Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1132 | 1133 | (Page 1134) | 1135 | 1136 | .... | 3348 | newer

  0 0


  SIMU.TV: Agizo la waziri wa TAMISEMI George Simba Chawene kwa mkoa wa Iringa kuwataftia na kuwatengea makazi ya kudumu waathirika wa mafuriko latekelezwa.https://youtu.be/ZUMGQg2vSow

  SIMU.TV: Naibu waziri wa nishati na madini Dr.Kalemani atumbua jipu kwa mwekezaji wa kiwanda cha chumvi kigoma huku akitoa maagizo mazito. https://youtu.be/vXBc2IG1nQw

  Wakazi wa vijiji 6 wilayani Namtumbo mkaoni Ruvuma hawana mawasiliano ya barabara baada ya mvua kuharibu daraja walilokuwa wakitumia hivyo kuwasababishia adha kubwa.https://youtu.be/pQYEb7aGj1k  

  SIMU.TV: Mahakama kuu divisheni ya ardhi imehairisha kutoa hukumu ya zuio la kesi ya kutobomolewa kwa nyumba za wakazi wa jimbo la Segerea hadi mwezi marchi mwaka huu.https://youtu.be/uF0nv2ISOUw

  SIMU.TV: Serikali wilayani Mbulu mkoani Manyara kwa kushirikiana na shirika la Farm Afrika linalojihusisha na uhifadhi wa mazingira wakabidhi hati miliki za kimila kwa ajili ya umilikaji wa ardhi kwa kaya 100 wilayani humo. https://youtu.be/VCHm_HHwIjo

  SIMU.TV: Ukosefu wa dawa katika zahanati mbalimbali hapa nchini umeelezwa kuwa changamoto katika uhamsishaji wa wananchi kujiunga katika mfuko wa afya ya jamii CHF kutokana na wananchi kukata tamaa. https://youtu.be/Wblc8OqRtQg

  SIMU.TV: Halamashauri ya mji wa Bariadi yajipanga kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati 6979 kwa shule za msingi na 1837 kwa shule za sekondari katika kuondoa kero za wananfunzi kukaa chini ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais.https://youtu.be/fq9eEnQsgDw

  0 0

  Serikali imelitika Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kuhakikisha linayafikia malengo iliyojiwekea ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana hapa nchini.
  "Kama baraza mna jukumu la kufanya kazi kwa bidii na vitendo ili kuwawezesha wananchi kiuchumi na kupunguza tatizo la ajira," Waziri Mhagama alitoa wito huo mwishoni mwa wiki alipoitembelea sekretarieti baraza hilo jijini Dar es Salaam. 
  Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inapenda kuona kazi zinafanyika kwa vitendo na matokeo yake yanawanufaisha wananchi na siyo vinginevyo. 
  Alisema baraza ni chombo kikubwa cha kitaifa na kimepewa dhamana kubwa ya kuwawezesha wananchi kumiliki uchumi wao na kuondoa tatiazo la ajira kwa vijana , hivyo wanawajibu wa kutekeleza majukumu yao kwa vitendo.
  “Tukiweza kuwawezesha watanzania kiujuzi, mitaji na vitendea kazi kulingana na makundi yao kwa kushirikiana na wadau wetu, tutakuwa tumewatendea haki watanzania na sisi tutakuwa katika nafasi nzuri”,alisema Bi. Mhagama.
  Alisema makundi hayo ya vijana wanajishughulisha na kilimo, ufugaji, ujenzi, vijana wa vyuo vikuu, Vijana wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na vija wote wakiwemo badaboda na biashara mbalimbali.
  "Tukiwafikia hawa wote  taifa hili badala ya kutembea litakuwa linakimbia na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025,"alisema.
  Waziri Mhagana alilitaka baraza hilo kujiwekea muda wa utekelezaji wa programu zake ili kwenda na wakati sababu serikali inataka kila programu ianze kwa muda mwafaka na kwisha kwa muda mwaka.
  Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Bazara hilo, Bi. Beng’i Issa alisema baraza limejipanga kutekeleza maagizo ya waziri na mipango yake kwa ufanisi na kwa muda uliopangwa kuhakikisha azma ya kuwawezesha watanzania kiuchumi inafikia malengo.

  “Baraza hadi sasa linatekeleza mkakati wa kitaifa wa uwezeshaji ambao tayari umeshasambazwa kwa watekelezaji” na pia kunamwongozo wa kitaifa wa mafunzo ya ujasiriamali ambao upo mbioni kuanza kufundishwa kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu, aliongeza kusema.Bi Issa. 
  Aidha alisema baraza pia linatekeleza mwongozo wa makakati wa kitaifa wa uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NMSFEE), madawati ya uwezeshaji yameanzishwa katika ngazi ya kitaifa,mikoa, halmashauri na sekta mbalimbali kufuatilia taarifa za uwezeshaji.

  Pia alisema programu ya majaribio ya  kijana jiajiri imenaza kutekelezwa kwa kutoa mafunzo, malezi na mitaji kwa vijana wa miaka 18 hadi 35 kwa mikoa ya Mtwara, Lindi, Dar es Salaam na Morogoro na unalenga kusambazwa nchi nzima.
  Suala la watanzania katika kushiriki katika uwekezaji unaofanyika nchini kutoka nje (local content) katika sekta zote unashughulikiwa kwa kushirikiana na wizara zinazohusika na masuala haya ili watanzania wasiweze kuachwa nje ya uchumi wao.
  “Sekta zilizopewa kipaumbele katika jambo hilo ni pamoja na madini,mafuta na gesi asilia, ujenzi, biashara ya maduka, Kilimo na viwanda na biashara,”alisema Katibu Mtendaji huyo.

