Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

WIZARA YALAANI MAUAJI YA MTOTO MARIAM DEOGRATIUS (4) ALIYEBAKWA NA KUUAWA ENEO LA MAKOKO, MUSOMA MKOANI MARA

0
0
Wizara inalaani vikali tukio la kubakwa na kuuawa kikatili kwa mtoto Mariam Deoratius, umri miaka 4, ambaye alifanyiwa ukatili huo na watu wasiojulikana, eneo la Makoko, Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, mapema wiki hii.  

Wizara imesikitishwa na mazingira ya mauaji ya mtoto huyo mdogo asiyekuwa na hatia, ambaye aliokotwa kwenye banda linalojengwa akiwa ameharibiwa sehemu zake za siri, kutokwa na damu nyingi na akiwa amefariki dunia. Mauaji haya ni ukiukwaji mkubwa wa haki ya kuishi ya mtoto ambayo ndiyo ni haki yake ya msingi. Haki hii inapovunjwa inarudisha nyuma jitihada za Taifa letu kufanya jamii zetu kuwa mahali salama kwa watoto kuishi. 

Wizara inaamini kuwa, Mamlaka zinazohusika na ulinzi wa watoto dhidi ya ukatili katika Mkoa wa Mara hususan Manispaa ya Musoma, kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka, na kuwa fundisho kwa wanaoendeleza ukatili wa watoto. Kwa tukio hili, jamii inahimizwa kubadilika na kuhakikisha kuwa ulinzi wa watoto ni jukumu la wazazi, walezi na watu wote katika jamii. 

Wizara inatoa pole kwa wazazi, ndugu, marafiki na familia ya mtoto Mariam aliyeuawa katika umri mdogo na tunawaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.


TAASISI YA KIISLAMU YA MUZDALIFAT YATOA VIFAA MBALIMBALI VYA HOSPITALI ZANZIBAR

0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Salum katikati akipata maelezo kwa Muakilishi wa Taasisi ya Helping Hand Mohammad Habibu kuhusiana na Vifaa mbalimbali vya Hospitali vyenye Thamani ya Dola za kimarekani 3,45000 (laki tatu arobaini na tano Elfu)vilivyotolewa na Taasisi ya Kiislamu ya Muzdalifat kwa kushirikiana na Taasisi yake yenye makao Makuu nchini Marekani.hafla iliofanyika Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Muzdalifat Farouk Hamadi akitoa hotuba ya kumkaribisha Mgeni rasmi katika Hafla ya kutoa Vifaa mbalimbali vya Hospitali iliofanyika Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Salum akikabidhiwa Vifaa mbalimbali vya Hospitali vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 3,45000 (laki tatu Arobaini na Tano Elfu) na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Muzdalifat Farouk Hamadi.wa kwanza kushoto ni Muakilishi wa Taasisi ya Helping Hand yenye makao makuu Nchini Marekani Mohammad Habibu.
Wanafunzi wa skuli ya Sekondari ya Farouk Aktas Muslim iliopo kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja wakihudhuria katika Hafla ya Utoaji wa Vifaa mbalimbali vya Hospitali vyenye Thamani ya Dola za kimarekani 3,45000 (laki tatu arobaini na tano Elfu)kutoka Taasisi ya Kiislamu ya Muzdalifat kwa kushirikiana na Taasisi ya Helping Hand yenye makao Makuu nchini Marekani.

TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA JPC NA ZAMBIA.

0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga akiwakaribisha wageni waalikwa ambao ni Viongozi na Maafisa wa Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zambia katika Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia (JPC) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa muda wa siku mbili kuanzia leo.
Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mhe. Judith Kapijimanga (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Balozi Grace Mujuma wakijadili jambo wakati wa mkutano huo.
Sehemu ya maofisa wa Serikali ya Tanzania wakifuatilia Mkutano.
Serikali za Tanzania na Zambia zinakutana katika kikao cha siku mbili kujadili na kukubaliana maeneo ya ushirikiano ambayo watayasimamiakwa pamoja kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi hizo mbili. Kikao hicho kinachojulikana kama Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia (JPC) kinafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia leo.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi alieleza kuwa uhusiano wa Tanzania na Zambia ni mzuri na kufanyika kwa kikao hicho ni uthibitisho dhahiri.

