Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1125 | 1126 | (Page 1127) | 1128 | 1129 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge amezionya Halmashauri za Wilaya za Njombe na Mbarali kuhakikisha fedha za miradi ya maji zinazotolewa na Serikali, zinasimamiwa vizuri na kutekeleza miradi ya maji na si vinginevyo.

  Mhe. Lwenge alisema hayo mwishoni mwa juma katika ziara yake ya Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, alipotembelea Wilaya ya Njombe, mkoani Njombe na Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya katika ziara yake ya kukagua utekelezaji na maendeleo ya miradi ya maji na upatikanaji wa huduma hiyo.

  “Naagiza Halmashauri za Wilaya zihakikishe fedha zilizotengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji, zisimamiwe vizuri na zitumike kufanya hivyo na zisitumike kwa miradi mingine. Mhe. Rais Magufuli ameazimia kutatua kero ya maji nchini na hatatutakuwa na sababu yoyote ya kutotimiza lengo hilo, na ifikikapo mwaka 2020 tuwe tumefikia asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini katika kutoa huduma ya maji na hili lipo ndani ya uwezo wetu”, alisema Mhe. Lwenge.

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji alisema ni wajibu wa watendaji wote wa Serikali kuwajibika ipasavyo katika nafasi zao kila moja, kwani Serikali ya Awamu ya Tano ni ya vitendo na si maneno. Huku akiendelea kusisitiza suala la maendeleo ya Sekta ya Maji ni shirikishi kati ya Serikali na wananchi, na si Serikali pekee ili kuhakikisha tatizo la maji linapatiwa ufumbuzi kwa haraka na mafanikio.

  Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dr. Rehema Nchimbi amemuhakikishia Mhe. Lwenge kuwa wataiunga mkono Serikali kwa kuhakikisha wanashirikiana na wananchi kutunza mazingira na vyanzo vya maji, ili rasilimali hiyo iwepo ya kutosha kwa miaka mingi ijayo na maendeleo ya sekta hiyo yawe endelevu. Dr. Nchimbi alisema  watafanya jitihada za kumaliza changamoto za shughuli za kibinadamu zinazoendana kinyume na Sera na Sheria za Mazingira na  Maji nchini.

  Katika ziara yake hiyo Mhe. Lwenge aliweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maji wa vijiji cha Peruhanda, Wilaya ya Njombe na Ubampa, Kata ya Ubaruku, Wilaya ya Mbarali, ikiwa ni kati ya miradi 1,800 inayotekelezwa na Serikali kitaifa na kati ya miradi hiyo, 1,200 ikiwa imekamilika.

   Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ubampa, Kata ya Ubaruku, Wilaya ya Mbarali, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Abbas Kandoro (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Gulamhussein Kifu.
   Mradi wa Maji unaohudumia Kijiji cha Peruhanda, Wilaya ya Njombe.

   Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge mara baada kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa Kijiji cha Ubampa, Kata ya Ubaruku, Wilaya ya Mbarali na Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Mhe. Haroon Pir Mohamed. 
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akitakata utepe na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji katika Kijiji cha Peruhanda, Wilaya ya Njombe, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Saraha Dumba.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akikagua chanzo cha maji cha Nyenga kinachohudumia Mji wa Njombe, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Njombe (NJUWASA), Inj. Daudi Majani. 

  0 0

   Mbunge wa jimbo la Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya maafa ya maruriko yaliyotokea Rufiji, Mkoani Pwani, kutokana na mvua kubwa kunyesha. 
  Baadhi ya watendaji na viongozi wa serikali wakikagua
  sehemu ambayo imepata athari ya mafuriko.
  Mbunge wa Jimbo la rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa amebeba gunia la mahindi kwa ajili ya kutoa msaada kwa wahanga wa mafuriko hayo.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameitaka kampuni ya Sino-tAN Renewable Energy ya kuzalisha umeme wa upepo katika eneo la Makambako Mkoani Njombe kuihakikishia Serikali kuwa ina uwezo wa kufanya hivyo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo 15 Februari mpaka 15 Machi 2016.

