hifadhi pia wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji ambapo alibainisha  kuwa  hili ni tatizo kubwa  linaloikabili hifadhi hiyo kwani maji ni uhai ,kuanzia kwa binadamu na hata kwa wanyama .

“Ni kweli ili nitatizo kubwa lakini pia tumeanza kuandaa mipango mathubuti  kwa ajili ya kutatua tatizo hili ambapo kwa upande wa binadamu tupo kwenye mkakati wa kuanza kuchimba visima virefu ili kuweza kupa maji mengi ambayo pia maji hayo yataweza kukusanywa kwa pamoja kwa ajili pia ya wanyama wetu,pia tunampango wa kuongeza mabwawa yaliyopo ndani ya hifadhi ili kuakikisha pia tunaondokana na changamoto hiyo”alisema Mnyagatwa

Aidha alibainisha kuwa mbali na changamoto hiyo pia wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa miundo mbinu ya barabara pamoja na nyumba za kuishi watumishi ambapo alisema kuwa mpaka sasa zaidi ya familia tisa zinaishi ndani ya hifadhi  huku familia zingine zikiishi nje ya hifadhi ,pamoja changamoto hizo ameiomba Halmashauri ya same kupitia Tanroad kurekebisha barabara ya kuelekea hifadhini ili iweze kupitika kwa urahisi kwa kipindi chote.

Mnyagatwa alibainisha kuwa kwa lengo la ujirani mwema wananchi ambao wamekuwa wakizunguka hifadhi wamekuwa wakipatiwa mafunzo maalumu ya kutambua umuimu wa utunzaji wa hifadhi pamoja na kutambua mipaka ya hifadhi na athari za kuingiza wanyama hifadhini ,mathara ya uaribifu wa mazingira ambapo alisema wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwaelimisha na elimu hii imesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uhalifu ndani ya hifadhi.

Sherehe ya Kipindi cha Sports headquarters kutimiza mwaka mmoja wa mapinduzi ya michezo

0
0
 Efm 93.7 Radio kupitia kipindi chake cha Sports headquarters kimesheherekea  kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake  February 2015, hafla hiyo ilifanyika pale City Sports Lounge na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo akiwemo Waziri wa Habari, utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kama mgeni rasmi. Nikipindi pekee kilicholeta mapinduzi zaidi ya michezo kwa utangazaji na uchambuzi yakinifu nchini. 
Pichani Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikata keki ya birthday ya kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Head Quarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es Salaam.Kipindi hicho kimetimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwake
Mkurugenzi Mtendaji wa EfmRadio Frances Ciza akimlisha keki mgeni rasmi wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja kwa kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Head Quarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa na watendaji wa kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Headquarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es Salaam.Kipindi hicho kimetimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwake
Watendaji wa kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Headquarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio wakiserebuka kwa furaha City Sports Lounge jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Simba SC Haji Manara akimsikiliza Afisa habari wa TFF,Baraka Kiziguto akihutubia kwenye hafla hiyo

SHULE YA WASICHANA YA JOSIAH BUKOBA WAFANYA IBADA YA SHUKRANI SHULENI KWAO LEO

0
0
Mkuu wa Shule amewapongeza sana Wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka 2015 na kwa Ufaulu mzuri. Pia amewamwagia sifa kemkem Walimu kwa ujumla huku akipongeza Wazazi, uongozi wa shule hiyo kwa kufanikisha siku hii ya leo kwa kumshukuru Mungu kwani amejibu Sala zao na kuwawezesha wote kufaulu vizuri mtihani wao wa Taifa. Mwaka 2015 Wanafunzi 47 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Taifa kidato cha Nne, Wanafunzi 36 wamefaulu kwa Daraja la kwanza na Wanafunzi 11 wamefaulu kwa daraja la pili. Katika matokeo haya Shule imekuwa ya 2 kati ya shule 192 Kimkoa na ya 17 kati ya Shule 3452 Kitaifa. Aidha , wanampongeza Mkuu wa Shule, Mkurugenzi na Uongozi mzima kwa uwezeshaji mkubwa sana hadi kufikia mafanikio hayo.
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi-Bukoba Abedinego Kesho mshahara ndiye aliyeongoza Ibada Shuleni hapo leo.
Wanafunzi wakiimba Wimbo wa Kwaya ya RC Josiah SS wakati wa Ibada ya Shukrani leo hii jumamosi
Wanafunzi wa Josiah wakifuatilia kwa karibu Ibada hiyo
Mwenyekiti wa bodi ya shule, Johansen Rutabingwa akiongea wakati wa Ibada hiyo.  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