Aidha, Balozi Mwinyi alieleza kuwa kufanyika kwa kikao hicho kunatoa fursa kwa wajumbe kuchambua kwa pamoja hatua zilizofikiwa na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa maeneo yaliyoafikiwa wakati wa kikao cha 8 cha JPC kilichofanyika Lusaka Juni 2006. Maeneo hayo ni pamoja na biashara, viwanda, mawasiliano, uchukuzi, nishati, uhamiaji, kilimo, elimu, michezo, madini, utalii, maliasili na utamaduni.

“Haya ni baadhi ya maeneo ambayo nchi zote mbili zinayapa umuhimu mkubwa ili kuharakisha maendeleo ya pande zote mbili Katika majadiliano yetu tutalenga zaidi maeneo haya ili tubuni utaratibu mzuri wa kushirikiana katika utekelezaji kwa lengo la kuleta tija kwa nchi na wananchi wake”. Balozi Mwinyi alifafanua.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo na Mashirika ya Kimataifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Zambia, Bw, Sylevester Mundanda alieleza kuwa Tanzania na Zambia zimejaliwa kuwa na maliasili lukuki kama vile ardhi, madini, maji na wanyama pori, hivyo, endapo kama zitatumiwa vizuri zinaweza kubadilisha uchumi wa nchi hizo kwa ajili ya kuwaletea maisha bora wananchi wake.

Alisisitiza umuhimu wa kukubaliana maeneo machache ya kipaumbele na kuyawekea mikakati ya utekelezaji na ubunifu bila kusahau kujiwekea utaratibu wa kupima ufanisi kila baada ya muda.

Bw, Mundanda alihitimisha kwa kusema kuwa vikao vya JPC ni fursa nzuri kujadili changamoto za kiuchumi na kubuni mikakati ya pamoja kukabiliana nazo ili uchumi uweze kukua kwa faida ya wananchi wa pande zote.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Timu ya Tenisi ya Tanzania yashika namba mbili Afrika

0
0
Na Lilian Lundo  - Maelezo

Timu ya mchezo wa Tenisi kwa walemavu (wheelchair tennis) ya Tanzania imeshika namba mbili Afrika katika mashindao ya mchezo huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Nairobi.

Hayo yalisemwa na kocha wa timu hiyo Bw. Riziki Salum leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na vyombo vya habari juu ya ushindi walioupata.

“Tumeshiriki zaidi ya mashindano mawili jijini Nairobi na tumekuwa washindi wa pili Afrika, timu zote mbili za wanawake na wanaume zimeingia fainali zikiwa na na jumla ya wachezaji saba wakiongozwa na nahodha Juma Mohamedy,” alisema Salum.

Salum aliongeza kwa kusema, chama cha Dunia cha mchezo huo kimeahidi kuwapa mualiko wa kushiriki mashindano ya Dunia yatakoyofanyika Japan mwaka huu kulingana na ratiba itakayopangwa.

Aidha, Bw.Salum alimshukuru mfadhili Bi. Latya Nassoro ambaye ameiwezesha timu hiyo kwenda kushiriki mashindano hayo kwa kuwalipia nauli ya kwenda na kurudi pamoja na malazi na chakula.

Kwa upande wake Bi. Latya Nassoro aliwahimiza na kuwaomba watu binafsi na makampuni kujitokeza kufadhili timu za Tenisi ili mchezo huo ufike mbali nchini na kupata ushindi ambao utarejesha makombe nyumbani na kuiletea nchi sifa na kuitangaza miongoni mwa mataifa kupitia mchezo huo.

Timu hiyo ya Tenisi ilishiriki mashindano ya Dunia yaliyofanyika mwaka 2013 nchini Uturuki na kushinda kombe la timu bora zilizoshiriki katika mashindano hayo.

