Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1126 | 1127 | (Page 1128) | 1129 | 1130 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Mhe. JaJi Francis S.K. Mutungi amevitaka vyama vya Siasa nchini kuhakikisha kuwa Katiba na Kanuni za Vyama vya Siasa zinaheshimiwa na kufuatwa katika utendaji wa kila siku wa chama cha siasa ili kuepuka migogoro na migongano ndani ya vyama.  Hayo ameyabainisha kwenye barua yenye Kumb. Na. HA.322/362/01/103 aliyoiandikia vyama vya siasa mapema leo.

  “Nimeona ni vyema nitumie fursa hii kuviasa Vyama vya Siasa kuhusu hali hii, kwani hali hii ya kufanya mambo kiholela pasipo kufuata Katiba na Kanuni kama itaachwa iendelee hivi ndani ya vyama kwa hakika italeta migogoro na mipasuko mikubwa ndani ya Vyama vya Siasa husika.”

  “Wakati huu ambapo nchi yetu inasubiri marudio ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, nimeandikiwa barua na pia kupata nakala za barua kutoka kwa baadhi ya Vyama vya Siasa kuhusu migongano ya wanachama na viongozi au viongozi wenyewe kwa wenyewe kuhusu suala la kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar. “alisema Jaji Mutungi
  Barua hiyo ilibainisha  kuwa suala hilo la migongano limejitokeza pia kwa wingi kwenye Vyombo vya Habari, ambapo wanachama na viongozi au viongozi wenyewe kwa wenyewe wametofautiana na kupingana hadharani.

  Jaji Mutungi amesema kwa mujibu wa Kanuni ya 3(1) ya kanuni za Usajili wa Vyama vya Siasa za mwaka 1992 (GN.No. 111) Vyama vya Siasa vinaposajiliwa vinapaswa kuwasilisha Katiba na Kanuni zake kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

  “Ikumbukwe kwamba, suala la msingi hapa ni kwamba,sharti la kuwepo kwa Katiba na Kanuni katika chama, kimsingi ni mwendelezo wa kukuza na kudumisha dhana ya kuendesha Vyama kitaasisi kulingana na mwongozo uliokubalika na kuasisiwa kichama kwa mfumo wa Katiba na Kanuni za chama na si kuendesha chama kiholela kama inavyoelekea kuota mizizi kwa baadhi ya Vyama vya Siasa hivi sasa.”ameongeza Jaji Mutungi

   Jaji Mutungi amevisihi Vyama vyote vya Siasa, kuhakikisha kwamba matamko ya chama hususan yahusuyo msimamo wa chama kuhusu jambo zito la kisera, kitaifa n.k., mathalan kama lilivyo la uchaguzi huu wa Zanzibar basi yatolewe rasmi na mtu mwenye mamlaka ya kuongea kwa niaba ya chama. Na endapo kuna mwananchama au kiongozi ambaye ataenda kinyume achukuliwe hatua haraka iwezekanavyo na chama husika kwa kuzingatia   katiba na kanuni zake ili kuepusha sitofahamu inayokuwa imejitokeza katika jamii.

  “Ni vyema misimamo kama hiyo ya chama itokane pia na vikao halali vya chama na siyo matakwa ya kiongozi mmoja au mwanachama mmoja au wachache.  Vinginevyo kama tutapeleka na kufanya uendeshaji wa vyama kiholela tutachangia kuwachanganya wananchi na kupoteza kabisa imani na heshima ya Jamii iliyokuwa imeanza kujengeka kwa Vyama vya Siasa”. Amesisitiza Jaji Mutungi

  Aidha vyama vvya Siasa vimeaswa kuchua hatua  ya haraka iwezekanavyo kwa mwanachama au kiongozi  wa chama anayefanya mawasiliano ama kutoa matamko bila idhini ya mamlaka na pia vyama  vimeonywa kutowajengea wananchi tashwira ya kwamba kuna makundi yanagombania madaraka  na kuendeleza maslahi binafsi  kwa sababu jambo hilo linashusha hadhi ya vyama vya Siasa nchini.

