Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1122 | 1123 | (Page 1124) | 1125 | 1126 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mnamo Mei mwaka huu, shirika la ndege la la Etihad linategemea kufungua sehemu mpya ya mapumziko katika stesheni ya tatu ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi kwa ajili ya wageni wake wa “Daraja la Kwanza”, wasafiri wenye kadi maalum za Platinum za Etihad, wasafiri wenye kadi maalum za Platinum kutoka washirika wa Etihad na wale watakaotumia huduma ya “Makazi” iliyopo katika ndege zake aina ya Airbus A380. Etihad imewekeza sana katika kutimiza lengo hili kwa ajili ya wageni wake wa hadhi ya juu wanaopenda huduma zenye viwango bora zaidi.

  Peter Baumgartner, Afisa Mkuu wa Biashara, alisema: “Huduma hii itakuwa kito katika taji letu hapa Abu Dhabi, ni nafasi nzuri kuonesha umahiri wetu kwenye ubunifu na uvumbuzi. Ni muhimu kwetu kuhakikisha msafiri anapata huduma bora kwanzia uwanjani hadi angani mpaka anaposhuka. Tuna imani huduma na bidhaa tutakazotoa nje ya ndege zitajizolea umaarufu kama za ndani ya ndege na tunategemea wateja watafurahia yote tunayowaandalia.”

  Sehemu hii ya mapumziko itapambwa kwa mtindo wa Kiarabu na itaendana na umaridadi na umahiri uliozoeleka na kuhusishwa na jina la Etihad. Sehemu hii itaonesha uzoefu na ustadi wa Etihad na jinsi walivyojikita katika kuleta huduma yenye ukamilifu, kuanzia angani hadi ardhini.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga akiwatambulisha watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akisisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akiagana na viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mara baada ya kumaliza ziara ya kikazi aliyoifanya Makao Makuu ya TASAF mapema leo. 

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) ameuagiza Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili kusaidia jitihada za serikali za kuwaondolea wananchi kero ya umaskini.

  Mhe. Kairuki amesema TASAF inayo dhima kubwa ya kuhakikisha kuwa huduma inazozitoa kwa wananchi zinakwenda sambamba na misingi ya uadilifu na utawala bora ili hadhi ya mfuko huo iendelee kuwa kubwa. 

  Waziri Kairuki ameyasema hayo alipotembelea Makao Makuu ya TASAF jijini Dar es salaam ambako alizungumza na watumishi wa mfuko huo ikiwa ni mwendelezo wa ziara za kikazi katika taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora ambayo amepewa dhamana ya kuisimamia baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John P. Magufuli.

  “Ninawasisitiza muhakikishe kuwa, walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wananufaika vilivyo na fedha zinazotolewa ili hatimaye waweze kuondokana na umaskini” alisema Kairuki.

  Aidha, Mhe. Kairuki ameuagiza uongozi wa TASAF kuweka utaratibu utakaowezesha ukaguzi wa mara kwa mara wa walengwa wa Mpango huo nchini kote ili kuhakikisha kuwa watu wasiostahili wanaondolewa kwenye utaratibu wa ruzuku na kupunguza malalamiko yasiyokuwa ya lazima.

  Mhe. Kairuki ameonya vikali dhidi ya uwezekano wa kuweko matumizi mabaya ya fedha kwa kutoa ruzuku kwa watu wenye uwezo jambo ambalo amesema halipaswi kufumbiwa macho na pale itakapobainika wahusika wachukuliwe hatua za kuwaondoa kwenye Mpango na kisha kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

  Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki ameuagiza uongozi wa TASAF kutoa mapendekezo ndani ya siku 30 ya namna ya kukabiliana na malalamiko yanayoelekezwa kwa watendaji wa ngazi za vijiji,kata,na hata wilaya ambao wamekiuka taratibu za kuwabaini na kuwaorodhesha walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini ili hatua zichukuliwe haraka iwezekanavyo.

