Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

Mama Salma Kikwete reaffirms her commitment to working with George W. Bush Institute to fight Reproductive Health Cancers

0
0
 Former First Lady of Tanzania Mama Salma Kikwete earlier today held talks with Ms. Natalie Gonnella - Platts and Toun Olateju who paid a courtesy call to WAMA Foundation offices at Kawe area in Dar es salaam. Natalie works with the First Ladies Initiative while Toun works with Pink Ribbon Red Ribbon at the George W. Bush Presidential Centre.

Mama Salma Kikwete partnered with Mrs. Laura Bush, former First Lady of US to launch the First Ladies Initiative in Dar es Salaam three years ago. Mama Kikwete champions efforts to curbing  the spread and morbidness associated with breast and cervical cancers in Tanzania which is one of the key priorities of the Bush centre through Pink Ribbon Red Ribbon initiative. 

Speaking at the meeting, Mama Kikwete reiterated her commitment to continue supporting women and girls in the areas of education, health and economic empowerment. These are the three pillars that cannot be tackled separately if we wish to transform the lives of women in Tanzania, Said Mama Kikwete. 
WAMA understands and embraces this concept to the extent that they constitute part of the four strategic objectives of the organization. 
“I am looking  forward to continue working with Mrs. Laura Bush, Former US First Lady, President Bush and other colleagues at Bush Institute to increase awareness and expand treatment services for cervical and breast cancer. 
"Having made significant investment in health services, awareness becomes a very important strategy in mobilizing masses to come forward and utilize screening and treatment services from early signs. We are also keen to continue working with other partners to roll-out vaccination to young girls” Mama Kikwete said. 
Mr. Daudi Nasib, WAMA Executive Secretary on his part explained WAMA’s resolve in championing the national HPV vaccination program for young girls.   He highlighted the progress made by the Government of Tanzania in introducing Human Papilloma Virus (HPV) for young Girls aged 9 to 13. The vaccination program was officially launched in Kilimanjaro Region by Mama Salma Kikwete, then First Lady and WAMA Chairperson, in 27th April 2014 during the National Immunization Week.

“Since then the WAMA Chairperson has been engaging herself in  advocacy all over the country in rolling out the vaccination program around the country. WAMA has mobilized resources to conduct mass screening and treatment campaigns for cervical and breast cancer in Tanzania” Mr. Nasib said

 Ms. Toun Olateju Country Programs of Pink Ribbon Red Ribbon manager expressed her great appreciation to the WAMA Foundation Chairperson, Mama Salma Kikwete and staff for their  excellent performance in implementing the Pink Ribbon Red Ribbon Initiative on Prevention and treatment of Cervical Cancer in Tanzania. 
“I would like to convey Mrs. Laura Bush greetings to Mama Salma Kikwete and WAMA Staff. They are all committed to this initiative and will continue collaborating with you to improve the health of women in Tanzania” Ms. Olateju said. 

 Ms. Natalie Gonnella, Manager of the First Ladies Initiative from the George W. Bush Institute added that Mrs. Laura Bush was very active and eager to continued relationship with WAMA Chairperson. 
She informed mama Kikwete that the George W. Bush Institute and the International Center for Research on Women (ICRW) are now working on a research study on the role and influence of the First Ladies in improving their people’s lives. Since she is a great example of what the First Ladies could do to improve lives of the communities, they would like to engage her in this research”. Natalie told Mama Salma Kikwete. 
The Pink Ribbon Red Ribbon initiative was introduced in Tanzania in 2013 during the African First Ladies Summit, themed Investing in Women: Strengthening Africa that was held in Dar es Salaam from July 02-03, 2013. WAMA Foundation partners with Medical Women’s Association of Tanzania (MEWATA), T-MARC Tanzania, Tanzania Youth Alliance (TAYOA) and the Mbeya HIV/AIDS Network to implement the Pink Ribbon Red Ribbon Initiative in Tanzania.  

 H.E. Former First Lady of Tanzania Mama Salma Kikwete earlier in talks witn  Ms. Natalie Gonnella - Platts and Toun Olateju who paid a visit to WAMA Foundation offices at Kawe are in Dar es salaam. Right is Mr. Daudi Nasib, WAMA Executive Secretary.
H.E. Former First Lady of Tanzania Mama Salma Kikwete shakes hands with Ms. Toun Olateju,  Country  Manager of Programs of  the Pink Ribbon Red Ribbon 
H.E. Former First Lady of Tanzania Mama Salma Kikwete with Ms. Natalie Gonnella - Platts of the First Ladies Initiative and Ms. Toun Olateju,  Country  Manager of Programs of  the Pink Ribbon Red Ribbon 

NYUMBA TATU MWANANA ZINAUZWA WAZO HILL JIJINI DAR ES SALAAM ZINAUZWA

0
0
 Nyumba tatu nzuri zinauzwa maeneo ya wazo hill  jijini Dar es salaam ambazo zina vyumba vitatu vya kulala kimoja master room, pia kuna public toilet, kitchen na store zipo kwenye viwanja  tofauti na kila kimoja kina ukubwa wa square meta 700. 
Nyumba zote zina hati , maji ya dawasco na maji ya kisima cha uhakika, umeme wa uhakika. Bei ni rahisi.
kwa yeyote anayehitaji   mawasiliano  piga 0713776461 na  0756666708.



