Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1127 | 1128 | (Page 1129) | 1130 | 1131 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea Song Geum Young alipomtembelea Ofisini kwake mtaa Luthuli, Jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba akiongea na Balozi wa Korea Nchini Bwana Song Geun Young alimpomtembelea Waziri huyo Ofisini kwake leo, Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira Richard Muyungi.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba akizungumza na Balozi wa Korea Nchini Song Geum - young alimpomtembelea Ofisini kwake kujitambulisha wa kwanza kulia ni Msaidizi wa Balozi Songwon Shin.

  0 0

  KAMATI ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka imewatangaza waimbaji wengine watakaopanda jukwaa la tamasha hilo linalotarajia kufanyika mikoa ya Geita, Mwanza na Wilaya ya Kahama ikiwa ni muendelezo  wa maandalizi ya kuelekea sikukuu hiyo.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama wameongeza idadi ya waimbaji katika tamasha hilo ambao ni Christopher Mwahangila na Joshua Mlelwa.

  Msama alisema wamepanga tamasha hilo litakaloanza Machi 26 mkoani Geita kwenye ukumbi wa Desire huku Machi 27 litafanyika jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba na Machi 28 litamalizia Uwanja wa Taifa ulioko Wilayani Kahama.

  Msama alitumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha malengo ya tamasha hilo ambayo ni pamoja na kusaidia wenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu  na wajane.
  Aidha Msama alisema mwaka huu kamati yake imejipanga kugawa baiskeli zaidi ya 100 kwa walemavu ikiwa ni sehemu ya tamasha hilo.

  "Tamasha la Pasaka linawajali wenye uhitaji maalum kama walemavu, yatima na wajane ambao wanapata misaada kupitia mapato ya mlangoni kupitia viingilio," alisema Msama.

  Msama aliwataja waimbaji wengine waliothibitisha kushiriki tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Faustine Munishi, Anastazia Mukabwa na Jennifer Mgendi.

  0 0
 • 02/17/16--01:43: BEI YA MADAFU HII LEO.

 • 0 0

  The host of the workshop, Executive Director of ESRF, Dr. Tausi Kida, presents a paper; The Tanzania human development report experience. The session highlighted the Tanzania report experience in producing the Tanzania human development report 2014/2017.
  UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative in Tanzania, Mr.Alvaro Rodriguez, delivers his speech when opening a four-day regional workshop on making an impact with human development reporting at Ramada Resort in Dar es Salaam, February 16, 2016.

  Executive Director of Economic and Social Research Foundation, ESRF, Dr.Tausi Kida congratulates the UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative in Tanzania, Mr.Alvaro Rodriguez, after he had delivered his opening remarks.


  0 0

  Today, the German Ambassador to Tanzania handed over an aircraft to the Tanzanian Minister of Natural Resources and Tourism. The Husky aircraft will be deployed by Frankfurt Zoological Society (FZS) for surveillance of the Serengeti National Park to support TANAPA’s fight against poaching.

  „We are seeing the large mammals of our protected areas under a severe threat of local extinction because of poaching,“ said Minister Jumanne Maghembe on the occasion of the handover in Seronera. He thanked the German government for the support in countering the recent upsurge in poaching.

  “Stringent law enforcement, community involvement and ecosystem management are key in the fight against poaching”, said the German Ambassador Egon Kochanke. “I am very proud to be able to hand this aircraft over to the Tanzanian authorities and FZS. This is an important cornerstone of our close and longstanding cooperation.”

  Frankfurt Zoological Society will operate the aircraft in close cooperation with the Serengeti National Park Authority. With aerial support, poacher camps and illegal activities can be detected and the pilots can provide critical information to reaction forces on the ground.

  Tanzanian wildlife authorities are faced with a dramatic upsurge of poaching threatening the country’s populations of elephants and rhinos. To counter this threat and to support wildlife and habitat monitoring, the German Government through the German Federal Ministry for Economic Cooperation and Development (BMZ) has provided funding for the acquisition of three aircraft.

  The other two Husky A-1C Aircraft will be deployed in the Tanzanian Selous Game Reserve and the Zambian North Luangwa National Park. The Husky is well suited for monitoring and anti-poaching surveys as it operates at low heights and slow speeds.