  Awali akitoa maelezo kwa Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga amesema Mfuko umefanikiwa kuandikisha zaidi ya walengwa Milioni 1.1 ambao wanaendelea kupata ruzuku na kuwa hadi kufikia mwezi Januari 2016 zaidi ya shilingi Bilioni 204 zimetolewa kwa walengwa ambapo matokeo chanya yameanza kuonekana hususani katika Nyanja za elimu, afya na makazi.

  Bwana Mwamanga amesema licha ya changamoto zilizopo hususani katika upatikanaye wa fedha za kukidhi idadi kubwa ya walengwa ,Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF )umeendelea kufanya juhudi za kutafuta fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo na kuiomba serikali kuona namna inavyoweza kuunga jitihada hizo ili hatimaye vita dhidi ya umaskini iweze kufanikiwa .

  Kuhusu Mpango wa kunusuru kaya maskini, Bw. Mwamanga amesema walengwa wa Mpango huu wamehamasika kwa kiwango kikubwa huku wengi wao wakionyesha uwezo katika kufuata masharti na taratibu za Mpango hivyo suala la upatikanaji wa fedha kwa uhakika lina umuhimu mkubwa ili kutowavunja moyo walengwa hao.

  0 0

  Na Nizar Visram 

  HATIMAYE mazungumzo ya amani kuhusu Syria yaliyokuwa yakifanyika jijini Geneva yamesitishwa bila mafanikio. Msuluhishi kutoka Umoja wa Mataifa (UN), Bw Staffan de Mistura kuanzia tarehe 31 Januari mwaka huu alikutana na pande zinazopigana – upande wa serikali ya Rais Bashar Assad na upande wa waasi kutoka makundi mbalimbali. 

  Kulikuwepo na waasi waliounda kile walichokiita kamati kuu ya mazungumzo (High Negotiations Committee - HNC) inayoungwa mkono na Saudia. Kamati hii inaongozwa na Riad Hijab. Wao walimwambia Mistura kuwa hawatashiriki mazungumzo mpaka serikali ya Syria itakapositisha mabomu yake na kuruhusu misaada ifikishwe kwa “raia waliokuwa wamezingirwa na majeshi ya Syria” 

  Kikundi cha Wakurdi wa Syria walizuiliwa na Uturuki kwa sababu inawahesabu kama magaidi. Wakurdi hawa wana nia ya baadae kuungana na Wakurdi wenzao walioko Iraq na Uturuki ili kuunda taifa lao la Kurdistan. Hii ndio sababu ya kimsingi kuchukiwa na utawala wa Uturuki

  Upande wa serikali uliongozwa na Balozi al-Jaafari ukajibu kwa kusema hilo halina tatizo, kwani pande zote zinapaswa zikubaliane  kama raia wa Syria. Jaafari ni balozi wa Syria huko UN. Yeye alisema Mistura ameshindwa kutoa orodha ya wapinzani watakaoshiriki katika mazungumzo. Hivyo kuna uwezekano mazungumzo haya yakashidikana kama ilivyokuwa wakati wa mazungumzo ya mwaka 2014
  Mazungumzo yalichelewa kuanza kutokana na mgawanyiko miongoni mwa wapinzani wa rais Bashar al-Assad.  Bw Mistura alishinikizwa na Marekani pamoja na Saudia, Uturuki na Qatar ambao walilazimisha kuwa HNC peke yao watambuliwe badala ya kuwaachia Wasyria wajiamulie wenyewe. Hii HNC iliundwa na utawala wa Saudia ili kuwakilisha wapinzani wote wa rais Assad

  Wakamweka Riad Hijab kama kiongozi wa HNC. Huyu aliwahi kuwa waziri mkuu wa rais Assad. Inasemekana alishawishiwa na nchi za magharibi kujiunga na upinzani, baada ya kupewa sanduku la minoti kutoka majasusi wa Ufaransa

  Msemaji mkuu wa HNC ni Mohammed Alloush, ambaye anaongoza kikundi cha Jaysh al-Islam, Hawa ni wafuasi wa madhehebu ya Wahabi ambao wanashirikiana kwa karibu na Al Qaeda kupitia kikundi cha Jabat al-Nusra pamoja na ISIL/Daesh.