BILLIONI 60 KUFUFUA GENERAL TYRES ARUSHA

0
0

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles John Mwijage akijibu hija mbalimbali toka kwa wabunge katika kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.

Habari na picha na Raymond
 Mushumbuai MAELEZO.
Shillingi Billioni 60 zinategemea kutumika kufufua kiwanda ya matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha ambacho kimesharudi mikononi mwa Serikali, na fedha hizo zitatumila kurekebisha mitambo ya umeme ya kiwanda hicho na kupata mitambo mipya itakayoendana na teknolojia ya utengenezaji wa matairi duniani.
Akijibu swali la Mhe. Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) lililouliza ni lini serikali itafufua kiwanda cha matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha kwani ni tegemeo kwa ajira kwa wananchi wa Jijini la Arusha,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles John Mwijage amesema kiwanda hicho kimesharudi mikononi mwa Serikali na wako mbioni kukifufua ili kianze kufanya kazi ya kuzalisha matairi nchini.
“ Tumeanzisha viwanda nchi ili kuzalisha bidhaa na kutoa ajira kwa watanzania na sio kuwatesa wananchi kwa kukosa ajira au kuagiza bidhaa ambazo tunaweza kuzalisha hapa hapa nchini, hivyo basi Serikali kupitia Wizara yangu tutatenga fedha kwa ajili ya kufufua kiwanda hiki ili kianze kufanya kazi mara moja”
“ Sio tu tutafufua kiwanda cha General Tyres pekee bali tunafatilia viwanda vyote ambavyo vimekiuka sheria na kanuni kwa kutoviendeleza viwanda hivyo ili kuvirudisha mikononi mwa Serikali au kuwatafuta wawekezaji wengine watakaoweza kuviendesha viwanda hivyo” Alisema Mhe. Mwijage.
Aidha Mhe. Charles John Mwijage amesema ni kweli makampuni mengi yaliyobinafsishwa hayakufanya vizuri katika uendeshaji wake ukiacha mifano ya makampuni machache yanayofanya vizuri yakiwemo Tanzania Breweries Limited (TBL),Morogoro Polyester 21st Century na Tanzania Cigarette Company Limited (TCC), hivyo Wizara yangu ikishirikiana na Msajili wa Hazina juu ya Viwanda ilifanya tathmini iliyoonesha kuwa mashirika mengi yaliyobinafsishwa hawakutekeleza mikataba ya mauziano kikamilifu.
Ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha makampuni yote haya yanazalisha kwa tija ili tupate bidhaa,kodi ya Serikali na ajira kwa wananchi wa Tanzania ili kutimiza adhma ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ya kuwa na Tanzania yenye viwanda kwa maendeleo ya taifa.
Serikali kupitia Wizara yetu inaboresha mazingira ya uwekezaji hali itakayowajengea imani kwa wawekezaji na kupelekea kupanua zaidi shughuli zao za kibiashara na pia kuendeleza mpango wa Viwanda vidogo na vya kati unaoshirikisha SIDO na Halmashauri za Wilaya na Mikoa ili kuanzisha Viwanda vya Mkoa vya kuongeza thamani ya bidhaa za Kilimo,Uvuvi na ufugaji kupitia njia hii ajira nyingi zitaongezeka na kupunguza tatizo la ajira nchini.

Mhe Freeman Mbowe atangaza baraza kivuli la mawaziri wa kambi ya upinzani bungeni

0
0
Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe, ametangaza baraza lake kivuli la Mawaziri na kuwasihi wahusika kutoa Ushirikiano kwa Baraza hilo alilolitangaza bungeni baada ya Maswali na Majibu.

Waliotangazwa Katika Orodha hiyo ni Pamoja na;


Wizara ya Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri – Jaffar Michael
Naibu Waziri – Joseph Nkundi na Ruth Mollel

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira 
Waziri – Ali Saleh Abdalla
Naibu Waziri – Pauline Gekul


Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu

Waziri – Esther Bulaya
Naibu – Yusuph Makame na Maftah Abdalla


Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

Waziri – Magdalena Sakaaya Naibu
Waziri – Emmaculate Swari


Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Inj. James Mbatia
Naibu Waziri Willy Kombucha


Wizara ya Fedha na Mipango 
Waziri – Halima Mdee
Naibu Waziri – David Silinde


Wizara ya Nishati na Madini 
Waziri – John Mnyika
Naibu Waziri – John Heche

Wizara ya Katiba na Sheria Waziri 
Tundu Lissu Naibu
Waziri Abdalla Mtolela

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri – Peter Msigwa
Naibu Waziri – Riziki Shaghal


Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Waziri – Juma Omari
Naibu Waziri Mwita Waitara

Wizara ya Mambo ya Ndani 
Waziri – Godbless Lema
Naibu Waziri Masoud Abdalla


Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Waziri – Wilfred Lwakatare
Naibu Waziri – Salum Mgoso

Wizara ya Maliasili na Utalii 
Waziri Esther Matiko
Naibu Waziri– Cecilia Pareso

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Anthony Komu
Naibu Waziri Cecil Mwambe

Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi
Waziri – Suzan Lyimo
Naibu Waziri Dkt. Ali Suleiman Yusuph


Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Waziri – Dkt. Godwin Mollel
Naibu Waziri Zubeda Sakul


Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo

Waziri – Joseph Mbilinyi
Naibu Waziri – Devotha Minja

Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri –Hamidu Hassan
Naibu Waziri– Peter Lijualikali

"The Second Coming:" Shairi la W. B. Yeats

0
0
NA Profesa Joseph Mbele


"The Second Coming," shairi la William Butler Yeats wa Ireland, ni kati ya mashairi maarufu kabisa katika ki-Ingereza. Yeats aliliandika shairi hili baada ya vita kuu ya kwanza ambayo ilisababisha vifo vya mamilioni ya watu na uharibifu mkubwa. Simanzi ilitanda ulimwenguni, na ilikuwa rahisi kukata tamaa kuhusu hatima ya binadamu na ulimwengu. 

Hisia hizi zinajitokeza kimafumbo katika "The Second Coming." Kinachoshangaza ni jinsi shairi hili lilivyoonekana kubashiri majanga yaliyoikumba dunia miaka iliyofuata. Adolf Hitler aliibuka na himaya yake ya ki-Nazi iliyosababisha mauaji ya mamilioni ya watu na kisha ikaja vita kuu ya pili. 
"The Second Coming" ni shairi ambalo wengi tulilisoma tulipokuwa sekondari, na wengi wetu tunakumbuka lilivyonukuliwa na Chinua Achebe mwanzoni mwa riwaya yake ya Things Fall Apart. Kati ya mambo mengi, riwaya hii nayo ilielezea mtafaruku uliotokea katika jamii ya asili ya ki-Afrika kufuatia kuingiliwa na wazungu. 
Kila mtu anaweza kulisoma shairi hili la "The Second Coming" kimya au kwa sauti. Jaribu kulisoma kwa sauti, uone linasikika vipi na linatoa maana au hisia gani. Haiwezekani kwa shairi hili kusomwa kwa namna ile ile lilivyokwishasomwa, hata kama msomaji ni yule yule. Lazima zitajitokeza tofauti, hata kama ni ndogo sana. 
Hata mimi ambaye nimerekodi usomaji wangu katika video niliyoiweka hapa, siwezi kurudia kulisoma shairi hili sawa sawa kama nilivyofanya. Jambo hili linatulazimisha kujiuliza: kusoma ni nini? Bila shaka kusoma ni kutafsiri, na kila usomaji wa shairi kama hili ni tafsiri tofauti na nyingine yo yote. 
Tunaweza kujiuliza masuali mengine. Kwa mfano, Je, shairi linabaki lile lile kila linaposomwa? Tunaposema shairi, tunamaanisha nini? Nini maana ya kusema "The Second Coming" ni shairi? Inakuwaje liitwe shairi lile lile iwapo kila usomaji wake unaleta maana na hisia tofauti? 

Watu wengi wanaamini kuwa inawezekana kuelezea maana ya shairi na kuhitimisha. Wanaamini kuna ujumbe katika shairi ambao unaweza kufafanuliwa. Ni lazima tujifunze kutafakari zaidi masuala haya kwa kusoma nadharia mbali mbali za fasihi badala ya kuridhika na dhana zilizozoeleka.
Nisikilize ninavyolisoma shairi la "The Second Coming." Nilirekodi video hii jana, ghafla tu, bila mazoezi, nikaiweka kwenye ukurasa wangu wa Facebook. Watu wamejitokeza kutoka pande zote za dunia wakionyesha kuipenda. Siwezi kujua ni nini kilichowagusa; labda ni shairi lenyewe, au labda ni usomaji wangu, na hata hivyo, ni lazima kila mtu ameguswa kwa namna tofauti na mwingine. Ni kitendawili.

The Second Coming

Turning and turning in the widening gyre
The falcon cannot hear the falconer;
Things fall apart; the centre cannot hold;
Mere anarchy is loosed upon the world,
The blood-dimmed tide is loosed, and everywhere
The ceremony of innocence is drowned;
The best lack all conviction, while the worst
Are full of passionate intensity.

