Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 110 | 111 | (Page 112) | 113 | 114 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick M. Werema akitoa nasaha wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya majadiliano kwenye mikataba ya kimataifa. Kushoto ni Lawrence Masha na kulia ni Michael Kamba Mkurugenzi wa Mikataba.
  Baadhi ya mawakili wa serikali waliohuduria mafunzo ya majadiliano ya mikataba ya kimataifa wakimsikiliza Mwansheria Mkuu wa Serikali(hayupo pichani) Jaji Frederick M. Werema. Mafunzo hayo yanaendelea Shule ya Sheria Tanzania.
  Jaji Frederick M. Werema Mwanasheria Mkuu wa Serikali akijadili jambo na Lawrence K. Masha mmoja ya wabia wa kutoka DLA Piper waliowezeha mafunzo ya majadiliano ya mikataba ya kimataifa yanayoendelea katika Shule ya Sheria Tanzania.
  Mwanasheri Mkuu wa Serikali Jaji Frederick M. Werema(wa katikati) akibadilishana mawazo na wawezeshaji wa mafuzno ya majadiliano ya kimataifa kutoka DLA Piper. Kulia mwenye miwani ni Jaji Dkt. Gerald Ndika Mkuu wa Shule ya Sheria.
  Mwansheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick M. Werema(wa tatu kutoka kushoto waliokaa) kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo ya majidiliano ya mikataba ya kimataifa kutoka DLA Piper.

  0 0

  It is now Six Years since you left us. May Good Lord Rest Our Sweet Mother Omwana Maria’s Soul in peace Amen.

  Omwana Maria is fondly missed by her children, family and friends.

  Real in memory of our sweet mother, you were a precious gift from God above. So much beauty, grace and love. You touched our hearts in so many ways. Your smile so bright even on the bad days.

  You heard God’s whisper calling you home, you didn’t want to go and leave us alone. You loved us so much, you held on tight, till all the strength was gone and you could no longer fight. You knew you couldn’t make him wait anymore. So you gave your hand to God and slowly drifted away. Knowing that with our love we will be together again someday.

  But little by little, we begin to remember not just that you died, but that you lived. And that your life gave us memories too beautiful to forget. You can only have one Mother Patient kind and true, no other friend in all the world will be the same to you. May your souls rest in Peace,

  Dear Family and Friends, There will be a memorial mass service at St. Joseph Cathedral (Dar es Salaam) on Thursday from 1300-1330hours 25th April 2013 and on Sunday 28th April 2013 any mass you wish to attend.

  0 0

  Mchungaji mtarajiwa John Shabani (kushoto) akikabidhiwa shahada yake na Askofu Kitonga (Kiongozi wa makanisa ya Redeemed duniania), baada ya kuhitimu Mafunzo katika chuo cha kimataifa cha huduma (International school of Ministry - ISOM) chenye makao makuu New York Marekani. Ilikuwa ni siku ya furaha kwa mwalimu huyo wa muziki wa injili Afrika mashariki bwana John Shabani, baada ya kuhitimu mafunzo yake hayo kwenye chuo hicho cha kimataifa. John ambaye amekuwa na ndoto za kujiendeleza sana katika elimu mbalimbali, amekuwa miongoni mwa wanafunzi waliofanya vizuri katika chuo hicho. Mchungaji huyo mtarajiwa anategemea kujiunga na chuo kimoja huko marekani ili kuendelea zaidi na masomo yake, pia amewahasa waimbaji wenzake wa injili kuwa na mpango wa kujiendeleza ki-elimu. Mahafali hayo yamefanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ki-dini na serikali. Makao makuu ya chuo yaliwakilishwa na Dr. Lee kutoka Marekani.
  Picha ya pamoja 