  0 0

  WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la ‘Amsha Mama Tanzania’ linalotarajiwa kufanyika Machi 5 katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke jijini Dar es Salaam .

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy record yenye makao Mkuu yake nchini Kenya ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo Joe Kariuki amesema wameamua kuleta tamasha nchini ili kuwapa fursa akina mama wa Tanzania kujiinua kiuchumi .

  “ Akina mama mjitokeze kwa wingi katika tamasha hili mahususi kwenu kwa kuwa mtapata fursa mbalimbali na mtaweza kupata mambo mbalimbali ikiwemo elimu” .Alisema Kariuki.

  Kwa upande wake balozi wa Amsha Mama nchini Khalid Ramadhani (Tundaman), amewaomba wakinamama wachangamkie fursa kwani watajifunza mambo mengi 

  “Nawaomba Mama zangu mjitokeze kwa wingi kwani tumepata bahati ya pekee ya kupendelewa kuletewa tamasha nchini kwani ni adimu kutokea,” 
  .alisema Tundaman.

  Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika pia katika uwanja wa Ranchi ya Kedong uliopo jiji la Naivasha nchini Kenya marchi 25-27 huku likitarajia kukutanisha akinamama kutoka nchi zote za Afrika .

  Aidha kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii kama vile Juma Kassim ‘’Juma Nature’’, Khadija Kopa, Roma Mkatoliki, Young Killer, Msagasumu, Man fungo,Sharo mwamba,Q-Chief,Mr Blue,Snura,Tundaman,na Ally Choki.

  Tamasha la Amsha Mama linatarajiwa kukutanisha akinamama mbalimbali kwa lengo la kujifunza kuhusu kujikwamua kiuchumi kwani wao ndio chachu ya mafanikio.

  Alisema wamejipanga kuwapa radha tofauti watoto wa temeke na majirani zake ,hasa kwa akina mama kupata fursa ya kujielewa na kujitambua hasa katika kuendeleza familia zao.

  0 0
 • 02/12/16--05:46: Article 15


 • 0 0

  10% of tell me !!! 
  120% is comming soon . 
  Stay tuned
  TZK Tunawatakia wiki nje njema yenye furaha 
  Mnaweza kupata kuona Utengenezaji wa video ya ngoma ya tell me yenye vionjo vya House music na kiswahili unaendelea .
  Pata kionjo kidogo....

  0 0

   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura akipokeza zawadi ya jezi ya timu ya Taifa ya Tanzania kutoka kwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji , Said Mohamed.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wamburaakizungumza na viongozi na wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake "Twiga stars" leo alipotembelea TFF.

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura leo ametembela ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kupata kujionea shughuli mbalimbali zinazondeshwa na shirikiso hilo.

  Akiongea na viongozi na wachezaji wa timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” waliopo kambini kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake dhidi ya Zimbambwe, Wambura amesema Serikali itashirikiana na TFF kuhakikisha timu inapata ushindi katika mchezo huo wa awali utakaochezwa Machi 4, 2016.

  Wambura amewataka wachezaji wa Twiga Stars kuwa na nidhamu ndani na nje ya uwanja, kujituma na kuiipenda kazi yao hiyo ambayo kwa sasa ni ajira itakayoweza kuwasaidia kuendesha maisha yao.

  Aidha Wambura amesema anaamini kuwa Twiga Stara bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo unaowakbalili, na kuwaomba kupambana zaidi kuhakikisha inapanda na kushinda nafasi ya kwanza Afrika katika soka la wanawake.

  Pia amesema wizara yake inashugulikia maombi ya TFF kuiomba wizara ya TAMISEMI ikasimishe mchezo wa mpira wa miguu katika mashindano ya UMITASHUMITA na UMISSETA yaweze kusimamiwa na TFF kwani wao ndio wenye utaalamu wa mchezo huu.