Surely some revelation is at hand;
Surely the Second Coming is at hand.
The Second Coming! Hardly are those words out
When a vast image out of Spiritus Mundi
Troubles my sight: somewhere in sands of the desert
A shape with lion body and the head of a man,
A gaze blank and pitiless as the sun,
Is moving its slow thighs, while all about it
Reel shadows of the indignant desert birds.
The darkness drops again; but now I know
That twenty centuries of stony sleep
Were vexed to nightmare by a rocking cradle,
And what rough beast, its hour come round at last,
Slouches towards Bethlehem to be born?

Source: The Collected Poems of W. B. Yeats (1989)

SIMU TV: uchambuzi wa Habari za Magazetini leo February 6, 2016.

RAIS DKT MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WAKATI AKIELEKEA DODOMA

KUMBUKUMBU

0
0
OMWANA THERESIA NYAMICHWO RUTAGERUKA

LEO 6 – FEBRUARI 2016, UMETIMIZA MIAKA 22 TANGU MWENYEZI MUNGU ALIPOKUTWAA TOKA HAPA DUNIANI.  PAMOJA NA KWAMBA KIMWILI HAUPO NASI, KIROHO TUNAKUKUMBUKA DAIMA. 

TUNAADHIMISHA KUMBUKUMBU HII TUKIOMBA MWENYEZI MUNGU AWAKUTANISHE KWENYE RAHA YA MILELE NA MUME WAKO MPENDWA MWALIMU NOVATI RUTAGERUKA AMBAYE SIKU ZOTE ALIKUKUMBUKA KATIKA SALA ZAKE KABLA YA NAYE KUTWALIWA NA BWANA TAREHE 5 MEI 2010. 

MNAKUMBUKWA DAIMA NA WATOTO WENU FROLIDA, ILLUMINATA, LIBERATA, DUNSTAN, JOYCE NA EDWIN PAMOJA NA WAKWE, WAJUKUU, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WOTE.

IBADA YA MISA YA KUMBUKUMBU ITAADHIMISHWA JUMAMOSI TAREHE 6 - FEBRUARI - 2016 KATIKA KANISA LA MTAKATIFU GASPER, MBEZI BEACH, DAR-ES-SALAAM SAA 1.00 ASUBUHI.

BWANA ALITOA, BWANA ALITWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE. 
AMINA


SIMU TV: MAPITIO YA MAGAZETI LEO

INTRODUCING VYA BUBE VINAUZWA BY SHINER

KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA CCM ZAENDELE HIVI SASA NDANI YA UWANJA WA NAMFUA MKOANI SINGIDA

0
0
 Katibu Mku wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM,Rais Mstaafu wa awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singida.

  Mwenyekiti wa CCM,Rais Mstaafu wa awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete akiwapungia mkono Wananchi waliofika kushuhudia maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM  mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, mkoani Singida.
 Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ukiwasili ndani ya uwanja wa Namfua mapema leo asubuhi kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singida
 Katibu Mku wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Rais Dkt John Pombe Magufuli mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singida
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akimkaribisha Rais Dkt John Pombe Magufuli mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singid,pichani kati ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi alipokuwa akiwasilia mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua,mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singida .

 
 Badhi ya Wananchi mbalimbali wakifuatilia yanayojiri ndani ya uwanja wa Namfua mkoani Singida hivi sasa. 

PICHA NA MICHUZI JR-MMG-SINGIDA



TAMASHA LA PASAKA MWAKA HUU KUFANYIKA MACHI 28 WILAYANI KAHAMA.

0
0

Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Tamasha la Pasaka litakalofanyika  Mkoani Shinyanga Wilayani Kahama Machi 28 mwaka huu ambapo Tamasha la Pasaka mwaka huu halitafanyika jijini Dar es Salaam na baadala yake kufanyika mikoani. 

Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama wakati akizungumza nao leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

TAMASHA la Pasaka mwaka huu kufanyika Machi 28 Mkoani Shinyanga katika viwanja kahama wilaya ya Kahama, ambapo tamasha hilo limewapa kipaumbele waimbaji wa ndani ya nchi yetu.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Msama amesema kuwa Kauli mbiu ya Tamasha la Pasaka mwaka huu ni "UMOJA NA UPENDO HUDUMISHA AMANI KATIKA NCHI YETU". ambayo itatawala katika tamasha hilo hapa nchini.

Msama amesema kuwa Mwimbaji wa nyimbo za Injiri Bonfasi Mwaitege amethibisha kutumbuiza katika tamasha hilo pamoja na Mwimbaji wa nyimbo za Injiri Rose Mhando.

 Aidha Msama amelishukuru  Balaza la Sanaa Tanzinia(BASATA) kwa kuruhusu kufanyika Tamasha la Pasaka wilayani Kahama pia amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika tamasha hilo mkoani humo.