  This support is part of longer-term financial and technical development cooperation measures implemented by FZS, GIZ, KfW, in collaboration with Tanzania Wildlife Authority TAWA, Tanzania National Parks TANAPA, and the Zambian Department of National Parks and Wildlife DNPW.
  Minister for Natural Resources and Tourism Prof. Jumanne Maghembe (right) receive Germany Ambassador in Tanzania Egon Kochanke during the handing over event of the Husky Surveillance aircraft to Serengeti National Park over the weekend.
  The Husky surveillance aircraft donated by Germany to Serengeti National Park to enhance patrol activities.
  Minister for Natural Resources and Tourism Prof. Jumanne Maghembe greet Serengeti National Park Tourism Warden Godson Kimaro during the handing over event.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan, akizungumza na Uongozi wa shirikisho la michezo la mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi (SHIMMUTA) ulioongozwa na Mwenyekiti wa shirikisho hilo Khamis Mkanachi, wakati ujumbe huo ulipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Februari 17, 2016.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika Picha ya pamoja na uongozi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma Taasisi na Makampuni Binafsi wakati ujumbe huo ulipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Februari 17, 2016.
   (Picha na OMR)

  0 0


  0 0

  Kamishina wa Elimu,Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa akizungumza na waandishi habari (Hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko akizungumza na waandishi habari (Hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishina wa Elimu,Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa.

  Baadhi ya Waandishi habari wakimsikiliza Kamishina wa Elimu,Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam 

  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya Jamii).

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. 
  KAMISHINA wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa amemuagiza Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko kuwavua madaraka Wakufunzi Wakazi Watatu (3), wa Elimu ya Watu Wazima kutokana na kukiuka utaratibu wa kuchagua wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza kuwaingiza katika Mfumo wa Elimu ya Watu Wazima. 

  Profesa Eustella ameyasema hayo leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , amesema kuwa wakufunzi hao wamedanganya kutokana na kuingiza huo utaratibu wa kuwapata wanafunzi wa elimu ya watu wazima. 

  Amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakishirikiana na Halmashauri baada ya kuchagua wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wamefanya vizuri wao kuchukua wanafunzi waliofeli na kuwapeleka katika shule za serikali wakadai kuwa wanafunzi wamechaguliwa katika chaguo la pili. 

  Amesema wazazi wamekuwa wanachanganywa na mkanganyiko huo baada ya kuchaguliwa wanafunzi hao wakifika shule wanadaiwa ada wakati serikali imesema bure. 

  Wakufunzi waliopata na kadhia hiyo ni Wotugu Mganda (Dar es Salaam), Senorina Kateule (Dodoma),Steward Ndandu Geita na (Mwanza). 

  Profesa Eustella amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakidandia matokeo ya kidato cha kwanza kwa kufanya upotoshaji kwa wazazi wakati wanafunzi wanaosoma katika elimu ya watu wazima ni hiari kutokana sera ya elimu. 

  Wanafunzi ambao wamechaguliwa kwa mwaka huu wamekuwa wakidai ada ya sh. 80,000 hadi 250,000 na ndipo malalamiko yakaanza kwa wazazi baada ya kudaiwa ada hiyo. 

  Profesa Eustella, amesema kuwa mmoja wanafunzi katika Mkoa wa Dar es Salaam aliambiwa amefaulu katika chaguo la pili katika shule ya sekondari ya Oasterbay na baada ya kufika wanafunzi wanakuta mambo tofauti kwa kudaiwa ada na kuambiwa awasiliane na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. 

  Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko amesema kuwa watu hao wakivuliwa madaraka wanakuwa walimu wa kawaida wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na kukaimisha nafasi zao.

