Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110006 articles
Browse latest View live

HOJA YA HAJA: Wanaoishi Jana Wanatusumbua Leo; Tutaiokoaje Kesho?

$
0
0
[​IMG]

Na. M. M. Mwanakijiji
Mojawapo ya changamoto kubwa zinazoikabili serikali ya Rais J.P. Magufuli inapozidi kujipanga kuleta mabadiliko makubwa ya kimfumo na kifikra katika kuimarisha utendaji wa utumishi wa umma kuelekea 2020 ni watendaji na viongozi ambao bado wanaishi jana wakati nchi iko leo na hivyo wanatishia hatima ya taifa letu kesho.
Jana yetu ni miaka ya nyuma ambapo watendaji waliweza kufanya lolote bila kujali sana matokeo (with impunity) na wafanyakazi walijua watendaji wao walikuwa "hivi na vile" kiasi kwamba watumishi wa chini nao baadhi yao walianza kufanya mambo bila kujali matokeo. Mtu alipopata nafasi ya ajira au kupandishwa cheo fikra za kwanza ambazo inaonekana watu walikuwa nazo ni vipi katika nafasi hizo watachuma kwa haraka haraka kabla mambo hayajabadilika.
Taratibu za ajira na utendaji kazi zilifuatwa kama vile ni jambo la hiari (optional) kiasi kwamba ulazima wa kusimamia sheria na taratibu ulionekana ni usumbufu mkubwa. Mwananchi alipoamua kwenda kupata huduma fulani kwenye taasisi ya serikali ni lazima afikirie mara mbili na kujiandaa kiakili (pyschologically) na usumbufu wowote ambao ataupata. Mwingine inabidi aulize kwanza kama kuna mtu yeyote anayemfahamu huku au kama anafahamu mtu anayeweza kuwa anafahamiana na mtu mwingine huko anakotaka kwenda. Sehemu nyingine katika kutafuta mtu wa kufahamiana naye mtu aliweza kwenda hata kipeo cha tatu na cha nne cha marafiki. Akipatikana anayejuana na fulani huko basi mtu anaweza kua na imani kuwa anaweza angalau kusikilizwa; akikosekana bajeti ya kulainisha mifumo inabidi ifikiriwe tena.
Maisha haya ya jana yamejionesha kwa kiasi kikubwa katika utendaji wa uzembe na usiojali fedha za wnaanchi kama ambavyo ripoti mbalimbali za CAG zimekuwa zikituonesha tangu 2006. Hii jana watu walikuwa wameizoea kiasi kwamba leo haikuruhusiwa ifike kamwe; watu waliipenda jana sana kiasi kwamba hata wakati wa kampeni za uchaguzi bado lilikuwepo kundi la watu ambao waliitamani leo lakini hawakuwa tayari kuiachilia jana.

Matukio karibu matatu yaliyotokea Alhamisi iliyopita yametudokeza kuwa bado tuna tatizo la watu wanaoishi jana. 


Muhimbli ilitarajiwa uongozi mpya kuanza kuondoa kero ambazo si za lazima; hii siyo tu uongozi wa Muhimbili bali pia Wizara ya Afya; lakini inaonekana mazoea magumu. Bado watu wamekutwa tena wamejazana wodini kama vile wako kwenye behewa la Daraja la tatu wakielekea Bara. Hivi kweli bado hakuna mtu mwenye akili za 'kawaida' tu kuwa watu wanaohitaji huduma safi, salama na mazingira mazuri kabisa ya tiba ni kina mama na watoto - kwa sababu ya udhaifu (vulnerability) yao? Kama watu hawa wanashindwa kuliweka hili kama ajenda yao nambari 1 hivi huko kwingine watapanga nini? Kama inabidi kufuta posho na mishahara ya viongozi wote ili kina mama na watoto wetu wapatiwe huduma sahihi na bora basi na liwe hivyo; lakini hili halieleweki?

