Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1120 | 1121 | (Page 1122) | 1123 | 1124 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Na Lorietha Laurence-Maelezo

  Serikali imebaini wizi wa  takribani  shilingi Milioni 700 katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kupitia kampuni ya Wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo visiwa vya Komoro.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa ameeleza kuwa wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo.

  “Kufuatia upotevu huo Serikali  imechukua hatua thabiti ikiwemo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi  cha polisi  kitengo cha usalama mtandaoni  ili kubaini mtandao mzima uliohusika  ” alisema Prof.Mbarawa.

  Aidha aliongeza kuwa kwa utaratibu wa kawaida wa  shirika hilo wakala anapewa ruhusa ya  kuuza tiketi za ndege kuanzia kiasi cha shilingi milioni 15 tu na pale anapomaliza mauzo anarudisha fedha kwa shirika na baadaye kupewa ruhusa tena.

  Prof.Mbarawa anasema kwa sasa wameanza na shirika la Ndege la Tanzania kwa kwa lengo la kulifufua kwa kununua ndege mpya na kuwa na wafanyakazi wachapakazi na waadilifu.

  “Siku mbili zilizopita nilifanikiwa kukutana na menejimenti ya ATCL na kubaini mapungufu mengi na hivyo kuamua kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha shirika hii linarudi kutenda kazi kwa udhabiti kwa kuwashughuikia wale wote wanaoenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma” alisema Prof.Mbarawa.

  Vilevile aliongeza kuwa Serikali imemuagiza  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kufanya uchunguzi kwa mawakala wengine wote wa Shirika hilo kubaini kama fedha za uuzaji wa tiketi hizo zinarudishwa kama inavyotakiwa.

   Prof.Mbarawa ametoa wito kwa wananchi kuachana na wizi kwa  njia ya mtandao kwa kuwa sheria ya mtandao iliyoanzishwa mwaka jana inatumika katika kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanafikishwa katika mkondo wa sheria na kuchukuliwa hatua stahiki. 

  0 0

  Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya(kushoto)akimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwera(kulia)Wakati alipotembelea chumba cha maktaba ya kutunzia nyaraka alipofanya ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam.Wapili toka kushoto Mkurugenzi Msaidizi  wa Wizara hiyo Eng.Enock Kayani na  Mratibu wa maktaba ya Nacte, Clara Kihombo. 
    Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) jijini Dar es Salaam kujionea maendeleo ya utendaji wa baraza hilo.
   Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya(wapili kulia)akimsikiliza Vicent Jacob Mtaalam wa Mtandao wa Udhibiti wa Utoaji wa vyeti vya Satifiketi na Diploma kwa Baraza la Taifa na Ufundi(Nacte) wakati alipofanya ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam, kujionea maendeleo ya utendaji wa baraza hilo.Watatu toka kulia Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwera.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (kulia) na Jiji Mkuu Tanzania  Mohammmed Chande Othman wakati alipowasili viwanja vya Victoria Garden katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar.
   Mwanasheria Mkuu zanzibar Said Hassan Saidi akitoa maelezo mafupi na kumkaribisha jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman  Makungu wakati wa sherehe za kilele cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.
   Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha kitabu cha Sheria ya mwaka Zanzibar (ZANZIBAR YEARBOOKOF LAW) Volume 4 baada ya kukizindua rasmi leo katika  sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,(kulia)Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,(kushoto) naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Ali Abdalla,Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman Chande.
  {Picha na Ikulu.]

