Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI WA FEDHA MH. ASHATU KIJAJU AFUNGUA MKUTANO WA MWAKAA WA 25 WA WANACHAMA NA WADAU WA PPF.

0
0
Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Katika hotuba yake ya Ufunguzi huo, Mh. Kijaji ameupongeza uongozi mzima wa PPF kwa kazi nzuri wanayoifanya katika suala zima la kuihudumia jamii, pamoja na kuipongeza ameutaka mfuko huo kuwakumbuka Wakulima kule vijijini kwa kuwaunganisha katika mtandao na kuwaingiza katika mfuko huo ili nao wapate kunufaika na mafao ya uzeeni.PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wmwaka wa 25 wa wanachama na wadau wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko"unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mmoja wa Wadau wakubwa wa mfuko wa PPF, Bwa.Bakari Kaoneka aliyekuwa akifanya kazi katika Ofisi ya Msajili wa Madawa akitoa ushuhuda wake mbele ya wadau wa mfuko huo kuhusiana na namna alivyonufaika na Fao la Uzeeni kupitia mfuko huo, Bw. Bakari ametoa angalizo kwa vijana wengi wanaojishughulisha na kazi mbalimbali kuwa wafikirie ipo siku moja na wao watastaafu,kwa hivyo ni lazima wajiwekee akiba ya uzeeni.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", ulioanza leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu Rais Muungano na Mazingira Atembelea Ujenzi wa Mtaro Uwanja wa Mnazi Mmoja na Kutembelea Jangombe Eneo Ilikozama Nyumba.

0
0
Kijicho cha Kampuni ya Ujenzi Mtaro huo kikiwa kazini katika uchimbaji wa mtaro huo nyambu ya pili pwani ya kizingo Zanzibar. 
Makalbi ya mtaro wa kupitishia maji kutoka katika viwanja vya mpira mnazi mmoja yakitandikwa, na kulia ni mabomba ya mtaro huo ya zamani yaliokuwa yakitoa huduma hiyo ya kupitisha maji kutoka katika uwanja huo. 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe.Luhaga Mpina akiangalia ujenzi huo wakati wa ziara yake kutembelea miradi huo.
Mradi wa Ujenzi wa Mtaro wa maji katika uwanja wa mpira wa mnazi mmoja unaoendelea na ujenzi wa mtaro huo
Imetayarishwa na Othman Mapara.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

WAZIRI MKUU AFANYA TENA ZIARA YA GHAFLA BANDARINI.

0
0
*Aibukia kitengo cha mita za kupimia mafuta Kurasini
*Akuta mafundi wakizitengeneza, akuta zimejaa kutu
*Ataka barua ya maelezo ifikapo saa 11 leo jioni


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara ya ghafla kwenye kitengo cha upimaji mafuta bandarini (Oil Flow Metres) na kukuta zimejaa kutu baada ya kutelekezwa kwa miaka zaidi ya mitano. Pia alitembelea mita za kupimia mafuta zinazoendelea kujengwa Kigamboni.

Aidha, Waziri Mkuu amempa saa nne tu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Bi. Magdalena Chuwa aandike barua ya kujieleza ni kwa nini aliamua kufunga mita hizo zisitumike kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita na amletee barua hiyo ofisini kwake ifikapo saa 11 leo jioni.

“Nataka unieleze ni kwa nini ulitoa maelekezo ya kufunga mita hizo, na kwa nini jana uliamua kubadili uamuzi huo? Ni kwa nini umeamua kuchukua maamuzi haya baada ya kupokea ujumbe wa simu ya mkononi (sms) wakati mita zimekaa bila kufanya kazi kwa miaka mitano? Ni kwa nini umeamua kufanyia kazi ujumbe wa sms wakati unajua Serikali inafanya kazi kwa maandishi rasmi?” alisema Waziri Mkuu.

“Umesema mlikuwa mnatumia utaratibu wa kupima kwa kijiti. Huu hauna uhakika na huwezi kutegemea taarifa ya mtu mwingine au kuingia kwenye meli ya mtu na kuanza kuchukua vipimo hadi ujiridhishe. Nataka kujua ni kwa nini mlikuwa na utaratibu wa ku-bypass mafuta ili yasipite kwenye mita za kupimia mafuta? Ni kwa nini umetoa amri zianze kutengenezwa jana na siyo mwaka 2012 au 2013?” alihoji Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu alisema mita hizo za Kurasini zilinunuliwa na Serikali kwa gharama za dola za marekani milioni 1.2 (wakati huo) na haiwezekani kuacha kuzitumia wakati watu wanachezea mifumo na kuongeza mianya ya kupoteza mapato kwa Serikali. Ameagiza mita hizo zianze kufanya kazi mara moja.

