Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1111 | 1112 | (Page 1113) | 1114 | 1115 | .... | 3282 | newer

  0 0

  By Hassan Saudin

  The on-going rift between the Government of Tanzania and owners of private schools over the government’s decision to regulate and dictate tuition and other  fees charged by private schools in the country calls for an urgent need on the part of the  government and parliament to re-assess and re-define the role of government in private education. 

  Without denying the fact that regulation is crucial to enforcing government policy designed at meeting specific goals, there are now strong indications that the government’s decision to dictate fees and other charges by the private schools and institutions of higher learning will only do more harm than good.

  On the outset, an apparent goal of such a policy is to make private education more accessible to the masses but a critical assessment of such a policy and the current approach only suggest that such a stance will only lead to making the sector unattractive and unjustifiable from investment perspective which will potentially lead to depriving Tanzanians of that alternative. The broader implication is the potential diminishing of Tanzania’s reputation as a preferred investment destination of choice in the region. One fact is obvious, no private investor is going to offer quality education without a decent return on investment.  

  Cost of service delivery significantly varies from school to school depending on factors such as what the school offers in terms of academics and extra curriculum activities, standard of facilities, strategy on staff recruitment and retention and so on, this is a universal reality. The decision by the government to come up with nation-wide fees completely contradicts this reality and only creates an environment that encourages private schools to focus on cost cutting at the expense of quality education.

  With the emergence of a growing Tanzanian middle class, families are willing and able to pay a premium for quality education. The government needs to accept the fact that Tanzanians are capable of making rational decisions and comparisons on whether or not fee charged by the private schools are justified or otherwise. Depriving parents of such an option will only encourage parents who believe in investing in quality education to send their children to neighboring countries, a decision that could cost the country not only revenues going into the sector but also talent because upon graduation companies are quick at grabbing employees from top notch schools.


  0 0

  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, akichangia majadiliano ya Bodi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto ( UNICEF) hapo siku ya jummane. Katika mchango wake, Balozi amewaeleza wakuu wa UNICEF kwamba, mabadiliko ya kweli yanayolenga kuboresha hali bora ya maisha ya makundi yote ya jamii, wakiwamo watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali hayawezi kufanyika kwa mashinikizo kutoka nje bali yatafanyika kwa ushiriano na ubia wa dhati baina ya Serikali, Wadau wa Maendeleo na Wananchi wenyewe. Vile vile Balozi Manongi akasisitiza kwamba UNICEF inapashwa kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia bajeti iliyojipangia badala ya kutegemea misaada kutoka kwa wahisani, hususani Asasi zisizo za kiserikali kwa kile alichosema, mara nyingi Asasi hizo hutoa misaada yao kwa malengo ya kushinikiza ajenda zao na maslahi binafsi, Mkutano huo pia ulipokea na kupitisha mpango kazi wa utekelezaji wa miradi ya UNICEF pamoja na rasimu ya Ripoti ya Tanzania ambayo imeainisha masuala mbalimbali pamoja na miradi ya maendeleo inayorajiwa kutekelezwa na UNICEF kwa Tanzania. Aliyeketi na Balozi ni Afisa wa Uwakilishi Bi.Ellen Maduhu
  Meza kuu ya Wakurugenzi na Watendaji wa UNICEF wakati wa mkutano wa Bodi hiyo uliofanyika siku ya jumanne na kuhudhuriwa na wajumbe wa Bodi hawapo picha pamoja na wajumbe wengine waalikwa. Tanzania ilialikwa katika mkutano huo kama msikilizaji.

  0 0

  Shirika la Kimataifa la maendeleo la Sweden( SIDA), limeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya Umeme inayofahiliwa na Shirika hilo hususan usambazaji wa umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini REA kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini( Tanesco), katika maeneo mbalimbali nchini.

  Mkuu wa Shirika la Kimataifa la maendeleo la Sweden( SIDA) Maria Van Berlekom amesema hayo mara baada ya kuona maendeleo ya wananchi wa vijijini wakati wa ziara yake ya kutembelea utekelezaji wa miradi hiyo katika mikoa ya kanda ya kaskazini .
  Mtambuzi wa miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijini, Mhandisi Elneema Mkumbo akitoa maelezo juu ya utekelezaji wa miradi ya REA, kwa Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden( SIDA) Maria Van Berlokom ( aliyeweka mikono kifuania) ambao ni miongoni mwa wafadhili wa miradi hiyo akiwa na ujumbe wake pamoja na wadau wengine wa maendeleo ikiwemo Shirika la Maendeleo la Ujerumani( GIZ) wakati wakikagua utekelezaji wa miradi ya REA katika mikoa ya kanda ya kaskazini.
  Muonekano wa nyumba zilizounganishwa na huduma ya umeme unaotekelezwa na Wakala wa Nishati vijijini REA katika kijiji cha Kwedizinga mkoani Tanga.