  Maagizo hayo yametolewa ofisini kwake wakati wa kikao baina ya Wizara na Kampuni hiyo iliyofika kuelezea changamoto inazokumbana nazo katika kutekeleza mradi huo wa kuzalisha Megawati 100 za umeme.

  Akizungumzia lengo lao la kuonana na waziri Muhongo, Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Alex O. Lema alisema upo mgogoro wa kuachia ardhi katika Kijiji cha Mtewele wilaya ya Wanging’ombe pamoja na kwamba  halmashauri husika ilishatoa kibali kwa kampuni hiyo.

  Bw. Lema ameeleza kuwa theluthi mbili za eneo la mradi zinapatikana katika wilaya ya Makambako wakati theluthi moja inayobaki ipo katika Wilaya ya Wanging’ombe ambako hasa ndiko kwenye mgogoro huo.

  Aidha Bw. Lema alitumia fursa hiyo kuiomba Wizara ya Nishati na Madini kuwa kiungo katika kuhakikisha mradi unafanikiwa kwa kuwashirikishawadau wengine ambao ni Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbunge wa eneo husika pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe.

  Baada ya maelezo toka kwa Mwenyekiti huyo, Prof. Muhongo alimtaka Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia nishati jadidifu, Edward L. Ishengoma kuteua maafisa wawili ili kufika katika eneo lenye mgogoro na kujionea sababu za wanakijiji hao kupinga eneo hilo kutumiwa na mradi huo na kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku mbiliza ufuatiliaji.

  Aidha, Prof. Muhongo ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imebadili namna yake ya utendaji na kuwataka wawekezaji hao kuwasilisha mpango kazi wao ndani ya mwezi mmoja kutokana na uhitaji mkubwa wa nishati ya umeme wa kutosha na wa uhakika.

  Mradi huu wa uzalishaji wa Umeme wa upepo wa Makambako umechukua miaka 10 tangu mwaka 2004 hadi sasa, ambapo  miaka mitano ya awali walikuwa wakifanya utafiti na kuandika ripoti iliyobainisha kuwa uzalishaji wa umeme wa upepo katika eneo hilo ni dhahiri na hivyo kibali kutolewa kwa wawekezaji hao kuanza utekelezaji ambao unakwamishwa na suala la ardhi kwa hivi sasa. 

  Bi Juliet Kairuki, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC (Tanzania Investment Centre) akihoji kuhusu kampuni hiyo kujihakikishia kuzalisha umeme wakati wa mkutano wao na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.

  Profesa Sospeter Muhongo akifuatilia maelezo ya Mkurugenzi wa Kampuni ya uwekezaji wa umeme wa upepo mjini Makambako Luka Buljani alipokuwa akitoa maelezo kuhusiana na mradi huo.

  0 0

  Waziri Mkuu Mhe.  Kassim Majaliwa akipokea nakala yake ya  fomu ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kutoka kwa Kamishina wa Maadili, Jaji Mstaafu Salome  Kaganda ambayo aliitia saini na kuipeleka kwenye Secretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambako ilitiwa saini na kamishina huyo. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Februari 15, 2016
   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Secretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambao walikwenda ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 15, 2016 kumpatia nakala yake  ya fomu ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma  ambayo aliitia saini  na kuipeleka kwenye Secretarieti  hiyo ambako ilitiwa saini na Kamishina wa Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda (wapili kulia).Kushoto ni Katibu wa Idara ya Viongozi Watumishi wa Umma, Secretarieti ya Maadili , John Kaole na kulia ni Katibu wa Idara ya Viongozi wa Siasa, Secretariet ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Waziri Kipacha. 
  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