Kabla hatujatulia Mhe. Mwigulu Nchemba naye kazukia huko Pugu (kwa mara nyingine) kufuatilia machinjio. Akakuta kati ya ng'ombe 200 waliokuwa wanaenda kuchinjwa (au sijui wameshachinjwa) ni 20 ambao walikuwa na vibali; huku wale wengine wote kama wamelipiwa basi wamelipiwa kwenye mifuko ya mtu na labda kwa kiasi cha chini kidogo na hivyo kuikosesha serikali mapato; na hilo ni siku moja tu! Hawa watu wa machinjioni walikuwa wanaamini basi ile ya kwanza ni nguvu ya soda basi wacha waendelee kama ilivyokuwa (status quo was maintained). Hawakuwa tayari kuamini kuwa mtu atarudi tena na inawezekana hata watakaoingia bado watafikiria Mwigulu hatawazukia tena na hivyo wataanza na wao kutafuta 'mitkasi' ya hapa na pale. Warudi jana.

Na kabla hata hatujatulia Waziri Mkuu Kassim "Tabasamu" Majaliwa (nimempa jina la 'tasabamu' kwa sababu tabasamu lake linadanganya watu) karudi tena Bandari ambako nako akakuta madudu mengine yale yale na tena safari hii ikitisha zaidi. Kwamba, mpango wake wa kwenda huko kwa kushtukizwa baada ya kutoshwa na watumishi safi ukatibuliwa na 'mmbeya' mmoja kiongozi wa juu tu ambaye aliamua kuwadokeza na hivyo kutaka kusaidia kuficha madudu huko.
Nakubaliana na wengine wote kuwa Kiongozi  huyo akithibitika kweli ametuma ujumbe wa kumtonya mama Chuwa ili ajaribu kuvuruga ushahidi basi Magufuli hana jinsi; ni lazima amuondoe bila kujali uwezo wake, ujiko wake, au sifa zake. Serikali hii haipaswi na haitakiwi hata kuuliza "mwenzetu ilikuwaje ukavuruga mipango ya waziri Mkuu". Hii ni hujuma ya ndani (internal sabotage). Tena hili inapaswa lifanyiwe kazi mapema sana ili kuleta heshima na woga kwa viongozi wengine. Magufuli akipepesa macho tu na kujikwaa tu atajitengenezea udhaifu usio wa lazima.

Nina uhakika wapo viongozi wengine na watumishi wengine ambao bado na wenyewe wanaombea kuwa safishasafisha hii haitowafikia na kwamba, hizi zote zilikuwa nguvu za soda. Siku 100 baadaye nguvu za soda bado zinachemka na kama tulisikia dokezo kidogo Bandari ni moja tu ambako kunahitaji kusafishwa ili safisha hii iendelee maeneo mengine. Hawa wa sehemu nyingine kama wana akili timamu wanapaswa ama kuanza kujiondoa wenyewe au wasubiri shoka la Magufuli liwekwe kwenye mashina yao!
Jana imepita; waliotumikia fikra za wa jana wajue kuwa siku mpya imefika. Hili nililisema mwanzoni lakini bado watu hawaamini kuwa kuna siku mpya. Hawaamini kuwa kiongozi huyu siyo yule na fikra zinazomuongoza siyo zile. Waliozoea kubebana, kufichiana na kusaidiana kufika hujuma, rushwa, magendo na hujuma za kila namna wakati wao uliishia jana.

Ni lazima washughulikiwe leo kama tunataka kesho iliyo bora; kama tunataka watoto wetu na vijana wetu wanafikiria kutumikia umma kuwa na misingi mizuri, ni lazima uchafu wa jana usafishwe. Usafishwe na kila mtu ajue kuwa tunahitaji utumishi wa umma ulio msafi na ambao uchafu kidogo tu ukitokea hauchelewi kushughulikiwa. Na katika kushughulikia ni lazima tuwatoe mfano wale wenzetu wote ambao tulidhani wanaijua leo lakini bado kifikra wametiwa pingu za jana na bado hawajaziachilia; kwani hawa ni hatari kwa kesho yetu na ya keshokutwa ya watoto wetu na mtondogoo wa watoto wa watoto wetu.
Siku mia zimepita lakini siku mamia bado zinakuja. Mwendo wa kurudisha heshima katika utumishi wa umma na weledi wa watumishi unapaswa kuongeza kasi. Mpaka Watanzania tuheshimiane na tuheshimu utumishi wa umma.
Hadi hivi sasa hakuna majuto.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA FEBRUARI 12, 2016