  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Salim Amiri akimkabidhi fedha kiasi cha milioni mbili (2,000,000) Nahodha wa timu hiyo,Hamis Mbwana “Kibacha” zilizotolewa na Mfadhili wa timu hiyo,Alhaji Salim Bajaber ambaye ni mkurugenzi wa kiwanda cha Unga cha Pembe Tanga wanaoshuhudia ni viongozi wa timu hiyo makabidhiano hayo yalifanyika viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mara baada ya kumalizika mazoezi ya jana jioni.
  Nahodha wa timu ya Coastal Union, Hamis Mbwana “Kibacha” akionyesha juu fedha alizizokabidhiwa milioni mbili (2,000, 000) kama motisha baada ya kuifunga timu ya Yanga zilizotolewa na Mfadhili wa timu hiyo,Alhaji Salim Bajaber ambaye ni mkurugenzi wa kiwanda cha Unga cha Pembe Tanga wanaoshuhudia ni viongozi wa timu hiyo makabidhiano hayo yalifanyika viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mara baada ya kumalizika mazoezi ya jana jioni.
  Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union, Salim Amiri akitoa nasaha kwa wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo yao inayofuata ili waweze kumaliza Ligi kuu wakiwa nafasi za juu mara baada ya kupokea kitita cha sh.2,000, 000 kama motisha baada ya kuifunga timu ya Yanga zilizotolewa na Mfadhili wa timu hiyo,Alhaji Salim Bajaber ambaye ni mkurugenzi wa kiwanda cha Unga cha Pembe Tanga wanaoshuhudia ni viongozi wa timu hiyo makabidhiano hayo yalifanyika viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mara baada ya kumalizika mazoezi ya jana jioni kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa timu hiyo, Salim Bawaziri na wa kwanza kushoto ni Kocha Mkuu wa timu Ally Jangalu na wajumbe wa kamati ya utendaji wa timu hiyo.
  Kaimu Katibu Mkuu wa timu ya Coastal Union,Salim Bawaziri akitoa nasaha zake kwa wachezaji mara baada ya kukabidhiwa fesha kiasi cha milioni mbili (2,000, 000)kama motisha baada ya kuifunga timu ya Yanga zilizotolewa na Mfadhili wa timu hiyo,Alhaji Salim Bajaber ambaye ni mkurugenzi wa kiwanda cha Unga cha Pembe Tanga wanaoshuhudia ni viongozi wa timu hiyo makabidhiano hayo yalifanyika viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mara baada ya kumalizika mazoezi ya jana jioni. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Coastal Union.

  0 0
 • 02/02/16--22:27: kumbukumbu
 • Leo, ilikuwa saa, siku, mwezi, hatimae miaka 26 imepita toka baba yetu mpendwa ututoke ghafla trh 3/2/1990 nyumbani kasulu kigoma, lkn kimwili kaupo nasi ila kiroho upo nasi, tutakukumbuka baba yetu kwa upendo,ukarimu, uchangamfu wako, unakumbukwa na mkeo Monica nkaliguye, wanao Rose, Ruth, sara, Edina, Rutegama, Eliwaja na Barnabas na wajukuu Steven na wakwe zako, misa ya kumuombea Marehemu itakuwa kanisa la kkkt kitanda relini jumapili hii, Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake litukuzwe, Ameni

  0 0


  0 0


  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Mkuranga.

  WAKAZI na wananchi wa vijiji vinavyounda Kata ya Panzuo, wilaya Mkuranga, mkoani Pwani, wameendelea kuililia barabara mbovu inayoanzia Kijiji cha Kimanzichana, hali inayowalazimu akina mama kujifungulia njiani na kuuweka uhai wao rehani.