  0 0

  Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (kulia) akimkabidhi msaada kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto Bi. Jack Omary(kushoto) ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii kituo cha taifa cha kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kurasini, hafla hii imefanyika katika siku ya wapendanao. Misaada hyo imetolewa na vijana wa UN Clubs Tanzania Network kwa kanda ya Dar es salaam pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.(Picha na Geofrey Adroph)

  UN Clubs Tanzania Network kanda ya Dar es Salaam wakishirikiana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wametoa msaada kwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Kurasini kwenye siku ya wapendanao ili kuonesha upendo mkubwa kwa watoto hao. 
  Vijana hao wa UN Club Tanzania Network wanafanya kazi siku ya wapendanao nchi nzima za kusaidia jamii na vijana wa jijini Dar es salaam wameungana na watoto wa kituo cha Kurasini kwa kutoa msaada na wanafunzi hao wametoka katika shule za sekondari za Zanaki, Azania, Benjamin na Jangwani. 
  Akizungumzia msaada huo, Afisa Ustawi wa Jamii katika kituo hicho. Jack Omary aliwashukuru kwa kuwatembelea siku ya wapendanao maana kuna watu wengine wanaitumia siku ya wapendanao kwenye starehe na hata kutumia pesa bila kuangalia kuna watu wanahitaji msaada. 
  Nae Stella kutoka UN Clubs Tanzania amesema lengo la kuja katika kituo cha watoto yatima cha Kurasini nikujumuika na hao watoto ambao hawana wazazi na pia watoto wenye shida mbalimbali.
  Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (kushoto) akiwakabidhi misaada watoto wa Kituo cha Kurasini, katikati ni mtoto Aboubakary Seif ambaye alipokea kwa niaba ya watoto wenzake. 
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiongoza shughuli ya kuhamisha vifaa katika jengo la Wizara ya Afya-Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto ambalo lipo katika eneo la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili 


   Askari wa wakihamisha vifaa kutoka katika jengo la Wizara ya Afya-Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto ambalo lipo katika eneo la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya Rais John Magufuli kutoa siku mbili wafanyakazi wa wizara hiyo wahame mara moja kwenye jengo hilo.
  Askari wa wakihamisha vifaa kutoka katika jengo la Wizara ya Afya-Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto ambalo lipo katika eneo la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya Rais John Magufuli kutoa siku mbili wafanyakazi wa wizara hiyo wahame mara moja kwenye jengo hilo.

  0 0


  0 0


  Rais John Magufuli afanya uteuzi wa nafasi mbalimbali wakiwemo mabalozi watatu, makamishina wa polisi na kaimu mkurugenzi mtendaji wa NIDA.https://youtu.be/Kzk84GFQIB8  

  Agizo la Rais Magufuli lakutaka jengo la ofisi katika hospitali ya muhimbili ligeuzwe kuwa wodi ya wazazi latekelezwa huku likiongwa na waziri wa afya.https://youtu.be/9BltPkmakRU  

  Watu wawili wamefariki dunia akiwemo askari polisi baada ya kupigwa risasi na majambazi wakati yalipovamia duka kwa lengo la kupora fedha mkoani Tanga.https://youtu.be/d8BYDBSrf8Q  

  Kasi ya utendaji kazi wa Rais John Magufuli yaendelea kuwashukia watumishi wa umma baada ya watumishi na watendaji wa TAKUKURU kutakiwa kuorodhesha mali zao baada taarifa walizotoa awali kukataliwa.https://youtu.be/hjG7ZCadx-o  

  Chama cha waandishi wa habari mkoani Mtwara chalaani vikali kitendo cha polisi mkoani humo kumkamata mwandishi wa CH10 na kushikilia vifaa vyake vya kazi. https://youtu.be/buQ4T9Veug8  

  Waziri Ummy Mwalimu awasimamisha kazi wakurugenzi 4 wa bohari kuu ya dawa kwa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi bilioni 1.5;https://youtu.be/6yzY5ugw6pk  