OMBAOMBA TISHIO ANAYEOMBA KWA KUTUMIA KISU IRINGA ANASWA

0
0
Askari polisi  mjini Iringa akiwa ameshika kisu baada ya kufanikiwa  kumnasa kijana Mohamed Iddy (18) mkazi  wa mjini Iringa kutokana na kutishia maisha ya  wakazi wa mji  wa Iringa akiwa katika  shughuli yake ya kuomba  ambapo hudaiwa  kuhatarisha maisha ya  wananchi kwa  kuwafukuza kwa kisu pindi anaponyimwa pesa ,
Kijana  huyo  omba  omba tishio akipelekwa  kituo cha polisi pamoja na kisu anachotumia kutishia  wananchi  wakati  akiomba  pesa kibabe. 

JUST IN: IGP AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI KWA BAADHI YA MIKOA

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu amefanya Mabadiliko kwa baadhi ya Makamanda wa Polisi wa mikoa na vikosi hapa nchini.


Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Leonard Paul amehamishwa  kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ulrich Matei aliyekuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.  Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mihayo Msikhela  aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia dawa za kulevya. 
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Ramadhani Mungi anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari na nafasi yake inachukuliwa na   Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Wilbrod Mtafungwa ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe. 
Aliyekuwa Afisa mnadhimu Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Prudenciana Protas anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe. 
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga ACP Ramadhan Ng’azi.   
Aidha,  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Camilius Wambura anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam  na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Francis Massawe kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam. 
Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gilles Mroto anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gemini Mushi aliyehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam. 
Wengine ni pamoja na Naibu Kamishna wa Polisi DCP Hezron Gimbi anayetoka Upelelezi Makao Makuu Dar es  Salaam kwenda kuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Costantine Massawe anakwenda kuwa Mkuu wa Oparesheni wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.


Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa Sheria,  kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi.


 Imetolewa na:

Advera Bulimba-SSP

 Msemaji wa Jeshi la Polisi (T)


 Makao Makuu ya Polisi.

LY 88 ya Mbuyuni Primary school WAFANYA SHEREHE YA KUUKARIBISHA MWAKA 2016

0
0
Wanafunzi waliosoma katika Shule ya Msingi Mbuyuni iliyopo jirani na Kanisa la St. Peter Oysterbay jijini Dar es Salaam wakiwa katika sherehe ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016 katika mgahawa wa Samaki-Samaki uliopo Posta mpya jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Katika hafla hiyo waliagana namwenzao anayeishi nchini Marekani, Emma  Kasiga ambaye anatarajiwa kuondoka Februari 28. (Picha na Habari Mseto Blog)
Wadau wakipata msosi.
................ilikuwa ni siku ya furaha.
Marafiki wakiwa katika hafla fupi ya kupongezana kwa kuingia mwaka 2016.
Tumaini Mgaya akiwa na Alex Chalamila.

LUKUVI AWAAGIZA VIONGOZI KULINDA MAENEO YA WAZI

0
0
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kizungumza na Madiwani na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa (hawapo pichani) juu ya kuwawezesha viongozi katika ngazi ya Mitaa kusimamia na kulinda maeneo ya wazi ,miundombinu na maeneo mengine ya umma.( Katikati) ni  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi na kulia ni Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Profesa.John Lupala
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwaonesha  Ramani Madiwani na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa
Sehem ya Madiwani na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa wakiwa  katika mkutanohu uklio fanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA SIMBA PLATINUM SUPPORTERS

0
0
Uongozi wa Simba Platinum Supporters (SPS) unawatangazia wadau wake wote  kuhudhuria bila kukosa mkutano mkuu wa Tawi siku ya Jumapili February 29, 2016 saa 4:00 asubuhi ukumbi wa Sigara/CDS,Chang'ombe Dar Es Salaam. 
Nyote mnakaribishwa.
Imetolewa na;
Madam Amina Poyo
MWENYEKITI SPS.