  Mwendesha bodaboda Ramadhan Rajab akijaribu kupita katika barabara mbovu inayotokea Kimanzichana, kuelekea vijiji vya Mnyonzole na Kibesa,wilayani Mkuranga, mkoani Pwani, nauli kwa safari moja wakitoza Sh 20,000 hadi 30,000 kwa safari moja. Nyakati za mvua barabara hiyo haipitiki hali inayozidisha ugumu wa maisha kwa wananchi hao.


  Vijiji hivyo ni Marui, Kisegese, Mbezi Muungwana, Msanga Visiga, Kibayani na vinginevyo vinavyoitumia barabara hiyo inayopitika wakati wa jua kali na zinapoanza mvua mawawasiliano yao kutoka katika maeneo yao hadi kwenye barabara Kuu ya Lindi Dar es Salaam kukosekana.

  Mkazi wa kijiji cha Mnyonzole Kibesa, Cosmas Kisabo, akizungumza jambo kuhusiana na kero kubwa ya barabara wanayokutana nayo wananchi hao, inayaopelekea akina mama wengi kujifungulia njiani, mvua kubwa zinapoanza kunyesha.

  Mwandishi wa mtandao huu ametembelea katika maeneo hayo na kujionea hali mbaya ya barabara hiyo ambayo inaweza kuwa chanzo cha kuinua uchumi wa wananchi hao endapo itakarabatiwa japo kwa kiwango cha changarawe ngumu.


  Akizungumza jana wilayani hapa, dereva wa bodaboda anayejulikana kama Ramadhan Rajab, alisema kwamba mvua kubwa inaponyesha huwezi kutoka ulipokuwa kwenda sehemu yoyote, kwa sababu barabara inakuwa mbovu.
  Mkazi wa kijiji cha Kibesa, Bi Sofia Michael anayejishughulisha na kilimo na biashara ndogo ndogo, akiwa nje ya kibanda chake akizungumza na mtandao huu. Bi Sofia anasema maisha yamekuwa magumu zaidi kutokana na kukosa barabara.

  0 0

  Mwanasaikolojia Anti Sadaka amewafunda wanawake wa Zanzibar wanaoshiriki mafunzo ya ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalamu kutoka taasisi ya Manjano Foundation na Zanzibar Chamber of Commerce yanayoendelea Zanzibar kwa wiki nzima.

   Anti Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo yao waliojiwekea.

   Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake hao kujitambua wao ni nani wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la kufikia malengo yao.Pia amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mjini Zanzibar kuchangamkia FURSA zinazowazunguka. 

  Semina hiyo inawanufaisha wanawake wa Zanzibar kwa lengo la kuwaongezea kipato na pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira. 

  Anti Sadaka amewashauri wanawake wasiache kujifunza na kujibweteka baada ya mafunzo haya kuisha isipokuwa wawe makini kutafuta elimu zaidi ya kujiongezea ujuzi katika kazi zao.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  JESHI LA POLISI TANZANIA.

  TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA.
  · MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MATATU KUGONGANA JIJINI MBEYA.

  · JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA WAWILI WA NCHINI ETHIOPIA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

  · JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 08 KWA MAKOSA MBALIMBALI.

  KATIKA TUKIO LA KWANZA:
  MTU MMOJA [DEREVA] WA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 321 CSV AINA YA TOYOTA COASTER AITWAYE LWIMIKO MWANSASU [36] MKAZI WA UYOLE ALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 877 CWE AINA YA SCANIA BASI MALI YA KAMPUNI YA SUPERSHEM LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA EMANUEL JOHN [42] MKAZI WA MWANZA KUGONGANA NA GARI HILO NA KISHA KULIGONGA GARI JINGINE LENYE NAMBA ZA T. 321 CSV AINA YA TOYOTA HIACE LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AMBAKISYE MBOMA [45] MKAZI WA AIRPORT.

  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 06:30 ASUBUHI HUKO ENEO LA SOWETO, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. 

  CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI WA BASI HILO LILILOKUWA LINATOKA MBEYA KUELEKEA MWANZA. DEREVA AMEKAMATWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. UPELELEZI UNAENDELEA.

  TAARIFA ZA MISAKO:
  JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA 1. AYNO ASATA [21] NA 2. CHARU SUMESO [18] KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

  WAHAMIAJI HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO ENEO LA MAJENGO, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAENDELEA.

  JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO 1. HAIDAN RODRICK [35] 2. JULIUS BUTEMELE [53] 3. VISENT MAPILE [29] 4. DOTO MWASHITETE [25] NA 5. JOSEPH BUTEMELE [40] WOTE WAKAZI WA ISANGAWANA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA WAKIWA WANAKUNYWA POMBE MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [5].