  0 0

  Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

  Maofisa wakuu wa Polisi  wanatarajia kukutana jijini Dar es Salaam kesho katika kikao kazi cha siku mbili kujadili na kupanga mikakati mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu na wahalifu hapa nchini.

  Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Msemaji wa Jeshi la Polisi,  Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Advera Bulimba alisema kikao hicho kitawakutanisha maofisa wakuu wa makao mkauu, makamanda wa Polisi wa mikoa yote,  vikosi bara na Zanzibar ili kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utendaji katika kipindi cha mwaka uliopita na kuweka mikakati mipya ya kupambana na uhalifu kwa mwaka huu.

  Aidha, Bulimba alisema mbali na utaratibu wa mawasiliano ya kila siku katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao, Jeshi la Polisi pia lina utaratibu wa kukutana kila mwaka kwa pamoja ili kubadilishana uzoefu na mbinu za wahalifu kwa lengo la kuhakikisha kuwa usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika hapa nchini.

  “Katika kikao hicho Inspekta Jenerali wa Polisi atatoa maelekezo ya kiutendaji ambayo lengo lake ni kuhakikisha kuwa kila ofisa,  mkaguzi na askari anawajibika kwa nafasi yake katika kuhakikisha uhalifu unapungua hapa nchini” Alisema Bulimba.

  Bulimba alisema kikao kazi hicho kinatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga ambapo kauli mbiu katika kikao hicho ni “Badilika kifikra, acha kufanya kazi kwa mazoea”.

  0 0
 • 02/16/16--07:13: SHUKRANI
 • Mwaka mmoja umepita tangu mama yetu mpendwa ,Febronia Mshomba Mlekwa ,ulipoitwa na Mwenyezi Mungu tarehe 16/02/2015 na kupumzishwa  Goba ,Dar es salaam tarehe 19/02/2015 

  Umetuacha katika majonzi makubwa lakini tukiwa na matumaini ya kuonana tena tukimtukuza Mungu pamoja na Malaika na Watakatifu wote Mbinguni.

  Hatutasahau upendo,ucheshi,upole,hekima,moyo wa kujitoa kuwahudumia wengine na kutokupenda makuu.

  Unakumbukwa na Mume wako Prof Victor M.Mlekwa, watoto wako Michael, Mary,Julius,Deus na Noel,wakwe zako Netiwe na Rachael, wajukuu wako Michaela,Victor na Febronia,dada zako Marselina na Maria , mdogo wako Imelda,ndugu ,marafiki na majirani.

  Tunatoa shukrani kwa ndugu,jamaa,marafiki ,majirani,madaktari na wauguzi  wa hospitali ya Taifa Muhimbili na Hubert Kairuki , Uongozi mzima wa Parokia ya Mtakatifu Maximilian Maria Kolbe Mwenge ,Kanda ya Mlalakuwa ,Jumuiya ya Mtakatifu Inyasi wa Antiokia,Chuo Kikuu cha Dar es salaam ,Taasisi ya Elimu Tanzania na wote waliotufariji kwa hali na mali katika kipindi chote cha msiba. 

  Ibada ya Misa ya shukrani itafanyika  Jumamosi tarehe 20/02/2016 kuanzia saa 11: 00 Jioni nyumbani Survey Mwenge .

  Raha ya Milele Umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele umwangazie, Apumzike kwa Amani,Amina.

  0 0
 • 02/16/16--07:21: PAMOJA APP Launched in Dar
 • This year’s Valentine’s Day at Quality Centre Mall was celebrated with a bang! Thousands of eager residents of Dar es Salaam had gathered inside the mall, gazing in wonder at the splendid decorations of large hearts all around. They blended right in with the bongo-flavored music, with the emcees bringing in the cool vibes, turning the event into a party of sorts. 

  Their curiosity lingered, until the reigning Miss World-Tanzania arrived in a luxurious car, stopping right in front of the mall. 