Wazir Mkuu alisema matumizi ya mita hizo yaliafikiwa na Serikali baada ya kubaini upotevu mkubwa wa kodi kwenye mafuta yanayoingizwa nchini na baada ya kuona hakuna tija ya kuendelea na ukadiriaji au kupokea taarifa za waagizaji peke yao.
  
Waziri Mkuu ambaye aliwasili Kurasini leo saaa 4: 30 asubuhi (Alhamisi, Februari 11, 2016) kwenye kitengo hicho kilichopo Kurasini (Kurasini Oil Jetty), alikagua mita hizo na kisha kwenda kukagua meli iliyokuwa ikishusha mafuta bila kutumia mita hiyo ya kupima mafuta yanayopokelewa kwa sababu mafundi walikuwa bado wanaendelea na ukarabati.

Akiwa Kurasini, Waziri Mkuu alielezwa na Bibi Chuwa kwamba mita hizo zilianza kufanyiwa ukarabati jana na leo asubuhi moja imekamilika ambayo ni ya kupokelea mafuta ya petroli. Ya dizeli ilikuwa inafunguliwa na mafundi na kukutwa imejaa kutu sababu ya kutotumika kwa muda mrefu.

“Hii ya dizeli imefunguliwa leo na ile ya mafuta ya kula, haijawahi kufanya kazi tangu ilipofungwa mwaka 2011,” alielezwa Waziri Mkuu na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Eng. Aloyce Matei.

Alipoulizwa ni kwa nini aliamua kuzifungia mita hizo ziisifanye kazi, Bi. Chuwa alijibu kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko kwamba zinawapunja wateja. Hata hivyo, hakufafanua ni wateja gani au wa aina gani.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa, ametembelea na kukagua mita mpya za kupimia mafuta ambazo zinajengwa Kigamboni. Mita hizo zimegharimu dola za marekani milioni 6 (sawa na sh. bilioni 12.96/- za sasa).

Akiwa hapo, Waziri Mkuu alielezwa kwamba ujenzi huo ambao ulianza miezi nane iliyopita, unatarajiwa kukamilika ifikapo katikati ya mwezi Machi, 2016. “Tunajitahidi kazi hii ikamilike ifikapo katikati ya mwezi ujao,” alisema Eng. John Bura, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya BQ Contractors Ltd ambayo inasimamia ujenzi wa mita hizo.

Vilevile, Waziri Mkuu alitembelea sehemu ya kuchukulia mafuta yanayotoka bandarini (TPA Manfold) iliyoko Kigamboni na kukagua mitambo ya kusambazia mafuta kwenye matenki ya mafuta ya kampuni ya TIPER yaliyoko Kigamboni yanayomilikiwa kwa ubia bainaya Serikali na kampuni ya Oryx Energies.

Katika ziara hiyo ilibainika kuwa Kampuni ya TIPER imejiunganishia bomba la moja kwa moja kutoka kwenye bomba kubwa la mafuta linalotoka bandarini hali iliyomlazimu Waziri Mkuu kuagiza kwamba bomba hilo litolewe kwenye maungio hayo ndani ya mwezi mmoja.

“Natoa mwezi mmoja hili bomba liondolewe kwenye mfumo huu na kama yapo mabomba mengine pia yaondolewe,” alisema huku akionyesha karatasi iliyokuwa mfukoni kwake yenye mchoro unaobainisha kuwa kuna bomba jingine la inchi 10 limeungwa kinyemela kwenye bomba kuu.

“Kila mmoja anapaswa aje kuchukua pale kwenye manfold ili tujue nani kachukua nini. Msajili wa Hazina hili ni eneo lako na wewe unamiliki TIPER kwa asilimia 50, hebu simamia hili. Ninyi TPA leteni mapendekezo yenu Serikalini ili tuone tunaweza kudhibiti vipi vitendo kama hivi,” alisema Waziri Mkuu.

Pia alimtaka Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru awasiliane na Mwanasheria Mkuu ili waangalie upya mkataba na umiliki wa matenki hayo uwe chini ya Serikali kwa asilimia 100 ili mafuta yanayoagizwa na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency) yaweze kuhifadhiwa huko.

