Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110090 articles
Browse latest View live

TAARIFA KUTOKA DRFA

$
0
0
Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam hatua ya sita bora imeendelea leo kwa michezo mitatu, ambapo kwenye Uwanja wa Kinesi, Abajalo imeifunga Friends Rangers bao 1-0. 
Bao hilo limefungwa na Waziri Omary katika dakika ya 35. Abajalo sasa wamefikisha pointi 7 wakishika nafasi ya pili. Kwenye Uwanja wa Makurumla, Boom FC imetoka sare ya bao 1-1 na Read Coast. 
Bao la Red Coast limefungwa na Idrisa Pandu katika dakika ya 28 wakati lile la Boom limefungwa na Janka Ally katika dakika ya 41.Red Coast wanaendelea kuongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 8.
 Kwenye Uwanja wa Airwing, Sharif Stars imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Day Braek. Bao hilo limefungwa na Dovan Kanyinda katika dakika ya 89 na hivyo kufikisha pointi 6 katika michezo minne iliyocheza. 
 Kila timu hadi sasa imecheza michezo minne na ligi hiyo itafikia tamati Aprili 27 ili kupata timu tatu za juu zitakazocheza hatua ya Kanda. 

 Imetolewa na Mohamed Mharizo
 Ofisa Habari wa Chama cha Mpira wa Miguu 
Mkoa wa Dar es Salaan (DRFA)

mambo ya mzungu kichaa

$
0
0
Mzungu Kichaa aka Espen Sørensen is a Danish singer and musician. He was born in Denmark, but grew up in Tanzania, where his parents worked in the field of Development Cooperation. They went there when he was six years old. In Tanzania he learned to speak Swahili fluently and later on he got involved in music and particularly in the production of Bongo Flava at Bongo Records. The latest outcome of his interest in East African music is his first solo album "Tuko Pamoja".

Article 5

Ngoma Azipendazo Ankal

$
0
0


Ngoma ya 'Embakasi' ya Les Mangelepa lazima italiza wengi

INTRODUCING KUTOKA MAKTABA YA GLOBU YA JAMII

$
0
0
Kutokana na maombi ya wengi, Globu ya Jamii inatii amri ya wadau ya kuanzisha makala ya KUTOKA MAKTABA itayoenda sambamba na Ngoma Azipendazo Ankal kila siku. Kwa kuanzia hapa ni Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam mwaka 1990 wakati wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani walipojiunga na maelfu ya wananchi kumpokea Nelson Mandela alipotembelea Tanzania mara tu baada ya kuachiwa huru.

