Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

TBC YAPATA BODI MPYA YA WAKURUGENZI, Balozi Herbart Mrango Mwenyekiti

$
0
0
(Video na Benedict Liwenga-Maelezo)
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mosses Nnauye akiongea na wanahabari kuhusu uteuzi  wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya TBC Balozi Herbart Mrango ambao umefanywa na Rais John Pombe Magufuli,uteuzi huoumeanza kuanzia tarehe 19/02/2016, kulia ni Mkurugenzi msaidizi Usajili wa magazeti Bw. Raphael Hokororo

MKUTANO WA MHE. NAPE MOSSES NNAUYE, WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO NA WAANDISHI WA HABARI


TAREHE 20/02/2016


Dondoo za Kuzungumzia;

Napenda kuwafahamisha kuwa kufuatia Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kumaliza Muda wake, uundwaji wa Bodi Mpya umekamilika. Ni vyema kuwafahamisha kuwa katika utaratibu wa kisheria wa kuunda Bodi ya TBC mwenye Mamlaka ya kisheria ya Kumteua Mwenyekiti wa Bodi ni Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania.

Napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TBC iliyomaliza muda wake, Prof. Mwajabu Possi na wajumbe wake wote kwa kazi waliyoifanya kwa muda wote wa uhai wa bodi hiyo. Ninaamini Bodi Mpya itaendeleza yale mazuri yote yaliyofanyika na Baodi iliyopita na kubuni mambo mengine mapya ili kuongeza tija kwa Shirika.

Baada ya kutoa maelezo haya ya awali, sasa nichukue fursa hii kuwajulisha yafuatayo;

1.   Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Mhe. Balozi Herbert E. Mrango (pichani) kuwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya TBC. Uteuzi huu unaanza tarehe 19/02/2016 kwa kipindi cha miaka Mitatu.

Balozi Mrango kielimu ana shahada ya Uzamili katika uendelezaji wa Mifumo (MSc – Systems Development) aliyoisomea Chuo Kikuu cha Dublin Nchini Uingereza. Aidha amehitimu Shahada ya kwanza ya Takwimu za Kiuchumi katika Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Tanzania.

 Balozi Mrango alishashika nyadhifa mbalimbali, zikiwemo kuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara  ya Miundombinu Kuanzia Februari, 2011 hadi September, 2013.
 Nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Balozi Mrango kwa kuaminiwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huu muhimu. Aidha nimhakikishie Mwenyekiti huyu Mpya wa TBC kwamba kwa kuwa Shirika la TBC liko chini ya Wizara yangu, tutampa ushirikiano wa kutosha ili kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika shirika letu la Utangazaji.

2.   Kwa mujibu wa Sheria iliyounda TBC, baada ya Mhe. Rais kumteua Mwenyekiti wa Bodi, Waziri mwenye dhamana na shughuli za utangazaji,  anateua Wajumbe sita wa Bodi. Katika uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina ilishatupatia vigezo vya utaalamu wa wajumbe wakati wa uteuzi.


Hivyo basi, mimi Nape Moses Nnauye, nikiwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, kwa kuzingatia vigezo vilivyobainishwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kwa kufuata taratibu zingine za kufanya uteuzi, nimewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya TBC; 


(i)                Bw. William Steven Kallaghe; Mtaalamu wa Uchumi.  (M.A – Economics; Head of Public Policy: NBC Bank  Tanzania ).


(ii)             Bw. Mustapha Kambona Ismail; Mtaalamu wa Sheria.(LLB - UDSM; Associate Director, Litigation & Investment – Bank of Tanzania; Advocate of the High Court of Tanzania).


(iii)           Bi. Elimbora Abia Muro; Mtaalamu waUhasibu. (CPA, MBA: Senior Internal Auditor, Tanzania Investment Centre).


(iv)           Bw. Mick Lutechura Kiliba; Mtaalamu wa Rasilimali watu. (MBA – Public Service Mgt; Director of Management: President’s Office – Public Service Management).