JK AONGOZA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA CCM MKOANI SINGIDA

0
0
 Mwenyekiti wa CCM,Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt  Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wakazi wa Singida na vitongoji vyake ndani ya uwanja wa Namfua,wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM,mkoani Singida.Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi Mbalimbali wa Kitaifa,akiwemo Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,Waziri Mkuu,Mh.Kasim Majaliwa.
 Baadhi ya Wananchi na wafuasi wa chama cha Mapinduzi (CCM) wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikisomwa na Mwenyeki wa chama hicho,Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 39 tangu kuanzishwa kwake ndani ya uwanja wa Namfua leo mchana mkoani Singida.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwenye uwanja wa Namfua kushuhudia sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya CCM mapema leo mchana mkoani Singida
 Rais John Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
 Rais John Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa CCM Namfua, mjini Singida leo.
 Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa katika maadhimisho hayo.
 Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameongozana na Rais Dkt John Pombe Magufuli wakishuka jukwaani kwa pamoja mara baada kuhitimisha shughuli za maadhimisho ya miaka 39 ya chama hicho mkoani Singida,nyuma ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Rais Dkt John Pombe Magufuli.


DC MAKONDA ATOA SIKU 20 WENYEVITI WOTE WA SERIKALI ZA MITAA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM WAPEWE RAMANI ZA MITAA YAO

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza na Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wa wilaya hiyo kwenye mkutano uliofanyika Dar es Salaam leo kuhusu jinsi ya kutatua na kukomesha kero za ardhi
Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Makonda (hayupo pichani)


Na Dotto Mwaibale
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ametoa siku 20 kwa Wenyeviti wote wa Serikali za Mitaa  Manispaa hiyo kuwa na ramani ya mitaa ili kuyatambua maeneo ya wazi.
Makonda amewataka watendaji wa Manispaa hiyo kwenda na kasi ya serikali ya kuwatendea haki wananchi katika kumaliza migogoro ya ardhi.
Akizungumza Dar es Salaam leo mchana na Wenyeviti zaidi ya 100 wa Serikali za Mitaa ya9 Manispaa ya Kinondoni ,Makonda alisema baadhi ya watendaji wanatanguliza maslahi mbele kuliko mahitaji ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Alisema migogoro ya ardhi ni kero kila sehemu  misibani, harusini na kwenye mazishi suala kubwa ni la ardhi na kuongeza kuwa mabaraza ya ardhi ya Kata hayana uhalali wa kuamua kesi hizo kwa kuwa baadhi yao hata uelewa wa masuala hayo hawana na yamekuwa  yakiongeza matatizo.
"Leo tumekutana hapa kwa sababu ya migogoro ya ardhi na kuanzia sasa ndani ya Wilaya ya Kinondoni nataka kurudisha heshima ya Wenyeviti wa Serikali za  Mitaa nawaagiza kuanzia sasa mtu yeyote kutoka Wizarani,Manispaa au hata mwekezaji lazima apitie kwanza kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa,"alisema.
Alisema watendaji wengi Manispaa ndio chanzo cha migogoro ya ardhi kwa kutotimiza wajibu wao na wameshindwa kuonyesha dira ya kuwasaidia wananchi.
"Kibaya zaidi ili kujitengenezea mazingira ya ulaji wenyeviti hawashirikishwi katika hatua za awali wanahusika zaidi pale kunapotokea mgogoro,"alisema.
Aliongeza kuwa "Sina hofu wala uoga wala sina sifa ya kupendwa wala kutafuta kupendwa hivyo nitahakikisha ninatumia Mamlaka niliyopewa kufanya migogoro hii ya ardhi Kinondoni na kuwa historia na nikitaka jambo huwa sishindwi"alisema.
Alisema baada ya wenyeviti hao kupewa ramani atahakikisha anakutana na Wazi ri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilium  Lukuvi na maofisa wa ardhi.
"Hapo sasa watakaobainika kuhusika katika michezo michafu na kuchochea migogoro basi Waziri Lukuvi aondoke nao maana wameshindwa kazi"alisema
Makonda aliwataka wenyeviti hao kuonesha maeneo ya wazi na yale yaliyovamiwa ili kuchukua hatua kwani wenye dhamana wapo ofisini huku wananchi wakiwa wanateseka na migogoro hiyo.
Mkuu wa Idara ya Mipango Miji  Manispaa ya Kinondoni  Juliana Letara alisema Wenyeviti wote watapewa ramani za mitaa yao ndani ya wiki mbili kwa kuwa zipo kwenye kompyuta ofisini hivyo atawapatia ramani hizo.
Alisema kutokana na migogoro mingi ya ardhi anapendekeza kufanyike mapendekezo ya mabadiliko ya sheria kwa kuwa kesi zote za mabaraza ya kata zinaigharimu serikali zaidi ya  milioni tatu kwa siku.
Alizitaja kesi hizo kuwa ni za ardhi ya hifadhi,ardhi ya kawaida na ile ya kimila 
"Tulikopa benki ya TIB mkopo kwa  ajili ya kupima Viwanja likiwemo eneo la Mabwepande lakini kila siku tunatozwa riba ya sh.milioni tatu jambo ambalo ni gumu na ipo siku litashindikana na ndio maana tunauza Kiwanja hadi milioni 20 na 30,"alisema. 