A Perfect Penumbral Eclipse on April 25

WAZIRI GHASIA ATAKA USIMAMIZI MAKINI KATIKA MASUALA YA MANUNUZI

$
0
0
. Habari na Picha na John Nditi, Morogoro WAZIRI wan chi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ( TAMISEMI) Hawa Ghasia, amezitaka Kamati za Fedha na Uongozi za Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji nchini kuhakikisha wanasimamia masuala ya manunuzi kwa uadilifu na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha kuwa fedha za umma zinawanufaisha walengwa. 
 Pia amezitaka Kamati hizo kuepuka kashfa zisizokuwa na sababu wakati wa manunuzi unapofanyika katika Halmashauri zao na kutaka wazingatie sheria , kanuni na utaratibu mzima katika hatua zote za suala hilo. Waziri Ghasia alisema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi mafunzo yaliyohusu mambo muhimu ya kuzingatia katika ununuzi kwa Wenyeviti wa Kamati za Fedha na Uongozi wa Halmashauri zote za Tanzania Bara. 
Wenyeviti hao na viongozi wa Kamati hizo walishiriki mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza Aprili 22 na kufukia tamati Aprili 24, mwaka huu mjini Morogoro ambayo yaliandaliwa na Uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Ununuzi wa Umma ( PPRA). 
 Alisema , lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha fedha zinazotumika ziweze kuleta manufaa zaidi kwa walengwa ambao ni wananchi ambao wanatarajia kupata huduma zilizo bora na kwa gharama nafuu. Waziri Ghasia alisema ,asilimia zaidi ya 70 ya bajeti ya kawaida na asilimia 100 ya bajeti ya maendeleo imekuwaikitumika katika kufanya manunuzi. 
 Kwa mujibu wa Waziri hiyo, takiwmu nyingine zinaonesha kuwa ununuzi unaweza kugharimu takriban asilimia 15 hadi 20 ya pato la taifa (GDP). 
 “ Hali hii, inaonesha ni jinsi gani Serikali yetu inavyotumia fedha nyingi katika sekta hii muhimu kwa ajili ya kuleta maendeleo yanayolenga ufanisi wa kiutendaji “alisema Waziri Ghasia na kuongeza. 
 “ Jambo hili litaleta tija katika uwajibikaji na kuleta hali bora ya maisha kwa raia wote tunaowatumikia” alisisitiza Waziri huyo. 
 Alisema , Serikali inatambua umuhimu wa Kamati hizo katika kutekeleza majukumu yaliyoainishwa kwa mujibu wa sheria , kanuni na taratibu zilizowekwa. Waziri Ghasia alisema, mafunzi hayo na maboresho ya mfumio wa ununuzi lengo kuu ni kupata thamani inayilingana na ubora pale fedha za umma zinapotumika kununu bidhaa , huduma au kandarasi za ujenzi. 
 “ Utafiti unaonesha kuwa endapo hizi Kamatyi zitapata mafunzo ya sheria ya Ununuzi kutaongeza ufanisi na tija katika uendeshaji wa Halmashauri zetu” alisema Waziri Ghasia. 
 Hivyo aliwataka Viongozi wa Kamati hizo kuhakikisha kuwa mafunzo waliyopata mara akirejea katika Halmashauri zao waashirikishe Madiwani ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo ili watambue wajibu wao wa kusimamia fedha za umma.
 Waziri wa Tamisemi, Mhe Hawa Ghasia akikaribishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo ( kushoto) akimwongoza Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia baada ya kufungua mafunzo. Wa pili kulia ni Nkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe Joel Bendera.
 Waziri wa Tamisemi,  Mhe Hawa Ghasia akiwahutubia wenyeviti na viongozi wa kamati za fedha na uongozi za Halmashauri za Wilaya nchini

Waziri wa Tamisemi, Mhe Hawa Ghasia ( mwenye ushungi ) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Morogoro na wenyekiti na viongozi wa Kamati za fedha na uongozi za Halmashauri zote nchini

SUZA establishes Doctor of Medicine Degree

$
0
0
 The State University of Zanzibar (SUZA) will start offering the Doctor of Medicine degree programme with effect from the forthcoming academic year commencing in October, 2013. 
 Prof. Idris A. Rai, the SUZA Vice Chancellor, accompanied by the Principal Secretary of the Ministry of Health and the Principal Secretary of the Ministry of Education and Vocational Training announced this during a recent stakeholders meeting held at Vuga Campus to work on Doctor of Medicine (MD) curriculum for SUZA. 
This five year programme plus one for internship in reputable hospitals will start with between 20 and 30 students at its initial batch. The classes will be run by a team of newly employed medical staff at SUZA and with the help of Medical Professors from Cuba who are already in Zanzibar teaching at Zanzibar Medical School (ZMS). This initiative will however, bring no negative academic upshot to ZMS.

Medical Science stakeholders meeting discussing the 
establishment of Doctor of Medicine programme at SUZA

Regarding infrastructure and facilities required for the course, the Vice Chancellor informed that so far SUZA has adequate reference books in its libraries for the programme especially those of Biology and the budget for purchasing suitable resources including health science books is allocated. For clinical and practical work, the students will use the facilities at Mnazimmoja Hospital, which will also cater for teaching hospital. In addition, the programme emphases community based training whereby students will be exposed to medical cases facing the community starting their first year of studies.

The introduction of this programme is to large extent expected to minimize the scarcity of skilled health personnel in the isles. This new initiative is among the implementing measures of the State University of Zanzibar to the directive of Dr. Ali Mohamed Shein, the President of Zanzibar who is also the Chancellor of the University who urged SUZA to think of offering other useful disciplines beneficial to Zanzibar, Prof. Rai declared.

 

In diversifying its programmes, the State University of Zanzibar has introduced a few new programmes to begin 2013/2014 academic year. These include, two postgraduate, four undergraduate and two non-degree programmes at diploma and certificate level.