(v)             Dkt. Ayub Rioba; Mtaalamu wa Sekta ya Utangazaji na Utangazaji.  (PhD – Mass Communication; Associate Dean: School of Journalism, University of Dar Es Salaam) na


6. Bw. Assah Andrew Mwambene; Mtaalamu wa Sekta ya Habari.( MSc – Media Research and Analysis; Director of Information: Ministry of Information, Culture, Arts and Sports).


Uteuzi wa wajumbe hawa ni kuanzia tarehe 19/02/2016 kwa muda wa miaka mitatu.


3.   Nimalizie kwa kuwapongeza tena wote waliopata uteuzi huu. Tuna matumaini makubwa toka kwao kwa ajili ya kuboresha ufanisi wa TBC katika tasnia ya Utangazaji katika ulimwengu wa Teknolojia inayobadilika kwa kasi kubwa duniani. Ni imani yangu kwamba Bodi hii mpya italeta msukumo mpya katika utendaji wa Shirika ili hata watumishi wanaofanya kazi katika shirika hili waendelee kujivunia kuwa ndani ya TBC lakini pia Umma wa Watanzania wajivunie viwango vya utendaji wa Shirika hili.


TANZIA TASWA: MWANAHABARI WA MICHEZO NA BURUDANI FRED MOSHA 'MKUU' AFARIKI DUNIA LEO

$
0
0
Habari wadau, 
Kwa masikitiko makubwa naomba kuwajulisha kuwa mwanafamilia mwenzetu katika uandishi wa habari za michezo na burudani Fred Mosha ‘Mkuu’ (pichani) amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa.
Naomba tushirikiane na familia katika kipindi hiki kigumu. Marehemu alikuwa akiishi Mbagala Saku kwa Mkongo. Mipango tutajulishana kadri nitakavyopata taarifa. Marehemu alikuwa akifanya kazi Redio Tumaini, hivyo naamini tutapata taarifa vizuri muda si mrefu.

                                                            Ahsanteni,
Katibu Mkuu TASWA
20/02/2016

EAC Elections Observer Mission's Preliminary Statement to the Uganda General elections

"TRANSCATHETER " NJIA SALAMA ZAIDI KWA TATIZO LA TUNDU LA MOYO KWA WATOTO

$
0
0
DK. C.S Muthukumaran, mtaalamu wa magonjwa 
ya moyo kwa watoto kutokahospitali za Apollo.

Watoto wachanga wanaozaliwa na tatizo la tundu kwenye moyo, linalosababishia kudumaa katika ukuaji wao na hata kuwa na matatizo ya moyo wanashauriwa kupata matibabu ya kuziba tundu hilo kwa njia ya mrija bila kufanyiwa upasuaji. Hayo yamesemwa na DK. C.S Muthukumaran, mtaalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka hospitali za Apollo.
(VSD) ni tundu katika ukuta unaotenganisha ventriko ya upande wa kulia na kushoto katika moyo. Ni tatizo linalotokea mara nyingi wakati wa kuzaliwa kwa mtoto na linaweza tokea lenyewe au kama ugonjwa.
Ni kawaida kwa watoto wote kuzaliwa na tundu dogo katikati ya atria mbili na mara nyingi tundu hilo huziba ndani ya wiki chache. Mara nyingi hakuna tundu kati ya ventiko hizo mbili, ila baadhi ya vichanga huzaliwa na tundu hilo ambalo linakuwa ni chanzo cha magonjwa ya moyo na ndio sababu kubwa  ya watoto wachanga wengi kuonana na wataalamu wa magonjwa ya moyo. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