  0 0

  Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, Mchumi Mwandamizi wa Mkakati wa kupunguza umasikini Afrika Bw. Yutaka Yoshino pamoja na mchumi wa Wizara ya Fedha Bw. Patrick Pima wakibadilishana mawazo wakati wa chakula hicho.
  Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Silvacius Likwelile, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Burundi na Uganda Bw. Philippe Dongier pamoja na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa pia Gavana wa Banki kuu alikuwepo mwisho kulia.
  Kutoka kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Harry Kitilya pamoja na Katibu wa Waziri wa Fedha Bw. Omary Khama wakati wa chakula cha pamoja.
  Ujumbe wa Tanzania katika chakula cha pamoja. Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano Ubalozi wa Tanzania-Washington DC Bi Mindi Kasiga, Afisa Itifaki Wizara ya Fedha Bw. Cyprian Kuyava, Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Prof. Longinus Rutasitara, watatu wanaofuata ni wachumi wa Wizara ya Fedha Bw. Erasto, Patric Pima, Veronica Maina na mchumi wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Dickson Lema.
  Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, Mdau wa Ubalozini Bw. Baraka Daudi na Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Fedha Bi. Eva Valerian wakitabasamu mara baada ya chakula cha pamoja katika ofisi za ubalozi wa Tanzania Washington DC.
  Baadhi ya viongozi wa Tanzania waliohudhuria mikutano ya majira ya kipupwe katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania Washington DC. Waliokaa, kutoka kushoto ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Harry Kitilya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu, Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa Kaimu Balozi wa Tanzania Washington DC Bibi. Lily Munanka na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba.
  Ujumbe wa Tanzania katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania Washington DC aliyevaa blauzi nyekundu Bibi. Lily Munanka baada ya chakula cha pamoja.

  0 0  Huawei’s Technologies Tanzania Product Manager Zeng Tao (left) briefs the Ministry of Communication Science and Technology, Assistant Director Manyiri Isack (right) on one of Huawei’s new products during the road show event held at Kilimanjaro Hotel in Dar es Salaam yesterday. (Photo by our correspondent)  
  ========  =======  ========
  Huawei showcases convergent communication solutions in Dar es Salaam


  By Our Correspondent

  HUAWEI, a leading global information and communications technology (ICT) solution provider yesterday held a one day road show in Dar es Salaam geared towards showcasing the company’s various products.

  The company during the event exhibited its unique omnipresent connectivity technology, including Smart Fixed-Mobile Convergence (FMC) bearer network and the SIngleFAN solutions, eSpace IVS (intelligent video surveillance ) and Video conference Solution, Huawei Storage and Server Portfolio, Huawei Distribute Cloud Data Center Solution, Huawei Container and Modular Data Center(IDS) Solution and Huawei Virtual Desktop Infrastructure(VDI) Solution among others.

  Speaking during the event graced by the Assistant Director, Manyiri Isack from the Ministry of Communication, Science and Technology, the Huawei’s Technologies Tanzania Channel Director Mr. Moses Hella said the rapid development of mobile technologies has accelerated mobile broadband from megabit to gigabit levels via the generation of various service applications.

  “Mobile broadband has redefined the way we communicate and live. With new and innovative business models emerging, mobile broadband presents the telecom industry with significant challenges and opportunities,” he said.

  Mr Hella said Huawei has developed the value growth solution that will see local operators benefiting significantly from Mobile Broadband (MBB) and its offerings.

  He reiterated that Huawei will continue with the road shows the whole week. Road shows will also be conducted at the Airtel Tanzania, Tigo and Vodacom offices.  

  He underscored his company’s commitment in supporting growth of Tanzania’s ICT sector urging that ICT is an enabler of technology innovation, driving social and economic development, and creating value for individuals and society as a whole.

  “We have seen companies in the telecom industry striving to bridge the digital divide - so everyone can afford to enjoy the benefits of communications. Some have moved farther to shift their focus from ‘a phone for everyone’ to ‘broadband for everyone’, to enable users to tap the infinite possibilities that a connected world presents,” he said.

  On his part, the Assistant Director from the Ministry of Communication, Science and Technology, Mr Manyiri Isack said the development of ICT sector in the country will enable easy and effective communication among people.

  “We thank Huawei for supporting our government especially in the ICT sector in making sure our people have better and effective ways of communication. We believe that the introduction of these new technologies will help people have easy access to information and have more open communication,” said Isack.

  The road show apart from attracting Dar es Salaam residents, targeted telecom service providers that included Tigo, Airtel Tanzania, and Vodacom Tanzania.