  Naye Mkurugenzi wa Mfuko wa Uwezeshaji (Empowerment Fund),Bw. Edwin Crisant alisema kuanzia mwaka 2007 hadi 2015 baraza limetumia Tsh. bilioni 2.5 kudhamini mikopo iliyotolewa na Benki ya CRDB yenye thamani ya Tsh. bilioni 10.47 kwa wajasirimali 10,769 na vikundi 300.
  Pia baraza limeingia mikataba zaidi na benki na taasisi mbalimbali zikiwemo za Benki ya Posta, NSSF, Jeshi la Kujenga Taifa na Benki ya maendeleo ya Kilimo kutoa mafunzo kwa vijana na kudhamini mikopo yao kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira ,Vijana na Walemavu, Bi.Jenista Mhagama kushoto akikaribishwa na Katibu Mtendaji wa Bazara Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi.Beng’i Issa, wakati alipofanya ziara ya kwanza ya kukutana na watumishi wa sekretarieti ya Baraza la hilo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira Vijana na Walemavu, Bi.Jenista Mhagama kulia akizungumza na watumishi wa sekretarieti ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) hawapo pichani, mara baada ya kufanya ziara yake ya kwanza ya kujifunza kazi za baraza hilo, kushoto Katibu Mtendaji wa Bazara hilo, Bi.Beng’i Issa.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira ,Vijana na Walemavu, Bi.Jenista Mhagama akizungumza na watumishi wa sekretarieti ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), mara baada ya kufanya ziara yake ya kwanza ya kujifunza kazi za baraza hilo mwishoni mwa wiki, kushoto Katibu Mtendaji wa Bazara hilo, Bi.Beng’i Issa.

  0 0

   Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakis(mwenye kofia) akizungumza jambo na Mkuu wa Shule ya sekondari ya Shimbwe iliyopo wilayani Moshi vijijini,Jacob Costantine muda mfupi baada ya kukabidhi msaada wa Mashine ya kudurusu karatasi.kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Mch Marco Silemu.
   Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakis akimkabidhi Mkuu wa Shule ya sekondari ya Shimbwe iliyopo wilayani Moshi vijijini,Jacob Costantine, msaada wa Mashine ya kudurusu karatasi iliyotolewa na kampuni ya Vodacom ikiwa ni ahadi iliyotolewa kwa shule hiyo kupitia programu ya Pamoja na Vodacom.wengine ni walimu na wanafunzi wa shule hiyo.
   Mkuu wa Vodacom Tanzainia kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakis akimuelekeza Mkuu wa Shule ya sekondari ya Shimbwe iliyopo wilayani Moshi vijijini,Jacob Costantine namna ambavyo mashine ya kudurusu karatasi iliyotolewa na Vodacom shuleni hapo inavyoweza kufanya kazi.
   Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakis akimkabidhi Mkuu wa Shule ya sekondari ya Shimbwe iliyopo wilayani Moshi vijijini,Jacob Costantine, msaada wa Mashine ya kudurusu karatasi iliyotolewa na kampuni ya Vodacom ikiwa ni ahadi iliyotolewa kwa shule hiyo kupitia programu ya Pamoja na Vodacom.wengine ni walimu na wanafunzi wa shule hiyo. 
  Shule ya sekondari ya Shimbwe iliyopo wilaya ya Moshi vijijini,Imenufaika na msaada wa mashine yenye uwezo wa kufanya kazi zaidi ya tatu ikiwemo kudurusu karatasi kupitia  mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Tanzania”Vodacom Foundation”. 
  Msaada wa mashine hiyo (Photocopier) yenye thamani ya zaidi ya sh Mil 12 ni sehemu ya msaada wa vifaa mbalimbali ambavyo kampuni hiyo kupitia mradi wa “Pamoja na Vodacom” imekabidhi shuleni hapo zikiwemo Kompyuta mpakato 30.

  Mbali na msaada wa Kompyuta na Mashine hiyo kampuni hiyo pia ilitoa wataalamu kutoka shirika lisilo la kiserikali la Learning  in Sync kwa ajili ya kuweka program maalumu katika kmpyuta za kufundishia na kujifunzia. 
  Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakis alisema kutolewa kwa mashine hiyo ni muendelezo wa msaada ambao Vodacom kupittia mradi wa Pamoja na Vodacom imeendelea kutoa kwa nchi nzima.

  “Huu ni muendelezo wa msaada ulitolewa awali ,Kampuni ya Vodacom tunarudisha sehemu ya faida kwa wananchi na wateja wetu,pamoja na hayo ni kusaidia wadogo zetu kuingia katika digitali wakiwa na umri mdogo na kuwaandaa na maisha ya baadae,”alisema Tzamburakis. 
  Alisema Mashine hiyo ya kisasa itasaidia kupunguza changamoto zilizokuwa zikiikabili shule hiyo hususani katika maandalizi ya mitihani pamoja na machapisho mengine ambayo shule ili lazimika kuingia gharama kubwa kuchapisha.

  Katika kuhakikisha walimu wa shule hiyo wanaweza kutumia vyema mashine hiyo Tzamburakis alisema ofisi ya Vodacom kanda ya Kaskazini itatoa mtaalamu kwa ajili ya kufundisha namna ya kuitumia. 
  “Ofisi ya kanda ya Vodacom ina wataalamu wa IT ambao watasaidia katika kutoa mafunzo kwa walimu ya namna ya kutumia mashine hizi na tutaweka utaratibu wa kufika mara moja kwa mwezi katika shule hii ili waweze kubadilishana uzoefu na walimu wa masomo hayo.”alisema Tzamburakis. 
  Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Shimbwe,Jacob Costantine aliishikuru kampuni ya Vodacom kwa msaada huo huku akieleza changamoto zilizoikabili shule hiyo ikiwemo ya kuchapisha mitihani kwa gharama kubwa .