$
0
0
Simu.Tv: Shirika la umeme nchini TANESCO laagizwa kupeleka umeme katika kituo cha afya cha Upuge Tabora ili kiweze kutoa huduma ya upasuaji;https://youtu.be/uteSuCCjT6c 
 Simu.Tv: Vyama vya siasa vyaendeleza ukandamizaji wa makundi maalum ndani ya vyama hususani katika nafasi za uongozi; https://youtu.be/6MJzYrpT2EU
 Simu.Tv: Upanuzi wa barabara eneo la Meli nne wasababisha uharibifu wa miundombinu ya maji hali iliyoleta athari kwa wakazi wa eneo hilo;https://youtu.be/dETBa40mFYw   
 Simu.Tv: Mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga kurindima leo katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam; https://youtu.be/P9K5cYjPzrc 
Simu.Tv: Fahamu mengi kutoka kwa wadau wa baraza la Sanaa la taifa BASATA wakikujuza mengi kuhusu masuala ya usajili wa wasanii:https://youtu.be/a5LaAIL9X9U
 Simu.Tv: Jifunze mambo mengi kutoka katika jumuiya ya vijana visiwani Zanzibar yanayokuhusu vijana ususani Fursa kwa vijana: https://youtu.be/gpNUUbI75V8


Baraza la Michezo Tanzania (BMT) limemteua Bwana Said Kiganja kuwa Katibu Mtendaji mpya wa Baraza

$
0
0

Baraza la Michezo Tanzania (BMT) limemteua Bwana Said Kiganja kuwa Katibu Mtendaji mpya wa Baraza hilo kuanzia leo, ili kujanza nafasi ya aliyekuwa Katibu Mtendaji Baraza hilo ambaye uteuzi wake umetenguliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye na kumrudisha Wizarani ili aweze kupangiwa majukumu mengine.
Uteuzi huo ni kwa mujibu wa Sheria iliyoundwa na BMT kifungu namba 5(1) ambacho kinampa mamlaka Mwenyekiti wa BMT kuteua Katibu Mtendaji baada ya kupata idhini ya Waziri mwenye dhamana. 
Kabla ya uteuzi huo Bwana Kiganja alikuwa ni Afisa Michezo Mkuu katika ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuanzia mwaka 2015 mpaka uteuzi wake ulipo fanyika. Pia bwana Kiganja aliwahi kufanya kazi kama Afisa Mwandamizi Michezo wa Baraza la Michezo Tanzania na Afisa Michezo Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu.
Bwana Kiganja ana shahada ya kwanza ya elimu upande wa masuala ya michezo na utamaduni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
Imetolewa na Mwenyekiti wa BMT
Deonis Mallinzi
19/02/2016

PUNDE NDANI YA CCM KIRUMBA NI WENYEJI TOTO AFRICANS v KAGERA SUGAR....

$
0
0
Punde ni Toto Africans yenye maskani yake hapa Jijini Mwanza dhidi ya Wakata Miwa Kagera Sugar ya Bukoba ambayo mpaka sasa inatumia Uwanja wa Shinyanga kama wa Nyumbani baada ya Uwanja wa Kaitaba kuwe kwenye marekebisho ya Ujenzi ili uwe wa kisasa. Mtanange huu unategemewa kuanza saa 10:30 jioni hii kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.Taswira mchana huu Uwanja wa CCM Kirumba unavyoonekana

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO MAALUM WA WANARUKWA NA KATAVI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Februari 20, 2016 kufungua mkutano Malum wa Wanarukwa na Katavi.
 Waziri Mkuu, Kasim Majlaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda wakifurahia ngoma baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Februari 20, 2016 kufungua mkutano Malum wa Wanarukwa na Katavi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakitazama baadhi ya magari ambayo baba wa taifa , Mwalimu Julius Nyerere aliyatumia kwenye miaka ya 1950 na 1960 baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Februari 20, 2016 kufungua mkutano Malum wa Wanarukwa na Katavi
 Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akizungumza katika mkutano Maalum wa Wanarukwa na Katavi uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam Februari 20, 2016
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akifungua   mkutano Maalum wa Wanarukwa na Katavi  kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam Februari 20, 2016. 
 Baadhi ya wananchi wa Mikoa ya Katavi na Rukwa wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majliwa wakati alipofungua  mkutano maalum wa  Wanarukwa na Katavi  kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam Februari 20, 2016.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akionyesha Tuzo Maalum aliyotuzwa na  Wanarukwa na Katavi katika mkutano wao maalum uliofunguliwa na Waziri Mkuu,  Kassim Majalwa kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam Februari 20, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