Mapema, Waziri Mkuu ambaye alifuatana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alikagua eneo la manfold ya Mamlaka ya Bandari iliyopo Kigamboni na kukuta ni kampuni nne tu zenye matenki Kigamboni ambazo zinachukua mafuta yao hapo.

Kampuni hizo ni HASS, WORLD OIL, LAKE OIL na MOIL. TIPER haikutaka kufuata mfumo huo licha ya kuwa nafasi ya kufanya hivyo ipo. Kampuni nyingine zenye matenki yake nchi kavu, zinachukulia mafuta kwenye manfold ya Kurasini.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Mhandisi, Aloys Mtei (kulia) kuhusu  mabomba yanayotawanya mafuta kwenda kwenye matangi makubwa ya makampuni mbalimbali kwenye eneo la Kigambo jini Dar es salaam Februari 11, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo ambalo mafuta hufunguliwa na kufungwa ili kwenda kwenye matangi ya kuhifadhia mafuta ya makampuni mbalimbali yanayoagiza mafuta toka nje ya nchi wakati alipokwenda enero la Kigamboni jijini Dar es salaam kuonamianya inayotumika kukwepa kodi za mafuta yanayoagizwa nje ya nchikupitia bandari ya Dar es salaamFebruari 11, 2016.  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Flow Meter eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam Februari 11, 2016. Mtambo huo utatumika kupima wingi wamafuta yanayotoka kwenye meli na kuingizwa hapa nchini. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymound Mushi.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA DAMBAYA.

0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa familia ya mwandishi wa habari za michezo nchini Hamis Dambaya kufuatia kufiwa na mkewe, mwanae pamoja mama mkwe wake.

Katika salamu hizo, TFF imempa pole Dambaya kwa msibu huo mzito uliomfika na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini, Shirikisho liko pamoja nao katika kipindi hichi kigumu cha maombelzo ya misiba hiyo.

Mkewe Hamis Dambaya, mwanane na mama mkwe wake wamefariki katika ajali ya bus la Simba Mtoto iliyotokea leo asubuhi katikati ya eneo na Muheza na Hale wakati wakiwa safarini kuelekea jijini Dar es salaam wakitokea mkoani Tanga.

RAIS DKT. MAGUFULI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA TANGA.

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mama Mwantumu Mahiza, kufuatia vifo vya watu 11 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyosababishwa na Basi la Kampuni ya Simbamtoto kugongana uso kwa uso na Lori lililobeba mchanga katika eneo la Pandamlima, Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga.


Ajali hiyo imetokeo leo tarehe 11 Februari, 2016 majira ya saa 1:15 asubuhi katika eneo hilo lenye mteremko, ambapo basi la Kampuni ya Simbamtoto lilikuwa likisafiri kutoka Tanga kwenda Dar es Salaam na Lori lililokuwa limebeba mchanga, lilikuwa likielekea kiwanda cha Saruji cha Tanga.

Rais Magufuli amewapa pole Ndugu, Jamaa na Marafiki wote waliofikwa na msiba huo na amewataka kuwa wavumilivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu.


"Nimepokea taarifa ya vifo hivi kwa mshituko mkubwa, na kupitia kwako Mkuu wa Mkoa wa Tanga, napenda kuwapa pole nyingi wote waliofikwa na msiba huu mkubwa na naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo"alisema Rais Magufuli.


Dkt. Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, na amewapa pole majeruhi wote 21 walioumia katika ajali hii.

Aidha, Rais Magufuli amewakumbusha watumiaji wote wa barabara hususani madereva wa vyombo vya moto, kuwa makini watumiapo barabara kwa kuzingatia sheria zote zinazosimamia usalama barabarani ili kuepusha ajali.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam.


11 Februari, 2016.

Wadau wa Filamu waipongeza Serikali kwa kuwapa ushirikiano

0
0
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akimsikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Didas Entertainment Bibi. Khadija Seif (Dida) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Kampuni hiyo inajishughulisha na udhamini wa wasanii nchini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni inayojishughulisha na uandaaji wa Filamu ya Didas 
Entertainment Bibi. Khadija Seif (Dida) (akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo wakiwa katika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam.

Na: Frank Shija
SERIKALI imepongezwa kwa namna inavyotoa ushirikiano na kusaidia wasanii na wadau wa tasnia ya Filamu hapa nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Didas Entertainment Bibi. Khadija Seif (Dida) alipotembelea ofisi za Bodi ya Filamu leo jijini Dar es Salaam.