  “Tumepewa mashine ya Photocopy ikiwa ni ahadi ya mgeni rasmi kutoka Vodacom baada ya kumueleza kuwa tumekuwa tukitumia gharama kubwa hasa kipindi cha mitihani ,kuchapisha mitihani yetu ya mihula na ile ya mwisho wa mwaka”alisema Costantine. 
  Alisema kupatikana kwa mashine hiyo ,sasa shule itakuwa na uwezo mkubwa wa kuchapisha machapisho mbalimbali vikiwemo vitabu ambavyo upatikanaji wake umekuwa mgumu kwa ajili ya wanafunzi hao kujifunzia. 
  Mkuu huyo wa shule alisema wamekuwa wakitumia zaidi ya shilingi Milioni nne kwa ajili ya maandalizi ya mitihani shulebi hapo na kwamba kwa sasa adha ya kuandika ubaoni mitihani ya majaribio itatoweka.

  0 0  0 0


  Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya katikati akiwa na Naibu Waziri wa Ujenzi,
  Uchukuzi na Mawasiliano katikati  Eng. Edwin Ngonyani wakitembelea Bandari ya Tanga .

   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katikati  Eng. Edwin Ngonyani kwenye shuti akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya kushoto akimuelezea namna wanavyofanya kazi kulia ni Moni Jafuri ambaye ni PRO wa Bandari ya Tanga wakati alipofanya ziara ya kuitembelea 
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kwenye shuti katikati akitembelea bandari ya Tanga kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitazama matishari yaliyonununuliwa na Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga yanayotumika kwa ajili ya ukuaji wa mizigo. Picha na Tanga Raha Blog.


  0 0

   The accomplishment of ten years of research, training and service at the Bagamoyo Branch of Ifakara Health Institute was described as a “great hope and bright future” for Tanzania and on international level. Speaking at the symposium to celebrate The Decade of IHI at Bagamoyo, the Director of Preventive Medicine in the Ministry of Health, Gender, Children & Elderly, Dr. Neema Rusibamayila said the future was bright for shaping up the health of the people.
  The symposium was held at the conference hall of Kingani, an ultra modern complex where clinical trials and training are conducted. Speaking on behalf of Deputy Minister Hon. Dr. Hamis Kigwangala who could not attend the function due to other pressing duties, Dr. Neema said local Tanzanian Scientists in collaboration with international institutes and agencies were doing a great work.

  She remarked that the ten years of establishment and service was a contribution towards global health value.

  The Director of the IHI, Dr. Salim Abdulla  who is one of the pioneer in the growth of the institute from ground level said in his presentation; “ over just ten years, these humble beginnings have grown into an international centre of excellence”.  He told his audience in his power point presentation that Bagamoyo was firmly established as a world-class research centre.

  Speaking in both English and Kiswahili, Prof. Marcel Tanner who is Director of Swiss Tropical Institute & Public Health spoke of his satisfaction at the growing trend of the IHI in Bagamoyo and wished everyone a note of congratulation.

  Earlier on the Director  General of COSTECH and Chairman of the Board of IHI, Dr. Hassan Mshinda warmly invited all the stakeholders, collaborating institutes and agencies, members of the public to the symposium. A photographic display of the IHI works and future plannings were arranged as an exhibition for the people.

  Ifakara Health Institute receives most of its financial resources in the form of research grant from competitive calls. Core funding from the Government of Tanzania COSTECH and the Ministry of Health and other significant grants have been received from not less than fifty well known international institutes, agencies of the UN and friendly Governments. 

  Director of Preventive Medicines in the Ministry of Health, Gender, Children and Elderly, Dr. Neema Rusibamayila opening the Symposium Ten Years of IHI in  Bagamoyo
   Director of IHI Dr. Salim Abdulla one of the key role players in the establishment and management of the world-class research centre. He presented a powerpoint narration of the history of IHI Bagamoyo.
  A cross section of scientists, doctors, stakeholders and coordinators who attended the symposium in Bagamoyo, IHI research centre

  0 0

  Sweden imeipongeza Tanzania katika juhudi zake zake za kuhakikisha huduma za kifedha zinasambazwa nchi nzima hadi maeneo ya vijijini, ambapo hayafikiwi na huduma hizo kufuatia huduma za kifedha zinazotolewa na benki ya CRDB, Fahari Huduma, ambazo zimesambaa katika vijiji vyote, hivyo kuifanya Tanzania kuongoza katika nchi za Afrika ya Mashariki kufikisha huduma za kifedha katika maeneo mengi ya vijijini. 
  Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje wa Bunge la Sweden, Bw. Kenneth Forslund, aliyeongoza ziara ya Wabunge wa Sweden, kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofadhiliwa na serikali ya Sweden.  
  Mhe. Forslund, ameisifia Tanzania, kwa jinsi Tanzania inavyotumia vizuri misaada ya kimaendeleo ya Sweden, katika kutimiza malengo yaliyokusudiwa, ambapo moja ya taasisi zilizofadhiliwa na Sweden, ni FSDT inayoifadhili benki ya CRDB, kusambaza huduma za kibenki za Fahari Huduma. 
  Afisa uendeshaji wa Benki ya CRDB Microfinance,  Samson Keenja, amesema baada ya CRDB  kugundua kuwa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania, umewafikia wananchi wachache sana tena wa mijini tuu,  ndipo Benki ya CRDB,  kwa kushirikiana na Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha (FSDT)  wakaanzisha Wakala wa Huduma za Kifedha, (Agents Banking) na CRDB kuanzisha huduma ya Fahari Huduma ambapo mawakala wa Fahari Huduma wametapakaa mpaka vijijini, hivyo kusogeza huduma za kifedha karibu na wananchi. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha nchini FSDT, Bw. Sostenes Kewe, amesema mfuko wake unalenga katika kupanua wigo upatikanaji wa huduma za kifedha kuwafikia watu wengi zaidi, ambapo wameshirikiana na benki ya CRDB katika usambazaji wa huduma hizi. Amesema huduma za kifedha ni muhimu sana katika kuendesha maisha ya wananchi, ni muhimu katika ukuzaji na uendelezaji biashara ndogondogo na za kati, katika ukuaji wa uchumi, utengenezaji ajira na upunguzaji umasikini. 
  Wajasiliamali Mainda Mwakalinga na mumewe, Frank Mwakalinga ambao ni waendeshaji wakala wa Fahari Huduma eneo la Kibamba, wameishukuru benki ya CRDB kuwasogezea huduma za kifedha karibu na maeneo yao, kwa sababu kabla ya hapo, watu wa Kibamba walilazimika kusafiri hadi Mbezi Mwisho au Kibaha kupata huduma za kifedha lakini sasa CRDB imewaletea huduma mpaka mlangoni. 
  Naemjasilamali mdogo, Bi Janet Tomaslisha, anayefanya biashara ndogo ndogo, aliishukuru CRDB kwa kuwasogezea huduma za kifedha na kuwapatia mikopo midogo midogo ya ujasiliamali bila dhamana, aqkasema mikopo hiyo ni midogo mno, hivyo kuwaingizia kipato cha kuendesha tuu maisha yao, lakini akaiomba benki ya CRDB kuwapatia mikopo mikubwa wajasiliamali wadogo wadogo ili waweze kukua na kufanya biashara kubwa kubwa. 
  Naye Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo kwenye Ubalozi wa Sweden nchini, Maria Van Berlekom, akizungumza kwa Kiswahili fasaha, amesema Wabunge hao, wa Sweden wamekuja kujionea hali halisi ya matumizi ya fedha za misaada ya kimaendeleo inayofadhiliwa na Sweden, ili kujiridhisha kama misaada yao inatumika vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa.