YANGA YAIUA SIMBA KWA BAO 2-0 UWANJA WA TAIFA LEO

$
0
0
 Dakika 90 za Mtanange wa Watani wa Jadi, Simba na Yanga zimemalijika jioni hii hapa uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam kwa kutoka kifua mbele kwa timu ya Yanga baada ya kuchapa Simba bao 2-0. Magoli ya mchezo huo yametiwa kimiani na washambuliaji Donald Ngoma (Dakika ya 38 kipindi cha kwanza) na goli la pili limefungwa na Amissi Tambwe (Dakika ya 34 kipindi cha pili) na kufanya matokeo kubaki hivyo hadi mwisho wa mchezo.PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donald Ngoma (11) akimpiga chenga Golikipa wa Timu ya Simba, Vicent Angban na kupachika bao la kwanza kwa timu yake wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0. 
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donald Ngoma akishangilia Goli aliloipatia timu yake, wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0. 
Golikipa wa Timu ya Simba, Vicent Angban akiwa amejiweka tayari kuokoa mpira uliokuwa ukielekezwa langoni kwake.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Haruna Niyonzima akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya Simba, Kessy Ramadhan, wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0. 

Wingi wa vizuizi wawakera wafanyabiashara wa mazao ya misitu

$
0
0
Na. Ahmad Mmow,Lindi.

Wingi wa vizuizi vya ukaguzi barabarani umetajwa kusababisha rushwa na usumbufu kwa wafanyabiashara wanaosafarisha mazao ya misitu.

Hayo yalielezwa jana na wafanyabiashara wa mbao na magogo kwenye warsha ya wafanya biashara wa mbao na magogo wa uwanda wa Selous hadi Ruvuma, iliyofanyika jana katika manispaa ya Lindi.



Wakizungumza kwenye warsha hiyo iliyoandaliwa na mashirika ya kiraia ya Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF), Mtandao wa Kijamii wa Usimamizi wa Misitu(MJUMITA) uhifadhi, usimamizi na maendeleo ya mpingo(MCDI) kupitia kampeni ya mama misitu inayofadhiliwa na serikali ya Finland kupitia ofisi za WWF zilizopo nchini, walisema vizuizi hivyo vinasababisha rushwa, usumbufu na kuwapotezea muda.


Frank Nganyanyuka alisema wingi wavizuizi unasababisha wafanyabiashara hao kupoteza muda mwingi barabarani.


Alisema kutoka Nachingwea hadi Dar-es-Salaam kuna vizuizi takribani 19, ambavyo vinasababisha wachelewe barabarani

"Wastani kila eneo lenye kizuizi tunatumia saa moja, maana yake siku mzima inakwisha kwa ajili ya kusimama, vizuizi vipunguzwe havinafaida zaidi ya kuchochea rushwa tu," alisema Nganyuka.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

WAZIRI NAPE AONGEZA HAMASA MECHI YA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (kushoto)walipokutana katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.(Picha na: Frank Shija,WHUSM)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.
Mabeki wa Timu ya Simba wakiokoa mpira wa hatari katika lango lao wakati wa mechi dhidi ya Yanga iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imeisha kwa wenyeji Yanga Afrika kuibuka kidedea kwa mabao 2:0.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba akishangilia mara baada ya Donald Ngoma kuiandikia Yanga bao la kwanza mnamo Dakika ya 38 ya mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0.
Mbunge wa Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mhe. Venance Mwamoto akifuatilia mchezo kati ya Yanga Afrika na Simba SC uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0.
Mashabiki wa Timu ya Simba SC wakifuatilia mchezo kati yao na Yanga Afrika uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0.

Waimbaji wazidi kumiminika Tamasha la Pasaka

$
0
0
Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd ambao ndio waandaaji wa tamasha la Pasaka,Bwa.Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ofisi kwake kuhusiana na tamasha lake ambalo wanasanii wengi wameanza kumiminika kuunga mkono tamasha hilo.