  0 0

  Magari yaliyowasili hii leo katika Uwanja wa Kaitaba yaliyoleta vifaa kwa ajili ya Umaliziaji wa Ujenzi wa Uwanja ambao ujenzi wake ulikuwa ukisua sua kutokana na kukwama kwa Vifaa hivyo Jijini Dar es salaam.
  Mesh rubber crumb
  Mshauri wa ufundi Bwana Rutayunga Peregrinus akiteta jambo na waandishi wa habari(kulia) leo kwenye Uwanja wa Kaitaba juu ya Umaliziaji wa Uwanja huo muda mfupi baada ya Vifaa hivyo kuwasili hii leo. Picha Na Faustine Ruta wa bukobasports.com.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Mgeni rasmi katika Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mkutano huo Meneja wa Rasilimali watu na Utawala wa Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam (DIT), Sebastian Ndahani Inoshi, mara baara ya kufunga Mkutano huo leo Februari 12, 2016, kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam . Wanaoshuhudia toka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA), Irene Isaka, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya SSRA, Juma Muhimbi. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
   Mgeni rasmi katika Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama akitoa hotuba yake ya kufunga mkutano huo, uliofanyika kwa siku mbili kuanzia jana February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
  Washriki wa mkutano huo na Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini hotuba fupi ya kufunga mkutano huo iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama, uliofanyika kwa siku mbili kuanzia jana February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah akiwakaribisha watoa mada mbalimbali katika Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, uliofanyika kwa mbili, na kufungwa rasmi leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama.
  Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0  Na Woinde Shizza, Arusha
  Bendi mpya ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina Filomena  music Band  ambayo makazi yake ni mkoani Kilimanjaro inatarajia kuwapagawisha wakazi wa jiji la arusha na vitongoji vyake  ndani ya usiku wa wapendanao (valentine day).
  Akizungumza na waandishi  wa habari jijini hapa mkurugenzi wa bendi hiyo Swaumu Kileo alisema kuwa bendi hiyo inatarajia kutua jijini Arusha kwa kishindo kwa ajili ya kuitambulisha rasmi bendi hiyo kwa wakazi wa jiji la arusha pamoja na kuwapa  burudani ya nguvu wakazi wa jiji hilo ambapo  alibainisha kuwa burudani watakayo itoa itakuwa ya kihistori na aijawai kutokea.
  Alisema kuwa  hii ni mara ya kwanza kwa bendi hii  kufanya show ndani ya jiji hili la Arusha kwa hivyo wanaimani wakazi wa jiji  hili na vitongoji vyake wataipokea kwa furaha na wataikubali kwakuwa hii ndio bendi ya kwanza kubwa iliopo  kanda ya  kaskazini.
  "ujio huu wa filomena bendi utakuwa ni wakihistoria kwani kwanza ni bendi kutoka  mikoa hii hii ya kanda ya kaskazini pia ipo nyumbani kwaiyo ninaimani watafurahi na wakazi wa jiji la arusha na vitongoji vyake wajitokeze kushuhudia bendi hii kwani hii ndio bendi yao ya nyumbani “alisema Swaumu
  Aidha alibainisha kuwa katika siku hii ya valentine day  wameiandaa maalumu kwa ajili ya kuwaonyesha washabiki wao kuwa wanawajali hivyo watatumia siku hiyo kuwatambulisha washabiki wa mziki huu wa dance nyimbo za bendi hiyo   ambapo pia alisema watawaonyesha staili nyingi mpya ambazo azijachezwa na bendi zingine hapa nchini ikiwa ni pamoja  na kuonyesha jinsi kila mtu anavyotakiwa kutingisha yakwake.
  Aidha alibainisha kuwa show hiyo itafanyika ndani ya ukumbi wa milestone garden uliopo jijini hapa huku akibainisha kuwa kwa upande wa viingilio V.I.P watalipa shilingi 20000 huku kawaida wakilipa shilingi 10000 kwa kila mmoja na kusema kuwa kwa wapenzi watakao pendeza kuliko wote wataondoka na bonge la zawadi.
  kwa upande wa kiongozi wa bendi hiyo sety Mbeki alisema kuwa timu  yake yote imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi wa Arusha  na kuwapa staili mpya ikiwemo ile ya kila mtu atingishe yakwake   ambapo alisema kuwa wameiboresha na imekuwa ya kiufasaha  zaidi  na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili tamu  pamoja na maneno matamu.
  Alisema kuwa lengolao kubwa la kufanya onyesho hili ndani ya jiji la arusha ni pamoja kujitambulisha kwa wakazi wa la arusha na kuwaambia wasio wapweke tena kwani wamepata bendi mpya kutoka nyumbani kwao bendi ambayo ni yao  inatoka ndani ya kanda yao na ni watoto wa o.
  Aliwasihi wakazi wa jiji la arusha na kanda ya kaskazini kwa ujumla kuwapokea kwa mikon o miwili na kuwapa ushirikiano ili waendelee kuwapa burudani zaidi.