SHEIKH GHALIB MONERO NA UJENZI WA MSIKITI NA KITUO CHA WATOTO MKURANGA

$
0
0
Alhamdullilah tunaendelea vyema na Project yetu No 2 , tunamshukuru M/Mungu katika Majengo yetu Matatu. Tumeweza malizia Jengo la Msikiti , Madrasa na fremu kama mnavyo ona katika picha .

Kwa uwezo wa Mungu na kwa kuunga Mkono kwenu ki Michango ya hali na mali tunaingia katika hatua nyengine mpya ya kuandaa maandilizi ya masomo na mazingira bora la kupokea vijana, Kituo chetu tutasomesha hasa vijana ambao wapo katika Mazingira magumu na wale wanaoishi vijijini ambao wamekosa fursa ya elimu. Tunawakaribisha katika kushiriki kukamilisha jambo letu hili katika hatua hii muhimu.

Ombi letu kwenu:
1.Magodoro Madogo - tayari yamepatikana ya kuanzia.

2.Neti za Mbu , shuka , mito n.k

3.Vyombo vya kupikia na vyombo muhimu vya kutunzia maji .

4.Vyakula  vya Nafaka kwa mwanzo wa safari.

5.Fenicha za ofisi yetu , Computer na vifaa muhimu ambavyo tunaweza vitumia katika Project yetu.

Tunawakaribisha mtembelee kituo chetu kwa atakae kuwa na nafasi .

Michango zaidi tunayo ihitaji ni ya ki  UJENZI (Vifaa)hasa CEMENT kwani baada ya kukamilika yote tuliyo yataja juu kutakuwa na zoezi la kuzungusha uzio na  Alhamdulillah tofali 10,000 zipo site Mapungufu yetu ni Cement na Gharama za Mafundi. Kwa yeyote aliye tayari katika kheir hii Tafadhali .

Mawasiliano 0673800772 (Tigo Pesa)
0715800772 (Tigo -Pesa)

0689604780 (Airtel - Money)
Namba zote Usajiri jina GHALIB MONERO.

Kwa walio nje waweza tuma Mchango wakupitia Western Union .

RECIVER NAME :- GHALIB NASSOR MONERO.

Waweza tembelea facebook kwa Updates zaidi :-  Kijana wa Kiislam Dsm.

NAWASHUKURU MUNGU AWALIPE KHEIR NA MRATIBU MSIMAMIZI . GHALIB NASSOR MONERO.
 MSIKITI KWA MBELE
JENGO LA OFISI ZA KITUO
 Madrasa kwa muonekano wa mbele

 JENGO LA MSIKITI KATIKA HATUA ZA MWISHO KUMALIZIKA
NDANI YA MSIKITI

SHOP FOR LEASE AT SAMORA TOWERS ALONG SAMORA AVENUE IN DAR ES SALAAM

$
0
0

👉🏿50 TO 70 SQMTS
👉🏿SAMORA AVENUE
👉🏿IDEAL FOR JWELLERS AIRLINES,MOBILE &ACCESSORIES,PHARMACY,OPTICS AND MORE
👉🏿CALL OR SMS +255 784 786 455
FOR VIEWING AND F
 SAMORA TOWERS ALONG SAMORA AVENUE IN DAR ES SALAAM
URTHER DETAILS

Article 19

MASHINDANO YA NGUMI YA TAIFA YAFANYIKA TANGANYIKA PACKERS

$
0
0
Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare katikati akimkabidhi Kocha wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' mchango uliotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya rambirambi ya kifo cha marehemu Mohamed Chibumbuli kilichotokea jana Mkoa wa Mtwara Wilaya ya Masasi. kushoto ni katibu Mkuu wa shirikisho hilo Makole Mashaga.
Bondia Selemani Kidunda kushoto akimshambulia Mustafa Mtoro wakati wa mashindano ya taifa yaliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam. Kidunda alishinda kwa K.O ya raundi ya kwanza.