WAIMBAJI  wa nyimbo za Injili Tanzania Sifael Mwabuka na Goodluck Gozbert wamethibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka 2016 linalotarajia kufanyika baadhi ya mikoa ya Kanda ya ziwa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi  ya tamasha hilo, Alex Msama  waimbaji hao ni muendelezo wa kufanikisha ibad hiyo inayotarajia kufanyika mikoa ya Geita (Machi 26), Mwanza (Machi 27) na Kahama (Machi 28).

Msama alisema wanaendelea na maandalizi ya kufanikisha tamasha hilo ambalo lina dhamira ya kukemea mauaji ya walemavu wa ngozi ‘albino’ kupitia waimbaji wa muziki wa Injili watakaopanda jukwaani siku hiyo.

Msama alitoa wito kwa wakazi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kwa sababu sehemu ya mapato ya tamasha hilo yanalengwa kusaidia kununulia baiskeli zaidi ya 100  za walemavu ambazo zitagawiwa kwa wahusika.

Aidha Msama alitaja viingilio katika mchezo huo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na shilingi 2000 kwa watoto.Msama alisema hivi sasa waimbaji mbalimbali waliothibitisha kushiriki tamasha hilo wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya tamasha hilo.

VIDEO YA KIPINDI MAALUM: RAIS MAGUFULI ALIPOKUTANA NA MAKUNDI MBALIMBALI IKULU

In Loving Memory of Miss Neema Edward Mkwelele

$
0
0
  On behalf of the Neema’s family, Friends and Neema Memorial Foundation we are hereby  inviting you to remember and celebrate the death and life of  their beautiful  girl whose life was shortly  taken from this world very much too soon on February 21, 2011 in London, this is her  fifth anniversary.
Here is Neema at the age of 7 years old reading newspapers at her parents’ house at Mbezi Beach in Dar-es-salaam, Tanzania.  Neema loved to read, and reading shaped her career choice. She studied her degree in Broadcasting in the United Kingdom; she wanted to be an Editor and a Travel writer.

At the age of 7 years old Neema already knew what she wanted to be; she worked very hard. She thrilled and excelled.  She nicknamed herself as ‘UNBROKEN DIVINE’, graduated with BA Honours in Broadcasting at the University of Falmouth in the United Kingdom.  
Neema was ready to contribute to the world.   “I worked in the International Office at Falmouth University.  I worked with Neema when she came to Falmouth University.  She was a wonderful person, who received one of very few scholarships as an outstanding student.  I also worked with her to set up the study abroad in Canada, where Neema again made a big impression.  I am sorry to hear of her passing and her loss to you, her family, and wider world of such a beautiful and talented person” (2011),   a quote from  Stuart Westhead  –  an  International Student Officer  at  Falmouth University  – in the  UNITED  KINGDOM. 
We ask that everyone reading this memorial to know that with our great joy Neema’s  legacy continues,  because Neema Memorial Foundation will do the job Neema wanted to do in her life.


We will love you Neema forever, and we will miss you Neema forever, but one day we will be together again, our almighty GOD bless you. 


.TASWIRA ZA MTANANGE WA AZAM FC NA MBEYA CITY FC, AZAM WASHINDA 3,0 UWANJA WA SOKOINE JIJINI MBEYA

$
0
0
   Hizi ni Taswira katika Mtanange wa Azam fc na Mbeya City fc wakoma kumwanya mara baada ya Azam fc kuibugiza Timu ya Mbeya City ikiwa ni muendeleo wa Ligi kuu Tanzania Bara wafungaji ni Kiplee Cheche Goli la kwanza, John Boko Adebayo Goli la Pili na Farid Mussa Goli la Tatu katika mchezo ulio chezwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. 
 Refa akiangalia tu wakati mchezaji wa Timu ya Azam Mwantika akijibizana na Mchezaji wa Timu ya Mbeya City Haruna Mosh Boban mara baada ya kufanyiana Madhambi katika Mchezo huo.
 Baadhi ya Mashabiki wa Mbeya City wakiwa Sanjari na Vikinga Mvua vyao mara baada ya Mvuwa kubwa kunyesha Uwanjani hapo.
Wawa katika Ubora wake..
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.