  Dressed in a long red flowing gown and glittery silver stilettoes, Miss Lilian Kamazima looked her part. She was given a grand red carpet welcome, after which, she was escorted to the stage, by the organizers of the event, Purple Cow Media Ltd. She was presented with a bouquet of gorgeous red roses, which enhanced her beauty.

  The ‘Impress Me’ contest, sponsored by Pamoja, Tanzania’s first Swahili Dating Mobile App, is certainly impressive, to say the least. Before the event proceeded further, Lilian gave a short demonstration on how to download and use the Pamoja app, and talked about how the app will help users to have fun and meet up. There were also small leaflets illustrating the Pamoja app, distributed all over the mall, at various entries, such as Funspot, Restaurants and the movie theatre.  

  The main part of the event was for the crowd to come up and impress Lilian with their words or actions. Many participated, some sang, some danced, some read poems, and some said lovely words, as the crowd cheered along. There was one lady, who tried to impress Lilian by doing a catwalk. The highlight of the event was when Lilian suddenly stood up at this moment, and taught the crowd how to catwalk, which encouraged everyone to join her. 

  All were winners in the eyes of Lilian, as they received exclusive gift hampers, free movie tickets and entry to Funspot, all sponsored by the Quality Centre Mall and Pamoja. 

  The event was a success, and closed with all participants gathering up to take a ‘Selfie with Lilian’.

  0 0

  Na Lucas Mboje; Morogoro

  MADEREVA wote wa magari ya Jeshi la Magereza nchini wametakiwa kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani wakati wote wanapoendesha magari ili kujiepusha na ajali zisizo za lazima.

  Rai hiyo imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja wakati akizungumza kwenye hafla ya kufunga Mafunzo ya Udereva Kozi ya Msasa kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa yote Tanzania Bara yaliyofanyika katika Chuo cha Udereva na Ufundi, Kingolwira Mkoani Morogoro.

  Jenerali Minja amewaagiza Wahitimu wa Mafunzo hayo kuhakikisha kuwa wanawajibika pia kuyatunza magari watakayokabidhiwa kuyaendesha ili yaweze kudumu kwa muda mrefu kama ilivyokusudiwa.

  "Nawataka mjiepushe na uzembe wakati mnapoendesha magari ya Jeshi letu ikiwa ni pamoja na kutokujihusisha na ulevi na kuendesha magari hayo kwa mwendo kasi bila kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani". Alisema Jenerali Minja.

  Aidha Jenerali Minja amezungumzia upungufu mkubwa wa magari katika Jeshi hilo ambapo katika kushughulikia changamoto hiyo Jeshi la Magereza kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa limesaini Mkataba na Kampuni za Ashok Layland na Jeep na magari mia tisa na tano(905) yanategemewa kupokelewa mapema mwanzoni mwa mwezi Mei Mwaka huu. 

  Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Udereva na Ufundi Kingolwira, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Osmond Ndunguru kupitia risala yake kwa Mgeni rasmi amesema kuwa Wahitimu hao wamejifunza Mafunzo yote yaliyopo kwenye Mtaala wa Mafunzo ya Udereva kwa nadharia na vitendo ikiwemo mbinu mbalimbali katika fani ya Udereva wa Magari ambapo jumla ya Wanafunzi 125 wamehitimu Mafunzo hayo miongoni mwao Wanaume ni 133 na wa kike ni 2.

  Aidha Kamishna Msaidizi wa Magereza, Nduguru alieleza changamoto mbalimbali ambazo Chuo hicho kinakabiliana nazo ikiwemo upungufu wa magari ya kujifunzia pamoja na uchakavu wa miundombinu ya majengo hali inayoathili utoaji taaluma ya mafunzo hayo.