Msanii wa filamu, Shamsa Ford  kushoto akipambana na Mtangazaji wa Radio TIMES FM, KHADIJA SHAIBU "DIDA' wakati wa mashindano ya taifa ambapo wao walioneshana umwamba

Msanii wa filamu, Shamsa Ford  kushoto  na MTANGAZAJI WA TIMES FM,KHADIJA SHAIBU "DIDA' wakinyooshwa mikono juu baada ya mpambano wao wakati wa mashindano ya taifa ambapo wao walionesha umwamba katika mechi ya kirafiki.

Kero za wananchi wanaozunguka mgodi wa Acacia North Mara kutathminiwa kwa siku 30

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika kikao na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Mkuu wa wilaya Tarime na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (wa pili kushoto) kilicholenga kutatua kero wanazokumbana nazo wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia NorthMara pamoja na Mgodi husika. Kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga. Wa kwanza kulia Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi, Mhandisi Juma Sementa, Wa pili kulia ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje na Wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Leseni,John Nayopa.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (kushoto) wakijadiliana jambo mara baada ya kumaliza kikao kilicholenga kutatua kero za wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia NorthMara pamoja na Mgodi husika.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kulia) akitembelea maeneo yanayolalamikiwa na wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia NorthMara wakati alipofanya ziara ya kikazi wilayani Tarime. Kulia kwa Waziri ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, na kulia kwa Mbunge ni Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Nyakungulu wilayani Tarime ambaye alikuwa akiwasilisha kero za wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara wakati Profesa Muhongo alipofanya ziara ya kikazi wilayani Tarime.

MWENYEKITI WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA AFANYA ZIARA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

$
0
0
Februari 12, 2016), Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga akiambatana na baadhi ya viongozi wa Tume hiyo ametembelea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wake, Mhe. Jaji (Mstaafu), Damian Lubuva kuhusu uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.

Katika ziara hiyo, Mhe. Nyanduga alipata fursa pia ya kumweleza Mhe. Lubuva kuhusu uangalizi uliofanywa na Tume katika uchaguzi huo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Lindi na Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Mstaafu), Damian Lubuva akieleza jambo mbele ya ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (hauko pichani), ujumbe huo ulipoitembelea ofisi yake jana (Februari 12, 2016).
Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Bahame Tom Nyanduga na Katibu Mtendaji wa Tume, Bibi Mary Massay wakimsikiliza kwa makini Mhe. Jaji (Mstaafu) Lubuva.
Mhe. Jaji (Mstaafu) Lubuva akimsikiliza Mhe. Nyanduga (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo yao.
Mhe. Bahame Tom Nyanduga na Mhe. Jaji (Mstaafu), Damian Lubuva wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Tume, Mhe. Dkt. Kelvin Mandopi na Bibi Mary Massay.
Mhe. Bahame Tom Nyanduga na Mhe. Jaji (Mstaafu), Damian Lubuva wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa THBUB na baadhi ya maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
(Picha zote na Germanus Joseph wa THBUB).

DAWASCO YAJIVUNIA SIKU 100 ZA RAIS MAGUFULI MADARAKANI

$
0
0
Na Joseph Mkonyi -DAWASCO

Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), imesema imeweza kutekeleza mipango na maagizo mbalimbali yaliyotolewa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli, hivyo kuwezesha kupunguza kero na kuboresha huduma ya Majisafi na uboreshwaji wa Majitaka Jijini Dar es Salaam ndani ya siku 100 tangu Rais Dkt Magufuli aingie madarakani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio yaliyopatikana ndani ya siku 100 za utawala  wa  Rais Magufuli, Afisa mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja ametaja mambo yaliyofanikiwa ni pamoja na Kufungua njia za Maji zilizofungwa kutokana uchakavu wa miundo mbinu , Kuzuia mivujo mikubwa na midogo ,kuunganishia wateja wapya huduma ya Maji, ufufuaji wa Mita kuu (Bulk meters), uboreshaji  wa mfumo wa malipo ,uboreshaji wa migao ya Maji pamoja na uboreshaji wa huduma kwa wateja.