  0 0


  0 0
 • 02/10/16--04:59: Article 8


 • 0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  TATIZO la utumiaji wa dawa za kulevya kwa  vijana unaanzia  katika shule, hivyo kunahitaji kupimwa wanafunzi wakiwa shuleni katika kuweza kutokomeza tatizo la utumiaji wa dawa hizo.
  Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii jinsia na Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati makabidhiano ya  Gari ya Kituo cha  Kuratibu  Matumizi ya Sumu lilitolewa na nchi ya Japan kwa ofisi ya  Mkemia Mkuu wa Serikali,  amesema kuwa tatizo la utumiaji wa dawa unaanzia shule hivyo ofisi mkemia mkuu wa serikali anaweza kupima wanafunzi kila baada ya muda na kuweza kugundua chanzo cha dawa hizo.
  Amesema kuwa wanafunzi wakipimwa kila baada ya muda mkemia anaweza kujua na serika ikaweza kudhibiti juu ya matumizi ya dawa  za kulevya kutokea shuleni.
  Waziri, Ummy amesema vijana wanaotumia dawa za kulevya  wengine walianzia katika shule na kuweza kuwafundisha wengine na kuwa ongezeko la watumiaji wa dawa za kulevya na kusababisha nchi kukosa nguvu kazi ya vijana kutokana na kuathirika dawa hizo.
  Aidha amesema katika kazi data ya kuweka taarifa za vinasaba vitasaaidia kupunguza watoto wa mitaani kutokana wazazi watambuliwa na vinasaba mara baada ya kupima.
  Ummy, amesema kuwa ofisi ya mkemi mkuu wa serikali ni ana kazi kubwa ya kutoa haki kwa kushirikiana na vyombo vingine ikiwemo majanga moto kwa kuweza kutambua watu baada ya kutokea,  vinasaba vya watoto ambao wanakuwa katika mgogoro na kubaini mhusika.
  Nae Mtendaji wa Maabara wa Ofisi ya Mkemia Mkuu, Profesa Samwel Manyere amesema kuwa kupata gari hilo watafanya kazi kwa kiwango cha juu kutokana na jinsi walivyojipanga.
  Aidha amesema kuwa wameweza kupata cheti cha utoaji huduma kwa kiwango cha Kimataifa (ISO) hivyo kitu chochote kikifanyika kinaendana na viwango hivyo.

  0 0

  Mshindi wa pili wa mashindano ya Techno Own Stage, Faustina Mfinanga aka Nandy,akiwa uwanja wa ndege wa Mwalimu Juliusi Nyerere , baada ya kuwasili kutoka Nageria katika mashindano hayo, jana jijini Dar es Salaam. 
  Mshindi wa pili wa mashindano ya Nandy Techno Stage, Faustina Mfinanga, akiwa kabebwa juu mara baada ya kuwasili kutoka Nigeria,jana jijini Dar es Salaam.
  Nandy akiwaonesha wananchi waliofika kumpokea uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere , jana jijini Dar es Salaam.
  Mshindi wa pili wa mashindano ya Techno Own Stage, Faustina Mfinanga, akiwa katika picha ya pamoja na ndugu zake jana jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya Jamii)

  Mshindi wa pili wa mashindano ya Techno Own Stage, Faustina Mfinanga aka Nandy,akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ushindi alioupata nchini Nigeria baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege majira saa sita usiku wa kuamkia leo ,jijini Dar es salaam.

  0 0

   Kikundi cha ngoma za asili ya kigogo cha Chamwino Ikulu Dodoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mkoa wa Dodoma ya kugawa vyandarua vya bila malipo kwa kaya Februari 9, 2016.
   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akigawa vyandarua vya bila malipo kwa wananchi wa kijiji cha Chamwino Ikulu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ugawaji vyandarua Mkoani humo Februari 9, 2016.
   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akiwafundisha wananchi wa Chamwino Ikulu namna bora ya kuwakinga watoto dhidi ya mbu na malaria kwa kuwalaza kwenye vyandarua wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ugawaji vyandarua Mkoani humo Februari 9, 2016.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir ambaye amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.
  Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir akimuombea Dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Rais Dkt. Magufuli kumjulia hali Hospitalini hapo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa Dua na ndugu na jamaa mbalimbali ambao walifika Muhimbili kuwaona wagonjwa wao.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea katika Wodi ya Wazazi kufanya ukaguzi wa ghafla mara baada ya kuwasili akitokea Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wagonjwa waliolazwa katika Wodi ya Wazazi na amewahidi kutatua kero zao ndani ya muda mfupi ujao.PICHA NA IKULU

  0 0


  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Bw. Reginald Mengi (kulia), wakati akisisitiza jambo katika mkutano na wadau wa Sekta Binafsi uliofanyika Wizarani hapo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akimsikiliza kwa makini Rais wa Wakala wa Forodha ya Tanzania (TAFFA), Bw. Steven Ngatunga wakati wa Mkutano wa Waziri huyo na Wadau wa sekta binafsi.
  Wadau wa sekta binafsi wakijadiliana jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa katika mkutano wao uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Mdau wa sekta binafsi Bw. Felix Mosha (wa kwanza kulia) akifafanua jambo katika mkutano wa wadau hao. (Kushoto) ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Bw. Reginald Mengi.