  0 0


  Waziri mkuu mstaafu, Mh. Frederick Sumaye akizungumza kwenye sherehe za mahafali ya sita ya wahitimu 1029 wa chuo cha ualimu mjini Singida. Kulia ni kaimu mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi na kushoto ni mmiliki wa chuo cha ualimu Singida, Martin Makuza.
  Mkurugenzi mtendaji wa Prime Education Network (PEN) Tanzaia, Martini Mkauza akitoa nasaha zake kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo cha ualimu cha Singida mjini. Kulia ni waziri mkuu mstaafu,Frederick Sumaye.
  Waziri mkuu mstaafu, Mh.Frederick Sumaye akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu 1,029 wa chuo cha ualimu Singida.
  Baadhi ya wahitimu wa chuo cha ualimu Singida,wakifuatilia kwa makini hotuba ya waziri mkuu mstaafu Mh. Frederick Sumaye (hayupo kwenye picha) wakati akizungumza kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo hicho.
  Kikundi cha uhamasishaji cha kijiji cha Manguanjuki manispaa ya Singida kikitoa burudani kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo cha ualimu mjini Singida.
  Mmoja wa waandishi wa habari,Damiano Mkumbo akiwajibika kupata picha safi kwenye sherehe za mahafali ya sita ya chuo cha ualimu mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).

  0 0

  MWENYEKITI WA TUME YA KUDHIBITI UKIMWI TANZANIA DR FATMA MRISHO AKIMKABIDHI BI KHADIJA MWANAMBOKA -MWENYEKITI WA TANZNAIA MITINDO HOUSE BARUA YA KUTAMBUA MCHANGO WAO WA KUPIGA VITA UGONJWA WA UKIMWI NCHINI NA KUSAIDIA WATOTO TAYIMA WANAOSHI NA VIRUSI VYA UKIMWI KULIA NI KAMISHNA WA TACAIDS BI FARAJA KOTTA NYALANDU.

  0 0

   Wakazi wa Mji wa Shinyanga Mjini,wakiwa wamebebelea Vikombe vya Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager kule nchini Ghana hivi karibuni.Safari Lager ipo katika ziara ya kuutembeza ushindi huo mikoani kwa wanywaji wa Bia hiyo,ambapo leo hii wapo Mkoani Shinyanga wakisherehekea ushindi huo na wakazi wa Mkoa huo.
  Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Shinganya Mjini wakiwa wamekusanyika kwenye Stendi Kuu wa Mabasi yaendayo Mikoani kushuhudia Burudani iliyokuwa ikitolewa na Kundi la Muziki wa Dansi la Safari Lager ambalo lipo katika ziara hiyo ya kutembeza Vikombe vya ushindi wa Bia yao ya Safari Lager.


  0 0


  0 0

  Mnamo tarehe 23 April, 2013 majira ya saa tisa alasiri, huko wilayani Liwale mkoani Lindi, kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni wakulima wa Korosho walijaribu kuzuia gari lililokuwa na malipo ya korosho wakipinga malipo ya pili ya Korosho na kuanza kufanya vurugu na uhalibifu mkubwa wa mali, ambapo mpaka sasa taarifa za awali zinaonyesha kuwa nyumba kumi na nne (14) zimechomwa moto, baadhi ya mifugo imejeruhiwa na kuangamizwa na kufanyika uharibifu wa miundombinu ya barabara.

  Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema ametuma timu maalum ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCP Issaya Mngulu kwenda kuongeza nguvu mkoani humo kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa katika kuhakikisha kuwa hali ya amani na utulivu inarejea haraka na wale wote waliohusika kufanya vitendo vya uhalifu wanakamatwa na kufikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake, mpaka sasa jumla ya watuhumiwa kumi na tisa (19) wamekamatwa kwa mahojiano.

  Aidha, Jeshi la Polisi nchini linalaani vikali vitendo hivyo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi na badala yake kuwataka wananchi kufuata njia ya kufanya majadiliano pale ambapo kutakuwa na migogoro ya aina yoyote ndani ya jamii. Majadiliano yatasaidia kuepusha madhara yanayojitokeza ikiwemo watu kupoteza maisha, uhalibifu wa mali na misongamano ya wahalifu magerezani.

  Wakati hatua hizo za kisheria zinaendelea kuchukuliwa, Jeshi la Polisi linawaomba wananchi kuwa watulivu na waendelee kutoa ushirikiano ili kuweza kuwabaini wahalifu hao wachache wanaochochea vitendo vya vurugu na kufanya uhalibifu wa mali ili hatiamae waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Taarifa zaidi juu ya tukio hili zitaendelea kutolewa na uongozi wa mkoa wa Lindi baada ya tathmini ya uharibifu uliofanyika kukamilika.