  WATUHUMIWA KWA PAMOJA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 14:45 MCHANA HUKO KIJIJI NA KATA YA ISANGAWANA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. 

  MTU MMOJA MKAZI WA IYULA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMANNE HAONGA [32] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA KUMI [10]. 

  MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 11:20 ASUBUHI HUKO KIJIJI, KATA NA TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. 

  MTU MMOJA MKAZI WA ILOLO WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DANIEL NZUNDA [30] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA POMBE MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [5].

  MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 13:40 MCHANA HUKO KIJIJI NA KATA YA ILOLO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. 

  WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WAGENI KUFUATA TARATIBU ZILIZOWEKWA ZA KUINGIA NCHINI ILI KUJIEPUSHA NA MATATIZO.

  Imesainiwa na:
  [AHMED Z. MSANGI – SACP]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Innocent Mungy, akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kutambua Simu Feki na kudhibiti uingiaji wa Simu hizo Tanzania na kueleza mwisho wa matumizi wa simu hizo Nchini Tanzania ni Juni 2016. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilima Zanzibar na kuwashirikisha waandishi wa Vyombo mbali mbali vilioko Zanzibar. 
  Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Thadayo Ringo akionesha mfano wa simu orijino kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
  Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
  Imetayarishwa na Othman Mapara.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0
 • 02/03/16--03:47: BEI YA MADAFU HII LEO.

 • 0 0

    Mafundi wakiendelea na ujenzi wa barabara ya Bagamoyo kipande cha kilometa 4.3 cha Mwenge – Morocco, leo jijini Dar es Salaam, ambayo ni kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Pombe  Joseph Magufuli.
   Scavertor kikichota undongo na kupakia katika magari kwenye barabara ya Mwenge hadi Morocco kwa kuongeza njia mbili za lami leo jijini Dar es Salaam.

  Fundi akitoa maelekezo kwa mwendasha Scavertor katika barabara ya Mwenge hadi Morocco kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni matumizi ya Fedha za Uhuru zilizoagizwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kutengeneza Barabara hiyo.  (Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii).

  0 0

  Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto, Dkt. Ulisubisya Mpoki akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Siku ya saratani, huadhimishwa duniani kote kila mwaka ifikapo tarehe 4 ya Mwezi februari. 

  Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani mwaka huu ni ‘TUNAWEZA, NINAWEZA. KWA PAMOJA TUWAJIBIKE KUPUNGUZA JANGA LA SARATANI DUNIANI.” (We can, I can. How everyone, as a collective or as an individual can do their part to reduce the global burden of cancer). 

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Julius Mwaiselage akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na huduma za matibabu zinazotolewa na Taasisi ya Ocean Road.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto, Dkt. Ulisubisya Mpoki leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii. 

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

  WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Ocean Road pamoja na wadau mbalimbali  kuadhimisha siku ya Saratani kuanzia kesho kwa kutoa elimu ya umuhimu wa kuzuia na kujikinga na madhara mbalimbali yatokanayo na maradhi ya Saratani ambayo hufanyika kila Februali 4 ya kila mwaka . 


  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Ulisubisya Mpoki amesema kuwa Saratani ni ugonjwa ambao unaathiri watu wa rika na jinsia zote; watoto, watu wazima, wake kwa waume. 

  Amesema takwimu za Shirika la Kimataifa la Atomiki la Utafiti wa Saratani (IARC) na Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaelezea kwamba kila mwaka duniani kunatokea wagonjwa wapya wa saratani wanaokadiriwa kufikia milioni 14.1, kati ya hao, zaidi ya wagonjwa milioni 8.2 hufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Saratani, hii husababishwa kwa wagonjwa kuchelewa kufikishwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Vifo vya ugonjwa wa Saratani ni asilimia 13 ya vifo vyote vinavyotokea duniani (WHO). 

  Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Saratani duniani mwaka huu ni ‘‘Tunaweza , Ninaweza.Kwa pamoja tuwajibike kupunguza janga la saratani duniani’’. 

  Dk.Mpoki amesema kuwa hatua madhubuti za kinga, uchunguzi wa mapema na tiba stahiki hazitachukuliwa haraka, tatizo la Saratani litaongezeka na kufikia makadirio ya wagonjwa wapya milioni 24 ifikapo mwaka 2035, huku ongezeko kubwa likiwa katika ukanda wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. 

