Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kufadhili Michuano ya Kimataifa ya Timu za JKU na Mafunzo kwa Kununua Tiketi Zote za Michezo hiyo na kutowa Bure kwa Wananchi Kujionea Michuano Hiyo ya Kombe la CAF Zanzibar

$
0
0

 Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhiwa  Tiketi ya Mchezo wa JKU na Gaborone United Club na Kiongozi wa Timu ya JKU Khamis Mohammed, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar 
 Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhi Milioni tano fedha za mauzo ya Tiketi ya Mchezo wa JKU na Timu ya Gaborone United Club Kiongozi wa Timu ya JKU Khamis Mohammed, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar 
Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhi Milioni tano fedha za mauzo ya Tiketi ya Mchezo wa Mafunzo na AS Vita Club ya Congo Kiongozi wa Timu hiyo Khamis Ali Machenga, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar 
Meneja wa Makampuni ya Hoteli ya Zanzibar Ocean View Zanzibar Jacob Makundi akimkabidhi Milioni tano fedha za mauzo ya Tiketi ya Mchezo wa Mafunzo na AS Vita Club ya Congo Kiongozi wa Timu hiyo Khamis Ali Machenga, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Kampuni ya Zanzibar Ocean View Imenunua tiketi hizo zote za mchezo huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wapenzi wa Michezo Zanzibar kujionea Michuano hiyo ya CAF kujionea bure. makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Kilimani Zanzibar.

JK AIFAGILIA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM

$
0
0



SIMU.TV:  Viongozi wa CCM Mwanza wametakiwa kuhakikisha kuwa wanajenga ofisi katika ngazi zote za uongozi mkoani humo; https://youtu.be/NpTr_r90wgw
 SIMU.TV:  Tarafa ya Idodi mkoani Iringa ipo hatarini kukumbwa na mafuriko kufuatia mkondo wa maji wa mto Mapogoro kuhama; https://youtu.be/AfSbtI7MOy0
 SIMU.TV:  Mkuu wa wilaya Manyara alazimika kupiga marufuku ulaji wa nyama machinjoni kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kimeta;https://youtu.be/NKxuqyprRFQ
 SIMU.TV:  Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi jaji Lubuva amesema uchaguzi wa 2015 ulikuwa na mafanikio makubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma;https://youtu.be/wuSaqbH_dGo
 SIMU.TV:  Muajiri ampa kipigo mfanyakazi wa ndani na kumsababishia majeraha yaliopelekea mfanyakazi huyo kulazwa hospitali; https://youtu.be/ZV_G2Ce72o8
 SIMU.TV:  Ama kweli kufa kufaa, ucheleweshwaji wa mradi wa mabasi ya haraka Dar es salaam waleta shangwe kwa wafanyabiashara jijini; https://youtu.be/1X3qeYZVsWY
 SIMU.TV:  Askari watatu wafariki na watatu wengine kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisindikizia msafara wa viongozi kupinduka;https://youtu.be/wHZSv8SydlI
 SIMU.TV:  Shirikisho la ngumi nchini limewaomba wadau kujitokeza kusaidia mashindano ya klabu bingwa taifa yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam;https://youtu.be/2fb9c5LOCzk
 SIMU.TV:  Waziri mkuu Mh.Kassim Majaliwa amewataka waislamu pamoja na wananchi wote kusaidiana na Rais Magufuli katika kupambana na rushwa:https://youtu.be/eor6Jehuz_I
 SIMU.TV:  Zaidi ya kaya 60 mkoani Lindi zimeathiriwa na mvua kubwa iliyoambatana na mafuriko na kusababisha athari katika kaya hizo: https://youtu.be/-UiU7YGagKg
 SIMU.TV:  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro amezindua kampeni ya upandaji miti wilayani Rombo ili kuepuka uharibifu wa mazingira: https://youtu.be/CQZML8BtnFI
 SIMU.TV:  Wakazi wa Tabata kisiwani wameilalamikia serikali kutokana na ubovu wa barabara ambao umesababishwa na ujenzi wa viwanda:https://youtu.be/Gem44OvGwqk
 SIMU.TV:  Wazazi nchini wameombwa kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika mchezo wa tenisi ili kukuza vipaji vyao: https://youtu.be/527a3HxBQ5A


KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI PROF. JUSTIN NTALIKWA AFANYA ZIARA KATIKA KISIWA CHA SONGOSONGO KUSHUHUDIA UCHIMBAJI WA GESI ASILIA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PanAfrican Energy David K. Roberts (kulia) akimuelezea jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa wakati wa ziara yake huko Songosongo katika visima vya gesi asilia.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa katika visiwa vya Songosongo.