  Imetolewa na:-
  Advera Senso- SSP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi (TZ).

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wanne wanaoziwakilisha nchi zao hapa.Walioziwasilisha hati zao ni pamoja na Balozi Mpya wa Morocco nchini Tanzania Mhe.Abdelilah Benryane, Balozi mpya wa Hungary Mhe.Sandoz Juhasz,Balozi mpya wa Austria Mhe. Christian Hasenbichler na Balozi Mpya wa Chille nchini Mhe.Konrad Paulsen.Pichani Balozi Mpya wa Morocco Mhe.Abdelilah Benryane akiwailisha hati zake za utambulisho kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.(picha na Freddy Maro)
  Balozi Abdelilah Beryane wa Morocco.
  Balozi mpya wa Hungary Sandoz Juhasz.
  Balozi Mpya wa Austria nchini Tanzania Christian Hasenbichler.
  Balozi Mpya wa Chile nchini Tanzania Konrad Paulsen.

  0 0

  UONGOZI wa Yanga umewataka mashabiki wao kujitokeza kwa wingi kwenye mechi yao dhidi ya Coast Union siku ya Mei Mosi kushangilia kutawazwa rasmi mabigwa wapya wa Tanzania.

  Yanga ambayo ina pointi 56 imebaikiza pointi moja kuwavua rasmi wapinzani wao Simba ubingwa wa Tanzania na kwamba mchezo huo wa Coast Union ni muhimu kwao kwa vile ndio utakaoamua mustakabari wa ubingwa wao.

  Katibu mkuu wa Yanga Laurance Mwalusako alisema kuwa mashabiki wao wajitokeze kwa wingi ili kuwatia hamasa wachezaji wao na kuweza kutoka na pointi tatu muhimu katika mchezo huo.

  Alisema pamoja na kwamba bado pointi moja watangaza ubingwa lakini malengo yao ni kuakikisha wanachukua pointi zote sita walizobakiza na kuchukua ubingwa kwa kishindo.

  Mwalusako alisema mashabiki wao wanatakiwa kuja kwa wingi siku hiyo ili kushuhudia timu yao ikikabidhiwa ubingwa wa halali walioupata baada ya safari ya miezi 10 kutoka mwaka jana mwezi wa nane.

  Hata hivyo uenda Yanga ikatawazwa mabingwa mapema kama Coast Union wataifunga Azam katika mchezo wao utakaochezwa kesho katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

  Katika hatua nyingine Uongozi wa Yanga umekabidhi cheti cha shukurani kuwa kuitumikia Yanga kwa miaka 11 mfululizo toka miaka ya 1960 aliyekuwa mchezaji wa klabu hiyo ambaye pia ni marehemu Athuman Kilambo kilichotokea Machi 10 mwaka huu.

  Mwalusako alisema kuwa cheti hicho kimekwenda sambamba na rambi rambi ya shilingi 500,000 ambayo walitoa siku ya msiba.

  Alisema klabu hiyo imeamua kuwatunza vyeti wachezaji wake wa zamani na kwamba wameanza kwa mchezaji huyo ambaye ni marehemu na wanaendelea kutoa vyeti hivyo kwa wachezaji wengine ambao wameitumikia Yanga kwa kipindi kirefu.

  0 0

  Wazii wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Samia Suluhu, akizungumza na Balozi wa Uingereza Nchni Tanzania, Diana Melrose, wakati alipofika Ofisini kwa Waziri Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam, leo Aprili 24, 2013 kwa mazungumzo. Picha na Ali Meja