  0 0


  0 0

   Mshindi wa Droo ya mwezi Desemba 2015, Daniel Mugasa, akisaini kwenye kitabu maalumu baada ya kukabidhiwa  vocha ya manunuzi yenye thamani ya shilingi Milioni 1 na   Meneja Masoko na Uhusiano wa Duka la nguo la Woolwoorths Tanzania, Edwina Barongo,  wakati wa hafla  iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ili mteja  aweze kushiriki katika shinadano hilo ni lazima awe na card maalumu ya inayomwezesha   kununua bidhaa katika  maduka ya Woolworths (Wreward Loyalty Card).
    Mshindi wa Droo ya mwezi Desemba 2015 , Daniel Mugasa , akikabidhiwa  na  Meneja Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Woolwoorths Tanzania, Edwina Barongo vocha ya manunuzi yenye thamani ya  shilingi Milioni 1 ,  baada ya kuibuka mshindi  . Ili mtena  aweze kushiriki katika shinadano hilo ni lazima awe na card maalumu ya inayomwezesha   kununua bidhaa katika  maduka ya Woolworths (Wreward Loyalty Card) . Hafala hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
   Meneja Masoko na Uhusiano wa duka la nguo la Woolwoorths Tanzania, Edwina Barongo ( Kulia)  akimuonyesha bidhaa mpya  mshindi wa  Droo ya mwezi Desemba 2015  , Daniel Mugasa    wakati alipofika katika Duka la Woolworths  jijini Dar es Salaam, kumkabidhi zawadi yake vocha ya manunuzi yenye thamani ya shilingi milioni 1 baada ya kuibuka  mshindi  katika droo ya Woolworths ya Desemba 2015. Ili mteja  aweze kushiriki katika shinadano hilo lazima na card maalumu ya kuweza kununua bidhaa katika  maduka ya Woolworths (Wreward Loyalty Card)  Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Kulia ni mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na baadhi ya viongozi wa uwanja wa samora.

  NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
  Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa (IRFA) kiko mbioni kujenga uwanja wake wa kisasa utakaosaidia kuendeshea ligi mbalimbali zikiwemo ligi za kimataifa hali itakayosaidia kuinua soka la mkoa huo .

  Akizungumza ofisini kwake mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava alisema wameamua kujenga uwanja wao ili kuepukana na adha wanayopata kutokana na kukosa sehemu ya kuendeshea ligi mbalimbali .

  Alisema tayari wameshapata eneo la hekari 14 katika eneo la kitwiru ndani ya manispaa ya Iringa na sasa kinachosubiriwa ni kumaliza mazungumzo kati ya chama hicho na manispa ya Iringa ili kuweza kumilikishwa eneo hilo ili liwe mali yao kabisa tofauti na apo awali ambao manispaa hiyo ilikuwa inataka kuingia nao ubia.

  “Tayari hili swala liko katika hatua za mwisho na tayari tumesha fanya mazungumzo tunataka tujenge uwanja wetu wenyewe wa kisasa ambao tunaweza kucheza mechi za kimataifa kwani tumekuwa tukipata tabu ya viwanja vya kuchezea na hii imechangia kwa kiasi kikubwa kuuwa soka la mkoa wetu ”alisema Kuyava.

  0 0

   Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kati, Balikulije Mchome(wakwanza kushoto)akisaidia kutandika shuka katika wodi ya Watoto hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma mara baada ya kukabidhi msaada wa mashuka na magodoro pamoja na vitu mbalimbali jana ktoka Vodacom Foundation wenye thamani ya zaidi shilimgi milioni 18,Katikati Doris Mollel mwanzilishi wa taasisi ya kusaidia watoto ya Doris Foundation,na Mkuu wa Idara ya watoto ya hospitali hiyo Dkt.David Mzava.
   Mganga Mfawidhi hospitali ya Rufaa ya Dodoma Dkt. Zainabu Chaula (kushoto)akikabidhiwa msaada wa mashuka na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kati,Mruta Hamisi jana kwa ajili ya wodi ya watoto hospitalini hapo,Vodacom Foundation ilitoa msaada wa mashuka 200,mito 200 na magodoro 100 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh milioni 18.
   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Chiku Galawa (katikati) akikabidhiwa msaada wa magodoro 100 na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kati,Mruta Hamisi (kushoto)Jumla ya magodoro 100 ,mashuka 200 na mito 200 vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 18 vilitolewa msaada na Vodacom Foundation hospitalini hapo kwa ajili ya wodi ya watoto, Anayeshuhudia kulia Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Zainabu Chaula.
   Mganga Mfawidhi hospitali ya Rufaa ya Dodoma Dkt. Zainabu Chaula (kushoto)akikabidhiwa msaada wa muto wa kulalia na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kati,Mruta Hamisi jana kwa ajili ya wodi ya watoto hospitalini hapo,Vodacom Foundation ilitoa msaada wa mashuka 200,mito 200 na magodoro 100 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh milioni 18 .Katikati Doris Mollel mwanzilishi wa taasisi ya kusaidia watoto ya Doris Foundation.