  0 0


  East African Community

  Your Excellency Dr. Richard SEZIBERA - Secretary General of the East African Community;
   Honorable Minister of EAC Affairs of the Republic of Uganda;

  Honorable Members of the East African Legislative Assembly;

  Experts from the Partner States;

  Participants from Civil Society;

  Staff from the EAC Secretariat;

  Stakeholders from the press;

  Ladies and Gentlemen,

  Secretary General, let me to join you and your staff in mourning the sudden demise of Ms Isabelle Waffubwa, who had been a visible feature in the promotion of Democratic processes in the region. May her soul rest in eternal peace.

  Ladies and Gentlemen

  It is my honour and pleasure to announce to the people of the Republic of Uganda about the arrival of the East African Community (EAC) Election Observation Mission (EOM) to 18 February 2016 general elections in the Republic of Uganda. The Mission is in the country following the invitation by the Government of the Republic of Uganda and in fulfillment of the relevant provisions of the Treaty. It comprises 50 short-term observers drawn from the East African Legislative Assembly, national Human Rights Commissions, Electoral Management Bodies, Civil Society, EAC Youth Ambassadors and Officers from EAC Secretariat.

  Ladies and gentlemen, 
  The EAC Election Observation Mission arrived in Kampala on 7 February 2016 and will remain in the country until 21 February 2016. It was preceded by a team of election experts from the EAC Partner States who arrived on 30 January 2016. The Mission will observe the concluding stages of the campaign process and engage with various stakeholders as well as observe the voting and counting processes on 18 February 2016.

  In its assessment of the electoral process, I would like to highlight that the EAC Election Observation Mission will be guided by the democratic principles and values outlined in the African Charter for Democracy, Elections and Governance and the EAC Principles for Election Observation and Evaluation. To this end, the assessment of the electoral process in the Republic of Uganda will be carried out in an impartial and objective manner, informed by the principles and guidelines stipulated in the aforementioned standards as well as the legal framework governing the conduct of elections in the country.

  Ladies and gentlemen,
  On this day, we are deploying a total of of seventeen teams of EAC observers in the various regions of Uganda to assess the level of preparedness of the elections as well as the polling process.  The Mission will issue a statement of its preliminary findings of the elections on 20 February 2016 through a press conference. Subsequently, the EAC will release a final and comprehensive report through its policy organs after the end of the electoral process in the Republic of Uganda.

  Distinguished Colleagues from the Press, 
  I would like to inform you that there is a Spokesperson for the Head of Election Observer Mission - Dr. Abdullah Makame who is a Personal Assistant to me. He will be responsible with the press related issues, kindly cooperate with him during the entire process.

  Ladies and gentlemen, 
  May I take this opportunity to wish the citizens of Uganda success in choosing their future leaders through this important democratic exercise.

  Long Live Uganda!

  Long Live The East African Community.

  Thank you very much for your attention
   H.E Ali Hassan Mwinyi, former President of the United Republic of Tanzania and Head of Mission of the EAC Election Observation Mission makes his speech at the launch of the mission, flanked by the EAC Secretary General Amb. Dr Richard Sezibera (R) and Hon. Peter Mathuki, EALA​ MP.
   EAC Secretary General Amb. Dr Richard Sezibera addresses the Media during the Media Launch of the EAC Election Observer Mission as former President of the United Republic of Tanzania and Head of the EAC Elections Observation​ Mission, H.E Ali Hassan Mwinyi and Hon. Peter Mathuki, EALA MP look on.
  Hon. Peter Mathuki , EALA MP makes his remarks during the Media Launch of the EAC EOM as former President of the United Republic of Tanzania and Head of the EAC Election Observation Mission​, H.E  Ali Hassan Mwinyi (Middle) and EAC Secretary General , Amb. Dr Richard Sezibera look on. 