  Serikali yawataka watendaji nchini kutoa taarifa juu ya hospitali zinazokabiliwa na tatizo la uhaba wa vitanda vya wagonjwa; https://youtu.be/79wqvN7VSS0  

  Rais John Magufuli afanya uteuzi wa mabalozi watatu katika wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,https://youtu.be/JkO0ONi2R4A  

  Serikali yauagiza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam kukamilisha ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Majimatitu;https://youtu.be/W52zYmIla-E  

  Kampuni ya Ensol Tanzania yalikabidhi shirika la utangazaji Tanzania TBC  mitambo ya umeme wa jua iliyoko mkoani Ruvuma;https://youtu.be/lmvOSTsMu5E  

  Askari wa jeshi la polisi aliyepigwa risasi wakati wa majibizano na majambazi mkoani Tanga afariki dunia wakati akipatiwa matibau hospitalini;https://youtu.be/0MQSwqtjrgo  

  Serikali yazitaka halmashauri za Temeke na Ilala kutumia mashine za kieletroniki katika ukusanyaji wa mapato; https://youtu.be/P62ghd4CMW8  

  Shirika la viwango nchini TBS laendesha msako mkali kwa wafanyabiashara wa vifaa vya magari; https://youtu.be/NoJtAEz_ues  

  Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa  michezo ya shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF inatarajiwa kukutana kesho kupitia taarifa juu ya michezo ya ligi daraja la kwanza ; https://youtu.be/mXXD041zbaY  

  Inaelezwa kuwa Penati aliyoipiga mchezaji wa wa Barcelona, Lionel Messi wakati wa mchezo wa ligi kuu Uhispania  baina ya Barcelona na Celta De Vigo  yazua gumzo katika vyombo vya habari duniani;https://youtu.be/m9eM9eLIzF0  
    
  Walimu visiwani Zanzibar washauriwa kukaa karibu na wanafunzi katika ili kuweza kuwasaidia matatizo yanayowakabili; https://youtu.be/UVYiKGbzHMA  0 0
  0 0

   

  Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikpokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw. Clement Mshana aliupowasili katika ofisi za TBC Mikocheni leo jijini Dar es Salaam.


   

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kikao na uongozi wa TBC leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC  Bw. Clement Mshana
  Na Frank Shija, WHUSM 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Shirika la Utangazaji la Taifa TBC kutokana na utendaji usioridhisha. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBC leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape amewataja watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio Bwana Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi Bibi. Edna Rajab ambao wote kwa pamoja wasimamishwa kazi na uamuzi huo utafikishwa kwa Bodi ya TBC kwa hatua zaidi. 
  “ Tunachukua uamuzi wakuwasimamisha kazi watendaji hawa ili kujenga upya Idara hii muhimu katika ustawi wa TBC na habari kwa ujumla” Alisema Nape 
  Aidha Waziri huyo amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBC kuwachukulia hatua watumishi wengine walio chini ya Idara hiyo kwakuwa wako chini ya mamlaka yake na kutoa mrejesho wa hatua alizochukua dhidi ya wale wote wilioonyesha utendaji mbovu. 
  Alisema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu juu ya utendaji mbovu na wakutoridhisha viongzi na baadhi ya watumishi wa Idara hiyo hiyvo hatua hizo zimechukuliwa ikiwa ni kujenga upya na kuboresha Idara hiyo muhimu katika uendeshaji wa Shirika lolote lile la Habari na kuongeza ufanisi.  
  Idara ya Habari na Matukio ya TBC inaundwa na Mkurugenzi wa Idara, Meneja wa Vipindi Wahariri na Waandishi wa Habari ambapo tayari Mkurugenzi na Meneja wa Vipindi wamesimamishwa kazi leo tarehe 15 Februari 2016 na watumishi wengine watachukuliwa hatua kufuatia agizo la Mhe. Waziri wa Habari kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC alilolitoa leo wakati akitangaza kuwasimamisha kazi viongozi hao.