Baadhi ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa ambao walipata nafasi ya kuzungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo walimtaka Makonda kuondoa majipu sugu katika Manispaa hiyo likiwemo la maofisa mipango miji.
Alisema  wako tayari kufanyazi na Makonda lakini sio wafanyakazi hao kitengo cha ardhi kwa kuwa wamekuwa chanzo cha migogoro mikubwa ya ardhi.

KUTOKA MAKTABA: MWALIMU NYERERE ALIPOFANYA ZIARA YA KISERIKALI NCHINI UINGEREZA MWAKA 1975


MAHAFALI YA KUWATAMBUA MAFUNDI WALIOTOKA MTAANI NA UJUZI WAO KISHA KUPATA MAFUNZO RASMI NA CHUO CHA UFUNDI VETA YAFANA SANA JIJINI MBEYA

0
0
Mgeni Rasmi wa Hafra hiyo Bwana Jastine Ruta Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi Veta kanda ya Mbeya akihutubia katika Hafra hiyo ya Wahitimu wa Mafunzo Rasmi ya Veta kwa walio kuwa na ujuzi katika Nyanja Mbalimbali ikiwemo Upishi, Uwashi, Ufundi wa Magari pamoja na Chakula na Vinywaji.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Veta kanda ya Mbeya Ndugu Lameck Padrii Kihinga akizungumza jambo katika Hafra hiyo ya Mahafari ya Mafunzo Rasmi yaliyo tolewa na Chuo cha Veta kwa Vijana na Watu Mbalimbali wenye Fani hizo za Ufundi kujiendeleza Kifani na kupata Cheti.
Baadhi ya wahitimu wakisoma Lisala kwa Mgeni Rasmi ikiwa ni miongoni mwakuhitaji Elimu ifike mpaka Vijijini juu ya ujasiliamali, Kujiajili au Kuajiliwa mara baada ya kuhakikiwa Kimafunzo, Mafunzo endelevu na kujiunga katika Vikundi Mbalimbali vya Ujasiliamali, Ubora wa kazi na Usalama, Kupata Mikopo na Sehemu Nzuri za kufanyia Mafunzo pia kusaidiwa Kutangaza shughuli zao katika Vyombo Mbalimbali vya Habari ikiwemo, Redio, Magaazeti, Vituo vya Terevisheni, Blog Mbalimbali Vipeperushi na Magari ya Matangazo.
Baadhi ya wahitimu wakiwa katika Ukumbi Mdogo wa Chuo cha Ufundi Veta iliyopo Ilomba Jijini Mbeya.
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.

TPDC yawajengea uwezo wanahabari Mtwara

0
0
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) liliandaa semina ya waandishi wa Mkoa wa Mtwara, Semina hiyo ililenga kuwajengea uwezo waandishi hao kuielewa sekta ya mafuta na gesi asilia mchini.

Akifungua semina hiyo kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Meneja wa Mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellemu alisema semina hiyo anaamini itawajengea uwezo waandishi hao hasa wanapo toa taarifa za mafuta na gesi asilia kwa wananchi.

Watoa mada katika semina hiyo kutoka TPDC walitoa mada zilizo gusa shughuli nzima za Shirika kuanzia utafiti wa gesi asilia na mafuta hadi matumizi ya rasilimali hizo.

Kwa upande wao waandishi wa habari walioshiriki semina hiyo wameipongeza TPDC kwa jitihada hizo za kutoa mafunzo kwao, zaidi waandishi hao wametaka mafunzo hayo yawe endelevu kwao.

 Meneja wa Mawasiliano kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Marie Msellemu akifungua semina ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Mtwara, semina hiyo ilifanyika Manispaa ya Mtwara Mikidani huku ikilenga kuwajengea uwezo waandishi hao katika kuilewa tasnia ya mafuta na gesi asilia nchini.

Meneja wa Biashara ya Gesi kutoka TPDC Emmanuel Gilbert (kulia) akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mtwara.

 Waandishi wa habari kutoa Mkoa wa Mtwara walioshiriki semina hiyo.

Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari Mtwara Bw. Brayson Mshana akichangia jambo katika semina hiyo.

 Wawezeshaji wa semina kutoka TPDC wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari kutoka Mkoa wa Mtwara.