YANGA YAENDELEZA UBABE KWA CERCALE DE JOACHIM YA MAURITIUS, YAITUNGUA 2-0 TAIFA LEO

0
0
Wachezaji wa timu ya Yanga, wakishangilia sambamba na mashabiki wao, baada ya kufunga goli la pili dhidi ya timu ya Cercale De Joachim ya nchini Mauritius, katika mchezo wao wa marudiano wa Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika, Uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda 2-0. Picha zote na Othman Michuzi.
Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe akiondoka na mpira na kumuacha Beki wa Timu ya Cercale De Joachim ya nchini Mauritius, katika mchezo wao wa marudiano wa Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika, Uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda 2-0.
Mchezaji wa Yanga, Geofrey Mwashiuya akiwatoka Mabeki wa timu ya Cercale De Joachim ya nchini Mauritius, katika mchezo wao wa marudiano wa Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika, Uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda 2-0.

TANZIA: AFISA UHUSIANO TTCL AFARIKI DUNIA

0
0
Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga enzi za uhai wake.

AFISA Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga, amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia Jumamosi Februari 27, 2016. Taarifa ya kifo cha Bi. Amanda imethibitishwa na Meneja Uhusiano wa TTCL, Bw. Nicodemus Thom Mushi.

 "...Ni kweli, Bi Amanda amefikwa na umauti akiwa likizoni mkoani Mbeya alikokwenda kuwasalimu ndugu zake.. Aliugua ghafla Alhamisi hii na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya hadi usiku wa kuamkia Jumamosi ambapo Mungu alimchukua," alisema Bw. Thom Mushi.

 Alifafanua kuwa mwili wa marehemu utasafirishwa siku ya Jumapili, kutoka Mbeya kwenda Njombe na Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu tar 29.02.2016 katika Kijiji cha Mlangali, Ludewa, Mkoa wa Njombe. Mtandao huu unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Bi. Amanda Fredrick Luhanga kwa msiba mkubwa uliowafika.  Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Apumzike kwa Amani.

KIWANDA CHA A TO Z CHA ARUSHA KUTOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 70

0
0

Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Luhaga Mpina amekiamuru kulipa faini kiwanda cha A to Z cha mjini Arusha , chenye kufanya kazi ya kuzalisha nguo na bidhaa za plastiki kutokana na ukiukwaji wa utekelezaji wa sheria namba 20 ya mwaka 2004 ya utekelezaji na usimamizi wa mazingira.
Mh Mpina alitoa agizo hilo jijini Arusha Jumamosi  katika ziara yake ya kukagua usafi wa mazingira, kupanda miti na kutembelea viwanda,ambapo alibaini kuwa mnamo septemba mwaka 2015 kiwanda hicho kilipewa adhabu ya kulipa faini  ya shilingi milionni 70 na kukaidi kufanya hivyo kwa kipindi cha miezi sita sasa.
Mh Mpina amekitaka kiwanda hicho kulipa faini hiyo kwa kipindi kisichopungua siku saba kinyume na hapo kiwanda hicho kitafungiwa.
Aidha Naibu Waziri Mpina alitembelea viwanda vya Sunflug na Lothia Steel vya jijini humo  na kujione namna ambavyo vinakabiliana na utunzaji wa mazingira katika uzalishaji wao na changamoto ya kuzimikazimika kwa umeme jijini Arusha.
Mh. Mpina alikitaka kiwanda cha Chuma cha Lothra Steel kupima moshi unaotoka katika kiwanda hicho ili kujua kama una athari kwa mazingira na viumbe vinavyozunguka maeneo ya kiwanda hicho.
Ziara na Mh waziri katika jiji la Arusha ni matokeo ya utekelezaji wa agizo la Mh Rais John Pombe Magufuli la usafi wa mazingira unaotakiwa kufanyika kitaifa kila Jumamosi ya mwisho wa
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina akiwa ziarani kukagua baadhi wa viwanda jijini Arusha Jumamosi. 
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
mwezi

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: Nimekuchagua Wewe- Bob Rudala

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images