 

 
Source: Public Relations Unit 
of the State University of Zanzibar


THE UN SECRETARY-GENERAL MESSAGE ON WORLD MALARIA DAY

$
0
0
Since world leaders adopted the Millennium Development Goals in 2000, a broad partnership of governments, United Nations entities, philanthropies and businesses has combined to protect hundreds of millions of people from malaria. Increased international funding, matched by growing political commitment in endemic countries, triggered a massive increase in preventive interventions and expanded access to diagnostic testing and life-saving medicines, averting more than a million deaths.

The MDG target of halting and reversing the incidence of malaria is now in sight, and 50 countries are on track to reduce their malaria burden by at least 75 per cent by 2015. However, major challenges remain. Malaria continues to inflict a major toll on least developed countries – primarily in Africa – and millions of people still lack access to life-saving interventions.

In Africa, malaria kills a child every minute. Weak surveillance systems mean that cases are vastly under-reported; and governments and the World Health Organisation have too little information about where malaria occurs and how trends are changing, although improvements in data collection are under under way. Emerging resistance of the malaria parasite to drugs, and mosquitos to insecticides, are further complicating efforts to combat this persistent threat to lives and productivity.

Recently, global funding for malaria control has plateaued. Although half the resources needed to achieve near-zero deaths from malaria by the 2015 MDG deadline have been committed, there is still a near-$3 billion annual shortfall. This is starting to slow the scale-up of key malaria interventions in Africa, particularly the distribution of long-lasting insecticide treated mosquito nets.

To prevent malaria from resurging, and to continue to alleviate suffering, especially in the 10 countries with the highest malaria burden, the international community needs to provide the necessary funding to protect all at-risk groups and support research and innovation to develop new tools. Replenishment of the Global Fund to Fight AIDS, Tuberculosis and Malaria should be a priority. .

The theme for this year’s global World Malaria Day campaign is “Invest in the future. Defeat malaria”. Controlling malaria does more than improve human health. It boosts social well-being and economic development. I urge the global health community, including political leaders in endemic countries, to maintain their commitment to provide universal access to malaria interventions and end needless suffering from this preventable and treatable disease.

RUVU SHOOTING, SIMBA SASA KUKIPIGA MEI 5

$
0
0

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyokuwa ichezwe leo (Aprili 25 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sasa itafanyika Mei 5 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.

Mabadiliko hayo yametokana na Serikali kuutumia uwanja kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Muungano ambazo kitaifa zitafanyika kesho (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi washabiki kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo na ghafla. Ratiba ya mechi nyingine za VPL zinabaki kama zilivyo.

Ligi hiyo inaendelea kesho (Aprili 26 mwaka huu) kwa mechi kati ya Coastal Union na Azam itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Jumapili (Aprili 28 mwaka huu) itakuwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Simba dhidi ya Polisi Morogoro.

Rais Kikwete aongoza harambee ya maendeleo jimbo la Ukonga.Achangia 110m/

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza harambee ya kuchangia mfuko wa maendeleo jimbo la Ukonga jana jioni ambapo jumla ya Shilingi 462m/ zilipatikana ikiwa ni ahadi na fedha taslimu. Rais Kikwete alichangia jumla ya shilingi 110m/-Wakati wa harambee hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana jioni.Kulia ni mbunge wa ukonga Eugen Mwaiposa na wapili kushoto ni mwenyekiti wa ukonga SACCOS Advera Ruge (picha na Freddy Maro).

KUMBUKUMBU

$
0
0
MAREHEMU STANLEY THOMAS MBUYA 
MPENDWA WETU STANLEY LEO UMETIMIZA LEO MWAKA MMOJA TANGU ULIOITWA NA MUUMBA WAKO KUTOKA DUNIA HII. MIOYO YETU BADO IMEJAA SIMANZI NA MAJONZI MAKUU KWA KUONDOKEWA NAWE.

ULIKUWA NGUZO IMARA KATIKA FAMILIA NA TUNAKOSA HEKIMA,USHAURI NA BUSRA PIA UONGOZI WAKO KWETU SISI.