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimfafanulia jambo Mwekezaji kutoka Bara la Ulaya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje wa Kampuni ya Vifaa vya Zimamoto nchini Ubeligiji, Jan Schampheleer (kulia) na Rais wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Ulaya, Dk. Erick Gohl (wapili kulia), wakati wawekezaji hao walipomtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya uwekezaji nchini mahususi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Ujio wa wawekezaji hao umeratibiwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Daraja la Umoja kati ya Bara la Ulaya na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)-(ESSB). Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa ESSB, Dk. Alawi Swabury, na wapili kushoto ni Mwakilishi wa TPSF ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Uraghibishaji wa Taasisi hiyo, Edward Furaha. 
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimsikiliza Mwekezaji kutoka Bara la Ulaya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje wa Kampuni ya Vifaa vya Zimamoto nchini Ubeligiji, Jan Schampheleer (kulia) wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi wa majukumu mbalimbali wanayoyafanya katika kampuni yake. Kulia kwake ni Rais wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Ulaya, Dk. Erick Gohl. Wawekezaji hao walipomtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya uwekezaji nchini mahususi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Ujio wa wawekezaji hao umeratibiwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Daraja la Umoja kati ya Bara la Ulaya na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)-(ESSB). Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa ESSB, Dk. Alawi Swabury. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji kutoka Bara la Ulaya, ambao ni Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje wa Kampuni ya Vifaa vya Zimamoto nchini Ubeligiji, Jan Schampheleer (kulia), Rais wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Ulaya, Dk. Erick Gohl (wapili kulia), Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Daraja la Umoja kati ya Bara la Ulaya na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc)-(ESSB), Dk. Alawi Swabury, na wapili kushoto ni Mwakilishi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Uraghibishaji wa Taasisi hiyo, Edward Furaha. Wawekezaji hao walikutana katika ofisi ya Waziri Kitwanga, jijini Dar es Salaam leo.
   Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Picha kwa hisani ya maktaba

  Na Woinde Shizza,Arusha
  Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkurlu amesimamisha shughuli za uchimbaji katika machimbo ya moramu katika kata ya Moshono Mkoani Arusha kwa kipindi cha mwezi mmoja kupisha wakandarasi kuweka sawa machimbo hayo ambayo yanachimbwa bila kufuata utaalamu hali ambayo inadaiwa inaweza kuhatarisha uhai wa maisha yao.

  Katika kipindi cha mwaka 2013 machimbo hayo yaliuwa wachimbaji 13 hali ambayo ilimfanya waziri mkuu mstaafu Peter Pinda kuyafunga mpaka yatakaporekebishwa ndiyo wachimbaji hao waendelee na uchimbaji ingawa inadaiwa wachimbaji hao hawakufuata maagizo mpaka hivi sasa kwani waliendelea na shughuli za uchimbaji.

  Akizungumza wakati akifunga machimbo hayo mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhil Nkurlu alisema kuwa mazingira ya wachimbaji hao ni mabaya na yanahatarisha maisha yao kwa kiasi kikubwa na kwamba hawana utaalamu wa kutosha juu ya namna bora ya uchimbaji wa moramu hiyo mbali na kuchimba kinyemela toka kauli ya waziri mkuu kutamkwa.

  Alisema kuwa ameamua kufunga machimbo hayo kutokana na oanagezeko kubwa la vifo linalosabibishwa na uchimbaji wa moramu usiozingatia sheria na kanuni .

  Naye kamishina msaidizi wa madini kanda ya kaskazini Elias Kadabila alichukuwa fursa hiyo kuwaomba wananchi kufuata maelezo ya mkuu wa wilaya ili waweze kuchimba kuchimba kwa usala ambapo alisema kuwa pia iatawasaidia kuepukana na maafa au vifo vinavyotokana na uchimbaji holela.

  Aidha pia aliuomba uongozi wa mtaa pamoja na wachimbaji hao kutoa ushirikiano ili kuweza kuwapisha wakandarasi kutengeneza machimbo hayo kwa muda wa mwezi mmoja .

  Gazeti hili pia liliweza kuzungumza na baadhi ya wachimbaji hao ambapo walisema kuwa hawakubaliani na agizo hilo la mkuu huyo kwakuwa uchimbaji huo ndiyo ambao unawafanya kumudu gharama za maisha na kusomesha watoto na kwamba serikali iangalie namna nyingine.

  "kwakweli tunaomba serekali iangalie tena na tena swala hili kwani sisi wananachi ndio tunategemea maachimbo haya kwani ndio yanatusaidia tunaweza kula ,kusomesha watoto ,kujenga naweza sema kiujumla kuendesha maisha yetu"Alisema Lowayani Metili

  Ipo haja ya wachimbaji hao kupisha marekebisho hayo yatakayofanywa na serikali kwa manufaa yao na uhai wao kwani kuendelea kuchimba wakati wanahatarisha maisha yao ni jambo la hatari Zaidi kwani wahenga wanamsemo usemao UHAI NI BORA KULIKO KIFO.