Dida amesema kuwa kama mdau wa Filamu anaishukuru na kuipongeza Serikali namna ambavyo inathamini na kutambua mchango wa wadau wa tasnia hiyo hapa nchini.

“ Naishukuru Serikali kwa namna ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano kwetu sisi wadau wa tasnia ya filamu hapa nchini” Alisema Dida.

Aidha Dida amesema kuwa kupitia Kampuni yake ya Didas Entertainment yenye ofisi zake jijini London ipo katika uaandaaji wa Filamu mbili ambazo ni “Dida” na “Black Belt” zitakazo tengenezewa hapahapa nchini. 

Nakuongeza kuwa filamu hizo zitakuwa shirikishwa baadhi ya wasnii kutoka Nigeria na zitakapo kamilika Filamu ya Black Belt inatarajiwa kuzinduliwa katika nchini nne tofauti ambazo ni Uingereza, Nigeria, Ghana na Tanzania

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesma kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa tasnia Filamu wandani na njje ya nchi ili kutanua wigo wa tasnia hiyo kukua kwa kasi.

Fissoo ametoa wito kwa wadau wa Filamu kuja kuwekeza katika tasnia Filamu hapa nchini ili kutanua wigo wa filamu za Kitanzania 

Didas Entertaiment imekuwa msaada mkubwa kwa tasnia za Filamu na Muziki ambapo mpaka sasa imewezesha takribani wasanii 30 kupata maonyesho nchini Uingereza, na imefanikiwa kutengeneza Filamu moja ya “Mateso yangu Ughaibuni”ambayo inafanya vyema katika soko.Kampuni hii imefungua milango kwa wasanii wa Filamu ili kutanua wigo wa Filamu za Kitanzania.

TEASER JOTO LA ASUBUHI LA EFM 93.7EFM KUANZIA SAA 12 ASUBUHI

Valentine Affair kutoa Pete ya Tanzanite ya Milioni nne

0
0
Na Mwandishi Wetu

Pete iliyotengenezwa kwa madini ya Tanzanite yenye thamani ya shilingi za kitanzania Milioni nne, huenda ikawa mali ya  wapendanao watakaokuwa na bahati,  maana ni miongoni mwa zawadi nono zitakazotolewa katika onesho la wapendanao lililopachikwa jina la Valentine Affair linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa King Solomon jijini Darv Salaam katika siku ya Wapendanao Jumapili hii.

Akiongea na wanahabarti, Mratibu wa Matukio wa kampuni ya King Solomon Events, Bi Hellen Kazimoto amesema Kampuni hiyo inayokuja kwa kasi katika mambo ya burudani, baada ya kukonga nyoyo za mashabiki kwa matamasha yake yaliyoonesha mapinduzi katika sekta ya burudani nchini, yakiwemo ya Party in The Parking na ziara ya mwanamuziki WizKid jijini Dar es salaam, sasa wanakuja na tamasha jingine kubwa zuri na la kusisimua katika msimu huu wa wapendanao.
Tamasha limepewa jina la Valentine Affairs ambapo litawapa nafasi wapenda burudani na wapendanao kwa ujumla kujumuika pamoja kwa ajili ya chakula chenye hadhi ya nyota tano na muziki wa kutumia ala utakaoshirikisha wanamuziki mahiri wa miondoko laini nchini, wakati huo huo zawadi za aina yake zikitolewa ukumbini hapo.


Onesho hilo litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomons, Jumapili ya Tarehe 14 Februari, 2016, kuanzia saa 12 jioni na kuendelea linatarajiwa kupambwa na wanamuziki BenPol, Grace Matata pamoja na mkongwe Patricia Hillary.


Wanamuziki hawa watakuwa wakipigiwa muziki maalum kwa ajili ya wapendanao kwa vyombo vya ala, na watakuwa wakiburudisha wapendanao muda wote watakapokuwa katika eneo la tukio kuanzia kuwasili kwao, mpaka muda wa chakula n ahata wakati wa kupeana zawadi.


Zawadi zitakazotolewa ni pamoja na pete kwa wapendanao watakaokuwa na bahati, ni Pete yenye thamani ya shilingi Milioni nne, iliyotengenezwa kwa madini ya tanzanite, kutoka Gift Jewelers. Zawadi nyingine ni malazi ya siku mbili kwa wapendanao katika Hoteli ya Regency Park Hotel ambao pia ni wadhamini wa onesho hilo la aina yake ya wapendanao.