Toto Africans na Kagera Sugar ngoma droo CCM Kirumba Mwanza

$
0
0
TIMU za Toto Africans na Kagera Sugar jana zimetoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ambapo Toto Africans ilitangulia kufunga bao dakika ya 24 mfungaji akiwa Japhary Vedastus. 
Mfungaji alimalizia kazi nzuri ya Miraji Athumani kabla ya Kagera kusawazisha dakika ya 66 mfungaji akiwa Mbaraka Yusuph. Kikosi kilichoanza cha Timu ya Toto Africans cha Jijini Mwanza dhidi ya Kagera Sugar


Kikosi kilichoanza cha Kagera SugarTayari kipute kuanzishwa
Kocha wa Kagera Sugar Mohamed Richard Adolph akiwa kwenye wasiwasi baada ya Timu yake kuwa nyuma ya bao 1-0 katika kipindi cha kwanza bao lililofungwa dakika ya 24. Wachezaji wa Toto wakipongezana kwa bao. 




Mmiliki Wa Mjengwablog Akabidhi Misaada Ya Wana-Iringa Kwa Waathirika Wa Mafuriko

$
0
0
Mmiliki wa Mjengwablog.com na mwongozaji wa kipindi cha ' Nyumbani Na Diaspora' akikabidhi mbele ya Mwenyekiti wa kijiji cha Kisinga, Ndg. Shabani Mtimbwa na Mtendaji Kata ya Mlenge, Bi. Sarah Mbilinyi misaada iliyotolewa na Wana- iringa na watembeleaji wa mtandao wa Mjengwablog.com wakiwamo wafuatiliaji wa kipindi cha ' Nyumbani na Diaspora' kinachorushwa TBC1.
Misaada  iliyokabidhiwa ni pamoja na mahema 9 na magodoro mapya 20. Kuna mabegi mengi ya nguo na viatu vya watoto, wanawake, wanaume. Misaada ina thamani ya shilingi milioni tatu na nusu. Shukran za pekee kwa ndugu Ahmed Salim ' Asas' kwa kufanikisha lojistiki ya kufikisha Pawaga misaada hiyo.