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola akizungumza  katika mkutano wa kazi na viongozi hao uliofanyika makuu ya ofisi hiyo mapema leo. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akimsikiliza kwa umakini.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akifungua mkutano wa kazi wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika makuu ya ofisi hiyo mapema leo.
  aziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wakaguzi wa kanda wa TAKUKURU mara baada ya kufungua mkutano wa kazi wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika makuu ya ofisi hiyo mapema leo.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  WAZIRI wa Nchi, Ofisi Rais Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki  amesema kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ina baadhi ya watendaji ambao wametumia nafasi zao vibaya na kufanya chombo hicho kukosa uaminifu  hivyo kukifanya  kuwa na ‘majipu’ ambayo yanatakiwa kupasuliwa.
  Mhe. Kairuki  ameyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa utendaji kazi wa Takukuru uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, amesema  chombo hicho ni muhimu lakini kuna baadhi wametumia nafasi zao vibaya katika kufanya kazi na taarifa anazo hivyo atashughulikia ikiwemo na kuandika kiapo cha mali zao na kama walifanya warudie kujiridhisha.
   Amesema kuwa Takukuru inatakiwa kufika wilayani na mikoani kutokana na fedha nyingi za miradi ya serikali zinakwenda huko ambapo ameutaja mkoa wa Kilimanjaro  unawatendaji ambao wametumia madaraka vibaya wa ubadhirifu wa fedha za serikali hivyo Takukuru lazima ichukue hatua dhidi yao.
  Amesema kuwa ikitokea kuwepo na  kutowajibika kwa chombo hicho serikali iamweza kuwandoa wote kutokana na kuwepo kwa watu wenye sifa wa kufanya kazi hiyo.
  Aliongeza kuwa katika Takukuru inatakiwa kujiridhisha na uchunguzi na  sio kuwa idadi nyingi za kesi ambazo mwisho wa siku kesi hizo wanashindwa kutokana kuushindwa  kuwa na uchunguzi wenye ushahidi.
  Aidha amesema kuwa baadhi ya mahakimu watakosa kazi kutokana na baadhi ya kesi wameendesha kwa kupindisha na kuwapa  washitakiwa haki wasio kuwa nayo.
  Waziri Angela amesemaTakukuru wafanye kazi kwa waadilifu kwa kuwalinda watoa taarifa ili waendelee kutoa taarifa kwa watu wanaojua kuwa wanahujumu nchi kwa kutumia madaraka yao.
  Amesema watumishi wa Takukuru wana masilahi mazuri kuliko wa wafanye kazi wengine ikiwa ni kuwaondoa katika ushawishi wa kuwa na tama kutokana unyeti wa chombo hicho.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishina (CP), Valentino Mlowola amesema wameokoa sh. Bilioni Saba (7) ambazo zilikuwa ziingie kwenye mifuko ya wabadhirifu wachache ambao wanatumia nafasi zao vibaya kwa masilahi yao.
  Amesema walipokea malalamiko 4,675, uchunguzi uliokamilika wa majalada hayo ni 667, majalada yaliyokwenda kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), ni  278,   majarada yaliyorejeshwa na DPP, ni 172 kwa ajili ya  vibali vya kufungua mashitaka  na kesi mpya 314 nchini kote, na kesi zilizoshinda 132 ambao wamefungwa na wengine kulipa faini.

  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

  Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).

  Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau. 
   Vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.
  Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:

  1.      Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam. Kamishna Sirroanajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.
  2.      Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na Lojistiki. Kamishna Nyamuhangaanajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
  3.      Naibu Kamishna wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Intelijensia. Kamishna Mikomangwaanajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
  4.      Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Nsato Marijani Mssanzyaambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Mafunzo na Operesheni. Kamishna Mssanzya anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Paul Moses Chagonja aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.

  Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) katika Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimbaanajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

  Teuzi zote zinaanzia leo tarehe 15 Februari, 2016


  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dar es salaam

  15 Februari, 2016

  0 0

   Lady in Red iliyofanyika siku ya Jumamosi Februari 13, 2016 jijini London, uingereza maalum kwa siku ya wapendanao iliyoandaliwa na ClubMalibu na kufanywa na mama nguli wa mitindo Asya Idarous Khamsini huku ikinogeshwa na msanii wa Bongo Flava Rich Mavoko.
   Mlimbwende akipita mbele ya mashabiki wa mitindo jijini London kwenye onesho la Lady in Red ililofanywa na mama mitindo nguli Asya Idarous Khamsini mwenye maskani yake mji wa Houston jimbo la Texas, Onesho hilo lililohudhuriwa na mashabiki wa mitindo jijini London lilinogeshwa na msanii wa Bongo Flava Rich Mavoko.
   Walimbwende wakipita mbele ya mashabiki wa mitindo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

    Katibu Mkuu Chama cha NRA Tanzania Bara Hassan Almasi Kisabya (wa pili kushoto) akitoa tamko la chama chake kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar March 20 ya waandishi wa Habari(Hawapo Pichani)leo Jijini Dare s salaam katika ukumbi wa Habari Maelezo.
  Baaadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano ulioitishwa na Chama cha NRA kuelezea ushiriki wao katika uchaguzi wa marudio Zanzibar.
  Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO 

  Na Nyakongo Manyama MAELEZO

  Chama Cha National Reconstruction Alliance (NRA) kutoka Zanzibar kimethibitisha kushiriki uchaguzi wa marudio wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Machi 20, mwaka huu baada ya kikao kilichofanyika Februari 15.

  Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Tanzania Bara Hassan Almasi Kisabya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa Chama hicho kitashiriki uchaguzi wa marudio na kusisitiza kuwa tamko lililotolewa na mgombea wao la kutoshiriki uchaguzi wa marudio lipuuzwe kwani ni tamko lake binafsi na sio msimamo wa chama.

  “Tamko lililotolewa tarehe 14/02/2016 Si Tamko la chama cha NRA bali ni tamko binafsi na wale waliomuagiza kwani yeye hana mamlaka ya kukisemea chama wala wagombea wengine wa chama pasipo Baraka na vikao halali vya chama” alisema Kisabya.

  Amesisitiza  kuwa maamuzi ya chama ni sharti yatoke katika chama na sio kwa mgombea na ikiwa yeye amejitoa anatakiwa afuate taratibu za kisheria katika kujitoa kama alivyofuata sheria katika kugombea nafasi hiyo.

  Aidha, Chama kinatoa taarifa kwa wagombea wote Zanzibar kujiandaa na wapiga kura kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20, mwaka huu ili kutimiza haki yao kikatiba na kuchagua viongozi wao kwa kipindi cha miaka mitano ijayo

  Chama cha NRA ni miongoni mwa vyama 14 vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa  Oktoba 25 mwaka jana katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofutwa kwa nafasi ya Rais.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Kibo Mining, Louis Coetzee ( wa pili kutoka kulia) akielezea mikakati ya kampuni hiyo katika uwekezaji wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia makaa ya mawe mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( kulia) akimweleza Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Kibo Mining, Louis Coetzee (kushoto) fursa za uwekezaji nchini kwenye sekta ya umeme.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo katika kikao hicho.
  Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Kibo Mining, Louis Coetzee akifafanua jambo katika kikao hicho.

  Na Greyson Mwase, Dar es Salaam.

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amezitaka taasisi  zinazosimamia miradi ya umeme nchini  kuongeza kasi  ya utendaji kazi ili  Tanzania  iweze kupata umeme wa uhakika.
  Profesa Muhongo aliyasema hayo katika kikao chake  kilichokutanisha Kampuni ya Uchimbaji Madini  ya Kibo Mining na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo la  Taifa (NDC) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wizara ya Nishati na Madini.