  CRDB Microfinance ni kampuni tanzu ya Benki ya CRDB inayojishughulisha na huduma mbalimbali ikiwemo utoaji wa mikopo kwa wajasiliamali wadogo na wakati, huduma za bima, ushauri wa kiuchumi  nan die msambazaji mkuu wa huduma za Fahari Huduma hadi vijijini.

  Afisa uendeshaji wa Benki ya CRDB Microfinance,  Samson Keenja,  akielekeza utoaji huduma za kifedha vijijini kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje wa Bunge la Sweden, Bw. Kenneth Forslund, aliyeongoza ziara ya Wabunge wa Sweden Kibamba, Dar es salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha nchini FSDT, Bw. Sostenes Kewe, akiongea katika ziara hiyo ya wabunge wa Sweden huko Kibamba, Dar es salaam
  Wajasiamali wafaidika wa huduma za Fahari Huduma wa Kibamba kwenye picha ya pamoja na Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje wa Sweden waliowatembelea leo asubuhi.
  Wajasiliamali Mainda Mwakalinga na mumewe, Frank Mwakalinga wakitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje wa Bunge la Sweden, Bw. Kenneth Forslund ,Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha nchini FSDT, Bw. Sostenes Kewe
  M/kiti wa Kamati ya Bunge la Sweden, Bw. Kenneth Forslund, ujumbe wa Wabunge wa Sweden, akipokelewa  na Mjasilamali mwanamke, Mainda Mwakalinga anayeendesha Huduma Fahari Kibamba

  0 0

  Ms Irina Bokova, Director-General of UNESCO
  The theme of the 2016 International Mother Language Day is “Quality education, language(s) of instruction and learning outcomes.”

  This underlines the importance of mother languages for quality education and linguistic diversity, to take forward the new 2030 Agenda for Sustainable Development.

  In Sustainable Development Goal 4, the 2030 Agenda focuses on quality education and lifelong learning for all, to enable every woman and man to acquire skills, knowledge, and values to become everything they wish and participate fully in their societies. This is especially important for girls and women, as well as minorities, indigenous peoples, and rural populations. This is reflected in UNESCO’s Education 2030 Framework for Action, a road-map to implement the 2030 Agenda, encouraging full respect for the use of mother language in teaching and learning, and the promotion and preservation of linguistic diversity.

  Multilingualism is essential to drive these objectives forward – it is vital for success across the 2030 Agenda, regarding growth, employment and health, as well as sustainable consumption and production, and climate change.

  UNESCO brings the same focus to advancing linguistic diversity on the Internet, through support to relevant local content as well as media and information literacy.  Through the Local and Indigenous Knowledge Systems (LINKS) programme, UNESCO is highlighting the importance of mother and local languages as channels for safeguarding and sharing indigenous cultures and knowledge, which are vast reservoirs of wisdom.

  Mother languages in a multilingual approach are essential components of quality education, which is itself the foundation for empowering women and men and their societies. We must recognize and nurture this power, in order to leave no one behind, to craft a more just and sustainable future for all.


  This is UNESCO’s message on this International Mother Language Day.  