  Chuo cha Udereva na Ufundi cha Kingolwira, kilichopo Mkoani Morogoro kinamilikiwa na Jeshi la Magereza ambacho hutoa Mafunzo ya Udereva kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza ambao huendesha magari ya Jeshi hilo na katika Taasisi mbalimbali za Umma hapa nchini.
  Kamishna Jenerali John Casmir Minja akipokea Salaam ya Utii kutoka kwa Gadi Maalam iliyoandaliwa na Maofisa wa Jeshi la Magereza, Wahitimu wa Mafunzo ya Udereva(hawapo pichani) katika Chuo cha Udereva Kingolwira Mkoani Morogoro. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Chuo hicho 16 Februari, 2016.
  Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum iliyoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Udereva katika Chuo cha Uderevau na Ufundi Kingolwira, Mkoani Morogoro.
  Wahitimu wa Mafunzo hayo wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika mwendo wa kasi kama wanavyoonekana katika picha.


  0 0


  CCP Banner Tanzania 040216(1)

  The contact promotion program inakukaribisha kuhudhuria event itakayohusisha makampuni kutoka Mauritius watakaokuja kuonesha bidhaa zao hapa Tanzania. Hii event ina dhumuni kubwa la kuwaleta pamoja wafanya biashara wakubwa na wadogo pia (buyers na investors) wa nchi zote mbili (Tanzania & Mauritius), itawaleta viongozi wa sekta tofauti pamoja na kuwapa nafasi ya kuzungumzia biashara zao.

  BIDHAA ZITAKAZOKUWA ZINAONESHWA NI ZA SEKTA ZIFUATAZO ::Light Engineering, Agro Products, Paint&chemicals, Textile&Accessories

  Hii event itakuza mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Mauritius.

  ITAFANYIKA :: JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVENTION CENTRE

  TAREHE 22 HADI 23 FEBRUARY 2016

  KIINGILIO NI BUREE KABISA!

  USIKOSE KWENDA KUJICHANGANYA NA WATU TOFAUTI WA HAPA TANZANIA NA WALE KUTOKA MAURITIUS ILI UWEZE KUJIKUZA ZAIDI KATIKA BIASHARA. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

   0 0

   Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Jumamosi kati ya watani wa jadi Simba SC dhidi ya Yanga SC utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku kiingilio cha chini kikiwa ni Shilingi elfu saba tu (7,000).
   Kiingilio cha juu cha mchezo huo kitakua shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, Elfu Ishirini (20,000) VIP B & C, Elfu Kumi (10,000) kwa viti vya rangi ya machungwa (Orange), na Elfu Saba (7,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.

    Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa saa 2 kamili asubuhi katika vituo vya TFF (Karume), Buguruni Olicom, Ubungo Oilcom, Kidongo Chekundu (Mnazi Mmoja), Posta (Agip), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Taifa, Makumbusho Stand, Kivukoni Ferry.
   Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi wote wenye beji za FIFA, mwamuzi wa katikati Jonesia Rukyaa (Kagera), akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Samwel Mpenzu (Arusha), mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) huku Kamisaa wa mchezo huo akiwa Khalid Bitebo (Mwanza).
   Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea Jumamosi kwa michezo sita, Young Africans v Simba (Taifa), Mbeya City v Azam (Sokoine), Stand United v JKT Ruvu (Kambarage), Toto Africans v Kagera Sugar (CCM Kirumba), Mgambo Shooting v Tanzania Prisons (Mkwakwani) na Majimaji FC v Mtibwa Sugar (Majimaji).
   Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa michezo miwili, Mwadui FC v Coastal Union uwanja wa Mwadui Complex, huku Ndanda FC wakicheza dhidi ya African Sports uwanja wa Nagwanda Sijaon mjini Mtwara.

   0 0

   Serikali imesema itachukua hatua kali kwa kampuni ya Halotel kama itashindwa kutekeleza makubaliano ya mkataba wa kusambaza huduma za simu na mtandao katika ofisi za Serikali katika kila Wilaya nchini kote.

   Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa wilayani Maswa wakati akizungumza na watendaji wa sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mkoani Simiyu na kusisitiza kutoa ushirikiano unaostahili kwa kampuni hiyo.

   “Makubaliano yetu kati ya Serikali na Halotel ni kuunganisha ofisi za Umma kwa mtandao zikiwemo shule tatu katika kila Wilaya, Hospitali, Mahakama na Ofisi za Polisi ili kuwezesha mkakati wa mawasiliano vijijini kutekelezeka”, amesema Prof. Mbarawa.