DAIMA TUNAIOMBEA ROHO YAKO IPATE PUMZIKO LA AMANI TUKIWA NA MATUMAINI KWAMBA TUTAKUTANA TENA KATIKA UTUKUFU WA MUNGU MBINGUNI.UTAENDELEA KUKUMBUKWA NA MKEO NA WATOTO, BABA, DADA, KAKA, SHEMEJI, WAKWE, WAJOMBA, SHANGAZI, WANAWAWAMA, WANATOSA, WANA KVD, NA WANAJUMUIA WENZIO, MARAFIKI WA MAFIA, UKOO WOTE WA MBUYA, NDUGU NA MARAFIKI WOTE.

KUTAKUWA NA IBADA YA KUMWOMBEA MAREHEMU TAREHE 26 APRIL HUKO KILEMA KIMARORONI KUANZAIA SAA 6 MCHANA.

RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWAANGAZIE.APUMZIKE KWA AMANI!

AMINA.

KINANA AKUTANA NA BALOZI WA UBELGIJI LEO

$
0
0
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akizungumza na Balozi wa Ubelgiji hapa nchini, Koen Adam, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, jijini Dar es Salaam, leo, Aprili 25, 2013. Wapoli kulia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. (Picha na Bashir Nkoromo).

RAIS KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WA BANGLADESH, SLOVAK, UGIRIKI NA KUWAIT LEO

$
0
0
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bw John haule  kwa Balozi wa Bangladesh nchini Mhe Wahidur Rahman baada ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa  kwa Balozi wa Kuwait  nchini Mhe Yacoub Y. Alsanad na Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage  kabla ya ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na  Balozi wa Kuwait  nchini Mhe Yacoub Y. Alsanad kabla ya ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam. Kushoto ni Bw Abdul Rahman Al-Hashim, Meneja wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait aliyeongozana na balozi huyo.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho toka kwa balozi wa Slovak Mhe Michal Mlynar   leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Balozi wa Ugiriki nchini Mhe Elefthereios Kouvaritakis baada ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam
PICHA NA IKULU.

Mshindi wa Mahela atoa rai kwa Watanzania

$
0
0
Rai imetolewa kwa Watanzania kuwa na matumizi sahihi ya fedha wanazopata kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mashindano ya michezo ya kubahatisha ili kuweza kujiletea maendeleo na kuondoka katika wingu la umasikini, Rai hiyo imetolewa na mmoja ya washindi wa promosheni ya Vodacom MAHELA Bi. Catherine Gumbo mkazi wa Pugu Kajiungeni - Jijini Dar es Salaam inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania. 
Akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea nyumbani kwake Pugu Bi. Catherine amesema kuwa ushindi wa shilingi milioni tano kwake umekuja muda muafaka huku wakati akiwa amekwama kuendelea na shughuli za ujenzi kwa miaka kadhaa. Bi Catherine ametanabaisha kuwa ni vyema sasa watanzania wakawa na mipango na matumizi sahihi ya fedha wanazoshinda kwani ni fedha ambazo zinakuja wakati mtu hajategemea.
 "Ushindi wa milioni tano kwangu umekuwa ni faida kubwa, hadi sasa nimefanikiwa kumalizia sehemu kubwa ya ujenzi wa nyumba yangu ambao ulikwama kwa muda mrefu, nimenunua madirisha ya aluminium (9)na nyavu zake ambazo zimegharimu kiasi cha shilingi milioni 2 kama mnavyoona, nikanunua vigae vya ndani na kutengeneza mfumo wa maji ndani ya nyumba na niko katika hatua za mwisho kuvuta umeme kama ambavyo mmeshuhudia mpembuzi kutoka Tanesco akiwa hapa, alifafanua Bi. Catherine na kuongeza kuwa, " Ni vyema sasa Watanzania tukawa na matumizi sahihi ya fedha ambazo wanashinda kutokana na Promosheni hizi zinazoendeshwa na makampuni mbalimbali hapa nchini,kwani ni fedha ambazo zinakuja wakati mtu hujatarajia, Pia ni vyema hata kampuni ambazo zinaendesha promosheni hizi kuweka mipango maalum ya elimu kwa wateja au hata mafunzo ya ujasiliamali au kilimo kwa washindi wanaokuwa wanapatikana ili fedha hizo ziwe na manufaa kwa watanzania, alihitimisha Bi Catherine. 
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Bw. Matina Nkurlu, amesema kuwa hakika watu aina ya mama Catherine ni mfano wa kuigwa miongoni mwa watanzania kutokana na mafanikio ambayo ameyapata hadi sasa. 
"Vodacom tunajivunia sana mafanikio ya mama Catherine, kwa maendeleo ambayo ameyafanya kwa kiasi kidogo alichokipata ni dhahiri kuwa promosheni hii imekuwa na mafanikio na kubadili maisha ya Watanzania," alisema Nkurlu.
 Hadi sasa washindi zaidi ya 332 wamepatikana huku 26 wakijinyakulia milioni 5 na wengine 249 wakijinyakulia milioni 1 kila mmoja na kufikisha Shilingi Milioni 380 zilizotolewa hadi sasa huku milioni 100 zikiwa zimesalia kufikia tamati ya promosheni hiyo tarehe 29 ya Mwezi huu ambapo mshindi wa jumla ataibuka na fedha taslimu shilingi milioni 100.
 Bi Catherine Gumbo (49 ) Mkazi wa Pugu - kajiungeni Dar es Salaam, akimuonyesha Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw. Matina Nkurlu Sehemu ya nyumba ambayo anaendelea kuijenga kutokana na  fedha za Ushindi alizopata kupitia promosheni ya Mahela inayoendeshwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania. Vodacom ilimtembelea Cathrine nyumbani kwake jijini dar es salaam kuona jinsi fedha za ushindi zilivyosaidia kuboresha maisha yake.