  0 0


  0 0
  0 0

  Na Jumbe Ismailly, Singida 
  TIMU ya soka ya Singida United ya mjini Singida hatimaye imekata tiketi ya kucheza ligi daraja la kwanza mwaka huu baada ya kuifunga bila huruma timu ya Abajalo F.C. ya wilayani Igunga,Mkoani Tabora kwa jumla ya magoli 2-0.
   Katika mchezo huo mkali na wa kusisimua uliofanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya michezo wa Namfua mjini Singida na  kuhudhuriwa na wapenzi na washabiki wa soka wachache. Inadaiwa kuwa mchezo huo uliokuwa na mahudhurio hafifu kwa kiasi kikubwa yaliathirika na mchezo kati ya Yanga na Simba za jijini Dar-es-salaam. 
   Singida United iliyocheza ligi kuu mwaka 2000 na kushuka daraja miaka miwili baadaye ililazimika kusubiri hadi dakika ya 50 ndipo ilipopata goli la kwanza kupitia kwa Hassani Mseka. Mseka alifunga goli hilo baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa timu ya Abajalo na kuachia shuti kali lililomshinda kipa Alli Mashaka. 
   Timu ya Abajalo ilianza kulishambulia mfululizo lango la Singida baada ya kufungwa goli hilo la kuongoza,huku ikijikuta ikikosa magoli ya wazi katika dakika ya 69,73 pamoja na 78,kutokana na washambuliaji wake kutokuwa makini pindi walipokuwa wanalikaribia lango la wapinzani wao. 
  Hata hivyo timu ya Singida United ilifanya shambulizi la kushitukiza katika dakika ya 82 na kufanikiwa kufunga goli la pili kupitia kwa Davidi Gregory aliyetokea bechi. 
  Songa Jared wa Singida United aliyeng'ara katika mchezo huo aliwalamba chenga walinzi watatu wa Abajalo na kutoa pasi safi kwa Gregory ambaye alisukumia mpira huo upande wa kushoto wa lango la Abajalo huku kipa Mashaka akijikuta akilamba vumbi upande wa kulia. 
   Katika dakika ya 81 mwamuzi wa mchezo huo kutoka mjini Dodoma Doto Ibrahimu alimtoa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu Ramadhani Mrisho wa Abajalo baada ya kumchezea vibaya Yusuph Kagoma wa Singida United. 
   Wakati huo huo, Singida United imeanza mazoezi makali kwa ajili ya kwenda kuilambisha timu ya Simba ya jijini Da-es-salaam feb,28,mwaka huu zitakapokutana kwenye mchezo wa FA.
   Timu ya soka ya Abajalo F.C. kutoka wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora iliyofungwa jumla ya magoli 2-0 na Singida United juzi kwenye uwanja wa michezo wa kumbukumbu ya Namfua mjiniKwa ushindi huo. Singida United imekata tiketi ya kushiriki ligi daraja la kwanza mwaka huu
  Timu ya soka ya Singida United muda mfupi kabla ya kuifunga Abajalo ya wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora kwa jumla ya magoli 2-0 kwenye mechi ya ligi daraja la pili Taifa na kwa ushindi huo Singida United iliyowahi kucheza ligi kuu mwaka 2002 na kushuka 2002,imekata tiketi ya kucheza ligi daraja la kwanza mwaka huu.
  Hekaheka uwanjani
   Askari polisi wa mjini Singida wakimwokoa mshika kibendera namba moja kupigwa na wachezaji wa Timu ya Abajalo ya mkoani Tabora. Abajalo walipandwa na hasira baada ya kufungwa goli la kwanza na Singida United.
  Wapenzi wa soka wa mjini Singida waliohudhuria pambano kali na la kusisimua kati ya Singida United na Abajalo ya mjini Igunga,Mkoani Tabora

  0 0

  HALMASHAURI ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora inatarajiwa kukusanya jumla ya shilingi 40,324,170,000/= kutoka katika vyanzo vyake vya ndani,ruzuku kutoka serikali kuu pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa mwaka wa  fedha wa 2016/2017.
  Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora,Rustica Turuka katika taarifa iliyosomwa kwa niaba yake na mweka hazina wa Halmashauri ya wilaya,Gordon Julius Dinda kwenye kikao maalumu cha bajeti cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
  Aidha Mkurugenzi mtendaji huyo aliweka bayana kwamba taarifa ya mapendekezo ya mpango na bajeti ya Halmashauri ya Igunga ya mwaka 2016/2017 yameandaliwa kwa kuzingatia mwongozo wa uandaaji wa mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
  Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo kutokana na vyanzo vya ndani,Halmashauri inakisia kukusanya jumla ya shilingi 2,678,218,000/= ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia  11.84 ikilinganishwa na makisio ya mwaka 2015/2016.
  “Ruzuku kutoka serikali kuu kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo ni shilingi 35,905,165,000/= na ruzuku kutoka kwa wahisani ni shilingi 1,745,787,000/=”alifafanua mkurugenzi huyo.
  Kuhusu matumizi ya makusanyo hayo,Turuka alibainisha kuwa jumla ya shilingi 29,913,325,000/= ambazo ni sawa na asilimia 74.18 zinatarajiwa kutumika kulipa mishahara ya watumishi,wakati shilingi 3,721,909,000/= sawa na asilimia 9.23 zinatarajiwa kutumika katika matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo zinatarajiwa kutumika shilingi 6,688,936,000/= sawa na asilimia 16.59.
  Alisema Halmashauri hiyo inatarajia kupokea kutoka kwa wadau wa maendeleo shilingi 1,745,787,000/=kutoka Mfuko wa pamoja wa Afya,shilingi  622,971,000/=,Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) shilingi 55,914,000/=,Mradi wa Maendeleo ya Sekta ya Maji shilingi 878,652,000/=,Mradi wa Usafi Binafsi (WASH) shilingi 54,000,000/= na Mfuko wa Umwagiliaji wilaya (DIDF) shilingi 134,250,000/= na hivyo kufanya jumla ya shilingi 1,745,787,000/=.
  Wakati huo huo,Mkuu wa wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora,Zipora Pangani alisisitiza kwamba bajeti iliyopendekezwa 2016/2017 iangalie barabara za baadhi ya  kata mpya zilizoanzishwa mwaka jana ili ziweze kupitika na kuirahisishia kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo inapokwenda katika maeneo hayo kushughulikia changamoto mbalimbali kusiwe na vikwazo vya kupita.
  Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Manonga,Seif  Hamisi Gulamali hakusita kusisitiza juu ya umuhimu wa bajeti hiyo kuhakikisha miradi viporo inakamilishwa kwanza badala ya kuanzisha miradi mingine mipya.
  Hata hivyo mbunge huyo aliwatahadharisha pia watendaji wa Halmashauri hiyo kwamba hatakuwa tayari kuvumilia watendaji wabadhirifu wa fedha za wananchi na kwa yeyote yule atakayebainika ajiandae kufikishwa katika vyombo vya sheria,ikiwa ni pamoja na kufikishwa Mahakamani.