  0 0


  0 0

  Njile Gonga (28) Huyu ndiye Jangili anadaiwa kutungua helkopta katika pori la Akiba la Maswa lililopo katika Wilaya ya Meatu Mkoani, ambapo katika tukio hilo rubani wa helkopta hiyo Rodgers Gower (37) raia wa uingereza huku Mwenzake Nicholas Beste (43) raia wa Afrika Kusini akinususrika kifo.
   
  Iddy Mashaka (49) ambaye ndiye alikuwa Mkuu wa kitengo cha Interejensia katika hifadhi ya taifa Ngorongoro, ambaye anadaiwa kuwa kiunganishi Mkuu wa kutekeleza tukio la kutunguliwa kwa helkpta hiyo.
   Hali ya ulinzi na usalama ilivyokuwa imehimarsihwa mahakamani pamoja na kituo cha polisi Bariadi leo hii.
   Watuhumiwa wakiwa ndani ya gari la polisi, baada ya kufikishwa kituo cha polisi Bariadi wakitokea wilayani Meatu kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.
  WATUHUMIWA wa tukio la kutungua ndege aina ya Helkopta na kumuua rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa uingereza lilitokea mnamo tarehe 29/01/2016 katika pori la akiba Maswa wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, leo (jana) wamefikishwa mahakani kusomewa mastaka yanayowakabili.

  Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama ya Mkoa wa Simiyu, chini ya ulinzi wa mkali wa askari polisi, huku umati mkubwa wa wananchi wa mji wa bariadi waifurika kushuhudia watuhumiwa hao.

  Akiwasomea mashtaka watuhumiwa hao Wakili mwandamizi wa serikali Mkoa wa Simiyu Yamiko Mlekano alisema kuwa washitakiwa wote 9 wanakabiliwa na kesi tatu ambazo ni Uhujumu uchumi, mauaji pamoja na umiliki wa siraha bila ya kibali cha serikali zenye mashtaka tofauti.

  Katika kesi ya Uhujumu uchumi iliyosomwa chini ya Hakimu mkazi mfawidhi mwandamizi wa mahakama hiyo John Nkwabi katika shtaka la kwanza mtuhumiwa namba moja Iddy Mashaka (49) anatuhumiwa kujihusisha na kuratibu tukio la uhujumu uchumi kinyume na kifungu 4(1)(d) sura (57) (1) na 60 (2) cha makosa ya uhujumu uchumi sheria namba 200 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

  Mlekano alisema kuwa katika kosa hilo mshitakiwa kati ya tarehe 6 januari na 1/02/2016 katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu aliwashauri Mshitakiwa namba mbili Shija Mjika (38) kuua wanayama wasiyoruhisiwa kama tembo.

  Katika shtaka la pili wakili huyo aliwataja watuhumiwa namba mbili hadi tisa ambao ni Shija Mjika (38) Njile Gunga (28), Dotto Pangali (42) Moses Mandagu (48) Dotto Huya (45), Mwigulu Kanga (40) Mapolu Njige (50) pamoja na Mange Barumu (47), watuhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi.
  Katika shtaka hilo wakili aliieleza mahakama kuwa kati ya tarehe 21/01/2016 na 29/01/2016 katika wilaya ya Meatu, watuhumiwa hao walipanga na kuratibu tukio la kuwinda wanyama aina ya tembo bila ya kibali cha serikali.