  0 0

   Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akifungua Mafunzo Elekezi kwa Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini  Dar es Salaam leo tarehe 12 Febuari, 2016. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson.

   Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti Mhe Hawa Ghasia akizungumza wakati wa ufungunzi wa mafunzo elekezi kwa waheshimiwa Wabunge. Katikati ni Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai na kulia ni Naibu Spika Mhe Dkt Tulia Ackson.

   Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia ufunguzi wa Mafunzo elekezi
   Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia ufunguzi wa Mafunzo elekezi

  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiteta jambo na Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson mara baada ya kufungua Mafunzo Elekezi kwa Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  0 0


  Taswira ya Kazi za upanuzi wa Mtambo wa Ruvu juu zikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi

  0 0


  0 0

  Herieth Paul mwanamitindo wa Kitanzania anayeishi jijini New York, Marekani ambako anafanyia kazi zake ameingia mkataba na kampuni ya vipodozi ya kimataifa ya MAYBELLINE ya New York, Marekani na kutangazwa kuwa BALOZI wake wa kimataifa  kuanzia mwezi Februari 2016; shughuli ambazo zitamfanya kwenda maeneo mbalimbali yakiwemo Bara la Ulaya, Marekani, Afrika, Asia na kwingineko duniani. Kampuni ya Maybelline ilimtangaza rasmi hivi karibuni, Mwanamitindo wa Kimataifa Herieth Paul, akiwa ni Mtanzania wa kwanza Mwanamitindo kuunyakua ushindi huu mkubwa.

   Herieth mwenye umri wa miaka 20 aligundulika kuwa na kipaji hicho akiwa na umri wa miaka kumi na nne (14) akiwa nchini Canada alipokuwa akisoma na kuishi na wazazi wake.

  Mbali na uteuzi wa kuwa BALOZI wa kampuni ya Vipodozi ya Maybelline, Herieth Paul amefanikiwa kufanya kazi na makampuni mbalimbali ya mitindo na vipodozi duniani ikiwepo kampuni ya Diane Von Furstenberg, Lacoste, Tom Ford, Zac Posen, Phillip Lim, Mac, Sephora nk...,

  Mwanamitindo wa Kimataifa Herieth Paul ambaye ameipeperusha Bendera ya Tanzania Dunia nzima anafanya masomo yake ya Chuo kwa njia ya mtandao na pia akijihusisha na shughuli za kijamii nyumbani alikozaliwa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwasaidia watoto yatima na wale wenye mazingira magumu  ili waweze kutimiza malengo yao ya kimaisha ikiwa ni pamoja na elimu na mahitaji yao ya kila siku.

  Mafanikio ya Herieth ni mfano wa kuigwa na vijana wa Kitanzania kwa kuwa na uamuzi sahihi, malengo dhabiti na bidii ya kazi, ni vichocheo muhimu vinavyoweza kufanya mtu afanikiwe katika maisha. 
  Gazeti la GLAMOUR la New York, Marekani lilifanya mahojiano na Bi Herieth Paul wakati wa sherehe fupi ya kuteuliwa kwake iliyofanyika jijiji New York Marekani:

  Lipstick:     Hongera kwa kuteuliwa kuwa Balozi wa Maybelline na kuwa mmoja kati ya wasichana waliokwisha kufanya kazi na kampuni hii. Je, kati ya wasichana waliowahi kufanya kazi na Maybelline ni nani anayekuhamasisha sana?.

  Herieth:    Sijui niseme ni nani kati ya Christy Turlington na Jourdan Dunn. Christy ni mwanamke mwenye bidii ya kazi, ni mzazi na anasaidia mashirika yanayohudumia wasiojiweza. Jourdan pia ni mzazi na anatoa misaada kwa watu wengine.
         
  Lipstick:    Ni mwanamke gani anayekuvutia sana kwa urembo?