  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0

   Mafundi wakiendelea na kazi ya kulaza mabomba ya Maji eneo la Mbezi Beach jijini Dar es salaam. Mabomba hayo ambayo sasa yamekamilika kwa urefu wa kilometa 54.8 kati ya 55.9 yatatumika kusafirisha maji kutoka mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
  Mkurugenzi wa Usimamizi na Ufundi wa DAWASA, Romanus Mwang’ingo (katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya Mradi wa ujenzi  wa bomba hilo la kusafirishia Maji kutoka Ruvu Chini  kuelekea matangi ya kuhifadhia maji ya Chuo Kikuu cha Ardhi ambao umefika eneo la Mbezi Beach jijini Dar es salaam
  Maneja wa Kampuni ya Gauff Consultants, Thorsten Seitz akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu maendeleo ya Mradi wa ujenzi  wa bomba hilo la kusafirishia Maji kutoka Ruvu Chini.

  ( Na. Aron Msigwa - Dar es salaam)

  Huduma ya Usambazaji wa Maji Safi katika jiji la Dar es salaam inatarajiwa kuimarika kwa kuwafikia wananchi wengi zaidi mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu kufuatia kukamilika kwa kilometa 54.8 za mradi wa Ujenzi wa Bomba kubwa la kusambazia Maji kutoka chanzo cha Maji cha Ruvu Chini.

  Mradi huo unajengwa na Kampuni ya JBG Gauff Ingenieure kwa gharama ya shilingi Bilioni 141 ambazo zimetolewa na Serikali ya Tanzania una jumla ya urefu wa kilometa 55.9. 

  Akizungumzia mradi huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Usimamizi na Ufundi wa DAWASA, Romanus Mwang’ingo amesema kuwa mpaka sasa ujenzi wa bomba hilo kuelekea matangi ya kuhifadhia maji ya Chuo Kikuu cha Ardhi umefika eneo la Mbezi Beach jijini Dar es salaam na huku ikiwa imebakiza kilometa 1.1.

   Amesema ujenzi wa mradi huo kutoka mtambo wa Ruvu Chini ndiyo utakuwa suluhisho la tatizo la maji katika jiji la Dar es Salaam na maeneo ya mkoa wa Pwani na kuongeza kuwa utakapokamilika utazalisha lita milioni 270 kwa siku kutoka lita milioni 182 ambazo zote zitasukumwa kuja jijini Dar es salaam.

   Aidha, amesema kasi ya mkandarasi ya kulaza bomba hilo inaridhisha licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazochelewesha kazi hiyo zikiwemo za ufinyu wa eneo linapojengwa bomba hilo kuwezesha mitambo kufanya kazi vizuri katika eneo la mbezi Beach, mvua zinazoendelea kunyesha ,changamoto ya makazi ya watu kuwa ndani ya mradi ambapo kulikuwa na kesi 17 Mahakamani zikihusisha madai mbalimbali ya wananchi katika maeneo hayo.

  “Ni kweli zipo changamoto zilizosababisha mradi kukawia kumalizika zikiwemo za wananchi kufungua kesi 17  Mahakama ya Ardhi, hadi sasa DAWASA tumeshinda kesi 14  ndiyo maana tumepata haki ya kutumia njia hii kukamilisha upanuzi wa mradi” Amesema Mwang’ingo.

  Ameongeza kuwa lengo la mradi huu nikuongeza uzalishaji wa maji na kuboresha huduma kwa wakazi wa maeneo ya uwekezaji (EPZ) Bagamoyo, Chasimba, Buma, Zinga, Kerege na Mpiji mkoa wa Pwani. 

  Maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huo kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni Bunju, Wazo, Salasala, Madale na Kinzudi Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani, Mikocheni, Mlalakua, Masaki, Sinza, Kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni, Kigogo na Vingunguti.