 PanAfrican Energy Operational SH Engineer, Onestus Mujemula akielezea jambo kwa wana habari katika ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini huko Songosongo kwenye visima vya gesi, kutoka kushoto ni PanAfrican Energy Country Chairman Patrick Rutabanzibwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa na CSR Manager Andrew Kashangaki (wakwanza kulia)

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa akipata maelezo ya mradi kutoka PanAfrican Energy Operational SH Engineer Onestus Mujemula kuhusu mradi wa uchimbaji gesi asilia katika visima vinne uliomalizika kwa kutumia mtambo wa kisasa wa “RIG”
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa akiongea na wana habari wakati wa ziara yake ya kikazi katika visiwa vya Songosongo.

SIMU TV: UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA LEO

Balozi Seif Ali Iddi aongoza matembezi ya kuadhimisha siku ya Sheria Zanzibar

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa wito kwa Majaji na Mahakimu Nchini kuacha kugugumizi katika utoaji wa haki ili kuondoa au kupunguza zaidi muda mrefu  unaochukuliwa na Majaji na Mahakimu hao katika kutoa hukumu kwa kesi zinazopelekwa Mahakamani.
Alisema kigugumizi hicho mbali ya kulalamikiwa kwa kipindi kirefu na Wananchi   walio wengi lakini pia kinachangia sana kuuondolea  Heshima yake Muhimili huo ukiwa miongoni mwa  Mihimili Mitatu ya Dola.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa wito huo wakati akizungumza na Majaji, Wanasheria na Mahakimu ndani ya Jumla la Sheria Zanzibar baada ya kuyaongoza Matembezi ya maadhimisho ya Siku ya sheria yaliyoanzia Mahakama Kuu Vuga kupitia Benbella, Michenzani, Kituo cha Polisi madema na kumalizikia katika Viwanja vya Michezo vya Maisara Mjini Zanzibar.
Alisema zipo kesi zinazolalamikiwa na Wananchi walio wengi kama Dawa za kulevya na udhalilishaji wa Kijinsia unaowakumba zaidi watoto wadogo na wanawake ambazo hupelekwa Mahakamani lakini hatma yake inaishia hewani na wahusika kuwaona wakiendelea kutanua mitaani.
Balozi Seif alieleza kwamba ushahidi wa wazi katika baadhi ya kesi zinazopelekwa kwa Mahakimu hutolewa na wahusika lakini kinachojitokeza kwa baadhi ya Majaji na Mahakimu kueleza kuwa ushahidi bado haujakamilika.
Katika kukabiliana na vitendo hivyo Balozi Seif amewakumbusha watendaji wa Mahakama kubeba jukumu lao kwa kuchukuwa hatua za haraka za kutoa maamuzi ili kupunguza mrundikano wa majalada ya kesi yaliyopo mezani kwao.
“ Majaji na Mahakimu wanapaswa kujiepusha na malalamiko ya mrundikano wa mashauri yanayowahusu ambayo yamekuwa yakilalamikiwa sana na Wananchi ”. Alisema Balozi Seif.
Akizungumzia suala la mazoezi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitahadharisha kwamba kitendo cha watumishi wa Sheria kukaa maofisini kwa muda mrefu na baadae kuishia nyumbani bila ya kufanya mazoezi ni hatari kwa afya zao.
Alisema ni vyema kwa watumishi hao kujipangia utaratibu muwafaka wa kufanya mazoezi ya viungo hata kwa siku moja ndani ya wiki ikiwezekana sio mbaya kuyafanyia nyumbani iwapo muda wa kufanya hivyo umekuwa finyu.
Balozi Seif alieleza kwamba mazoezi ni afya kubwa inayomsaidia Jaji, Mwanasheria na Hakimu kufikiri  vyema katika utekelezaji wa jukumu lake zito kwa Umma.
Mapema akimkaribisha mgeni rasmi katika falya hiyo Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu maadhimisho ya Wiki ya Sheria Zanzibar yameamua kuingiza matembezi  kwa mara ya kwanza katika ratiba yake ili kutoa fursa kwa watendaji wa taasisi hiyo.
Jaji Mkuu Makungu alisema miili inahitaji mazoezi na hata matembezi na ilionekana na Uongozi wa Mahakama Kuu kutokana na watendaji waliowengi wanakaa muda mrefu maofisini jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.
Alisema changamoto hii ya ukosefu wa kufanya mazoezi kwa baadhi ya watendaji wa Sekta ya Sheria itatoa ushawishi kwao kuanza ukurasa mpya wa kuamua kujiingiza kwenye eneo hilo muhimu.

Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akiongoza matembezi ya kuadhimisha siku ya Sheria Zanzibar yalioanzia Mahakama Kuu Vuga Mjini Zanzibar na kuishia Viwanja vya Maisara.Kulia ya Balozi Seif ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu na Kushoto yake ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Said Hassan Said na Mkuu wa Wiulaya ya Kati Nd. Vuai Mwinyi.
Sehemu ya Vikundi vya mazoezi ya Viungo Zanzibar vikijumuika pamoja na watumishi wa Sekta ya Sheria kwenye  matembezi ya siku ya Sheria Zanzibar.
 Vikundi vya mazoezi vikipasha mwili katika Viwanja vya Maisara Suleiman baada ya kukamilisha matembezi ya siku ya Sheria Zanzibar.
 Vikundi vya mazoezi vikipasha mwili katika Viwanja vya Maisara Suleiman baada ya kukamilisha matembezi ya siku ya Sheria Zanzibar.
 Kamanda wa Polisi Mkoa Mjini Magharibi Kamishna Msaidizi wa Polisi Mkadam Khamis Mkadam akiwa miongoni mwa wanakikundi cha mazoezi cha Ziwani walioshiriki matembezi ya siku ya Sheria akifuatilia  kwa makini hotuba ya mgeni ramsi kwenye hafla hiyo.

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu akijiandaa kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kuzungumza na washiriki wa matembezi ya Siku ya Sheria Zanzibar hapo Maisara Suleiman.
 Balozi Seif  akizungumza na washiriki wa matembezi ya Siku ya Sheria Zanzibar  yaliytoshirikisha watumishi wa sekta ya Sheria pamoja na vikundi vya mazoezi ya Vioungo Nchini hapo Maisara Suleiman. Wa kwanza kutoka kushoto  ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mheshimiwa Omar Othman Makungu.

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

$
0
0
SIMU.TV: Zaidi ya wanawake elfu 9 waliokwenda kujifungua katika vituo vya afya mkoani Singida kati ya mwaka 2013/ 2015 wabainika kuwa wamekeketwa. https://youtu.be/0FL0wjNjssA

SIMU.TV: Jeshi la polisi mkoani Lindi labainsha kupungua kwa matukio ya uhalifu mkoani humo katika kipindi cha mwaka 2015 ukilinganisha na mwaka 2014. https://youtu.be/odjf3yUstTU

SIMU.TV: Asasi za kiraia nchini zatakiwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya utoaji wa elimu ya mpiga kura ikiwa ni sambamba na kushirikiana na tume ya uchaguzi NEC katika kuelimisha umma juu ya wajibu na haki za msingi. https://youtu.be/rlHb5ln5VkA

SIMU.TV: Kaya zaidi ya 60 mkoani Lindi zakumbana na adha baada ya mafuriko kufunika makazi yao pamoja na mali zao ikiwemo mashamba. https://youtu.be/cRGW94n4EWg

SIMU.TV: Chama cha mapinduzi mkoani Iringa chawataka wabunge kuwasilisha matatizo ya wananchi wao wawapo bungeni badala ya kutupiana vijembe visivyojenga taifa.https://youtu.be/scbvHCzU3CU

SIMU.TV: Wazazi na walezi nchini waaswa kuhakikisha watoto wao wanapita katika misingi ya dini ili waweze kujifunza mambo mema yatakayo waepusha na vitendo viovu kama matumizi ya dawa za kulevya. https://youtu.be/HIat7EvwIBo

Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupambana na vitendo vya ukeketaji yafanyika mkoani Dodoma

$
0
0
Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupambana na vitendo vya ukeketaji yamefanyika Mjini Dodoma, huku Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh Ummy Mwalimu akiwa mgeni rasmi. 

Maadhimisho hayo yalianza kwa maandamano yaliyoanzia viwanja vya Nyerere Square mpaka ukumbi wa Hazina Ndogo ambapo, Mh Ummy alitoa Tamko la msimamo wa serikali kuhusu ukatili wa ukeketaji na mipango ya Serikali ya awamu ya Tano kukabili ukiukwaji wa haki kutokana na vitendo hivi. 

ikiwemo mpango wa serikali kutunga na kuzifanyia marekebisho sheria kandamizi ili kuleta usawa wa jinsia. sheria hizo ni pamoja na sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 ya mwaka 2001, kifungu cha 158 (1) (a) na sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009ambayo inazuia ukeketaji kwa mtoto wa kike.

Maadhimisho haya yaniandaliwa na Children's diginity forum pamoja na shirika la kimataifa la UNFPA pamoja na serikali.