“Shirika limeweza kupeleka Maji katika maeneo mengi zaidi ya jiji la Dar es Salaam ambayo hayakuwahi kupata Maji au huduma ilisitishwa kwa sababu ya uchakavu wa miundo mbinu. Katika Kipindi hiki cha Mh.Rais Dkt John Pombe Magufuli, jumla ya maeneo 52 yameweza kupata Maji kwenye wilaya zote tatu za Kinondoni, Ilala na Temeke mfano maeneo ya Temeke sokota, Kimara B, na Buguruni mnyamani na mengine mengi maana Rais aliagiza tumtue Mama ndoo kichwani”.

“Pia tumeendelea kutekeleza agizo la kufikisha wateja milioni 1 ifikapo juni 2016 hivyo tumeanza kuunganisha wateja wapya na mpaka sasa tumeweza kuunganisha wateja 3500, lakini mradi wa Ruvu chini unatarajia kuisha Februari 2016 mwishoni na kuongeza upatikanaji wa Maji toka lita za ujazo 300milioni mpaka lita 450 milioni hivyo sehemu ambazo hawajafikiwa na huduma ya Maji wataweza kufikiwa”.

“kwa upande wa miradi kwa siku 100 za Mh Raisi Kuna miradi miwili imeshakamilika ambapo ni Mradi wa Kibamba shule uliopo kibamba ambapo unahudumia wananchi takribani  na Mbweni teta uliopo wilaya ya kinondoni ambao nao unahudumia wananchi takribani….

Pia tumeweza kupunguza upotevu wa Maji( Non Revenue Water) kutoka asilimia 57 mwanzoni mwa mwezi September 2015 mpaka asilimia 42 kwa mwezi January 2016 na juhudi zinaendelea kupambana na upotevu wa Maji ili tufikie lengo la chini ya asilimia 20 ifikapo 2018.

 “Tumeweza kuwabaini watumiaji maji 1250 walio nje ya utaratibu (informal Water users) ambao ni watengeneza bustani, watengeneza matofali, hotel na lodge ambazo walikuwa hawalipii huduma ya Maji na kuzisajili rasmi na sasa wana mita kabisa na wanalipia huduma ya Maji kila mwezi hivyo kuongeza Mapato ya Shirika” aliongeza Mhandisi Luhemeja wamekamatwa waliokuwa wanatumia Maji kiholela bila kuunganishiwa na Dawasco”.

“Makusanyo yameongezeka ndani ya siku 100 Shirika limeweza kuongeza mapato yake kutoka bilioni 4 mpaka bilioni 7 kwa mwezi  pia tumeboresha kitengo cha huduma kwa wateja na hivi sasa kinafanya kazi kwa muda wa masaa 24 na hivyo kutoa nafasi kubwa kwa mteja kupata huduma muda wowote anapo pata tatizo au msaada” . Alisema  Mhandisi Cyprian Luhemeja.

UTT PROMOTED COMPANIES HOLD FIRST ANNUAL GENERAL MEETING IN DAR ES SALAAM

$
0
0

Chief Executive Officer, (CEO), with UTT-Project and Infrastructure Development PLC, Dr.Gration Kamugisha, (First-R), speaks during a joint news conference prior to the first annual general meeting of UTT promoted companies at Julius Nyerere International Convention Centre in Dar es Salaam Saturday February 14, 2016. Other sister companies include UTT-AMIS, and UTT-Microfinance. Others from left to right is UTT Microfinance’s CEO James Washima, UTT-AMIS’ CEO, Dr. Hamis Kibola, ane Finance Management Officer from the Office of Treasury Registrar, Edgar Rugaimukamu. (Photos:K-VIS MEDIA/Khalfan Said)