  0 0

  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,wama, Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Jhpiego nchini Tanzania, Bi Maryjane Lacoste kwenye hoteli ya Doubletree huko Masaki kulikofanyika sherehe ya kutimiza miaka 40 ya shirika hilo tarehe 23.4.2013.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Dr. Maryrose Giattas, Cervical Cancer Prevention Program Adviser wa Shirika la Jhpiego kwenye maonyesho ya huduma mbalimbali zitolewazo na shirika hilo. Maonesho hayo yalifanyika katika hoteli ya Doubletree ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 40 ya shirika hilo.
  Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Dr. Hokororo wa shirika la JHPiego juu ya kuhifadhi vifaa vinavyotumika katika suala zima la afya ya mama na mtoto.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na baadhi ya viongozi waliohudhuria sherehe ya kutimiza miaka 40 ya shirika la Jhpiego huko Doubletree hotel Masaki. Kulia kwa Mama Salma ni Dr. Leslie Mancuso, Rais na Mtendaji Mkuu wa Jhpiego akifuatiwa na Bi Sharon Cromer, Mkurugenzi wa Shirika la USAID nchini Tanzania. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid akifuatiwa na Dr Allan Damiba, Jhpiego Senior Vice President na wa mwisho ni Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Sophia Mjema, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
  Baadhi ya wageni waalikwa kwenye sherehe za kutimiza miaka 40 ya shirika la Jhpiego wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akihutubia kwenye sherehe za kutimiza miaka 40 ya shirika la JHPiego kwenye hoteli ya Doubletree huko Masaki jijini Dar es Salaam tarehe 23.4.2013.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwashirikiana na viongozi wengine kukata keki ya kutimiza miaka 40 ya shirika la Jhpiego zilizofanyika katika hoteli ya Doubletree. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID Bi. Sharon Cromer, Rais na Mtendaji Mkuu wa Jhpiego Dr. Leslie Mancuso, Mama Salma, Bi Maryjane Lacoste, Mkurugenzi wa Jhpiego nchini Tanzania, Dr. Seif Rashid, Naibu Waziri wa Afye na Ustawi wa Jamii na Dr. Allan Damiba, Jhpiego Senior Vice President.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akigongainisha glass yake na Rais na Mtendaji Mkuu wa Jhpiego Dr. Leslie Mancuso ikiwa ni kusherehekea kutimiza miaka 40 kwa shirika hilo.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipongezana na Rais wa Jhpiego Dr. Leslie Mancuso mara baada ya kukata keti ya kutimiza mika 40 ya shirika hilo katika sherehe zilizofanyika huko Doubletree hotel tarehe 23.4.2013.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaaga kwa kuwapungia mikono washiriki waliohudhuria sherehe za kutimiza miaka 40 ya shirika la Jhpiego. PICHA NA JOHN LUKUWI

  0 0

  Warembo watakaowania taji la Redd's Miss Dar Indian Ocean wakimsikiliza kwa Umakini Mkurygenzi Mkuu wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga wakati alipowatembelea warembo hao kwenye kambi yao ya Mazoezi.Kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania,Albert Makoye.

  HATUA za awali za kumsaka Redd’s Miss Tanzania sasa zinaanza kushika kasi, wakati wiki hii kutakapokuwa na kinyang’anyiro katika vitongoji kadhaa vya kusaka warembo wao.

  Kazi kubwa itaanza Morogoro, wakati atakaposakwa Redd’s Miss High Learning atakayeuwakilisha mkoa huo katika kumpata mrembo kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu, shindano litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Sirvoy.

  Wakati Morogoro Miss High Learning akipatikana kesho, shughuli pevu ipo keshokutwa (Jumamosi) pale kutakapokuwa na shindano la kumsaka Redd’s Miss UDOM, litakalofanyika katika Ukumbi wa Kilimani, Dodoma.

  Siku hiyo pia atapatikana mwakilishi wa vyuo vya elimu ya juu kutoka Kagera na Mwanza, shindano ambalo litafanyika Yacht Club, Mwanza.

  Akizungumzia kuhusu Redd’s Miss Morogoro High Learning, mratibu wa shindano hilo, Verdian Kamugisha alisema kila kitu kimekamilika na kutakuwa na burudani za kufa mtu.

  “Tumekamilisha kila kitu na warembo wote wako katika hali nzuri na kutakuwa na burudani za kumwaga, wakazi wa Morogo wanatakiwa kuja kwa wingi kushuhudia kile kitakachotukia,” alisema.

  Mratibu wa Shindano la Redd’s Miss UDOM, Rachel Matina naye alisema kila kitu kwao kipo tayari na watu wanatakiwa kufika kwa wingi kushuhudia jinsi warembo kutoka Chuo Kikuu Dodoma, walivyopania kulitwaa taji la Redd’s Miss Tanzania mwaka huu.

  Joseph Rwebangira wa anayeratibu shindano la wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mikoa ya Kagera na Mwanza naye alikiri kukamilika kwa maandalizi yote na kutakuwa na burudani za kila aina siku ya onyesho.