  Akifunga kikao hicho maalumu cha bajeti,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Peter Onesmo aliwahimiza watendaji kuongeza jitihada katika ukusanyaji wa mapato huku akisisitiza pia madiwani kusimamia matumizi ya fedha za serikali pamoja na wahisani.

  0 0

  SERIKALI wilayani Mkalama,Mkoani Singida imemuagiza afisa mtendaji wa Kata ya Ilunda,tarafa ya Nduguti kuwasaka na kuwakamata mara moja viongozi wa Vijiji na Vitongoji wanaotuhumiwa kuuza chakula kilichotolewa msaada na serikali kwa watu wanaokabiliwa na tatizo la njaa kwa bei ya shilingi 2,000/= badala ya shilingi 1,000/= kwa kilo 20. 
   Agizo hilo limetolewa na Mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki,Allani Kiula kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nkungi, kufuatia malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wananchi kwamba licha ya chakula hicho kutakiwa kuuzwa kwa bei ya shilingi 50 kwa kilo lakini wamekuwa wakiuziwa kwa bei ya shilingi 2,000/=. 
   Kwa mujibu wa mbunge huyo kutokana na chakula hiho kuuzwa kwa bei ya juu kuliko walivyotegemea,idadi kubwa ya wananchi hao wamekuwa wakipata taabu ya kukinunua,jambo ambalo limewaumiza kwa sasa kutokana na kutokuwa na fedha katika kipindi hiki kigumu wanachokabiliana na tatizo hilo la njaa. 
   Kwa upande wake mmoja wa watu wenye ulemavu wa viungo,Eliasi Manya akitoa malalamiko hayo kwa Mbunge huyo alisema kwamba kutokana na kukosa chakula hicho cha msaada huku wao wakiwa hawana uwezo,kumechangia wao kuishi maisha ya kuombaomba huku wakiwa hawana uhakika wa hata mlo mmoja wa chakula.
  “Juzi tumepewa posho hapa tuliambiwa posho hii inauzwa kwa kilo shilingi hamsini,ajabu nilipewa debe moja nikawa nimelipa shilingi elfu mbili sijui ndiyo nimenunua hela ngapi kwa kilo moja sijaelewa”alifafanua mzee huyo. 
   Hata hivyo Manya hakuishia kulalamikia suala la chakula cha msaada peke yake bali alizungumzia pia kitengo cha kunusuru kaya maskini kwamba baada ya kupokea fedha zinazotolewa na mfuko huo walitakiwa kukatwa shilingi 10,000/- kila mmoja kwa ajili ya kujiunga na Mfuko wa afya ya jamii (CHF ). 
   Alifafanua zaidi mwananchi huyo alibainisha kwamba licha ya kukatwa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kunufaika na huduma za matibabu,lakini mpaka sasa wanapokwenda hospitalini watakiwa kulipa shilingi 30,000/=,jambo ambalo alishindwa kufahamu zile alizokatwa zimeingia katika mfuko gani. 
   Naye Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kiduguwi, Christopher Gyunda anayetuhumiwa kuuza chakula hicho cha msaada kwa bei kubwa,licha ya kukiri kuuza chakula hicho kwa bei ya shilingi 800 badala ya shilingi 50 kwa kilo,lakini alikanausha kuhusika na tuhuma zilizoelekezwa kwake kwamba ameuza chakula hicho kwa bei ya shilingi 2,000/=
   Mmoj ya wananchi waliohudhuria kwenye mkutano wa mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki kumsikiliza alipokuwa akizungumzia masuala ya maendeleo ya jimbo hilo.
   Wananchi waliohudhuria kwenye mkutano wa mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki kumsikiliza alipokuwa akizungumzia masuala ya maendeleo ya jimbo hilo.
   Wananchi waliohudhuria kwenye mkutano wa mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki kumsikiliza alipokuwa akizungumzia masuala ya maendeleo ya jimbo hilo.
   Mbunge wa jimbo la Iramba mashariki(CCM)Bwana Allani Kiula (aliyeshika karatasi) akitoa maagizo ya kukamatwa kwa viongozi waliouza chakula cha msaada katika Kijiji cha Nkungi,tarafa ya Nduguti,wilayani Mkalama.


  0 0

  Na Jumbe Ismailly,Singida   
  CHAMA Cha Mapindizi  Mkoa wa Singida kinatarajia kufanya uchaguzi wa kuziba pengo la nafasi ya mwenyekiti CCM Mkoa lililoachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho,Mgana Izumbe Msindai aliyehamia CHADEMA. 
  Mkutano huo maalumu unaotarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 900 utafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki mjini Singida. 
  Katibu wa CCM Mkoa wa Singida,Mary Maziku alisema kuwa maandalizi yote muhimu yamekwisha kamilika na kwamba kinachosubiriwa ni muda tu utakapowadia. 
  Aidha Maziku alifafanua pia kwamba mkutano huo unaotarajiwa kuanza rasmi saa nne asubuhi,unatarajiwa kusimamiwa na mjumbe wa kamati kuu Halmashauri kuu Taifa CCM,Dk.Mohammed Seif Khatibu akisaidiwa na Saidi Bakari Is-hak pamoja na Saidi Mhando. 
  Kwa mujibu wa Maziku waliogombea nafasi hiyo na kuteuliwa na kamati kuu ni pamoja na Narumba Barnaba Hanje, Juma Hassani Kilimba, Mohamed Missanga, Hamisi na Martha Mosses Mlata. 
  “Wagombea wetu hawa wapo na wapo tayari kabisa kushiriki kwenye kinyang’anyiro hicho kwa utulivu mkubwa na nadhani wote wanatambua kwamba mwisho wa zoezi mmoja wao atakuwa mshindi”,alisisitiza Katibu huyo.
   Wajumbe wa UWT wilaya ya Mkalama wakiwa kwenye ukumbi wa mkutano wa ofisi za chama hicho mjini Nduguti
   Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida,Bi Martha Mosses Mlata katika mkutano wa wanawake wa UWT wilaya ya Mkalama kwenye moja ya mikutano yake ya kukiimarisha chama cha Mapinduzi.
  Mbunge wa viti maalumu(CCM) Mkoa wa Singida,Bi Martha Mosses Mlata(wa kwanza kutoka kushoto) akiongea na kijana mwenye ulemavu wa ngozi(albino) akimzawadia zawadi ya fedha taslimu zitakazomsaidia kununua mafuta ya ngozi na wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Iramba,Bi Miano