Zawadi nyingine ni vocha yenye thamani ya shilingi laki mbili za kitanzania kutoka kampuni ya King Solomons ambayo inaweza kutumika katika mgahawa wa Eaters Point au Wantashi.



Usiku huu wa Valentine Affair umefanikishwa na wadau mbali mbali kwa kushirikiana na King Solomons Events ambao ni Wantashi, Coca Cola, Eaters Point, EATV,EARadio,Regency Park Hotel,Gift Jewelers pamoja na twenty4 Printers.


PICHANI JUU: Kuroka kushoto Mratibu wa matukio wa King Solomon Events, Bi Hellen Kazimoto, Ben Pol, Patricia Hillary na muwakilishi wa Mgahawa wa eaters Point Chef Suba

WAKULIMA, WAFUGAJI NA WAVUVI WAJADILI NA KUTOA MAONI YA UCHAMBUZI WA MWONGOZO WA KUANDAA MPANGO NA BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA WA FEDHA 2016/17

0
0
Mwongozo wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2016/17 umeandaliwa kwa kuzingatia Kifungu Na. 21 cha Sheria ya Bajeti Na. 11 ya Mwaka 2015. Aidha, Mwongozo wa Mpango na Bajeti wa Mwaka 2016/17 umejikita katika kujenga Taifa lenye uchumi wa viwanda kama ilivyoainishwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 pamoja na Mpango Elekezi wa Miaka 15. 


Warsha hiyo ambayo imeandaliwa na ushirikino wa mashirika matano ambayo ni Oxfam, Policy Forum, ANASAF, Action Aid na TGNP zaidi ikiwa ni kuwaleta pamoja wakulima hao wadogowadogo katika kupitia mwongozo na kuujadili kwa ukaribu pamoja na kuuchambua kwa kina zaidi.

Wakati akitoa majumuisho kutoka ukurasa wa 14-20 Bi Flora Mathias Kutoka Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkulima mdogo ameomba Mkulima ameiunga mkono hoja ya mwanamke kuthaminiwa na kupata nafasi ya kuuza Bidhaa zake, kupewa nafasi ya kujitambua na kumiliki Ardhi, huku akiulalamikia mwongozo huo wa bajeti elekezi kutoweka wazi kuhusu mfuko wa wanawake katika kusaidia uzalishaji na kuomba bajeti inayokuja izingatie hilo.

Mzee Namagono Hassan kutoka kundi la wakulima ametoa maelezo kutoka ukurasa wa 6-9 kuhusu mambo muhimu katika mwongozo wa Bajeti 2016/17, kuwa pamoja na kuanzishwa kwa Benki ya wanawake, isitazame tuu wanawake wa mjini bali na vijijini kwani wao ndio wazalishaji zaidi wa Chakula kuliko waishio mijini.

Kwa upande wake Datius Pastory Inshansha Mwanaharakati na Mkulima mdogo ukurasa wa 20-23 amepitia ukurasa 23-24 unaotoa maelekezo mahsusi kwa sekretarieti za mikoa na mamlaka ya serikali za mitaa na kushauri kuwepo uwazi wa mapato na matumizi ya Serikali za Mitaa, pia Bajeti ielekezwe zaidi vijijini kulipo mjini na kudhibiti fedha za uvuvi,kilimo na ufugaji zisiishie kwa watu wachache bali wahusika kwa ujumla.

Maelezo mengine yametolewa na Bwana Adam Simwinga kuhusu ukurasa wa 9-15 kipengele cha Maelekezo ya Maandalizi ya bajeti kwamba amegundua hakuna mkakati wa kuongeza mapato kupitia simu, mkakati wa msamaha wa kodi, hivyo wameshauri kilimo kiwe ni sehemu ya eneo wezeshi na malighali katika viwanda nchini Tanzania na katika mpango wa maendeleo na kuongeza kuwa asilimia 30% hazijitoshelezi kukuza sekta ya kilimo nchini.

Wanaharakati hao wameishauri serikali kutowasahau katika kuwawezesha mikopo ili kukuza sekta zao kimaendeleo huku wakilalamika wakulima kutoshirikishwa kikamilifu.

“Tunaomba mkopo wa Magari ya wabunge upungue kutoka Mil 90 hadi Mil 20 ili zile mil 70 zitumike katika shughuli zingine za maendeleo ikiwemo na kilimo na pia kuwe na viwanda vidogo vidogo katika mikoa mbalimbali mfano kiwanda cha Machungwa” aliongeza Bi. Kidani Mhenga wanajadili ukurasa wa 3-5 mapitio ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti.