   Waziri Prof. Mbarawa ameeleza kuwa ifikapo mwaka 2017 kila eneo hapa nchini litakuwa na huduma ya mawasiliano ya mtandao na kuwezesha wananchi wote kunufaika na huduma hizo.

   Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua Ujenzi wa Barabara ya Lamadi-Bariadi KM 71.8 na Bariadi-Maswa KM 49.7 na kuwapongeza makandarasi wanaojenga barabara hizo kwa kazi nzuri wanayofanya.

   “Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya, hakikisheni kazi yenu inauwiana na thamani ya fedha na kuhakikisheni wafanyakazi wazawa wanapewa kipaumbele katika kazi wanazoziweza na kupewa mikataba stahiki ya kazi wanazozifanya”, amesititiza Prof. Mbarawa.

   Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amemuagiza mkandarasi anaejenga barabara ya Maswa-Mwigumbi KM 50.3 kuhakikisha nyumba zinazojengwa kwa ajili ya mkandarasi zinajengwa kwa ubora ili zitumike kwa muda mrefu.

   “Nakuagiza Meneja wa TANROADS, hakikisha nyumba hizi baada ya mradi wa barabara kukamilika unazikabidhi kwa jeshi la polisi ili waweze kuzitumia kwa ajili ya makazi na ofisi”, amesema Prof. Mbarawa.

   Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Eraston Mbwilo amemwomba Waziri Prof. Mbarawa kuelekeza nguvu za ujenzi wa ofisi na nyumba za watumishi katika mkoa huo.

   Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Bi. Rosemary Kirigini amemuomba Waziri Prof. Mbarawa kuwawezesha Wakala wa Majengo nchini (TBA) kukamilisha mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo unaojengwa sasa kwa miaka mitano ili kuipunguzia Wilaya hiyo adha ya kutumia jengo chakavu ambalo si salama hasa kipindi cha mvua.

   Waziri Prof. Mbarawa pia amekagua Kiwanja wa Ndege kilichopo Mkoa wa Shinyanga na ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kiwanjani hapo na kusisitiza kuwa Serikali iko katika hatua za kuboresha uwanja huo kuwa wa kisasa ili kuvutia mashirika mengi ya ndege kutumiwa kiwanja hicho.

   Waziri Prof. Mbarawa yupo kwenye ziara ya kukagua miradi ya ujenzi kwenye sekta za barabara, nyumba, viwanja vya ndege na mkongo wa taifa wa mawasiliano katika mikoa ya kanda ya ziwa ambapo ametembelea Wilaya za Busega, Bariadi na Maswa mkoani Simiyu.

    Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mkandarasi anayejenga barabara ya Lamadi-Bariadi Km 71.8, mkoani Simiyu.

    Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (aliyevaa koti la bluu), akisikiliza maelezo ya mkandarasi kuhusu ujenzi wa mtambo (hauonekani pichani) wa kusaga kokoto kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Maswa-Mwigumbi Km 50.3.

    Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akiongea na vibarua wanaofanya kazi kwenye mradi wa barabara ya Maswa-Mwigumbi Km 50.3, mkoani Simiyu.

    Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na wafanyakazi wa sekta za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuhusiana na mkakati wa Wizara wa kuongeza mapato mkoani Simiyu.

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akitazama kifaa cha kupima hali ya hewa katika uwanja wa ndege wa Shinyanga. Kushoto ni Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) mkoani Shinyanga Bw. Omary Khamis na katikati ni Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga Eng. Augustino Philipo. 

   Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.


   0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Bi. Maniza Zaman (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake mapema leo.
    Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Bi. Maniza Zaman (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipomtembelea waziri huyo ofisini kwake mapema leo.

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akisisitiza jambo wakati wa maongezi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Bi. Maniza Zaman (hayupo) alipomtembelea waziri huyo ofisini kwake mapema leo. 