ZAWADI DOTTO AIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO YA URIMBWENDE YA "MISS ALBINISM 2016"

$
0
0
Mshindi wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni Jalia Mtani ambae alikuwa Jaji Mkuu akitaja Majina ya washindi. Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.
Mshindi wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni Jalia Mtani ambae alikuwa Jaji Mkuu akitajana Majina ya washindi. Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.
Katikati ni Mshindi wa Kwanza, Kulia Mshindi wa Pili na Kushoto Mshindi wa Tatu
Kampuni ya Visimbuzi (Ving'amuzi) ya StarTimes ilikuwa miongoni mwa makampuni yaliyosaidia kufanikisha mashindano hayo. Mwenye Kinasa sauti ni Erick Makonya ambae ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Kanda ya Ziwa akitaja zawadi zilizotolewa kwa washindi na Kampuni hiyo ambapo Mshindi wa Kwanza amejinyakulia Simu ya StarTimes  aina ya Solar5, Mshindi wa Pili simu aina ya P40 StarTimes na Mshindi wa tatu amejishindia simu aina ya B27 zote zikiwa ni android kutoka StarTimes.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakiongozwa na Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, wakiwa katika picha ya Pamoja na washindi.

Wananchi waifagilia"Ongea Deilee" ya Vodacom Tanzania

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao (wa pili kulia)  akiwa na maofisa wakuu wa kampuni  hiyo wakitembea kuelekea kutoa elimu kwa wateja wao sehemu mbalimbali za la  jijini Dar es Salaam,Kuhusiana na promosheni ya “Ongea Deilee”,ambayo inayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 2 bure kila siku pindi wakiongea  jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom.
 Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao   akimkabidhi fulana, Ramadhan Mohamed katika mitaa ya kariakoo wakati wa kutoa elimu kwa wateja mtaani baada mteja huyo kujiunga na Promosheni ya “Ongea Deilee”, Inayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea  jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom. Mteja anatakiwa kujiunga kwa kupiga namba *149*01#.  
 Mwendesha bodaboda eneo la Morocco jijini Dar es Salaam, Abdul Juma akielekezwa na mmoja wa wafanyakazi wa Vodacom  Tanzania,jinsi ya kujiunga na Promosheni mpya ya “Ongea Deilee”, Inayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea  jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom. Mteja anatakiwa kujiunga kwa kupiga namba *149*01#. 
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao (kushoto) akimwelekeza mama Enes Kalinga  ambaye ni mfanyabaishara katika soko la Kariakoo jinsi ya kujiunga na Promosheni mpya ya “Ongea Deilee”, Inayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea  jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom,Mteja anatakiwa kujiunga kwa kupiga namba *149*01#. 


 Wafanyabiashara wa nyama katika  soko la Kariakoo jijini Dar es Salaa wakimsikilza Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Joyce Tarimo  wakati alipokuwa akitoa elimu juu ya Promosheni mpya ya “Ongea Deilee”, Inayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea  jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom. Mteja anatakiwa kujiunga kwa kupiga namba *149*01#.
Askari  wa Usalama barabarani akiwa katika mitaa ya Kongo karibu na kituo cha mabasi Cha Mwananyamala akipewa elimu na Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania walipoingia mtaani kutoa elimu kwa wadau wa mtandao huo,Kuhusiana na  Promosheni mpya ya “Ongea Deilee”, Inayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea  jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom. Mteja anatakiwa kujiunga kwa kupiga namba *149*01#.

PPF WAKABIDHIWA RASMI JENGO JIPYA LA KISASA WALILOJENGA JIJINI ARUSHA LENYE THAMANI YA BILIONI 32.5

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa PPF  Bw. William Erio (kushoto) akipokea michoro ya jengo jipya la PPF Jijini Arusha kutoka kwa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Bw.  Dudley Mawalla (kulia) kutoka kampuni ya   MD Consultancy Ltd ya Dar es Salaam, katika hafla fupi ya makabidhiano rasmi ya jengo kutoka kwa mkadarasi wa kichina CREJ (EA) Ltd. Anayeshuhudia Katikati ni Injinia wa Miradi ya PPF, Injinia Marko Kapinga.

Sehemu ya muonekano wa mbele wa jengo

Mpaka kufikia kukabidhiwa kwake hii leo, tayari ukaguzi wa mamlaka za Jiji na Usalama wa Majengo umeshakamilika na ruhusa ya matumizi kutolewa. Tayari jengo hilo limeshapata wapangaji watatu ambao wapo kwenye jengo tayari zikiwemo benki za TIB na FNB, huku asilimia 21 ya wapangaji wengine wakiwa wamekwisha saini mikataba na PPF na wapangaji wengine 24 wakiwa katika mazungumzo.
Aidha kwa maelezo ya Mratibu wa PPF Kanda ya Kasakazini, Bw Onesmo Rushahi, Ofisi za Kanda ambazo kwa sasa ziko maeneo ya Kaloleni Jijini hapa zitahamishiwa katika Jengo hili jipya, huku mkakati wa PPF ukiwa ni kuhakikisha baada ya mwaka mmoja jengo hilo liwe limefanikiwa kupata wapangaji maeneo yote kwa shughuli za ofisi na biashara. 