  Amesema tatizo la Saratani limekuwa likiongezeka na kukua, kila mwaka, Takribani wagonjwa wapya wapatao 44,000 hugundulika na saratani za aina mbalimbali nchini, hii ni sawa asilimia 10 tu (4,400) kati ya wagonjwa wote wanaofanikiwa kufika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ili kuweza kupata tiba. Kati ya hao wanaobahatika kufika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (takribani asilimia 80) hufika wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa (Hatua ya 3 na ya 4), hali ambayo hupunguza uwezekano wa wagonjwa kuweza kupona maradhi hayo. 

  0 0
 • 02/03/16--04:32: WELCAB VEHICLE FOR SALE
 •   This vehicle  can be used for a handicapped person (Someone who has difficulties  to walk without help, he/she will sit in the passenger’s seat and can go anywhere without having some assistance by another person). The car can store the wheel chair in the back.  The lift  for  this wheel chair is installed in the trunk area. 
  Details: Toyota Ractis, 2009y model 
  51,000km, at,ac,ps,pw,cl,Navi, 
  radio/CD, air bags, Special seat, lift in the trunk. 
  Blue color Grade 4.0.  
  Price - CIF us $ 7,000.

   For More details contact 
  +255 754 400606 or +255 658 856351
   Trunk
   Side and back view
   Front and side view
  Front seats

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 3, 2016.

  Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akizungumza Bungeni Mjini Dodoma Februari 3, 2016.

  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Abuu Jumaa (katikati) na Mbunge wa Bukoba Vijijini Jasson Rweikiza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 3, 2016.
   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Jogoo akiwa katika harakati za kutafuta chakula mara baada ya kutahamaki huku akinaswa na Kamera yetu.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

   ke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 

  Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.

   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhiwa taarifa Bw. Ojuku Mgedzi, Mkuu wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana kwa furaha na wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.

  PICHA NA IKULU


  Na Magreth Kinabo –MAELEZO
  MKE wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Janeth Magufuli ameziomba na kuzimahamasisha taasisi za Serikali na zisizo za Serikali kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu Wasiojiweza kijulikanacho kwa jina la Nunge,viwemo vingine.

  Aidha alisema vituo hivyo jumla vipo 17, katika maeneo mbalimbali nchini.
  Kauli hiyo imetolewa leo na Mama Magufuli wakati alipotembelea makazi hayo yaliyoko Kigamboni eneo la Vijibweni jijini Dares Salaam, ambapo alisema changamoto wanazokabiliana nazo amezisikia na na aliwaahidi kuwa atashirikiana na wadau wote kuzitafutia majibu yake.

  Mama Magufuli alizitaja baadhi ya changamoto hizo, ni kuwa uchakavu wa miundombinu, uhaba wa rasilimali fedha na watu, pamoja na maslahi duni ya watoa huduma, upungufu wa vitendea kazi na huduma za jamii, pamoja na uvamizi wa eneo la kituo.

  Aidha Mama Magufuli alimwomba Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema kulishughulikia taizo la uvamizi wa eneo hilo na kulitafutia ufumbuzi.

  “ Natumainni zawadi tuliyoileta ni ndogo na haiwezi kumaliza matatizo yote mliyonayo. Lakini ni matumaini yangu kuwa zawadi hii inaweza kuwa chachu ya kuhamsha hamasa ya watu na vikundi vingine kujitoa kusaidia watu wasiojiweza. Ni imani yangu kuwa endapo watu wote tutajitoa kwa dhati tutaweza kuwahudumia wazee na watu wasiojiweza na hivyo kuwapunguzia makali ya maisha.

  0 0


  0 0

   Jaji wa Mhakama Kuu ambae pia ni Mkuu wa Chuo cha Mahakama cha Lushoto Jaji Ferdinand Wambali, akisaini kitabu cha wangeni alipotembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF, katika Maonesho ya Wiki ya Sheria leo jijini Dar es Salaam. 
   Ofisa mawasiliano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) Luhende Singu akitoa maelekezo kwa wananchi juu ya kujiunga na mkuko huo, katika Maonesho ya Wiki ya Sheria leo jijini Dar es Salaam.
  Wananchi wakiwakiwa katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) katika Maonesho ya Wiki ya Sheria leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii

older | 1 | .... | 1111 | 1112 | (Page 1113) | 1114 | 1115 | .... | 3282 | newer