   0 0

   Mabalozi wa Huawei wakipozi siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
   Balozi wa Huawei akikabidhi zawadi kwa mteja siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
   Balozi wa Huawei akikabidhi zawadi kwa mteja siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam.
   Baadhi ya wateja wakipata picha ya ukumbusho na balozi wa Huawei siku ya uzinduzi wa promotion ya Valentine ya wiki 3 inayoendeshwa na kampuni ya Huawei Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mlimani City Dar es Salaam. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

   0 0


   0 0

   Egypt has committed to improve areas of cooperation between herself and the East African Community.
   Egypt's new Ambassador to the Tanzania and the EAC, H.E. Mohammed Yasser Ala'Eldeen El Shawaf, said his country was eager to boost trade and technical cooperation with the EAC Partner States.
   Amb. Shawaf made the remarks after he presented his credentials to the EAC Secretary General, Amb. Dr Richard Sezibera, at the EAC Headquarters in Arusha today.
   Welcoming the Egyptian ambassador, Dr. Sezibera described Egypt as an important trading partner for the EAC and praised its outstanding role in promoting negotiations for the Tripartite Free Trade Area (FTA) between the EAC, COMESA and SADC.
   Dr Sezibera noted that the Tripartite FTA when fully implemented would move the African Continent from the margins of Global Trade, adding that it was a good basis for the Continental Free Trade Area envisioned by the African Union.
   The Secretary General thanked Egypt for making a tariff offer to the EAC and went on to request Egypt to encourage the other member states to negotiate as a bloc instead of doing so as separate entities saying this would hasten the operationalization of the Tripartite FTA.

    The new Egyptian Ambassador to Tanzania and the EAC Mohammed Shawaf holds talks with EAC Secretary General Amb. Dr. Richard Sezibera at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania.
   EAC Secretary General Amb. Dr Richard Sezibera with the Egyptian Ambassador to Tanzania and the EAC Mohammed Shawaf after the envoy presented his credentials to the Secretary General.


   0 0
   0 0
   0 0


   0 0

    Umati wa watu ukisheheni katika tamasha la Mchizi wangu  la 93.7 Efm Radio, lililofanyika siku ya wapendanao tarehe 14/02/2016 katika viwanja vya Posta Kijitonyama Dar es salaam, likiongozwa na mziki wa mchiriku na singeli Msaga Sumu. Tamasha hilo lilisheheni Wasani kibao wakitumbuiza huku wakiongozwa na msaga sumu na skide mtoto wa mama shante.
    Tuvituvitu vilivyojitokeza katika tamasha la mchizi wangu 
    Amsha amsha kutoka kwa baadhi ya mashabiki wakionyesha nyuso za furaha wakati wakipata burudani.
    Raisi wa singeli Suleiman Jabir a.k.a Msaga Sumu akitumbuiza mashabaki waliofika kwenye tamasha la Mchizi Wangu.
   Vijimambo vingine vilivyotokea katika tamasha hilo

   0 0


   0 0
  • 02/16/16--12:30: Article 2
  •  


   0 0
  • 02/16/16--23:00: RIP JONI WOKA

  • Ras Lion + John Woka Feat Chief Kimweli " Yalaah!! " Emptysoulz Production

   0 0


   Kaimu Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Gladyness Mkamba (katikati) akizungumza wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Gen. Gaudence Milanzi katika ufunguzi wa Mkutano wa mapitio ya kukamilisha mradi wa Kitaifa wa Uendelezaji Misitu na Ufugaji Nyuki nchini (NFBKP II) unaofadhiliwa na Serikali ya Finland kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika Chuo cha Taifa cha Utalii Tawi la Bustani Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Februari, 2016. Kushoto ni Mshauri wa masuala ya Malisili kutoka Ubalozi wa Finland hapa nchini Bw. Mikko Leppanen.
   Sehemu ya washiriki wa mkutano huo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na TAMISEMI. 
   Picha ya pamoja.
   Na Hamza Temba, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii.