Mkandarasi Mkuu ni kampuni ya CRJE (EA) Ltd akisaidiwa na wakandarasi wengine kwa huduma za jengo kama vile ICT na Usalama - SSTL Group Ltd, Lifti - S.E.C (EA) Ltd, AC - M.A.K Enginering Co. Ltd, Mfumo wa maji safi na maji taka - Jandu Plumbers Ltd, na Umeme ni Central Electrical International Ltd. Pia kulikuwa na mamlaka za kiserikali kama wasimamizi wa usalama makazini OSHA, Idara ya maji Asurha - AUWSA, NAESCO, Halmashauri ya Jiji na Bodi za Ukaguzi kama AQRB na CRB. 

Injinia Marko Kapinga, Meneja wa Utekelezaji wa Miradi ya PPF akikagua makabrasha yaliyokabidhiwa na mkandrasi kama michoro halisi ya namna jengo lilivyo kwa sasa
Kiongozi mkuu wa Kampuni ya CRJE (EA) Ltd, Bw Hu Bo (kulia) ambaye kamapuni yake ndio ilikuwa mkandarasi mkuu wa mradi akikabidhi funguo kwa Director General wa PPF Bw William Erio kama ishara ya makabdihiano ramsi ya jengo la PPF Plaza la Jijini Arusha Jumamosi. 

Ngoma azipendazo Ankal: La Bionda - "One for you, one for me"

Introduding "LANDAA" by Smaina and Mariana

$
0
0
Wimbo unaitwa LANDAA Producer Dege Touch ni wimbo uliobeba maneno ya kabila jamii ya Wasandawe na wimbo wa asili ambao umejumuisha mila, desturi, vyakula, vijiji na Koo za Kisandawe

WAZIRI MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI KURUDI KAZINI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawsiliaano Prof.Makame Mbarawa (Wa pili kushoto), akitoa maelekezo kwa Meneja bishara wa kampuni ya Malaysia inayojenga vichwa vya treni Srinivasan Rajmohan (Wa kwanza kulia) kuhusu kufanya kazi hiyo kwa haraka ( Wa pili kushoto) ni katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Eng.Leonard Chamuriho na (Wapili kulia) ni Naibu Waziri Eng.Edwin Ngonyani.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka Makandarasi waliosimamisha kazi za ujenzi wa barabara nchini kuendelea na ujenzi baada ya Serikali kuanza kuwalipa madai yao.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Magole-Turiani yenye urefu wa kilomita 48.6 Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, Prof. Mbarawa amesema tayari Serikali imeshalipa makandarasi mbalimbali nchini shilingi bilioni 400 na itaendelea kufanya hivyo ili kumaliza madeni yao kwa haraka.

“Hakikisheni mnarejea kazini na kuwapa mikataba ya ajira wafanyakazi wenu katika kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa ili ujenzi wa barabara na madaraja ukamilike kwa mujibu wa mkataba na hivyo kuondoa usumbufu kwa watumiaji wa barabara hii”, amesema Prof Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mvomero Sadick Murad (kushoto) wakati akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa barabara ya Magole-Turiani yenye urefu wa Km 48.6. Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Edwin Ngonyani.

Profesa Mbarawa amemhakikishia mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation anayejenga barabara ya Magole-Turiani kuwa tayari serikali imeshamlipa zaidi ya kiasi cha dola za kimarekani zaidi ya laki 735 na Shilingi za kitanzania zaidi ya Milioni 795 hivyo ni wakati wa kukamilisha ujenzi huo hususan sehemu za madaraja kabla ya mvua za masika kuaanza.

Akizungumza katika ukaguzi huo Mbunge wa Mvomero Mhe. Sadick Murad ameiomba Serikali kumalizia daraja la Diwale lenye urefu wa mita 75 ili liweze kupitika.

Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua karakana ya ujenzi wa vichwa vya treni mjini Morogoro na kumtaka mkandarasi anayekarabati vichwa hivyo kufanya kazi hiyo kwa haraka na kutoa kazi nyingine kwa watanzania ili kuwajengea uwezo wa kazi hizo.
Sehemu ya juu ya daraja la Diwale lenye urefu wa mita 75 likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake kama linavyoonekana.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

PROFESA KILLIAN WA CHUO CHA MKWAWA ASHINDA SAFARI KUTAZAMA BUNDESLIGA UJERUMANI NA STARTIMES

$
0
0
 Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo, akichezesha droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).
 Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia) akiandika namba ya mshindi wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo.
 Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akipiga namba ya simu ya mshindi aliyepatikana katika droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia). 

 Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo akizungumza na mshindi kwa njia ya simu aliyepatikana wakati wa uchezeshwaji wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).

Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Chuo cha Ualimu cha Mkwawa cha mkoani Iringa ambacho ni chuo kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bernadeta Killian (50) amefanikiwa kuibuka mteja wa kwanza mwenye bahati kwa kujinyakulia tiketi ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga kutoka kwa kampuni ya StarTimes katika droo iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza kwa njia ya simu Profesa Killian baada ya kutangazwa kuwa ni mshindi amesema kuwa anayo furaha isiyoelezeka kupata taarifa hiyo ya ushindi ambao hakufikiria kama kuna ofa hiyo nzuri kwa wateja.
“Ninajisikia furaha kwa kutangazwa kuwa mshindi kwani sikutarajia kama wateja wa StarTimes tunaweza kupewa kubwa kiasi hiki ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ‘Live’. Naweza kusema mwaka umeanza vizuri kwa kuonyesha dalili ya neema kama hii, ni fursa kubwa kwangu mimi kama mteja kwani kuna maelefu ya wateja ambao wangependa kupata fursa hii. 

Nawashukuru kwa hili kwani wameliendesha zoezi bila ya upendeleo na sisi wateja wao tunafurahi na kuwapongeza sana na tutandelea kuwaunga mkono.” Alieleza Profesa Killian
Mshindi huyo wa kwanza wa droo iliyopewa jina la ‘Pasua Anga na StarTimes’ alipatikana baada ya kujiunga na kifurushi cha Super ambacho ni shilingi 36,000/- katika dishi. Lakini pia mteja yoyote wa StarTimes anaweza kuibuka mshindi kwa kujiunga na kifurushi chochote kuanzia cha shilingi 5,000/- na kuendelea kwa upande wa ving’amuzi vya dishi na antenna. Na kwa wateja wapya pindi wajiungapo na huduma za kampuni hiyo wamekuwa wameunganishwa moja kwa moja na droo ya bahati nasibu.
“Ningependa kutoa wito kwa wateja wenzangu waendelee kujiunga kwani bado nafasi zimebaki kushindaniwa na zote zipo kwa ajili yao, hivyo wasilaze damu. Ninaahidi kuitumia fursa hii ipasavyo kwa kuenda kutazama wenzetu wa ulaya wanafanya nini kwa upande wa soka kwani kwa muda mrefu tumekuwa tukitazama kupitia kwenye luninga, pongezi tena kwa StarTimes kwa kuifanya ligi ya Bundesliga ionekane kupitia ving’amuzi vyake kwa gharama nafuu kabisa ambayo kila mtu anaweza kuimudu. Wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuipa ligi hiyo umaarufu nchini kwani sasa kwa kiasi kikubwa michezo yote inaonekana ‘Live’ na kufuatiliwa na watu wengi.” alihitimisha Mkuu huyo wa Chuo cha Ualimu Mkwawa

Naye kwa upande wake Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amebainisha kuwa, “Hii si mara ya kwanza sisi kuchezesha droo ya bahati nasibu kwa kuwazawadia wateja wetu ni zawadi mbalimbali, hivyo basi huu ni muendelezo tu wa ofa nyingi zinazoendelea kumiminwa kwa wateja wetu waaminifu. Safari hii wateja wetu tumeamua kuwazawadia safari itakayolipiwa gharama zote na kampuni kwenda Ujerumani kutazama ligi ya Bundesliga ambayo kwa Afrika ndio kampuni pekee yenye hakimiliki ya kuionyesha ‘Live’.”
“Makubaliano baina ya wamiliki wa ligi hiyo ya Ujerumani na kampuni ya StarTimes yaliingiwa kwa dhumuni kubwa la kuifanya ligi hiyo maarufu barani Afrika kama ligi zingine. Na ni kwa kupitia StarTimes pekee hilo linaweza kufanikiwa kutokana na wingi wa wateja wetu, ubora wa huduma na gharama nafuu ambazo mwananchi yoyote wa kipato cha chini anaweza kuzimudu,” alisema Bi. Hanif na kumalizia, “Hivyo basi nampongeza mshindi wa leo na nawasihi wateja wetu waendelee kujiunga nasi au walipie vifurushi vyao ili waingie kwenye droo ya bahati nasibu na kujishindia safari hii kubwa kwenda Ulaya kutazama mechi moja kwa moja pamoja na mashabiki wengine ulimwenguni.”