  0 0


  0 0

   HAYA SHIME WADAU WA BONGO MOVIE MNAOMBWA KUMPIGIA KURA SINGLE MTAMBALIKE "RITCHIE RITCHIE" AWEZE KUSHINDA TUZO ZA FILAMI ZA AFRICA MAGIC HUKO NIGERIA WIKI IJAYO. UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUINGIA KATIKA TOVUTI YA AMVC KWA LINK HII 
  KISHA KAMA UNA ACCOUNT YA DSTV FUATA MAELEKEZO. 
  KAMA HUNA ACCOUNT DSTV JISAJILI  http://africamagic.dstv.com/  
  KISHA NENDA SEHEMU YA AMVCA VOTE KWA CATEGORY ZINAZOONEKANA HAPO CHINI.
  HAYA WADAU NA TUFANYE KWELI ILI RITCHIE AKATUPEPERUSHIE BENDERA YETU NIGERIA!!  0 0


  0 0

  Wadau wa filamu nchini tunaomba muendelee kuipigia kura filamu yetu ya Mpango Mbaya ilichezwa na washiriki wachanga kabisa ambao ni zao la Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Msimu wa Kwanza.

  Filamu ya Mpango Mbaya ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu na ndio sababu kubwa iliyopelekea kuingia katika Kinyanganyiro cha African Magic Viewers Choice Awards 2016 katika kipengele cha BEST MOVIE - EAST AFRICA.

  Jinsi ya Kupiga Kura tembelea tovuti hii http://amvca2016 awards.dstv.com/nominees/best-movie-east-africa_2 

  Na kama hauna akaunti DSTV unachotakiwa ni kujisajili kupitia kiunganishi hiki http://africamagic.dstv.com/ halafu nenda sehemu ya AMVCA halafu pigia kura kipengele cha BEST MOVIE - EAST AFRICA chagua MPANGO MBAYA hapo utakuwa umeiwezesha filamu ya MPANGO MBAYA kuisaka nafasi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania nchini Nigeria. Tuendelee Kupiga Kura Ili Tulete Heshima Nyumbani ni Zamu ya FIlamu sasa.

  0 0

   Meza kuu ikifuatilia kwa makini yanayojiri katika kikao cha uzinduzi wa Mwongozo wa kwanza wa kitaifa wa elimu na ulinzi kwa mtumiaji wa huduma za fedha” (N-FEF).
   Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.
   Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania akieleza jambo wakati wa uzinduzi Mwongozo wa kwanza wa kitaifa wa elimu na ulinzi kwa mtumiaji wa huduma za fedha” (N-FEF).
  Bi. Susan Rutledge, Mtafiti na Mshau
  ri wa masuala ya fedha, akieleza umuhimu wa elimu ya masuala ya fedha kuelekezwa kwa wananchi.

  BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), kwa kushirikiana na Mfuko wa Kuendeleza Huduma za Kifedha Tanzania (FSDT), imezindua Mwongozo wa taifa wenye lengo la kuongeza uelewa kuhusu elimu ya mambo ya fedha kwa wananchi.

  Uelimishwaji wa wananchi kuhusu mambo ya fedha utatekelezwa kupitia “Mwongozo wa kwanza wa kitaifa wa elimu na ulinzi kwa mtumiaji wa huduma za fedha” (N-FEF)

  Gavana Prof. Beno Ndulu ameuzindua rasmi mwongozo huu ambao utajikita katika kutatua changamoto zilizobainishwa katika utafiti uliopima uelewa wa mambo ya fedha kwa watu wazima nchini Tanzania. Utafiti huu unaitwa “Uwezo wa Kifedha Tanzania” wa mwaka 2014. 

  Utafiti huo umebainisha kuwa watanzania wengi hawana elimu na ujuzi mahususi wa  masuala ya mambo ya fedha kwa ujumla, hivyo kuwanyima fursa ya kutumia huduma za kifedha kwa faida yao. 

  Katika utafiti huo imeonyeshwa kuwa upatikanaji wa huduma za fedha umekuwa na changamoto katika maeneo mengi huku zile zitolewazo kwa njia ya mitandao bado hazikidhi matarajio ingawa zinawafikia  wateja wengi kwa sasa. 

  Sambamba na hilo kumekuwa na uhaba wa nyenzo na miundombinu ya kuhifadhi na kufikisha taarifa za fedha kwa watumiaji wa huduma hizo  kwa kuzingatia namna sahihi ya kutoa taarifa, kuwaelimisha na kuwalinda.

  Kutokana na utafiti wa “Uwezo wa Kifedha Tanzania” wa mwaka 2014 wananchi kutoka makundi mbalimbali katika jamii hawana ujuzi wa hesabu za kawaida  ambao ndiyo msingi mkuu katika nadharia ya masuala yahusuyo mambo ya fedha.  

  Elimu msingi katika masuala ya fedha umekuwa kikwazo kwa waliowengi  hasa katika uandaaji wa bajeti, kutunza kumbukumbu ya matumizi, kupanga fedha kwa matumizi yasiyotegemewa ama ya ziada na muhimu zaidi kutunza kiasi kwa ajili ya matumizi ya uzeeni (baada ya kustaafu).