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MIKOA YA MWANZA, GEITA NA KAGERA

0
0
● Aziagiza Halmashauri kushughulikia migogoro ya ardhi .
● Azitaka kulisaidia Shirika la Nyumba ili lijenge nyumba za gharama nafuu ● Asema Halmashauri zinunue nyumba zinazojengwa na NHC kwa ajili ya watumishi wao.
● Alipongeza NHC kwa kasi ya ujenzi wa nyumba bora katika Halmashauriza Miji na Wilaya.
mab01
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akisalimiana na Watumishi wa Hamashauri ya Mji wa Buchosa alipowasili kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi
MAB1
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akipewa maelezo na mtaalam wa mifumo ya uwekaji kumbukumbu za umiliki wa ardhi alipotembelea idara ya ardhi Wilayani Misungwi. Aliyoko katikati ni Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Bw. Mshana.MAB2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula na Mbunge wa Chato Mhe.Dkt Medard Kalemani wakikagua eneo la Kijiji cha Rusungwa lenye mgogoro mkubwa wa ardhi unaofanya wananchi wa kijiji hicho kukosa ardhi ya kulima na uwekaji huduma za jamii kama shule baada ya eneo la ekari 500 la kupewa mwekezaji.

Ofisi ya Uhusiano, Kitengo cha Masoko TANESCO waelimisha umma

0
0
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha VETA NJIRO, waliohudhuria kwenye mafunzo ya usalama na wizi wa umeme wa kwanza (Kushoto) ni Afisa Huduma kwa wateja Bw. Juma Msuya.
 Mwanafunzi wa Chuo cha Veta kilichopo Oljoro mkoani Arusha akiuliza swali kwa wataalamu wa TANESCO katika mafunzo hayo.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi  Oldonyo Sambu ya Mkoani Arusha wakiwa na zawadi zao walizopewa na wataalam wa TANESCO kama zawadi za kushiriki vyema katika mafunzo hayo na kujibu na kuuliza maswali, kushoto ni Afisa Mahusiano na Wateja Mkoa wa Arusha Bw.Fred Mbavai.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

WAZIRI MBARAWA AZITAKA TAASISI ZA WIZARA YAKE KUSHIRIKIANA

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amezitaka taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo kufanya kazi kwa uwazi, weledi na uaminifu ili kuongeza mapato na kutimiza adhma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.

Prof. Mbarawa ametoa wito huo mkoani Kilimanjaro katika majumuhisho ya ziara yake ya mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro iliyolenga kukagua miradi ya ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, Posta, TTCL, TBA na TEMESA.

“Kila mfanyakazi wa wizara hii namtaka afanye kazi kwa kufikiria uzalishaji wa mapato na ubora wa huduma ili kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano”, amesema Prof. Mbarawa

Waziri Mbarawa amewataka mameneja na wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupima utendaji kazi wa kila mfanyakazi na kusisitiza zile taasisi zinazozalisha upimwaji utazingatia ukusanyaji wa mapato.

Amesema Serikali iko katika mkakati wa kufufua Reli ili mizigo mikubwa inayotoka bandarini isafirishwe kupitia njia ya reli na hivyo kupunguza uharibifu wa barabara.

“Takribani tani milioni 6 zinazopakuliwa bandarini, tani milioni 5.7 zinasafirishwa katika barabara hali inayosababisha uharibifu wa mara kwa mara kutokana na baadhi ya wasafirishaji kuzidisha uzito hivyo nawataka TANROADS kusimamia vituo vya mizani kikamilifu ili kulinda barabara”, amefafanua Waziri Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Amos Makala amemweleza Waziri Mbarawa kuwa Serikali ya mkoa itahakikisha maelekezo yake katika sekta ya miundombinu yanapewa kipaumbele ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa wakati.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya KMT-Machame yenye urefu wa Km 14.9 kujionea hali ya barabara hiyo na kusisitiza kuwa Serikali itatoa kipaumbele kwa barabara hiyo kutokana na umuhimu wake katika utalii na hivyo kukuza uchumi.