Bi Flora Mathias Kutoka Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkulima mdogo akitoa majumuisho kutoka kipengele cha namna ya kudhibiti Bajeti za Serikali kutoka katika mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017 ukurasa wa 14-20, picha ya juu ni wanakundi wakiwa wanajadili swala hilo. Picha ya juu ni baadhi ya mama Shujaa wa chakula ambao wanatoka katika Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Oxfam Tanzania pamoja na wadai wengine wa kilimo .

Mzee Namagono Hassan Kutoka kikundi namba moja akitoa maelezo kutoka katika mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2016/2017 kutoka ukurasa wa 6-9 unaoelezea mambo muhimu katika mwongozo wa Bajeti 2016/17.
 

Maugo, Dulla Mbabe kumsindikiza Cheka February 27

0
0
Mabondia, Mada Maugo na Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe' watapanda ulingoni kusindikiza pambano la Francis Cheka na Geard Ajetovic la ubingwa wa mabara wa chama cha WBF Februari 27.

Cheka na Ajetovic watawaniaubingwa wa super middle katika pambano la raundi 12 lililopangwa kufanyika kwenye viwanja vya Leaders Club.

Kwa mujibu wa Meneja wa Cheka ambaye pia ni Mkurugenzi wa Advance Security, Juma Ndambile, Pazi na Maugo watawania ubingwa wa Afrika wa uzito wa super-middle na tayari WBF wamekwisha toa Baraka kufanyika kwa pambano hilo na watalisimamia.

Alisema kuwa siku hiyo pia, Mohamed Matumla atazipiga na Ibrahim Class katika pambano la raundi nane la uzito wa light-weight.

Ndambile alisema kuwa mapambano hayo yatasimamiwa na waamuzi kutoka Ujerumani na Afrika kusini ambao watawasili nchini Februari 23 pamoja na rais wa WBF, Howard Goldberg.

"Waamuzi  watawasili na ndege ya Afrika Kusini, Februari 23 Ajetovic atawasili pia tayari kwa pambano hilo la kimataifa," alisema Ndambile.

Cheka tayari yuko Dar es Salaam ambako amepiga kambi chini ya kocha wake, Abdallah Salehe 'Comando' kujiweka fiti na pambano hilo.

 Awali mabondia hao walizichapa 2008 nchini England na Cheka kupigwa kwa pointi mjini Manchester.
 Mapema Jana, wakati wakitambulisha pambano lao, Maugo na Dullah Mbabe walitaka kuzichapa kavu kavu kabla ya kuamliwa na Mlinzi aliyeambatana nao, Chrispin stephano.

Wakizungumzia pambano hilo, Maugo na Dullah Mbabe kila mmoja alitamba kumsambaratisha mpinzani wake watakapozichapa siku hiyo.

 "Namheshimu Dullah, ni Bondia mzuri lakini ajipange siku hiyo, hasira zangu za kukosa ubunge nitazimalizia kwake," alitamba Maugo.

Wakati Dullah Mbabe akimtahadharisha Maugo na kubainisha kwamba atamuonyesha kwa vitendo ulingoni siku hiyo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Advanced Security Company Limited, Juma Ndambile (watatu kutoka kulia) na mratibu wa pambano la ubingwa wa mabara kati ya Francis Cheka na Msebia Geard Ajetovic Jay Msangi wa tatu kutoka kushoto, wakiwatambulisha mabondia watakaozichapa kwenye masumbwi ya utangulizi, wakati wa pambano la ubingwa wa mabara kati ya Francis Cheka na Msebia Geard Ajetovic, litakalofanyika Februari 27 kwenye viwanja vya leaders club, jijini Dar.

TRA YAKAMATA SHEHENA KUBWA YA BIDHAA ZA MAGENDO

0
0
Na Jacquiline Mrisho-Maelezo.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukamata bidhaa za magendo kwenye maeneo mbalimbali yaUkanda wa wa Bahari ya Hindi, Ziwa Viktoria na mipaka mingineyo nchini.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Bw. Richard Kayombo wakati akifanya mahojiano na Mwandishi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kuhusu juhudi za operesheni ya kutokomeza bidhaa za magendo nchini.

Bw. Kayombo ameeleza kuwa, katika Mkoa wa Lindi TRA imefanikiwa kukamatamashua katika bandari ya Lindi ambayo ilisheheni bidhaa za magendo zenye thamani ya shilingi 159,361,046.