  0 0

  KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi ya Ligi (Kamati ya Saa 72) imekutana jana (Februari 16, 2016) kupitia taarifa za mechi mbili za Kundi C la Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya JKT Kanembwa na Geita Gold SC, na Polisi Tabora na JKT Oljoro ambapo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilisimamisha matokeo yake hadi taarifa hizo zitakapopitiwa.

  JKT Kanembwa ilifungwa mabao 8-0 na Geita Gold SC katika mechi iliyofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, wakati Polisi Tabora ilishinda mabao 7-0 dhidi ya JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

  Baada ya kupitia taarifa hizo na vielelezo vingine, Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imeonyesha mashaka kutokana na kuwepo viashiria vya upangaji wa matokeo (match fixing).

  Kwa vile suala hilo linahusisha masuala ya kinidhamu, na kwa kuzingatia Ibara ya 50(1) na (11) ya Katiba ya TFF na Ibara ya 69 ya Kanuni za Nidhamu za TFF, Kamati ya Saa 72 imemuelekeza Katibu Mkuu wa TFF apeleke suala kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa ajili ya uchunguzi na hatimaye kufanya uamuzi.


  0 0


  0 0
 • 02/17/16--05:32: Article 11


 • 0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kushoto) akipokea ripoti ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa ajili ya Jeshi la Polisi kutoka kwa Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa. Mpango huo unatarajiwa kuanza rasmi hivi karibuni kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akisaini ripoti aliyokabidhiwa na Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa (kulia), kwa ajili ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa Jeshi la Polisi. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Mpango huo unatarajiwa kuanza rasmi hivi karibuni kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu.
  Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya kumkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) ripoti ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa ajili ya Jeshi la Polisi. Issa alisema Mpango huo unatarajiwa kuanza rasmi kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kulia) akzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) na Maafisa wa Jeshi la Polisi baada ya kukabidhiwa ripoti ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa ajili ya Jeshi la Polisi. Katika hotuba yake, aliwataka Polisi wahakikishe wanautekeleza Mpango huo na kila wiki ameagiza apewe ripoti ya utekelezaji huo unaotarajiwa kuanza katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni na baada ya hapo utasambaa nchi nzima. Kulia ni Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa. Wapili kushoto meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu. Kushoto meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati), ripoti ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa ajili ya Jeshi lake. Waziri Kitwanga alikabidhiwa ripoti hiyo na Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa (kulia) katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Mpango huo unatarajiwa kuanza rasmi kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni na baada ya hapo utasambaa nchi nzima. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Rais wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) (TWA), Irene Kiwia (katikati ) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu uzinduzi wa kampeni ya uwiano wa kijinsia ambayo ni kauli mbiu kuelekea kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, kushoto kwake ni Balozi wa kampeni ya uwiano sawa kijinsia Inspk.Prisca Komba na kulia kwake ni Mwenyekiti wa TWA, Sadaka Gandi kwenye mkutano uliofanyika mapema leo  jijini Dar es salaam. 

  Mwenyekiti wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA), Sadaka Gandi  akifafanua jambo kuhusu  uzinduzi wa kampeni ya usawa wa kijinsia kwenye mkutano na waaandishi wa habari uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.

  Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Rais wa  TWA Irene Kiwia kuhusu uzinduzi wa kampeni ya usawa wa kijinsia katika mkutano uliofanyika mapema leo Jijini Dar es salaam.

  Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA)  imetangaza uzinduzi wa kampeni ya uwiano wa kijinsia kwenye kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani ya Wanawake inayotoa wito kwa kila mtu kuchukua hatua za dhati kusaidia upatikanaji wa usawa wa jinsia kwa kasi zaidi ili kuwasaidia wanawake na wasichana kufikia malengo yao.
  Hali kadhalika inatoa wito kwa jamii kuwa na uongozi ulio na usawa wa kijinsia, kuheshimu na kuthamini tofauti bainia ya jinsia, kuanzisha  utamaduni jumuishi na  kuondoa upendeleo kwenye sehemu za kazi.

  Akizungumza leo kwenye mkutano wa waandishi wa habari kwenye ofisi za TWA jijini Dar es Salaam Rais wa TWA, Bi. Irene Kiwia alisema kuwa  lengo la Kampeni ya Uwiano wa Kijinsia ni kutoa wito kwa wanawake na wanaume kuungana pamoja  kusaidia wanawake kufikia hali ya usawa kwa idadi kubwa na  kutambua mchango wao usio na ukomo  wanaoutoa kwenye uchumi duniani kote kwa ujumla hususani  nchini kwetu Tanzania.