Prof. Mbarawa amehitimisha ziara ya siku tano kwa kukagua miradi na taasisi zilizo chini ya wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katka mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro na kuzitaka taasisi hizo kufanya kazi kwa ushirikiano.
Meneja wa Wakala wa Barabara mkoa wa Kilimanjaro Eng. Marwa Rubirya akitoa taarifa ya utekelezaji wa TANROADS kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa wakati alipotembelea taasisi hiyo mkoani Kilimanjaro. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Amos Makala akifatilia.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na watendaji wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kuhusu kufanya kazi kwa uwazi, weledi na uaminifu ili kuongeza mapato.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Amos Makala akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) katika kikao cha viongozi wa sekta zilizo chini ya Wizara hiyo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAIS WA GUINEA BISSAU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA TANZANIA.


MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, SAID MECK SADIKI AZINDUA DUKA LA HUAWEI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang, akizungumza na wandishi wa habari hawapo picha juu ya mbinu zilizotumika na kampuni ya  Huawei, ambapo wanajitahidi  kuwa Karibu zaidi na wateja wake na kuendeleza zaidi uzoefu katika matumizi ya bidhaa za Huawei. 

"Ili kuwahudumia Zaidi wateja wake Huawei tume fungua Maduka Mapya ya Huawei pamoja na huduma za matengenezo ya simu za mkononi jijin Dar es Salaam,baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei na kuhakikisha kuwa na vifaa vya uhakika na orijino vinapatikana kwa wateja wao kirahisi.leo jijini Dar es Salaam" amesema Zhangjunliang.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akipatiwa maelekezo na Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu , Samora leo jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania leo jijini Dar es Salaam. 

(Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya jamii).

NOTICE TO MEMBERS OF THE ASSOCIATION ON CONTRIBUTIONS TO THE EDUCATION & HEALTH SECTORS

0
0

                                                                                 

TATOA-Logo.jpg
During his speech to the Dar-Es-Salaam elders on 13th February 2016, President Dr. John Pombe Magufuli pledged to contribute part of his salary towards supporting universal free education endeavours in Dar-Es-Salaam Region which has been hit by an influx of students. This is after the 5th phase Government decided to make universal primary school education free. The influx has brought about challenges of insufficient class rooms, desks and even books in some schools.

To support President Dr. Magufuli’s endeavours TATOA would like to request all our members to support this gesture as initiated by the President. Members are requested to voluntary contribute to a fund created by the association for this purpose. Contributions collected will be used to support the Government’s efforts in purchasing education essentials such as desks, books and also help in the construction of classes by donating construction materials. Apart from the support to the education sector the association will also support Government’s efforts in supporting the health sector in areas of hospital beds, mattresses and other essentials pertaining to health services. All companies that will contribute towards this fund will be recognized and their names submitted to the Government as an appreciation for their good deed. They will also be invited to participate in the handing over exercise should they wish to do so. Certificates of appreciation will be given.

Contributions should please be made as follows ;
  1. By direct payment to our offices along Pugu Road where a receipt will be issued
  2. By direct remittance to MPESA (0763365847)/TIGOPESA (0712907812)
  3. By deposit to our Stanbic Bank account number 0140005088001 under the name TATOA.
We thank you.

Emmanuel Kakuyu
Chief Executive Officer
Tanzania Truck Owners Association
Dar-Es-Salaam

WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA VIFAA VYA HOSPITALI KUTOKA MAKAMPUNIYA PEPSI, COCACOLA NA AZAMCOLA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam  Cola  na Pepsi Cola- SBC  katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kulia  kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea moja ya vifaa vya hospitali kutoka kwa wawailishi wa makampini ya Vinywaji baridi ya Coca Cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC  katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto  Mkurugenzi wa Pepsi, Avinash Jha,Wapili kushoto ni  Reginald Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na Wapili kulia ni Basil Gadzios wa Coca cola Kwanza.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam  Cola  na Pepsi Cola- SBC  katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kulia  kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana   baadhi ya viongozi vya makampuni ya vinywaji  baridi ya Coca Cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC  katika makabidhino ya vofaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi bilioni 10 yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Pepsi, Avinash Jha, Reginald Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na Basil Gadzios wa Coca cola Kwanza.  Kulia    ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

FEBRUARY 25, 2016 SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

NBA launch of "jr. NBA" league program on Saturday, February 27 at 1:00 pm.