Ameongeza kuwa katika operesheni hiyo, TRA imefanikiwa kukusanya kodi ya jumla ya shilingi 10,500,678 kutoka katika bidhaa zilizokuwa katika nyaraka za forodha (manifest) ambapo pia inategemea kukusanya kodi ya shilingi 19,529,500 kutoka katika bidhaa ambazo zilikuwa katika nyaraka za forodha lakini thamani yake ilikuwa chini ya beo halisi.

Akitaja bidhaa hizo za magendo zilizokamatwa katika mashua hiyo ni mifuko 3,725 ya sukari yenye thamani ya shilingi 127,070,562, betri katoni 50, mchele mifuko 3,087, mafuta ya kula madumu 80, majokofu manne ya mtumba, baiskeli za mitumbo nne pamoja na katoni 20 za hamira.

‘’Mashua hiyo ilikamatwa katika bandari ya Lindi tarehe Mosi Februari, 2016 baada ya wasamaria wema kutoa taarifa ya kuwepo bidhaa za magendo ndani ya mashua hiyo ambapo upakuaji wa shehena hiyo ulianza mara moja’’, alisema Kayombo.

Kayombo kaongeza kuwa kwa upande wa jijini la Dar es Salaam, TRA kwa kushirikiana na Kikosi cha doria cha Jeshi la Wanamaji wameweza kukamata Jahazi lenye jina la ‘Takbiri’ lenye usajili wa namba Z-875 likiwa limesheheni lita 19,700 za dizeli ambapo thamani yake bado haijapatikana kwakuwa imepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya Uchunguzi zaidi.

Aidha, majahazi mengine matatu yamekamatwa katika eneo la Kigombe mkoani Tanga ambayo yalikuwa na bidhaa za magendo yenye thamani ya shilingi 99, 682, 273, 48 ambamo ndani kulikuwa na magunia ya sukari, mchele, mafuta ya kula, matairi ya magari, nyaya za kuzuia mbu, jokofu, jiko la umeme, rangi za kupuliza, betri na biskuti ambapo majahazi hayo yalitaifishwa baada ya wahusika kujitosa ndani ya maji na kutoroka.

Aidha, TRA kwa kushirkiana na Jeshi la Polisi metoa wito kwa umma kuwa inafanya doria saa 24 kila siku katika maeneo yote yaliyoshamiri upitishaji wa bidhaa za magendo ambapo imeunda Kanda Maalum katika maeneo ya Mbweni, Msasani, Kunduchi pamoja na Kigamboni.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 11.02.2016

PROF. MBARAWA AKAGUA CHUO CHA MABAHARIA (DMI)

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Chuo cha Mabaharia cha Dar es Salaam (DMI) Eng. Yassin Songoro katika ziara yake ya kukagua Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Mabaharia cha Dar es Salaam (DMI) Eng. Yassin Songoro (katikati) akimuongoza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kukagua madarasa ya Chuo hicho.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua dira ya kuongozea meli (compass) katika moja ya darasa la Chuo hicho. Kulia ni Mkuu wa Chuo cha DMI Eng. Yassin Songoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (mwenye tai) akikagua mitambo ya kuongozea meli katika moja ya madarasa ya chuo cha DMI wakati wa ziara yake chuoni hapo.

SIKU 100 ZA DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI MADARAKANI

PUBLIC NOTICE: STATE MINING CORPORATION

0
0
STATE MINING CORPORATION


On 4th February, 2016, STAMICO received a written notice of Force Majeure from Tanzania American International Development Corporation (2000) Limited (TANZAM) suspending mining operation at Buckreef Gold Mine located in Geita region.

 TANZAM notice claims ‘’forceful occupation by several hundred illegal miners on the mining property including the South Pit and other areas within the Buckreef site thereby endangering TANZAM employees.’’ TANZAM is our joint venture partner and an operator in the re-development of Buckreef Gold Mine following signing of the joint venture agreement in 25th October, 2011. 

We are deeply concerned by the decision of TANZAM to suspend mining operations at Buckreef due to the fact that neither STAMICO nor the Buckreef Board of Directors have ever received a formal complaint regarding such events before issuing the Force Majeure notice.

In recent times, STAMICO has been urging TANZAM to pay delay penalties that remain due to their failure as an operator to commission the project within the timeline stipulated under the JV Agreement. TANZAM was to commission production by the end of 30th month following effective date of signing the JV agreement with STAMICO on 25th October 2011. The 30th month expired on 21st May, 2014 and by that time the operator had not yet commissioned the mining and plant operations. Though todate, some mining activities have taken place, yet the work progress is not satsifactory. 