Mama Mzazi wa Mshindi wa promosheni ya Mahela, Bi.Grace Gumbo akimuonyesha Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni ya Vodacom Bw.Matina Nkurlu, Jumla ya pointi alizojikusanyia hadi sasa kutokana na ushiriki wake katika promosheni hiyo inayoendelea kwa wateja wa Vodacom nchi nzima. Kushoto ni Catherine Gumbo aliyejishindia Sh 5 Milioni, Vodacom ilimtembelea Cathrine nyumbani kwake jijini dar es salaam kuona jinni fedha za ushindi zilivyosaidia kuboresha maisha yake.

Balozi Kamala Akutana na Wanafunzi kutoka Tanzania wanaosoma katika Taasisi ya Elimu ya Maji ya UNESCO

$
0
0
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye miwani) akiwa na Wanafunzi kutoka Tanzania wanaosoma masuala ya Maji katika Taasisi ya Elimu ya Maji ya Kimataifa (UNESCO), Delft Uholanzi. Watanzania kumi na Sita kutoka Tanzania wamehitimu katika fani za usambazaji wa maji, maji na mazingira, usimamizi wa raslimali za maji na utatuzi wa migogoro ya maji.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akutana kwa mazungumzo na Rais wa Comoro

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (kulia), akisalimiana na Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Ikililou Dhoinine mara baada ya kuwasili kwenye Ikulu ya nchi hiyo. Mhe. Maalim alitembelea Comoro hivi karibuni kwa madhumuni ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
Mhe. Maalim akizungumza na Mhe. Rais Dhoinine.
Mhe. Maalim (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Rais Dhoinine (katikati) mara baada ya mazungumzo yao.

mkataba wa ununuzi wa kivuko cha Dar-Bagamoyo watiwa saini leo

$
0
0

Waziri wa Ujenzi  Dr. John Pombe Magufuli (watatu kulia) na Balozi wa Denmark Tanzania  wakishuhudia utiaji saini mkataba wa ununuzi wa kivuko cha Dar Bagamoyo leo. Kivuko hicho kitajengwa na kampuni ya johs Gram-Hanssen A/S ya Denmark. Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 300 kwa pamoja na kinatarajiwa kukamilika miezi minane kutokea leo.

waliongia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 watangazwa.