  “Kampeni ya Uwiano wa Kijinsia inamaanisha kutoa wito kwa wadau wote vikiwemo vyombo vya habari, watu binafsi, serikali na mashirika yote kutambua na kujenga uelewa kuhusu mianya inayozuia mchakato wa kuwepo usawa wa kijinsia na kutaka kuchukua hatua za dhati kuharakisha mabadiliko,” alisema Kiwia.

  “Mwaka 2014 Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum -WEF) lilitabiri kuwa usawa wa jinsia duniani utafikiwa mwaka 2095. Lakini mwaka mmoja baadaye, yaani 2015 lilikadiria kuporomoka kwa hatua husika na kupunguza kasi ya kufikia uwiano kuwa pengo la kijinsia linaweza kuzibwa ifikapo mwaka 2133. Hii inamaanisha kusubiri kwa miaka 117 ambayo ni mingi sana. Kutokana na hali hiyo TWA inaungana na wito wa dunia wa kuitaka kila nchi kuliweka suala la jinsia kwenye ajenda zake na kuharakisha kasi ya kufikia lengo la usawa wa kijinsia .” alisema Kiwia.

  Akitoa wito kwa watu binafsi, mashirika  na wadau wengine kushiriki kwenye kampeni  hiyo Mwenyekiti wa TWA Bi. Sadaka Gandi alisema Kampeni itahusisha matembezi ya kilomita sita asubuhi ya siku ya tarehe Tano mwezi March kuanzia kwenye `Viwanja vya Mbio za Mbuzi´ maarufu kama ‘Uwanja wa Farasi’ kupitia kwenye makutano ya  Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), kuelekea Kanisa Katoliki la Mt. Petro  na kupitia Ubalozi wa Kenya nchini na kurudia sehemu yalipoanzia.

  Bi. Sadaka Gandi aliendelea kusema kuwa matembezi hayo yatafuatiwa na mkutano wa kusherehekea siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani ambao utafanyika Machi 6, 2016 kwenye Hoteli ya Regency Kilimanjaro.

  Bibi Gandi alisema, “Mkutano huu utawakutanisha  wanawake na wanaume kutoka sehemu tofauti ambao watashirikiana na kushawishiana kuungana na harakati hizi, vile vile tutaonyesha mafanikio yaliyopatikana mpaka sasa kutoka Mkutano wa Beijing miaka 21 iliyopita, na hali kadhalika ni kasoro gani ambazo bado zipo na ni kwa namna gani ushirikiano wa pamoja unaweza kuharakisha mabadiliko. Tunaamini mchango wako sio tu kwamba utachangia msingi wa maendeleo ya wanawake  bali pia utaonesha ni jinsi gani kampuni yako  inachangia kwenye  upatikanani wa usawa wa kijinsia kwa ujumla”.

  Bibi Gandi alisema kuwa mkutano huo utazungumzia masuala mbalimbali yanayomhusu mwanamke kwa kuzingatia elimu, afya, uongozi, haki na sheria na uchumi.

  “Usawa wa jinsia  ni muhimu kwa sababu umefungamana na kukua kwa uchumi kwani maendeleo ya wanawake na uongozi ni nguzo ya ufanisi kwenye biashara na ustawi wa uchumi”, alihitimisha.  0 0

  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- kwa lengo la kukagua jengo la watoto pamoja na jengo la wazazi namba mbili ( Maternity Block Two) ili kuona utendaji kazi na utekelezaji wa maagizo ya Rais John Magufuli . 
   Mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais Magufuli aliagiza watumishi wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , wazee na Watoto kitengo cha afya ya mama na mtoto kuhama katika jengo hilo ili kupisha Hospitali ya Taifa Muhimbili kulitumia kama wodi ya wazazi . 
   Waziri Ummy ambaye ameambatana na Naibu Waziri Dokta Hamis Kigwangala ameelezea kuridhishwa na ukarabati unaoendelea katika majengo hayo . 
  “Jengo la watoto tatizo kubwa lilikuwa ni miundombinu ya maji lakini naona ukarabati unaendelea vizuri na nina imani kuwa ukarabati utakamilika kwa wakati” amesema Waziri . Akizungumzia kuhusu jengo la wazazi namba mbili.
  Waziri huyo wa afya amesema kuwepo kwa jengo hilo ni faraja kwa kina mama na kusisitiza kwamba hakuna mama mjamzito atakayelala chini . Mpaka sasa kina mama 53 tayari wamehamia katika jengo hilo na wanapatiwa huduma zote.
   Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk Hamisi Kigwangalla wakikagua wodi mpya ya wazazi ambayo awali ilikuwa ofisi za kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo.