0
0

NANI:              Amadou Gallo Fall–Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu – Africa

Allison Feaster - Mchezaji nyota na Mwandamizi wa WNBA

Paul Hinks –Mtendaji Mkuu wa Symbion Power                


NINI:               Kuanza rasmi kwa Ligi ya Mpira wa kikapu kwa vijana (Jr.NBA Basketball League) nchini Tanzani


LINI:                Saa saba Mchana, Siku ya Jumamosi; Tarehe 27,2016


WAPI:            Kituo cha Vijana cha Michezo Jakaya M. Kikwete jijini Dar es Salaam  


Shirikisho la Mpira wa Kikapu litazindua rasmi msimu wa kwanza wa ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana kwenye kituo cha vijana cha Michezo cha JMK jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 27 Februari mwaka huu.


Sherehe hii ya ufunguzi ambayo itahudhuriwa na Mchezaji Nyota na Mwandamizi wa WNBA aitwaye Allison Feaster itakuwa ni uzinduzi rasmi wa ligi ya Mpira wa Kikapu ya Vijana wenye umri kati ya miaka 12 na 14. Ligi hii itajumuisha shule kutoka maeneo ya karibu zipatazo thelathini (30) kila shule ikiwakilisha moja wapo wa timu 30 zinazoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani.


Wanahabari ambao watapenda kushiriki kwenye uzinduzi huu wanapaswa kutoa taarifa ( RSVP) kwa adi.raval@jmkpark.org kabla ya tarehe 25 Februari saa kumi na moja jioni. Kituo kinachoruhusiwa kushiriki kinapaswa kuwa na hadhi stahiki.


Ligi ya mpira wa kikapu ya vijana (Jr. NBA League) Ni ligi ya NBA ya kidunia inayoshirikisha mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana ; wavulana kwa wasichana na inafundisha stadi za msingi za mchezo wa mpira wa kikapu pamoja na maadili muhimu ya mpira wa kikapu kwa wachezaji wanaoanza. Lengo likiwa ni kusaidia kukuza na kuboresha uzoefu wa Wachezaji, Makosha na Wazazi


Kwa maelezo zaidi kuhusu kituo cha Michezo 
cha Vijana tafadhali tembelea www.jmkpark.org.


*** FURSA ZA MAHOJIANO NA UCHUKUAJI PIA ZINAPATIKANA***

   
* * *Hii ni sherehe ya watu maalum – kama ilivyoainishwa hapo juu, Waandishi wahabari wanaohitaji kuudhuria WANAPASWA kutoa taarifa mapema (RSVP) kwa  adi.raval@jmkpark.org kabla ya kumi na moja ya siku Alhamisi ya Tarehe 25 Februari 2016 ili waweze kupewa ruhusa kabla ya sherehe. Tafadhali mtumie Adi barua pepe kama una swali lolote. 
Kwa Mawasiliano zaidi:

Pawel Weszka, NBA, pweszka@nba.com


Adi Raval, Symbion Power, adi.raval@jmkpark.org

TEASER JOTO LA ASUBUHI IJUMAA FEBRUARY 26, 2016 KUANZIA SAA 12 HADI SAA TATU

Breaking News.... Tanzia: Mwanamuziki Mkongwe Kassim Mapili afariki dunia leo jioni

0
0

Nimepokea kwa Masikitiko Makubwa Taarifa za Kifo cha Mzee wetu Mzee Mapili (Pichani kulia) baada ya kuonekana hajatoka Chumbani kwake kwa Muda Mrefu.... Ndipo mlango ukavunjwa nyumbani kwake Tabata Matumbi jijini Dar es salaam na kukuta Mzee wetu hatunaye tena... 
Mzee atakumbukwa kwa Kibao cha "Napenda Nipate Lau Nafasi" na "Rangi Ya Chungwa" na vingine nyingi...Pia alikuwa kiongozi wa kwanza wa Tanzania Dance Music Association ama Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA). 
Mara ya mwisho hadharani Marehemu Mzee Kassim Mapili alionekana akiongoza wanamuziki katika mazishi ya mwanahabari nguli wa burudani Marehemu Fred Mosha katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam, ambako pamoja na kushirki mazishi aliimba kwa hisia beti kadhaa za kumuenzi marehemu Fred.
Taarifa zaidi za msiba huu mzito  zitawajia kadri zitavyopatikana.
Kwa mawasiliano zaidi kwa wasanii wa Tanzania piga namba 0744150000 
 Nawaomba wanamuziki wote Tujitoe 
kwa wingi kumpa heshima Mzee wetu Kassim Mapili....!! 