   JAMII hapa nchini imeaswa kutumia fursa iliyopo ya ufugaji wa nyuki na upandaji wa miti kibiashara ili kujikwamua kwenye lindi la umasikini.

   Hayo yamesemwa jana na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Gladyness Mkamba akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam.

   Bi. Mkamba alisema kuwa Tanzania ina fursa kubwa ya kuzalisha asali kwa wingi duniani ambayo ikitumiwa ipasavyo itasaidia kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

   "Kwa sasa Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika ambapo inazalisha asali tani 34,000 kwa mwaka baada ya Ethiopia inayozalisha tani 56,000. Hata hivyo kiwango hicho ni kidogo kwa kuwa Tanzania ina uwezo wa kuzalisha asali tani 1,038,000 kwa mwaka" Alieleza.

   Akizungumzia changamaoto kuu inayosababisha kiwango hicho kisifikiwe kirahisi, amesema ni utashi hafifu wa jamii kujishuulisha na kazi za ufugaji nyuki na uhifadhi wa mazingira ikiwemo upandaji wa miti.

   Bi. Mkamba aliongeza kuwa Jamii ikihamasishwa vya kutosha juu ya faida za ufugaji nyuki na upandaji wa miti inaweza kutoa matokeo ya haraka kwa kuwa asali ina faida kubwa ikiwemo za kiafya na za kiuchumi.

   Kwa upande wake Bi. Magdalena Muya ambaye ni Mratibu Msaidizi wa mradi wa Kitaifa wa Misitu na Ufugaji wa Nyuki nchini (NFBKP II) ameeleza kuwa changamoto zingine zinazokwamisha mafanikio katika sekta ya ufugaji nyuki nchini ni ukosefu wa teknolojia za kisasa za ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali pamoja na ukosefu wa mitaji ya kuanzisha miradi mikubwa ya ufugaji wa nyuki.

   Nae mshauri wa masuala ya Malisili kutoka Ubalozi wa Finland hapa nchini Bw. Mikko Leppanen, ameeleza kuwa Misitu ya Tanzania inakabiliwa na changamoto ya uharibifu mkubwa unaosababishwa na shughuli za kibinadamu ambapo hupelekea ukame na kuathiri pia uzalishaji wa asali ambao hutegemea malighafi za misitu.

   Mshauri huyo ameiasa jamii hapa nchini kutunza mazingira ya misitu, kupanda miti kibiashara na kuhifadhi mazingira ambayo yatasaidia kuweka mazingira bora ya kuishi ikiwa ni pamoja na kuwezesha ufugaji wa nyuki kibiashara na kuwainua watu kiuchumi.

   Wakati huo huo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili Bi. Gladyness Mkamba akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Gen. Gaudence Milanzi wakati akifungua mkutano wa siku moja wa mapitio ya kukamilisha Mradi wa Kitaifa wa Misitu na Ufugaji wa Nyuki nchini (NFBKP II) ameishukuru Serikali ya Finland kwa kusaidia ufadhili wa mradi huo.

   Ameeleza kuwa mradi huo ambao bajeti yake ni Euro Milioni 19.5 ambazo ni zaidi ya Tsh. Bilioni 47 kwasasa unafadhili mpango wa miaka minne wa Misitu binafsi katika Mikoa ya Iringa, Njombe na Morogoro kwa lengo la kuinua kipato cha wananchi wa vijijini katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania, Mikoa hiyo ni shemu ya Mikoa saba ya jumla inayofadhiliwa na mradi huo.

   Amesema hayo yatafanyika kwa kuanzisha misitu ya uhakika yenye faida na kuongeza thamani ya mazao yake kwenye mtiririko wa uzalishaji kuanzia mbegu za miti hadi kwenye bidhaa bora za mbao.

   Mradi huo ulianza Oktoba mwaka 2013 hadi Oktoba 2015 na kuongezewa muda wa ziada wa miezi minne ambapo unakamilika mwezi huu wa Februari 2016.

  older | 1 | .... | 1126 | 1127 | (Page 1128) | 1129 | 1130 | .... | 3272 | newer