   Hata hivyo wakili huyo alieleza kuwa katika shtaka la tatu watuhumiwa namba mbili hadi tisa waliotajwa hapo mwanzo, watuhumiwa kujihusisha na uwindaji wa wanyama wasiyoruhusiwa kinyume na kifungu 47(a)(aa) cha sheria namba 5 ya mwaka 2009 sambamba na sura 14 (a) na kifungu 57 (1) cha uhujumu uchumi sura 200 iliyofanyiwa marekebisho 2002.

  Alisema katika shataka hilo mnamo kati ya tarehe 26/01/2016 na 29/01/2016 katika hifadhi ya Mwiba katika kijiji cha Makao wilayani Meatu watuhumiwa walimuua tembo mwenye dhamani ya shilingi Milion 32,891,100 bila ya kibali cha serikali.

  Katika shtaka la nne watuhumiwa namba mbili hadi tisa wanatuhumiwa kwa kosa la kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria namba 86(1)(2)(b) cha uhuwifadhi wa wanyama pori sheria No 5/2009 sambamba na sura ya 14(d) na sura 57(1) cha uhujumu uchumi sura ya 200.

  Katika maelezo ya kosa hilo ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa kati ya 29/01/2016 na tarehe 6/02/2016 katika wilaya ya meatu mkoa wa simiyu walikamatwa na nyara za serikali ambazo ni meno ya tembo yenye uzito wa kilo 31 yenye thamani Milioni 32,891,100 bila ya kibali cha serikali.

  Katika shtaka namba tano watuhumiwa namba moja na mbili ambao ni Iddy Mashaka (49) pamoja na Shija Mjika (38) wanatuhumiwa na uuzaji wa nyara za serikali kinyume na kifungu cha sheria 84(1) cha uhuwifadhi wa wanyama pori sheria No 5/2009 sambamba na sura ya 14(b) na sura 57(1) cha uhujumu uchumi sura ya 200.
   
  Katika kosa hilo wakili alisema kuwa kati ya tarehe 6/01/2016 na tarehe 1/02/2016 katika wilaya a Meatu Mkoani Simiyu, watuhumiwa walikamatwa wakiwa wanajihusisha na uuzaji wa nyara za serikali bila ya kibali.

  Hata hivyo katika kesi namba mbili ya Mauaji wakili Mlekano aliiambia mahakama kuwa watuhumiwa ambao ni Shija Mjika (38), Njile Gunga (28) Dotto Pangali ( 42) pamoja na Moses Mandago (28) wanashtakiwa kwa kosa la mauaji kinyume che sheria ya 196 na 197 cha kanuni ya adhabu namba 16 iliyofanyiwa mwaka 2002.

  Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao mnamo tarehe 29/01/2016 katika hifadhi ya Mwiba kijiji cha Makao wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu walimuua rubani wa ndege aina ya helkopta rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa uingereza.

  Katika kesi zote Mbili kwa mujibu wa hakimu huyo alisema kuwa watuhumiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo, ambapo keshi hizo zilihairishwa mpaka terehe 24/02/2016 mpaka zitakapotajwa tena.

  Sambamba na hayo katika kesi ya tatu ambayo ni kukutwa na siraha kinyume cha sheria na pasipo leseni ilisikilizwa katika mahakama hiyo chini ya Hakimu mfawidhi wa wilaya Bariadi Mary Mrio ambapo watuhumiwa walikabiliwa na mashitaka matano.

  Watuhumiwa hao ni Mange Buluma,Shija Mjika,Dotto PanganiNjile Ngunga,Moses Mandagu,Dotto Huya na Mwigulu Kanga ambapo baadhi yao walikiri kumiliki siraha kinyume cha sheria pamoja na riasi akiwemo njile aliyetungua helkopta hiyo.


  Watuhumiwa hao ambao Shija Mjika, Moses Mandagu, Njile Ngunga pamoja na Dotto Pangani walikiri mashtaka mawili ambayo ni kukutwa na siraha aina ya bunduki Riffle 303 Namba 06490 kinyume cha sheria pamoja na risasi mbili.

  Hata hivyo Njile Ngunga pamoja na Moses Mandagu walikiri pia katika shtaka la tatu, nne pamoja na tano la kukutwa na siraha bila ya kibali, kumiliki risasi bila ya kibali, pamoja na kumiliki tena risasi kinyume cha sheria huku wengine kati ya hao wakikana makosa hayo.