RAIS WA ZANZIBAR AWAANDALIA CHAKULA VIJANA WA HALAIKI LEO

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na viongozi wakiimba wimbo maalum alipokaribishwa na vijana wa halaiki chakula maalum kwa Vijana hao walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  alipowaandalia katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo 
 Vijana walioshiriki katika halaiki  ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakichukua Chakula  katika hafla ya iliyoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo
 Vijana walioshiriki katika halaiki  ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakichukua Chakula  katika hafla ya iliyoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo
 Vijana walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakiwa katika hafla ya chakula maalum iliyoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakitia chakula wakati wa hafla maalum ya chakula aliyowaandalia Vijana walioshiriki katika Halaiki ya sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar iliyofanyika leo katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja. Picha na IKULU, Zanzibar

EALA CONCERNED ABOUT REPUBLIC OF BURUNDI …Cease all atrocities and killings legislators say, as EAC Summit urged to concert efforts in finding solutions to the humanitarian crisis

0
0
East African Legislative  Assembly
The East African Legislative Assembly holds that there are serious and sufficient grounds showing gross human rights violations have taken place and continue in the Republic of Burundi unabated. 
The Assembly views that the EAC under the Treaty obligation, the African Union under the Constitutive Act, the United Nations and other international players owe a duty of care and responsibility to protection of the people of Burundi. In addition, EALA requests the Summit of the EAC Heads of State to do all that is possible to stop the humanitarian, human rights and political crises in the country.

The Assembly late yesterday debated and adopted the Report of the Committee on Regional Affairs and Conflict Resolution on the deteriorating human rights and humanitarian situation in Burundi.

With it, the Assembly lauded the commitments taken by the African Union (AU) on the issue of sending a high level mission to Burundi to discuss deployment of an African Union preventive and protection force to secure the wellbeing of citizens. In the same vein, it underscored the need for the continental bloc to deploy a non-partisan preventive and protection force to secure the wellbeing of the citizens and to stop the gross human rights violations. 
The Assembly also urged the EAC Summit of Heads of State to affirm that EAC has a duty of care and responsibility to protect the people of Burundi from violence and to guarantee their safety and security.

Of equal importance is the need for the EAC Summit to consider and support establishment of a credible investigative mechanism to independently investigate all allegations of human rights violations in Burundi.  While supporting the work of the Office of the mediator, H.E. Yoweri Kaguta Museveni, the Assembly is emphatic that an all-inclusive, participatory and credible process of dialogue in and outside of Burundi shall bring peace to the country. 
The Report of the Committee follows the recent Public Hearing workshop on Burundi which delved into the Petition presented to the EALA Speaker by the Pan African Lawyers Union (PALU) and other regional Civil Society Organisations on the subject matter in November 2015.

On January 14-15, 2016, the Committee received the oral presentation from the petitioners as well as the contributions from representatives of the opposition Political Parties and civil Society Organisations.    On January 25th, 2016, a high powered delegation from the Government of Burundi, also came to Arusha to make their submissions. before the Committee retreated to make its report. 
The stakeholders who spoke on 15th January 2016 broadly agreed with the petition, elaborated arguments asserting that the crisis in Burundi was a political problem. They further clarified how the situation had mutated into an ethnic problem, citing parallels with the 1994 genocide in Rwanda. Most presenters according to the Report gave a gruesome picture of the nature of the crimes and human rights abuses including details on refugees and internal displacements, arrests and detentions.

“Pictures of some of the notable instances of murders were further shown and submitted for record,” Hon Abdullah Mwinyi, Chair of the Committee on Regional Affairs and Conflict Resolution said.
On its part, the Government of Republic of Burundi that appeared before the Committee on January 25, 2016 took a long-term view of the Burundi crisis including the post-colonial history. 
The delegation led by Hon Leontine Nzeyimana, Minister for EAC Affairs in Burundi however included a mix of representatives from government, political parties, and civil society. On her part, the minister noted: ‘As it has been happening in Burundi since the early 1960’s, the electioneering period was marked by negative propaganda intended to create in Burundi a political and institutional instability. 
According to the Report, the delegates submitted that EALA has a major role to play in helping Burundi to restore order. While presenting the report to an attentive House yesterday, Hon Mwinyi noted numerous outstanding issues that require resolution and careful thinking through. Among these areas are political with all presenters at the hearing acknowledging, that Burundi faces a crisis. With regards to human rights violations, delegates pointed out to instances of human rights abuse – albeit attributing them to either side.

They included rape, extra-judicial killings, assassinations, detentions, and unexplained disappearances. Evidence of mass graves and gruesome pictures of unspeakable mutilations were put on record.The Committee further remarked it was not aware of any homogeneity among the youth. 
“There is now enough credible evidence from UN and other Human Rights sources that confirm that Imbonerakure (Youth group) plays the function of a party militia”, a section of the report said. 
“Indeed, it has been repeatedly reported that they have been involved in "arbitrary" arrest of members of the opposition "under the guise of national police or SNR officers.  Their presence is so strong it may have overshadowed the presence of youth groups affiliated to other parties who, as the Committee heard, also exist. Not only have Imbonerakure been involved in the gradual breakdown of law and order, this context has allowed more merchants of violence who are not necessarily active disputants or members of the Imbonerakure to also partake to a gradually deteriorating political environment”, a section of the report said. 
The importance of this crisis to the EAC, the Report added, was brought home by accusations leveled against a Partner state by the Government-led delegation. Except for one Report, the delegation was unable to provide adequate evidence to the Committee to validate the claim that the Republic of Rwanda is hosting and militarily training Burundi refugees. 
“They also claimed that the Secretary General of the EAC was biased but did not provide any evidence for the claim”, Hon Mwinyi said. 
At debate time,  Hon Abubakar Zein remarked that the report had pricked the conscience of the Assembly and lamented that not much had been done to contain the humanitarian and political crisis. He said it was time for the region to move fast with regards to operationalising the East African Parliamentary Institute in order to build capacity for Parliamentary Democracy and the enhancement of peace and security initiatives.