Chief Executive Officer with UTT-AMIS, Dr. Hamis Kibola, display the reports of UTT-PID, and UTT-Microfinance, during a joint news conference prior to the first annual general meeting of UTT-Promoted companies at Julius Nyerere International Convention Centre in Dar es Salaam, Saturday February 14, 2016
UTT-PID's Acting Board Chairperson, Elipina Mlaki, walks through the meeting agenda
 Participant reads UTT-PID's  annual report for the year ended 30th June 2014.
 A cross section of participants. For more CLICK HERE

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majliwa afunga mafunzo ya pili ya watendaji wakuu waandamizi na wakuu wa kiraia na kijeshi kwenye Chuo cha Kijeshi Kunduchi jijini Dar es salaam

$
0
0
 Waziri Mkuu Mhe Kassim Majliwa akizungumza wakati alipofunga mafunzo ya pili ya watendaji  wakuu waandamizi  na wakuu wa kiraia na kijeshi kwenye Chuo cha Kijeshi Kunduchi jijini Dar es salaam Februari 12, 2016. 
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majliwa akizungumza wakati alipofunga mafunzo ya pili ya watendaji  wakuu waandamizi  na wakuu wa kiraia na kijeshi kwenye Chuo cha Kijeshi Kunduchi jijini Dar es salaam Februari 12, 2016. 
 Washiriki wa  mafunzo ya pili ya watendaji  wakuu waandamizi  na wakuu wa kiraia na kijeshi wakGimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majliwa wakati alipofunga mafunzo hayo kwenye Chuo cha Kijeshi Kunduchi jijini Dar es salaam Februari 12, 2016.
Waziri Mkuu Mhe. Kasim Majliwa akiwa katika picha ya pamoja na  washiriki wa mafunzo ya pili ya watendaji  wakuu waandamizi  na wakuu wa kiraia na kijeshi  baada ya kufunga mafunzo hayo  kwenye Chuo cha Kijeshi Kunduchi jijini Dar es salaam Februari 12, 2016. 
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

MUONEKANO WA KITUO KIPYA CHA KUSUKUMA MAJI RUVU DARAJANI KIKIWA KIMEKAMILIKA

$
0
0
IMG-20160213-WA0000IMG-20160213-WA0001IMG-20160213-WA0002Muonekano wa kituo kipya cha kusukuma maji kilichopo eneo la Ruvu Darajani kikiwa kimekamilika ambapo kitakuwa kinasukuma maji kwenda katika mtambo wa Ruvu Juu.
Pampu moja ya kituo hicho inauwezo wa kusukuma maji lita milion 60 kwa siku kuna jumla ya pampu mpya tatu na pampu mbili zitakuwa zinafanya kazi kwa wakati mmoja.

Article 11

FAHAMU JINSI RADIOTHERAPIA INAVYOWEZA KUOKOA MAISHA YAO

$
0
0
Dk. Mahadev, mshauri mwandamizi wa 
radiotherapia kutoka Hospitali za Apollo.

Matibabu ya kawaida ya saratani huwa yanahusisha upasuaji, radiotherapia na kemotherapia. Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa kwenye tiba kwa njia hizo mbili. Katika hatua za mwanzo, saratani huwa ni ugonjwa unaotibika kwa dozi moja mahususi lakini saratani iliyosambaa au kukomaa inahitaji dozi zaidi ya moja katika kuitibu. Radiotherapia, ni tiba iliyopo katika mfumo maalumu unaoleta matokeo katika mwili mzima.
Dk. Mahadev , mshauri mwandamizi wa tiba ya uvimbe kwa mionzi kutoka hospitali za Apollo anaeleza kwamba radiotherapia inahusisha chembe chembe ndogo za mionzi ya gamma au X-rays katika kutibu saratani na hata matatizo ambayo sio ya saratani pia. Mionzi hii imegawanyika katika ile mionzi ya mbali (external radiotherapy) ambayo chanzo cha mionzi kinakuwa mbali na mwili na ile mionzi ya karibu ambayo mionzi inawekwa karibu ili kuchoma sehemu yenye uvimbe peke yake.