STAMICO believe that the matter will be resolved amicably by exploring all available possibilities for the interest of both parties. STAMICO remain firmly committed to work closely with Tanzam in developing the mine for the mutual benefit and the benefit of the entire Tanzania populace.

For Further details contact: 
Acting Managing Director, 
State Mining Corporation,
Plot No 417/418,

UN Road,
P.O. Box 4958,
Dar es Salaam,

Tanzania. 
Telephone: +255-22-2150029.

WAZIRI MWAKYEMBE ATEMBELEWA NA BALOZI JAAP WA UHOLANZI.

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Bw. Jaap Frederiks alipomtembelea ofisini kwake leo 12/2/2016 jijini Dar Es Salaam kwa mazungumzo.
Waziri Mwakyembe alimwelezea balozi huyo shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara na balozi Jaap aliahidi kushirikiana na Tanzania kwenye masuala ya kisheria ya kimataifa.

Katibu Mkuu TUCTA asifia Sheria za Kazi

0
0

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Nicholas Mgaya akiongea na Wajumbe wa Kikao cha Tathmini ya Utendaji kazi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi wakati wa Ufunguzi wa Kikao hicho leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ulimwenguni kwa nchi za Tanzania, Kenya, Burundi, Rwanda na Uganda Bi. Mary Kawar akichangia mada wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Tathmini ya Utendaji Kazi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Masuala ya Walemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiongea na Wajumbe wa Kikao cha Tathmini ya Utendaji kazi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi wakati wa Ufunguzi wa Kikao hicho leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Mhe. Shaaban Lila akichangia mada wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Tathmini ya Utendaji Kazi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Kikao cha Tathmini ya Utendaji kazi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi wakifuatilia uwasilishwaji wa mada toka kwa viongozi mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa Kikao hicho kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI MHANDISI STELLA MANYANYA AFANYA ZIARA KATIKA MAMLAKA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (VETA) MAKAO MAKUU, CHANG`OMBE JIJINI DAR ES SALAAM.

0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wafanyakazi wa VETA Makao Makuu (hawapo pichani) alipofanya ziara katika mamlaka hiyo Changombe jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Geofrey Sabuni na kulia ni Wakurugenzi wa Wizara hiyo walioongozana na Naibu waziri.
Wafanyakazi wa VETA Makao Makuu wakimsikiliza Naibu Waziri Mhandisi Stella Manyanya wakati wa ziara hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Geofrey Sabuni akimkaribisha Naibu Waziri Mhandisi Stella Manyanya kuzungumza na wafanyakazi wa VETA Makao Makuu wakati Naibu waziri alipofanya ziara katika Mamlaka hiyo.

Efm yaja tena na Mchizi Wangu Concert Jumapili siku ya wapendanao viwanja vya posta kijitonyama Dar es salaam

0
0
Kwa mara nyingine tena EFM Radio 93.7 inakuletea tamasha la siku ya wapendanao MCHIZI WANGU CONCERT, litakalofanyika jumapili ya Tarehe 14/2/2016 katika viwanja vya posta-kijitonyama jijini Dar es Salaam. 
Tamasha hilo linalolenga kudumisha upendo sio tu kwa wapenzi ila kwa ndugu, jamaa na marafiki. 
Kutakuwa na burudani kibao kutoka kwa wasanii kibao wa mchiriku na singeli, pia uzinduzi wa klabu za mashabiki kutoka sehemu mbalimbali za jijini Dar es salaam na Pwani kwa nia ya kuwaweka karibu wasikilizaji wetu. 

WAZIRI WA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE. UMMY MWALIMU AMTEMBELEWA LEO NA MABALOZI WA SWITZERLAND NA KOREA OFISINI KWAKE.

0
0
 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akizungumza na Balozi wa Korea Nchini Tanzania (Song, Geum-Young) wa kwanza kushoto akiwa na Katibu wake Songwon Shin wa pili kushoto. 
 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania, Florence Tinguely Mattli wa kwanza kushoto akiwa na Mkuu wa Sekta ya Afya ya Ubalozi wa Switzerland, Thomas Teuscher wa pili kushoto.
Balozi wa Korea Nchini Tanzania, Song, Geum-Young akizungumza na Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, wa pili kushoto ni Katibu wake Songwon Shin.
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live




Latest Images