Hon Hafsa Mossi said it was important to stand in solidarity with the Republic of Burundi.  “We cannot have solutions by imposing sanctions on the EAC Partner State”, she said.Hon Peter Mathuki said it was vital for the region to find solutions to the happenings in Burundi while Hon Nancy Abisai called for a participatory approach involving all stakeholders. Hon Odette Nyiramilimo said insecurity in one of the Partner States would easily lead to insecurity in another and appealed for peaceful solutions to the crisis, sentiments which were also shared by Hon Taslima Twaha and Hon Angela Kizigha. 
Hon Mumbi Ngaru remarked that leadership was key at this point in time and said it was wrong to point fingers at each other.Hon Isabelle Ndahayo requested the Assembly to enable the Committee to visit Burundi to further assess the situation.
The Minister for EAC, Burundi, Hon Leontine Nzeyimana thanked the Committee and the Assembly for the report and for handling the entire process which was difficult due to the sensitivities with objectivity.
 Hon Abubakar Zein contributes to the debate on the Report of the Regional Affairs and Conflict Resolution Committee on the humanitarian situation in Burundi
 Hon Dr. Martin Nduwimana contributes to the debate 
The Chair of the Regional Affairs and Conflict Resolution Committee, Hon Abdulla Mwinyi reads the report to an attentive House

MHE UMMY MWALIMU MGENI RASMI KATIKA MAADHIMSHO YA SIKU YA KUPINGA UKEKETAJI DUNIANI, MKOANI DODOMA

0
0
Mheshimiwa Ummy Ally Mwalimu (Mb.) Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukeketaji Duniani yanayofanyika tarehe 5 Februari kila mwaka. Maadhimisho hayo kwa Mkoa wa Dodoma yalifanyika katika Ukumbi wa Hazina Dodoma, kwa kuratibiwa na Mtandao wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayopinga Ukeketaji Tanzania.
Wakati wa maadhimisho hayo Mhe Waziri Ummy Mwalimu alieleza kuwa Kwa mujibu wa Takwimu za Demografia na Afya Tanzania (Tanzania Demographic and Health Survey - TDHS 2010) asilimia 15  ya wanawake Tanzania wamefanyiwa Ukeketaji. Ukeketaji ni ukatili dhidi ya watoto wa kike na wanawake. Na ni kosa la jinai. Madhara ya ukeketaji ni pamoja na vifo, vilema na maradhi kama fistula na mengineyo.

Alieleza kuwa Serikali itaendelea kukemea na kupambana na vitendo hivi katika jamii zetu. Na itaongeza jitihada za kutoa elimu kwa jamii sambamba na kuwachukulia hatua wote wanaojihusisha na vitendo hivi.

Mhe Waziri Ummy Mwalimu aliwataka Maafisa Maendeleo ya Jamii katika Mikoa, Wilaya na Kata kuongeza nguvu ktk kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa lengo la kuhakikisha wazazi/walezi, mangariba na wote wanaojihusisha na vitendo vya Ukeketaji wanafikishwa ktk vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake.

Aidha, alitoa wito kwa kila mwananchi kushiriki katika mapambano haya hasa katika kutoa taarifa na ushahidi Mahakamani.
Mheshimiwa Ummy Ally Mwalimu (Mb.) Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (mstari wa mbele katikati), Mkuu wa wilaya ya Dodoma  Dkt. Jasmine Tisekwa ( Kulia) na Muwakilishi wa UNFPA, Bi Christine Mwanukuzi ( Kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Mtandao wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayopinga Ukeketaji Tanzania, wakati wa maadhimisho ya Siku ya kupinga ukeketaji kwa 
Mheshimiwa Ummy Ally Mwalimu (Mb.) Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akipokea maandamano ya wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Mtoto katika viwanja vya ofisi za Hazina Dodoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya kupinga ukeketaji kwa wanawake na watoto wa kike.wanawake na watoto wa kike.

Mheshimiwa Ummy Ally Mwalimu (Mb.) Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akihutubia wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Mtoto, wakati wa maadhimisho ya Siku ya kupinga ukeketaji kwa wanawake na watoto wa kike.
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images