  Inaonekana kuwa upatikanaji wa taarifa za masuala ya fedha hutegemea zaidi vyombo vya habari kama redio, televisheni na magazeti lakini vyombo hivi kwa sehemu kubwa,  hufikisha zaidi taarifa za biashara na masoko kuliko ambavyo vinaelimisha jamii kuhusu matumizi na upangaji wa mapato yao.

   “Haya ndiyo masuala mahususi ambayo  mwongozo huu wa taifa kuhusu elimu ya huduma za fedha unalenga kushughulika nayo,” alisema Prof Ndulu.

  Pamoja na kuwepo ongezeko la upatikanaji wa huduma za kifedha, mpaka asilimia 58  mwaka 2013 kutoka kiwango cha asilimia 17 mwaka 2009, miongoni mwa watu wazima nchini, bado mwongozo huu ni muhimu ili kuleta mfumo imara wa sekta ya fedha na Zaidi sana ili kuleta ustawi wa maisha ya watanzania kwa ujumla.

  Prof. Ndulu anasema kutatua changamoto za kielimu kwa ujumla na hususan elimu ya huduma za fedha italiwezesha taifa kuwa katika mwelekeo mzuri wa kukabiliana na umasikini na kufikia malengo ya kukuza uchumi.

   “Tunapaswa kujiuliza: ni kwa namna gani wananchi hasa wale masikini na wasiokuwa na elimu za kifedha  za wanapambana kuendeleza biashara zao katika mazingira ya soko huria na lenye ushindani kila uchwao” alisisitiza Prof. Ndulu.

  Hivyo, mwongozo huu utahakikisha watanzania wapata elimu sahihi na ya uhakika ya huduma za kifedha pamoja na njia anazoweza nazo kujilinda katika ushindani huu.

  Vilevile mwongozo huu umeundwa ili kutatua changamoto za kifedha zinazohusiana na maamuzi miongoni mwa watumiaji wa huduma hizi na kuwa jumuishi na wenye tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.

  Mwongozo wa taifa kuhusu elimu ya huduma za fedha umeandaliwa kwa kujumisha washikadau kutoka Tanzania bara na Zanzibar.

  Unabainisha changamoto zinazohusuana na uwezo wa kifedha ambazo zinahitaji kutatuliwa kwa uwepo wa elimu ya fedha. Pia, unatoa taratibu wakufanikisha utekelezaji wa elimu ya fedha, na mwongozo wa kitaifa wa kuratibu elimu ya fedha nchini.

  Lengo la mwongozo wa elimu ya huduma za fedha ni kuwa na wananchi na kaya zenye uwezo kifedha nchini.

  0 0

   Mlalamikaji wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya ubunge jimbo la kigoma kusini David Kafulila akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama ya hakimu mfawidhi mkoa wa Kigoma baada ya Jaji kuhairisha kesi yake
   Wakili wa kafulila profesa safari akiongea na waandishi nje ya mahakama ya hakimu mfawidhi wa mkoa baada ya jaji kuhairisha kesi.
  Baadhi ya wananchi wa mkoa wa kigoma wakiwa nje ya viunga vya mahakama ya hakimu mfawidhi wa mkoa kwaajili ya kusikiliza kesi ya David Kafulila wa NCCR Mageuzi ya kupinga matokeo ya ubunge dhidi ya Hasna Mwilima wa CCM


  Na Editha Karlo wa blog ya jamii Kigoma

  KESI No. 2 ya mwaka 2015 ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma kusini iliyofunguliwa na mlalamikaji  David Kafulila dhidi ya mbunge Hasna Mwilima,Msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria mkuu wa serikali imeahirishwa leo na mahakama kuu kanda ya Tabora mpaka  marchi 9, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa tena.

  Kesi hiyo ambayo ilikuwa  ianze mapema leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kigoma,  Mbele ya Jaji Dr Wambari ambae pia ni Mkuu wa chuo cha sheria lushoto mkoani Tanga, imeahirishwa kwasababu mshatakiwa Hasna pamoja na wakili wake Kennedy Fungamtama pamoja na mawikili wa serikali kushindwa kufika mahakamani hapo, kwa madai ya kuchelewa kupata wito wa mahakama hyo, huku mlalamikaji David Kafulila akifika na wakili wake Prof Safari.

  Katika mazingira hayo Jaji Wambari aliagiza mawasiliano yafanyike kwa pande hizo ili kujua ni lini kwa hakika mawakili hao wataweza kushiriki katika kesi hiyo.

  Kutokufika kwa mlalamikiwa  na mawakili wake na wale wa upande wa serikali ilipelekea zoezi la kusikiliza kesi hiyo kusimama kwa saa mbili kutoka saa tano asubuhi  mpaka saa saba mchana na baada ya hapo hakimu mfawidhi wa Mkoa wa Kigoma kwa niaba ya Jaji silivesta Kahinda alisema  kuwa kesi itaendelea march 9 mwaka huu na kwamba kwakuwa tarehe hiyo imependekezwa na mawakili na pande zote mbili.

  Akiongea na mtandao huu mlalamikaji wa kesi hiyo David Kafulila alusema luwa anakubiana na uamuzi wa mahakama hivyo aliwataka wananchi wawe na subiri hadi hiyi tarehe 9 march mwaka huu.

  ""Jaji mkuu na Jaji kiongozi wamekuwa dhamira  kwa sasa kuwa kesi za uchaguzi zimalizike haraka na hivyo kufikia tarehe hiyo ya march 9,  kesi inatarajiwa kusikilizwa mfululizo hadi itakafik

older | 1 | .... | 1132 | 1133 | (Page 1134) | 1135 | 1136 | .... | 3348 | newer