  Kwa upande wake Meneja Mradi wa Kampuni inajenga bomba hilo nchini Muhandisi Eric Omuruli akizungumzia mradi huo amesema kuwa yeye kama Meneja mradi atahakikisha anashughulikia changamoto zilizopo ili kukamilisha kwa wakati.

  Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika eneo la mradi hasa eneo la Mbezi Beach jijini Dar es salaam kampuni ya JBG Gauff Ingenieure inafanya kila linalowezekana ili mradi huo ukamilike mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.

  “Tumejipanga kufanya kazi hadi usiku kupunguza muda,kazi iliyobaki ni ndogo, tunawahakikishia DAWASA tutaimaliza kazi hii mwishoni mwa mwezi huu” Amesisitiza.

  0 0

  Katibu Mkuu Chama cha NRA Tanzania Bara Hassan Almasi Kisabya (wa pili kushoto) akitoa tamko la chama chake kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar March 20 ya waandishi wa Habari(Hawapo Pichani)leo Jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Habari Maelezo.
  Baaadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano ulioitishwa na Chama cha NRA kuelezea ushiriki wao katika uchaguzi wa marudio Zanzibar. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Chama Cha National Reconstruction Alliance (NRA) kutoka Zanzibar kimethibitisha kushiriki uchaguzi wa marudio wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Machi 20, mwaka huu baada ya kikao kilichofanyika Februari 15.

  Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Tanzania Bara Hassan Almasi Kisabya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa Chama hicho kitashiriki uchaguzi wa marudio na kusisitiza kuwa tamko lililotolewa na mgombea wao la kutoshiriki uchaguzi wa marudio lipuuzwe kwani ni tamko lake binafsi na sio msimamo wa chama.

  “Tamko lililotolewa tarehe 14/02/2016 Si Tamko la chama cha NRA bali ni tamko binafsi na wale waliomuagiza kwani yeye hana mamlaka ya kukisemea chama wala wagombea wengine wa chama pasipo Baraka na vikao halali vya chama” alisema Kisabya.

  Amesisitiza kuwa maamuzi ya chama ni sharti yatoke katika chama na sio kwa mgombea na ikiwa yeye amejitoa anatakiwa afuate taratibu za kisheria katika kujitoa kama alivyofuata sheria katika kugombea nafasi hiyo.

  Aidha, Chama kinatoa taarifa kwa wagombea wote Zanzibar kujiandaa na wapiga kura kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20, mwaka huu ili kutimiza haki yao kikatiba na kuchagua viongozi wao kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani akizungumza katika mkutano wa wadau kujadili maendeleo ya tafiti, elimu, matibabu na mafunzo kuhusu ugonjwa wa sikoseli nchini katika kipindi cha miaka 10 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Profesa Makani pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Sikoseli ni ugonjwa wa kurithi kutoka kwa wazazi wenye vinasaba vya ugonjwa huo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia) akizungumza na baadhi ya wadau walioshiriki mkutano kujadili maendeleo ya tafiti, elimu, matibabu na mafunzo kuhusu ugonjwa wa sikoseli nchini katika kipindi cha miaka 10 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
  Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani (wa pili kushoto), ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) akiwa na baadhi ya wadau walihudhuria mkutano kujadili maendeleo ya tafiti, elimu, matibabu na mafunzo kuhusu ugonjwa wa sikoseli nchini katika kipindi cha miaka 10 jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni, Prof. Japhet Killewo, mhadhiri kutoka MUHAS, Dk, Namala Mkopi, daktari bingwa wa watoto na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Watoto (PAT) na Promise Mwakale, Ofisa Uhusiano katika taasisi ya sikoseli.   


older | 1 | .... | 1125 | 1126 | (Page 1127) | 1128 | 1129 | .... | 3272 | newer