  Herieth:    Mama yangu, ana uzuri wa asili, ngozi ya mwili ambayo ni nyeupe kidogo kuliko yangu ambayo inameremeta. Lakini pia anampenda Beyoncé.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitaka maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo na Mizani, Bibi Magdalena Chuwa (kulia) kuhusu sababu zilizomfanya azuie matumizi ya flow Meter katika kuhakiki kiwango cha mafuta yanayoingia nchini kupitia bandari ya Dar es salaam wakati alipofanya ziara kwenye badari hiyo Februari11, 2016.

  SERIKALI imeamua kuwasimamisha kazi watendaji wawili kutoka Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kuanzia leo ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa mafuta bandarini kutokana na zuio la kufunga kwa mita kwa zaidi ya miaka mitano.

  Waliosimamishwa kazi ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Bi. Magdalena Chuwa na Meneja Vipimo Kitengo cha Bandari, Bi. Bernadina Mwijarubi. Bi. Mwijarubi ndiye anashughulikia kitengo cha mafuta bandarini.

  Akitangaza uamuzi huo kwenye kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika leo (Ijumaa, Februari 12, 2016) ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Adelhelm Meru awaandikie barua za kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi huo.

  “Katibu Mkuu Viwanda, waandikie barua za kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi. Katika kipindi hiki hawatatakiwa kusafiri kwenda popote hadi uchunguzi utakapokamilika. Pia utafute mtu wa kukaimu nafasi hiyo ili kazi ziendelee,” alisema.

  Waziri Mkuu pia amesema ofisi yake itawaandikia barua ofisi ya TAKUKURU na polisi ili wafuatilie suala hilo mara moja na ikithibitika kuwa walihusika hatua rasmi zitachukuliwa na itathibitika hawakuhusika basi watarudishwa.Waziri Mkuu pia aliagiza mfumo wa upimaji mafuta kwa kutumia flow meters uendelee kutumika na ule upimaji wa kukadiria uache kutumiwa mara moja.

  Jana (Alhamisi, Februari 11, 2016) Waziri Mkuu alifanya ziara kukagua flow meters za zamani zilizopo Kurasini (Kurasini Oil Jetty) na kisha akatembelea na kukagua flow meters mpya ambazo zinajengwa Kigamboni. Mita hizo zimegharimu dola za marekani milioni 6 (sawa na sh. bilioni 12.96/- za sasa).

  Pia Waziri Mkuu alitembelea sehemu ya kuchukulia mafuta yanayotoka bandarini (TPA Manfold) iliyoko Kigamboni na kukagua mitambo ya kusambazia mafuta kwenye matenki ya mafuta ya kampuni ya TIPER yaliyoko Kigamboni yanayomilikiwa kwa ubia baina ya Serikali na kampuni ya Oryx Energies.

  Katika ziara hiyo ilibainika kuwa Kampuni ya TIPER imejiunganishia bomba la moja kwa moja kutoka kwenye bomba kubwa la mafuta linalotoka bandarini hali iliyomlazimu Waziri Mkuu kuagiza kwamba bomba hilo litolewe kwenye maungio hayo ndani ya mwezi mmoja.

  “Jana niliagiza kuwa bomba hilo ling’olewe. Nimetoa mwezi mmoja ili kurekebisha mfumo huo. Simamieni vizuri na kuhakikisha kuwa na wao pia wanarudi kwenye manfold kama ilivyo kwa wengine,” alisema Waziri Mkuu.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM.
  IJUMAA, FEBRUARI 12, 2016.