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI IBADA YA KUMSIMIKA ASKOFU MKUU WA PILI WA EAGT, DKT MWAKIPESILE, APANGA KUKUTANA NA VIONGOZI WA DINI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ataitisha kikao cha viongozi wa dini zote hivi karibuni ili wapange na kuainisha ni mambo gani ambayo wanaweza kutoa ushauri kwa Serikali na kupata njia bora ya kuwahudumia Watanzania. 
Ametoa ahadi hiyo leo mchana (Jumapili, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na mamia ya waumini walioshiriki ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Askofu Dk. Brown Abel Mwakipesile iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT la Mlimwa West nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Waziri Mkuu Majaliwa ambaye alihudhuria ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli alisema: “Hivi karibuni nitaitisha kikao cha viongozi wa dini zote kitakachojumuisha Maaskofu Wakuu, Masheikh na baadhi ya wachungaji ili tukae na kubaini ni nini kifanyike ili kuisadia Serikali namna nzuri ya kuboresha maisha ya Watanzania.”

Akijibu risala iliyosomwa na Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Leonard Mwizarubi, Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kufanya mapitio ambayo yatawawezesha Watanzania kupata huduma kwa urahisi. 
“Katibu Mkuu pamoja na Baba Askofu Mkuu wamegusia suala la upandaji wa gharama za vifaa vya ujenzi pamoja na suala la makazi bora. Mwezi ujao tunaanza vikao vya Bunge vya kupitia bajeti ya Serikali, tutaliangalia hili kwa kumshirikisha Waziri wa Fedha… tutafanya mapitio katika hili ili mwananchi wa kawaida aweze kumudu maisha,” alisema huku akishangiliwa na waumini hao. 
Aliwaomba viongozi wa kanisa hilo pamoja na waumini wake waendelee kuiombea nchi pamoja na viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kwani kazi ya kutumbua majipu waliyoianzisha ina mitihani mikubwa.

“Kutokana na maombi yenu kwa viongozi wakuu wa kitaifa nina imani Taifa hili litafika tunakotaka liende. Endeleeni kutuombea kwa sababu kazi ya kutumbua majipu ina mitihani mikubwa. Lakini pia napenda niwahakikishie kuwa Serikali hii itatumbua majipu hayo kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa. Hakuna mtu ambaye ataonewa,” alisisitiza Waziri Mkuu. 
Kuhusu mgogoro wa kiwanja cha kanisa hilo kilichopo eneo la Ipagala, Waziri Mkuu aliahidi kulishughulikia suala lao kesho asubuhi kabla hajaondoka kurejea Dar es Salaam. “Kesho asubuhi nitamuita Mkurugenzi Mkuu wa CDA na kumtaka anipe taarifa sahihi kuhusu mgogoro huu. Najua suala hili liko mahakamani, lakini naamini Mkurugenzi anaweza kuwa kiungo kizuri kati ya wananchi waliojenga eneo hili pamoja na kanisa ambao mnamiliki kiwanja husika”. 
“Kama atapata eneo jingine na kupima viwanja, kisha akawapatia hawa wananchi anaweza kuwa amesaidia kuondoa mgogoro huu. Wananchi walienda mahakamani huku wakijua eneo lenu limewekewa uzio, sasa wanagoma kutoka kwa sababu hawana mahali pa kwenda,” aliongeza. 
Mapema, akitoa hotuba yake, Askofu Mkuu Dk. Mwakipesile alisema kanisa litaendelea kuiombea Serikali ya awamu ya tano ili nchi idumu katika amani na utulivu. 
Aligusia eneo la kanisa lililopo kiwanja na 34, kitalu ‘E’, Ipagala East, Dodoma, ambalo ujenzi wa shule yake umesimama kutokana na mgogoro baina yao na wananchi waliovamia eneo lao kwa kujenga nyumba za kuishi licha ya kuwa eneo hilo lilikwishawekewa uzio. 
“Kama kanisa tumeshindwa kukamilisha ujenzi wa shule kwa sababu wananchi hao walifungua kesi mahakamani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Tunaomba uamuzi wa kesi hii uharakishwe,” alisema huku akishangiliwa. 
Alisema kanisa hilo lina majengo 4,670 nchini kote na viwanja 420 ambavyo ni vya kujenga makanisa na vituo vya kutoa huduma mbalimbali za kijamii. 
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Mwizarubi alisema katika risala yake kwamba wanaiomba Serikali ifikirie kushusha bei ya vifaa vya ujenzi ili wananchi waweze kuwa na nyumba bora za kuishi.