  Hata hivyo mahakama haikuweza kutoa hukumu juu ya watuhumiwa hao waliokiri kutokana na vielelezo kutokuwepo mahakamani hapo, ambapo kesi hiyo ilihairishwa mpaka kesho (Leo).
  Watuhumiwa wote walirudishwa rumande.

  0 0
 • 02/11/16--02:42: BEI YA MADAFU HII LEO.


 • 0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Ndg ,Hassan Khatibu Hassan kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,kabla alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Ndg. Hassan Khatibu Hassan baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja, kabla alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba.
  [Picha na Ikulu.]

  0 0

  Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya sekta ya afya unaofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, wadau hao wa Sekta ya afya wanajadiliana mambo mbalimbali na baada ya kumalizika kwa mkutano huo kutakuwa na kusaini makubaliano yaliyofikiwa kwa utekelezaji katika sekta ya afya hapa nchini , Katika picha kulia ni Carol Hannon Mshauri wa Afya katika ubalozi wa Ireland nchini Tanzania.
  Carol Hannon Mshauri wa Afya katika ubalozi wa Ireland nchini Tanzania akizungumza katika mkutano huo Kushoto ni Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.
  Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katikati na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Suleman Jafo wa tatu kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya afya kwenye mkutano unaofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
  Mwaka 2015 Serikali ya Tanzania ilikamilisha Mpango wa Afya katika Jamii na kuanzisha mafunzo kwa kada mpya za Wahudumu wa Afya ya Jamii (Community Health Workers). Wafanyakazi hawa wana jukumu kubwa kuifikishia jamii huduma za afya za msingi.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
  MPANGO  mkakati  wa Sekta ya Afya  wa  Mwaka 2016 /2017 unahitaji sh.trioni 21 katika kuweza kutekeleza maeneo nane  ya utoaji wa huduma kwa wananchi.

  Akizungumza na wadau wa afya leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema serikali itahakikisha inakwenda sambasamba na mpango huo  kutokana na kugusa kila sehemu ikiwa ni lengo la kumfikia mwananchi wa kuweza kupata huduma ya afya.

  Amesema eneo mojawapo ni utoaji wa kinga ya afya kwa jamii pamoja na elimu juu ya magonjwa kwa kuweka wataalam wenye mafunzo kutoka sehemu husika.
  Ummy amesema serikali imeanza kutoa mafunzo kwa wafanyakazi 4000 ambao watafanya kazi na jamii moja kwa moja katika utoaji wa kinga ya afya pamoja na elimu juu ya magonjwa mbalimbali.
  Amesema katika eneo la pili ni mgawanyo wa rasilimali fedha kwa kuhakikisha kila kituo kinapata fedha na takwimu zake zitahifadhiwa juu ya fedha wanazozipata kwa ajili ya dawa na vifaa tiba.

  Waziri, Ummy, amesema katika eneo la tatu ni juu ya uchangiaji wa huduma ya afya bado ni changamoto hivyo katika mpango wanatarajia kupeleka mswaada bungeni kwa kuwa na mfuko  moja ambao kila mwananchi atachangia kwa ajili ya huduma ya afya.

  Aidha amesema katika mpango huo wataangalia watumishi wa sekta ya afya kuwa kila sehemu wanakuwepo katika kuweza kutoa huduma kwa wananchi ipasavyo pamoja na masilahi ya motisha kwa watumishi walio pembezoni.

  Waziri Ummy amesema katika eneo lingine katika mkakati huo ni kuweka ufumbuzi wa wa upatikanaji fedha na vyanzo vyake vikaeleka na uendeshaji pamoja na rasilimali watu wanapatikana.
  Amesema sehemu ya nane ni utoaji wa nyota  katika vituo vya afya ambavyo vitapimwa kutokana na utoaji wake kwa kuanzia nyota ya kwanza hadi ya nne.

  Mkuruegenzi Mtendaji wa Sikika, Irenei Kiria amesema hayo mambo yalikuwa yakisubiliwa kwa muda mrefu na sasa serikali imeamua kuwajibika katika utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi wake.

  Amesema kuwa mpango mkakati ukienda kama ulivyopangwa jamii ya kitanzania itaweza kupata huduma bora ya afya kutokana na mikakati iliyomo katika mpango huo.

older | 1 | .... | 1120 | 1121 | (Page 1122) | 1123 | 1124 | .... | 3278 | newer