$
0
0

Photo: Majina ya wasanii, waandaaji muziki na vikundi kwa ajili ya tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013   WIMBO BORA WA MWAKA    Dear God - Kala Jeremiah  Leka dutigite - Kigoma all star  Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe  Me n U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee  Pete- Ben pol   MSANII BORA WA KIUME   Ben Pol   Diamond   Linex   Mzee Yusuf   Ommy Dimpoz    MSANII BORA WA KIKE   Isha Mashauzi   Khadija Kopa   Lady Jaydee   Mwasiti   Recho        MSANII BORA WA KIKE - TAARAB   Isha Mashauzi   Khadija Kopa   Khadija Yusuph   Leila Rashid  MSANII BORA WA KIUME - TAARAB Ahmed Mgeni   Hashim Said   Mzee Yusuf    MSANII BORA WA KIUME - BONGO FLAVA     Ally Kiba   Ben Pol   Diamond   Linex   Ommy Dimpoz    MSANII BORA WA KIKE - BONGO FLAVA  Linah   Mwasiti   Recho   Shaa       MSANII BORA WA HIP HOP     Fid Q  Joh Makini Kala Jeremiah Profesa J Stamina  9. Msanii Bora wa Kiume - Bendi   Chalz Baba    Dogo Rama    Greyson Semsekwa    Jose Mara    Khaleed Chokoraa     Msanii Bora wa Kike - Bendi    Anneth Kushaba    Luiza Mbutu    Mary Lucos    Vumilia     Msanii Bora anayechipukia    Ali Nipishe    Angel    Bonge la Nyau    Mirror    Vanessa Mdee     Video Bora ya Wimbo ya Mwaka    Baadae - Ommy Dimpoz  Kamili gado - Professor J Feat Marco Chali  Marry Me - Rich Mavoko  Nichum - Bob Junior  Party Zone  - AY Feat Marco Chali  Mtunzi Bora wa Mashahiri - Taarab  Ahmed Mgeni   Hemed Omary   Khadija Kopa   Mzee Yusuf   Thabit Abdul    Mtunzi Bora wa Mashahiri - Bongo Flava  Ally Kiba   Barnaba   Ben Pol   Linex   Ommy Dimpoz    Mtunzi Bora wa Mashahiri - Hip Hop  Fid Q   Joh Makini   Kala Jeremiah   Mwana Fa   Stamina    Mtunzi Bora wa  Mashahiri - Bendi  Chalz Baba   Grayson Semsekwa   Jonico Flower   Jose Mara   Khaleed Chokoraa   Mtayarishaji Bora wa Mwaka - Muziki wa Kizazi Kipya  Bob Junior  Ima the boy  Man Water  Maneke  Marco chali  Mensen Selecta  Mtayarishaji wa Wimbo wa Mwaka - Taarab  Bakunde  Enrico   Mtayarishaji wa Wimbo wa Mwaka - Bendi  Allan Mapigo Amoroso  Mtayarishaji Chipukizi wa Mwaka  Imma the Boy Mensen Selecta Mr T Touch Sheddy Clever  Rappa Bora wa Bendi    Fagasoni    Greyson Semsekwa    J4    Jonico Flower    Sauti ya Radi         Wimbo wenye vionjo vya asili    Aambiwe - offside trick  Atatamani - AT  Boma la utete - Young D  Chocheeni kuni - Mrisho Mpoto Feat Ditto  Mdundiko - Momba Feat Juma Nature   Wimbo Bora wa Bendi    Chanzo ni sisi - Mapacha watatu  Jinamizi la Talaka - Mlimani Park Orchestra  Risasi kidole - Mashujaa band  Shamba la twanga - African Stars band       Wimbo Bora wa Reggae    Hii si ya waoga - Yuzzo  Kilimanjaro - Warriors from The East  NATAFUTA PARADISE  - Mac Malick Simba  Salvation - Delayla Princess  Tunda - Hardmad   Wimbo Bora wa Africa Mashariki   Fresh All Day - Camp Mulla  Make you dance - Keko Feat Madtrax  Maswali ya polisi - DNA  Still a Liar - Wahu  Valu Valu - Jose Chameleone   Wimbo Bora wa - Bongo Pop   Aifola - Linex Feat fundi Samweli  Baadae - Ommy Dimpoz Feat Angel  Chuki Bure - Sharo  Milionea Feat Dully Sykes  Marry Me - Rich Mavoko  Me and you - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee    Wimbo Bora wa Kushirikiana/kushirikishwa  Chuki Bure - Sharo Millionea Feat Dully Sykes  Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe  Me and U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee  Sihitaji marafiki - Fid Q Feat Yvonne  Single Boy - Alikiba Feat Lady Jaydee     Wimbo Bora wa Hip Hop    Alisema - Stamina Feat Jux  Bum kubam - Nikki wa Pili Feat G Nako  Dear God - Kala Jeremiah  Nasema Nao - Nay wa Mitego  Sihitaji Marafiki - FID Q Feat Yvonne  Wimbo Bora wa RnB  Amerudi - Belle 9 Kuwa na Subira - Rama Dee Feat Mapacha Maneno maneno  - Ben Pol Pete - Ben Pol   Wimbo Bora wa Ragga/ Dancehall   Je ni nani - Ras Six Muda upite - Susu Man Predator - Dabo Push Dem - Dr Jahson Take it down - Chibwa and Tanah  Wimbo Bora wa Taarab  Mjini chuo kikuu - Khadija Kopa Mpenzi chocolate - Jahazi [Mzee Yusuph] Si bure una mapungufu - Isha Mashauzi [Mashauzi Classic] Sina muda huo - Jahazi [Leila Rashid] Siwasujudii Viwavi jeshi -Isha Mashauzi [Mashauzi Classic]   Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba   Gubegube -Barnaba Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe Nashukuru umerudi - Recho Ni wewe - Amini Sorry  - Barnaba  Bendi Bora ya Mwaka CD1 African Stars Band  Mapacha wa tatu  Mashujaa Band Mlimani Park Orchestra [Sikinde]  Msondo Ngoma Music band  Kikundi Bora cha Taarab  Dar modern Taarab   Five stars modern Taarab   Jahazi Modern Taarab   Kings modern Taarab   Mashauzi Classic        Kikundi Bora cha Muziki wa Kizazi Kipya   Jambo squad Makomando Tip Top Connection Tmk wanaume family Weusi 
Mratibu wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 kutoka BASATA Bw. Luhala akitangaza majina ya walioteuliwa kuingia kwenye mchakato wa tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika Juni 8,  2013 pale Mlimani City jijini Dar.
 Meneja kilaji cha  Kilimanjaro Premium lager, Bw. George Kavishe akifafanua jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo jijini dar kuhusiana na mchakato mzima wa tuzo hizo za  Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013.
BOFYA HAPA kuona walioingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hizo.