MABONDIA MKOA WA RUVUMA - Mh. NAPE MOSES NNAUYE TUTUMBULIE JIPU CHAMA CHA NGUMI MKOA WA RUVUMA


MICHUZI TV: KIBUDA MTAANI - MAHAKAMA YA NDIZI MABIBO, DAR ES SALAAM

MAMA WA MITINDO ASYA IDAROUS KHAMSIN AFANYIWA MAHOJIANO BBC LONDON, LADY IN RED, RICH MAVOKO LEO PATAKUA HAPATOSHI

$
0
0

Mtangazaji idhaa ya Kiswahili BBC London Maryam akimfanyia mahajiano nguli wa mitindo Bi. Asya Idarous Khamsin jijini London siku ya Ijumaa Februari 12, 2016 mahojiano maalum kwa ajili ya Lady in Red itakayofanyika leo Jumamosi Februari 13, 2016 mjini humo. Onyesho hilo litakalo washirikisha wasanii mbalimbali wakiongozwa na msanii wa Bongo Flava Rich Mavoko litakua ni sehemu ya kusherehekea siku ya wapendanao ambayo mwaka huu imeangukia siku ya Jumapili.
 Kulia ni ClubMalibu ambaye ndiye mwenyeji na mdhamini wa Lady in Red itakayofanyika leo jijini London akiwa katika picha ya pamoja na mtangazaji mahiri wa idhaa ya Kiswahili BBC London Bwn. Salim Kikeke.
Kutoka kushoto ni msanii wa Bongo Flava Rich Mavoko, Mgalula Fundikila, Salim Kikeke na mama wa mitindo Asya Idarous Khamsini walipokua mjengoni idhaa ya Kiswahili BBC London.
 Mtangazaji wa idhaa ya Kiswahili BBC London Sakuma Kssim akiwa katika picha ya pamoja na nguli wa mitindo Bi. Asya Idarous Khamsin wakati mwanamitindo huyo alipokua mjengoni huko kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano.
 Kutoka kushoto ni Saluma Kassim, Maryam, Aisha Yahya wakiwa katika picha ya pamoja mama nguli wa mitindo Asya Idarous Khamsini.

YANGA SC YASHINDA 1-0 MAURITIUS

$
0
0

Na Princes Akbar, CUREPIPE

BAO pekee la mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma limeipa mwanzo mzuri Yanga SC katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuwafunga wenyeji Cercle de Joachim 1-0 mchana wa leo Uwanja wa Curepipe mjini Curepipe, Mauritius.
Kwa ushindi huo, Yanga SC sasa watakuwa na kazi nyepesi katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo mjini Dar es Salaam, wakihitaji hata sare ili kusonga mbele, ambako watakutana na mshindi kati ya APR ya Rwanda na Mbabane Swallows ya Swaziland.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa wa Madagascar, Hubert Marie Bruno Andriamiharisoa, Randrianarivelo Ravonirina Harizo na Augustin Gabriel Herinirina, Ngoma alifunga bao hilo dakika ya 17 tu akimalizia krosi maridadi ya beki wa kulia, Juma Abdul Jaffar. 

Kikosi cha Yanga SC kilichoilaza 1-0 Cercle de Joachim leo.
Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry



Yanga SC ilipata pigo kipindi cha pili, baada ya mpishi wa bao lake, Juma Abdul Jaffar kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Pato Ngonyani, aliyemalizia vizuri. 
Baada ya mchezo huo, Yanga SC inatarajiwa kupanda ndege ya ATC waliyokwenda nayo huko, kuelekea kisiwani Pemba kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu, Simba SC Jumamosi wiki ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Ally Mustafa 'Barthez', Juma Abdul/Pato Ngonyani dk70, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe/Paul Nonga dk68 na Deus Kaseke.
Kikosi kamili cha Yanga kinachokwenda kambini Pemba ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benedicto Tinocco.
Mabeki; Juma Abdul, Mbuyu Twite (DRC), Oscar Joshua, Mwinyi Hajji Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Vincent Bossou (Togo) na Pato Ngonyani.
Viungo ni; Said Juma ‘Makapu’, Salum Telela, Thabani Kamusoko (Zimbabwe), Haruna Niyonzima (Rwanda), Simon Msuva, Issoufou Boubacar (Niger), Godfrey Mwashiuya na Deus Kaseke.
Washambuliaji ni; Malimi Busungu, Paul Nonga, Amissi Tambwe (Burundi) na Donald Ngoma (Zimbabwe).
BENCHI LA UFUNDI; Kocha Mkuu; Hans van der Pluijm (Uholanzi), Kocha Msaidizi; Juma Mwambusi, Kocha wa Makipa; Juma Pondamali
Daktari; Nassor Matuzya, Meneja; Hafidh Saleh, Mchua Misuli; Jacob Onyango na Mtunza Vifaa; Mohammed Mpogolo.

Article 5

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi bin Ally aruhusiwa kutoka hospitali baada ya afya yake kuimarika

$
0
0
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi bin Ally leo ameruhusiwa kutoka katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Muhimbili ambako alikuwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji. 
Sheikh Abubakar ameishukuru Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na taasisi hiyo kwa kumpatia huduma nzuri za matibabu na kwamba afya yake hivi sasa imeimarika. Pia, amemshukuru Rais John Pombe Magufuli, Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwa kufuatilia afya yake kwa karibu, viongozi mbalimbali na watu wengine waliofika kumjulia hali hospitalini hapo. 
“Siwezi kuwasahau madaktari walionipatia matibabu akiwamo Dk Mwanga, Dk Juma Mfinanga ambaye ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya moyo, Profesa Mohamed Janabi na wauguzi kwa kunipatia matibabu mazuri,” amesema Sheikh Abubakar wakati akizungumza katika hospitali hiyo. 
Katika hatua nyingine, Sheikh Abubakar amemuomba Rais Magufuli kuwatazama madaktari wa hospitali hiyo na kuwaongezea vitendea kazi zaidi ili waendelee kutoa huduma bora za matibabu kwa wagonjwa. 
“Mwanzo nilikuwa siiamini hospitali hii kama ingeliweza kunipatia matibabu bora, lakini madaktari walinihakikishia watanitibu vizuri na kweli sasa afya yangu imeimarika. Kumbe tunaweza kutibiwa vizuri katika hospitali zetu za hapa nyumbani. 
"Kwa kuwa nilikuwa siiamini hospitali zetu mpaka leo nina tiketi ya ndege ambayo nilikuwa nimekata ili nikatibiwe nje ya nchi, lakini baada ya matibabu nimepata imani na hospitali zetu na kumbe Watanzania wanaweza kutibiwa hapa nyumbani badala ya kwenda nje ya nchi", alisema.
Naye Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kwamba serikali itaendelea kufuatilia afya ya sheikh huyo baada ya kuruhusiwa kurejea nyumbani. “Napenda kuwaahidi kwamba tutaendelea kufuatilia afya ya Sheikh Abubakar lengo kubwa ni kuhakikisha kwamba mambo yanakwenda vizuri,” amesema Ummy Mwalimu. 
Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akimualika Mufti Mkuu Sheikh Abubakar Zuberi bin Ally kuongea na wanahabari katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya madaktari kumruhusu kurejea nyumbani baada ya afya yake kuimarika.
Mufti Mkuu Sheikh Abubakar Zuberi bin Ally akizungumza na waandishi wa habari leo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya madaktari kumruhusu kurejea nyumbani baada ya afya yake kuimarika.

Masheikh wakiwashukuru madaktari bingwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya madaktari kumruhusu Mufti Mkuu Sheikh Abubakar Zuberi bin Allykurejea nyumbani baada ya afya yake kuimarika.
Viewing all 110006 articles
Browse latest View live




Latest Images