  0 0
 • 02/12/16--12:30: Article 3


 • 0 0

  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Makao Makuu tarehe 12/2/2016 imewafikisha washtakiwa wafuatao mahakamani, ambao pia ni maafisa waandamizi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL):

  1. Kipalo Amani Kisamfu, Mkurugenzi Mkuu wa TRL

  2. Jaspar hurbert Kisiraga, Mhasibu Mkuu wa TRL

  3. Mathias Andrew Massae

  4. Muungano Gabriel Kaupunda

  5. Ngoso Joseph Mwakilembe Ngosomwiles

  6. Pascal John Mafikiri

  7. Kedmon Peter Mapunda

  8. Felix Rwezaula Kashaigili

  9. Lowland Watson Simtengu

  10. Josepth Mlinda Syaizyagi

  11. Charles Florence Ndenge


  Washitakiwa hawa wakiwa Maafisa Watendaji Wakuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya na kutumia nyaraka kumdanganya Mwajiri kinyume na kifungu cha 22 na 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

  Kwa nyakati tofauti washitakiwa wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya na nyaraka kwa kuipatia zabuni Kampuni ya HINDUSTHAN ENGINEERING AND INDUSTRIES ambayo haikukidhi vigezo, kuleta mabehewa ya kokoto nchini.

  Fedha ambazo zimeshalipwa kwa Kampuni ya HINDUSTHAN ni dola za kimarekani 1,280,593.75 kati ya dola 2,561,187.50


  Washtakiwa wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kufunguliwa kesi namba 49/2016 inayosimamiwa na Mhe. Hakimu Mchaura. Kesi imepangwa kusikilizwa tarehe 25/2/2016.


  IMETOLEWA NA OFISI YA AFISA UHUSIANO

  TAKUKURU, MAKAO MAKUU

  12February 2016   Viongozi wa Kampuni ya Shirika la Reli nchini Tanzania (TRL), wakiwafikishwa  katika  mahakama ya  Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Dalaam tayari kwa kusomewa mashitaka 9 yanayowakabili likiwemo la  tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka. 

  Viongozi wa wa Kampuni ya Reli nchini Tanzania (TRL), wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam kusomewa mashitaka 9 yanayowakabili likiwemo la  tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, wa pili kulia ni aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika hilo,  Mhandisi Kapallo Kisamfu. 
  PICHA ZOTE NA KHAMIS MUSSA

  0 0


  0 0


  Mgeni Rasmi katika Sherehe ya Kutambulisha Rasmi Mafunzo ya Masomo ya Biashara yaliyo anza kutolewa na Chuo cha Sayansi na Teknolojia (MUST) Ndugu,Kisa Kwejo Muwakilishi wa Meneja wa (TRA) kwa Mkoa wa Mbeya akitoa Ufafanuzi katika Uzoefu wake katika Kazi juu ya Biashara na kuwatia Moyo Wanafunzi wanao Soma Masomo ya Biashara yanayoendelea kutolewa na Chuo hicho cha Sayansi na Teknolojia katika Nyanja Mbalimbali ikiwemo...,Ujasiliamali, Uwasibu,Lasilimali Watu,Manunuzi na Ugavi Pamoja na Biashara, hivyo Bi. Kisa Kwejo ameshauri kwa Wanafyunzi Mbalimbali wa Masomo hayo na watakao Jiunga na Masomo hayo kujikita katika Fulsa ya Kujiajiri mara baada ya kupata Mafunzo hayo ya Biashara,

  Mkuuu wa Darasa la Mafunzo ya Masomo ya Biashara Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST) kilichopo Jijini Mbeya akizungumza katika Hafla hiyo ya Kutambulisha Rasmi Mafunzo ya Masomo ya Biashara yanayoendelea kutolewa na Chuo hicho na kuwataka Wadau Mbalimbali wa Biashara, Wanafunzi, Wazazi, Waalimu na Vyombo Mbalimbali vya Habari kutambua kuwa Chuo cha Must Mbeya hakitowi Mafunzo ya Sayansi na Tecknolojia pekeyake pia kina toa Mafunzo ya Masomo ya Biashara na kinawakaribisha Wanafunzi kutoka Sehemu Mbalimbali kujiunga na Chuo hicho Kujifunza  Masomo ya Bishara.

  Mgeni Rasmi Bi. Kisa Kwejo akitoa Zawadi kwa Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo hicho cha Sayansi na Teknolojia (MUST) anaefanya vizuri katika Masomo ya Biashara....


                                                     Picha ya Pamoja.

                               PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA,
                                    KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

older | 1 | .... | 1122 | 1123 | (Page 1124) | 1125 | 1126 | .... | 3272 | newer