“Maisha bora maana yake ni kuwa na nyumba bora. Tunaiomba Serikali yako ipunguze bei ya vifaa vya ujenzi ili Watanzania waweze kuwa na makazi bora,” alisema huku akishangiliwa.

 Waziri kuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT,  Dkt.  Brown Abel Mwakipesile katika Ibada ya kumsimika Askofu  huyo iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West Mjini Dodoma Februari 7, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa  Pili wa EAGT, Dkt. Brown Abel Mwakipesile  iliyofanyika kwenye Kanisa la EAGT Mlimwa West mjini Dodoma Februari 7, 2016.
 Waumini wa EAGT wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt Brown Abel Mwakilpesile kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West mjini Dodoma Feb 7, 2016. 
 Waumini wa EAGT wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt Brown Abel Mwakilpesile kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West mjini Dodoma Feb 7, 2016. 
 Viongozi na waumini wa EAGT wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt Brown Abel Mwakilpesile kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West mjini Dodoma Feb 7, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya picha Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt.  Brown Abel  Mwakipesilie zawadi ya picha yenye maadishi ya neon la Mungu katika Ibada ya kumsimika Askofu huyo iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West  mjini Dodoma Februari 7, 2016. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

UWEKEZAJI WA MRADI MKUBWA WA MAJI SAFI NA SALAMA WA RUVU CHINI NA RUVU JUU SASA INAELEKEA KUKAMILIKA.

RAIS MAGUFULI AHUTUBIA KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 39 YA CCM SINGIDA

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AOMBOLEZA VIFO VYA ASKARI WALIOFARIKI DUNIA SINGIDA

NMB YASAIDIA MADAWATI SHULE MBILI ZA MSINGI JIJINI DAR.

$
0
0
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo (kushoto) akimkabidhi Ofisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni, Bi. Grace Mtesigwa (kulia) msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 yaliyotolewa juzi kwa Shule ya Msingi Upendo iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB pia ilikabidhi madawati 53 kwa Shule ya Msingi Kibwegere iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo (kushoto) akimkabidhi Ofisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni, Bi. Grace Mtesigwa (kulia) msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 yaliyotolewa juzi kwa Shule ya Msingi Upendo iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB pia ilikabidhi madawati 53 kwa Shule ya Msingi Kibwegere iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Shule ya Msingi Upendo wakifurahia mara baada ya shule yao kupokea msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 kutoka Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Shule ya Msingi Upendo wakifurahia mara baada ya shule yao kupokea msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 kutoka Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Shule ya Msingi Upendo wakiimba wimbo kwa furaha mara baada ya shule yao kupokea msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 kutoka Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Shule ya Msingi Upendo wakiimba wimbo kwa furaha mara baada ya shule yao kupokea msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 kutoka Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam.Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo (kulia) akizungumza wakati wa hafla ya Banki hiyo kukabidhi msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa Shule ya Msingi Upendo iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB pia ilikabidhi madawati mengine 53 kwa Shule ya Msingi Kibwegere iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo (kulia) akizungumza wakati wa hafla ya Banki hiyo kukabidhi msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa Shule ya Msingi Upendo iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB pia ilikabidhi madawati mengine 53 kwa Shule ya Msingi Kibwegere iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Rose Muhando naye amafuata Mwaitege Tamasha la Pasaka

$
0
0
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, Rose Muhando amekuwa wa pili kuthibitisha kushiriki katika Tamasha la Pasaka linalotarajia mikoa ya Geita, Mwanza na Wilaya ya Kahama.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama Muhando ameungana na mwenzake Bonny Mwaitege ambaye alikuwa wa kwanza kuthibitisha katika tamasha hilo.

Msama alisema tamasha hilo mwaka huu linatarajia kufanyika Geita (Machi 26), Mwanza (Machi 27) na Kahama (Machi 28) ambako alitoa wito kutoa wito kwa wakazi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.Aidha Msama alisema dhamira ya Tamasha la Pasaka ni wenye uhitaji maalum ambao ni yatima, walemavu na wajane.

Msama alisema sababu ya kupeleka Tamasha la Pasaka mikoa ya Kanda ya ziwa ni kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa wakazi wa mikoa hiyo sambamba na kupiga vita mauaji ya walemavu wa ngozi 'albino'.

"Tunalipeleka Tamasha la Pasaka mikoa ya Kanda ya ziwa kwa sababu ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa wakazi wa mikoa hiyo ambayo miaka iliyopita iligubikwa na mauaji ya walemavu wa ngozi 'albino'," alisema Msama.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images