Imetolewa na Addo November
 Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania..!!

THE BRIGHTER DAYS AHEAD FOR TANZANIAN GAS SECTOR

0
0
In order to understand the present scenario in Tanzanian oil and gas sector, it is important to take a traditional outlook from where our country is coming from
The past scenario for Tanzanian oil and gas sector
The 1950s- BP and Shell drilled and discovered dry hole
In1969-TPDC was established by government to help develop and handle oil and gas sector and also offered exploration permits with government  and could get into partnership with foreigner associates through Production sharing agreement
In 1969-AGIP began discovery offshore after finalized production sharing contract with TPDC
The 1970s- The nation was not easy to attract foreign companies that would provide know-how and financial commitment this was because of inadequate facilities and being far away from market
In 1974- Gas deposits was discovered at songo songo area (but was not commercial v viable)
The 1980s- Shell and variety of foreign companies did seismic and sunk hole onshore and offshore
In 1982- Another Gas reserve was found in Mnazi Bay
In 1983- There was low oil price and, for this reason, it become more difficult than ever to draw in worldwide investors.
The 1990s- The work a project based on the 1974 Songo Songo gas area began evolving
In 1992-Tanzania released a variety of power change projects, such as a National Energy Policy, which began out up kind of market participation in creating electricity

In 2004-little production began at songo songo field
The Current circumstances for Tanzanian oil and gas sector
Despite the recent low oil price, Tanzanian oil and gas sector has enhanced considerably over the last several years.

For long, it could not create its gas sources because the discoveries were not considered for commercial viable.

The foreign oil companies that had capability were simply not fascinated in making a financial commitment.

The first significant project, the Songo Songo gas-to-electricity project, only came into being with contributor assistance.
Nowadays, a variety of oil and gas companies working in Tanzania, such as some of them are giant oil players.
The nation, therefore, is based less on growth assistance for enhancing the oil market.

The change of the whole lawful and management structure that controls oil sources, which is continuous, indicates to a come back to a more effective part of the state.

The completions of Mtwara- Dar es salaam gas pipeline project in Oct 2015 plus the LNG place plan could put Tanzanian oil and gas sector t in the next level.

The attempt has been done by the govt to build up local content indication many Tanzanians would have fun with the whole sequence of oil and gas sector and the resources would benefit people and nation in common at the time production starts which is predicted at least in 2025.

There are brighter days ahead for Tanzanian oil and gas sector

Hussein Boffu
 Graduate in Petroleum Geoscience
Hussein.Boffu@Tanzaniapetroleum.com
0655 37 65 43/0689955711

TANZIA

0
0
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania wanasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzao, Sarah Sanga.

RAIS DKT. MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MWANAMZIKI MKONGWE NCHINI, MZEE KASSIM MAPILI

0
0
Marehemu Mzee Kassim Mapili enzi za uhai wake.

Mzee Kassim Mapili kuzikwa leo saa kumi kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar

0
0
 Baadhi ya Wamamuziki wakongwe wa Muziki wa Dansi hapa nchini, wakiwa kwenye Msiba wa Mwanamuziki Mwenzao, Mzee Kassim Mapili, Magomeni Mapipa Jijini Dar es salaam leo. Mzee Mapili anazikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kisutu.

KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI CHAFANYIKA LEO.

0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Jesh Lupembe akizungumza katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halamshauri hiyo.
Baadhi ya watendaji wa Halmashari ya Manispaa ya Moshi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Na  Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images