MWANANYAMALA HOSPITAL RECEIVES ASSISTANCE FROM AAR ON WORLD MALARIA DAY

$
0
0
AAR Tanzania Company Limited today has provided 92 mosquito nets and 42 Bed sheets worth 1.3 Million to Pediatric and Maternity block in Mwananyamala Hospital Dar-es-salaam as the way of showing support to the Society on World Malaria Day.

Speaking during the handling of the assistance, the AAR Insurance Marketing Manager, Tabia Massudi said “The Company is being operated with ethics and integrity. Being responsible to the community is one of the ethical activities that AAR Company would want to embrace. That is why AAR Insurance and Health Centers have collaborated and seen the need to provide this kind of assistance on this particular day”.

Malaria is one of the Major Challenges in the country and as one of the Major contributors in health services in Tanzania, it is our responsibility to show concern to infants and mothers who are mostly affected by the disease concluded Mrs. Massudi.

The assistance went along with the AAR Team, visiting Pediatric and Maternity Block in Mwananyamala hospital.

“We appreciate the concern AAR Company has shown today as the assistance has come at the right time when we are still facing a lot of challenges, one of them being insufficient equipments , I would like to urge other companies, organizations and the government as well to continue support Mwanayamala hospital as we depend on them for sustainability of our operations”. Said the Acting Chief Doctor, Kariamel John Wandi when receiving the assistance.
AAR Health Care Managing Director,Dr.Kandie Ng'ochoch handling bedsheets to the Mwanananyamala Acting Chief Doctor Kariamel John Wandi.
AAR Insurance Marketing Manager Tabia Massudi expressing to the press why AAR has decided to Provide the assistance to Mwanananyamala hospital Acting.
AAR Insurance Marketing Manager Tabia Massudi handling the assistance to the Mwanananyamala Acting Chief Doctor Kariamel John Wandi.
AAR Team having a group photo with Mwanananyamala Acting Chief Doctor Kariamel John Wandi during the provision of assitance on World Malaria Day.
AAR Insurance Marketing Manager Tabia Massudi on her right is AAR Health Care Managing Director Dr.Kandie Ng'ochoch showing support to the patients when visiting Mwanayamala Hospital on World Malaria Day.
Viewing all 110090 articles
Browse latest View live




Latest Images