   Waziri Ummy Mwalimu akimsikiliza mmoja wa wagonjwa wa figo waliolazwa katika jengo la watoto. 
   Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa watoto wanaougua ugonjwa wa saratani waliolazwa katika jengo la watoto lililopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

   Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Ufundi, Aksante wakati akimwelezea juhudi zinazoendela za kukarabati jengo la watoto ambalo lipo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya Rais John Pombe Magufuli kuaagiza. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla akimsikiliza mkururugenzi huyo. Leo Waziri Mwalimu na naibu waziri wa wizara hiyo, Dk Kigwangalla wametembelea Jengo la Watoto na Jengo namba mbili la wazazi kukagua utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli ambaye ametaka jengo la watoto linalovuja likarabatiwe haraka.
  Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk Hamisi Kigwangalla wakitazama jengo (pichani halipo) ambalo limeaanza kukarabariwa baada ya agizo la Rais John Pombe Joseph Magufuli.
  Picha zote na John Stephen-Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

  0 0

  Halmashauri ya Wilaya ya SONGEA Mkoani RUVUMA imemfukuza kazi mhandisi wa Wilaya hiyo, Mhandisi DAUDI BASILIO kwa kosa la kutumia vibaya madaraka yake kwa kuidhinisha fedha za ujenzi wa barabara kutoka MBINGA MHALULE hadi MPITIMBI pamoja na ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao la MGAZINI kinyume cha taratibu na kusababisha hasara ya zaidi ya milioni 38. Story kamili hii hapa RUVUMA TV.

  0 0

   Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza (kulia) akiwaongoza waombolezaji wengi wao wakiwa wasanii kubeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii, Michael Mhina 'John Walker' wakati wa kuutoa mwili chumba cha maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tayari kwa kuombewa na kuagwa katika Kanisa la Muhimbili, Dar es Salaam. Mwili wa Mhina ulisafirishwa kwenda kwao, mkoani Tanga kwa mazishi.

  0 0

  Wataalam wa Upasuaji wakiangalia namna ya kufanya upasuaji kwa njia ya vitundu wakati wa kuanza kwa huduma mpya ya kitabibu katika hospitali ya rufaa ya kanda ya Mbeya itakayomuwezesha mgonjwa kufanyiwa upasuaji kwa njia ya vitundu (Laparoscopic surgery) na hivyo kumuwezesha mgonjwa kupona mapema na kuwahudumia wagonjwa wengi kwa muda mfupi.

   Prof. Dr Med Henning Niebuhr kutoka Ujerumani akitoa maelekezo juu ya namna ya kufanya upasuaji kwa njia ya vitundu.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0


  Na Princess Asia, MOROGORO
  KOCHA Mganda wa Simba SC, Jackson Mayanja (pichani) amesema kwa mfumo wanaotumia Yanga SC anaweza kuwafunga hata mabao 3-0 Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.  
  Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Uganda, aliyejiunga na Simba SC katikati ya Januari baada ya kuondolewa kwa Muingereza, Dylan Kerr amesema kwamba amekuwa akiifuatilia Yanga inayofundishwa na Mholanzi, Hans van der Pluijm kwa muda mrefu, hususan kwenye michezo yao mitano iliyopita ya Ligi Kuu na haoni kwa nini asiwafunge Jumamosi.
  Mayanja aliyeiongoza Simba kushinda mechi zote sita za Ligi Kuu tangu atue Msimbazi akitokea Coastal Union ya Tanga, amesema kwamba anatambua umuhimu wa kushinda mchezo huo na anaamini itakuwa rahisi kwake kutimiza malengo hayo, iwapo wapinzani watacheza mfumo wao ule ule uliozoeleka wa 4-3-3.

older | 1 | .... | 1127 | 1128 | (Page 1129) | 1130 | 1131 | .... | 3283 | newer