  Upande wa kanda ya kaskazini mwa nchi kutakuwa na shindano la kumsaka mrembo wa kitongoji cha Hai ambapo shindano hilo linatarajiwa kufanyikia katika ukumbi wa Hotel ya Snow View na mkoani Mara katika kitongoji cha Tarime shindano litakuwa katika ukumbi wa JJ Club na maandalizi kwa sehemu zote husika yameshakamilika kwa kiwango kikubwa.

  Redd’s Miss Tanzania kwa sasa inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

  0 0
 • 04/24/13--09:41: Article 12
 • 0 0


  Jengo la ghorofa nane lililokuwa na viwanda vya nguo na maduka limeporomoka leo mchana nje ya jiji la Dhaka, Bangladesh, na kuua watu takriban 100 na kujeruhi wengine zaidi ya 1000, maafisa wamesema.
  Vikosi vya zimamoto na askari jeshi wanaendelea kufukua vifusi vya jengo hilo lililo maeneo ya Savar, ya jiji la Dhaka. TV zimeonesha wafanyakazi wanawake wakiokolewa wengi wakiwa wamepoteza fahamu. Askari wa zimamoto mmoja amenukuliwa akisema takriban watu 2000 walikuwamo mjengoni wakati linaporomoka
  Biashara ya nguo ya Bangladesh imekumbwa na majanga ya moto na ajali zingine kwa miaka kadhaa, licha ya juhudi za kuboresha usalama pahala pa kazi. Mwezi Novemba mwaka jana wafanyakazi 112 walikufa katika mlipuko katika kiwanda cha nguo na kuzua mkanganyiko kwa wafanyabaishara wa kimataifa wa nguo wanaopata bidhaa hiyo Bangladesh.
  Afisa mmoja katika chumba cha mikakati ya uokoaji kilichowekwa ili kutoa taarifa kwa watu, alisema watu 96 walikuwa wamethibitishwa kufa na zaidi ya 1000 kujeruhiwa. Madaktari katika hospitali za jirani wamekiri kuzidiwa na majeruhi walioletwa kwao.
  Mkuu wa polisi wa eneo hilo, Mohammad Asaduzzaman, alisema wamiliki wa viwanda hivyo vya nguo mjengoni humo walidharau onyo la kutoruhusu wafanyakazi mjengoni baada ya nyufa kuonekana katika baadhi ya kuta jana. Katika jengo hilo mlikuwa na viwanda vitano vilivyoajiri zaidi kinamama.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya akizungumza na timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Mifupa (MOI) mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kuhudumia mamia ya wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa ya Maweni mkoani humo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno akitoa neno la shukrani kwa kazi kubwa iliyofanywa na madaktari hao mpango ambao unatekelezwa na NHIF (Kutoka kulia kwake ni Dk. Vence wa MOI, Dk. Kisenge na Dk. Makia wa Muhimbili.
  Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi, Dk. Frank Lekey akieleza namna kazi ya huduma kwa wagonjwa ilivyotekelezwa na madaktari hao.


  0 0


  Habari wadau
  Anaitwa Edwin Moshi a.k.a Eddymoblaze.
  Ni mwanalibeneke  anayemiliki mtandao wa:
  Anapenda kuchukua fursa hii kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kumfikisha salama siku ya leo Jumatano April 24 ambapo anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa. Kwa wanalibeneke wenzie anawashukuru kwa ushirikiano wao katika hili bila kusahau familia yake

  Happy birthday Edwin Moshi!

  0 0  Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu 
  Katibu Mkuu wa CHADEMA  Mhe. Zitto Kabwe
  --
  Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba

  “Moja, mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama yetu mie najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma haitwi hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu.

  Pili, hili Ni suala la polisi. Lipo polisi na linashughulikiwa na polisi. Nisingependa kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na polisi. Mama yangu Ni mama wa kawaida wa kitanzania kama mama mwingine yeyote yule. Matukio ya namna hii yamezagaa nchi nzima. Hivyo suala lake litashughulikiwa kama yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote ya Watanzania. Polisi wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka zitachukuliwa.

  Ushauri- tuwe makini na “Agente provocatuers” au in English “provocation agents” nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against provocations. Nadhani mmenipata”

  Nawatakia Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa Taifa letu na kuimarisha Umoja na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini na ugandamizaji.

  Majibu haya ameandika kupitia mtandao wa Kijamii wa facebook.

older | 1 | .... | 110 | 111 | (Page 112) | 113 | 114 | .... | 3284 | newer