Tanzania inawaogeleaji wenye vipaji wengi - Penny Heyns

$
0
0
Muogeleaji bora wa dunia wa zamani na bingwa wa kuogelea wa Olimpiki, Penelope “Penny” Heyns amevutiwa na waogeleaji vijana na kusema wakiendeleza kwa kupata mafunzo ya kisasa, Tanzania itatwaa medali nyingi katika mashindano ya kimataifa. 
Penny alisema hayo katika semina ya siku tatu iliyaondaliwa na klabu maarufu ya Dar Swim Club yaliyoafanyika katika hoteli ya Coral Beach, Masaki jijini Dar es salaam.
Alisema kuwa amefarijika kuona waogeleaji wengi chipukizi aliofanya nao semina kama hiyo mwaka jana kuwa na viwango vya juu na kumpa faraja kubwa kuwa siku moja watakuwa waogeleaji bora Afrika na dunia kwa ujumla. 
“Hii ni mara yangu ya pili kufanya semina na Dar Swim Club, nilifanya nao mwaka jana na waogeaji wamepata maendeleo makubwa, ni muhimu kuwaendeleza kwa kupata mafunzo kama haya,” “Nimeambiwa kuwa klabu imepata mafanikio makubwa hapa nchini kwa kushinda medali na kuwa wa kwanza katika mashindano ya Taliss, haya ni matunda ya mafunzo bora,” alisema Penny. 
Penny pia aliipongeza Dar Swim Club kwa kuwa na utaratibu mzuri wa mazoezi na mafunzo na anaamini wataendelea kufanya vyema katika mashindano mbalimbali ya ndani na kimataifa. Mmoja wa waogeaji chipukizi wa klabu hiyo, 
Reuben Monyo alisema kuwa wamepata mwanga mkubwa katika mafunzo hayo na anaona mwanga wa mafanikio katika fani hiyo. Monyo (10) alisema kuwa lengo lake ni kuona Tanzania inafanya vyema na yeye kuwa muogeaji nyota katika hapa nchini na mashindano makubwa kama Jumuiya ya Madola na Olimpiki. Kocha mkongwe wa mchezo huo hapa nchini, 
Ferick Kalengela alisema kuwa mafunzo ya Penny yamewapa mbinu mpya katika mchezo huo na wana uhakika wa kufanya vyema hapa nchini na katika mashindano ya kimataifa. “Tumepata mafunzo mazuri tena ya kisasa, lengo letu ni kuona tunafika mbali katika mchezo na hasa kupitia msemo wetu, 
“Tunataka kila Mtanzania ajue kuogelea”,alisema Kalengela. Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Inviolata Itatiro alisema kuwa Wameandaa mafunzo hayo kwa lengo la kuendeleza mchezo huo hapa nchini mbali na klabu yao. 
Inviolata alisema kuwa wanajua umuhimu wa mafunzo kama hayo na kusaka wadau kusaidia ili kufanikisha pamoja na changamoto mbalimbali walizokutana nazo. “Maendeleo ya Dar Swim Club ni maendeleo ya mchezo huo hapa nchini, tunaamini kuwa tukifanya vizuri sisi, sifa itakuwa kwa nchi nzima,” alisema.
 Wachezaji wa klabu ya Dar Swim Club wakijiandaa kuanza kuogelea kwa kufuata malekezo ya bingwa wa zamani wa Olimpiki na Muogeleaji bora wa kike, Penny Heyns (hayupo pichani) katika  mafunzo yaliyofanyika Masaki jijini.
 Bingwa wa zamani wa Olimpiki na Muogeleaji bora wa kike, Penny Heyns (watatu kutoka kulia) akitoa somo la jinsi ya kuogelea kwa spidi kwa makocha na waogeleaji wa Dar Swim Club katika mafunzo ya siku tatu yaliyofanyika Masaki.
 Makocha wa mchezo wa kuogelea wa klabu ya Dar Swim Club  wakiwa darasani kumsikiliza bingwa wa zamani wa Olimpiki na muogeleaji bora wa kike duniani, Penny Heyns  katika semina iliyofanyika kwenye hotel ya Coral Beach jijini.
 Bingwa wa zamani wa Olimpiki na Muogeleaji bora wa kike, Penny Heyns (kulia) akielekeza jambo kwa mmoja wa makocha wa klabu ya Dar Swim Club, Radhia Gereza katika mafunzo yaliyofanyika Masaki jijini.
Bingwa wa zamani wa Olimpiki na Muogeleaji bora wa kike, Penny Heyns (wa pili kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na makocha wa klabu ya Dar Swim Club mara baada ya mafunzo yaliyofanyika Masaki jijini.

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGA MKUTANO WA MWAKA WA MAAFISA WAANDAMIZI JESHI LA POLISI NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), akipokelewa na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Ilala, SACP Lucas Mkondya, alipofika kufunga kikao  kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia), akipeana mikono na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, mara baada ya Katibu Mkuu huyo kumaliza kutoa hotuba ya kufunga Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza wakati wa kufunga kikao  kazi cha Maafisa Maandamizi wa Jeshi la Polisi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Wapili kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, akizungumza na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini wakati wa kufungwa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa hao uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wanne kushoto waliokaa), Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu (kushoto kwa Katibu Mkuu) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, mara baada ya kufungwa Mkutano wao wa Mwaka uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

TEASER JOTO LA ASUBUHI JUMATATU FEBRUARY 22, 2016 KUANZIA SAA 12 HADI TATU ASUBUHI

Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images